Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[299E]
Mtu wa Kuasi, na Ukengeufu
(Toleo La 1.0
20101030-20101030)
Kuja kwa Mwana wa Uharibifu kwenye Kanisa la Mungu katika Siku za Mwisho kuna maana kubwa sana na kuujua utambulisho wake ni jambo la muhimu sana kwa Kanisa ambalo ni Mwili wa Kristo.
Email: secretary@ccg.org
(Hakimiliki © 2010 Wade Cox)
(tr. 2012)
Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa
kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu,
ikiwa tu
Jarida hili
linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org
Mtu wa Kuasi, na Ukengeufu
Jina hili
la Mtu wa Kuasi au Mwana wa Uharibifu
linatokana na maandiko ya Mtume Paulo kwenye Waraka wake wa Pili kwa
Wathesalonike ambao aliwaandikia rasmi ili kuwaonya kwa tukio hili kuwaeleza
jinsi litakapotokea na kipindi chake na mambo yatakayotokea kabla ya kutokea
kwa Ukengeufu huu na Kurudi kwake Kristo.
Aliwaandikia
Wathesalonike akitumia maneno ya “Katika jina la Mungu, Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa hiyo andiko hili halipaswi
kutafsiriwa vibaya kana kwamba linatutia moyo kuamini imani ya miungu miwili
2Wathesalonike 1:1-12
1Paulo,
Silvano na Timotheo, Kwa kanisa la Wathesalonike mlio
katika Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo: 2Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo iwe
nanyi.
Kanisa la
Thesalonike lilikuwa na msingi imara wa kiimani na lilikuwa linaendelea vizuri
katika kumpenda Bwana na inaonekana kuwa watu wenye mafundisho yanayopinga
ulazima wa Amri na Sheria za Mungu maarufu kama Waantinomia walifaulu kuwapata
baadhi yao na walianza kueneza mafundisho haya mapotofu ya hawa Waantinomia.
Hadi hapo kanisani kwao na ndipo Paulo alipochukua
hatua hii ya kuwaandikia waraka huu akikusudia kuwaimarisha imani
3Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu sikuzote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu
imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa
mwenzake unazidi kuongezeka. 4Ndiyo
sababu miongoni mwa makanisa ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki
mnazostahimili. 5Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki na kwa sababu hiyo
ninyi mtahesabiwa kwamba mtastahili Ufalme wa Mungu, ambao ninyi
mnateswa kwa ajili Yake. 6Mungu ni mwenye haki: Yeye atawalipa mateso wale wawatesao ninyi 7na kuwapa ninyi mnaoteseka raha
pamoja na sisi, wakati Bwana Yesu atakapodhihirishwa kutoka mbinguni
katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. 8Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Yesu.
Walikuwa
wanaadhiwa kwa ajili ya kuzifuata na kutii sheria na
amri za Mungu na hawa Waantinomia walilishambulia kanisa wakisingizia kuwa
tendo lao la kuzitii zmri hizi ndicho chanzo cha malumbano na mapambano
Aliwaambia
kuwa wameahidiwa mapumziko mema atakaporudi Kristo na
atawapatiliza kuwahukumu wale wote waliokuwa wakilitesa kanisa. Hukumu watakayopewa
watu hao ni maangamizo ya milele na hawatakuwepo
kwenye Ufufuo wa
9Wataadhibiwa kwa uangamivu
wa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa uweza Wake, 10siku hiyo atakapokuja kutukuzwa
katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia
mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda
wetu kwenu. 11Kwa sababu hii,
tunawaombea ninyi bila kukoma, ili kwamba Mungu apate
kuwahesabu kuwa mnastahili wito Wake na kwamba kwa uwezo Wake apate kutimiza
kila kusudi lenu jema na kila tendo linaloongozwa na imani yenu. 12Tunaomba hivi ili
Jina la Bwana wetu Yesu lipate kutukuzwa ndani yenu, nanyi ndani Yake,
kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo.
Chanzo au
sababu za Waantinomia kulitesa Kanisa la Mungu vimeelezewasana kwenye jarida la
Jinsi
Waantinomia Wanavyozipinga Sheria Na Amri za Mungu (Na. 164D) (Antinomian Attacks on the Law of
God (No. 164D)] kwenye tovuti
ya: http://www.ccg.org/english/s/p164d.html.
Kipindi Hadi Kuja Kwa Masihi
Kisha Paulo anaendelea mbele hadi kuelezea ukweli ulivyo wa jinsi Kurudi Tena kwa Masihi kutakavyokuwa. Akaema kwamba
kutalazimika kwanza kuwepo kwa uasi mkuu na ukengeufu
utakaloliandama Kanisa na vuguvugu la kuzipinga Sheria ambazo pia ni Amri za
Mungu na kwamba hayo yatatokea kabla ya kuja kwa ile Siku yenyewe ya Bwana.
Unaweza kujionea na kusoma habari hii kwenye jarida la
Siku ya Bwana
Na Siku za Mwisho (Na. 192) [The Day of the Lord and the Last
Days (No. 192)] kwenye tovuti ya: http://www.ccg.org/english/s/p192.html.
2Wathesalonike 2:1-17
1Ndugu, kuhusu kuja
Kwake Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu pamoja mbele Zake,
tunawasihi, 2msiyumbishwe kwa
urahisi wala msitiwe wasiwasi na roho wala neno au barua inayosemekana kuwa
imetoka kwetu, isemayo kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwako.
Kwa hiyo, kulikuwa hakuna sababu ya kuweko waraka mwingine wowote au
neno vya kusema kuwa Bwana ameisharudi.
3Mtu ye yote na asiwadanganye kwa namna yo yote kwa maana siku ile haitakuja
mpaka uasi utokee kwanza na yule mtu wa kuasi adhihirishwe, yule ambaye
amehukumiwa kuangamizwa kabisa. 4Yeye
atapingana na kujitukuza juu ya kila kitu kiitwacho Mungu au
kinachoabudiwa, ili kujiweka juu katika hekalu la Mungu, akijitangaza
mwenyewe kuwa ndiye Mungu.
Maasi Makuu
lazima yaje kwanza ambayo ni maasi dhidi ya amri na
sheria za Mungu, maasi yatakayoanzishwa na kuendelezwa na huyu mwana wa
ukengeufu ambaye anafunuliwa kwa sasa. Neno hili “ukengeufu” kwa
lugha ya Kiyunani linaitwa “Apostasia” au Ukengeufu Mkuu ambao maana yake ni
kuondokana au kuachana kabisa na chembe yoyote ya ukweli wa Kiimani. Na imani
hii waliyoachana nayo wao ni ile ya kuzitii sheria na
amri za Mungu. Ndiyo! Mwana huyu wa ukengeufu ndiye huyu Mwana wa uharibifu, jambo ambalo
ni tendo la kuziasi Sheria za Mungu (1Yohana 3:4). Dhambi maana yake ni uasi, neno ambalo kwa Kiyunani linaitwa anomias ambalo maana yake ni mtu aishie bila kutiisheria. Wale wote
wayafuatayo mafundisho haya yanayosema kuwa sheria za Mungu hazina kazi kwetu leo na zilikoma wako kwenye kundi hili la waanomia, yaani ni
watu wanaoishi bila kutii sheria au
waantinomia ambayo maana yake ni wapinga
sheria. Ni walewale na ni kitu kile kile. Wamekuwa
ni wapinzani na wenye kulidharau Kanisa la kweli la
Mungu kutoka siku za nyuma karne ya kwanza. Tumewaona wakiendelea na kuzidi kuongezeka miaka hadi miaka. Ukengeufu huu
umetokana na Waingereza wa mrengo huu wa Kiantinomia na dini yao ya kumwabudu
mungu Attis au Adonias, au Osiris au Mithras au Baali na alijulikana na
kuabudiwa kwa kutumia majina ya namna mbalimbali lakini ni yeye huyu ndiye
aliyekuwa akiabudiwa. Ikafikia mahala pa kwamba hata Makanisa ya Mungu katika
mataifa ya magharibi yamepotoka na kujiingiza kwenye
imani ya Miungu miwili au mitatu, yaani Ubinitaria au Utrinitaria ambayo ni
imani ya hawa Waantinomia na kwa kuamini kwao hivyo wamejiondolea stahili
Kwenye zama mpya ya vuguvugu hili la nguvu za upotevu na Ukengeufu
kulianza na harakati potofu za kile kilichoitwa Mageuzi na Matengenezo ya
makanisa, harakati zilizoendelea hata kwenye Makanisa ya Mungu yaliyokuwa yanateswa
na Mfumo wa dini ya Kirumi. Wakafanyika kuwa ni
wapinga mfumo ule lakini wakigeuka na kushiriki kikamilifu kulifanyia ubaya na
kulitesa Kanisa la Mungu hali waliyoendelea nayo kwa karne kadhaa sasa.
Makanisa
haya yaliendelea kasi yake zaidi hasa wakiulinganisha mfumo wao na ule wa Makanisa ya Mungu yalivyokuwa kipindi cha zama ya
Wasardi baada ya kipindi hiki cha Matengenezo. Mfumo wa
kwanza ulishuhudia makanisa yakiangukia kwenye Ukengeufu pia. Hawa walikuwa ni Wanafunzi walojaribu kuisoma Biblia na kuyachunguza
maandiko ambao hatimaye walikujajiita kuwa ni Mashahidi wa Yehova. Watu hawa
walitangaza kuwa sheria za Mungu zimekoma na kupita wakati wake na kupinga
kabisa umuhimu wa kuzitunza Sabato na kuwa ni siku ya Kuabudu na wakajiondoa
kabisa kushirikiana na Makanisa ya Mungu ni hali kama hiyohiyo ndiyo ililikumba
Kanisa la Mungu (La Sabato ya Siku ya Saba) [Church of God (Seventh Day)].
Wakati kanisa la Waadventista wa Kisabato (SDA) walipojiengua kwenye Kanisa
hili la [COG (SD)] na kuachana na sheria nyingine za Mungu na wakashikilia
utunzaji wa Sabato ya juma tu na kuacha kuzizingatia amri nyingine
zilizoorodheshwa kwenye Amri ya Nne na hatimaye wakajiunga na mafundisho ya
Utatu kwa uoande wa Magharibi mwaka 1978 na kasha wakatokomea na kuingia zaidi
barani Afrika 2003-5.
Hata
Herbert Armstrong akiwa na kanisa lake la RCG/WCG alianza kwa kufuata mfumo huu
wa Ukengeufu na kulipotosha Kanisa la Mungu kwa kiasi kikubwa sana wakati
alipoifuata Kalenda potofu ya Hillel yenye kufuata mtazamo na mzunguko wa
Kibabeloni na wenye mahirisho wa zama za kabla ya ujenzi wa Hekalu. Akafundisha
mafundisho yenye mwelekeo wa Kiditheism,
yaani imani inayoamini uungu wa miungu miwili na hatimaye imani hii ya Kiditheism ilizaa mafundisho ya kuamini Miungu Miwili
yaani Ubinitaria na akayakumbatia na kuyaridhia pia mafundisho ya Utatu yaani
Utrinitaria. Hatimaye akawa ni Mcuungaji mwabudu sanamu na akalipeleka Kanisa
la Mungu kwenye ukengeufu wa hali ya juu sana kiasi cha kufikia kutangaza kuwa
Sheria na Amri za Mungu hazihitajiki tena na sio muhimu na akaikubali na
kuiridhia imani ya Utatu kuwa ni imani rasmi ya kanisa na kurithia vile
isemavyo kwamba Mungu ni wa utatu maka wasemavyo wakengufu wote wengine.
Kufikia
kwenye kiwango hiki cha kufundisha ukengeufu huu ndipo alikufa majuma 40
baadae, kwa siku na saa ileile aliyokuwa anafundisha
hivyo kwa mujibu wa wale walio fuatilia siku na saa aliyokuwa akihubiri ujumbe
huu na alivyokufa kwa maumivu makali. Makanisa yakaanza kuwa na
mfumo wa makanisa ya Wasardi na Walaodikia na yameliharibu Kanisa la Mungu
uoende wa Magharibi.
Hadi leo makanisa yanafundisha mafundisho haya Mapotofu ya imani
hii ya Kibinitaria na Kitrinitaria na yanaifuata Kalenda potofu ya Hillel na
wendine hata wameshindwa kujua ni kalenda gani waifuate kwenye mambo
fulanifulani. Ukengeufu huu utaendelea tangu sasa hadi kipindi kile cha
mashahidi na hatimaye kurudi kwa Masihi. Ni makanisa
haya mawili tu miongoni yale saba ndiyo yatashuhudia
watu wachache watakaoingia kwenye ule Ufufuo wa
Paulo anaelezea jinsi ile siri ya kuasi ilivyokuwa imekwishaanza kufanya
kazi katika siku zake.
2Wathesalonike 2 inaendelea kusema:
5Je,
hamkumbuki ya kwamba nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambia mambo haya? 6Nanyi
sasa mnajua kinachomzuia, ili kwamba apate
kudhihirishwa wakati wake utakapowadia. 7Maana
ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia
ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa. 8Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamteketeza
kwa pumzi ya kinywa Chake na kumwangamiza kabisa kwa
ufunuo wa kuja Kwake. 9Kuja kwa yule mwasi kutaonekana kana kwamba ni kutenda kazi kwake
Shetani ambaye hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo 10na kila aina ya udanganyifu kwa wale
wanaoangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa.
Kumbuka kuwa siri hii ilikuwa imefichwa lakini hatimaye iliruhusiwa
ifunuliwe. Nguvu
za imani hii ya Waantinomia inatoka kwa Shetani
mwenyewe. Ujio wa mwisho wa huyu Mtu wa kuasi
na Mwana wa Ukengeufu pia utawezeshwa na nguvu za Shetani na imani hii inaweza
kujulikana kwa urahisi kwa tabia na mafundisho yake ya kuzikataa Sheria na Amri
za Mungu. Imani na
mfumo huu vitaendelea miongoni mwa Wakristo na
Nguvu za Upotevu
Je,
itawezaje kuwa rahisi kwa Makanisa ya Mungu na
Ulimwengu wote wa Kikristo kuingia kwenye mtego huu wa kudanganywa? Na
itawezekanaje kwa wana Yuda waende sambamba na uongo
huu wa Waantinomia? Na je, itawezekanaje basi imani hii ya wana Utatu
kuchanganika na ile ya Yuda au ya Kiyahudi? Jibu ni hili:
11Kwa sababu hii, Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu, ili waendelee kuamini uongo 12na hivyo wote wahukumiwe ambao
hawakuamini ule ukweli bali wamefurahia uovu.
Dhambi ni ile tendo la kuziasi Amri na Sheria za Mungu. Haki na Utauwa ni ni kitu kimoja, yaani ni utii kwa amri za
Mungu. Hali ya kukosa kutenda haki ni dhambi na
zinajulikana kwa kigezo cha kupima kwenye Amri za Mungu.
13Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu
daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana, kwa
sababu Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho
na kwa kuiamini katika kweli. 14Kwa
kusudi hili Mungu aliwaita kwa njia ya kuhubiri kwetu
Injili, ili kwamba mpate kushiriki katika utukufu wa Bwana Yesu Kristo. 15Hivyo basi, ndugu wapendwa, simameni
imara na myashike sana yale mafundisho tuliyowapa
ikiwa ni kwa maneno ya kinywa au kwa barua.
Kwa hiyo, kwa kupitia Roho wake Mungu aliwachagua wale ambao
aliwakusudia tangu mwanzo na kwamba kamwe hawatapotezwa na Ukengeufu huu wa
hawa wa Antinomia
16Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba
yetu, aliyetupenda na kwa neema Yake akatupatia faraja ya milele na
tumaini jema, 17awafariji mioyo
yenu na kuwaimarisha katika kila neno na tendo jema.
Kwa hiyo,
hi kwa ajili tu ya faraja ya milele ambayo Mungu ametupatia kwa neema yake tu
kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambayo inatufariji mioyo yetu na kutuwezesha kufanya
kila tendo jema na neno, ambayo ni matendo ya wateule kwa kuzifuata na
kuzishika Sheria na Amri za Mungu na Ushuhuda wa Yesu Kristo.
Kisha
anamalizia waraka wake kwa kunapaswa kukaza mwendo na
kuendelea mbele na kushinda ili tuokolewe na watu waovu ambao hawajapewa imani
hii ambayo wamepewa watakatifu mara moja tu.
2Wathesalonike
3:1-18 insema:
1Hatimaye,
ndugu, tuombeeni ili kwamba Neno la Bwana lipate kuenea kwa
haraka na kuheshimiwa kila mahali, kama vile ilivyokuwa kwa upande wenu.
2Ombeni pia ili
kwamba tupate kuokolewa kutokana na watu waovu na wabaya, kwa maana si
kila mmoja ana imani. 3Lakini
Bwana ni mwaminifu, naye atawaimarisha ninyi na
kuwalinda kutokana na yule mwovu. 4Nasi
tuna tumaini katika Bwana ya kuwa mnafanya na
mtaendelea kufanya yale tuliyowaagiza. 5Bwana
aiongoze mioyo yenu katika upendo wa Mungu na katika
saburi ya Kristo.
Kwa hiyo,
sisi tuko kwenye maongozi ya kanisa yanayotuwezesha Kumpenda Mungu na kusimama imara kwa Kristo.
Kumbuka pia
kwamba uzembe ulikuwa ni sababu kuu katika kuwaathiri
watu wasio imara kwenye imani. Mtume Paulo anasema:
6Ndugu,
tunawaagiza katika Jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni na
kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapa. 7Maana ninyi wenyewe
mnajua jinsi iwapasavyo kufuata mfano wetu. Sisi
hatukuwa wavivu tulipokuwa pamoja nanyi, 8wala hatukula chakula cha mtu ye yote pasipo kukilipia.
Badala yake tulifanya kazi kwa bidii usiku na mchana,
ili tusimlemee mtu ye yote miongoni mwenu. 9Tulifanya hivi, si kwa sababu hatukuwa na haki
ya kupata msaada kama huo, lakini ili kusudi tujifanye sisi wenyewe kuwa
kielelezo.” 10Kwa maana hata
tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri ili kwamba:
‘‘Mtu ye yote asiyetaka kufanya kazi, wala asile.’’ 11Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi bali
hujishughulisha na mambo ya wengine. 12Basi
watu kama hao tunawaagiza na kuwaonya katika Jina la
Bwana Yesu Kristo wafanye kazi kwa utulivu na kujipatia mahitaji ya maisha yao
wao wenyewe.
Watu hawa
walikuwa pia walitokana na ndugu wale waliopata nasaha
kuwa wasiogope na kuacha kutenda mema. Kusema kweli, watu hawa wanaoendekeza
uvivu ni tatizo na ni mzigo kwa wapendwa wengine.
13Kwa upande wenu, ndugu, ninyi
kamwe msichoke katika kutenda mema.
Taratibu za
kanisa ni vema ziheshimiwe na wale wasiozitii
wanapaswa kukemewa na kuonywa.
14Ikiwa
mtu ye yote hayatii maagizo yetu yaliyoko katika barua hii, mwangalieni sana mtu huyo. Msishirikiane naye, ili
kwamba apate kuona aibu. 15Lakini
msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu. 16Basi, Bwana wa
amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa kila njia. Bwana awe nanyi
nyote. 17Mimi, Paulo, ninaandika
salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Hivi ndivyo niandikavyo. 18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe
nanyi nyote. Amen.
Tunajua
kuwa andiko hili liko wazi na kwamba kiini cha maneno
ya andiko hili kipo kwenye sura ya 2
Ni jambo
lililowazi
Alama au
Mhuri utakaopigwa Kanisa na hawa Waantinomia katika
Siku za Mwisho ulielezwa na Kristo. Aliutaja kuwa ni
haya mafundisho na imani ya Kiantinomia.
9“Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa
ajili yangu. 10Wakati huo, wengi
wataacha imani yao, nao watasalitiana kila mmoja na mwenzake na kuchu kiana.
Mathayo 24:11-12 inasema:
11Watatokea manabii wengi wa uongo, nao
watawadanganya watu wengi. 12Kwa
sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa,
Mathayo 24:24 inasema:
24Kwa maana watatokea makristo wa uongo na
manabii wa uongo na kufanya ishara kubwa na miujiza mingi ili kuwapotosha, hata
ikiwezekana wale wateule hasa.
Kwenye kipindi
cha miongo kadhaa iliyopita Makanisa ya Mungu yalidanganyika hasa yale yaliyokuwa kwenye ukanda wa magharibi ya dunia kiasi
kwamba hawa Waantinomia na wahubiri wa uwongo walijitokeza na kutapakaa
miongoni mwao. Historia ya mafundisho yetu iko wazi na
inaeleweka na wateule wote na hawawezi kudanganyika lakini wale walio katika
nchi za Magharibi wamepotoshwa na kudanganyika vibaya
Uwongo wa
Mwisho
Nguvu za Upotevu
zinaendelea kutenda kazi katika siku hizi za mwisho, kwa
uweza wote wa ishara na maajabu.
Sababu hizi ndizo
zitakazopelekea Wakristo na mambo mengine
yatakayosababisha hata Wayahusi wenyewe huenda wakadanganyika na kuacha
kusimama imara
Ukengeufu huu
umeishaanza kutenda kazi yake tayari na umekubalika
kwenye mfumo wa kipapa ili kuweka dhana potofu ya kwamba Sabato ionekane kuwa
ni sheria inayowahusu Wayahudi peke
http://www.ccg.org/english/s/p274.html
na la Siku Ya Juma’ah: Na Maandalio ya Sabato (Na. 285) [The Juma’ah: Preparing for the
Sabbath (No. 285)] kwenye tovuti ya: http://www.ccg.org/english/s/p285.html.
Kwa hiyo, kwa kanuni
zilizowekwa zinazojifanya kuonekana kama zinashabihiana na kuwezekana kuzitunza
kwa mujibu wa sheria na amri za Mungu lakini zinazipinga nyingi zake na na
kuizuia au kuinyima nafasi Sabato ya Mitume wa Kiyahudi, na ndipo nguvu kubwa
ya upotevu itawaingia wengi na huyu Mtu wa Kuasi atajiimarisha kwa kusaidiwa na
mafundisho potofu ya hawa Waantinomia na kusaidiwa na Wakristo Waliokengeuka na
Wayahudi Waliokengeuka na kuasi.
Amri za Mungu
Amri aliyotoa
Kristo ni kuvumilia hadi mwisho kwa uvumilivu wote na
watatambulika kwa kuvumilia kwao utakaotokana na kuzitunza kwao amri za Mungu
na imani ya ushuhuda wa Yesu Kristo. Walichoahidiwa ni
kuwa na amri ya kuula mti wa uzima na kuingia kwenye Mji wa Mungu.
13Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho
ndiye atakayeokoka.
12Hapa ndipo penye subira na uvumilivu wa
watakatifu, yaani, wale wanaozishika amri za Mungu na kudumu kuwa waaminifu kwa
Yesu.
14“Wamebarikiwa wale wafuao nguo zao, ili wapate haki ya kuuendea huo mti wa uzima na kuuingia huo
mji kwa kupitia kwenye malango yake.
Amri
ya Mungu inaendelea tangu mwanz
17Yesu akamjibu, “Mbona
unaniita mimi mwema? Hakuna aliye mwema ila Mmoja tu,
ndiye Mungu: Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.”
Zaburi 9-15 ni sehemu iliyo kwenye kundi la Zaburi inayojiri kumwelezea “Mtu wa Dunia.” Inafuatiwa na Zaburi 8 inayoishia na wazo-dhana ya kumtaja Mwana wa Wuasi: Aliyerudiwa.
Kitabu cha kwanza cha Zaburi hufananishwa na kitabu cha Mwanzo, 1-41.
Zaburi 1-8 inahusu Mwana na Mwana wa Adamu;
Zaburi 9-15 inahusu Mtu wa Dunia (Mpingakristo 10:18);
Zaburi 16-41 inahusu Mwanadamu Yesu Kristo.
Zaburi 9 inahusu Mtu wa Kuasi (Kwa Ujumla).
Zaburi 10 inahusu Mtu wa Dunia (Kwa ujumla wake).
Bullinger anaandika maoni yake kuihusu Zaburi hii ya 9 na 10 (ambayo kwa mujibu wa nakala ya Sptuagint ni sura moja tu). Ni zaburi yenye mshabihiano usio wa kawaida. Barua saba zimerukwa miongoni mwa mbili hizi. Alfabeti imevunjika na inaonekana visivyo kawaida kusomeka “kuhusiana na kipindi cha taabu na mateso.” Ni dhiki kuu inayoongelewa hapa. Somo moja limeenea kote.
Kipindi cha Mateso na Dhiki kimeelezwa katika sura na aya ya 9:9 kama kilivyotajwa kwenye Mathayo 24, Yeremia 30 na Zaburi 10:1 na inaonekana kwamba mwana huyu wa uharibifu atakuwa na sehemu yake pia katika kipindi hiki. Zaburi ya 9 na 10 zimewekwa kwa kanuni ya kiuandishi wa pamoja, na kila beti ya pili huanza kwa herufi iliyoimgizwa ya pekee ya alfabeti ya Kiebrania, mazingira yanayosaidia kuhesabia upungufu utokanao na kile kinachoonekana kuwa ni mwendelezo sanifu. Hata hivyo jambo hili linahitaji kulifanyia juhudi ya makusudi ya kulisoma ili kulijua jinsi lilivyo na kujua uhusiano wwke ulivyo na huyu mtu wa kuasi. Inaonekana kwamba mfumo wake umeungamanishwa pamoja kwenye mlolongo wote ulio kwenye taratibu za kishetani na ndipo huyu Mtu wa Kuasi atakapopewa uweza na Mpingakristo.
Zaburi 9:3-10 inaelezea jinsi uovu utakavyokomeshwa. Mlolongo wake utakuwa ni kukomeshwa kwake, hukumu na kusomewa kwake tena hukumu, na kukombolewa tena.
Mtu huyu wa Kuasi ameandikwa kwenye Zaburi ya 9:5, 16 na 10:2, 4, 13, 15 na kwa mujibu wa neno la Kiebrania lililoko kwenye kitabu cha fafanuzi cha SHD 7563 linaitwa “rasha” ambalo maana yake ni uovu au uhalifu kama inavyoweza pia kumaanisha ifuatavyo:
a) mwenye hatia, mwenye hatia ya uhalifu (mwalifu)
b) mwovu (mwenye kumchukia Mungu)
c) uovu, hatia ya dhambi (kumtenda Mungu au Mwanadamu) kwa mujibu wa kitabu cha fasihi namba 7561 neno linaonyesha kuwa mwovu, kufanya matendo maovu
a) kupenda ugomvi (Qal)
1) kuwa mwovu, kufanya matendo maovu
2) kukutwa na hatia, kulaumiwa
b) kujikunyata kwa aibu (Hiphil)
1) kuhukumiwa kwa hatia iliyofanyika (kwenye mahusiano ya kijamii)
2) kushitakiwa
3) kutenda maovu kinyume na maadili ya kidini)
Kwa maneno mengine ni
kwamba, kuziasi amri na sheria za Mungu ni kufuata ikikadi za Mpingakristo na
tendo hili amelielezea
Unaposoma kitabu chake, utaona kwamba amemtaja
huyu mtu wa kuasi akilinganisha na aya za zaburi sura
ya 9:6, 15. Ni muhimu
Kwa mujibu wa lugha
ya Kiebrania, Zaburi 9:9 na 10:1 inasomeka ukitaja hii
Zaburi 10:15 inasema Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya, mwite atoe
hesabu ya maovu yake ambayo yasingejulikana. na inahusiana
pia na Wachungaji wanaovitumikia Vinyago waliotajwa kwenye Zekaria 11:17.
Wale ambao hawajamsahau Mungu na wamebakia wanyenyekevu wanakumbukwa.
Zaburi 11 ni Maombi yenyemwonekano sawia na Zaburi 9 na 10.
Zaburi 12 inahusu Ubatili wa Mwanadamu.
Aya hii inafananisha pia na maneno ya udanganyifu wa mwanadamu na ule wa mtu wa kuasi aliyeko hapa duniani dhidi ya wateule waliosafi wazishiko amri za Mungu ambazo ni kamilifu.
Zaburi 12:6 inasema kuwa maneno ya Bwana ni maneno
Zaburi 13 ni maombi yenyekufanana tena na Zaburi 9 na 10. Aya za 1-4 ni maombi, aya za 5-6 ni sifa kwa Mungu.
Zaburi 14 inahusu Ukengeufu wa Mwanadamu na Zaburi 15 inahusu Ukamilifu wa Mwanadamu.
Huu ni mfano mwingine wa huyu Mtu wa Kuasi au Mtu wa Ukengeufu; ambaye pia ni Mpingakristo na mfumo wake wa Kiantinomia na mtu mkamilifu atakayeshinda na na kujivunia kwa kujigamba kwa ajili ya mfumo ule wa ukengeufu au wa Kiantinomia.
Mkakati wa
Waantinomia unaotokana na Imani ya watu wa imani ya Wakanamungu maarufu
Zaburi 14 inasema Mpumbavu anasema moyoni mwake, ‘‘Hakuna Mungu.’’ Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa, hakuna atendaye mema. Neno maovu limetumiwa hapa likimmanisha hali ya watu kujiharibu kwa kuzivunja amri za Mungu, na kwamba hakuna mtu aliyesafi, hakuna hata mmoja. (imeongezwa kutoka kwenye sura ya LXX).
Je, wanaofanya maovu wote hawajui kuwa wanafanya hivyo, au ni kweli kwamba hawajau kabisa kwamba wanakosea au hawazijui kabisa amri za Mungu?
Aya ya 6 inamaanisha kwamba watu hawa wamelidharau na kulipuuzia mashauri ya wale waliodhumuliwa ambao waliwadhulumu na kuwatesa. Kwa maneno mengine ni kwamba waliyapuuzia mashauri ya wateule na kuzidharau Amri za Mungu na kujiharibu wao wenyewe kwa kuwatesa wateule.
Zaburi 14 inashughulika na
hukumu ya walio kwenye kizazi cha wabezaji na waovu. Mjinga anayetajwa hapa sio
wale wenye tabia za kupuuzia mambo tu au wasiojua mambo, bali
ni wale ambao wamejiingiza kwenye atendo maovu kwa kiasi kikubwa mno na
kupotoka matendo
Andiko hili linatuonyesha kuwa Mungu anawarudisha waliopelekwa utumwani walio wake na kutoka uzao wa Israeli na Yuda ambao kwa pamoja watafurahia kuwa pamoja na kwa umoja.
Zaburi hii inaonekana kufanana na Zaburi ya 53 iliyolitaja neno Elohim mara tatu na Yehova mara nne hapa na jina la Elohimu limetajwa mara saba kwenye Zaburi 53) dika three Elohim and four Yahovah here) and seven x Elohim are used in ps. 53). Zaburi 53 ipo kwenye kitabu cha Kutoka na inamtaja pia Yakobo na Israeli.
Zaburi 15 inaunda andiko
lililotumika kwenye hotuba ya Mlimani (Mathayo sura 5 hadi 7). Inauhusiano na tangazo la Ufalme wa Mungu na
sio Kanisa la Mungu.
Mtu mkamilifu huzitii zmri za Mungu na hatazidharau.
Mambo yanayofuatia kutoka kwenye Zaburi 16 hadi 41 zinamtaja Yesu Kristo. Zaburi 16 inaelezea jinsi atakavyopokea sadaka zake.
Huyu Mtu wa
Kuasi ni Mpingakristo ambaye anajulikana wazi, na mfumo wake inajulikana, na
dalili zao ni itikadi yao ya kuzikataa amri za Mungu na wameyaeneza mafundisho
yao na kuwaharibu Wakristo na kudhoofisha maundisho ya kweli kwa kipindi cha
karne nyingi sana hadi sasa. Lakini mwisho wao umefika.
Hawa Waantinomia watakatiliwa mbali na kufutiliwa
mbali na Masihi hapo atakapokuja.
q