Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[014]
Zaburi 8
Toleo La 1.0 20000907-20000907)
Zaburi
8 ni sura muhimu kwenye maandiko ya kinabii na inatumika kumhusisha Masihi na
ni ya mhimu sana katika kuielewa Asili ya Mungu, Malaika wa Mbinguni na
uhusiano wao na Masihi na Mwanadamu kwa ujumla.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati
Miliki © 2000 Wade
Cox)
(tr.
2015)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Zaburi 8
Kwenye Yohana 5:18 tunaliona
andiko zuri saa.
Yohana 5:18 Basi kwa
sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu,
bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi
Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,
Maneno aliyoayasema
Kristo kuwaambia viongozi wa Wayahudi wa siku zile, yanaonysha kuwa walielewa
kuwa Elohim aliyetajwa kwenye Agano la Kale na aliyempa Torati nabii Musa,
alikuwa ni Malaika Mkuu, ambaye alikuwa pia ni mmoja wa wana wa Mungu.
Walilielewa pia andiko la Zaburi 45:6-7: lisemalo "Kwa hiyo MUNGU, Mungu
wako, amekupaka mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako" kuwa linamlenga
Masihi, ambaye alikuja na kuwa Mwana wa Mungu. Hii hatimaye imetokana na andiko
la Kiebrania, pia kwenye Waebrania 1:8-9, ambaye anachukuliwa kuwa ni elohim
mdogo au Kristo.
Mithali 30:4-5 inauliza swali ni kama lilivyo jina la Mungu na lililo jina la
mwana wake, na kisha inalipa jina Mungu wa Pekee wa Kweli kwa umoja kwenye aya
ya 5; imwitayo, Eloa.
kwa Kikaldayo, huyu alikuwa ni Elahh. Uwingi wake ulikuwa Elohim
na Elahhin kwa Kikaldayo.
Toleo hili la kimashariki la lugha, ambalo kikiujakuwa Kiaramu cha Kimashariki
na hatimaye likawa la Kiarabu, ndiyo sababu inayowafanya Waarabu kulitamka jina
la Mungu Allah'; na herufi mbili za h zinafanyika kuwa kama kivutio au kitu cha
hamu.
Mahali ambapo lugha ya Kiyunani inatumia neno 'aggelos’ lilitafsiriwa kama
malaika kwa Kiingereza, lilitumika kama wana wa Mungu, au elohim, kwa
Kiebrania. Tafsiri ya Kiyunani ya Septuagint (LXX) na kwenye Agano Jipya pia.
Jambo hili
limejtokeza nje kwa uzuri sana kwenye Zaburi 8 na matumizi yake kwenye maandiko
ya Kiebrania na kwenye tafsiri ya LXX.
Zaburi 8:1-9 Wewe,
MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka
utukufu wako mbinguni; 2 Vinywani mwa watoto wachanga
na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe;
Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi. 3 Nikiziangalia
mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha; 4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata
umwangalie? 5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu;
Umemvika taji ya utukufu na heshima; 6 Umemtawaza juu
ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. 7 Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; 8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho
njia za baharini. 9 Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi
lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Zaburi 8:2a imenukuliwa kwenye Mathayo 21:16. Jina au neno babes huenda
ni rejea kwa kipindi chake cha ujana na huenda pia lililo kwenye 1Samweli
17:14,33, 42,55,56. Andiko linaelezea maadui
kuwa ni washitaki wake maadui na neno mlipiza kisasi hapa ni mtu wa
kisasi.
Zaburi 8:4,5,6 imenukuliwa pia kwenye Waebrania 2:6-8 kama "Mtu ni kitu
gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? 5 Umemfanya
mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; 6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote
chini ya miguu yake."
Andiko hili hapa
kwenye aya ya 4 linamtaja mtu mwenye kuweza kufa ‘enosh na ‘adam kwa Kiebrania.
Tunaona kwenye
Waebrania 2:9 kwamba ilikuwa inamaanisha mateso ya kifo ambayo tulifanyika
kwayo daraja la chini kuliko walivyokuwa wadogo kidogo. Bullinger alichukulia
usomaji wa “kwa kiasi fulani” kwa kuliona hivyo andiko hilo. Kwa hiyo
linafanana na la Wafilipi 2:5-8.
Wafilipi
2:5-9 Iweni na nia iyo hiyo
ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye
yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu
kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya
kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu,
alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Kwa hiyo, hakujaribu
kujifanya kuwa sawa na Mungu au kuasi ila alifanyika kuwa mwanadamu na
akajinyenekeza hadi mauti. Alifanyika kuwa Mwana wa Mungu mwenye uweza kwa
kufufuka kwake toka kwa wafu (Warumi 1:4), kama tuonavyo kwenye (Wafilipi 2:9):
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno,
akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
Sasa, nano hili
linaitwa malaika kwenye Zaburi 8 na
hata kwenye Kiebrania, kama tunavyoona kwenye Kiebrania elohim na
linamaanisha miungu. Lilitafsiriwa
kama ‘aggelos (kwa wajumbe) kwenye tafsiri
ya Septuagint, na pia kutokana hilo kwenye maandiko ya Kiyunani na kwenye
Kiebrania, na linarudia kwa namna hiyohiyo kwene tafslri za Vulgate, Kisyria na
Kiarabu. Lilitafsiriwa kama malaika
kwenye tafsiri ya Kiingereza. Sababu yake iliyodaiwa kwa maana hiyo ni kwamba
liliwapendeza watafsiri wa Kiebrania cha kiasilia ili kuwataja wajumbe kwa kuwa
ilikuwa inahusisha uwingi wa wana wa Mungu kama elohim, zaidi kuliko Eloah.
Waamini Utatu wamefuata hii kwa kumfanya kama “malaika” na kuliruka neno
lisemalo “kwa maana ya muda mfupi” na pia kwa maana iliyo kwenye Kisyria na
Kiarabu. Sababu inayoonekana kuwa kwamba hakuna mmoja wao aliye tayetaka kujua
kuwa hawa elohim walikuwa ni viumbe waliobeba majukumu ya ziada nay a zaidi.
Hata hivyo, andiko hili linaonyesha wazi kwamba etohim aliye kwene Kiebrania
asilia, na Bullinger anaandika hilo kwenye mandiko yake kwenye kifungu au aya
iliyo kwenye tafsiri iitwayo Companion Bible. Makuhani walijua kwamba mwana wa
mtu alikuwa ni elohim aliyefanyika kuwa Mwana wa Mungu akijulikana kwa Kiyunani
kama monogenes theos au mwana wa pekee wa Mungu kwenye Yohana 1:18 (sawa na
ilivyo kwenye tafsiri ya Kiyunani na Kiingereza iitwayo Marshall's Greek
English Interlinear RSV). Maandiko yaliyo kwenye tafsiri ya Companion Bible kwenye
maandiko yanayofafanua mambo haya.
Wanamhusisha yeye kuwa anajifanya kuwa sawa na elohim, na kama hili
halikuotajwa kwenye lugha ya Kiyunani, lakini ya Kiaramu, tunapata andiko hili
kama elohi ambalo linafanana na kama malaika.
wana wa Mungu wote walikuwa elohim kama yanavyoonyesha maandko ya Agano la Kale
kwa jinsi walivyotumika. Elohim hawa walijulikana kama 'aggelos, au wajumbe, na
walitafsiriwa kuwa malaika kwenye lugha ya Kiingereza na kwenye maandiko
mengine. Hata hivyo, makuhani wa Hekalu hawakujizuia na mapokeo ya kipagani ya
Warumi kwa kipindi cha karne kadhaa kwa kipindi hiki, na kwa hiyo walijulikana
kuwa wanaonyyesha dalili za wazi kabisa.
Neno wana wa mtu
(sio kisarufi) lililotumika kwenye Zaburi 8, limetumika mara tatu kabla ya
andiko hili kwenye Hesabu 23:19; Ayubu 25:6; na 35:8. Ni mara 111 kwa umoja
kwene Agano la Kale na mara 39 kwenye uwingi. Pengine ilipojitokeza ni kwenye
Zaburi (Zaburi 49:2; 144:3) ni nino linguine tofauti. Hapa kwenye Zaburi 8:4
jina hili la kicheo linamaanisha utawala au mamlaka ya kidunia, na linaiumika
kwa maana hiyo kwene maandiko ya Kiebrania likimaanisha kuwa ni Masihi.
Andiko lililo
kwenye Zaburi 8:6 linataja mamlaka aliyopewa mtu wa kwanza, Adamu, na ambayo
yaliangukia kwenye anguko lake. Utawala, au mamlaka na marejesho ndilo lengo la
wokovu ambao tunapasa kuutilia maanani sana na kuutunza kwa umakini wote. Idadi
yake kwenye aya za 7 na 8 ni vitu sita, ambayo ni tarakimu ya kibinadamu.
Waebrania 2:1-18 Kwa
hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa. 2 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa
imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki, 3 sisi
je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa
na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; 4 Mungu
naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa
magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe. 5 Maana
hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao tunaounena, ila mtu mmoja
ameshuhudia hivi mahali fulani, akisema, 6 Mwanadamu
ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie? 7 Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, Umemvika taji ya
utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; 8 Umeweka
vitu vyote chini ya nyayo zake. Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake
hakusaza kitu kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hatujaona vitu vyote
kutiwa chini yake. 9 ila twamwona yeye aliyefanywa
mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa
taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya
kila mtu.
Kwa hiyo,
alifanyika kuwa mtu na akafa ili kutupatanisha na Mungu.
10 Kwa kuwa ilimpasa
yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta
wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa
njia ya mateso. 11 Maana yeye atakasaye na hao
wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu
zake; 12 akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu
zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa. 13 Na
tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama,mimi nipo hapa na watoto
niliopewa na Mungu.
Anayatangaza
majina yetu kwenye makusanyiko ya elohim, na haoni haya kutuita sisi ndugu
zake.
14
Basi, kwa kuwa watoto
wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa
njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, 15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu
ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. 16 Maana ni
hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. 17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo
yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu,
ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. 18 Na kwa
kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
Sababu ya kwamba
Mungu hafananishi na elohim waitwao malaika hapa, bali pia kwamba wana walio wa
uzao wa Ibrahimu, ni wale waliochaguliwa ili kutufanya sisi kuwa makuhani, na
inahusiana na kutufana sisi kuwa hivyo kwa kupitia kwa Kristo.
Hapa tunaliona
andiko kwenye Waebrania liitajalo sheria iliyotolewa na malaika. Mtu au kiumbe
huyu aliyeitoa Torati na kumpa nabii Musa alikuwa Kristo, na alijulikana hivyi
na Kanisa la Kwanza kuwa ni Kristo.
Kwa hiyo hatua
yenyewe ilikuwa ni ya kuutunza wokovu mkuu kuliko ilivyowezekana chini ya
Sheria bila Roho Mtakatifu.
Ndipo hivyo
kwamba \Krisuo alikuja kuutangaza wokovu huu mkuu. Mitume ambao walimshuhudia
kwa macho yao waliutangaza hivyo. Ulikuwa umeshuhudiwa kwa uweza wa Mungu kwa
njia ya Roho Mtakatifu kwa ishara na maajabu kwa kile tunachokiita leo kuwa miujiza.
Kwenye andiko
hili tunauona sasa ukweli, kwamba mamlaka au uweza wa kuutiisha ulimwengu ujao
hayakuwa yamepewa elohim kama malaika. Bali yalitolewa na akapewa Kristo kama
Mwana wa Mtu, na kwa wanadamu, ili tuweze kuonyesha uwezo wetu wa kuuingia
wokovu chini ya Kristo.
Hakuna mtu yeyote
awezaye kwenda kwa Baba isipokuwa Kristo.
Ilimpasa Kristo
afanyike mwanadamu, na kuonyesha utii wake na kutostahili kutuongoza sisi
kupitia mauti. Kwa kuwa kwa sisi, kuipata kwetu haki ya kuwa warithi pamoha
naye, kulilazimu kuwe na kifo kwanza cha mtu anayeweza kuitoa faida au hali
ile, aliyopewa na muumbaji kama mamlaka makubwa zaidi.
Tutawahukumu
malaika (1Wakorintho 6:3). Mapepo watahukumiwa na sisi katika ukamilifu wa dahari.
Ndipo nao watapatanishwa kwa kupitia Kristo.
Hiki ndicho
walichukuwa wanakitarajia kujiepusha kwa mapatano na kuyapatanisha Mapepo kwa
kila mtu kwa njia ya dini potofu za siri. Kama ingelikuwa hivyo basi
wangelibakia mbinguni bila kuhukumiwa.
Pia ni kwa mtazmo
huu kwamba yeye aliyejitoa sadaka, na wale waliotakaswa wana upya wa asili.
Hivyo, ilimpasa afanyike kuwa mwanadamu kutoka kwenye hali yake ya elohim na
afe, ili kufanya kuwe na utakaso wa wote wawill, yaani mwanadamu na elohim, au
mwanadamu na malaika, ili wapatanishwe na Eloah, ambaye anafanyika kuwa kiini
cha wote na ndani ya yote na katika yote (Waefeso4:6).
q