Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[033]

 

 

 

Zana za Muziki Kwenye Ibada

 

(Toleo La 1.0 20070730-20070730)

 

Watu wengine wameonea mashaka kuhusu utumiaji wa vyombo vya muziki na hata muziki wenyewe kwenye ibada. Kwenye jarida hili tutaona kwamba muziki kwa kweli ni kiini na sehemu muhimu ya ibada katika kumuabudu Mungu.

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 2007 Wade Cox)

(Tr. 2014)

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Zana za Muziki Kwenye Ibada



Utangulizi

Tumerudi nyuma hadi kwenye kitabu cha Mwanzo ili kuona rekodi ya kwanza ya matumizi ya muziki na zana za muziki kwenye Biblia.

 

Mwanzo 4:19-22

Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila. 20 Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama. 21 Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi. 22 Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma. Dada wa Tubal-kain alikuwa Naama. (inasema na kuelezea vyema biblia ya RSV)

 

Watu wengine wanaelezea mashaka yao kwamba kwakuwa msitari wa wanamuziki unakuja kutoka kwa Kaini, na Yubali alikuwa ndiye baba wa muziki kwenye rekodi za Biblia, kuna kitu kibaya hapa kwenye matumizi ya muziki kwenye ibada. Hata hivyo, tunaona hapa kwamba kulikuwa na mpangilio maalumu uliofanywa kwa uanzishwaji wa muziki kwenye rekodi ya Biblia.

 

Mungu yuko wazi sana kwamba katika Siku za Mwisho tutakabiliwa na “makelele” aliyoyasema Amosi, ambao umekwishaonekana – na kwamba kelele zipo juu yetu. Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa Mungu hapendezwi na muziki na utaratibu na uzuri kwenye ibada.

 

Wakati wa kukombolewa kwao wana wa Israeli tunaona kuwa ilijulikana kwamba matumizi ya muziki yalikuwa sahihi na kuwa sehemu ya shukrani kipindi cha Waamuzi.

 

Waamuzi 5:1-3

Ndipo Debora, na Baraka mwana wa Abinoamu, wakaimba siku ile, wakisema; 2 Kwa sababu wakuu walitangulia katika Israeli, Kwa sababu watu walijitoa nafsi zao kwa hiari yao, Mhimidini Bwana. 3 Sikieni, enyi wafalme; tegeni masikio, enyi wakuu; Mimi, naam mimi, nitamwimbia Bwana; Nitamhimidi Bwana, Mungu wa Israeli.

 

Ilikuwa pia ni sehemu ya sherehe ya kitaifa wakati Mungu alipolikomboa taifa kutoka kwa maadui zake.

 

1Samweli 18:6

6 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda.

 

Uonyeshaji wa furaha mbele za Bwana kwa kutumia muziki, na Daudi alianzisha Zaburi kama lugha ya msingi ya kinabii na kufurahia kwenye ibada.

 

2Samweli 6:5

5 Daudi na nyumba yote ya Israeli wakacheza mbele za Bwana kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa kayamba, na kwa matoazi

 

Daudi alifanya maandalizi maalumu kwa Walawi kuanzisha kwenye madaraja yao ya kihuduma kwa kuwachagua wanamuziki na watu wenye uwezo na ujuzi ambao waliimba muziki ukiwa ni sehemu ya ibada, na ambao nyumba zao ziliwekwa wakfu kwa ajili ya shughuli hii miongoni mwa Walawi Hekaluni. Waliongozwa na wafundishaji wanamuziki waliochaguliwa kutoka kwa wale walioujua vyema muziki.

 

1Nyakati 15:16-22

Kisha Daudi akamwambia mkuu wa Walawi, kwamba awaagize ndugu zao waimbaji, pamoja na vyombo vyao vya kupigia ngoma, vinanda, na vinubi, na matoazi, wavipige na kupaza sauti kwa furaha. 17 Basi Walawi wakamwagiza Hemani mwana wa Yoeli; na wa nduguze, Asafu mwana wa Berekia; na wa wana wa Merari ndugu zao, Ethani mwana wa Kishi; 18 na pamoja nao ndugu zao kwa cheo cha pili, Zekaria, na Yaasieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu; na Benaya, na Maaseya, na Matithia, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, mabawabu. 19 Hivyo hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu; 20 na Zekaria, na Yaasieli na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu, na Maaseya, na Benaya, wenye vinanda vya sauti ya Alamothi; 21 na Matithiya, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, na Azazia, wenye vinubi vya sauti ya Sheminithi, 22 waongoze. Na Kenania, mkuu wa Walawi, alikuwa juu ya uchukuzi; yeye aliusimamia uchukuzi, kwa sababu alikuwa mstadi.

 

Daudi na Walawi hawakuelekeza habari hii kwa urahisi au kwa mavazi yasiyo sahihi. Muziki wote uliandaliwa vizuri ukivaliwa vizuri kwa uvaaji mavazi ya Makuhani, na mfalme alikuwa vivyohivyo amevaa ngua safi ya hariri kwenye mstari wakati alipojitokeza pamoja nao kwenye ibada ya shukurani, iwe kwenye Hekalu au nje yake. Hii ilikuwa hasahasa ni hivyo wakati anapotokea na Sanduku la Agano, lililokuja kuwakilisha uwepo wa Roho Mtakatifu katikati ya wateule wa Mungu.

 

1Nyakati 15:27-29

Naye Daudi alikuwa amevaa joho ya kitani safi, na Walawi wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani. 28 Ndivyo Israeli wote walivyolipandisha sanduku la agano la Bwana kwa shangwe na kwa sauti ya tarumbeta, na kwa baragumu, na kwa matoazi, wakipiga sauti kuu kwa vinanda na vinubi. 29 Hata ikawa, sanduku la agano la Bwana lilipofika mjini kwa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi, akicheza na kushangilia; akamdharau moyoni mwake.

 

Kushereheka ni Baraka kuu lakini mara nyingi kuna wale ambao hawawezi kuliona hilo, na hilo lilikuwa ni kama alivyoona Mikali.

 

Ulikuwa ni wajibu wa mfalme kulipatia taifa furaha siku za Sabato na Daudi alifanya kile tunachokiona kimeandikwa kwenye kitabu cha nabii Ezekieli, sura ya 45. Sanduku la agno lilijengewa na lilikuwa ni kitovu cha ibada ni kama sisi tunavyokutanika leo kwa pamoja tukiwa kama Mwili wa Kristo ili tuabudu.

 

1Nyakati 16:1-43

Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. 2 Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Bwana. 3 Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu. 4 Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la Bwana, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, Bwana, Mungu wa Israeli; 5 Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi; 6 nao makuhani Benaya na Yahazieli wenye baragumu daima, mbele ya sanduku la agano la Mungu. 7 Ndipo siku hiyo Daudi alipoagiza kwanza kumshukuru Bwana, kwa mkono wa Asafu na nduguze. 8 Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake. 9 Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi; Zitafakarini ajabu zake zote. 10 Jisifuni kwa jina lake takatifu; Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana. 11 Mtakeni Bwana na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote. 12 Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake; 13 Enyi wazao wa Israeli, mtumishi wake, Enyi wana wa Yakobo, wateule wake. 14 Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu; Duniani mwote mna hukumu zake. 15 Likumbukeni agano lake milele, Neno lile aliloviamuru vizazi elfu. 16 Agano alilofanya na Ibrahimu, Na uapo wake kwa Isaka; 17 Alilomthibitishia Yakobo kuwa amri, Na Israeli liwe agano la milele. 18 Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Iwe urithi wenu mliopimiwa; 19 Mlipokuwa watu wawezao kuhesabiwa; Naam, watu wachache na wageni ndani yake. 20 Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine. 21 Hakumwacha mtu awaonee; Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao; 22 Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu. 23 Mwimbieni Bwana, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku. 24 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake. 25 Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote. 26 Maana miungu yote ya watu si kitu; Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu. 27 Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake. 28 Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu. 29 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu; 30 Tetemekeni mbele zake, nchi yote. 31 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, Bwana ametamalaki; 32 Bahari na ivume na vyote viijazavyo; Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo; 33 Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha, 34 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 35 Nanyi mkaseme, Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa zako. 36 Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi Bwana. 37 Basi akawaacha huko, mbele ya sanduku la agano la Bwana, Asafu na nduguze, ili watumike mbele ya sanduku daima, kila siku kama ilivyokuwa kazi yake. 38 Naye Obed-edomu, pamoja na ndugu zao, sitini na wanane; Obed-edomu na mwana wa Yeduthuni, na Hosa, wawe mabawabu; 39 na Sadoki kuhani, na nduguze makuhani, mbele ya maskani ya Bwana katika mahali pa juu palipokuwa huko Gibeoni, 40 ili kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa daima asubuhi na jioni, naam, sawasawa na yote yaliyoandikwa katika torati ya Bwana, aliyowaamuru Israeli; 41 na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru Bwana, kwa kuwa fadhili zake ni za milele; 42 na pamoja nao Hemani na Yeduthuni wenye baragumu na matoazi, kwa hao watakaovumisha sauti, na vinanda kwa ajili ya hizo nyimbo za Mungu; na hao wana wa Yeduthuni wawepo mlangoni. 43 Kisha watu wote wakaenda zao kila mtu nyumbani kwake; naye Daudi akarudi ili awabariki watu wa nyumbani mwake.

 

Baada ya Daudi kuwachagua Walawi na wasimamizi wao kwenye uanzishaji wa Maelekezo ya jinsi ya kuimba Kuuelekeza Muziki wa taifa, ndipo aliwabariki watu wa nyumbani mwake.

 

Muziki kwenye Unabii

Utaratibu wa Hekalu ulianzishwa ili kwamba unabii uendane sawasawa na muziki unavyopigwa kwenye kinubi na pamoja na kayamba na matoazi.

 

1Nyakati 25:1-8

Tena Daudi na maakida wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi sawasawa na utumishi wao; 2 wa wana wa Asafu; Zakuri, na Yusufu, na Nethania, na Asharela, wana wa Asafu; walioamriwa na Asafu, aliyetabiri kwa amri ya mfalme. 3 Wa Yeduthuni; wana wa Yeduthuni; Gedalia, na Seri, na Yeshaya, na Hashabia, na Matithia, [na Shimei], watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu Bwana. 4 Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi; 5 hao wote ndio wana wa Hemani, mwonaji wa mfalme, kwa maneno ya Mungu, ili kuinua pembe. Naye Mungu akampa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu. 6 Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa Bwana, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme. 7 Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia Bwana, wote waliokuwa wastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane. 8 Wakatupiwa kura ya ulinzi wao, sawasawa wote, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi.

 

Misho au ukomo wa kazi na shughuli hizi uliamuliwa kwa kupigiwa kura, kama ilivyokuwa kwa makuhani.

 

Zaburi

Daudi aliweka idadi ya waimbaji kwenye Zaburi, kama walivyoandikwa kwa Roho Mtakatifu.

 

Zaburi 49:1-6

Kwa kiongozi wa kwaya: Zaburi ya Wana wa Kora

 

1 Sikieni haya, enyi mataifa yote; Sikilizeni, ninyi nyote mnaokaa duniani. 2 Watu wakuu na watu wadogo wote pia, Tajiri na maskini wote pamoja. 3 Kinywa changu kitanena hekima, Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara. 4 Nitatega sikio langu nisikie mithali, Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi 5 Kwa nini niogope siku za uovu, Ubaya ukinizunguka miguuni pangu? 6 Wa hao wanaozitumainia mali zao, Na kujisifia wingi wa utajiri wao;

 

Kinubi kilitumika kwa unabii na suluhisho la matatizo la taifa kwa kupitia manabii wake kwenye muziki.

 

Zaburi 92:1-4

Zaburi ya Wimbo wa siku za Sabato. 1 Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu. 2 Kuzitangaza rehema zako asubuhi, Na uaminifu wako wakati wa usiku. 3 Kwa chombo chenye nyuzi kumi, Na kwa kinanda, Na kwa mlio wa kinubi. 4 Kwa kuwa umenifurahisha, Bwana, Kwa kazi yako; nitashangilia Kwa ajili ya matendo ya mikono yako.

 

Kwa hiyo tunaona kutoka kwenye Zaburi 92 kwamba ilianzishwa hasa kwenye Sabato na kuimbwa siku ile pamoja na zana za kuziki.

 

Kutokana na Zaburi 150, tunaona kwamba utaratibu wote wa kimuziki kwenye wimbo na zana na kucheza ulipaswa kufanyika katika kumfifu Bwana.

 

Zaburi 150:1-6

Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. 2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. 3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi; 4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; 5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. 6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.

 

Hekalu

Utaratibu ulihamishwa moja kwa moja Hekaluni kiusahihi baada ya kujengwa kwake katika siku za Sulemani.

 

2Nyakati 5:1-14

Hivyo ikaisha kazi yote Sulemani aliyoifanyia nyumba ya Bwana. Sulemani akaviingiza vitu alivyovitakasa baba yake Daudi; fedha, na dhahabu, na vyombo vyote, akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Mungu. 2 Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni. 3 Wakakutana watu wote wa Israeli mbele ya mfalme wakati wa sikukuu, katika mwezi wa saba. 4 Wakaja wazee wote wa Israeli, nao Walawi wakajitwika sanduku. 5 Wakalipandisha sanduku, na ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwamo Hemani, vitu hivyo makuhani Walawi wakavipandisha. 6 Mfalme Sulemani, na mkutano wote wa Israeli, waliokutanika kwake, walikuwako mbele ya sanduku, wakichinja dhabihu za kondoo na ng'ombe, wasiohesabika wala kujumlishwa kwa kuwa wengi. 7 Makuhani wakaliingiza sanduku la agano la Bwana mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi. 8 Kwa maana makerubi yalinyosha mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, makerubi yakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu. 9 Na ile miti ilikuwa mirefu, hata ncha za miti zilionekana sandukuni mbele ya chumba cha ndani, lakini hazikuonekana nje; nayo iko kuko huko hata leo. 10 Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili alizozitia Musa huko Horebu, Bwana alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka Misri. 11 Ikawa makuhani walipokwisha kutoka katika patakatifu; (kwani makuhani wote waliokuwapo, walikuwa wamejitakasa, wala hawakuzishika zamu zao; 12 tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;) 13 hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana, 14 hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana

 

Wakati kushehereka huku na muziki amoja na shukrani ukiendelea, ndipo wingu la Utukufu wa Bwana ulilijaza Hekalu wakati wa ibada ile.

 

Kisha, wakati wa kulipokuwa inafungwa Mungu aliutuma moto ukashuka chini kutoka Mbinguni na kuiteketeza dhabihu pamoja na sadaka za kuteketezwa.

 

2Nyakati 7:1-22

Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa Bwana ukaijaza nyumba. 2 Wala makuhani hawakuweza kuingia nyumbani mwa Bwana, kwa kuwa utukufu wa Bwana umeijaza nyumba ya Bwana. 3 Wakatazama wana wa Israeli wote, uliposhuka ule moto, utukufu wa Bwana ulipokuwapo juu ya nyumba; wakasujudu kifulifuli hata nchi sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele. 4 Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Bwana. 5 Mfalme Sulemani akatoa sadaka ya ng'ombe ishirini na mbili elfu, na kondoo mia na ishirini elfu. Ndivyo mfalme na watu wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Mungu. 6 Wakasimama makuhani sawasawa na malinzi yao; Walawi nao pamoja na vinanda vya Bwana, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru Bwana, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama. 7 Tena Sulemani akaitakasa behewa katikati, iliyokuwa mbele ya nyumba ya Bwana; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka za kuteketezwa, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba aliyoifanya Sulemani haikutosha kuzipokea sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na mafuta. 8 Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, toka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, muda wa siku saba. 9 Hata siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana walishika kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba. 10 Akawaruhusu watu waende hemani kwao siku ya ishirini na tatu, ya mwezi wa saba, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema wote Bwana aliomfanyia Daudi, na Sulemani, na Israeli watu wake. 11 Hivyo Sulemani akaimaliza nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme; na yote yaliyomwingia Sulemani moyoni ayafanye nyumbani mwa Bwana, na nyumbani mwake mwenyewe, akayafanikisha.

 

Walati Sulemani alipofikia mwishoni na sadaka zikiwa zimeteketezwa na Utukufu wa Mungu ulionekana, ndipo Bwana alijidhihirisha kwa kumtokea Sulemani. Alilitakasa Hekalu na utaratibu wake na akasema kwamba wakati watu watakapotubu na kujinyenyekeza mbele zake, ndipo atawasikia na kuwasamehe na kuiponya nchi kutokana na dhambi zake. Ni wazi sana kwamba matumizi ya zana za muziki na nyimbo za kusifu zilikubalika na kuruhusiwa kwenye taratibu za Hekalu na zilibarikiwa na kukubalika na Mung.


12 Bwana akamtokea Sulemani usiku, akamwambia, Nimesikia uliyoyaomba, na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu. 13 Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; 14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. 15 Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. 16 Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima. 17 Nawe, ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu; 18 ndipo nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli. 19 Lakini mkigeuka, na kuziacha sheria zangu na amri zangu nilizoweka mbele yenu, mkienda, na kuitumikia miungu mingine, na kuiabudu; 20 ndipo nitawang'oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote. 21 Na nyumba hii, iliyo juu, kila apitaye ataona ushangao, atasema, Mbona Bwana ameitendea hivi nchi hii, na nyumba hii? 22 Nao watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu, na kuitumikia; kwa hiyo ameyaleta mabaya haya yote juu yao.

 

Tunaona hapa kwamba Sulemani aliweka utaratibu huohuo kwa Walawi na manabii chini ya Gadi, mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii, pamoja na matoazi, vinubi na kayamba zilitumika kwa madhumuni maalumu. Makuhani walisimama na tarumbeta kama wito wa mamlaka. Hii iliendelea hadi kwenye Marejesho ya Hezekia na ilikuwa muhimu kwenye utaratibu wa Hekalu.

 

Anguko na Ukosefu wa Rehema

Yeremia anatukumbusha ukosefu wa rehema kwa Yuda. Pamoja na ukosefu huu wa rehema ulikuwa na ukomo wa muziki kwenye furaha na kusifu.

 

   Maombolezo 5:1-22

Ee Bwana, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu. 2 Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni; Na nyumba zetu kuwa mali ya makafiri. 3 Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; Mama zetu wamekuwa kama wajane. 4 Tumekunywa maji yetu kwa fedha; Kuni zetu twauziwa. 5 Watufuatiao wa juu ya shingo zetu; Tumechoka tusipate raha yo yote. 6 Tumewapa hao Wamisri mkono; Na Waashuri nao, ili tushibe chakula. 7 Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao. 8 Watumwa wanatutawala; Hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao. 9 Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu; Kwa sababu ya upanga wa nyikani. 10 Ngozi yetu ni nyeusi kama tanuu; Kwa sababu ya hari ya njaa ituteketezayo. 11 Huwatia jeuri wanawake katika Sayuni; Na mabikira katika miji ya Yuda. 12 Wakuu hutungikwa kwa mikono yao; Nyuso za wazee hazipewi heshima. 13 Vijana huyachukua mawe ya kusagia; Na watoto hujikwaa chini ya kuni. 14 Wazee wameacha kwenda langoni; Na vijana kwenda ngomani. 15 Furaha ya mioyo yetu imekoma; Machezo yetu yamegeuka maombolezo. 16 Taji ya kichwa chetu imeanguka; Ole wetu! Kwa kuwa tumetenda dhambi. 17 Kwa sababu hiyo mioyo yetu imezimia; Kwa ajili ya hayo macho yetu hayaoni vema. 18 Kwa ajili ya mlima Sayuni ulio ukiwa, Mbweha hutembea juu yake. 19 Wewe, Bwana, unadumu milele; Kiti chako cha enzi ni tangu kizazi hata kizazi. 20 Mbona watusahau sikuzote; Na kutuacha muda huu mwingi? 21 Ee Bwana, utugeuze kwako, nasi tutageuka; Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale. 22 Isipokuwa wewe umetukataa kabisa; Nawe una hasira nyingi sana juu yetu.

 

Iliendelea wakati wa utumwa, kama tunavyoona kutoka kwenye kitabu cha Danieli. Matumizi ya muziki yalitumika pia kwenye ibada za miungu migeni na pia na kwa wanaume waliotaka kuwa miungu.

 

Danieli 3:1-19

Nebukadreza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli. 2 Ndipo Nebukadreza akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha. 3 Ndipo maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, wakakusanyika ili kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha; wakasimama mbele ya ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. 4 Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi, 5 wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. 6 Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao. 7 Basi wakati huo, watu wa kabila zote walipoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, watu wote na mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. 8 Basi baadhi ya Wakaldayo wakakaribia, wakaleta mashitaka juu ya Wayahudi. 9 Wakajibu, wakamwambia mfalme Nebukadreza, Ee mfalme, uishi milele. 10 Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba kila mtu atakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, ni lazima aanguke na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu; 11 na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa katika tanuru ya moto uwakao. 12 Wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na Abednego; watu hawa, Ee mfalme, hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. 13 Basi Nebukadreza akatoa amri kwa hasira na ghadhabu, waletwe hao Shadraka, na Meshaki, na Abednego. Basi wakawaleta watu hao mbele ya mfalme. 14 Nebukadreza akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? 15 Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu? 16 Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. 17 Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. 18 Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. 19 Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto.

 

Tunapaswa kupambanua matumizi sahihi nay a kweli ya muziki kwenye ibada na sio kunaswa na ibada za sanamu na ibada nyingine za uwongo.

 

Marejesho

Wakati sadaka za kuteketezwa zilipoanza, wimbo wa kumuimbia na kumsifu Bwana ulianza pia. Kwa hiyo Muziki ulikusudiwa kuwa ni kiini cha utoaji wa sadaka kwa Bwana.

 

2Nyakati 29:25-30

25 Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa Bwana wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani Bwana aliamuru hivi kwa manabii wake. 26 Wakasimama Walawi wenye vinanda vya Daudi, na makuhani wenye mapanda. 27 Hezekia akaamuru kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Na wakati ilipoanza sadaka hiyo ya kuteketezwa, ukaanza na huo wimbo wa Bwana, na mapanda, pamoja na vinanda vya Daudi mfalme wa Israeli. 28 Na kusanyiko lote wakaabudu, waimbaji wakaimba, wenye mapanda wakapiga; haya yote yakaendelea hata ilipomalizika sadaka ya kuteketezwa. 29 Hata walipokwisha kutoa sadaka, mfalme, na hao wote waliokuwapo naye, wakasujudia, wakaabudu. 30 Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie Bwana sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainama vichwa, wakaabudu.

 

Kwa hiyo muziki na uimbaji ni kiini cha ibada na marejesho.

 

2Nyakati 34:12-14

12 Nao watu wakatenda kazi kwa uaminifu; na wasimamizi wao walikuwa Yahathi na Obadia, Walawi, wa wana wa Merari; na Zekaria na Meshulamu, wa wana wa Wakohathi, ili kuihimiza kazi; na wengine katika Walawi, wote waliokuwa wastadi wa kupiga vinanda. 13 Tena walikuwa juu ya wachukuzi wa mizigo, wakawahimiza wote waliotenda kazi ya huduma yo yote; na miongoni mwa Walawi kulikuwa na waandishi, na wasimamizi, na mabawabu. 14 Nao walipotoa ile fedha iliyoletwa nyumbani mwa Bwana, Hilkia kuhani akakiona kitabu cha torati ya Bwana iliyotolewa kwa mkono wa Musa.

 

Wanamuziki Walawi walikuwa hivyo pia kwamba waliuwa na ufundi kama wa watendakazi wengine, na, walipohudumu kikamilifu na kwa uaminifu, Bwana alifanya marejesho ya Torati ya Mungu na Roho ya Unabii kwa watumishi wa Mungu.

 

Torati au Sheria ya Mungu ilikuwa ndiyo kiini pia cha kulirejesha taifa. Wakati Ezra alipolirejesha taifa, hata kwa kuweka msingi wa Hekalu, huduma ilikuja moja kwa moja kwenye mavazi yao rasmi na baragumu na zana zingine za muziki sawasawa na utaratibu uliowekwa na Daudi, kama tunavyoona hususan kwenye kitabu cha Zaburi. Hii ilikuwa inafanyika kutka kwenye muandamano wa matukio ya Sikukuu.

 

Ezra 3:1-13

Hata ulipowadia mwezi wa saba, na wana wa Israeli walipokuwa katika miji yao, watu wakakusanyika pamoja huko Yerusalemu kama mtu mmoja. 2 Ndipo akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani, na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa Israeli, ili kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake, kama ilivyoandikwa katika torati ya Musa, mtu wa Mungu. 3 Wakaiweka madhabahu juu ya msingi wake; maana hofu imewashika kwa sababu ya watu wa nchi; wakamtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu yake, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni. 4 Wakaishika Sikukuu ya Vibanda, kama ilivyoandikwa, wakatoa sadaka za kuteketezwa za kila siku kwa hesabu yake, kama ilivyoagizwa, kama ilivyopasa kila siku; 5 na baadaye sadaka ya kuteketezwa ya daima, na za mwandamo wa mwezi, na za sikukuu za Bwana, zilizoamriwa na kuwekwa wakfu, na za kila mtu aliyemtolea Bwana sadaka kwa hiari yake. 6 Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba walianza kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa, lakini msingi wa hekalu la Bwana ulikuwa haujawekwa bado. 7 Tena waliwapa waashi na maseremala fedha; wakawapa watu wa Sidoni, na watu wa Tiro, chakula, na vinywaji, na mafuta, ili walete mierezi kutoka Lebanoni mpaka Yafa kwa njia ya bahari, kwa kadiri walivyopewa ruhusa na Koreshi, mfalme wa Uajemi. 8 Hata mwaka wa pili wa kufika kwao nyumbani kwa Mungu, huko Yerusalemu, mwezi wa pili, Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zao wengine, makuhani na Walawi, na watu wote, waliotoka katika uhamisho na kufika Yerusalemu, wakaanza; nao wakawaweka Walawi, hao wenye miaka ishirini na waliozidi, ili kuisimamia kazi ya nyumba ya Bwana. 9 Ndipo wakasimama Yeshua, na wanawe na ndugu zake, Kadmieli, na wanawe, wana wa Hodavia, pamoja, ili kuwasimamia hao wafanyao kazi katika nyumba ya Mungu; wana wa Henadadi, pamoja na wana wao, na ndugu zao, Walawi. 10 Hata wajenzi walipouweka msingi wa hekalu la Bwana, wakawaweka makuhani, wamevaa mavazi yao, wenye baragumu, na Walawi, wana wa Asafu, wenye matoazi, ili wamhimidi Bwana, kama alivyoagiza Daudi, mfalme wa Israeli. 11 Wakaimbiana, wakimhimidi Bwana, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi Bwana, kwa sababu msingi wa nyumba ya Bwana umekwisha kuwekwa. 12 Bali makuhani wengi, na Walawi, na wakuu wa mbari za mababa, waliokuwa wameiona nyumba ya kwanza, wakati msingi wa nyumba hii ulipowekwa mbele ya macho yao, walilia kwa sauti kuu; na watu wengi walipiga kelele za furaha; 13 hata watu wasiweze kupambanua kelele za furaha, na kelele za vilio vya watu; maana watu walipiga kelele kwa sauti kuu, na kelele zao zikasikilikana mbali sana.

 

Kwa hiyo, kwenye uwekaji wakfu wa kuta za Mji Mtakatifu wakati wa Nehemia, utaratibu huohuo ulifanyika, na ulitumika katika kuwatakasa watu na mji na kuta zake na malango yake.

 

Nehemia 12:27-30

27 Basi, walipouweka wakfu ukuta wa Yerusalemu wakawatafuta Walawi katika mahali pao pote, ili kuwaleta Yerusalemu, wapate kufanya wakfu pamoja na furaha, na kwa shukrani, na kwa kuimba, kwa matoazi, vinanda na vinubi. 28 Waimbaji wakakusanyika kutoka uwanda na viunga vya Yerusalemu, na kutoka vijiji vya Wanetofathi; 29 tena toka Beth-gilgali, na toka mashamba ya Geba na Azmawethi; kwa maana waimbaji hao walikuwa wamejijengea vijiji katika viunga vya Yerusalemu. 30 Makuhani na Walawi wakajitakasa, nao wakawatakasa watu, na malango, na ukuta.

 

Tunaona kwamba muziki ni sehemu ya kiini cha ibada kwenye utaratibu wa Mungu, na unaweza kutumika kwa wema au kwa ubaya. Katika Siku za Mwisho, Amosi 8:3 inaeleza matumizi yake kwenye ibada kama ni makelele tu. Namna nyingi za ibada za leo zimebadilika na kuwa howling, zinazofanya na watu wasiovaa kiheshima wakiingia kwenye nyumba za ibada na kutoa sauti zao kwa namna ambayo haistahili kufanywa kwenye ibada za kumuabudu Mungu. Yakobo 5:1 na kuendelea, inasema kwamba katika siku hizo matajiri watajitapa na kujisifu pia kwa matumizi mabaya ya Baraka zao na utajiri wao.

q