Makanisa ya Kikristo ya Mungu

 

[296]

 

 

 

Kujulikana Na Kukusudiwa Tangu Mwanzo

 

(Toleo La 2.0 20060807-20110806)

 

Biblia inasema kuwa sisi tumechaguliwa na Mungu na kwamba tumekusudiwa tangu mwanzo na kuitwa. Je, jambo hili linamaana gani hasa? Na linafanyika lini? Hebu na tuendelee kujifunza!

 

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hakimiliki  ©  2006, 2011 Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 

 


Kujulikana na Kusudiwa Tangu Mwanzo

 


Kuijua Hatima Yake

Dhana ya kamba Wateule Walijulikana na Kukusudiwa tangu mwanzo inajengewa hoja yake kutoka na tabia za Mungu kuwa Anajua Kila Jambo (Omnicience). Mungu anaaminika kuwa ni mwenye nguvu zote (Omnipotent), yaani ni kwamba yeye anauweza wote na kwamba ni yeye tu mwenye sifa na tabia hizi za kujua kila jambo na kuwa na uweza wote na kwamba hakuna kinachomshinda, na pia anawezo wa kuweko kila mahali kwa wakati mmoja. Anaweza kuwepo kila mahali kwa kumtumia Roho Mtakatifu ambaye utendaji kazi wake katika kuwepo kila mahali twaweza kuufananisha na mwendo wa umeme unavyoweza kwenda kwenye maeneo ulikokusudiwa kwenda na unakwenda kwa mara moja kutoka kwenye kituo kilichowekwa kitufe cha kuufungulia.

 

Pia hali hii ya Kujua kila jambo (Omniscience), inaweza kutafsiriwa kama uweza wa kujua ukweli wa kila neno au shauri. Ni ukweli kabisa wanadamu wameweza kuijua hatima ya mambo kwa kufuatia yaliyoandikwa kwenye historia. Biblia inatuambia pia kwamba hata mapepo wanauwezo wa kutabiri na kubashiri mambo na matukio yatakayotokea baadae (Matendo 16:16).

 

Mungu aliwakataza Israeli wasifanye hivyo. Mungu alimwambia Musa awaambie Israeli kwamba:

Kumbukumbu la Tirati 18:10 10Asionekane mtu ye yote miongoni mwenu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, atakayefanya uaguzi, ulozi, anayetabiri nyakati, anayejishughulisha na uchawi

 

Lakini Mungu pia alitumia roho ya unabii kuongea na Israeli kwa kupitia manabii wake, na manabii waliweka siku za Miandamo ya Mwezi kuwa ni muafaka kwao kuwaeleza watu kile walichoonyeshwa kwenye unabii wao na kuwaambia Israeli.

 

Je, hili lilikuwa ni jambo la kuwachanganya? Hapana, bali lilikuwahivyo kama kipimo cha kudhibiti na kuweka utaratibu wa Kimungu wa kutoa jumbe za kinabii za manbii wa kweli waliokubalika na Israeli, wakiwa ni watumishi wa Mungu wa Pekee na wa Kweli. Mapepo wanatumia mabashiri yaonekanayo kama unabii ili kuathiri uelewa na fikra za watu wnaowategemea. Mambo haya hayafanyiki kiurahisi tu. Kwa kweli wanafanya mambo haya kwa kuona matukio yanayokuja siku kadhaa mbele yao. Hata hivyo, uwezo wao wa kufanya hivyo huwa unakikomo mara nyingi.

 

Mtu anayetazama nyakati ndiye mtabiri huyu wa mambo ya nyota. Watu hawa wote wametajwa kwenye andiko lililowapiga marufuku la Kumbukumbu la Torati 18:10 na wamewekwa kwenye kundi moja ambalo Mungu amelikataza na kulichukia. Mapepo huongopa kila mara kana kwamba umekuwa ni mchezo kwao. Na waganga wa ramli mara nyongi hufanya ujanja wakati watu wanapowaendea kutaka mashauri kwao.

 

Hata hivyo, Mungu anatumia njia nyingine ya kuamua jambo gumu na lenye utata linapotokea kwa kutumia Urimu na Thumimu. Kwa njia hii, Roho Mtakatifu aliweza kuwaambia Israeli mambo yao kwa njia iliyoruhusiwa kipindi kile ambacho Roho Mtakatifu alikuwa hajatumwa kwao bado na hata kwa watu wengine.

 

Inakubalika pia kwamba Mungu alipanga Ummbaji na kuona mwisho tangu mwanzo, na kuutangaza mwisho ule tangu mwanzo. Ametajwa kwenye Biblia kwa kupewa jina la Mwanzo na Mwisho, yaani Alfa na Omega akwanza na Waccepted that God planned the (tazama kwenye jarida la Mamlaka ya Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na Omega (Na. 229) [Arche of the Creation of God as Alpha and Omega (No. 229)]. Alimpa uweza wote Kristo katika kufufuka kwake kutoka kwa wafu.

 

Mapepo hawanauwezo wa kujua kila jambo bali wanafanya hivyo kwa kuangalia zama na na mweleo wa nyakati. Hawaoni kitu cochote zaidi ya kuona giza tu, bali wanabashiri. Wanatumia muda mwingi kwa kutudadisi na kututazama sisi, na kuyatafiti yale yanayofanyika ama kutokea Kanisani, na kutaka kujua linayoyafanya Jeshi lote la Malaika wa Mbinguni na kuona na kuyajua mambo yaliyotofunuliwa.

 

Tunatakiwa tuendelee mbele na imani yetu na ndiyo maana ubashiri umekatazwa kabisa isipokuwa unabii utolewao na manabii wa Mungu na kwa namna inayokubalika na Biblia tu ndio tulioruhusiwa.

 

Mungu huwatumia wateule wake ili kutilimiza kusudi lake.

 

Mungu anawafanya watumishi wake kuwa kama wenye “uso wa gumegume” kwa maadui wa Israeli, na mara nyingine kwenye makutaniko ya Israeli wenyewe.

 

Siku kadhaa kabla ya kuwepo kwa Kanisa, Mungu aliwatumia watumishi wake manabii ili wayafanye mapenzi yake. Manabii hawa na kazi zao zilijulikana mapema hata kabla hawajatungwa mamba kwa mama zao. Kama tunajuavyojua kwamba nyingi ya nabii za Agano la Kale zilikwenda kutimilika baada ya maelfu ya miaka iliyofuatia mbele yao, kama tunavyoona maandiko ya vitabu vya Mwanzo na Isaya ambayo yalimtabiri Kristo kwa undani zaidi, na kama alivyofanya Daudi kwenye kitabu cha Zaburi. Kitabu cha Ufunuo kinamwelezea Mwana kondoo aliyechinjwa na anatajwa kwa maneno “kabla ya kuwekwa misingi ya dunia”. 

 

Aina hii ya unabii haikuishia kwa Masihi tu, bali tunaona pia kwamba hata nabii Yeremia aliambiwa kuwa alijulikana hata kabla ya kuzaliwa kwake.

 

Yeremia 1:1-19 inasema: Maneno ya Yeremia mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani katika mji wa Anatothi katika nchi ya Benyamini. 2Neno la BWANA lilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda, 3pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa kutawala kwake Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa kwenda uhamishoni. 4Neno la BWANA lilinijia kusema, 5“Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako nilikujua, kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalumu, nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.’’ 6Nami nikasema, “Aa, BWANA Mwenyezi, sijui kusema kwani mimi ni mtoto mdogo tu.’’ 7Lakini BWANA akaniambia, “Usiseme, ‘mimi ni mtoto mdogo tu. Utakwenda po pote nitakapokutuma na kunena lo lote nitakalokuagiza. 8Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asema BWANA. 9Kisha BWANA akaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako. 10Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kung'oa na kubomoa, ili kuharibu na kuangamiza, ili kujenga na kupanda.’’ 11Neno la BWANA likanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?’’ nami nikajibu, “Naona tawi la mti wa mlozi.’’ 12BWANA akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba nimelitimiza.’’ 13Neno la BWANA likanijia tena, “Unaona nini?’’ Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka kikiwa kimeinama mdomo wake kuelekea upande wa kaskazini.’’ 14BWANA akaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote waishio katika nchi. 15Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,’’ asema BWANA. “Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya enzi katika maingilio ya malango ya Yerusalemu, watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka na dhidi ya miji yote ya Yuda. 16Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi, kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine na kuabudu kile ambacho mikono yao imekitengeneza. 17Jiandae! Simama nawe useme cho chote nitakachokuamuru. Usiwaogope wao la sivyo nitakufanya uwaogope wao. 18Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote, dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo. 19Watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa kuwa niko pamoja nawe nami nitakuokoa,’’ asema BWANA.

 

Mungu alimfanya Yeremia kuwa nabii, na alimjua hata kabla ya kutungwa kwa mamba yake tumboni mwa mama yake. Yeremia hakukusudia tu kuwaona wafalme wa kasakazini wakija na kuweka kambi zao kwenye kuta za Yerusalemu na kuweka viti vyao vya enzi pale, bali alikusudiwa aende kwenye mataifa ili akayaharibu na kuyaangusha chini. Mungu aliliweka maneno yake kinywani mwa Yeremia na kumlinda na kumwokoa. Pia alitakiwa awatabirie wafalme na mji ya Yuda. Pia Yeremia alitakiwa ayatangazie hukumu mataifa ya kaskazini na Israeli. Akiwa kama nabii wa Mungu, Yeremia alifanya mji wenye ngome na maboma, nguzo ya shaba, na kuta za shaba, dhidi ya nchi yote na dhidi ya wafalme na pia dhidi ya watu wa Yuda.

 

Mungu alimjua na kuibariki kazi yake na kumfanya kuwa nabii wa watu wake mwenyewe, na pia awe ni nabii wa Mataifa ya kipagani. Alipewa mamlaka ya kuharibu na kuvunja. Kanisa pia limepewa mamlaka haya katika Siku hizi za Mwisho.

 

Je, wakati gani basi ambao mtu anakuwa amejulikana tangu mwanzo na Mungu na kuwa kwenye mawazo yake yeye Mungu?

 

Paulo anatuambia jambo hili ambalo pia liliandikwa na Yohana.

 

Waefeso 1:1-23 inasema: Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu, Kwa watakatifu walioko Efeso walio waaminifu katika Kristo Yesu. 2Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi. 3Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo. 4Kwa maana alituchagua katika Yeye kabla ya kuumbwa ulimwengu ili tuwe watakatifu na bila lawama mbele Zake. 5Kwa upendo alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo kwa furaha Yake na mapenzi Yake mwenyewe. 6Kwa hiyo tunamsifu Mungu kwa huruma zake kuu alizotumiminia kwa sababu sisi ni wa Mwanae Mpendwa.


Mungu
huyu wa Pekee na wa Kweli ni Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Alituchagua sisi tewe wake hata kabla ya kuwekwa kwa misingi ya Dunia. Neno ambalo kwa kujibu wa (SGD 2602) linaitwa katabole au kuishusha dunia chini/ kwa maneno mengine ni kwamba Biblia inassema kwamba uweza huu wa kujua kila jambo alionao Mungu uneenea hadi kwenye kuyajuamambo yote ambayo sio tu ya Yesu Kristo, bali kwenye mlolongo mzima wa uzao wa Adamu, tangia wa kwanza hadi wa mwisho. Kupitia kwenye ndoa zao na chanzo chao cha uzawa wa mwanadamu na makosa yake yote ya kiuandishi na makosa yao ya kiuchaguzi. Huo ndio uweza wa Mungu. Mapepo wanapata maarifa haya kipindi ambacho kwao sio cha kuweza kujua mambo yaliyofichika, bali mara nyingi wanaona mambo yajayo kimakosa na kwa kubahatisha tu. Wanajaribu kuzuia kwa  kutumia aina mbalimbali ya vizuizi ili kuzuia tusizaliwe, na kuendelea kutuzuia tusibatizwe. Watajaribu kutufungia nira kwa jinsi isiyo sawasawa wanaposhinda kutuua au kutuzuia tusizaliwe.

 

Paulo anaendelea kuelezea kuhusu wokovu tulioupata kwa dhabihu ya Kristo.

7Katika Yeye tunao ukombozi kwa njia ya damu Yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema Yake 8aliyotumiminia kwa wingi, kwa hekima yote na maarifa yote. 9Naye alitujulisha siri ya mapenzi Yake sawasawa na uradhi wa mapenzi Yake, ambayo alikusudia katika Kristo, 10ili yapate kutimizwa katika wakati mkalimifu utakapowadia, yaani, kuvitia vitu vyote vya mbinguni na vya duniani pamoja chini ya kiongozi mmoja, ndiye Krsto. 11Katika Kristo sisi nasi tumepata urithi, tukiisha kuchaguliwa sawasawa na kusudi la Mungu, Yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na mapenzi Yake. 12Ili kwamba, sisi tuliokuwa wa kwanza kuweka tumaini katika Kristo, tupate kuishi kwa sifa ya utukufu Wake.

 

Mpango wa Mungu umefunuliwa kwetu kama unavyoendelea hadi kufikilia utimilifu wa nyakati. Kwa maneno mengine twaweza kusema, alitufunulia sisi Siri za Ufalme wa Mungu, kama ulivyofunuliwa kwa kupitia mpango wake. Mpango huo na makusudi yake vilifanywa na Kristo, na mpango wake ulifunuliwa kwetu sisi ili tuweze kuutumika ,pango wa Mungu. Mambo haya yanafanyika kwa muiibu sawa na mapenzi ya Mungu na sisi tulijulikana tangu mwanzo na kuteuliwa tuishi kwa utukufu wake.

 

Kwa hiyo, sisi tulichaguliwa kutoka mwanzo ili tuitwe na kufunuliwa Siri za Mungu na kutumikia Siri hizo sawasawa na maongozi ya Mapenzi ya Mungu, kama yalivyofunuliwa kwetu na Roho Mtakatifu kwa sifa za utukufu wake. Paulo anatuambia sisi tiliolisikia neno la kweli, kwamba tumepigwa mhuri wa Roho Mtakatifu.


13Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia Neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha kuamini, ndani yake mlitiwa mhuri, kwa yule Roho Mtakatifu wa ahadi mliyeahidiwa, 14yeye ndiye amana ya urithi wetu hadi ukombozi wa milki yake kuwa sifa ya utukufu Wake. 15Kwa sababu hii tangu niliposikia juu ya imani yenu katika Bwana Yesu na upendo wenu kwa watakatifu wote, 16sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, nikiwakumbuka katika maombi yangu.


Kwa hiyo, Roho Mtakatifu ni hakika ya urithi wetu. Ni shuhuda wa upendo wetu kwa ndugu zetu. Ni kwa sababu hii, maandiko yanasema:

17Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi. 18Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu Wake kwa watakatifu 19na uweza Wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno 20ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamketisha mkono Wake wa kuume katika mbingu, 21juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia. 22Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu Yake na amemfanya Yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, 23ambalo ndilo mwili Wake, ukamilifu Wake Yeye aliye yote katika yote.

 

Kanisa ni mwili wa Kristo, na kwa kupitia kwa Roho Mtakatifu, anatimiliza yote kwa yote. Na hatimaye, Mungu anakuwa ni yote katika yote. Tumepewa roho ya hekima na ufunuo kwenye maarifa ya Mungu ili tuweze kulijua tumaini tuliloitiwa, na ili tuweze kulielezea tumaini hilo kwa ufunuo wa Mungu. Mungu ametupa sisi uweza huo tulioitwa na kumini kwa mujibu wa nguvu na kazi za Mungu. Uweze huu umetimilizwa na Kristo ambaye Mungu amemfufua toka kwa wafu na kumketisha upande wake wa kuume. Na Mungu akamuweka Kristo juu ya falme na malmaka zote, na juu ya kila jina, sio katika ulimwengu huu tu bali katika ulimwengu ujao. Mungu aliyaweka mambo yote chini ya miguu ya Kristo na kumfanya awe ni kichwa juu ya mambo yote kwa ajili ya Kanisa, ambalo ni mwili au Hekalu la Mungu, Hekalu ambalo ndio sisi leo. Mungu alitujua sisi hata kabla hatujazaliwa na alitujua tangu mwanzoni na akatuita.

 

Je, inakuwaje basi kwa wale wanaishindwa? Mtume Paulo analielezea jambo hilo kwenye waraka wake kwa Warumi kwenye ile sura ya 8, anapozungumzia kuhuru Torati na roho wa rehema waliyopewa wale walioitwa.

Warumi 8:1-39 inasema: Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu ya adhabu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu, wale ambao hawaenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho. 2Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti.

 

Hii haina maana kuwa anaitangua Torati, bali anatuweka huru na matatizo tunayokutananayo tunapojaribu kushughulikia madhaifu ya kimwili tunaposhughulikia dhambi, ambayo tafsiri yake ni uvunjiu au uasi wa Amri za Mungu (1Johana 3:4).

 

3Kwa maana kile ambacho sheria haikuwa na uwezo wa kufanya, kwa vile ilivyokuwa dhaifu katika mwili, Mungu kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwanadamu mwenye mwili ulio wa dhambi na kwa ajili ya dhambi, Yeye aliihukumu dhambi katika mwili, 4ili kwamba haki ipatikanayo kwa sheria itimizwe ndani yetu sisi, ambao hatuenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho

 

Mambo yanayoikamilisha au kuambatana na Torati ni haki na inatimilika ndani yetu. Tunatembea tukiongozwa na Roho na sio kwa kuufuata mwili, nah ii ndiyo tofauti anayotufundisha Paulo anaposhughulikia suala la sheria na imani katika Roho.

 

5Kwa maana wale wanaoishi kwa kuufuata mwili huziweka nia zao katika vitu vya mwili, lakini wale wanaoishi kwa kufuata Roho, huziweka nia zao katika mambo ya Roho. 6Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani. 7Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui na Mungu, kwa maana haiitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.

 

Mtume Paulo anafafanua hapa nia iliyotuama kwenye mambo ya kimwili ni uadui na Mungu, kwa kuwa hayawezi kuzitii Sheria au Amri za Mungu, na ni kweli kwamba hayawezi kuitii Sheria za Mungu. Na hii ndiyo sababu na chanzo cha matatizo kwa wale wanaohubiri kwamba Sheria za Mungu zimetanguka na hazina umuhimu tena, au kwamba zimegongomelewa mtini wakati Kristo alipokuwa akisulibiwa (Wakolosai 2:14). “Uandishi wa sheria au kanuni” ulikuwa ni tangazo la kufutiwa deni au kitu kinachoitwa kwa Kiingereza “Chierographon” yaani kitu kinachosimama kinyume chetu kwa ajili ya dhambi zetu tunazozifanywa kwa kuzivunja kwetu sheria na amri za Mungu.

 

8Wale wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kumpendeza Mungu. 9Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. 10Lakini kama Kristo anakaa ndani yenu, miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, lakini roho zenu zi hai kwa sababu ya haki.

 

Kwa hiyo, wale waliohai Kanisani wamekufa kwa kuwa dhambi ni tendo la kusivunja au kuziasi sheria na amri za Mungu, bali wako hai kwa sababu ya Roho kwa njia ya neema.

 

Mungu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu. Ni Roho ndiye anayekaa ndani yetu akiwa kama Roho Mtakatifu wa Mungu. Huyu ndiye Roho anayetupa uzima kwenye hii miili yetu inayokufa yaani isiyoishi milele.

 

11Nanyi ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya Roho Wake akaaye ndani yenu. 12Kwa hiyo ndugu zangu, sisi tu wadeni, si wa mwili, ili tuishi kwa kuufuata mwili, 13kwa maana mkiishi kwa kuufuata mwili, mtakufa, lakini kama mkiyaua matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.

 

Kwa hiyo matendo ya mwili huleta mauti. Tunaishi kwa kuifuata Roho na kweli inaleta uzima. Wateule wale wanaoongozwa na Roho ndio wana wa Mungu. Wamepokea roho ya kufanywa wana.

 

14Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio watoto wa Mungu. 15Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa iwaleteayo tena hofu, bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambaye kwa Yeye twalia, ‘‘Abba, yaani, Baba,’’ 16Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kwamba sisi tu watoto wa Mungu. 17Basi ikiwa sisi ni watoto, basi tu warithi, warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo, naam, tukiteswa pamoja Naye tupate pia kutukuzwa pamoja Naye.

 

Sisi ni watoto wa Mungu na warithi pamoja na Yesu Kristo. Tunakuwa wana na wenye mamlaka kamili ya kimungu, yaani elohim na kama tulivyoruzukiwa kuwa na mamlaka hii ya elohim, kwa vile tunavyotaabika naye ili tuweze kutukuzwa naye. Kisha mtume Paulo anazidi kwenda ndani zaidi kwa kuelezea mchakato wa kutukuzwa huku.


18Nayahesabu mateso yetu ya wakati huu kuwa si kitu kulinganisha na utukufu utakaodhihirishwa kwetu. 19Kwa maana viumbe vyote vinangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa watoto wa Mungu. 20Kwa kuwa viumbe vyote viliwekwa chini ya ubatili, si kwa chaguo lao, bali kwa mapenzi Yake Yeye aliyevitiisha katika tumaini, 21Ili kwamba viumbe vyote vipate kuwekwa huru kutoka katika utumwa wa kuharibika na kupewa uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.

 
Matatizo na misukosuko ya dunia tunayokutananayo leo hayastahili kufikiria tunapoendelea mbele kwenye utukufu wa Mungu kwenye ahadi tulizopewa kama wateule na wana wa Mungu. Uumbaji na watu wote vitashirikishwa pia ahadi hizi tulizopewa sisi.

 

Viumbe wanalia kwa uchungu kwa ajili ya dhambi. Sisi tulio ni limbuko la Roho tunalia kwa uchungu pia kwa kadiri tunapongojea kufanywa wana wa Mungu, hali tutakayopewa wakati wa ufufo wa miili yetu kutoka kwa wafu kwenye Ufufuo wetu wa Kwanza.

 

22Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote vimekuwa vikilia kwa uchungu kama utungu wa wakati wa mwanamke kuzaa hata sasa. 23Wala si hivyo viumbe peke yao, bali hata sisi ambao ndio matunda ya kwanza ya Roho, kwa ndani tunalia kwa uchungu tukisubiri kwa shauku kufanywa wana wa Mungu, yaani, ukombozi wa miili yetu.

Ni kwa ajili ya tumaini la ufufuo usioonekana kuwa tumeokolewa kwa imani.

 

24Kwa kuwa tuliokolewa kwa tumaini hili. Lakini kama kinachotumainiwa kikionekana hakiwi tumaini tena. Je, kuna mtu anayetumaini kupata kitu alichonacho tayari? 25Lakini tunapotumaini kupata kitu ambacho hatuna, basi twakingojea kwa saburi.

 

Tunalingojea jambo hilo kwa uvumilivu na subira kuu. Tunapokuwa tukingojea hivyo, Roho anatusaidia kutokana na udhaifu wetu. Hatujui jinsi ya kuomba bali huyo Roho hutuombea. Mungu huangalia mioyo yetu kwa kupitia kwa Roho.

 

26Vivyo hivyo, Roho hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu kusikoweza kutamkwa. 27Naye Mungu aichunguzaye mioyo, anaijua nia ya Roho, kwa sababu Roho huwaombea watakatifu sawasawa na mapenzi ya Mungu.


Mapenzi ya Mungu ndiyo maelekezo ya Roho Mtakatifu anayeyachunguza mawazo yetu na mioyo yetu. Kwa hiyo, mambo yote hufanyika kwa ajili ya wema kwa wale wanaompenda Mungu na kuitwa kwa kusudi lake. Na huu ndio msingi wa fundisho na imani ya kujulikana na kukusudiwa tangu.

 

28Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi Lake. 29Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa Mwanawe, ili Yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30Nao wale Mungu aliotangulia kuwachagua, akawaita, wale aliowaita pia akawahesabia haki, nao wale aliowahesabia haki, pia akawatukuza.


Hapa tunaona mtiririko wa dhana hii ya kujulikana tangu mwanzo.

  1. Mungu aliufanya mpango wake wa Uumbaji.
  2. Wana wa Kiroha wa Mungu walumbwa.
  3. Wateule waishia maisha ya Kiroho wanapewa uchaguzi wakiwa kama ni sehemu ya mpango uliofunuliwa.
  4. Ummbaji wa Kimwili ulifanywa.
  5. Theluthi moja ya Malaika Mbinguni waliasi.
  6. Mpango wa kumfanya Kristo aje duniani na kufanyika kama Mwana Kondoo wa kuchinjwa tangu kuwekwa msingi wa dunia ulikamilika.
  7. Malaika Waasi wanatatiza mchakato wa uumbaji. Na hali inakuwa ni ya kile kinachojulikana kama Tohu na Bohu.
  8. Kristo anaingilia kati kwa maelekezo ya Mungu.
  9. Adamu anfanya dhambi.
  10. Lusiferi analaaniwa na kupewa kipindi kifupi cha miaka elfu sita akiwa ni Shetani na mshitakiwa ndugu zetu.
  11. Kristo anapewa taifa la Israeli kama sehemu ya mpango huu. Inakuwa ni milki yake kama sehemu ya ahadi waliyopewa kina Nuhu na Ibrahimu.
  12. Kila mtu ambaye alikuwa hajaishi bado anakuwa ni sehemu ya kusudi la Mungu lililowekwa kwenye nia na mawazo ya Mungu. Wateule wanajulikana tangu mwanzo huu.
  13. Kadiri muda unavyoendelea kujongea, kila mtu aliyekusudiwa na kuitwa anaitwa sawa sawa na mpango wa Mungu ulkivyokuwa kwa kipindi watakachoupata wokovu.
  14. Kwenye mchakato huu wa kuitwa wanafundishwa na kuandaliwa kwa kuhesabiwa haki kupitia kwa Roho Mtakatifu anayefanya kazi pamoja na Kristo Kanisani kama ilivyoelekezwa na kuhesabiwa haki na Mungu.
  15. Wakati huu wa kuhesabiwa haki na Kristo na Roho Mtakatifu akifanya sawa sawa na mpango wa Mungu, ndipo wanatukuzwa wakiwa ni wana wa Mungu kupitia Ufufuo kutoka kwa Wafu.

 

31Tuseme nini basi kuhusu haya? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani awezaye kuwa kinyume chetu? 32Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja Naye?

 

Wateule waliojulikana tangu kabla na kuchaguliwa na kuitwa, hawashindwi. Inagwaje amesema kwamba “waitwao ni wengi bali wateule ni wachache”. Mungu hakuwaita watu ili washindwe na wala hakuwaitia kushindwa. Baadi wameitwa lakini hawakuchaguliwa. Wanakuwa hawapo kwenye hesabu. Bali watafufuliwa kwenye Ufufuo wa Pili, ambao ni wakati wa Mungu alioufanya kwa wao kuitwa kwa mara ya kwanza.


33Ni nani atakayewashtaki wale ambao Mungu amewachagua? Ni Mungu mwenyewe ndiye mwenye kuwahesabia haki.


kwa hiyo, ni nai atakayetuhukumu ikiwa Mungu ndiye anayetuhesabia haki?

 

Na tena, ni nani anayetulaumu ikiwa Kristo ndiye ametuokoa kwa kufufuka na kupaa kwake? Hakuna aina nyingine ya maombezi zaidi ya kuomba kwa jina la Kristo.

 

34Ni nani basi atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa, naam, zaidi ya hayo, ndiye aliyefufuka kutoka kwa wafu, yuko mkono wa kuume wa Mungu, naye ndiye anayetuombea.

 

Na hakuna atakayetutenga na Kristo na upendo wa Mungu, isipokuwa ni sisi wenyewe tu kwa vile tunafanyapo dhambi, na kutushusha chini kipindi kile tu ambacho Mungu alikiona tangu mwanzo kuwa kinafaa kwa sisi kutuleta kwake.


35Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je, ni shida au taabu au mateso au njaa au uchi au hatari au upanga? 36Kama ilivyoandikwa : ‘‘Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.’’ 37Lakini katika mambo haya yote tunashinda, naam na zaidi ya kushinda, kwa Yeye aliyetupenda. 38Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, 39wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine cho chote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

 

Paula ameulezea mtaratibu wote unaotoa mchakato wa kujulikana na kukusudiwa tangu mwanzo na kazi ya Yesu Kristo nay a Kanisa katika mpango wa Mungu. Kwa jinsi hii hii Mungu aliufunua utaratibu wa Kristo aliyemfunulia Yohana kwenye kitabu cha Ufunuo.

 

Ufunuo 5:1-14 inasema: Kisha nikaona katika mkono Wake wa kuume yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, kitabu kilichoandikwa ndani na upande wa nyuma kikiwa kimefungwa kwa lakiri saba. 2Nami nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kuu, akisema, “Ni nani anayestahili kuzivunja hizo lakiri na kukifungua hicho kitabu?” 3Lakini hapakuwa na ye yote mbinguni wala duniani au chini ya dunia aliyeweza kukifungua hicho kitabu wala hata kutazama ndani yake. 4Nikalia sana sana kwa sababu hakuonekana ye yote aliyestashili kukifungua hicho kitabu wala kutazama ndani yake. 5Kisha, mmoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa uzao wa Daudi, ameshinda, ili kwamba aweze kukifungua hicho kitabu na kuvunja hizo lakiri zake saba.’’ 6Ndipo nikaona kati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne na miongoni mwa wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba za Mungu zilizotumwa duniani pote. 7Huyo Mwana-Kondoo akaja na kukitwaa kile kitabu kutoka kwenye mkono wa kuume wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi. 8Alipokwisha kukitwaa kile kitabu, wale viumbe wenye uhai wanne pamoja na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu yaliyojaa uvumba, ambayo ni maombi ya watakatifu. 9Nao wakaimba wimbo mpya wakisema: “Wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuzivunja lakiri zake, kwa sababu ulichinjwa na kwa damu Yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila, kila lugha, kila jamaa na kila taifa. 10Wewe umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, nao watamiliki katika dunia.’’ 11Nami nikatazama, nikasikia sauti za malaika wengi wakiwa wamekizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne, idadi yao ilikuwa kumi elfu mara kumi elfu na maelfu ya maelfu. 12Nao wakiimba kwa sauti kuu, wakisema: ‘‘Anastahili Mwana-Kondoo, Yeye aliyechinjwa, kupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na sifa!’’ 13Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi na baharini na vyote vilivyomo ndani yake vikiimba: ‘‘Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake Yeye aketiye juu ya hicho kiti cha enzi na kwa Mwana-Kondoo, milele na milele!” 14Wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amen!’’ Nao wale wazee ishirini na wanne wakaanguka kifudifudi wakaabudu.

 

Wateule wanafanyika kuwa ni wafalme na makuhani na watatwala hapa duniani. Hii ni kutoka kwenye kipindi cha utawala wa Yesu Kristo wa milenia, na utawala huu utaanzia Yerusalemu, na umekaribia sana kupambazuka kwa ajili yetu. Na hili ndilo tumaini lililoko kwetu na tunalolitarajia na kulingojea.

 

Ufunuo 13:1-8 inasema: Nami nikamwona mnyama akitoka ndani ya bahari. Mnyama huyo alikuwa na pembe kumi na vichwa saba, akiwa na taji kumi kwenye hizo pembe zake na juu ya kila kichwa kulikuwa na jina la kukufuru. 2Mnyama yule niliyemwona alikuwa kama chui, miguu yake ilikuwa kama ya dubu na kichwa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu zake, kiti chake cha enzi na mamlaka makubwa. 3Kimojawapo ya vichwa vya huyo mnyama kilikuwa kama kilichokwisha kupata jeraha la mauti, lakini jeraha hilo la mauti likapona. Ulimwengu wote ukashangaa ukamfuata huyo mnyama. 4Watu wakaliabudu lile joka kwa sababu lilikuwa limempa huyo mnyama mamlaka yake, pia wakamwabudu huyo mnyama na kuuliza, “Ni nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana vita naye?’’ 5Huyo mnyama akapewa kusema maneno ya kujisifu na kukufuru na kutumia mamlaka yake kwa muda wa miezi arobaini na miwili. 6Akafungua kinywa chake ili kumkukufuru Mungu, akilitukana Jina lake na mahali aishipo na wale wakaao mbinguni. 7Pia akaruhusiwa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda. Akapewa uwezo juu ya watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa. 8Nao watu wote waishio duniani watamwabudu huyo mnyama, yaani, wale wote ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo aliyechinjwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

 

Kumbuka kuwa majina ya hawa wateule yameandikwa, hata kabla ya kuwekwa misingi ya dunia, kwenye kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo aliyechinjwa. Hakuna anayemlazimisha Mungu. Na hakuna anayeweza kuingia kwa kutumia mlango wa nyuma. Wateule walijulikana na kukusudiwa tangu mwanzo na walichaguliwa na kuitwa na kisha wakahesabiwa haki na kutukuzwa. Na ndiyo maana wanaitwa wateule au waliochaguliwa.

 

Mara nyingi, wateule wanaonekana kuwa ni watu duni sana na ni watu wanaodharauliwa mno kwenye macho ya walimwengu.

1Wakorintho 1:26-31 inasema: 26Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa mlipoitwa. Kwa kipimo cha kibinadamu, si wengi wenu mliokuwa na hekima. Si wengi waliokuwa na nguvu, si wengi waliozaliwa katika jamaa zenye vyeo. 27Lakini Mungu alichagua vitu vipumbavu vya ulimwenguni ili aviaibishe vyenye hekima, Mungu alichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili aviaibishe vyenye nguvu. 28Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko, 29ili mtu ye yote asijisifu mbele za Mungu. 30Mungu ndiye chanzo cha uzima wenu katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakaso na ukombozi, 31ili kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana.”

 

Mungu huwaita waliodharauliwa na watu dsuni wa dunia hii kwa sababu mbili kuu: kwanza ni ili wasiweza (au wasoweza) kujivuna ama kujitukuza kwa kujiona kwamba ilikuwa ni kwa juhudi zao, kwa nguvu ama uwezo wao, au ni kwa ajili ya uzuri au bidii yao ndivyo vimewafanya wao kuwa miongoni mwa wateule, na sababu ya pili, ni kwamba watu hawa wenye hekima, wenye nguvu na wenye uwezo wa hapa duniani wataona aibu kufanya toba. Kama kuna jambo tunalopaswa kujivunia au kujitumuza nacho ni kama ilivyoandikwa kwenye (Yeremia.9:23-24; Zaburi 44:8). Kama kuna jambo lolote jema kwetu basi ni yeye atufanyiaye, na katu sio sisi; na ni Roho wa Mungu ndiye anayewatia nguvu wateule. 

Zekaria 4:6 inasema: …. “Hili ni neno la BWANA kwa Zerubabeli: ‘Si kwa nguvu, wala si kwa uwezo, bali ni kwa Roho yangu,’ asema BWANA Mwenye Nguvu.

 

Wateule au walioitwa wameitwa na kutolewa kwa Kristo kwa wakati wake muafaka, na wanaruhusiwa kuyavumilia jambo lolote linalowapasa kulivumilia kwa Imani na utukufu wa Mungu. Iwapo kama watalazimika kwenda utumwani, ndipo watakwenda utumwani. Wateule wanahukumiwa kwa matendo yao na wale wanaotafuta kuwadhuru wanapojaribu kufanya hivyo watakemewa.

 

Wale wanaotaka kuwaua, watauawa kwa namna hiyohiyo. Wale wanaotaka kuwaangamiza, wataangamizwa kwa jinsi hiyi hiyo, na wale wanaotaka kuwadhalilisha na kuwaaibisha, watapata aibu ya milele. 

 

Ufunua 13: inaendelea kwa kusema hivi:

 Ufunuo 13:9-9“Yeye aliye na sikio na asikie. 10Ikiwa mtu ni wa kuchukuliwa mateka, atachukuliwa mateka. Ikiwa mtu ni wa kuuawa kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye wito kwa ajili ya saburi na imani ya watakatifu. 11Kisha nikamwona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika dunia. Alikuwa na pembe mbili kama mwana-kondoo, lakini akanena kama joka. 12Akatumia mamlaka yote ya yule mnyama wa kwanza kwa niaba yake, naye akawafanya wote wakaao duniani kumwabudu yule mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. 13Huyu mnyama wa pili akafanya ishara kuu na za ajabu, hata kusababisha moto kushuka toka mbinguni kuja duniani watu wakiona waziwazi. 14Kwa sababu ya zile ishara alizokuwa amepewa uwezo wa kufanya kwa niaba ya yule mnyama wa kwanza, akawadanganya wakaao duniani. Akawaamuru wasimamishe sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi. 15Akapewa uwezo wa kuipa pumzi ile sanamu ya yule mnyama wa kwanza, ili iweze kusema na kuwasababisha wale wote waliokataa kuiabudu hiyo sanamu kuuawa. 16Pia alimlazimisha kila mmoja, mdogo na mkubwa, tajiri na maskini, mtu huru na mtumwa, atiwe chapa kwenye mkono wake wa kuume au kwenye kipaji chake cha uso, 17ili kwamba mtu ye yote asiweze kununua wala kuuza isipokuwa amekuwa na hiyo chapa, ambayo ni jina la huyo mnyama au tarakimu za jina lake. 18Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na ahesabu tarakimu za huyo mnyama, kwa maana ni tarakimu za kibinadamu. Tarakimu zake ni 666.

 

(kumbuka kwamba tarakimu hii ya 666 imefafanuliwa kwenye jarida la Sheria za Wafalme Sehemu ya III: Sulemani na Ufunguo wa Daudi (Na. 282) [Rule of the Kings Part III: Solomon and the Key of David (No. 282C)].

 

Mungu ameyaona mambo yote yanaliyokuwa hayanabudi kuja na mambo yote yaliyokuwa hayana budi yatokee kwetu. Anaruhusu mambo mengine ili tuwe ushuhuda kwa Imani yetu na kuwajaribu wale walio wateule wake hata kwa njia ya mauti.

 

Basin a uwe hodari katika Imani nawe utasimama mbele ya kiti cha enzi kwa sehemu yako katika siku za mwisho.

q