Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[029]

 

 

 

Kondoo wa Mungu

(Toleo La 3.0 19940521-20000617-20071220)

Jarida hili liliandikwa na mchungaji aliyekuwa anawafundisha kondoo na mbuzi kwa kutumia filamu ya familia iliyopendwa na kusifiwa sana na iliyoshinda tuzo iliyojulinama kwa jina la Babe. Anafundisha na kutathimini masomo au mafundisho yanayohusiana na na dume la kondoo na ujumbe wa biblia kutoka uumbaji. Kazi na jukumu la kondoo na mchungaji yameelezewa pia. Mwenendo wa kondoo na matarajio ya mchungaji yameendelezwa. Tofauti iliyopo kati ya Wamisri na imani za kibilia na mandondoo ya kiroho yanaonyeshwa.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

(Hati Miliki © 1994 Storm Cox, ed. 2000, 2007 Wade Cox)

(tr. 2014)

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Kondoo wa Mungu



Utangulizi

Kutoka wakati wake wa ujana mwandishi alikuwa anaelezea kuhusu maisha ya msimamizi au meneja wa kondoo. Tangu ujana wake na kuendelea kwa kupitia chuo kikuu, na hatimaye kazi zilizofuatia baadae akiwa kama mkufunzi wa wanyama (wa kondoo na mbuzi kwenye sinema yake ya Babe), alishiriki kwa karibu kwenye usimamizi na upandishaji wa madume ya kondoo kwa ujumla, pamoja na shamba lingine la wanyama. Uzoefu wa kazi hii ulimfanya atafakari utaratibu wa mbinu za wafugaji na wakulima za kibiblia, ambao walionekana kuwa walikuwepo na waliishi kama wanaume nyakati za Agano la Kale. Uzoefu kama huu ulimpelekea mwandishi kufikiri kuhusu maana ya waliowatumia kwa kiasi kikubwa mfano elekezi wa kondoo na mchungaji, na kwenye jarida hili anajaribu kuhusisha mambo yalivyo kwenye Kanisa la Mungu.

 

Chanzo cha kundi

Katika siku ya tano ya uumbaji, Mungu aliamuru kwamba nchi iwe na viumbe hai.

 

Mwanzo 1:24-26 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. 25 Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

 

Neno la Kiebrania kuhusu wanyama wa porini ni miqneh (SHD 4735), ambalo linamaanisha pia milki, mali zilizonunuliwa au akiba. Neno hili linamaanisha pia kundi la mifugo na mifugo, ambalo hilo linahusisha kondoo, mbuzi, mifugo na wanyama wa miguu minne wengine wote (wenye miguu mingine) wanyama ‘safi’. Walitengwa kama wanyama ili watumike kwa kuliwa. Neno la Kiebrania la kondoo ni tso'n (SHD 6629), ambalo maana yake ni kondoo, mbuzi na ndama wa ng’ombe, kama neno hili halitakuwa kaseb (SHD 3775; Mwanzo 30:32,33,35; Walawi 1:10; 7:23; 22:19,27; Hesabu 18:17; Kumbukumbu la Torati 14:4), ambalo litakuwa na maana ya moja kwa moja kuwa kondoo kama tunavyowajua kondoo walivyo leo.

 

Raheli (7354) maana yake kusafiri na inamaana sawa na ole. Linaendana kuwataja majike ya wanyama na linaendana na neno kebes (3532) kwa madume.

 

Neno la Kiebrania kuhusu mifugo ni behemah (929), ambalo maana yake ni wanyama wa miguu mine. Suala hapa sio lingine ila ni neno kaseb, ambalo linatumika kwenye aya nane peke yake, maneno yanayotumika kwa ajili ya ng’ombe, mbuzi, pamoja na makund mengine yote ya wanyama safi na wa miguu minne walio sawa. Ni hivyohivyo, kwenye lugha ya Kiyunani, neno linalotuika kuita kondoo lililotumika kwenye Agano Jipya lote ni probaton (SGD 4263), neno la Kiyunani lililo sawa na neno la Kiebrania ni behemah, ambalo kama ilivyoelezwa, maana yake ni mnyama aliyetengwa kwenye wanyama wa miguu minne na pia linawahusu wanyama wote najisi.

 

Kuamua maeneo maalumu kumetumika kwenye aya yoyote iliyotolewa ni uamuzi kwa niaba ya mtafsiri, kutegemea na lengo la Maandiko Matakatifu.

 

Ng’ombe wote, kondoo na mbuzi wanahusiana kimaumbile ya uzao, kuwa wote ni wa kundi la jamii ya ki-bovidae. Tabia za wanyama wa jamii hii ni kwamba wao huwa:

1.    1. Wanaocheua,

2.    2. Wana kwato zilizochanika katikati na,

3.    3. Wote wana pembe zenye mbugu.

 

Kila moja inafikia masharti au vigezo vya kibiblia vya usafi (wa kimaandiko), kama ulivyoelezwa kwenye Mambo ya Walawi 11 na Kumbukumbu la Torati 14, na kwa hiyo wanaweza kuliwa.

 

Mwanzo wa mchungaji

Kata tunavyosoma kwenye Mwanzo 1:26, mwanadamu alipangiwa na Mungu tangu uumbaji awatawale wanyama. Kwa iyo, mtu anaweza kudhania kuwa ni sehemu ya wajibu wetu kufanya hivyo kwa utaratibu sahihi. Kwa hiyo, kuwepo kwa mchungaji lilikuwa ni jambo lililopangwa tangu mwanzo mwanzoni mwa kila jambo.

 

Neno la Kiebrania kuhusu mchungaji ni ra'ah (SHD 7462) na linamaana au kuelezwa maana yake kuwa ni:

... kuangalia au kuchunga kondoo, yaani kuwalisha; kuwaelekeza. Kuwapeleka malishoni (kuwashwa au mtini); kwa ujumla, kutawala kwa kuwa mfano, kushirikiana nao (kama marafiki):-* kuwaonya, kuwa mshirika, kushirikiana nao, kuwala, kula, kumtendea mbaya, lisha, kuwatumia kama marafiki, kufanya urafiki naye, kuwatunza (kondoo) (mtunza kondoo), mchngaji, + banda la kukatia manyoya, mchungaji, kustaajabisha, kupoteza.

 

Neno Ra'ah linatokana na neno ra', ambalo maana yake ni uadui, mateso, mbaya, maafa na uovu. Ra' maana yake ni kuharibu au kuangusha chini, ni kama neno ra'ah linayo linayo linayomaanisha kushikamana pamoja dhidi ya uadui. Neno ra'ah ni la kike na la kiume lake ni ra' (SHD 7451, kutoka kwenye 7489), na hivyo ni kinyume cha kidokezo.

 

Kwenye Kiyunani, neno hili ni poimen (pr. poy-mane; SGD 4166), ambalo lina maana tu ya mchungaji wa mifugo au mchungaji wa kiroho.

 

Kwa hiyo tunaona kutoka kwenye Biblia historia ya mahala pa mchungaji na usimamizi wa mchngaji na usimamizi wa wanyama walio safi ambao Mngu amewapa wanadamu na kuwaruhusu kuwala. Wanyama safi ni zawadi kutoka kwa Mungu aliyotupa sisi kuwa ni chakula chetu, ili tuishi juu ya Nchi au Dunia yake hii ndani ya mfumo na utaratibu aliouweka kwa mafanikio yetu. Na ndiyo saababu sadaka ya Abeli aliyomtolea Mungu ilimpendeza sana kuliko aliyoitoa Kaini machoni mwa Bwana, ni kama dhambi inavyohitaji kufunikwa au kuondolewa kwa dhabihu ya damu, na ilikuwa ni taswira ya damu ya Kristo (kama Mwanzo 4:3-5).

 

Je, kuna maana gani kuwa kondoo?

 

Katika nyakati za Biblia, kama ilivyo leo, kazi kubwa ya kondoo ilikuwa ni kutoa au kuzlisha sufi (Walawi 13:47-48; Ayubu 31:20), nyama (1Samweli 14:32), huficha (Kutoka 25:5; Waebrania 11:37), maziwa (Kumbukumbu la Torati 32:14; Isaya 7:21-22), na mazao mengi mengineyo kama vile pembe kwa ajili kutengenezea vikapu na zana za muziki (1Samweli 16:1; Yoshua 6:4).

 

Katika siku za zamani, sufu zilikuwa ni bidhaa ya thamani ilikuwa muhimu sana kibiashara. Tunaona na kujua hivyo kutoka kwenye 2Wafalme 3:4 kwa Meshaki, Mfalme wa Moabu, ilimpasa kumlipa Mfalme wa Israeli sufu kutoka kwenye mamia elfu ya kondoo zake kila mwaka.

 

Kondoo walichukuliwa pia kuwa ni utajiri wa mtu. Kwenye Biblia mtu alionekana kuwa amebarikiwa kama alionekana kumiliki makumi au mamia elfu ya kondoo (Zaburi 144:13).

 

Kutoka kwene Biblia, tunaweza kupata uelewa wa tabia na asili ya mnyama. Katika 2Samweli 12:3 tunaona kwamba kondoo walionekana kuwa ni viumbe wenye moyo wa kupenda. Kutoka kwenye Isaya 53:7, Yeremia 11:19 na Yohana 10:34, kondoo wanatajwa kuwa ni viumbe wapole na wasio na matata. Kwenye Mika 5:8 na Mathayo 10:16 kondoo wanaonekana kuwa hawana ulinzi, na ni la muhimu sana, kwenye Hesabu 27:17, Ezekieli 34:5 na Mathayo 9:36 na 26:31 tunaona kwamba kwa kweli walikuwa wanalindwa wakati wote na waliapewa uangalizi.

 

Kwenye Agano la Kale, wakati mchungaji na kundi lake wanapoelezewa au kutajwa, kwa kawaida ilikuwa ni kwa maana ya kawaida. Kwenye Agano Jipya, hata hivyo ilikuwa inamaanisha kwa lugha ya fumbo na mifano.

 

Kwenye kitabu cha fasihi cha International Standard Bible Encyclopedia(ISBE) kwenye ukurasa wake wa 464, kinainukuu Zaburi 95:7:

Na sisi tu watu wa malisho yake [Mungu], Na kondoo za mkono wake.

 

Na kinaendelea kwa kusema:

 

Maneno haya yaliyopangiliwa yanayotumia mifano ya kibiblia na yanayosisitiza kuelezea utegemezi wa wanadamu kwa Mungu kwa uwepo wao, kudumu kwao kwa nasibu, na mambo yao. Kitu chenyewe hutoa utambulisho wa kufurahisha kwa namna zote mbili, yaani kwa mahitaji ya mwanadamu kama kumbe na kwa utoshelevu wa Mungu akiwa kama muumbaji na mtoaji wa mahitaji ya watu wote. (ikifanya rejea kwenye 2Samweli 24:17, 1Nyakati 21:17, Zaburi 78:52, Ezekieli 34:31, Zekaria 11:4-17, 13:7 na Yohana 10:10-15).

 

Kutoka kwenye hii tunaona mlingano uliopo kati ya mahusiano ya moja kwa moja na yakimfano uliopo kati ya kondoo na watu wa Mungu.

 

Mishangao mingi iliyopo kwa watu wengi, ni kwamba kondoo kwa kweli ni mnyama mwenye akili nyingi. Kondoo wanafana mambo yao kimakosa na kwa kuchanganyikiwa kwenye wakati yanapotokea machafuko na wanyama wengine, ni kama walivyo na uwezo mdogo wa kimbinu kwa maeneo mengi ya nchi yaliyo mbali. Kutokana na hayo, kondoo wanakuwa hawako salama na wanakuwa ni wanyama waoga. Katika siku zetu hizi, mbinu za kiutawala au kusimamia makundi makubwa ya kutumia mbwa na pikipiki peke yake, huongeza hali ya kutoogopa mioyoni mwa wanyama.

 

Siku za zamani, usimamizi ulitumia mbinu tofauti kabisa. Mchungaji aliwaongoza kondoo mwenyewe akiwa ametangulia mbele yao. Kondoo walimsikia sauti yake na kumfuata, salama mwene uwepo wake. Wakati kondoo wakiwa salama watafanya yale yanayoonekana kama ndoto za mchana na watazishangaa sana, na kwa dhahiri kile kinachotokea karibu yao. Mwanadamu anaweza kuwakamata kondoo hawa kirahisi wakiwa kwenye majani au nyasi nyingi.

 

Kondoo wanaona, wanasikia, wanafikiri na kujifunza, kama wanavyofanya wanyama wengine wote. Kila mnyama anakiwango cha namna tofauti cha uelewa, kwa kiwango kikubwa kama alichonacho mwanadamu. Kama mfundishaji wa kondoo, mwandishi anagundua kwamba sio wanyama wote waliweza kuzipata baadhi ya tabia fulani walizotarajiwa kuwa nazo. Kondoo wengine walichukua kuda mrefu kubadilika na kuchukuliana nazo. Wengine walielewa na kuchukuliana nazo kwa haraka. Mara nyingi ilitegemea uzoefu wao wa zamani na wanadamu na uzoefu uliopo kwenye mazingira ya mafunzoni.

 

Maranyingi wanapokuwa na hamu zaidi ndipo mnyama aliyejitoa zaidi alivyoweza kujifunza na hivyo kupokea thawabu au zawadi yake yam lo mtamu. Kwa ‘hiyo, heri wenye njaa na kiu ya haki’. 

 

Inapendeza sana pia kujua kwamba kondoo aliyefunzwa anaporudishwa kwenye mazingira ya kundini, kutokana na maendeleo yake, atafanyika kuwa kiongozi kundini na wengine waliobakia watamfuata. Nasi ndipo tutafanyika kuwa ‘wavuvi wa watu’.

 

Iwapo kama kondoo atatendewa vizuri na wanadamu, basi atakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufikiri na kuhisi mambo, na hivyo ataweza kuwa na kuwasiliana kirahisi. Kama kondoo atakuwa ametendewa vibaya na kikatili na mwanadamu, ndipo atakuwa muoga na hatapenda kuwasiliana. Hata baada ya kondoo kufundishwa kwa miezi mingi, bado anaweza kukimbia na kutoroka iwapo kama mkufunzi atakuwa na moyo wa wasiwasi na asipende kuwasiliana hata baada ya kutoroka kwake, kama mfundishaji alikuwa na moyo wa wasiwasi na hajatulia au kama alisimama juu ya mnyama na kumkimbiza kwa mwendo kasi sana. Tulifundishwa kuwa tumuendeshe tu mnama kwa kuelekea mbele na kwa usawa wa macho, tukimpeleka kidogokidogo na kwa upole. Kama mfundishaji akiwa na moyo mbaya na hajatulia ilikuwa ni vyema asimfundishe mnyama hadi atakapokuwa na moyo mwema na uliotulizana. Ni rahisi kuahirisha wiki za kazi kwa kumpa mnama uzoefu asi, hata kama mnyama aliogopa kwa bahati mbaya.

 

Kutokana na hili tunaweza kuhitimisha kwamba kondoo ni wanyama makini, mwangalifu na mwenye tahadhari. Wana uwezo usioweza kukadiriwa wa kukumbuka na kondoo aliye makini zaidi atajifunza kwa masuala ya kazi au majukumu ya kama vile ya kusafiri kwa kupitia kwenye njia zene vikwazo, kupelekwa kwenye alama, kurudi kwa kuamriwa na pia kukwea kwene vizingiti.

 

Kondoo ni wanya salama na hivyo hawawindi wanama wengine. Wanaridhika kwenye mazingira salama, na hawana madhara na sio watukutu. Mahitaji yao ni rahisi na wanatoa sauti tu wanapokuwa na njaa au wanapoiona au kuhisi hatari.

 

Kondoo hushikamana na hukaa kwa kukaribiana ili kujilinda. Wakati kitu cha kusikitisha kinapomtokea kondoo, kama vile ugonjwa au kuondolewa (yaani kutoka au kuharibika mimba), ndipo kondoo mwingine jike watamtunza yule mtoto iwapo kama ile hatari haitakapokuwa kubwa sana. Mara nyingi, kondoo mwenye mimba au mnene kwa mafuta kuwa mengi anaweza kujiburuza kwa kutumia mgongo wake na hataweza kurudi nyuma kwa miguu yake. Kwa hiyo anategemea matunzo ya mwanadamu ili kumgeuza asimame kwa miguu yake. Ndege wadogo sana wanaweza kumuua kondoo iwapo kama watampiga kwa nguvu au kumjeruhi. Kukimbia ni mbinu pekee ya kujilinda ya kondoo. Ni mnyama mpole na mpenda amani kiasi hicho, na anayetegemea kwa ujumla urafiki wake na mwanadamu.

 

Biblia inaelezea kuhusu kondoo kwamba husikiliza na kuisikia sauti ya mchungaji (Yohana 10:3), na wachungaji huwaita kondoo zao kwa majina (soma jarida la Anawaita kwa Majina: Somo la Zaburi 23 (Na. 18)). Hii inaonyesha jinsi wachungaji na watu wote wanavyoweza kufanya, kwa kupitia utegemeano kati ya wanya wawili, unafanya ongezeko la kimahusiano na aina zote za wanyama wa porini kama sehemu ya mbinu zao za kiusimamizi. Na hii ndiyo sababu inayowafanya wanadamu wapende kufuga wanyama wa kucheza nao sana.

 

Inapasa kukumbuka kuonyesha kwamba Kansa lilitumiwa kwa mrengo wa kundi, na sio kwa muktada wa wanyama wa kufuga, bali ni kama kundi ambalo ninatenda kazi zake vizuri kama kundi lililoungana lote na kwa pamoja.

 

Mmoja anaweza kwenda mbele, lakini kwa hakika tunaweza kuusifia mlingano wake na Wakristo na kuiona sababu ufananishaji wa mchungaji wa kondoo ulitumika—kwa amani, bila madhara, kwa muunganiko, na kwa tahadhari kwa kuwahudumia wachungaji.

 

Kujua tabia ya kondoo kunaturuhusu na kutufanya tuunge mkono matendo na tabia na shughuli au wajibu na umuhimu wa kazi za mchungaji kwa zaidi sana.

 

Kunamaana gani basi kuwa mchungji?

Ili kulijua hilo, yatubidi kwanza kugundua au kuujua umuhimu wa majukumu yaliyowekwa kwenye vichwa vya wachungaji. Kama tungekuwa na kiasi kidogo tu cha chakula cha kujilisha sisi wenyewe na familia zetu kwa kipindi cha muda uliowekwa na pasipo kile tunachoweza kushinda na njaa, ndipo kwa hakika tungetumia kila namna zote zilizopo za kutetea namna zetu za akiba, na ingewezekana kwa mtu fulani kuvunja nyumbani mwetu na kujaribu kuiba.

 

Haya makundi yalikuwa ni damu ya kudumu ya familia za wachungaji. Makundi haya yalilisha na kuwatunza watu wote, wakiwemo wajane, yatima na walemavu. Kama wanyama watliibiwa au kufa ndipo hawakutoa vya kutosha kwa wote, na kwa hiyo kazi ya kuwa mchungaji kwa kweli ilikuwa kubwa.

 

Hatua nyingine nay a muhimu kuijua kabla hatujaendelea mbele ni nia au mtazamo wa kwamba utaratibu wa kuchunga unahusishwa.

 

Mwanzo 46:34 34 Semeni, Watumwa wako tumekuwa wachunga wanyama tangu ujana wetu, na hata leo, sisi, na baba zetu; mpate kukaa katika nchi ya Gosheni; maana kila mchunga wanyama ni chukizo kwa Wamisri.

 

Desturi ya Kiebrania ya kufuga kondoo ilichukiwa na mawazo ya Wamisri. Namna ya kifikra ya Warumi ilieleweka nab ado inaeleweka kwenye Biblia yote likiwa ni wazo lenye mchakato unaopingana na Mungu. Wamisri walikuwa matajiri wa taifa la kibiashara. Walikuwa ni mabepari (kwa maneno mengine wenye kujilimbikizia mali), walioutafuta utajiri na mali kwa mtindo wa vitu vya kimwili. Dhana hii uliwapelekea kuwafanya Israeli watumwa. Walifanyika kuwa matajiri kutoka kwenye kazi zao na kwa kuwadhuru wa mataifa mengine. Tumeona hilo kwenye vipindi vya karibuni zaidi pamoja na kuwafanya Waafrika kuwa watumwa wa Wamarekani, miongoni mwa mataifa mengine. Sababu iliyopelekea wachungaji wachukiwe ilikuwa ni kwa kuwa, kwenye usimamizi wa makundi yao na familia na uongozi wao kwa ujumla, walieleza kwa wazi mtindo wa kiuongozi wa kiutumishi wa kiserikali au uongozi. Huu ni utaratibu kinyume kwa Wamisri, na kwa hiyo ni ushahidi kamili dhidi ya utaratibu wao.

 

Mfundishaji wa wanyama anafanya kazi kwa masaa mengi kwa kila siku ili kuona kwamba mahitaji ya wanyama yanapatikana. Anafanyika kuwa mtumwa kwao, na ili kuweza kupata kutoka kwao inalazimu kutoa muda mwingi na nguvu. Wachungaji, ili kuwawezesha watu wao wale, inawapasa kufanya kazi kwa bidii na kujifanya watumwa kwenye makundi yao, hata kama itamaanisha kufa (Yeremia 49:19; Amosi 3:12; tazama hapo chini).

 

Wachungaji walikuwa ni watumishi tu wa watu wao, ni kazi inayohitaji unyenekevu mkubwa, kinyume na majivuno na kiburi cha Wamisri.

 

Kutoka kwenye Biblia tunajua kwama Yesu Kristo ndiye Mchungaji wetu, nasi tu kondoo wa kundi lake. Hata hivyo, hata sisi tumekusudiwa kuwa wachungaji kama alivyo Kristo. Hili limeelezewa kwenye Warumi 8:17, ambapo tunasoma hivi:

na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.

 

Kutokana na hili tunaweza kuhitimisha kwamba ni wajibu wetu kujifunza kuwa wachungaji kama Yesu alivyo mchungaji. Mfano wa kulinganisha ilitumika rasmi ili kwamba watu – ambao waliishi siku za nyuma kutoka kwenye historia ya umilikaji ardhi, kama tutakavyokuwa sisi kwenye kipindi cha Milenia – tungeona kanuni na mchakato wa uongozi au utawala wa kiroho kwenye mpangilio wa kawaida wakimwili ambao ulikuwa ni sehemu ya uwepo wao wa kila siku. Leo, wengi wetu hatuna starehe au utulivu ule.

 

Ni nini kazi ya mchungaji?

 

Kwa hali halisi na ya kweli, matendo ya msingi ya msimamizi wa shamba kwa maana ya kutunza konzoo zake linatuama kwenye makundi makuu mawili. Nayo ni:

1.    1.Lisha na kuwanywesha maji, na

2.    2. Linda na ganga

Hii ilikuwa, na bado inakuwa, shughuli ya wachungaji.

 

1. kulisha na kunywesha maji kondoo

Ulishaji wa kondoo ni wajibu mkubwa na wa muhimu wa mchungaji. Anapaswa kutiliwa maanani aina ya chakula kilicho na faida na cha mana zaidi kwa mnyama na kinachotoa faida ya virutubisho kwake.

 

Kazi ilikuwa ni kuwanenepesha au kuwaandaa kondoo kwa kuliwa au kumtumia, kama sadaka ya kukubaliwa kwa Bwana – kama tutatilia maanani mambo yaliyo kwenye mrengo wa kibiblia. Huu ni msingi wa sababu iliyosababisha hasira ya Mungu kwenye kitabu cha Malaki, ambako korban ya Mungu inaaminika kudharauliwa; tena, ni wajibu wa wachungaji wenyewe kujikita na kuandaa kile Mungu alichowapa kukisimamia. Biblia iko wazi kufundisha au kuelezea jukumu la mchungaji. Mchungaji anatakiwa kutafuta malisho kwa ajili ya kondoo zake (Ezekieli 34:2,9,13) na maji kwa kundi lake. Kondoo wanahitaji maji yaliyotulia (Zaburi 23:3). Kondoo, akiwa ni mnyama mwenye hisia kali na makini, hatakunywa tayari kutoka kwenye mito inayotiririsha maji kwa kasi. Mtu yeyote aliyejaribu kupitisha au kuyavusha makundi makubwa kwenye mito anaweza kuwa ni shuhuda wa jambo hili. Inaweza kuwa ndefu, kuchosha na wanachanganyikiwa mara nyingi.

 

Wakati maji yakiwa hayapo karibu na wao, ndoo ya ngozi au chombo cha kukatia mkate lilitumika (Mwanzo 30:38; Kutoka 2:16). Hii ni kazi ngumu na inahitaji umakini kama tutatilia maanani kwamba kila kondoo alihitaji kupewa maji angalau mara tatu kwa siku, pamoja na masaada wa zaida wakati wa alasiri kwenye kilele cha wakati wa joto la siku. Hii imeelezewa kwa ufasaha kwenye Mwanzo 29:2-10.

 

Shughuli na utendaji mkuu ni kuwalisha kondoo zake. Tunajua hilo kutoka kwenye Yohana 21:15-17.

Yohana 21:15-17 Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. 16 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. 17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.

 

Kristo alikuwa anasisitiza kuhusu kuwalisha kondoo wake. Ilikuwa hapa kwamba huduma iliamriwa ieneze neno la Kweli kama lilivyoelezewa kwenye Biblia. Kama wachungaji wema walivyotakiwa kuwalisha kundi, ndivyo pia huduma inatakiwa kulieneza Kweli kama malisho ya kondoo au kundi. Ni wajibu na kazi yetu kubwa kuieneza Injili ya Kweli. Kama tutakuwa hatufundishi Ukweli kama Mungu anavyotutaka tufanye, basi tutakuwa sawa na wezi. Kristo anatuambia jambo hilo kwenye Yohana 10:1.

 

Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang'anyi.

 

Yohana 10:10 inasema:

Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;

 

Mwizi anayeongelewa hapa anatudanganya na kutuibia taji yetu ili kwamba tusiungane na Kristo kwenye Ufufuo wa Kwanza wa wafu, na ndipo tustahili sehemu yetu tukiwa kama ni sehemu ya wteule.

 

2. Kuwalinda na kuwaganga kondoo

Kama tulivyoelezea mapema, kazi ya wachungaji ilikuwa ni ya muhimu sana; uhai wa watu wao ulikuwa vichwani mwao. Kwa hiyo, kuwalinda kondoo wao, ilikuwa ni sehemu muhimu ya kazi hii.

 

Yeremia 49:19  Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafula ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?

 

Maneno ya msingi hapa ni samba, mchungaji na kusimama. Aya hii inamtumia mchungaji kama mfano wa nguvu. Ni sawa na ilivyo kwenye Amosi 3:12 tunasoma hivi:

12 Haya ndiyo asemayo Bwana; Kama vile mchungaji apokonyavyo kinywani mwa simba miguu miwili, au kipande cha sikio; ndivyo watakavyopokonywa wana wa …

 

Uelewa wa jmla hapa ni kwamba mwandishi anatilia maanani jukumu la mchungaji, akihusianisha na kondoo zake, kuwa hivyo ndipo angewaburuza kondoo wake nje yam domo wa samba kwa mikono yake mitupu kama ikihijika kuwa hivyo. Kwa kweli, usalama wa kondoo ulichukuliwa zaidi sana kwa kumaanisha kama tungalivyoweza kudhania kwanza. Kwa Daudi, tunajikusanyia tena habari ya mchungaji wake aliyedai kumuua mnyama wa porini kwa mikono yake iliyokuwa tupu ili kuwaokoa kondoo wa Daudi. Licha ya ujumbe wa moja kwa moja wa hadithi hii, dalili iliyoko kwenye kusudi hili ni ukubwa wa wajibu wa kuwa mchungaji.

 

Kazi kubwa kuliko zote ya muchungaji ni kulilinda kundi. Leo tunafaidika ya kitekinolojia kama vile kuna zana za kuzungushia ukuta. Bunduki za kuwafukuzia au kuulia wanyama wa porini, tochi za kumulikia wanyama nyakati za usiku na kwenye maeneo ya dunia yenye watu wengi kuna mipaka iliyowekwa mwa mifumo iliyopangiliwa vizuri. Hatahivyo, jukumu la kuliangalia kundi kwa kila siku kuwatazama wagonjwa na wenye ulemavu unabakia kuwa ni muhimu kama ilivyo siku hizi na ni muhimu kuliko ilivyowahi kuwa huko kabla. Kazi hii ilikuwa ni ngumu sana kwa hiyo, lakini majukumu na wajibu yalijulikana. Bila mchungaji, kondoo wanakosa msaada. Hebu na tusome Hesabu 27:17.

17 atakayetoka mbele yao, na kuingia mbele yao; atakayewaongoza watokapo, na kuwaleta ndani; ili mkutano wa Bwana wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji. …

 

Wazo hilohilo limeelezewa kwenye 1Wafalme 22:17, 2Nyakati 18:16, Zekaria 10:2, Mathayo 9:36 na Marko 6:34.

 

Kila usiku wachungaji waliyapeleka makundi kwenye kile kinachoitwa zizi la kondoo (Mwanzo 31:39; 1Samweli 17:34). Hili zizi la kondoo inaelezewa kuwa ni kama:

Ni mahali palipofungwa vizuri kwa kuzuia hatari na misukosuko ya usiku inayotokana na wanyama wakali, na wezi au majambazi. Wakati mwingine ukusanyaji wa pamoja ulitumiwa kwa idadi wachungaji kwa uwingi au makundi na uliangaliwa na mtu mmoja kwa usiku wote, kisha kila mchungaji huwaita kondoo wa kundi lake kunapopambazuka asubuhi (Yohana 10:14). Mazizi makubwa kama haya yanaingiliwa kwa kupitia malangoni (Yohana 10:2) na linawezakuwa ni  eneo lililozungushiwa kwa kuta za mawe, zikionyesha juhudi iliyofananishwa na ile ya jingo la mji (Hesabu 32:16). (Kamusi mashuhuri iitwayo: The Interpreter’s Dictionary of the Bible, p. 316)

 

Mapango yalikuwa yakitumiwa pia kama mazizi ya pamoja (Isaya 24:3). Ufunguzi wa mapango kwa kawaida ulisimamiwa na mchungaji mwenyewe (Yohana 10:7,9).

 

Inafurahisha kuona kwamba Daudi, mchungaji, alikuwa na ujuzi mkubwa sana wa kombeo. Uwezo wake wa kumuua Goliathi kwa kutumia kombeo uliwaonyesha watu wake uwezo wake wa kupambana akiwa mchungaji, kama kombeo na fimbo au au bakora zilikuwa ni zana ambazo kwazo mchungaji alivitumia katika kuwalinda kondoo wake. Kwa hiyo, kwa kuwa kwake imara na uhodari, alionyesha kujitoa kwake au umahiri wake kwenye kazi yake kama mchungaji. Kwa hiyo, alistahili mara moja kuwaongoza Israeli. Hadithi hii ipo kwenye Isaya 17:49.

 

Njia kuu aliambayo mchungaji aliiweza kuitumia ili kulilinda kundi lake kwa usalama zaidi ilikuwa ni kwa kupitia mafunzo. Najua kutokana na uzoefu wangu nikiwa kama mkufunzi wa wanyama, kwamba baada ya kipindi fulani niliweza kuwaita kondoo wangu waje upande wangu wakati walipoanza kuweza kupambanua na kuitambua sauti yangu na kuijua kuwa ni sauti ya usalama nay a anayewapa chakula na maji. Inachukua kuda kufikia kiwango hiki hata hivyo.

 

Wakati tulipopewa kondoo kwa mara ya kwanza tuwafundishe, tulitumia kipindi cha saa moja hadi mawili kwa siku, tukitumia muda huo kwa kutembea na kukaa pamoja na mnyama, tukiongea wakati wote, ili kumhakikishia kuwa sisi tu watu wema kwake na tukimzoeza atuzoee kwa maneno na sauti zetu. Yohana 10:4 inasema:

Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.

 

Hii inaashiria mafunzo kama hayahaya na mbinu zake. Wakati wa kumfunga ukawasili.

 

Wakati wowote ambapo mkulima anapowaingiza ndani kondoo wake kwenye mlowesho wa maji au nyoa manyoya, huwahesabu mmoja mmoja ili kuhakikisha kuwa hakuna hata mmoja aliyeachwa kwenye majani mengi. Tukio kama hilihili ndivyo lilivyokuwa linatokea katika siku za Biblia. Kila usiku kama walivyokuwa wanaingia kwenye zizi la kondoo walikuwa wanahesabiwa na vivyohivyo kila asubuhi walipoondoka. Dhana hii imeenea sana (ISBE, Vol. 4, p. 464) kwamba kila kundi lililohesabiwa lilikuwa na wastani wa mifugo 100 (Mathayo 18:12; Luka 15:4). Tofauti yoyote iliyojitokeza kwenye idadi ya mifugo ilihesabiwa kuwa ni hasara ya wachungaji (Mwanzo 31:39; 1Samweli 25:15-21).

 

Yaonekana kwamba mchungaji mwema hakuwa anakula yeyote kati ya wanyama wake mwenye, haijalishi mazingira yako mabaya na magumu kiasi gani, lakini kwa ajili ya wajibu wake kwa watu wake (Mwanzo 31:38-40; Ezekieli 34:7-16; Amosi 3:12). Mashitaka ya Yakobo kwa Labani ni mfano tunaoweza kuufuata kwa kuwa kondoo hawakuwa wake (Mwanzo 31:38-40). Ezekieli 34:7-16 inatuonyesha kuwa tusifanyen hivyo. Yohana 10:12 inatuonyesha kiwango cha kujitoa alichokuwanacho mchungaji kwa kondoo zake.

 

Kwa suala la kuwaganga, tunaweza kutegemea wataalamu wa tiba za Wanyama au ma bwana Mifugo waliopo leo. Lakini haikuwa hivyo siku za nyuma. Mchungaji alipaswa kushiriki wajibu wa ubwana Mifugo. Tunajua kutoka kwenye Isaya 1:6 na Yeremia 8:22 kwamba marihamu, mafuta ya mzeituni, au mafuta ya mnyama yalihitajika, kama dawa, kwa kawaida wakati kondoo anaingia kwenye nchi yenye matatizo au kamsa (Ezekieli 34:5; Mathayo 12:11; 1Wafalme 15:4).

 

Mwongozo ulio wazi tulionao katika kuangalia usalama wa kondoo wa Mungu. Tunahukumiwa kwa jinsi tunavyotendea kila mmoja na mwenziwe, kwa mukutada wa namna zote mbili, yaani tukwa kama wachungaji na tukiwa kama kondoo. Hebu na tupendane kama Mchungaji wetu alivyo tupenda na anavyoendelea kutupenda sisi wote.

            q