Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[021B]
Ufafanuzi wa Kitabu cha Yoeli
(Toleo La 1.0 20140903-20140903)
Nabii Yoeli anashughulika na kuwaandaa wateule hasahasa wale wa \Masihi na
katika siku za mwisho. Huduma yake ina mambo muhimu yahusuyo utakaso wa kusanyiko
la Israeli kama Hekalu la Mungu na inafuatiwa na maneno a matendo ya kusifia
maandalizi ya maandiko ya nabii Ezekieli. Bullinger anakifananisha kitabu hiki
na cha nabii Ezekieli katika mwaka wa tano wa Yehoyakini kuwa utumwani lakini
hakikujulishwa tarehe wala mwaka wake. Marabi wengine wanakiweka kitabu hiki
mahali pengine popote. Wataalamu wa kanuni za maandiko wanakiweka kitabu hiki
katikati ya Hosea na Amosi.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 2014 Wade Cox)
(tr. 2014)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Ufafanuzi
wa Kitabu cha Yoeli
Jina Yoeli maana yake ni “Bwana ni Mungu” na lina maana sawa na lile la
Eliya.
Mapokeo yanahuasiana kati ya Hosea na Amosi kwenye Karne ya 8 KK,
kwa hiyo amekubalina na utaratibu wa kikanuni wa maandiko. Kiteolojia kitabu
chake kinahusiana na nabii Ezekieli na kinaonekana kuwa kinahusiana na mambo na
matukio yanayolingana.
Kitabu cha Hosea kilikuwa kinashughulikia makosa na hatia ya Israeli.
Kitabu cha Yoeli kimeegemea kwenye matukio ya dhiki yaliyowakumba Yuda kwa
ajili ya mafundisho yao ya uzushi na makosa kwa wakati huo na katika siku za
mwisho. Kinabeba mrejesho na kulitaja Helaku la Mungu katika Siku za Mwisho
chini na huduma yake ambayo ni Kanisa la Mungu. Mfululizo huo kwenye utaratibu
wa Kikanuni kwa vyovyote vile, hakuna sababu ya kudhania kuwa kiliandikwa na
nabii Hosea. Kinahusiana
na muundo wa kama;
Tunaona kurejea kwa Yuda huko Sayuni na Mungu anayashughulikia mataifa.
Haya yalikuwa ni maelekezo au maongozi kutoka mbinguni yaliyotoka kwa Mungu
mwenyewe akampa nabii Yoeli kama tunavyoona tangu aya ya 1. Ni jinsi ileile ya
jinsi Mungu alivyomtuma kwa Daudi kwenye Zaburi na maelekezo yake kama
tunavyoona kwenye Matendo 1:16. Maandiko yote hayawezi kutanguka (Yohana
10:34-36). Inatokea na itaendelea hadi kwenye siku za mwisho na kwenye kipindi
cha Milenia. Hekalu la Ezekieli la Milenia ambalo Yoeli anaendelea hadi kwenye
Milenia na Marejesho ya Yuda na Zekaria yanaonyesha kile kinachokwenda kutokea
mbele na kutoka Yerusalemu kwayo na kutoka kwenye marejesho ya Milenia.
Ni pasipo shaka kabisa msingi wa uhasama au uadui kamili ya Hadithi za
Kiislamu ya Waarabu kwenye Biblia na mafundisho ya kizushi ya watu wa Palestina,
Gaza na Lebanoni na Waarabu kwa ujumla katika Misri. Inaweza kuwa tayari na
maandiko mengine ya manabii katika kuona sawasawa jinsi Yahova atakavyorejesha upya
na kuwashughulikia Wamisri na wana wa Shemu pia.
Yoeli.1
1 Neno la Bwana lililomjia Yoeli, mwana wa
Pethueli.
Kwamba Mungu sasa anatangaza
kile anachokwenda kukifanya katika Siku za Mwisho na baada ya hapo kwa kupitia Yahova
wa Israeli (Kristo) kama tunavyoona kutoka kwenye Zekaria 2:1-9. Anasema kwa
watu wa kale wa Israeli wanaokumbuka, zaidi kuliko wazee rasmi wa baraza la
Sanhedrin, na kwa wakazi wa nchi, wote wawili, yani vijana kwa wakubwa, wanaume
kwa wanawake. Mungu anawapa changamoto na kuwaonyesha kuwa haijatokea wakati
alipowaandikia, yaani huenda ilikuwa chini ya Wababeloni lakini kabla ya
maangamizo.
2
Sikieni haya, enyi wazee; Sikilizeni, enyi wenyeji
wote wa nchi. Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu, Au katika siku za
baba zenu? 3 Waarifuni watoto wenu habari yake, Watoto
wenu wakawaambie watoto wao, Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine.
Kwa hiyo, unabii huu ulipaswa kutolewa
kutoka kizazi kimoja hadi kingine na ulikuwa ni kwa wakati cha mbali kwa siku
za mbele.
4
Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na
yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na
madumadu. 5 Levukeni, enyi walevi, mkalie; Pigeni
yowe, ninyi nyote mnywao divai; Kwa sababu ya divai mpya; Maana umekatiliwa
mbali na vinywa vyenu.
Maneno yasemayo Ninyi nyote mnywao
divai ni sahihizaidi kama vebu inayoifanyiza nauni. Haimaanishi kwamba
unywaji bali zaidi ni kwamba inamaanisha wale wanaoupenda mvinyo.
Unabii unasema na kutangaza maangamizo ya Israeli na Walevanti kwa sababu
ya vita. Nzige walionyesha ia kuwa ni kama ishara ya majeshi ya Kaskazini kwenye
Vita wakati kwamba hawa nzige hawakuja kiasili kutoka Kaskazini. Aina ne ya
nzige walisemekana na Karaite mfafanuzi wa Jepheth b. Ali kwenye ishara ya
mashambulizi manne ya Yuda ambayo yalikuwa kila mojawapo ni kubwa zaidi ya
lililotangulia mwanzo na hii ni huenda ndiyo maana hasahasa kwa matumizi ya neno
Ha Tsephoni linalomaanisha “atokaye
Kaskazini” kwenye sura ya 2:20. Tafsiri ya Soncino inaonyesha na kuandika hivyo
pia. Hesabu yaje ya tarehe, hata hivyo, inachukuliwa kuwa ni uwongo mtupu kama
sehemu yake kwenye kanuni ya maandiko yalisaidia kutoka kwenye mtazamo wa
waandishi wa wakati wa kina Ezra na Nehemia wakati ilipodhaniwa kuwa
iliandikwa. Wanazuoni wa siku hizi wanaiweka hii kwenye siku za baadae, kama
wanavyofanya kwenye nabii nyingine zote, kwenye mahali pa baada ya matukio
yanapotokea. Hata hivyo, hawawezi kufana hivyo kama ilivyoelezewa na Masihi nah
ii bila shaka iliandikwa vizuri kabla ya kufungwa kwa baraza lililoshughulikia
Kanuni ya kuyatambua maandiko sahihi mwaka 323 KK.
Yuda ilishambuliwa na kushindwa na Wamisri na Wababelini na Waajemi pia
wakawatawala lakini waliwaruhusu kulijenga Hekalu kipindi cha Dario II Mwajemi
na utoaji wa kuwezesha ujenzi na aaliyetoa agizo hilo alikuwa ni Artashasta II kwa
marejesho na matengenezo waliyoyafanya kina Ezra na Nehemia (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa
Hekalu (Na. 013).
Maangamizo makubwa yaliyowakumba na kuwatawanya Yuda ilikuwa ni Vita yao na
Warumi na maangamizo ya Hekalu ya mwaka 70 BK (soma jarida la Vita na Warumi na Kuanguka kwa Hekalu (Na. 298)). Waedomu walitokomezwa katika Karne ya
Pili KK kama ilivyotabiriwa mapema na nabii Obadia. Esau alikatiliwa mbali kama
taifa na kuangamizwa kwa kuondolewa kabisa kwenye Mlima wa Edomu. Walishindwa
vita na kuangamizwa na John Hyrcanus chini ya Wamakabayo na alichukua vyote katika
Yuda. Hawa walifanyika hatimaye kuwa ni jeshi kwa haki yao na wakatawala Yuda
kama Waidumeans chini ya Herode baada ya vita ya Actium aliyewafanya wawe watu
bora kutoka Roma. Alikuwa ni liwali wa mfalme wa Kirumi. Wanafikia sasa idadi ya
takriban theluthi moja ya Wayahudi wote wa tabaka la Hg J. Wengine wote ni
Waarabu.
6
Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu, Lenye
nguvu, tena halina hesabu; Meno yake ni kama meno ya simba, Naye ana magego ya
simba mkubwa.
Maangamizo
yaliyosababishwa na Warumi yalikuwa ni makubwa hasahasa kitendo cha kuifanya
nchi kuwa msitu na maganjo kwa kazi ya kuizingira iliyofanywa.
7 Ameuharibu mzabibu wangu;
ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini;
matawi yake yamefanywa kuwa meupe.
Marudio yaliyo kwenye aya za
8-12 ni mwito wa toba. Aya za 13-20 ni mwito wa toba.
8
Ombolea kama mwanamwali avaaye magunia Kwa ajili
ya mume wa ujana wake.
Sadaka au dhabihu ya daima
iliondolewa mbali mwaka 70 BK na sadaka ya nafaka na vinywaji ziliondolewa. Kisha
Hekalu lenewe liliangushwa na kuharibiwa kukafuatia na baa kubwa la njaa
iliyotokana na kuangamizwa kwa vinu vya kusagia kwa ajili ya vita kubwa ya
Wayahudi wenyewe ndani ya mji. Ulikuwa ni unabii ambao walikuwa wanautimiliza
wenyewe ndio ulikuwa unatimilika.
9 Sadaka ya unga na sadaka ya
kinywaji Zimekatiliwa mbali na nyumba ya Bwana; Hao makuhani, wahudumu wa
Bwana, wanaomboleza. 10 Shamba limeharibika, nchi
inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.
11 Tahayarini, enyi wakulima; Pigeni yowe, enyi
watunzaji wa mizabibu; Kwa ajili ya ngano na shayiri, Maana mavuno ya mashamba
yamepotea. 12 Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia; Nao
mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam, miti yote ya mashamba imekauka; Maana
furaha imekauka katika wanadamu.
Kuharibiwa kwa ardhi ya watu
wa Yuda na Wapalestina lilikuwa ni tukio la kimsingi linaloendelea hadi kufikia
Karne ya Ishirini. Yuda ndio walikuwa walengwa na walitawanywa ulimwenguni
kote. Taifa likaenda utumwani na kuwa kwenye mateso ya Warumi Wakatoliki tangu
hapo hadi kufikia Vita Kuu ya II ya Manazi. Kukawa hakuna nah ado halipo hata
sasa Hekalu katika Yuda. Hekalu pekee lililoko ni lile lililojengwa na Kristo
mwaka 27-30 BK na ni Hekalu la Mawe Yaliyohai.
13
Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe,
enyi wahudumu wa madhabahu; Njoni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi
wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji
Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.
Njia pekee nje ya utumwa huu ilikuwa
ni kwa huduma ya watu wa Mungu anayefanya kumuitaka au kumuomba Bwana. Ilipaswa
ifanyike kwa mambo mawili. Jambo la kwanza lilikuwa ni mchakato wa Utakaso na
wa pili ulikuwa ni tangazo la Kutaniko Takatifu kwenye Bodi ya Wateule na
Kutaniko la Israeli. Mfululizo wa Kwanza wa utakaso ulikuwa chini ya Masihi
tangu mwaka 27 BK hadi 30 BK wakati alipoanza mchakato wa Utakaso pamoja na
mitume na akalisafisha Hekalu kabla ya kuingia kwake mjini Yerusalemu akiwa
kama Mwanakondoo aliyetengwa mbali siku ya 10 ya mwezi Abibu. Tangu mwaka 30 KK
kipindi cha Miaka 40 kwa ajili ya toba ya Yuda yalianza na kuishia mwaka 70 BK.
Mlolongo huu wa mambo unafanyika pia katika siku za mwisho kwa ajili ya
kulitakasa Hekalu la Mungu, Hekalu ambalo ni sisi. Utakaso wa Hekalu umeagizwa na
Torati na unapasa uanze kuanzia siku ya 1 Abibu na kuendelea hadi siku ya 7
Abibu sawasawa na maelekezo ya Mungu yaliyonenwa na nabii Ezekieli (Ezekieli
45:20). Utakatifu wa watu au makutaniko matakatifu yafanywa kwenye Sikukuu,
Miandamo ya Mwezi Mpya na Sabato za Bwana (Ezekieli 45:17) na inaanzia kutoka
Siku ya Kwanza ya Mwezi wa Kwanza wa Abibu (Ezekieli 45:18). Hii inafanyika
kwenye mchakato wa ujenzi hadi kwenye Pasaka ambayo inafanyika kwa mlo wa Meza
ya Bwana siku ya 14 Abibu jioni. Inaandaliwa na kuadhimishwa kwa mahudhui ya
kukumbuka dhabihu ya Kristo jioni inayofuatia kama Mwanakondoo wa Pasaka. Hata
hivyo, utakaso unahitajika na Utakaso huu wa Kusanyiko ni lazima uambatane na
mfungo wa saumu kama tunavyoona kwenye kitabu hiki cha Yoeli, na Ezekieli
anatuambia kwamba wale ambao hawajui mema yoyote au wanaofanya makosa au
wasioelewa mchakato wa Hekalu kama vile saumu Fupi nay a kuyatubia Makosa au
dhambi zilizofanywa Kimakosa au pasipokujua, ni lazima wafunge saumu ili kwamba
kusanyiko lote liwe limetakasika kwa ajili ya maadhimisho ya Pasaka.
Kwa maneno mengine, sisi tunaweza kuwa sehemu ya suluhisho au tunaweza kuwa
ni sehemu ya tatizo. Sisi tu sehemu ya wateule wanaofunga saumu kwa ajili ya
watu ambao hawajui lolote la maana au tunaweza kuwa sehemu ya watu ambao
hawajui jema lolote. Hii ni amri ya moja kwa moja kwenye huduma ya Mungu katika
Siku za Mwisho katika kuliandaa Hekalu la Mungu liwe tayari kwa maombi na
kufunga saumu, Hekalu ambalo ndiyo sisi.
Kristo alistahili kuanzisha mfumo ambao uliweza kulitakasa kusanyiko
kufanya hivyo. Kipindi hiki cha utakaso sio cha upambanuzi. Kanisa la Mungu
lisilofanya havi halitakipata Kinara cha Taa cha Siku za Mwisho na Mungu
ataiuinua sehemu nyingine ya Mwili wa Kristo au kanisa.
Mchakato wa utakaso katika kulijenga hadi Pasaka wakati wote inahusu
mchakato wa kufunga saumu katika utakaso na wateule walifunga saumu mara nyingi
kwenye mchakato huu na ni ndiyo maana uliitwa na kanisa kuwa ni mwezi wa
kufunga saumu na ulikuwa ni mwezi wa majira ya baridi kama ilivyo Ramadan ya Waislamu
hadi ulipogeuzwa na kubadilishwa kimakosa na maandiko wanayoyaita Hadithi.
14 Takaseni saumu, iteni
kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa
Bwana, Mungu wenu, Na kumlilia Bwana,
Mchakato wa utakaso umeonekana
kutoka nyakati za kale zaidi za huko nyuma kama siku za Ayubu (Ayubu 1:5) ambaye
aliwatakasa watu wa familia yake kutokana na makosa au dhambi zao. Dhahibu
hazihitajiki tena, kwakuwa zimetimilizwa na Kristo lakini Utakaso kwa njia ya
kufunga saumu bado unahitajika na wakati wote umekuwa ukihitajika.
Mchakato huu wa Utakaso unaonyesha na kuhitajika kufanywa na wateule mapema
sana kabla ya Siku ya Bwana na unahitajika kufanywa na wote wa Nyumbani mwa
Mungu. Kumbuka kwamba mchakato huu unatakiwa uanzie na Huduma ya utakaso na
kuitisha saumu. Wanahitajika kushiriki mchakato huu kwa kuitisha kusanyiko
takatifu. Sababu ya kufanya hivyo ilikuwa ni baada ya kuanguka kwa Wathiatira,
Wasardi waliinuliwa baada ya zama za Matengenezo. Wasardi hawakuelezea tena Mwandamo
wa miezi kama Wathiatira walivyoutunza. Hawakuadhimisha kipindi cha Utakaso na
adhimisho ekee walilolifanya kwa umakini lilikuwa ni Ushirika wa Meza ya Bwana.
Hawakuiadhimisha sikukuu ya Pasaka kwa kipindi chote kamili cha siku nane.
Kundi la mwisho la imani ya Wasardi liliibuka kutoka kwenye Kanisa la Mungu (la
Siku ya Saba) yaani, Church of God (Seventh Day) kundi lililoongozwa na Herbert
Armstrong. Huduma yake iliharibiwa na imani ya ki Ditheism na waliichukua na
kuiamini Kalenda ya Hilleli na kufanya isiwezekane kabisa kuziadhimisha Siku
Takatifu kwenye siku zake sahihi kutokana na kile kinachojulikana kama mapokeo
ya kuahirisha. Wakati mwingine wanashindwa kuziadhimisha hata kwenye miezi yake
sahihi. Makundi yaha yote mawili, yaani makanisa ya mrengo huu na Wayahudi ni
mara chache sana wanamudu kuzishika sikukuu hizi kiusahihi na kanisa la WCG na
imani yake waliachana na kuadhimisha siku zote nane kamili za Sikukuu ya Pasaka
na Mikate Isiyotiwa Chachu katika mwaka 1965-1967. Kwa hiyo, ndipo
walipokipoteza kinara chao cha taa na wakatawanyishwa. Kwa hiyo mkosa haya
yapasa yaondolewe kutoka kwenye Makanisa ya Mungu mapema kabisa kabla ya kurudi
kwa Masihi kama ilivyotabiriwa hapa na nabii Yoeli. Itahitaji kuhusisha
ufungaji wa Saumu kama Utakaso na kuitisha Kusanyiko Takatifu la Pasaka na
Mikate Isiyotiwa Chachu.
15
Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya Bwana
inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi.
Aya hii inatoa kipindi maalumu kamili kama inavyofanya na kuonyeshwa kwenye
kitabu cha nabii Ezekieli. Kinafuatana pia na maafa katikati ya mataifa.
Utakaso pekee unaowezekana na Yuda ni kwa kupitia Mwili wa Kristo unaowezesha
mchakato huu katika Siku za Mwisho. Ujio wa \Mashahidi katika wakati ule watatoa
mwito kwa Yuda na Israeli na ulimwengu wote utubu.
16 Je! Chakula hakikukatiliwa
mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya
Mungu wetu? 17 Mbegu zinaoza chini ya udongo wake;
ghala zimeachwa ukiwa; mabanda yamevunjika; kwa maana nafaka imekauka.
Maafa haya yatafuatiwa na ukame ambao utaathiri kwa kiasi kikubwa malisho ya
nchi zetu.
18 Jinsi wanyama wanavyougua!
Makundi ya ng'ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya
kondoo yamepata mateso. 19 Ee
Bwana, nakulilia wewe; Kwa maana moto umeyala malisho ya nyikani, Na miali ya
moto imeteketeza miti yote ya mashamba.
Andiko linahusisha na kutokea kwa baa la asili la ukame na baa la moto
na maafa mngine kutokea ulimwenguni kote ambao utaathiri miti na wanyama wa
porini. Mlolongo huu wa matukio utaendelea na kuzidi na utakuwa kwenye kipindi
chote cha Mashahidi watakaohudumu huko Yerusalemu (soma jarida la Mashahidi pamoja na wale Mashahidi Wawili (Na. 135)).
Ni kipindi cha Baragumu la Tatu
kwenye Ufunuo na kisha kinaendelea hadi kwenye Kitasa cha Nne cha Ghadhabu ya
Mungu.
20 Naam, wanyama wa mashamba
wanakutwetea wewe; Kwa maana vijito vya maji vimekauka, Na moto umeyateketeza
malisho ya nyikani.
Hii inasababishwa na ongezeko la kiwango cha joto kitakachoamriwa kitokee
na ghadhabu ya Mungu. Wale wanaoitwa kuwa ni wanasayansi wanalaumu hali hii
kutokea kwenye harakati za wanadamu nah ii inasababisha hali ya joto. Kwa namna
ya kinyume chake hii ni sahihi kwa kuwa uasi wa wanadamu umechoza Hasira ya
Mungu iwaangukie. Ni kitu kinachoweka mzunguko lakini mzunguko huu Mungu
amewatuma malaika zake waimwage hasira ya Mungu kwenye jua ili lizidishe hali
ya joto kufanikisha mchakato huu (soma jarida la Mzunguko wa Kihistoria wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (Na. 218B)).
Mabadiliko ya Tabia Nchi yanayofanywa na binadamu ni shutuma za Kishetani
zilizohusisha wanadamu na mwenendo wake mbaya na utaelekea pabaya sana hadi
pale atakapotubu.
Sura inayofuatia inahusu ujio wa Siku ya Bwana
Yoeli 2
1 Pigeni tarumbeta katika
Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na
watetemeke; Kwa maana siku ya Bwana inakuja. Kwa sababu inakaribia; 2 siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu. Kama
mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano
wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi
vingi.
Vita vya Siku za Mwisho inaendelea kwenye majeshi yanayojumuishwa kwa
mitandao na maroboti na vifaa au silaha zenye uharibifu au maangamizi makubwa. Tunajua
kuwa majeshi ya Washami au Syria yanatumia silaha za sumu sasa na matumizi haya
yanaongezea umuhimu wake kwenye Vita vya Baragumu la Tano na la Sita. Mataifa
yenye silaha za Vita za Mfalme wa Kaskazini na Mnyama walikuja huko Mashariki
ya Kati kutoka Afghanistan mwaka 2001 na Iraq mwaka 2003 na anauandaa mwaka
2014 arudi tena huko Iraq. Ndivyo pia nchi ya Urusi ilivvyoivamia Ukraine. Wanaleta
maangamizo na uharibifu mkubwa. Ukosefu wa busara unaotokana na makosa ya
kimaandiko ya Uislamu wene itikadi kali unaleta maafa kwenye mataifa yale
yanayohusika kutokana na Malaika Wanne wanaoukausha mto Frati ambao wameamriwa
kuua theluthi moja ya wanadamu.
3 Moto unakula mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo
nchi inafanana na bustani ya Adeni mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu;
naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao.
Roboti hizi na vifaa
vya kiufundi vipo kwenye mchakato wa kutengenezwa kwa wingi sasa.
4 Kuonekana kwao ni kama
kuonekana kwa farasi; na kama wapanda farasi ndivyo wanavyopiga mbio. 5 Kama mshindo wa magari ya vita juu ya vilele vya milima,
ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto ilapo mabua makavu, kama
mashujaa waliopangwa tayari kwa vita. 6 Mbele yao watu
wanahangaika; nyuso zote zimegeuka kuwa nyeupe kwa hofu.
Ndvyo ilivyo pia
kwamba askari wanasaidiwa na vifaa hivi. Lakini vitendea kazl na maroboti
wanatumika kwa kiasi kikubwa sana siku hizi.
7 Hupiga mbio kama mashujaa; huupanda ukuta kama watu wa vita; nao
huendelea mbele kila mmoja katika njia zake, wala hawapotoshi safu zao. 8 Wala hapana mmoja amsukumaye mwenzake; huendelea mbele
kila mmoja katika njia yake; hujifanyizia njia kwa nguvu kati ya silaha, wala
hawaachi kuifuata njia yao. 9 Huurukia mji; hupiga
mbio juu ya ukuta; hupanda na kuingia ndani ya nyumba; huingia madirishani kama
aingiavyo mwivi. 10 Nchi inatetemeka mbele yao; mbingu
zinatetemeka; jua na mwezi hutiwa giza, na nyota huacha kuangaza;
Jeshi la Bwana
linatumwa liende likafanye uharibifu utakaosababishwa na huyu mnyama.
11 naye Bwana anatoa sauti
yake mbele ya jeshi lake; maana matuo yake ni makubwa sana; kwa maana yeye ni
hodari atekelezaye neno lake; kwa kuwa siku ya Bwana ni kuu, yenye kitisho
sana; naye ni nani awezaye kuistahimili?
Hata hivyo, Mungu
anaruhusu na anautaka ulimwengu utubu kwa maombi na kufunga saumu.
12 Lakini hata sasa, asema
Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa
kuombolea; 13 rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu,
mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma;
si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.
Anawataka watu watubu
hata baada ya kurudi kwa Masihi akiliongoza Jeshi la Mungu wanadamu hawatatubu
kama tunavyoona baada ya kila kufunguliwa Kitasa cha Hasira ya Mungu kilichoelezewa
kwenye kitabu cha Ufunuo kuwa kitamiminwa juu yao lakini bado hawatatubu (soma
jarida la Vita vya Siku za
Mwisho na Vitasa vya Ghadhabu ya Mungu (Na. 141B)).
14 N'nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma
yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa Bwana, Mungu wenu?
Kisha anaelezea
umuhimu wake wa kuitisha Saumu ya Kujitakasa. Tunaweza tu kujitakasa kwa
kufunga saumu. Dhana ya kwamba Kristo alifanya hivyo kwa ajili yetu ni upuuzi
wa kifikra kama saumu hii haikuitishwa tu kwa kipindi cha miaka 2000 baada ya
huduma yake lakini wakati atakaporudi tena kuja kutawala hapa duniani nab ado
yupo aliyaongoza majeshi ya Mungu. Mchakato huu unahitajika ili kwamba
ulimwengu wote ushiriki kwenye Kusanyiko Takatifu kwenye Kalenda ya Mungu (soma
jarida la Kalenda ya Mungu
(Na. 156)).
15 Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko
kuu; 16 Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko,
Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, Na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na
atoke chumbani mwake, Na bibi arusi katika hema yake. 17 Hao
makuhani, wahudumu wa Bwana, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na
waseme, Uwaachilie watu wako, Ee Bwana, Wala usiutoe urithi wako upate aibu,
Hata mataifa watawale juu yao; Kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao? 18 Hapo ndipo Bwana alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake,
akawahurumia watu wake 19 Bwana akajibu, akawaambia
watu wake; Tazameni, nitawaletea nafaka, na divai, na mafuta, nanyi mtashiba
kwa vitu hivyo; wala sitawafanya tena kuwa aibu kati ya mataifa;
Maandiko yaliyo kauanzia aya za 13-20 yanatumia maneno “Mungu wangu” na
“Mungu wenu” kana kwamba Mungu wa makuhani alikuwa ni tofauti na Mungu wa
manabii. Hivi ndivyo ilivyo kwenye siku za mwisho ambapo Mafundisho ya imani ya
Kiyahudi pamoja na imani ya Ukristo Mkongwe wa zamani na kwenye Makanisa mengi
ya Mungu yaliyopotoka ya iliyokuwa WCG na machipukizi yake.
Ni kwa toba ya watu
wake ambayo Mungu anapunguza hasira kwenye vuguvugu au harakati hizi yenye
madhumuni ya haraka ya kuwapelekea wao watubu na nyuma yao mataifa ya duniani.
Andiko linalofuatia linawataja walio upande wa kaskazini. Haya ni Majeshi
ya Kaskazini yaliyoandikwa kwenye Ufunuo 9 na Danieli 11, ambao ni nzige walioandikwa
kwenye sura ya 1:4. Nzige wa Waliotoroka hawatokei upande wa kaskazini bali ni
majeshi ya Kaskazini ndiyo yanayofanya hivyo.
.
20 lakini jeshi lililotoka kaskazini nitaliondolea mbali nanyi, nami
nitalifukuza mpaka nchi ya ukame na ukiwa; sehemu yake iliyo mbele itaingia
katika bahari ya mashariki, na sehemu yake iliyo nyuma itaingia katika bahari
ya magharibi; na uvundo wake utapanda juu, na harufu yake mbaya itapanda juu,
kwa sababu ametenda mambo makubwa.
Bahari ya Kusini ni bahari ya Chumvi (ambayo pia inaitwa Bahari Mfu)
(kama kwenye Ezekieli 47:18; Zekaria 14:8). Bahari yake kuu kabisa ni ile ya Mediterranean inayotia
maji au kuungana na Bahari ya Atlantic. Neno “zuia au epusha” lililoandikwa
kwenye Isaya 66:24. Hawa ni wale wagumu wa kutubu ambao hawatavishika Sabato na
Miandamo ya Miezi ya Mungu na ndiyo maana maadui zao wapo kule. Huwezi kuwa
sehemu ya wateule wa Mungu usipokuwa unazishika Sabato zake na Miandamo ya
Miezi (Isaya 66:23) na Sikukuu zake (Zekaria 14:16-19). Na inakupasa uwe na
sehemu kushiriki mchakato wa utakaso ukiwemo mfungo huu wa saumu.
21 Ee nchi, usiogope; furahi na
kushangilia; kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu. 22 Msiogope,
enyi wanyama wa kondeni; maana malisho ya jangwani yanatoa miche, na huo mti
unazaa matunda yake, mtini na mzabibu inatoa nguvu zake.
Dhana na wazo lililoko hapa ni
kwamba Yahova wa Israeli amejitukuza mwenyewe kwa kufanya mambo makuu; nchi itatengenezwa
na kufanywa upya baada ya Vitasa hivi vya Hasira ya Mungu.
23 Furahini, basi, enyi wana wa
Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya
masika, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya
vuli, kama kwanza.
Andiko hili linamaana ya kipimo
chake muafaka zaidi ya kumaanisha nyingi. Ipo kwa kipimo chake muafaka
kinachofaa kutumika kupimia mazao au mavuno.
24 Na sakafu za kupepetea
zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta. 25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na
parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu. 26 Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina
la Bwana, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu;
Ili kwamba hatimaye Mungu
aliwaleta na kuwaongoza kwenye toba. Ingawa kitend cha kuruhusu kuharibiwa kwa
mazao yao, aliifanyia marejesho mapya nchi yao.
Kisha anatoa ahadi kwamba atakuwa
katikati yao Israeli. Hawatatiwa kwenye
aibu au kuaibishwa tena. Huyu ni Yahova mdogo na msaidizi kwa Israeli aliyetajwa
kwenye Zekaria 2:1-9 na Zaburi 45:6-7 ambaye ni Masihi (Waebrania 1:8-9). Ametumwa
na Yahova wa Majeshi; Ha Elohim; Mungu.
Na
watu wangu hawatatahayari kamwe. 27 Nanyi mtajua ya
kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, wala
hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
Andiko linalofuatia linakwenda
nyuma kuelezea kinachofuatia baada ya unabii asilia kwa vizazi vinavyokuja. Hii
ilirudiwa kama unabii kutoka kwenye aya za 28 hadi 32a na Mtume Petro siku ya
Pentekoste wakati Roho Mtakatifu alipoletwa na kuwashukia wateule kwa kumpokea
kwao Masihi kama Mganda wa Kutikiswa (Matendo 3:18-26). Kama taifa lingetubu kama
ilivyoelekezwa na Petro matokeo yake yangekuwa ni tofauti kubwa sana. Maneno ya
manabii yangetimilika na Roho Mtakatifu angeweza kushuka kwa taifa na utaratibu
wa maandiko yanayofuatia yangeweza kutimilika pia katika Yuda. Ni kama
ilivyokuwa kwamba hawakufanya hivyo na walipewa miaka arobaini ya kutubu kwa
Ishara ya Yona na kisha wakazingirwa na Majeshi ya Warumi tangu siku ya 1 Abibu,
mwaka 70 BK na Hekalu likamoboshwa na Yuda wakatawanyika (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi tena wa Hekalu (Na. 13)).
Marejesho na Matengenezo
yaliyofanywa na kina Ezra na Nehemia na Nuru iliyowaka na kuenea kutoka kwa Masihi
(Isaya 42:7; Mathayo 4:12-16; Luka 2:32). “Siku za Mwana wa Adamu” ndipo zilikuwepo
(sawa na Luka 17:22). “Baada ya hapo” ni baada ya Marejesho yaliyoanzisha
mwanzo wa Siku za Roho kama zinavyoonekana katika Siku ya Pentekoste wakati
Yoeli 2:28-29 ilipoanza kutimilizwa. Hata hivyo, Kristo aliuawa na ni kama
ilivyokuwa kwa Yohana Mbatizaji. Malaki 4:3 kwa hiyo aliona mbele mbaali kwenye
ujio wa Eliya kaika Siku za mwisho.
Wanawake wamejumuishwa kwenye
jambo hili la karama za kiroho za Mungu pia. Wito wao na karama zao ziko
dhahiri kwa wateule pia (sawa na Hesabu 11:16,17,29).
28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba
nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake,
watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; 29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika
siku zile, nitamimina roho yangu.
30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika
mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.
31 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa
damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo. 32 Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la
Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika
Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika
mabaki, hao awaitao Bwana.
(maandiko yaliyokolezwa rangi yamerudiwa pia kwenye
kitabu cha Matendo; kama ilivyo pia kwenye Isaya 46:13; 59:20; Obadia 17; Zekaria
14:1-5; Waumi 11:26).
Tangu mwaka 30 BK, Roho Mtakatifu alitolewa kwa watu wa madaraja yote ya
watu wa Mungu, yaani kwa wazee, na kwa vijana. Kwa wote wanaotubu na kuti kwa
njia ya ubatizo na kwa sheria za Mungu pamoja
na kuwa na imani ya kutosha. Mungu atanena na kuwasiliana kwa jia ya ufunuo
kupitia ndoto na maono ambazo zilikuwa ni namna kuu mbili ya mafunuo ya kinabii
zilizotolewa hapo zamani kwa watu wachache sana miongoni mwa wanadamu kwa
makundi yote mawili, yaani makuhani na manabii.
Kristo aliufafanua mchakato huu kwenye aya ya 31 kuwa inafuatia mara moja
baada ya dhiki kuu ya siku za mwisho na itafuatiwa na ujio wa Masihi ulioandikwa
kwenye Mathayo 24:29; Marko 13:24; Luka 21:25 nk.
Baada ya kushindwa kwao kutubu Yuda mwaka wa 30 BK utaratibu wote
ulijielekezea wenyewe dhidi ya utawanyiko wao Yuda kwa kipindi cha Yubile 40 jangwani
kama walivyotumia miaka 40 jangwani naada ya tukio lao la Kutoka Misri. Ndivyo
pia Kanisa la Mungu lilipotumwa kule hadi katika Siku za Mwisho.
Kisha Mungu alitangaza kile atakachowafanyia wao (yaani katika Siku) za
Mwisho. Kipindi hiki kinajiri tangu siku ya 25 Kisleu mwaka 1917 kwa kipindi
cha tangu mwaka 2027 na kuendelea (soma jarida la Maneno ya Unabii ya Mungu (Na. 184)).
Yoeli 3
1 Kwa maana, angalieni, siku
zile, na wakati ule, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu, 2 nitakusanya mataifa yote, nami nitawaleta chini katika
bonde la Yehoshafau, na huko nitawahukumu kwa ajili ya watu wangu, na kwa ajili
ya urithi wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya
nchi yangu. 3 Nao wamewapigia kura watu wangu; na
mtoto mwanamume wamemtoa ili kupata kahaba, na mtoto mwanamke wamemwuza ili
kupata divai, wapate kunywa.
Katika siku hizo
inaelezea kipindi cha kupanua au kuweka kitambo cha unabii hadi kwenye hukumu
ya mwisho ya mataifa wakati Masihi atakapokuja tena katika utukufu wake (Mathayo
25:31-46). Neno la kuelezea kuhusu marejesho ya bahati hizi kwa kuwarudisha
tena watumwa kwa jinsi liliyotumika kwenye Kumbukumbu la Torati 30:3 (sawa
pia na 42:10; Zaburi 126:1,4; Ezekieli 16:53nk; Amosi 9:14). Ni sawa tu na kama
Kristo kuwachukua utumwani wafungwa au mateka. Hii ni idadi kubwa au kundi la
mataifa ya Ufunuo 21:24. (Nitawakusanya [pia] sawa
na Zekaria 14:2-4).
Mahali ambapo Yehoshafati (Yahova amehukumu) bado pamelindwa na kutunzwa
kwa jina la kijiji cha Sh’afat huko Wadi Siti Miriam au Wadi Far’aun iliyoko
kati ya Yerusalemu na Mlima wa Mizeituni. Hii itaenea hadi kwenye bonde wakati
wa kuja kwake Masihi. Yahova ataingia Kuwahukumu (sawa na Isaya 66:16; Ezekieli
38:22).
Mambo ambayo mataifa
waliwafanyia Yuda yataachwa vichwani mwao wakati wa hukumu kama tunavyoona
kwenye Mathayo 25 na sio kwa kuwahesabia haki kutokana na imani yao na ndiyo maana
sehemu ya pili inaelezea na kilichotokea kwa Watoro tangia kukomeshwa kwa nguvu
za Wafilisti hadi walipojitoa na kuwapa mamlaka Waarabu na kujichanganya kwao
kwenye makabila ya Waarabu. Ndiyo sababu ya makabila haya wanaitwa Wapalestina
hadi leo. Waarabu na mataifa waliotawanyika katika Yuda na pia wale
waliojichanganya kwa Wayunani na mataifa mengine watafanywa walipe
4
Naam, na ninyi ni kitu gani kwangu, enyi Tiro, na
Sidoni, na nchi zote za Filisti? Je! Mtanirudishia malipo? Au mtanitenda neno
lo lote? Upesi na kwa haraka nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu
wenyewe.
Tunaona kwamba katika kipindi
hiki kama Yuda walivyochanganyika na Wapalestina na Wayunani na Warumi na
kuuzwa nchi za ng’ambo, ndivyo pia wale waishio Gaza na Tiro na Sidoni na wa
Lebanoni wote watakavyo tawanyika kwa Wasabeani au Waarabu wa Sheba wa upande
wa Kusini Mashariki (kama ilivyo kwenye Ayubu 1:15; 6:19; Isaya 60:6), ilivyotokea
kwa kipindi cha millennia mbili za mwisho na sasa wanapaswa kuhamishiwa tena
kwa mwelekeo wa Ufalme wa Israeli utakaokuwa chini ya Kristo. Mungu atawaponya
majeraha yao Israeli na Yuda na kuwatoa kwenye mataifa yote ambako waliuzwa
kwayo (sawa na ilivyo kwenye Isaya 43:5,6 pamoja na 49:12; Yeremia 23:8).
5
Kwa kuwa mmetwaa fedha yangu na dhahabu yangu,
nanyi mmevichukua vitu vyangu vyema vipendezavyo, na kuviingiza katika hekalu
zenu; 6 tena watoto wa Yuda na watoto wa Yerusalemu
mmewauzia Wayunani, mpate kuwahamisha mbali na mipaka yao; 7 tazameni,
nitawaamsha wapatoke mahali mlipowauza, nami nitawarudishia malipo yenu juu ya
vichwa vyenu wenyewe. 8 Na mimi nitawauza wana wenu na
binti zenu, na kuwatia katika mikono ya wana wa Yuda, nao watawauzia watu wa
Sheba, taifa lililo mbali kabisa; kwa maana Bwana ndiye aliyesema neno hili.
Wakati huu Mungu aliyachochea
mataifa na kuwaleta chini kwenye bonde la kukata maneno.
9
Tangazeni haya kati ya mataifa; takaseni vita;
waamsheni mashujaa; watu wa vita na wakaribie; na wapande juu. 10 Yafueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe
mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari. 11 Fanyeni
haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande zote, jikusanyeni pamoja; na huko
watelemshe mashujaa wako wote, Ee Bwana.
Kumbuka kuwa mataifa yataletwa
chini mahususi kukutana na Jeshi la Mbinguni. Mgongano unaonekana kwenye
Danieli sura ya 12 mara moja na kwa haraka sana kufuatia vita vya Siku za
Mwisho.
12 Mataifa na wajihimize,
wakapande juu katika bonde la Yehoshafau; maana huko ndiko nitakakoketi
niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote.
Mungu anayaleta mataifa kwa
Yehoshafati ili kuyahukumu na kuyaangamiza majeshi yao na kisha kuyashughulikia
mataifa yasiyo na majeshi yenye silaha.
13
Haya! Utieni mundu, maana mavuno yameiva; njoni,
kanyageni; kwa maana shinikizo limejaa, mapipa nayo yanafurika; kwani uovu wao
ni mwingi sana. 14 Makutano makubwa, makutano makubwa,
wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya Bwana i
karibu, katika bonde la kukata maneno.
Maadui wa Mungu wanafananishwa kwanza na “mavuno yaliyoiva” ambayo wakati
wake wa kufyeka,
kisha kwenye “kipimo/kilichojaa tele” zabibu ambazo ulikuwa wakati wa kuvuna au
kupura. (sawa na Ufunuo 14:14-20, 19:15,18). Kwa hiyo Mungu atamtumia Kristo aende na kuuhukumu ulimwengu wote,
akiwashurutisha watubu kwa kutumia Vitasa vya Ghadhabu ya Mungu.
15 Jua na mwezi vimetiwa giza,
na nyota zimeacha kuangaza. 16 Naye Bwana atanguruma
toka Sayuni, atatoa sauti yake toka Yerusalemu; na mbingu na nchi zitatetemeka;
(kama kwenye Yeremia 25:30; Ezekieli 38:18-22; Amosi 1:2; mgurumo = radi)
Hata hivyo, kumbuka kuwa wanaokimbilia kwa Watu Watakatifu ni kwa Kristo
kwa uweza wa Mungu. “Mahali pa Salama” yuko mikononi mwa Mungu na sio mahala
pengine popote panapodhaniwa na mwanadamu (soma jarida la Mahali Salama pa Kukimbilia (Na. 194)).
Lakini Bwana atakuwa
kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli. 17 Hivyo ndivyo
mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu
mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena
ndani yake kamwe.
Nchi Takatifu inarejeshwa upya.
Panapowataja wageni wakipita kwenye mambo ambapo watu watakwenda huko maalumu
kwa malengo yaliyoelekezwa na Mungu kwenye unabii na chini ya maongozi lakini
hawata tangatanga tu ndani yake kama mahali pa kutumia. Ni Mahali Patakatifu.
Kuna tukio kubwa la Kutoka
kama lilivyotajwa kuwa litafanyika na nabii Isaya kwenye sura yake ya 65:17-25.
Watu Watakatifu watarejeshwa kwenye nchi kutoka ulimwenguni kote.
18 Tena itakuwa siku ile, ya
kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito
vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya Bwana,
na kulinywesha bonde la Shitimu.
Katika siku za mwisho Waislamu
wenye itikadi kali na mgawanyo wa Misri watasababisha dhiki kubwa kama inavyoonekana
sasa na itapunguzwa kwa hali ya umakini kama walivyokuwa Waedomu kwenye eneo
ambalo kwa sasa ni sehemu ya nchi ya Yordani. Masalia au mabaki ya Wafoinike.
19
Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu,
kwa sababu ya dhuluma waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu wamemwaga damu
isiyo na hatia katika nchi yao.
Mtafaruku utaisha kati ya mataifa na hasahasa Misri italipa kama watakavyofanya
Waedomu.
Haya sio matokeo ya mwisho kwa
iapo kama Misri au Edomu kama taifa la Misri itarefanywa upya na Masihi baada
ya Waashuru na Israeli wanaotoke upande wa kaskazini na kuifanya upya nchi kutoka
kaskazini ya mbali mwa Iraq kutoka Frati hadi Mto wa Misri na bahari ya Mediterranean
hadi kwenye Jangwa la Uarabuni linaloungana pia na nchi ya Yordani pamoja na Syria,
Gaza na Lebanoni. Taifa la Misri linafanywa upya na kuwa kama mshirika wa
Kusini ya washirika wake wa kibiashara wa mataifa matatu.
20 Bali Yuda atadumu milele, na
Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi. 21 Nami
nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana Bwana ndiye akaaye Sayuni.
Kwa hiyo wakosaji walio na
hatia watahukumiwa (kama inavyosema Kutoka 34:7; Hesabu 14:8; Waebrania. Nakah
haikutumika kusafishia. Tafsiri ya LXX nay a Wasyria zinaionyesha na kuitaja
hii “kuunda baraza ka mahakama ya kidini” kama kwenye 2Wafalme 9:7 na Waebrania.
Nakam ni kulipa kisasi kwanza Nakah).
Yahova wa Israeli kama Masihi kisha
anafanya makao yake katika Sayuni (Waebrania inasema Anakaribia kufanya
makao yake huko Sayuni). Ndipo inaishia kama inavyofanya Ezekieli 48:35.
Kwa hiyo ulimwengu unaendelea
kutoka Sayuni kama tunavyoona kwenye vitabu vya manabii Ezekieli na Zekaria (soma
jarida la Ufafanuzi wa Kitabu cha Zekaria (Na. 021K)).
q