Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[021E]
Ufafanuzi Wa Kitabu Cha Yona
(Toleo La 1.0
20140928-20140929)
Ishara ya Yona
ilikuwa ndiyo ishara pekee lililopewa Kanisa. Kwa hiyo ina umuhimu mkubwa sana
kwenye uelewa wa Imani.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 2014 Wade Cox)
(tr. 2015)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Utangulizi
Yona mwana wa Amitai ni mtu anajulikana kwa umahiri wake. Ametajwa kwenye 2Wafalme
14:25. Alikuwa ni mtu anayetokea huko Gath-hefa ambao ni mji wa mpakani wa huko
Zabuloni (soma Yoshua 19:13). Huenda unatajwa kwa pamoja na Khirbet ezZurra’ ambako
ni eneo kubwa lililo maili tatu Kaskazini Mashariki mwa Nazarethi, ambao ulikuwa
katika Galilaya. Maneno ya Mafarisayo kwenye Yohana 7:32 kwa hiyo yalikuwa
ni uwongo. Kristo alikuja akitokea kwenye eneo la Nazarethi katia Galilaya,
kama alivyokuwa Yona. Ilikaliwa katika Zama za Mawe awamu ya I na II yapata mwaka
1200-600 KK na kwa hiyo kwenye kipindi cha Yona na labla ya hapo kwenye kipindi
cha Mwishoni mwa zama ya Shaba tangu mwaka 1550 KK na kwenda mbele. Yona
alikuwa nabii aliyetabiri wakati wa Yeroboamu II mfalme wa Israeli (yapata
mwaka 793-775 KK) na miaka ya mwanzoni ya Uzia (mwaka 775-757 KK). Imejiri
kipindi kifupi kwa upande wa kaskazini na masalia ya kijiji cha Meshedi ambayo
ni uwanja wa kidesturi wa Kaburi la mahali alipolala Yona.
Unabii huu kama Ishara ya Yona ulikuwa
ni ishara pekee lililopewa Kanisa na Mungu na kwa hiyo ni muhimu kwenye uelewa wa
harakati na kifo cha Kristo na pia wa unabii uliotolewa kupitia nabii Danieli
kwa kuwa imejumuishwa na kufungamanishwa kwenye unabii wa Majuma Sabini ya
Mwaka kwenye Danieli 9:25, na
kuanguka kwa Hekalu mwaka 70 BK mwishoni mwa majuma 70 ya miaka. Uhusiano ule
umeelezwa kwenye jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu
(Na. 013).
Imejumuishwa pia
na siku za mwisho na kuingia kwa kanisa wakati wa Kurudi kwa Masihi kwenye
Ufufuo wa Kwanza wa wafu. Kristo amemuweka kwenye kiwango cha namna moja cha
uwepo wa wazi na Malkia wa Sheba na kutangaza ishara kwa yeye aliye wa pekee
aliyepewa kanisa (soma Mathayo 12:40). Wafafanuzi walio wengi hawajui ishara na
kwa hiyo wanajaribu kuonyesha umuhim. Kama maneno Kristo aliyoyasema yale
aliyopewa na Mungu, wakosoaji wanaoyakataa mafundisho ya Kristo wanatuama
kwenye uvunio wa Mungu.
Kristo alipaswa
afe kabisa kwa muda wa siku tatu usiku na siku tatu nyingine mchana na awe
kaburini kama Yona alipokuwa ndani ya samaki na kwa hiyo wote walipaswa kuwa
wamekufa na wafufuke toka kwa wafu. Kipindi cha siku tatu usiku na tatu
nyingine mchana hufanya kipindi kipana cha sehemu ya Siku na kutowezekana haiendani
kabisa na ile inayoitwa kuwa Ijumaa wa Mateso na Ufufuko wa Jumapili. Dhana ya
kufufuka kwa mungu Attia iliyoingia kwenye imani ya Kikristo kwa imani ya
madhimisho ya Easter au dini ya mungumke Cybele au Easter na kuna kutowezekana
(soma pia jarida la Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235)).
Luka 11:30 inaonyesha
kwamba Yona alikuwa Ishara ya watu wa Ninawi, kama Kristo alivyokuwa kwenye
ufufuko wake.
Wayahudi wa siku
za Kristo walikasirishwa na toba ya wanafunzi chini ya Kristo kama Yona
alivyokuwa kwa toba ya watu wa Ninawi.
Mungu alisema
kwamba angeyaweka maneno yake kinywani mwake yeye aliyemtuma na mara saba
Kristo alijaribiwa kwenye ukweli huo kwenye Injili ya Yohana (Yohana 7:16;
8:28, 46- 47; 12:49; 14:10, 24; 17:8).
Yona alikuwa
ameamriwa aende akawafariji Israeli (2Wafalme 14:25,26) na Ashuru ilikuwa kwenye
magumu makubwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi na sita na katika kipindi
hiki, ilimpasa Yona agundue kwamba Ashuru inaelekea kwenye toba ili waweze kuwa
fimbo ya kuwarekebisha Israeli. Kinachoonekana kuwa ni mtazamo uliodhahiri ni
kwamba Yahova alikuwa ni mkweli katika Neno lake na kwamba kama alifanya
tangazo kuwatangazia watu wa Ninawi na kuutaka mji utubu, ulipelekea kuanguka
kwa kishindo kwa Israeli, ambalo kwa kweli lilifanya. Kukimbia kwake kwa hiyo haukutokana
na woga wao bali ni kuwalinda watu wake na kuikubali hukumu ya Mungu.
Utaratibu na
mfumo wa kitabu upo kwenye migawanyo miwili ya minne:
Sasa tutaenda kwenye
sura nne na kutazama nia yake na msingi.
Sura ya 1 inahusika
na mahubiri na maelekezo ya Yona na matendo yake yaliyofuatia. Bilashaka kabisa
kwamba Yona alielekezwa na Mungu na kujua kwamba Mungu ndiye aliyemuelekeza
yeye.
1 Basi neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa
Amitai, kusema,
Usemi huu au kama
maneno unapatikana mara saba kwenye kitabu cha Yona, sura na aya hizi 1:1;
2:10; 3:1,3; 4:4,9, 10.
2 Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige
kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
Na kwa hiyo
inakuwa dhahiri kwa Yona kwamba Yahova alikuwa anakaribia kuwsahughulikia watu
wa Ninawi. Kwa hiyo mgongano huu wa mawazo kwa watu wake uliojitokeza ungeweza
kuwafanya watubu. Ninawi (kwa mujibu wa Mwanzo 10:11,12) ulikuwa ni mji mkuu wa
Dola ya Ashuru upande wa kushoto mwa Mto Tigri ulioitwa hapo mwanzoni Nina kwa
jina la mungumke waliyemdhania kuwa ni mlinzi wa mji huo. Ulikuwa na chimbuko
la Kibabeloni kutokana na koloni kutokana na Nina Kusini mwa Babeli. Khamurabi kutoka
kwenye kipindi cha zamani sana cha mwanzoni aliuita mji huu Ni-nu-a.
Bullinger anakinukuu
kitabu cha ufafanuzi kiitwacho Encyc. Brittanica (11th Cambridge
edition) kama ilivyoanza uchimbuzi ambao ulidhihirisha maandiko ya Nabi Yunus (nabii
Yona) akiwa kaburini hakuweza kutathiminiwa.
Aliamriwa apige kelele
kuuonja mji huu (kwa Kiebrania Kara’)
na kwa hiyo kufanya tangazo la jumla.
Ninawi
ulijulikana kutokana na imani yake wenyewe ulioshamishwa kwao kwa uovu wake na
ukatili wake (soma pia Nahumu 2:8-13). (Kiebrania kina neno la uwingi la
ra’a’.)
3 Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate
kujiepusha na uso wa Bwana; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda
Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi,
ajiepushe na uso wa Bwana.
Yona alijua kuwa
Ashuru ilikuwa ni upanga wa adhabu au mapatilizo ya Mungu dhidi ya Israeli na kwa
hiyo hakuwa kwenye ugomvi usiovumilika kwamba kama Ashuru haikuachwa salama
kupitia toba na Rehema ya Mungu kwa Israeli ilikwa budi iokolewe. Inaonekana kuwa
inawezekana sana kuwa ni sababu ya mapenzi yake na kukimbia kwake (soma pia
sura na aya za 4:1-3). Alikwenda
Yopa ambayo sasa inajulikana kama (soma Yoshua 19:46; 2Nyamati 2:16; Matendo
9:36) na akapanda meli kwenda Tarshishi. Na ndipo alikimbia na kwa kadiri
alivyoweza wakati ule ambako ni Tarshishi (soma 1Wafalme 10:22) ambao uko
upande wa kusini mwa Hispania na ulikuwa ni kitovu cha kibiashara ya Mwingiliano
katika Mediterranean kama tunavyojua vizuri sana na hadhari kuu leo. Ni nai
ajuaye mahali ambapo kwa hakika alikuwa anakusudia kwenda. Kwa hakika walikuwa
wanafanya biashara huko Kusini mwa Amerika kabla ya wakati ule. Meli (kwa Kiebrania
‘aniyah) ilikuwa ya ukubwa wowote wa meli za wafanya biashara na sio neno
hilohilo kama ilivyo kwenye aya ya 5.
4 Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa
tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika.
(Upepo ulikuwa ni
burudisho kubwa ya kiroho.)
Neno lililotumika
kuwaita Mabaharia kwenye aya ya andiko hili kwa Kiebrania huitwa mallachor salts. Ndipo manahodha walijulikana kama chumvi na kama ilivyokuwa
kawaida kwa Kiingereza.
5 Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba
mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza
uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu;
akajilaza, akapata usingizi.
Kila aloiyelia
kwenye maombi (Kiebrania Ze’ah (sio kama ilivyo kwenye aya za 2,14)) kwa mungu
huyu. Na walitupa shehena (yaani shehena kwa Kiebrania Keli, au kuipa mashiko
au kusaidia) baharini.
Neno lililotumika
kumuelezea mahodha hapa ni mkuu wa kamba ambaye ni nahodha, neno la kwa
Kifoenikiani lililotumika kumuita nahodha (kwa Kiebrania Rab hachobel). Kwa
majadiliano kwa kutokea kwa neno nahodha tazama kitabu cha Bullinger fn 6 Comp.
Bible p. 1248).
6 Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe
ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka,
tusipotee.
Hapa neno hili ni
Elohimu lenye niherufi eth linamaanisha Mungu wa kweli pia kwenye mwonekano wa
pili. Kwa hiyo nahodha alichukuliwa kuwa ni mungu wa Yona au Yunus kuwa ndiye
Mungu wa kweli.
Muundo au
utaratibu wa andiko la sura na aya zake kama hivi: 1:7-12 inaonyesha kujitoa
mhanga kama sadaka kwa Yona.
Aya ya 7 inaonyesha
upigwaji wa kura na Yona anachukuliwa.
Aya ya 8 inaonyesha
udadisi wa kuuliza sababu
Aya ya 9 inaonyesha
ukiri wake
Aya ya 10-11 inaonesha
hofu yao na kuchanganikiwa kwao.
Aya ya 12 inaonyesha
maamuzi ya Yona yanayotokana na matendo ya Mungu.
7 Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige
kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga
kura, nayo kura ikamwangukia Yona. 8 Ndipo
wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu
yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u
mtu wa kabila gani?
Kumbuka kuwa wanaomba
utaifa wake lakini anasema anasema tu kuwa Namcha Bwana Mungu. Hakutangaza
kwamba alikuwa ni nabii bali walikuwa wameghadhibika kwamba alikuwa
amewajulisha sana wao kwa hatari kama ile kama alivyowahi kuwaambia kwamba
alikuwa amemkimbia Mungu.
9 Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana,
Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu. 10 Ndipo
watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa
maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa
sababu alikuwa amewajulisha.
Kisha watu
wanatafuta ulinzi wake kama kwa namna atakavyoweza kutoroka au kuliepuka tatizo
lile ambalo yeye mwenewe amelisababisha. Hatimaye anaelewa ukubwa wake wa jinsi
lilivyo tisha na anasema “Niondoeni mimi” akiona mapatilizo na suluhisho.
11 Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari
itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. 12 Naye
akawaambia, Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itatulia; kwa maana najua
ya kuwa ni kwa ajili yangu tufani hii imewapata.
Licha ya ushauri
huu, watu wale bado walijaribu kumuokoa na kwa hilo hawakumcha Mungu wake.
13 Lakini wale watu wakavuta makasia kwa nguvu, ili
wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia sana. 14 Basi wakamlilia Bwana, wakasema, Twakuomba, Ee Bwana,
twakuomba, tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa
ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda.
Hatimaye
walimuomba Mungu kwa hofu kwa sababu walijua kuwa alikuwa ni mtu asiye na
makosa na kwamba amekimbia tu kutoka mbali kwa woga. Hawakujua uasi wake.
Walilazimika kukubaliana naye na wakamtupa kwenye kilindi cha maji. Bahari
ikaacha kuchafuka na jambo hilo liliwafanya wamuogope Mungu hata zaidi na kisha
walitoa sadaka kwa Mungu wa Waebrania.
15 Basi wakamkamata Yona, wakamtupa baharini, nayo
bahari ikaacha kuchafuka. 16 Ndipo wale watu
wakamwogopa Bwana mno, wakamtolea Bwana sadaka, na kuweka nadhiri. 17 Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye
Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku.
Mungu alijua kile
ambacho Yona alichokifanya na kile kingalichofanyika baada ya hapo na akamuandaa
samaki mkubwa ammeze Yona.
1 Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika
tumbo la yule samaki, 2 Akasema, Nalimlilia Bwana kwa
sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe
ukasikia sauti yangu. 3 Maana ulinitupa vilindini,
Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako
yote na gharika zako zote zimepita juu yangu. 4 Nami
nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu
lako takatifu. 5 Maji yalinizunguka, hata nafsini
mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu; 6 Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na
mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka
shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu, 7 Roho yangu
ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika
hekalu lako takatifu. 8 Watu waangaliao mambo ya
ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe; 9 Lakini
mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu.
Wokovu hutoka kwa Bwana. 10 Bwana akasema na yule
samaki, naye akamtapika Yona pwani.
Neno nyangumi halijaandikwa
popote na huyu alikuwa ni samaki mkubwa na Yona asingeweza kustahimili ndani ya
yule samaki kwa muda wa siku tatu za mchana na tatu za usiku. Aliomba na hatimaye alikufa kama Kristo alivyoomba
na hatimaye akafa. Alifufuka kutoka tumboni mwa samaki kama Kristo alivyofufuka
kutoka kaburini mwishoni mwa siku tatu za mchana na tatu usiku na Yona
alitapikwa nje kwenye nchi kavu pale ambapo Mngu alitaka awe.
Hapa tunaona amri
ya pili kwa Yona na mara hii anatii. Mlolongo wa matukio ya nyakati ni muhimu
kwenye huduma au misheni hii ya Kristo.
1 Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema,
2 Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri
habari nitakayokuamuru. 3 Basi Yona akaondoka, akaenda
Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake
mwendo wa siku tatu.
Ni mfululizo huu
wa matukio ndipo Ninawi kwa mwendo wa siku tatu kuingia ndani, Yona anaingia
mjini siku moja na kisha akahubiri kwa siku mbili akitangaza kwamba zimebaki siku
arobaini tu za wao kutubu au vinginevyo wataangamia.
4 Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja,
akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa. 5 Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza
kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. 6 Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika
kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi
katika majivu. 7 Naye akapiga mbiu, akatangaza habari
katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu
asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo;
wasile, wala wasinywe maji; 8 bali na wafunikwe nguo
za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na
wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. 9 Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na
kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?
Ndipo mji wote
ukatubu. Hili ndilo Yona aliloiogopa sana. Tukio hili lilifanya taswira ya
huduma ya Kristo. Mwandamano wa matukio ulikuwa hivi:
Siku ya 1=Mwaka
wa 1. Huduma ya Yohana Mbatizaji
Iliyoanza mwaka
27 BK na Kristo alikuja kubatizwa na kuchagua wanafunzi wake.
Siku ya 2 na ya 3
= mwaka wa 2 na wa 3. Kristo anafundisha kuanzia baada ya Pasaka ya mwaka 28 BK
wakati Yohana Mbatizaji alipokuwa amefungwa hadi Kristo alipouawa wakati wa
Pasaka ya mwaka 30 BK na kufufuka na kunena na kanisa alipofufuka.
10 Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia
yao mbaya. Basi Mungu akalighairi
neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.
Wale waliotubu
ambao walikuwa ni watu wote wa Ninawi walinusuriwa na Mungu. Walipewa siku
arobaini na walitubu kwa haraka. Yuda wamepewa miaka arobaini na hawakutubu na
waliangamizwa na kutawanyishwa tangu mwaka 70 BK.
Jambo hili
lilimkasirisha Yona na aliudhika sana kuona kuwa Mungu amewasamehe watu walewale
ambao wangefanyika kuwa kifaa cha kuiangamiza Israeli upande wa Kaskazini na
kuwaondoa waende mbali kupita Araxes.
Mungu hakujuta
kwa kuwa yeye Anajua kila kitu na anatuliza katika maafa au adhabu na
mapatilizo. Anasema alikuwa
anakaribia kuwaletea maafa au kufanya hivyo.
Hapa tunaona kuwa
Yona yupo kwenye majadiliano na Yahova wa Israeli kwa niaba ya Mungu wa Pekee
wa Kweli. Anamkumbusha Mungu kuhusu yale aliyoyasema kumwambia yeye alipokuwa
bado yuko huko Israeli na sababu iliyomfanya yeye akimbilie Tarshishi.
1 Lakini jambo hili lilimchukiza Yona sana, naye
akakasirika. 2 Akamwomba Bwana, akasema, Nakuomba, Ee
Bwana; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo
sababu nalifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nalijua ya kuwa wewe u Mungu
mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe
waghairi mabaya. 3 Basi, sasa, Ee Bwana, nakuomba,
uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.
Yona alija
kutokana na vitabu vya Torati (Kutoka 34:6; Hesabu 14:18-19); Daudi alijua (Zaburi
86:5); Hosea alijua (Hosea 11:8-9); Yoeli alijua (Yoeli 2:13) na Mika alijua
(Mika 7:18).
Angeweza kufa
kuliko kuishi. Hakuwa na furaha kuona kuwa hakuwa nabii aliyefanikiwa. Kwa kuwa
anaiokoa Ninawi aliipenda Israeli lakini imani yake kwa Mungu ilipasa iwe kubwa
zaidi.
4 Naye Bwana akasema, Je! Unatenda vema kukasirika?
Kisha Mungu
akamkemea kwa kuona kwake mambo kama mtoto mdogo. Hata hivyo, alikanganywa
akiwa kama nabii kwa watu wake.
5 Ndipo Yona akatoka mjini, akaketi upande wa
mashariki wa mji, akajifanyia kibanda huko, akakaa chini yake uvulini, hata
aone mji ule utakuwaje.
Hakuwapa tumaini
kwamba Ninawi ingerudia kutenda dhambi na kuangamia. Hatimaye akaketi kwenye
mretemu aone kitakachotokea na kuipata Ninawi. Hatimaye Mungu akamlinda alipokuwa
akingojea na kutumia hilo kama mfano kwa Yona.
6 Na Bwana Mungu aliweka tayari mtango, akaufanya
ukue juu ya Yona, ili uwe kivuli juu ya kichwa chake, na kumponya katika hali
yake mbaya. Basi Yona akafurahi sana kwa sababu ya ule mtango. 7 Lakini siku ya pili kulipopambazuka, Mungu akaweka tayari
buu, nalo likautafuna ule mtango, ukakatika. 8 Basi
ikawa, jua lilipopanda juu, Mungu akaweka tayari upepo wa mashariki, wenye hari
nyingi; jua likampiga Yona kichwani, hata akazimia, naye akajitakia kufa,
akasema, Ni afadhali nife mimi kuliko kuishi. 9 Mungu
akamwambia Yona, Je! Unatenda vema kukasirika kwa ajili ya mtango? Naye
akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika hata kufa. 10 Bwana
akamwambia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuuotesha;
uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja; 11
na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani
yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono
wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?
Upepo huu ulikuwa
kama ruach kama roho. Kwa hiyo, mfano
wa mmea na Ninawi ulitumika kuonesha rehema za Mungu. Angepaswa kwa hiyo kuwa
angejua kwamba kama Israeli wangelitubu wasingeweza kuchukuliwa utumwani
ng’ambo ya nchi yao.
Kama tulivyoona kutoka
kwenye jarida la Kuanguka Kwa Misri (Na. 036), mnamo mwaka 732 KK
Mwashuru Tiglath Pileser III aliitwa Dameski na kuifana Israeli na Yuda kuwa ni
nchi za kukusanya kodi. Mwaka 729 KK Tiglath Pileser III aliungana na Babeli na
ShalmaneserV (tangu kwama 724-721 KK) aliitwaa Israeli mwaka 722 KK. Mrithi
wake Sargon II aliyafukuza makabila kumi.
Mwaka 710 KK
Wacimeriani waliishambulia msafara wa Wacaucasi kutoka kwenye kingo za urusi.
Waliuangamiza Urartu na ufalme wa Frigia huko Anatolia. Mwaka 705 KK Sargon II aliuawa
alipokuwa akipigana na Wacimeriani. Mwaka 701 KK jeshi la Sennikarebu
liliondoka pasi kutegemewa kutoka kwenye kampani ya kuwaadhibu katika Yuda.
Mwaka 720 KK Sargon II alianzisha mji mkuu wa dola ya Ashuru huko Dur Sharrukinor Ngome ya Sargon. Mwaka 701
KK Sennikarebu aliondoka huko Fort Sargon na kuifanya Ninawi mji mkuu tena. Kwa
hiyo kuna kinachoonekana kuwa ni kutafakari kupya kuhusu unabii kuhusu Ninawi.
Shahidi wa Yona
alikuwa na miaka arobaini tangu kutawala kwa Yeroboamu II (mwaka 793-775) hadi
Uzia (mwaka 775-753) na tawala za pamoja na jumla kilikuwa ni kipindi cha miaka
arobaini pamoja na kipindi cha matazamio cha ziada kutoka mwaka wa tatu wa
utawala wa Uzia takriban mwaka 772-732 hadi hadhi ya Utozaji kodi ulipokuwa wa
Waashuru, Israeli walikwenda utumwani kwa Waashuru kwa kipindi cha kutoka mwaka
722 KK ambacho kilikuwa ni wastani wa miaka 40 na kisha miaka 50 au yubile moja
tangu unabii wa Yona kwa Israeli. Yona alipaswa ajfunze kutoka hudum yake ya
Ninawi na kuwaonya Israeli kuhusu kile Mungu alichowafanyia na kile kilichopasa
kuwatokea Israeli lakini hawakusikiliza kama Yuda walipoacha kusikiliza wakati
wa kipindi chote cha miaka arobaini walichopewa watubu (soma pia jarida la Mchanganuo wa Ratiba ya Nyakati (Na. 272)).
Kama Yuda
wangetubu wasingeweza kuangamizwa pamoja na Hekalu mwaka 70 BK na Yuda
wakatawanyishwa.
Yuda walipewa
miaka 40 kamili kwa hesabu za mwaka mmoja kwa siku moja kulinganishwa na iliyopewa
Ninawi. Ninawi ilitubu lakini Yuda hawakutubu. Walimuua Kristo mnamo siku ya 14
Abibu Mwaka 30 BK na Yerusalemu ukazingirwa na majeshi na kuhusuriwa siku ya 1
Abibu 70 BK na Hekalu likateketezwa huko Yerusalemu na Hekalu la Heliopolis huko
Misri lilifungwa siku ya 1 Abibu 71 BK.
Katika kila tukio
Mungu aliwapa Israeli na Yuda miaka 40 ya kutubu ambayo ni kiwango cha wastani
na hawakutubu. Tangu Kristo na kanisa lilipoanzishwa, Mungu ameipa dunia yubile
40 tangu mwaka 27 BK hadi 2027 ya kutubu na hawajatubu na hawatatubu na dunia
itaenda utumwani chini ya Masihi na Hukumu kwenye Milenia wakati wa Mapumziko
ya Sabato ya Mungu chini ya Kristo.
q