Makanisa ya
Kikristo ya Mungu
[298]
Vita Vya Warumi na Kunguka kwa Hekalu
(Toleo La 1.0 20060902-20060902)
Nabii Danieli alionyeshwa maono akionyeshwa
kipindi cha Majuma Sabini ya Miaka. Matukio ya juma la mwisho la miaka yalikuwa
ni maafa kwa Yuda na kwa Waedomu. Unabii huu unaweza kueleweka tu kuwa
unauhusiano na Hekalu. Wakristo wengi wameutafsiri kimakosa
E-mail: secretary@ccg.org
(Haki Miliki ©
2006 Wade Cox)
(tr. 2012)
Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa
kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani
yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo
atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote
atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo
zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya
sheria ya haki miliki.
Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye
wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org
Vita Vya Warumi na Kuanguka kwa Hekalu
Nabii Danieli anakitaja kipindi kijulikanacho kama cha Majuma Sabini ya Miaka ambacho kinahesabiwa kuanzia kipindi cha kutolewa amri ya kujengwa kwa Hekalu huko Yerusalemu hadi kile cha maangamizo yake mwaka 70BK. Historia hii imeelezewa kirefu kwenye jarida letu la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13)].
Danieli 9:25-27 inasema: 24Majuma sabini yameamriwa kwa ajili
ya watu wako na kwa ajili ya mji wako mtakatifu ili kumaliza makosa, kukomesha
dhambi, kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, kuleta haki ya milele, kutia
muhuri maono na unabii pia kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu
Tunajua kwamba mtiwa mafuta wa kwanza alikuwa
ni Nehemia, aliyeteuliwa na mfalme aende na kuwa liwali wa Yuda, na ndiye
aliyefanya kazi ya kusimamia ujenzi wa kuta na kulikarabati na kulirembesha kwa
mapambo Hekalu, kazi aliyoifanya akiwa na Ezra mwandishi. Hiki kilikuwa ni
kipindi cha utawala wa Artashasta II. Ezra alikufa mwaka 323KK, ni mwaka huohuo
ndio aliokufa Mfalme Iskanda Mkuu, na kazi ya kuyapitia na kuhakiki maandiko
ilihitimishwa na kufungwa mwaka 321.
Mwishoni mwa kipindi cha pili cha majuma sitini na mawili ya miaka kilishuhudia tukio la kuuawa kwa mtiwa mafuta mwingine naye alikuwa ni Yakobo (James) aliyekuwa ni Askofu wa Yerusalemu na ndugu wa Yesu Kristo. Baada ya kuuawa kwake Yakobo huko Yerusalemu, Kanisa liliachwa kwenye uongozi wa Simon (Simon mwana wa Yose) aliyekuwa ni binamu wa Yesu Kristo na mwana wa Mariamu na Klopa. Mariamu huyu alikuwa ni dada wa Mariamu mama wa Yesu Kristo. Na huyu Klopa alikuwa askofu wa Yerusalemu, kipindi kinachodhaniwa kuwa ni cha kati ya utawala wa Yakobo nduguyake Kristo (takriban mwaka 64BK) na inadhaniwa kuwa huyu Simon mwana wa Klopa na binamu ya Kristo (soma kitabu cha Hippolytus sehemu ya Nyongeza ya jarida la Kuanza Kwa Kanisa la Kikristo Nchini Uingereza (Na. 266) [Origin of the Christian Church in Britain (No. 266)].
Simon alichukua usimamizi wa Kanisa (baada
ya kifo cha Klopa) na walikimbilia mahala paitwapo
Maandiko yaliyo kwenye kitabu cha Danieli yanasema kwamba mfalme anayekuja atafanya agano thabiti na wengi kwa kipindi cha juma moja, na kwa kipindi cha nusu juma ataikomesha dhabihu na sadaka. Anaendela kwa kusema kuwa kwenye kipindi hiki cha chukizo la uharibifu, atakuja mtu atakayefanya uharibifu hadi kutakapotolewa amri itakayotangazwa na mharibifu huyu. Sentensi ya mwisho inaelezea kipindi muhimu ambacho hakihusiani na kipindi hiki cha Majuma Sabini ya Miaka ila inakiongelea kipindi ambacho mfumo huu unaoelezewa utakapokuwa umekomeshwa.
Kipindi hiki cha juma la miaka kinachoelezewa hapa ni cha kuanzia mwaka 62 hadi 69BK na mwaka wa mwisho ulikuwa ni ule wa 70BK.
Kilele chake kilikuwa ni mwishoni mwa miaka 490 ya Majuma Sabini ya Miaka kabla ya Pasaka ya mwaka 70BK, imeelezwa kwamba mnamo siku ya 1 mwezi wa Abibu, Jeshi la Warumi liliuzingira mji wa Yerusalemu. Huu ulikuwa ni Mwaka Mpya. Pia ulikuwa ni kipindi kamili cha mwisho wa “Miaka Arobaini ya Toba” walichopewa Yuda tangu Pasaka ya mwaka 30BK.
Juma la mwisho la miaka lilikuwa ni
miaka saba inayoendelea hadi leo. Katika
kipindi kile Kanisa lilikimbilia huko
Kwenye kitabu chake Emile Schürer (kinachoitwa
Historia ya Watu wa Jamii ya Kiyahudi
Kwenye Kipindi Cha Yesu Kristo, (History of the Jewish People in
the Age of Jesus Christ), Matoleo
ya. 1–3, ya T &T Clark, Rev. ed. Mwaka 1987) yanatoa historia hii kwa
kirefu sana na jarida hili linatuama kwenye maelezo ya Schürer na Josephus.
Liwali wa Yudea kipindi kile alikuwa ni
Gessius Florus (miaka ya 64-66BK). Alikuwa ni mtu muhimu na wa kuaminika sana
na maliwali wa Kirumi, na Josephus anashindwa kuwa na maneno ya kumelezea jinsi
alivyokuwa na uwezo mkubwa wa kimaongozi. Albinus alijulikana kuwa ni “mtu mwema
na mpenda haki” na alifananishwa naye. Albinus alikuwa anayashughulikia matendo
maovu kwa siri, bali Florus alikuwa anayaanika na kuyashughulikia hadharani
pasipo uficho, na hakuridhia matendo ya wizi kwa mtu yeyote, bali “aliiteka
miji yote na kuteketeza jamii zote zilizofanya hivyo. Lakini kadri wezi na
majambazi walipommshirikisha mambo
Kwa hiyo, Florus aliridhia
Tarehe hii ni ya muhimu
na siku inayofuatia, Florus aliwaamuru wananchi wawasalimie askari wa vikosi
viwili au wanajeshi wanapopita jiani wanaporudi nyumbani wakitokea Kaisaria. Wanajeshi
hawa walisalimiwa, ila waliwadharau wananchi hawa waliolazimishwa kwa amri ya
Florus. Ndipo wamanchi wakaanza kupiga makelele na kukashifu Florus kitendo
kilichowafanya wanajeshi waanze kuwaua hovyo raia hawa wakaingia mjini ambako
kulitokea mapigano ya mitaani mjini ambako watu wengi
Agrippa II alilelewa na kusomeshwa huko
Roma. Klaudio alimpa kiti cha ufalme cha mpwawake Herode wa
Katika kipindi cha maaasi, Agripa alikuwa
Agripa na Berenike walikuwa na hamu
Kisha Agripa alikwenda Misri kutoa heshima
kwa Wakuu wake wa kazi waliokuwa huko Misri ambao ni Tiberius Iulius Alexander.
Kisha Agripa alirudi haraka ambako yeye mwenyewe na dada yake walifanya juhudi
zao zote ilivyowezekana ili kuzuia machafuko haya na uasi visitokee. Walisimama
upande wa kupenda amani na tangu hapo na kuendelea wakasimama kidete kwenye
upande wa Warumi, na matokeo yake walipoteza idadi kubwa ya miji. Yeye na
wanajeshi wake walikuwa wanaelekea kufanya
Nero alifariki tarehe 9 Juni 68BK. (
Ndipo Tito alirudi kwa baba yake Vespasian,
na Agripa akaenda Roma. Baada ya Verspasian kuchaguliwa kuwa mfalme na Kundi la
watu waliotoka Misri na
Baada ya vita, mipaka ya nchi yake
iliongezwa, na mwandishi Josephus aliandika kuwa Maeneo haya ni ya pande za
Kaskazini mwa
Baada ya vita mwaka 75BK, Agripa na Bernike walifika Roma ambao Bernike alizirudia kazi zake alizokuwa amezianza alipokuwa na Tito katika Palestina. Malkia wa Kiyahudi aliishi na Tito katika Palestina wakati kwamba Agripa walipata upendeleo kwenye cheo cha uhakimu. Ilitarajiwa kuwa wangeoana lakini jinsi walivyoipokea hali hii huko Roma ilikuwa ni kinyume kabisa kiasi kwamba Tito alilazimishwa amfukuze na kumrudisha alikotoka.
Mwaka wa Yubile ulikuwa ni 77BK.
Kuteketezwa kwa mji wa Yerusalemu kulimalizika mwaka 70BK na Warumi walichukua
mamlaka na udhibiti wote kwenye kipindi hiki cha Sabato ya
Baada ya kifo cha Vespasian, Bernike alirudi
Roma tarehe 23 Juni 79BK, lakini Tito akiwa
Utawala wa Agripa wa ile dola yake
iliyopanuliwa ulidumu hadi ukaishia mwaka 86BK, wakati aliponyang’anywa
makoloni yaliyokuwa huko Uyahudini. Josephus anaelezea kisa hiki kwenye kitabu
chake kiitwacho Antiquities (xvii, 2, 2 (28)), akisema kwamba hatimaye
haawakuwa na sehemu yoyote kwenye dola hii. Anaonekana kuwa alitawala hadi
kipindi cha utawala wa Domitian. Schürer anadhani kwamba alikufa katika miaka
ya 92/93BK, na kwamba Photius sio mtu wa kutegemeka tena ilipofika miaka hii ya
100BK (soma ukurasa wake wa 481). Akiwa hata hana mototo mmoja, ufalme wake
haukuishikamana na majimbo ya
Vita hivi vya Warumi viliishia polepole tangu mwaka 66BK hadi 74BK, lakini nabii zilizotolewa zinahusiana na kuteketezwa kwa Hekalu na kuondolewa kwa mfumo wa kibinadamu, jambo ambalo liishia mwaka 70BK.
Maandalizi ya Vita
Agripa aliyanya matumizi ya mara kwa mara haki ili kuwateua na kuaweka Makuhani Wakuu, na aliwaweka na kuwateua Makuhani Wakuu hadi kilipofika kipindi cha maasi ya mwaka 66BK.
Katika kurudi kwao kutoka
Ndipo waasi walipoiteka na kuikalia
Kiwango cha uasi kilikuwa ni kukubwa
Katika uchochezi alioufanya Elieza mwana wa Anania Kuhani Mkuu, sadaka ya daima iliyokuwa inatolewa kilasiku na mfalme ilisimamishwa na hakuna tena sadaka kutoka kwa Mmataifa iliyoruhusiwa kuletwa. Hii ilikuwa ni rejea ya maombi yaliyofanywa na Sulemani alipomuomba Mungu wakati wa uzinduzi wa Hekalu, na kwa kufanya hivyo kulikuwa kunamaanisha tangazo la kuvunja mkataba wa muafaka walioufanya kati yao, yaani Israeli na Mungu kuhusu Wamataifa. Jambo hili limeelezewa vema kwenye jarida la Amri za Wafalme: Sehemu ya II: Sulemani na Ufunguo wa Daudi (Na. 282C) [Rule of the Kings: Part III: Solomon and the Key of David (No. 282C)] na iliwapasa kufikia mwenye tamati ya mbali.
Tendo la kuisimamisha na kuikataa sadaka ya mfalme lilikuwa na maana ya kufanya tangazo la wazi na la makusudi kwa mfalme la kusudio lao la kuasi dhidi ya utawala wa Kirumi. Juhudi zote zilizofanywa za kuwashawishi kutofanya hivyo viongozi wao, kuhani mkuu na Mafarisayo zilishindikana.
Baraza la amani lililojumuisha Makuhani wa vyeo vya juu, Mafarisayo maarufu na
Wahasmonia (Hasmoneans), yaani watu wanaohusiana na kuingia bila kizuizi kwenye
Nyumba ya Herode, pia walishindwa kuinusuru hali hii. Walikimbilia kufanya
juhudi za kuwalazimisha na kumsihi Mfalme Agripa ili awasaidie. Akatuma kikosi
cha askari 3,000 kilichoongozwa na makamanda wawili, yaani Dario na Philippus,
na kwa msaada wao walifanikiwa kushinda na kudhibiti Mji wa Juu wakati Waasi
walishinda na kuchhukua udhibiti wa sehemu ya Kilima cha Hekalu na sehemu ya
Chini ya Mji. Hatahivyo, majeshi ya mfalme walilazimishwa kuhamia kwenye Mji wa
Juu, na kwa kujilipiza kisasi waasi waliyachoma moto majumba ya kifahari ya
Kuhani Mkuu Anania, Agripa na Bernike. Siku chache baadae, mwezi wa Lous au Abu
sawa na katikati ya miezi ya Julai/Agosti. Waasi waliikamata ngome ya Antonia
na kuanza kuizingira sehemu ya juu ya jumba la Herode mahali ambapo majeshi ya
kulinda amani yalikuwa yamekimbilia.
Uwezekano wa kuwazuia haukuwepo na
wanajeshi wa Agripa walipewa hifadhi. Watu wa jamii ya daraja la juu wa Kirumi
walikimbilia kujificha kwenye maeneo matatu yaliyokuws ns ngome zenye minara
kwenye Ikulu ya Herode (kw mujibu wa Hippicus, Phasael na Mariamne). Majumba ya
kifahari yaliyobakia yalichomwa moto mnamo siku ya 6 ya mwezi Gorpiaeus (Eluli). Siku iliyofuatia Kuhani Mkuu Anania
alikamatwa kutoka mafichoni pake na akauawa. Kikosi cha wanajeshi wa Kirumi
chenye minara mitatu kililazimika kusalimu amri. Wanajeshi waliahidiwa kulindwa
na kuwa salama. Hatahivyo, waliposhusha chini mikono
Hivyobasi, Yerusalemu ukawa umeshinda.
Kwenye miji mingineya Yudea na Galilaya vita ya umwagaji mkubwa wa damu
iliendelea. Huku Wayahudi wakishinda kwa kuwauwa Wamataifa na pale Wamataifa
walipopata ushindi waliwauwa kwa kuwachinja Wayahudi. Josephus anasema kuwa madhara
ya maasi yalitokea Yerusalemu yalienea mbali hadi kufika maeneo ya mbali huko
Baada ya kipindi
kirefu cha kuelewa kilichoe; ezewa kuwa ni cha maandalizi, Cestius Gallus,
liwali wa Syria, alipelekwa Yudea ili akakomeshe maasi.
Akarnda na askari wa
Kikosi cha 12 na wanejeshi wanaume wapatao elfu mbili kutoka kwenye vikosi
vingine, na vikosi vingine sita na vikosi vine vya askari wapanda farasi pamoja
na idadi kubwa ya wanajeshi wa akiba walipelekwa kwa agizo la wafalme rafiki
akiwepo Agripa.
Majeshi yalioongozwa
na Gallus yaliondoka
Wayahudi
waliishambulia kambi ya Beth Horon na Warumi walikuwa kwenye hatari kubwa
lakini hatimaye mambo yakawageukia Wayahudi.
Kisha Gallus akahamia
eneo la karibu na Yerusalemu na kuweka kambi yake kwenye Mlima Scopus, ulio na
umbali wa takriban viwanja saba kutoka Yerusalemu, siku ya 26 mwezi wa Tishri.
Siku nne baadae, yaani siku ya 30 mwezi Tishri (Hyperberetaeus), aliiteka na
kuvidhibiti viunga vya upande wa kaskazini mwa Bezetha bila kukutana na
upinzani wowote, na wakauchoma kwa moto.
Hatimaye akajaribu
kuushambulia Mlima wa Hekalu bali akashindwa na akaamua kuuachia na kuondoa
majeshi yake. Josephus haelezei ni kwa nini alifanya hivyo. Huenda ni kwa
sababu hikuwa amejiandaa vema na alikuwa chini ya viwango vya kufaa kufanya
mashambulizi na kuuzingira.
Kisha alipumzika
kwenye bonde lililoko karibu na Beth Horon, ambako Wayahudi walikwenda na
kumzingira kabisa na kumshambulia kwa mashambulizi mabaya
Washindi walirudi
Yerusalemu siku ya 8 ya mwezi wa Dius, au Marcheshvan au Buli.
Baraza la usuluishi
la wapenda amani sasa walisalimu amri kabisa na kuamua kujiunga na waasi. Mbinu
za kimaandalizi zilianza zilizolenga kuwafanyia mashambulizi ya kujibu mapigo
ya Warumi. Kundi maarufu Hekaluni lilimchagua Joseph ben Gorion na Kuhani Mkuu Ananus
kuamuru mkakati wa kuulinda mji wa Yerusalemu.
Yesu bin Safia na Elieza
bin Anania (wote wawili wanatoka kwenye ukoo wa Kuhani Mkuu) walienda Idumea kuamuru
na kuusimamia mkakati wa kuulinda. Karibu kila moja miongoni mwa maeneo haya
kumi na moja au maeneo ambayo kwayo Yudea ilikuwa imegawanywa ilimpokea kamanda
wake. Yosufu bin Mathias, mwanahistoria wa siku za mbele, alitumwa kwenye
kamandi ya Galilaya.
Hii ilikuwa ni
komandi ngumu, kwa kuwa Warumi wakishambulia bilashaka watafika hadi huko
kwanza wakiwa na kikosi kamili cha majeshi ya Kirumi dhidi ya raia hawa
wasiopata mafunzo maalumu. Kamandi hii iliashiria kuwa na umaarufu fulani kwa
Josephus kwenye jamii bora na ya kikabaila ya Yudea. Na ingawa hakufundishwa
hili, aliikubali na kuianza kazi hii kwa moyo wa ujasiri na furaha.
Aliweka utaratibu wa
kiserikali huko Galilaya pamoja na muundo wa baraza la kidini maarufu
Baraza la watu saba liliundwa
kila kwenye mji ili washughulikie kusuluhisha mambo au kuamua penye mabishano.
Alipaswa kubomoa
Jumba la Kifahari la Tiberio, lakini waasi walikuwa wameshafanikiwa tayari
kufanya hivyo. Aliizungushia kuta na kuijengea ngome moji yote mikubwa ya
Galilaya kwa kuiwekea ulinzi zaidi na kuihakikishia usalama wake. Miji hiyo
ilikuwa ni Jotapata, Tarichea, Tiberias, Sepphoris, Gischala, Mlima Tabor, na
Gamala ulioko Gaulanitis na sehemu nyingine ndogondogo. Aliwaita watu 100,000
wanaume na kuwafundisha mitindo asilia ya Kirumi.
Umahiri wa Josephus na
umakini wake wa kuandaa vita ulipigwa kumbo na kupingwa na John wa Gischala, ambaye
alikuwa ni mpinzani wa Warumi mkubwa sana katika Galilaya.
Josephus hakuwa
amejiandaa vizuri kufanya upinzani na katika mji wa Tarichea, ambako Josephus aliweka
makao yake kulikuwa na machafuko makubwa
Hali ya uchungu wa
kisasi na kutomwamini tena Josephus vilionekana kuwa dhahiri. Maisha ya
Josephus yalitishiwa na kwa kutumia tu mbinu za kijanja na unyenyekevu
vilimsaidia kuepukana na hatari. Hatimaye, akiwa huko Tiberias alilazimika
kuwakimbiza na kuwafukuza wauaji waliotumwa wakamuue na mtu aitwaye John wa
Gischala.
Hatimaye, Gischala aliitangua
ahadi ya kukutana aliyoifanya Josephus, na jeshi la askari 2,500 likiongozwa na
makamanda maarufu wanne walitumwa waende Galilaya kwa lengo hili. Hivyo basi,
Josephus akafanikiwa kuitangua marufuku iliyowekwa na wajumbe wanne waliitwa
tena. Walipokataa kuja ndipo alikamatwa na kurudishwa nyumbani.
Wakazi na wenyeji wa Tiberias
waliokuwa wanaendelea kuasi, walinyamazishwa kwa lazima. Mji ukaasi siku chache
baadae mkakati ulifanywa na Agripa na Warumi ambao ulikomeshwa baadae kwa
kutumia mbuinu chafu na hila. Kwa mujibu wa Josephus, mji huu ulikuwa na wakazi
waliokuwa ni watu wenye damu mchanganyiko na baadhi
Mji wa Yerusalemu ulikitumia
kipindi hiki cha kusimamisha mapigani kwa kuwafundisha vijana matumizi ya
silaha na kutengeneza silaha kuzisambaza na kuwafundisha jinsi ya kuvizia na
kuteka. Katika kipindi cha Pasaka ya mwaka 67BK mji ulikumbwa na maafa makubwa kwa
mara ya pili kwa mashmabulizi makubwa kuliko yale ya kwanza.
Nero alikuwa huko Akaya
wakati habari za kushindwa vita kwa Cestius Gallus zilipomfikia. Akaihamisha
komandi ya kukandamiza na kukomesha uasi wa Wayahudi kwa Vespasian aliyekuwa na
uzoefu na kazi hii. Baada ya kushindwa kwake vita, Gallus alikufa kipindi
kifupi tu baadae.
Mchakato huu ulianza
kipindi cha kampeni cha majira ya baridi.
Vespasian na majeshi
yake wakaenda huko Antiokia na kuweka kambi la askari wake huko na akamtuma
mtoto wake Tito aende
Mara tu mwishoni mwa majira
haya ya baridi, alienda Ptolemais mahali alipokwenda kumngojea Tito, lakini
kabla Tito hajawasili, wajumbe wa amani kutoka Sepphoris ya Galilaya na kuomba askari
wa Kirumi waje kulinda amani ya mji. Ndipo Vespasian alifanya haraka kwenda na
kikosi cha askari 6,000 kilichokuwa kinaongozwa na Placidus ili kikaulinde mji
wa Sepphoris. Na pasipo hata kupiga mbiu ya kuhadharisha watu, Warumi waliuchukua
mji huu muhimu
Kipindi alipofika
Tito, alikuta wanajeshi wa komandi ya Vespesian wameigawanya kwenye makundi matatu
yanayojitegemea kama ifuatavyo: Komandi ya 5, 10, na 15; vikosi vilivyokuwa na divisheni
ishirini na tatu za nyongeza vikosi sita vya wapanda farasi na askari wengine
wa ziada walioongezwa na Mfalme Agripa, pamoja na Antiochus wa Commagene,
Soaemus wa Emesa, na Malchis II wa Nabataea, ambao jumla yao walikuwa ni jesgi
la wanaume 60,000.
Vespasian akaondoka
kutoka Ptolemais na kuweka kambi yake kwenye mpaka na Galilaya.
Wanajeshi wa Kiyahudi
yakiongozwa na Josephus waliweka kambi
Hari ya kushinda vita
iliwaishia wanajeshi wa Kiyahudi hata kabla wanajeshi wa Kirumi hawajajitokeza,
na wakatawanyika. Upande wa nyanda za chini wa Galilaya ukaangukia mikononi mwa
Warumi pasipo hata kutumia upanga hata mmoja.
Josephus alilazimika
kwenda kupumzika huko Tiberias. Na sasa Vespasian akaifanya kazi iliyokuwa rahisi
Josephus akatuma
ujumbe akiwaasa wakazi wa Yerusalemu watafute
Sehemu kubwa ya
wanajeshi wa Josephus walikuwa huko Jotapata. Josephus akasema kwamba Warumi
watajenga barabara itakayotumiwa na askari wapanda farasi watakapokuja, jambo
ambalo walilifanya kweli kuanzia siku ya 17 hadi 21 mwezi wa Iyari. Inaaminika
kuwa Josephus alifika huko siku ya 21 mwezi wa Artemesius (Iyari) mwaka 67BK. (Muda
huu ulikuwa ni mwishoni mwa maadhimisho ya Pasaka ya Pili ambayo ingefuatiwa
pia na Idi ya Mikate Isiyotiwa Chachu). Vespasian alifika kwenye mji huu jioni
ya siku iliyofuatia. Jesephua anasema kuwa mzingiro huu ulidumu kwa kipindi cha
siku 47 (B.J. iii, 7, 33 na 8, 9 na yaliishia siku ya 1 Panemus (B.J.
iii, 7, 36).
Josephus anasema wazi
kabisa kwamba mji ulitekwa siku ya 1 Panemus. Pia anasema wazi tu kuwa kipindi
cha kuzingirwa kwake mji huu kilidumu kwa siku 47. Anaeleza pia kwamba kazi ya
ujenzi wa barabara ilichukua siku nne kabla ya kuwasili kwake siku ya 21 mwezi
wa Iyari. Kwa hiyo, vikosi zaidi vya Warumi vya kuja kuulinda mji na kuuzingira
viliwasili siku ya 14 mwezi wa Iyari au katika kipindi cha maadhimisho ya
Pasaka ya Pili. Mara tu baada ya barabara kujengwa, mkakati wa kuuzingira mji
ulipaswa uenndelezwe na usonge mbele na watu wa Vespasian. Sababu ya kufanya
maadhimisho ya Pili ya Pasaka mwezi wa Iyari kwa operesheni zote mbili kuu ilikuwa
ni kuwafanya wasiwapoteze wanafunzi wa Biblia. Mungu anaruhu hali hii itokee ili
ashughulike na watu wa Yuda.
Mji wa Jotapata ilitekwa
na kutwaliwa siku ya Mwandamo wa Mwezi wa Nne (Tamuzi) mwaka 67BK. Ulikuwa ni
mji uliozungushiwa kuta mande zote katika Israeli tangu kipindi cha Yoshua (
Mashambulizi ya
kwanza yalilipuka huko. Kisha Warumi wakaanza kufanya utaratibu wa kuuzingira. Josephus
anaelezea uzingiraji huu kwa undani kwenye kitabu chake cha Vita vya Wayahudi (Wars of the Jews)
Hatimaye, licha ya
kutumia mbinu za kijanja na hata uwongo na hila za kutuma watu wakiwa wamevaa
ngozi za wanyama wanapikwenda kuchukua mahitaji yao saa za usiku, na kutumia
mafuta ya oili chafu iliyochemshwa ya moto na uwatu wakivitumia kama vifaa vya
kutimiza kwenye mkakati wao wa kuwazingira na kuweka utelezi kwenya madaraja na
kuwapa askari zana za kujikinga au ngao, na kuweka mashujaa wa kuwazuia,
havisaidia bali hatimaye mji ulianguka. Wataalamu wa kutafuta na kufukua miili
walioshughulika kwenye uzingiraji huu walimuona hata Vespasian mwenyewe akiwa
amejeruhiwa. Mji ulisalitiwa na hali ya uhitaji na maafa yaliyogundulika kuletwa
na wakazi asilia waliokula njama na Warumi.
Walinzi waliochuku zamu zao asubuhi walikaa macho hadi asubuhi na
hawakulala. Ndipo Tito akiwa na jeshi dogo akaingia mjini humo kwa werevu na mbinu
kipindi cha mabadilishano ya zamu ya asubuhi na wakawaua walinzi na mji ukashindwa
kuwazuia washambuliaji waliokuwa wanashambulia kutoka nje.
Wanaume wengi
waliuawa na kufichwa kwenye mapango. Waliuawa kwa kuchinjwa na Warumi au
walijiua wenyewe. Kwenye vitabu vyake Josephus anasema kuwa yeye alinusurika
kwa kile kinachosemekana kwamba alipigiwa kura kwa kudhaniwa alikuwa ni mtu wa
mwisho miongoni mwa wale waliojiua wenyewe waliokutwa mle pangoni, na kudhaniwa
kuwa huyu aliamua kujisalimisha. Alifanya mambo yakr kana kwamba alikuwa nabii na
ilithibishwa kwamba yeye ndiye aliyetabiri hapo kabla kipindi ambacho mzingiro
ule utachukua. Josephus alitabiri kwamba Vespasian ndiye akatayerithi kiti cha
ufalme, na kwamba yeye atayetawala kwa huruma nyingi.
Warumi walifanya
maangamizi makubwa mno kiasi kwamba waliwaua wanaume wote na kuwaacha mateka
wachache tu na waliwaacha hai watoto wakiume wachache na mama zao wakiwa
Tarehe 4 Panemus,
Vespasian alienda Kaisaria akipitia njia ya Ptolemais na kuwaruhusu wanajeshi
wake wapumzike wakati huu anapokwenda Agripa iliyoko Kaisaria Filipi. Walikuwa
na kipindi kirefu cha kusherehekea kilichodumu kwa muda wa siku ishirini. Kisha
Tito akaamuru kikosi cha wamajeshi kutoka Kaisaria Maritima na wakaelekea huko Tiberias.
Mji huu ukasalimu amri na ukatawaliwa kwa huruma kwa heshima ya Agripa.
Kisha wakauelekea mji
mwingine wa Tarichea. Kwa nguvu na kujiamini kwingi, Tito aliuchukua mji huu
mwanzoni mwa mwezi wa Gorpiaeus au Eluli.
Kwa hiyo, Miandamo ya
Mwezi na maadhimisho ya Pasaka ya Pili yanamaana
Hadi kipindi hiki tunaona
kuwa ni Galilaya na Gischala tu na Mlima Tabori (Itabyrion) ndizo zilkuwa
zimebakia hadi kipindi hiki zikiwa na maboma na kuzungushiwa kuta imara na
muhimu za Gamala iliyoko Gaulanitis.
Hatimaye Warumi
waliushambulia Gamala baada ya mji ule, na mwanzoni walionekana kufanikiwa na
wakaingia mjini. Hata hivyo, mashambulizi ya kujilipiza yalikuwa yamepangwa na
yakawalenga Warumi kwa kiasi kikubwa
Mnamo siku ya 23 mwezi
Tishri (Hyperberetaeus), ndipo hatimaye mji wa Gamala ulianguka. Na Mlima
Tabori pia ulitekwa na kikosi cha askari kikapelekwa huko kipindi hiki cha kuuzingira
mji huu wa Gamala.
Tito akatumwa kwenda Gischala
akiwa na kikosi cha askari wa deraya 1,000. Mji ukasalimu amri kwa Tito siku ya
pili yake. Yohana na Uzelote wake wakalikimbia na kujiepusha usiku wake na
wakakimbilia Yerusalemu.
Vespasian akawachukua
wanajeshi wake na kuwapeleka kwenye jumba la mapumziko ya majira ya baridi.
Yeye mwenyewe pamoja na Vikosi vyake Kombania ya 5 na 15 waliweka kambi
Kwa hiyo, majira ya
baridi ya mwaka 67BK, pande zote za kaskazini mwa Palestina ulikuwa mikononi
mwa Warumi.
Viongozi wa waasi ndio
walioanza kuonekana kuwa ni viongozi wanaoyumba yaani kuwa mguu mmoja ndani na
mwingine nje au waliokuwa ni sehemu ya wale wanaotafuta muafaka. Wale wenye
msimamo mkali wa kutetea na kujivunia utaifa walitwao Wazawa au Wazelote (Zealots)
wakaanza kuwalaumu kwa kusababisha maafa makubwa vile na kusalimu amri mwanzoni
kabisa mwa vita. Wakalaumiwa kwa kutoiongoza vita kwa kwa umakini na umahiri wa
kutosha. Mawazo haya na lawama zote hizi zilionekana kuwa ni za kweli na za
msingi.
Kisha Wazelote hawa
wakaanza kuchukua hatamu za uongozi na kuhitilafiana na viongozi wao wa siku za
nyuma. Hawakupenda kuonyesha utii tena kwa moyo wao wote kwa viongozi wao hawa
na hatimaye vita kuu vya umwagaji damu mkuu vya wenyewe kwa wenyewe vilifuatia
na kupiganwa kuanzia majira ya baridi ya mwaka 67-68BK.
John wa Gischala ndiye
alikuwa kiongozi wa watu hawa wa mrengo wa Kizelote. Alinusurika na kuponyoka
na kukimbia na wanajeski wake hadi Yerusalemu kwenye kipindi cha mwanzoni mwa mwezi
Novemba. Aliwakusanya vijana na kuwajenga moyo wa vita na kuwashirikisha
matendo makuu anayokwenda kuyafanya. Manajeshi na wapenda vita wa mrengo huu wa
Kizelote waliokuwa wamekimbilia pande za kaskazini wakamiminika mjini Yerusalemu
pamoja na wale wa kujitolea waliotoka kila mahali. Mara, Wazelote hawa
wakaudhibiti mji wa Yerusalemu.
Mkakati wao wa kwanza
ulikuwa ni kuwaondoa wale wote wanaodhaniwa au kuonekana kuwa wanawapenda au
kuwapendelea au kujikomba kwa Warumi. Idadi kuwa ya watu maarufu akiwemo Antipas
kutoka kwenye jamii ya Nyumba ya Herode walichukuliwa kuwa ni watu wa aina hii
na waliuawa gerezani.
Kuhani Mkuu mwingine
alichaguliwa kwa kupigiwa kura
Kuhani Mkuu aliyechaguliwa
Phannias, kutoka Apthia (pia alijulikana
Viongozi
walioshikilia madaraka ya Yerusalemu, yaani Gorion ben Joseph, Simon ben
Gamaliel Farisayo, na Makuhani Wakuu wawili, yaani Ananus ben Ananus na Jesus
ben Gamaliel walijaribu kujiondoa na kujitenga mbali na baraza la Wazelote kwa
nguvu. Na kwa kuwa walikuwa wachache walilazimishwa kuingia kwenye uwa wa ndani
wa Hekalu na kwa kuwa hakuna mtu aliyetaka kuleta ghasia kwenye malango
matakatifu wakafungiwa ndani.
Wazelote hawa
wakatuma ujumbe kwa wapenda vita wa jamii ya Idumeans. Hawa ni wana wa Esau
waliokuwa wamepigwa na kushindwa vita na John Hyrcanus na wakaongoka na kuingia
dini ya kiyahudi kipindi cha karne mbili na nusu zilizopia. Asilimia kubwa ya
wakazi wa Yudea walikuwa ni hawa wa jamii ya Idumaean, na walikuwa ni Wakulima
na Wafugaji (Na ni Hasmonaeans) wao wenyewe.
Hawa Idumeans wakaja
wakitokea kwenye kuta za Yerusalemu bali hawakuruhusiwa waingie ndani. Kulipofika
majira ya usiku, vurugu kubwa ilitokea iliyotumiwa
Walifikia pia kwenye
kiwango cha kulazimisha kuweko kwa majaribio ya kawaida ya kuhalalisha na
kuwapa heshima wauaji hawa, lakini mahakama ilitoa hukumu ya kuwafutia
mashitaka washitakiwa akina Zacharias ben Baruch, na ndipo Wazelote hawa
wakamuua kwa madai kwamba “sisi tuna kura zako pia” (kitabu cha Schürer, ukurasa
wa 497-498).
Hawa Idumeans kwa
sasa wakagundua kuwa kile kinachoitwa hali tete ya kiusalama ilikuwa ni
kisingizio tu cha kuanzisha sheria zinzokusudia kuwabana wananchi. Hatimaye
wakaamua mujiondoa.
Wazelote wakaendelea
na utawala wao wa kiimla na kigaidi na usiojizuia. Wakamuua Gorion na sehemu ya
waliojiuliza wafenye nini sasa, na viongozi hawa walikuwa wanawatishia kuwa
hakukuwa nakizuizi tena. John wa Gischala akawa ni mtu mwenye kuogofya na tishio
mjini Yerusalemu.
Jinsi Kanisa la Pella Lilivyolindwa
Kanisa lilikuwa
limeshaonywa kuhusu maafa haya kupitia unabii wa Danieli. Kabla ya kuzuka kwa
vita, na baada ya kifo cha James, chini ya Simon ndugu yake Kristo lilikimbilia
mahali paitwapo
Eusebius ananukuu
aliyoyaandika Josephus (kwenye kitabu chake cha HE III, V-VI) akielezea kwa
undani matukio ya kutisha waliyofanyiwa watu mjini. Kanisa likalindwa na mambo
ya kutisha ya Wazelote na kipindi cha kutisha cha njaa ambacho kiliharibu mji
na muundo wake wa kihari.
Ndipo majenerali wa
vita wa Kirumi wakaona umuhimu kwamba mji wa Yerusalemu ulipaswa kushambuliwa
haraka
Vespasian aliona kuwa
vi vema na busara kuuacha mji uendelee hadi kiasi kibaya na mambo
Mungu ameupa mji wa Yerusalemu miaka 40 ya kutubu kwa mujibu wa unabii wa Ishara ya Nabii Yona, na walikuwa wanakwenda kupata kila siku ya nyingine nyingi zilizoazimiwa kwao (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13)].
Wangeweza kutubu na
Mungu angewasamehe na kuwaokoa, hadi kwenye kipindi cha mwisho.
Badala yake, Vespasian
alielekeza mawazo yake huko Peraea, mahali ambako ndiko ulikokuwako mji wa
Vespasian alipeleka
jeshi huko kutoka Kaisaria hata kabla ya majira ya baridi kufika. Alifika huko
tarehe 4 Dystrus, au mwezi wa Adari wa mwaka 68BK na kuuchukua mji. Hatimaye
alirudi Kaisaria. Vespasian akaacha kikosi cha kiasi cha wanajeshi 3,000 vijana
na wenye hari ya kazi na askari wapanda farasi 500 wakiongozwa na Placidus, na
hivyo kuhitimisha hali kuuitiisha mji wa Peraea pamoja na Machaerus. Hali hii
ilikuwa na madhara katika kuhakikishia kwamba Kanisa limeachwa na amani na
kuona kwamba hakuna mtihani mbaya unaotokea huko Yudea, Galilaya na Idumea.
Wakati majira ya
baridi yakiwa yamekamilika na kuendelea, Vespasian aliondoka tena kutoka
Kaisaria. Lengo
Akautwa na kuukalia
mji wa Antipatris, na kuiteka miji ya Lydda na Jamnia. Akapeleka Kikosi cha
wanajeshi Kombania ya 5 likaweka kambi yake nje ya mji wa Emmaeus. Kisha akaushambulia
ghafla mji wa Idumaea. Akiwa anarudi na kuelekea upande wa kaskazini, akiwa
njiani akipitia Emmaeus, alienda hadi akafika
Kipindi hiki Yudea ulikuwa
umeshatiishwa na kuacha jeuri kabisa. Sasa Vespasian aliweza kurudisha mawazo
yake kwenye suala la Yerusalemu (
Vespasian alisubiri
kupewa taarifa, na kwenye kipindi cha majira ya baridi ya mwaka 68/9BK alipokea
taarifa kwamba Galba ametangazwa kuwa mfalme. Akampeleka motto wake Tito aende
Roma aende kumpa heshima na pongezi mfalme huyu mpya na kungojea amri yake. Kwa
hiyo, ni Tito peke yake ndiye aliyewahi kufika maeneo yote hadi huko Korintho
wakati alipoarifiwa kuwa Galba ameshambuliwa mnamo tahere 15 Januari 69BK.
Ndipo Tito alirejea
kwa baba yake huko Kaisaria. Vespasian aliendelea kuvuta subira.
Jinsi matukio
yalivyokuwa yalimlazimisha Vespasian aamue kuondoka na kwenda Yudea wakati Simon
Bar-Giora (mwana wa mwongofu) ambaye alikuwa na mwenendo na tabia sawa na zile
za ho John wa Gischala – aliyekuwa ni Mzelote asiyeweza kuchukuliana na wengine-na
ambaye ameanza kukusanya kikosi cha wafuasi ili kukomesha mapigano. Kwa hiyo,
yeye na wafuasi wake wakaanza kuenea pande za kusini mwa Palestina, akifanya
uporaji na kuiba popote walipokwenda.
Basi wakauangamiza
mji ule
Hatimaye, Vespasian akalazimika
kuuhusuru. Mnamo tarehe 5 Daisius, au Siwani mwaka 69BK, baada ya kipindi cha
mwaka mmoja kamili wa mapumziko, akaja tena kutoka Kaisaria. Akayadhibiti
majimbo ya ya Gophna na Acrabata na miji ya Betheli na Efraim. Akauendele na
kuukaribia mji wa Yerusalemu wakati ndugu yake Cerealis akiushinda na kuuteka
na kuuteketeza kabisa mji wa
Mji wa Yerusalemu ulikuwa
umechoshwa
Badala ya kuwekwa
huru na kuokolewa na matisho na mateso ya John, wakajikuta wakiwa na watu
tishio wawili sasa ambao wote hawa walimuona kila mtu mwenye hela kuwa ni adui
wao mkubwa.
Mungu atafanya kitu
kwa lengo la kuupa Yerusalemu kipindi kamili cha kutubu na kuwapa Yuda fursa ya
kubakia.
Wakati Vespasian
alipokuwa anarudi Kaisaria, habari zikamfikia kuwa jimbo la Magharibi limemtangaza
Vitellius kuwa mfalme. Jimbo la Mashariki likaamua kuwa ni vema wawe na Vespasian
kuliko kuwa na mtu mwenye uchu na mlafi Vitellius.
Tarehe 1 Julai 69BK,
Vespasian alitangazwa kuwa ni mfalme wa Misri. Siku chache bade Majimbo ya Palestina
na Syrian yakafuatia. Kabla ya katikati ya Julai alitawazwa rasmi kuwa mfalme
wa pande zote za Mashariki.
Ndipo Vespasian aliona
ni mhimu kwanza aanze kwa kukusanya nguvu zake na kuachana na habari ya uasi wa
Wayahudi hadi baadae. Muda ulipaswa uendane kwa mujibu sawa na makusudi ya
Mungu na kalenda yake.
Vespasian alipokea
wajumbe akiwa huko Berytus na kisha akaelekea Antiokia. Na akiwa huko alimtuma Mucianus
aende kwa njia ya bara hadi Roma pamoja na jeshi na baadae akaelekea
Akakaa mjini
Kwenye kipindi kibaya
cha mwaka hali ya mambo ilikwenda vibaya
Na badala ya kuwa na
makundi mawili tu Tishio na ya wataabishaji, wakajikuta sasa wana makundi
matatu. Kukawa na kundi la Elieza, ambaye alikuwa ni mototo wa Simon
lililotokana na kujiengua kutoka kwenye kundi la John Mzelote. Mji ukawa sasa
umegawanyika makundi matatu. Simon alidhibiti upande wa Juu wa Mji na sehemu
kubwa ya pande za Chini za Mji. John akadhibiti Milima wa Hekalu, na Elieza
akadhibiti sehemu ya uwa wa Hekalu. Watu hawa watatu walikuwa na mizozo
endelevu na mji mzima ukawa ni uwanja wa vita usiokoma.
Badala ya kuruhusu
hali ya kila mmoja aweze kuingia kwenye utaratibu wa mgao wa chakula kwa ghara
ma ya wengine, wakachoma moto kwenye maghala yasiyojulikana ya nafaka ya Yerusalemu
na kuufanya mji uwe kwenye kipindi cha baa la njaa. Wakahakikisha kwamba mji
uwe kwenye kipindi cha nja kali jambo litakalowafanya washindwe kustahimili kipindi
watakapouzingira Warumi, na kuwafanya wachanginikiwe na kuwa na usuni
utakaowafanya kushindwa kustahimili mapigano.
Walistahili kila
mmoja wao kupatwa na maafa haya ya makali ya upangawa, na kipindi hiki upanga
ulikuwa umekaribia
Jeshi hili
lililoongozwa na Tito liliundwa kwa mkusanyiko wa kombania nne. Mbali na
kombania za Vespasian za Vikosi namba 5, 10 na 15, yeye alikuwa na kingine cha
12, ambacho kilitokana na kikosi kilichokuwa huko
Makamanda wa Vikosi
vya Vespasian walikuwa ni:
Sextus Vettulenus
Cerealis Kombania ya 5
A. Larcius Lepidus
Sulpicianus Kombania ya 10
M. Tittius Frugi Kombania
ya 15
Kamanda wa Kombania
ya 12 hajulikani.
Liwaliwa wa zama ni
wa Yudea, Tiberius Iulius Alexander, alimsaidia Tito.
Alitoa amri kwa
makamanda wa majeshi haya wakutanenaye mjini Yerusalemu huku yeye mwenyewe na
kamati yake kuu wakaondoka na kwenya Kaisasria. Kikosi cha 5 kikaenda Emmaus na
cha 10 kikaelekea njia ya Yeriko. Huku akiwa na kikosi kizima cha jeshi cha
washirika wake kilichoongezewa, na ambacho kilitiwa nguvu, Tito alikuwa na
jumla ya jeshi la wanaume 2,000 waliotoka Misri na 3,000 waliochukuliwa kutoka
kwenye jeshi la vikosi vya Frati.
Schürer anasema
kwamba Tito alifika kwenye kuta za Yerusalemu siku chache kabla ya Pasaka ya
mwaka 70BK (kwenye kitabu chake ukurasa 502); na vyanzo vingine vinasema
alifika siku ya 1 mwezi wa Abibu mwaka 70BK. Hii ilikuwa ni kwa kufuata
mpangilio wa kipindi uliokusudiwa. Haina maana yoyote na wala haibadilishi
maana yake halisi hata
Tito ameenda mbele
akitumia jeshi la askari wapanda farasi 600 na alikuja kukiwa na pigo kuu
Ushujaa wa kishabiki
wa Wayahudi uliheshimiwa
Mapigano ya ndani kwa
ndani yaliendelea kupamba moto mjini. Chini ya Warumi hawa, mauaji makubwa
Mwandishi Schürer anatoa
maelezo kuhusu kilichotokea humu mjini kwenye kitabu chake cha 1 kwenye ukurasa
wa 503 na anatumi pia nukuu za Josephus (B. J. ukurasa wa 4) akisema
yafuatayo:
“
Siku tano baada ya
kutekwa kwa ukuta wa kwanza, ukuta wa pili uliangushwa kwa nyundo kubwa na
Warumi. Tito aliingia na wanajeshi maalumu walioteuliwa lakini akazuiwa na kurudishwa
nyuma na Wayahudi
Siku nne baadae
aliuchukua tena na wakati huu akauchukua moja kwa moja. Tunaona tena jinsi siku
hizi za 12 na 16 za mwezi wa Iyari zlivyomuhimu wake kwenye maagimisho ya
Pasaka ya Pili.
Hatua ya pili ya Tito
ilkuwa ni kuzijenga ngome mbili ili kujilinda dhidi ya watu wa mjini na
nyingine mbili za kujilinda dhidi ya Antonia.
Kila kikosi kimoja miongoni
mwa vikosi hivi walipewa kazi ya kujenga ngome moja. Simon Bar-Giora alikuwa
ndiye amiri wa Mji wa Juu na John wa Gischala alikuwa ni amiri wa Antonia (B.
J. v 9,2).
Kisha Warumi walimpa Josephus
kazi ya kuwaasa watu wanaoishi ndani ya mji huu wiajtsalimishe, kazi ambayo
haikuzaa matunda yoyote, maana hawakumsikiliza.
Hatimaye chakula
kikaisha mjini na masikini waliojaribu kutoka kwenda kujitafutia huko nje ya
mji walikamatwa na kuteswa mbele ya macho ya watu waliokuweko mjini. Na wakati mwingine
walikatwa viongo vyao na kurudishwa kwa nguvu mjini (B. J. v 10, 2-5).
Warumi walimaliza
ujenzi wa ngome zao siku ya 29 Iyari mwaka 70BK.
Wayahudi wakiwa chini
ya John na Simon, waliendelea kukaidi hadi ujenzi wa ngome hizi ulipoisha kabla
hawajakomeshwa na mji kuangamizwa.
John alichimba barabara
ya chini kwa chini kwenye ngome hizi hadi Antonia na kisha akaichoma moto minara
kwa wakati wake muafaka. Matokeo yake barabara hii ya chini kwa chini ilianguka
na ngome zikaangukia kwenye wimbi la mwako wa moto na ukateketea. Siku mbili
baada ya Simon Bar-Giora kushambuliwa na kuteketezwa, pia ngome za Mji wa Juu
ukateketezwa (B. J. v 11, 4-6).
Kisha Tito akauzungushia
mji kwa ukuta imara na wakudumu wa mawe kabla hajaanza kujenga ngome mpya.
Alifanya hivyo kuwa ni mbinu ya kuutenga mji huu ubaki upweke ili usiweze kupata
mahitaji yake toka nje na kisha ukumbwe na baa la njaa na hatimaye
ujisalimishe. Na kilikuwa ni kipindi cha kushangaza cha aina yake kilichodumu
kwa siku tatu na jeshi lililoulinda mfululizo likizuia asiwepo hata mmoja wa
kutoroka. (B. J. v 12, 1-32)
Hali mbaya ya njaa
iliyoukumba nji huu ni jambo ambalo Mungu aliwahi kuwaambia hapo kabla (Law.
26:29; Kum. 28:29; Yer. 19:9; Eze. 5:10) na
Mafuta matakatifu ya
mzeituni yaliyokuwa kwenye “Chumba cha Myumba ya Mafuta” kilichokuwa upande wa
kusini magharibi mwa sehemu iliyokuwa inajulikana
Na kwa kipindi cha
takriban siku ishirini, ngome ilikuliwa imeisha kujengwa na kipindi hiki
nyingine nne zilikuwa zimeshajengwa dhidi ya mji wa Antonia. Wakati huu, mbao
zililetwa kutoka umbali wa stadia 90 (mwendo wa saa 4.5) hadi kuleta kwenye
kiwanja wa ujenzi iliyokuwa wazi.
John wa Gischala akalijaribu
kuwashambulia siku ya 1 mwezi Panemus au siku ya Mwandamo wa Mwezi Tammuz au
Wanne lakini akashindwa, hali
iliyosababishwa na ukosefu wa ujasiri na mori wa vita kutokana na mauaji yaliyotokea
na Warumi kuwa na ujasiri na nguvu kubwa na morari wa vita (B. J. vi 1,
1-3).
Wayahudi wakaondoka
na mafuriko ya maangamizi kaanza. Ilipoanza haikuonyesha mafanikio lakini
hatimaye ukuta ulianguka kwa namna yake wenyewe na kufanyika kuwa umeanguka
Mnamo siku ya 3
Panemus (Tammuz) Tito aliwaamumrisha wanajeshi wake wauchukulie hatua, na
askari wa Kisyria aitwaye Sabinus na washiriki wenzake kumi na moja
waliuangusha fell (B. J. vi, 1, 3-6). Siku ya 5 mwezi Panemus, kiasi cha
takriban askari ishirini au thelathini walupima ukuta majira ya usiku na kuwaua
asakari wa kikosi cha kwanza cha kulinda doria. Ndipo Tito akaendelea mbele kwa
haraka mbele
Jweshi la Warumi
lilirudishwa nyuma pia tena lakini waliiteka Antonia na wakafanya uwezekano wa
kuuangusha chini (B. J. vi 1, 7-8).
Wayahudi walizewa
kuudhibiti shughuli zite za utoaji wa sadaka za kila siku za asubuhi na za
jioni ingawje walizikomesha zile sadaka za Wamataifa ilipofika mwaka 66BK, kipindi
yalipoanza maasi.
Na ilipofika siku ya
17 ya mwezi wa Nne au wa Panemus au wa Tammuz, kukawa hakuna wanaume wa kutosha
kuendelea na shughuli ya utoaji sadaka na wakaingia kwenye mkumbo uliowapata wa
janga la ukosefu wa chakula uliosababisha baa kuu la njaa, jambo lililopelekea
utaratibu wa kutoa sadaka usimame. Licha ya juhudi zilizofanywa za kuirudisha
hali hii kwenye maasi ya Bar Kochba, haikuwezekana kuirudisha hali hii kwa
mafanikio yake.
.
Mungu akaondoa na
kukomesha utoaji wa sadaka na akaliondoa Hekalu lililokuwa linaonekana kwa
macho, na kumfanya Masihi kuwa ndiye Hekalu, yaani Kanisa. Na ule utaratibu wa
kutoa dhabihu ya wanyama wa kuchinjwa utarejeshwa tena mjini Yerusalemu baada
ya kurudi kwake Masihi na kuurejeshamarejesho mapya mji wa Yerusalemu na
kipindi ambacho Hekalu litarejeshwa upya kwa mujibu wa sawa na unabii wa
Ufunguo wa Daudi (pia soma jarida la (Ufafanuzi wa Kitabu cha Zekaria (Na. 297) [Commentary
on Zechariah (No. 297)].
Josephus
akatakiwa afanye juhudi ya kuwasihi tena ili wasalimu amri, lakini juhudi yake
haikuzaa matunda tena hata mara hii.
Mashambulizi
zaidi ya kulishambulia Hekalu saa za usiku yalishindwa na Tito hakuwa na namna
nyingine bali kuamua kufanya mashambulizi makubwa ya sehemu zote.
Hekalu lilikuwa
limejengwa vizuri na lilizungushiwa na ngome imara, ambayo ilikuwa ni ya mraba na
yenye nguzo zilizojengwa kwenye kuta nene. Uwa wa ndani pia ulizungushiwa na
kuta nene, na kufanya safu ya pili ya ulinzi baada ya kuta za nje zikianguka.
Tito alianza kwa
kujenga ngome nne kwenye kuta za nje. Wakati huu vifaa vya ujenzi vililetwa mbali
kiasi cha urefu wa stadia 100 kutoka Yerusalemu.
Wayahudi
hawakuwa wavivu wa kufanya kazi. Waliazimu kuzungushia safu ya nguzo kwenye
ukuta wa upande wa magharibi kwa kutumia vifaa mchanganyiko vya ujenzi na
vyenye kuweza kuwaka kiurahisi na wakaifanya ionekane
(B. J. vi 3, 1-2).
Ngome hizi
ziliisha mnamo siku ya 8 Abu au mwezi Lous. Wanajeshi wakaletwa na kusonga
mbele na kazi ya kuuzingira ikaanza tena. Kuta zilikuwa hafifu
Hadi kufikia
siku ya 9 Abu, malango yote yalikuwa yameteketezwa kabisa. Josephus anadhania
kwamba baada ya hapo Tito aliunda baraza la Vita ambalo lilishauri kuwa
waliache Hekalu peke yake (B. J. vi 4, 3).
Siku ya 10 Abu
Wayahudi wakafanya mashambilizi mawili ya kujipizia yaliyotokea kwenye Ua wa
Ndani wa Hekalu iliyokuwa kama ngome
Wakiwa
wanajilinda kwa kujihami na mashambulizi haya ya pili, mwanajeshi mmoja wa
Kirumi ambaye alikuwa kwenye mahangaiko makubwa akarusha kizinga cha moto
kupitia kwenye safu ya nguzo ambacho kilienda hadi kwenye Helaku na kuanza
kuwaka
Josephus anadai
kwamba baada ya Tito kufahamishwa habari hii kwa haraka alimuamuru kamanda wake
aende haraka na wanajeshi wake ili wakajaribu kuuzima mto huo na kuliokoa
Hekalu. Alipotoa amri hii muhimu na inayohitaji kutekelezwa maarufu
Anaelezwa kuwa
alitoa amri kadhaa ili kuliokoa Hekalu, lakini inaelezwa kwamba askari wake
waliokuwa wamekasirika na kuchoshwa na vita sio tu kwamba walipuuzia tu amri
zake bali inaelezwa kuwa waliendelea kutupa makombora kadhaa ya moto ndani
yake. Inaelezwa kuwa Tito alikuwa ameingia ndani na kuliangalia kabla
halijateketezwa (B. J. vi 4, 6-7).
Josephus
anaitaja tarehe ya kuteketezwa kwa Hekalu hili kuwa ni siku ya 10 Abu (B. J.
vi 4, 5). Hata hivyo, kwa mujibu wa mapokeo ya marabi, siku hii ya kuteketezwa
kwa Hekalu inatajwa kuwa ilianzia jioni ya siku ya 9 Abu (m Taan. 4:6), yssni
msjira ya jioni (b Taan. 29a) na ilikuwa ni mwishoni mwa maadhimisho ya siku
takatifu ya Sabato.
Lakini ukweli ni
kwamba, inawezekana
Schürer anasema
kwamba Valeton anaukosoa mtazamo huu mpotofu wa Josephus kwa kushindwa kwake
kuchukua na kuyaandika vizuri matukio ya vile baraza la Vita.lilivyoamua
kulichukua na kulikalia Hekalu na jinsi walivyolichukua kwa nguvu na
walivyoliteketeza kwa makusudi kama walicyoweza. Mwanahistoria mwingine Valeton
anadai kwamba tendo hili lilitokana na maelekezo na amri aliyoitoa Vespasian
lakini baraza hili lingeweza kabisa kuubatilisha uamuzi huo na kuupinga.
Askari wa miguu
wa Kirumi waliletwa ndani ya Hekalu na kutweka bendera
Vyumba
vilivyokuwa kwenye kuta za Hekalu vilikuwa vikitumiwa na makuhani nao
walikuwepo bado. Walilazimishwa washuke chini kutoka mafichoni walikojificha
wakiwa na kiu kali na hatimaye waliuawa wote.
Tito akawaambia
Wayahudi waliomshambulia kwa maneno wakimlaumu kwa kujaribu kumlazimisha mambo
kwa kuamuru mashambulizi na kuuteketeza mji wa Yerusalemu. Warumi walichoma
moto maeneo yote muhimu na pia mji wa Acra, hadi kwenye jumba la halmashauri na
mji wa Ophlas.
Watu kutuka jamii ya
daraja la juu walimsihi tena na akaruhusu baadhi
Josephus aliandika
taarifa za unyama mkubwa waliofaunya waasi wa Kiyahudi kwenye mji huu kwa wakati
ule. Wazelote walikimbilia
kwenye Mji wa Juu. Hatimaye mji ulifanyiwa matendo ya unyang’anyi na uporaji na
uharibifu ulifanyika kwenye Mji wa Juu na Warumi walichukizwa wakiamini kuwa
matendo yale ya unyang’anyi na uporaji yalikuwa yamepangwa na kukusudiwa.
Wazelote walitumia
udhaifu wa Warumi ili kuwapiga, wakatuama kwenye maeneo ya kujificha na
wakafanya mauaji ya kumchinja kila mtu aliyejaribu kutoroka na kwenda kwa
Warumi. Hakukuwa na mahala mjini kote ambapo hapakuchafuliwa na mtapakao wa
maiti ya wale waliokufa kwa njaa au kwa kuchinjwa. Walijaribu kujificha kwenye
mahandaki mjini na waliyachoma maeneo mengi kwa moto kwa kiasi kibaya mno
kuliko hata walivyofanya Warumi wenyewe. Watu waliokimbi nje ya nyumba zao ili
kujiepusha na moto waliuawa na Wazelote hawa pasi na huruma. Walikula vyakula
vilivyotekwa kwa mwagiko wa damu na unyang’anyi. Josephus anasema kwamba
anaamini kuwa iwapo
Mnamo siku ya 20
mwezi Abu, Tito alitoa amri ya kuzingira kingo na kuzitenganisha na maeneo ya
Juu ya Mji ya Mlima Sayuni.
Vikosi vine vya
wanajeshi vilikwenda na kuweka kambi zao upande wa Mashariki mwa mji mkabala na
Jumba la Ikulu ya Kifalme. Mabaki ya wanajeshi hawa pamoja na maboma yaliyotoka
Xystus hadi kwenye daraja na mnara ambao Simon aliujenga na kuuimarisha ili
ajilinde dhidi ya John.
Mpango wa kujaribu
kuudhoofisha uliofanywa na Idumeans ulikubaliwa na Tito, lakini Simon aliuzuia
na watu wane walipokuwa wakirudi na waliuawa na viongozi wakatiwa jela. Hata
hivyo, matendo ya uteketezaji na maafa vilizidi kupamba moto.
Waliwaacha kwenye
mateso na familia zao. Kima cha kuwanunua watumwa kilipungua chini bei yake kwa
kuwa walipungua thamani
Kingo za kuzungusha
kwenye mji huu ziliisha kujengwa siku ya
Josephus aliamini
kuwa ilikuwa ni Mungu mwenyewe tu ndiye aliwaondoa kwenye minara ile baada ya
walivyoondoka toka mjini. Walifanya haraka kukimbia ili wajiponye kwenye bonde
lililokuwa huko Siloam. Waliwashambulia ili kujilipiza kisasi kwa Warumi ila
walikuwa ni dhaifu na walichoshwa na kukatishwa tama na walinzi.
Kisha Warumi wakaenda
mjini na kuanza kuwaua na kuchoma moto kila mahali na kila waliyemuona humo
mjini. Mawindo
Watu walionusurika
walikuwa ama wameuawa, au walipelekwa migodini au walihifadhiwa kwa kuvalishwa
kombati za wanamgambo.
Machimbo haya yalikuwa
nchini Misri na kwa hiyo, ile ahadi ya Mungu kuwa atawarudisha tena Misri kwa
kosa lao la kulivunja agano
Na
Tito alisherehekea
tukio hili kwa kuwagawia zawadi wanajeshi wake, na kutoa sadaka na kwa kufanya
sherehe kubwa za nderemo.
Mtiririko wa matukio ya Vita
tangu Mwaka 71 hadi 74BK
Tito akakiacha Kikosi
cha 10 kwa walinzi wa mji wa Yerusalemu.
Akaondoka na wanajeshi
wealiobakia hadi Kaisaria Maritima, ambako mateka na wafungwa waliwekwa kwenye
gereza salama.
Tito akaenda Kaisaria
Filipi, kumuona Agripa, ambako baadhi ya wafungwa walilazimishwa kupigana na
wanyama wa porini, au kuchukua sehemu
Wafungwa wa Kiyahudi
walilazimishwa wauane kwenye sherehe hii iliyofanyika kwenye mji wote wa Antiokia.
Kisha wakaondoka na kuelekea Zeugma iliyoko Frati na kurudi Antiokia. Kisha
wakarudi kutoka Misri na kuviacha vikosi vyao vya wanajeshi huko
Wafungwa maarufu
wapatao mia saba wakiwemo Simon na John walihifadhiwa kwa ajili ya kuwatumia
kwenye shughuli za sherehe. Na ingawaje waliweza kushunda mara kadhaa, lakini Vespasian,
Domitian na Tito waliweza kuwashinda kwa pamoja mnamo mwaka 71BK. Kwa kufuatia
destuiri za wahenga wa hapo zamani, baada ya sherehe hii ilibidi Simon alichukuliwe
kutoka gerezani na akauawe.
Miongoni mwa tunu
zilizotolewa kuwapa mashujaa waliosababisha kushunda kwa vita ile vilikuwa ni
tunu mbili za dhahabu zilizotolew kutoka Hekaluni na ndizo zilikuwa ndiyo
zawadi kuu kupewa mashjaa hawa (na zilitolewa mbele ya macho ya Wayahudi
wenyewe wakishuhudia). Navyo vilikuwa ni Meza ya Mikate ya Wunyesho na vichala
Vespasian akaviweka
vinara hivi kwenye Hekalu la Mungu-mke wa Amani (Pax) aliyokuwa ameijenga na
ambayo hatimaye ilichomwa moto na kuangushwa chini na Wanajeshi watiifu (Herodian
i 14, 2, sawa na anavyosema Schürer, ukurasa wa 510, pia ukurasa wa 132).
Schürer anaamini
kwamba Geiseric aliwachukua na kuwapeleka Afrika baada ya kipindi ambacho Vandals
waliuteka na kuuchukua mji wa Roma mwaka 455BK, na hatimaye wakasafirishwa hadi
Palestina ilikuwa haijasalimu amri yote bado ingawa mji wa Yerusalemu na upande wake wa kaskazini ulikuwa umeteketezwa kabisa.
Ngome za Herodium,
Machaerus na iliyokuwa sasa ni mashuhuri ya
Lucilius Bassus, liwali
wa Palestina, alikuwa amepewa kazi ya kuwapunguza waasi hawa.
Josephus anaonyesha kwamba mkakati wa kuwazingira
na kuwashinda uliobuniwa na Herodium ilikuwa umekamilika bila matatizo makubwa
(B. J. vii 6, 1). Machaerus ilichukua kipindi kirefu lakini hatimaye
nayo ilisalimu amri pia kabla ya shambulizi la mwisho halijatokea. Machaerus ulikuwa
upande wa kusini ya mpaka wa Peraea ikifuaatiwa na jimbo la Nabataean. Ilikuwa
ni siku ya sherehe ya kupeana zawadi ya Khirbet el Mukawer. Mwanzoni kabisa
ulilindwa kwa ngome ya Alexander Jannaeus, ambayo iliaharibiwa na kuangushwa na
Gabinus (kitabu cha Antiq., xiv 5, 4). Hatimaye ikajengewa ngome tena na
Herode Mkuu (B. J. vii 6, 2 sawa na asemavyo Schürer 1, ukurasa wa 511,
na. 135, re
Kijana aliyejulikana kwa jina la Eleaza alijitathmini
na kutaka kuulinda lakini alikamatwa. Warumi walimtisha na hatimaye
walimsulibisha mbele ya lango la ngome na hatimaye watu waliokuwa ndani ya
ngome hiyo wakaamua kujisalimisha. Hili lilikuwa ni tendo geni kuwahi kutokea,
lakini ngome ikabakia ukiwa ikiwa imekimbiwa na wakazi wake hadi
Lucilius Bassus alikufa kwenye kampeni hii
na kazi yake akapewa mrithi wake Flavius Silva ili aendelee na mkakati wa kuupunguza
Huu Masada (ambao maana yake ni ngome ya mlimani) ulipunguzwa baada ya kampeni ya siku nyingi. Kazi ya kuuzingira ya mwaka 73BK inaonekana hadi sasa (hadi sasa kuna sahani zinazoonekana). Ingeweza kukabiliwa tu kwa kutumia mwelekeo wa upande mmoja tu (pia tazama kitabu cha Strabo xvi 2, 44 na Schürer kilikile., ukurawa 137).
Upande unaoelekea Bahari ya Chumvi una maporomoko na hauwezi kusogelewa na wazingiraji. Ni mahali pamoja tu kwenye maporomoko ambapo watu hawa waliokuja kuuteketeza mji wangeweza kuteketezwa, na wahanga wakuuhami mji walikuwa wametegemea tayari wanategemea kuvunjika na kusimamishwa kwa lundo la kuni na dunia ambalo lilikuwa sawa kama na mnyumbuliko ambao maporomoko yalikuwa ni makubwa sana dhidi yake (kwa kujibu wa kitabu cha Schürer).
Warumi walifanikiwa
kukipunguza kizuizi hiki kwa moto.
Ndipo Eleaza akaona
kuwa bilashaka Warumi wangeweza kuwashinda. Akawashauri kwa maneno kuwa kikosi
kizima cha ulinzi wa mji kiwaue watu wa nyumbani wao wenyewe na kasha wajiue
wenyewe (kitabu cha B. J. vii, 8, 6).
Walitii na kufanya hivyo,
na Warumi wakaingia kenye ngome ya mlimani ya watu waliokufa na wakakuta
wanamgambo wao wote wake kwa waume na watoto wamekufa. Waliacha aswira ya
mauaji ya kuchinja kusiko na huruma walikokufanya.
Josephus anaelezea
kuwa mauaji haya makuu ya kujitoa mhanga yaliyofanywa kwa kujichinja huko
Maana ya jambo hili
lilikuwa dhahiri na kamili. Baada ya Malaika wa Kifo kupita mbali na Yuda kwenye
Pasaka hii siku ya 15 Nisan, ikawakuta wao wameisha mkataa Kristo na Dhabihu
yake. Watu walipewa miaka arobaini ya kufanya toba. Lakini hawakufanya hivyo na
kipindi cha nusu ya mwisho ya majuma ya mwisho ya miaka yalishuhudia kuanza kwa
vita. Siku ya 10 Abu, Hekalu liliteketezwa. Kwenye kipindi cha Pasaka ya mwaka
74BK, uwezo wao wa kuzuia na kushindana waliokuwanao watu wa Yudea ulikoma na
kwisha kabisa na taifa zima likawa kwenye mtafaruku na mtawanyiko.
Jambo lisilosameheka
ni kwamba mataifa yaliyokuwa karibu yake yalikichukulia kipindi hiki cha maasi
kuwa ni kizuri kwao na cha kuwafanyia mambo ya ukatili Wayahudi na kisha
wakaanza kuwaua kwa kuwachinja Wayahudi kila mahali. Katika mji wa
Wayahudi walikuwa
wanateswa kwa moto na kubanwa kwenye vitu asili yachuma hadi kufa. Baaadhi yao
walitolewa waliwe na wanyama wakali wa porini lakini waliokolewa kimiujiza, ni
wachache wao tu ndio waliliwa, na walipopona walipelekwa tena kwa wanyama hawa
kwa mara ya pili huku wakijiburudisha kwa vile wanavyoraruliwa na wanyama hawa
na wao wakiona jambo hilo nikama burudani tu kwa umati uliokusanyika kuja
kushuhudia (kitabu hikihiki cha B. J.). kwa jinsi hii walikuwa
wamedhalilishwa
Baada ya kuanguka kwa
Kisha Sicarii akakimbilia
Sicarii, akiwa na mtu
aitwaye Jonathan, pia aliwachochea waasi waliokuwa huko
Kisha Catallus akaenda
Roma kuwachukua Jonathan na wafuasi wake pamoja na mateka wao wote. Alitaraji
kukabili mashitaka lakini Vespasian akatoa ombi maalumu la kuondoa mashitaka ya
Wayahudi walioshitakiwa na Catallus na Jonathan. Kisha Jonathan akateswa na
kuumizwa akiwa hai. Vespasian hakumuadhibu Catallus, bali Catallus alipatwa
ugonjwa na kufa kwa hali ya kushangaza
Kwa hiyo, Viya vya
Wayahudi iliishia kwa maangamizi ya watu wa Yuda, na nchi ikasambaratika. Kila
jaribio lililofanywa kulirejesha upya taifa hili na kulijenga Hekalu lile
lilishindwa na kuishia patupu. Kania liliteswa pia lakini tangia kipindi hiki
limeendelea kudumu likiwa jangwani kwa kipindi cha miaka elfu mbili.
Lakini marejesho
mapya na wongofu wa watu wa Yuda unakuja na kipindi hiki cha Siku za Mwisho
tutajionea marejesho ya mfumo wa Masihi huko Yerusalemu.
q