Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[034]

 

 

 

 

Roho ya Kufanywa Wana

(Toleo La 2.1 19940604-20000620)

Jarida hili linahusika kuelezea dhana ya wokovu kwa kufanyika kuwa Mwana wa Mungu. Fundisho la Kuzaliwa Mara ya Pili limechambuliwa na dhana yenyewe kama ilivyokuwa kwenye Kanisa la kwanza na jinsi ilivyoendelezwa. Historia ya Agano la Kale imechambuliwa na mchakato wa kukubalika na Baba unaonyeshwa. Mchakato wenyewe unahitaji unyenyekevu kamili kwa Baba ambao unahitaji tendo la ukombozi.

                  

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 1994, (ed. 1997), 2000 Christian Churches of God)

(tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Roho ya Kufanywa Wana



Utangulizi

Makanisa ya mwanzoni baadhi yetu tungeweza kufundishwa kwamba Mungu “anajiongeza mwenyewe” kwa kupitia kwa mwanadamu. Ilifundishwa kwamba mchakato huu wa “kuzaliana” ulichapishwa kupitia kwenye mlinganisho wa utungaji wa mimba na uzazi au kuzaliwa. Kwa uwazi kabisa ilisemwa kwamba wakati mtu anapobatizwa na kumpokea Roho wa Mungu, ndipo anakuwa “ametungwa mimba” akiwa kama kiumbe muhimu wa Mungu. Mawazo ya mwanadamu na roho vilifananishwa kama kiluwiluwi au yai ndani ya mwili wa mwanamke. Roho wa Mungu anafananishwa kama “seli takatifu ambayo ni mbegu pia” inayoingia kwenye lile “yai” na, kwa hiyo kutunga mimba ya kiumbe kipya cha kiroho.

 

Kanisa kwa upande mwingine lilifananishwa na mwili wa mwanamke, na hasahasa tumbo lake. Kiumbe kipya anayefanyiwa mtungo wa mimba na Mungu kinatakiwa kiwe kimeambatanishwa kiuimara kwenye “ukuta wa kupitishia mkojo” wa mama—na ndivyo ilivyo kwamba Wakristo wanahitaji kushikamana kwa uimara wote na Kanisa na kupata malisho kutoka kwenye maelekezo ya huduma na sharika zao zinazofananishwa na mwili. Iwapo kama Mkristo ataachana na bodi ya Kanisa, inaweza kuwa kama “utoaji mimba” wa kiroho na matokeo yake yatakuwa ni “kifo au mauti ya kiroho” ya Mkristo Yule. Iliwapasa Wakristo wakulie kwenye mwili ambao ni Kanisa, hadi kufikia ufufuo wa kwanza wa wafu wakiwa “wamezaliwa mara ya pili” wakiwa kama viumbe kwenye ulimwengu war oho. Rejea za Agano Jipya kuhusu “kuzaliwa mara ya pili” kwa kweli zilikuwa zinataja na kuuelezea mchakato,huu wa “mwenendo wa kiroho na kuzaliwa kwenye ufufuo wa wafu".

 

Yote kwa yote ulikuwa ni mlinganisho wa wazi na ufafanuzi wa mchakato wa uongofu wa Mkristo na mpango mzima na kusudi la Mungu.

 

Hata hivyo, ilikuwa ni ukweli wa mlinganisho usio wa kibiblia.biblia haisemi wala kuuelezewa mchakato wa wongofu wa Mkristo na kukua kwa mambo ya kifikra wakati wa ubatizo na kuzaliwa kwenye ufufuo wa wafu. Ilikuwa ni kwa ajili ya kutolielewa neno lililotumika kwenye Kiingereza cha Zmani kuhusu neno uzawa ambalo linaonekana kwenye tafsiri ya KJV, linalopelekea mlinganisho huu mpotofu. Neno kuzaliwa halimaanishi mtungo wa mimba; bali linamaana ya kwa baba. Mlinganisho wa kibiblia wa kzaliwa mara ya pili ni kwamba tunakuwa tumezaliwa upya au tumezliwa upya kwa njia ya wongofu na ubatizo. Tangu hapo inatupasa kukua kimwili na kifikra kama Wakristo hadi tufikie kikamilifu tabia ya Yesu Kristo.

 

Lakini sio tu kuwa ulikuwa ni mlingano huu usio wa kibilia, bali ililazimisha pia uelewa mpotofu wa vifungu vingine vya Maandiko Matakatifu. Kwa mfano, kwenye Warumi 8:15 tunasoma:

Warumi 8:15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.

 

Ilisemekana kwamba neno lililotafsiriwa kuwa kufanywa wana kwenye kifungu hiki halimaanishi kufanywa wana kabisa, bali zaidi sana linamaanisha uwana – ambavyo kwamba Mungu anajiongeza mwenyewe na kwamba sisi tunafanyika kuwa wana halisi, na sio kuwa ni wana wake kwa kuasiliwa. Msaada wa hilo umechukuliwa kutoka kwenye uwezekano wa tafsiri mwenza kama vile ya RSV ambayo inasema hivi:

Warumi 8:15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.

 

Ni kweli, aya ya 23 ya sura hiyohiyo kwenye RSV haikunukuliwa! Inasomeka hivi:

Warumi 8:23 Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.

 

Kwa hiyo, kwenye tafsiri moja tuna neno kuasili, na kwenye nyingine tunapata maana mbili zote za kuasili na kufanywa wana na bado kuna nyingine (kama vile Moffatt) neno uwana linatumika kiutofauti kabisa. Je, habari ya kweli hapa ni ipi? Je, ni kweli kwamba sisi ni wana wa kie na wa kiume wa Mungu, au ni watoto tulioasiliwa tu? Je, Paulo anajua lolote kuhusu “kuzaliwa mara ya pili” na ulinganisho wake? Je, tafsiri hii nyingine iliyo kati ya hizi nyingine nyingi zinamakosa kwa kuwa watafsiri wake hawakujua ukweli kuhusu makusudi ya Mungu kwa mwanadamu, au kwa kuwa walikuwa wanajaribu kulificha? Kutumia usemi kwamba,  "Ni mtego kiasi gani?"

 

Msimamo wa Kisomi na uaminifu wa kutumia akili

Kwa kuhusianisha na jambo hili au dhana ya “kuzaliwa mara ya pili” kura waliojulikana wakisema kama tukiliiodhoa mlinganisho wa dhana hii ya “kuzaliwa mara ya pili” ya tutungwa mimba wakati wa ubatizo na kuzaliwa tena kwenye ufufuo wa wafu, ndipo tunakuwa tunaiharibu kabisa dhana iliyoko kuhusu “Familia ya Mungu”. Zaidi sana, ni kwamba kama hatutakubaliana kwamba Wakristo wata “zaliwa mara ya pili” kama viumbe wa kiroho kwenye ufufuo wa wafu; kama hatutakubali kuwa wongofu kwa hakika ni “kutungiwa mimba” kiroho na kwamba maisha ya Mkristo ni sawa na "kipindi cha mtungo wa mimba" ndani ya mwili au tumbo la mama (ambalo ni Kanisa), ndipo dhana yote ya Mungu kujiongeza mwenyewe itakosa mashiko – na sambamba yake ni, ‘Familia ya Mungu".

 

Hata hivyo, mtindo huu we kufikiri na kujiuliza hauna maana. Mtu huyu amechukua kile ambacho haya hivyo, ni mlinganisho, na tafsiri iliyoaminika na kuwa na mashiko katika karne ya ishirini kwenye vifungu fulani vya Biblia, na vkakubalina na kutiliwa mkazo kuwa ni kweli. Kwa kweli, kuielewa Biblia kama ilivyokusudiwa ieleweke, kwa kujumuisha desturi na mpangilio wa siku zilivyowekwa wakati ilipoandikwa, na kumruhusu Roho Mtakatifu atuongoze kuielewa na kwa kuelewa huko na kweli, wengine wanaamua badala ya kuyapa kipaumbele mawazo na tafsiri ya wanadamu kuwa ni kama mwongozo mtakatifu usio na makosa kwa kile kilicho kweli. Watajikita kushikilia mawazo yaliyopita na fafanuzi zake, licha ya makosa yaliyomo ndani yake.

 

Kwenye Makanisa ya Kikristo ya Mungu, lengo letu ni kutafiti, kufundisha, na kuitangaza kweli bila woga au kumpendele mtu yeyote. Tunajitahidi kuwa waaminifu kiakili, na kuwa na uelewa wa kutosha kimafundisho kwenye utafiti wetu na kuwa tayari kuukubali na kuupokea ukweli ulio kwenye Biblia, hata kama “utaumiza” au kwma utaendana kinyume na mawazo ya zamani, na haijalishi ni kwa kiasi gani “yalipendwa” na sisi. Petro na Paulo wanatuonya sisi kwa kusema hivi:

1Petro 4:10-11 kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. 11 Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.

 

2Timotheo 2:15 Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.

 

Mungu anajiongeza mwenyewe

Kabla hatujasoma somo hili la kufanyika kuwa wana tunapaswa kujua kwamba Mungu kwa kweli anajizidisha, au anajiongeza mwenyewe, kwa maana ya kwamba anawaumba watu wakiwa ni viumbe wanaoongez na ambao wanashiriki asili yake, kwa jinsi amnavyo tabia zake zimewekwa. Mungu kwa kweli anajiongeza mwenyewe kwa wengi, wana wengi wakiume. Kristo alikuwa mzaliwa wa kwanza wa wanawe na ni wa uzao uliotokana na asili ya Mungu:

2Wakorintho 4:4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

 

Wakolosai 1:12-15 mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. 13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; 14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; 15 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.

 

Waebrania 1:3 Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;

 

Inafurahisha kuona kwamba kwenye Kiyunani neno lililotafsiriwa kujiongeza kikamilifu kiuzao hapo juu ni tabia (SGD 5481) ambalo kutoka kwalo ndipo tumepata neno la Kiingereza lenye maana ya mwenendo. Tafsiri ya Thayer ya Lexicon yenye mchanganyiko wa Kiyunani na Kiingereza inatoa maana ifuatayo kuhusu hii:

1.      Kifaa kilichotumika kuchongea au kuwekea umbo

2.      alama iliyowekwa kwenye kifaa kile au kileondolewa mbali ya hiyo

a) alama au kitu kilichochosemwa kwenye (Walawi 13:28) au kilichowekwa juu yake, kuonyesha.

b) uonyesho halisi (kilicholengwa) cha mtu yeyote au kitu, kilionyesha kufanana, ongezeko halisi la kiuzazi kwa kila chenye kutamanika, yaani nukushi.

 

Kwa hiyo, Kristo alikuwa na tabia za Mungu au asili “iliyowekwa ndani yake” kwenye uzaoi chake (uliotajwa hapo juu kama akishirikishwa kwenye utukufu wa Mungu).

 

Inafurahisha sana pia kuona kwamba neno la Kiyuani lililotafsiriwa kama kuchukua sura na umbo na kuichukua hali kufanywa wana hapo juu ni eikon kutoka kile tunachopata kwenye neno la Kiingereza icon. Lina maana ya sura, umbo, kufanana; mfano wa vitu vya mbinguni; nk. Imetumika katika kumuelezea Kaisari kwenye picha zilizotumiwa kuandikwa kwenye sarafu za Warumi (Luka 20:24), wakristo walio na sura na tabia za Adamu na Adamu wa Pili (1Wakorintho 15:49), sura na mafano wa wanadamu na wanyama iliyoyumiwa kwenye ibada za sanamu (Warumi 1:23), na “Sura na Mfano wa Mnyama” (Ufunuo 15:13). Kwenye kila tukio inaelezea kitu ambacho ni nakala ya kitu fulani kingine kinachotokana na kitu asilia kwenye muonekano na au kazi na utendaji wake. Kristo ni mjumbe wa Mungu kwa maana ya asili na tabia zake na mwenendo wake.

 

Kwa jinsi hiyohiyo, Wakristo wanabadilishwa kwenye nakala, kufanana, au sura na tabia ya Kristo (na kwa hiyo kuwa na sura na mfano wa Mungu). Kwa hiyo, Mungu anajiongeza mwenyewe moja kwa moja kwa maana ya asili yake na tabia yake kwa wanadamu. Tumeumbwa kwa “sura na mfano wa Mungu” tayari kutokana na inavyosema Mwanzo 1:26 na 1Wakorintho 11:7 na kutoka hapo tunakuwa tunakuwa na uwezo kama Mungu wa kimawazo, kufikiri, na uwezo wa kufanya maamuzi na kujijengea tabia.

 

Mwanzo 1:26   Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

 

1Wakorintho 11:7 Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.

 

Lakini tumebadilishwa kutoka kwenye umbo hili lenye kuwa na mpaka wa kiuwezo na kuwa na umbo lenye tabia kamilifu ya Mungu na asili yake.

 

2 Wakorintho 3:18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.

 

Wakolosai 3:10 mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.

 

Huu ni mchakato ambao hautakamilika hadi ufufuo wa wafu.

1Wakorintho 15:49 Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.

 

Suala ni kwamba Mungu anajiongeza mwenyewe ndani ya wanadamu/ amekwisha jiongeza tayari kwa wenyi – huenda kwa mamia na mabilioni ya watoto wa kiroho ambao tunawaita kuwa malaika na ataukamilisha mchakato na wanadamu kwa kipindi chake alichokikusudia kwenye mpango wake wa wokovu.

 

Warumi 8:29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

 

Waebrania 2:10-11 Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso. 11 Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;

 

Kile tunachokishughulikia wakati tunapotathimini somo hili la kufanwa wana sio tu kule kuwa I kaama Mungu anajiongeza mwenyewe au sivyo, lakini zaidi tu ni ulinganisho utakaotusaidia kuelewa mambo fulani yaliyo kwenye mpango wa Mungu wa wokovu.

 

Vifungu vya Maandiko

Neno hili kufanywa wana linaonekana kwenye maandiko yafuatayo ya Biblia:

Warumi 8:15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.

 

Warumi 8:23 Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.

 

Warumi 9:4 ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake;

 

Wagalatia 4:5 kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.

 

Waefeso 1:5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.

 

Neno lililotafsiriwa hapa kama kuasiliwa linatoka kwenye lugha ya Kiebrania la huiothesia (SGD 5206). Lilikuwa ni neno la viwango linalomaanisha kuasiliwa katika karne ya kwanza. Ilionekana kuwa ni neno la jumla linalomaanisha kuchakuliwa kama mwana.

 

Kwa Kiingereza, neno kufanywa wana limechukuliwa kutoka neno la Kilatini adoptare linalomaanisha kuchagua. Kwa upande mwingine, uwana linatokana na kutoka kwenye neno lenye chimbuko la lugha mchanganyiko ya Kihindo na Ulaya (Indo-European) linalomaanisha kuzaa. Tofauti iliyopo kati ya maneno ni kwamba maana moja ya kuchaguliwa, kuwa mwana na lingine ni kuwa mwana kwa kuzaliwa. Kwa hiyo inapotokea kutafsiri kuwa huiothesia, tafsiri sahihi zaidi ni kufanywa mwana na sio uwana ni kwa sababu kwenye desturi ya Warumi na Wayunani, dhana ya kuasiliwa lilitumika zaidi sana zaidi ya vile inavyofanya katika siku zetu. Ilikuwa inamaanisha kufanyika mwana au binti wa baba aliyemuasili kwa namna isiyotofaitshika na kutokana na kuwa mwana au binti kwa kuzaliwa. Hii itafafanuliwa kwa undani zaidi na kikamilifu kama tunavyoendelea.

 

Historia rejea ya Agano la Kale

Kitabu cha fasiri ya Biblia cha International Standard Bible Encyclopedia (ISBE), kwenye makala yake kuhusu Kuasili mtoto [Adoption] (Vol. 1, p. 53) inasema kwamba:

Desturi iliyoaminika kwa Wayunani, Warumi, na watu wengine wa zama kale (wakiwemo Wahurrians; soma jarida la ABRAHAM III); lakini haionekani kwenye Sheria au Torati ya Wayahudi.

 

Hakukuwa na posho maalumu inayojulikana bayana kwa shughuli hii ya kumuasili mtoto kwenye vitabu vya Torati. Hata hivyo, kuna mifano kadhaa ya kuasili watoto kwenye Agano la Kale:

 

Kinachofurahisha kuhuau mifano hii ni kwamba inatokea tu nje ya Palestina – katika Misri na Uajemi, nmbako desturi ya kuasili watoto ilikuwa imeshamiri. Kinachofurahisha zaidi pia ni kwamba kwenye Agano Jipya dhana hii inatokea kwenye nyaraka za Paulo, na hasa hasa zile zilizoelekezwa kwenye makanisa yaliyo nje ya Palestina. Ilionekana kwa hiyo kwamba zaidi ya kufanya mfano wa Agano la Kale au historia, Paulo alikuwa anatilia maanani au kulinganisha na uelewa wake wa ulimwengu wa Warumi ambako desturi hii ilikuwa inafanyika kwa kiasi kikubwa na ilikuwa na maana. (Wayunani, kama ilivyoelezewa, pia walifanya pia, lakini ilionekana kutoka kwenye waraka ambao ulikuwa na mfano wa Warumi aliokuwanao mawazoni mwake.)

 

Kufanywa wana – kwa sasa na zama ijazo

Paulo aliandika kuhusu kufanywa wana huku kuwa kutafanyika kwa zama zote mbili, yaani kwa mtazamo wa sasa na kwa zama ijayo. Kwenye Warumi 8:15 Paulo anasema kwamba tumapokea tayari roho ya kufanywa wana.

 

Warumi 8:15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.

 

Neno roho limeandikwa kwa herufi kubwa kwene bilib ya KJV, lakini kwenye Kiyunani asilia kulikuwa hakuna jinsi ya kutofautisha. Hii inaeleweka vyema kabisa kama “mmepewa roho (inayoshirikisha mawazo, nia, jinsi ya kufikiri) ya kufanwa wana”. Inadbaniwa kuwa uwepo wa Roho wa Mungu ambaye sisi tumefanywa kwaye au kuchaguliwa kuwa wana wa Mungu mwenyewe, na tunaweza sasa kumuita asi kukosea na kwa jina la uhusiano wa karibu kuwa ni Aba ambalo ni neno la Kiaramu lenye maana ya Baba. Kuwa na Roho wa Mungu kunabadilisha njia au namna yetu ya kufikiri. Inaonyesha pia ni kama mmoja wa wana wa nyumbani mwa Mungu, na ni sehemu ya familia yake.

 

Waefeso 2:19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.

 

Wadhifa wetu mpya umehuhudiwa hivyo kwa Roho wa Mungu na roho zetu.

 

Warumi 8:16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

 

Kwakuwa Mungu ni Baba yetu, nasi ni watoto wake (kwa usemi wa kawaida), basi tunakuwa pia ni warithi, tuurithio kila alichonacho.

 

Warumi 8:17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.

 

Lakini mchakato wetu wa kufanywa wana haujakamilika bado.

 

Warumi 8:23 Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.

 

Ufafanuzi wa kile anachokimaanisha Paulo kwa hii umetolewa kuelekea mwishoni mwa jarida hili.

 

Kufanywa wana huku kunafanywa na Baba

Biblia ya ISBE inasema kwamba:

Nia na msukumo wa kufanywa wana huku kila mara kunatuama kwa baba anayetufanya kuwa wana, na ambaye anafanya upungufu wa kizazi asili na kukidhi madai ya kufanyika hivyo na kidini, na hamu na kufanya mamlaka makubwa ya kiubaba au kuendeleza familia yake. (ibid.)

 

Mwenendo na msukumo wa kufanywa wana mara zote unaendana na kitendo hiki cha kufanywa wana na baba. Nia ya baba ilikuwa ni kusaidia kuliendeleza jina la familia, na kukithi mahitaji yake binafsi na hamu ya kuonyesha athari au madhara kwa mtoto wake.

 

Tunaanza kuona hapa kwa nini Paulo alitumia mlinganisho huu kushughulikia wito wa Mkristo na wongofu wake. Mungu ndiye anayewezesha wito wetu. Lakini sisi hatuwezi kuliwezesha hilo. Hatuweze tu kuamka siku moja na kuchagua kuwa Wakristo. Mungu ndiye anayepandikiza ndani yetu ile hamu ya kufanya hivyo na hata ile shauku ya kuitafuta kweli. Sio kwa ajili ya “wema” wetu, kwa kweli au kufikiri kwetu, kulikompelekea Mungu atuchague sisi.

 

Waefeso 2:8-9 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.

 

Yohana 6:44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho.

 

Yohana 6:65 Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.

 

Zaidi sana ni kwamba, Mungu anafanya hivyo kutokana na shauku yake ya kuiongeza familia yake, na kutuonyesha sisi upendo wake na athari zake.

 

Waefeso 2:4-7 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; 5 hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. 6 Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; 7 ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.

Mungu analiweka jina lake juu yetu.

 

Yohana 17:11 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

 

Ufunuo 3:12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.

 

Ufunuo 14:1 Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.

 

Kama Mkristo, tunapoipokea roho ya kufanywa wana, tunaungana na familia ya Mungu, tukiwa na sehemu ya baraka zake, na tunalikubali pando lake

.

Masharti muhimu makuu yanayotangulia kabla ya kufanyika wana

Tendo la kuasiliwa kwenye imani na utaratibu wa Warumi, wakati wote ulitanguliwa na masharti fulani muhimu yafuatayo:

 

Kitendo hiki cha kuasili watoto kilifanyika pia kama kigezo cha kustahilisha uhalali wa kuzipa nchi au dola fulani fulani stahili na haki zao. Mambo yote yaliwekwa juu ya uraia wa Warumi walioasiliwa ikiwa ni mchakato wa makini sana na sio kitu kilichofanywa kijuujuu.

 

Tena tuweza kunona hapa la kujifunza sisi.

 

 

Majina yetu yametajwa mbinguni, mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, mara nyingi sana tena na tena. Mungu hana kigeugeu au kubadilika kwa maana ya jinsi anavyowateua na kuwachagua watu wake. Kwa hiyo, ni kama wale waliochaguliwa na kuchaguliwa, hatupaswi pia sisi kufanya maamuzi kiranisi sana hivyo.

 

Waebrania 2:1 Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa

 

Waebrania 2:1 Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa. Vinginevyo tutafanana na meli inayopita mandarini ikiwa na mavunjiko.

 

Kujinyenyekeza kikamilifu kwa Baba

Tendo la kumuasili mtoto kwenye familia ya Kirumi kilimaanisha kuwa na unyenyekevu kamili kwa baba mpya. Biblia ya ISBE inaeleza kwamba Warumi walikuwa na neno maalumu kuhusu jambo hili, lililojulikana kama patria potestas, na lilimaanisha kunyenyekea kikamilifu kwa baba mpya, kiasi cha kufanana baribu kama mtumwa na bwana wake, kwa kipindi cha kadiri baba alivyokuwa hai anaishi.

 

Tendo la kuasiliwa na Mrumi kinatufundisha mambo makuu nay a muhimu mawili.

 

Tunapaswa kujinyenyekeza kikamilifu kwa Mungu kwa kila jambo.

 

Unyenyekevu huu na ushirika wa familia ya Mungu unapaswa kuendelea kwa kadiri Mungu aishivyo na, kwa kuwa Mungu ni wa milele, tunajua kwamba sehemu yetu tukiwa kama watu wa numbani mwake Mungu ni ya milele.

 

Mwanzishi wa Waebrania anaandika hivi:

Waebrania 12:7-10 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? 8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. 9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? 10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.

 

Sisi tunajinyenyekeza sasa kwa baba yetu kwa namna zote mbili za muadibisho, na kwenye urithi, na kwa njia nyingine yoyote kama tulivyofanyika kikamilifu kuwa ni wana na binti za Mungu ambavyo ndivyo tulivyo. Mahali petu tukiwa kama watu wa nyumbani mwake Baba na familia yake ni wa milele kwa kweli na ni hakika.

 

Zaburi 23:6  Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.

 

Kurehesha mahusiano yaliyopita

Desturi ya kuasili mtoto ya Kirumi ilihitaji mtu anayeasiliwa aseme wazi kabisa na akiri kwamba anaukana uhusiano na haki zote za familia aliyokuwako zamani huko nyuma, zikiwa ni pamoja na uhusiano wa kisiasa, na imani zote za zamani za kidini na kila alichokuwa anakitumikia.

 

Wakati akifanya hivi, mtoto aliyeasiliwa anahamisha kile rasilimali alizonazo kwa wakati huo na hata madeni na vingine atakazomudu kuzipata baadae kwa wazazi wake hawa wapya. Neno maalumu la kisheria lililokuwa linatumika kuelezea kitendo hiki, lilikuwa, per universitatem kuonyesha kwamba mchakato wote wa kubadilishana umekamilika. Sasa, hii haiwezi kuonekana kuwa ni wazo jema, lakini kulikuwa na motisha kwa mtoto aliyeasiliwa kwamba uhamishaji huu wa mali na stahiki ulikuwa unahusisha pia na madeni aliyokuwa anadaiwa, ili kwamba mtoto aliyeasiliwa aweze kuwa huru kutokana na madeni yake ya zamani.

 

Tunaweza kuyatendea kazi mambo haya kwa sisi wenyewe kwa hatua sababu na namna zifuatazo:

 

Mambo haya yameelezewa kwenye vifungu kadhaa vya maandiko.

 

1Petro 4:1-2 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. 2 Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.

 

Warumi 12:1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

 

Waebrania 13:15-16 Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake. 16 Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.

 

Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

 

Wakolosai 2:13-14 Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; 14 akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;

 

Yaliyohitajika na ya muhimu kwa ukombozi

Tendo la kumuasili mtu lilihitaji kuwa na mtu aliyehiyari kuasiliwa na mtu huyo anapaswa anunuliwe au akombolewe kutoka kwa wazazi wake asilia, na kwa kweli, mchakato wa kumuasili haukukamilika hadi pale hawa wazazi wapya watakapokuwa wameutimiza mchakato huu. Biblia ya ISBE inasema kwamba:

... kuasili kikamilifu (adoptio) ulikuwa ni mchakato ambao kwamba mtu alihamishwa kutoka kwenye mamlaka ya baba yake halisi na kuhamishiwa kwa yule baba mpya aliyemuasili, na ilifanywa kwa mauzo ya namna fulani yam toto huyo, na kitendo chake cha kujiachia au kujisalimisha kutoka kwa baba yake wa asili na sasa kuwa kwa baba mpya aliyemuasili. (ibid.)

 

Paulo alielezea jambo hili la matendo ya Warumi kwenye waraka wake kwa Wagalatia.

Wagalatia 4:4-5 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, 5 kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.

 

Mara tu ukombozi unapokuwa umefanyika, ndipo tendo la kuasili lilikuwa limekamilika. Kwa kweli, kitendo cha kumuasili kilikuwa kimekamilika na kilikuwa ni kilele cha mchakato huu, na mabadiliko ya wazazi yalichukuliwa kuwa ni kweli kabisa, na kwamba mtoto asliyeasiliwa alihudumiwa kwa muktada sawa na kama alikuwa ni mtoto asili na mzaliwa wa kwenye familia hiyo. Mtu aliyeasiliwa, anapofikisha umri tarajiwa au daraja tarajiwa la kimaisha, alichukua jina au daraja la kimaisha alilokuwanalo baba yake mpya aliyemuasili, na kulikuwa hakuna mamlaka yeyote iliyoweza kupunguza au kuyapuuzia mabadiliko haya.

 

Nasi kama Wakristo, tunampokea roho wa Baba yetu mpya, na kumuira kwa jina la Baba. Alianza maisha mapya, akiwa kama mtoto mpya wa Mungu, aliyezaliwa upya katika maisha ya kimakuzi na kimaendeleo cchini ya matunzo na uangalizi wa Baba yetu.

 

Warumi 6:4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

 

1Petro 1:3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu;

 

1Petro 1:23 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.

 

1Petro 2:2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;

 

Waefeso 4:13-15 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.

 

Matendo ya siri; kudhihirika kwake baadae

Hatimaye, hili ni jambo linalopendeza sana la desturi ya matendo ya Warumi ya kuasili watoto. Mchakato huu ulijumuisha na tendo la siri la kuasili, na ambalo hatimaye linafikia kwenye mdhihiriko wa wazi. Hii ndiyo aliyokuwa anafikiria Paulo alipokuwa anaandika waraka wake huu:

Warumi 8:23 Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.

 

Wakati unakuja, unaotajwa kuwa ni wa ufufuo wa wafu, wakati wale wote tuliowaasili wakiwa kama wana wa Mungu watatangazwa kwa wazi, nao watapokea utambulisho wa wazi. Lee dunia haitutambui kabisa kuwa sisi ni watoto wa Mungu kama ulivyomtambua Kristo. Lakini wakati unakuja wakati ukombozi wa miili yetu, ambao ni wa kubadilishwa kwetu na kuwa viumbe wa kiroho tulio mfano wa Kristo, na madai yetu ya kuwa ni wana kiume na wa kike wa Mungu watajulikana kwa wazi.

 

1Yohana 3:1-2 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.

 

1Wakorintho 15:49-53 Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni. 50 Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika. 51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.

 

Wafilipi 3:20-21 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; 21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.

 

Ufunuo 3:9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.

 

Wazo hili la kutangazwa au kudhihirika wazi kuwa ni wana wa kweli wa kiume na wa kike wa Mungu kwenye ufufuo wa wafu uliotajwa kwenye vifungu vingi kadhaa vya biblia vinavyohusisha uwana hu na ufufuo wa wafu, kwa matukio yote mawili, yaani ufufuo wa Kristo na Wakristo.

 

Warumi 1:3-4 yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili, 4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu;

 

Luka 20:34-36 Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; 35 lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; 36 wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.

 

Hitimisho

Kwa hiyo sasa tunaweza kuelewa ni kwa nini Paulo alitumia mfano wa kuasiliwa kwenye nyaraka zake. Ni kama mfano wa kimafundisho wa mifano ya Kristo, iliwasaidia kuelewa Wakristo wa wakati ule waliokuwa wanazisoma nyakara zake ujumbe na somo muhimu na la maana kuhusu kuingia kwenye familia ya Mungu na kuhusu mpango wa Mungu wa wokovu. Mlinganisho huu hauna namna nyingine wa kupungua kutoka kwenye ukweli wa kwamba kujiongeza mwenyewe kwa Mungu au kujiendeleza kwake kupitia wanadamu. Zaidi ya kuwa inaongeza kwenye uelewa wetu kuhusu Ubaba wa Mungu na uwana wa Wakristo.

 

Kwa neno la kisheria, huiothesia maana yeke ni mchakato wa kuasili mtoto, mchakato wa kumpeleka kwenye uwenyeji wa nyumba mpya. Kwa maisha halisi, inamaana ni hali ya kufanya ibada kamili, ambayo haina namna nyingine ya tofauti na ile inayotokana na kuzaliwa. Uhusiano uiliopo kati ya mzazi na mtoto ni sawa kabisa uwe imara kwa mambo yote mawili.

 

Paulo alikuwa anafundisha kwamba mtu ambaye hajafanyika kuwa mkazi wa nyumbani mwa Mungu kwa sasa ni mtoto wa kweli na ni mrithi stahiki, na hakuna namna ya kumtofautisha na Yesu Kristo. Paulo alitumia mlinganisho wa desturi ya Warumi ya kuasili watoto ili kuyapa uzito madai yetu ya kuwa ni wana wa Mungu kwa namna yoyote iwezekanayo, na kwamba haki yetu ya kisheria ya kuurithi na kutawala ulimwengu tukiwa pamoja na kiongozi na kaka yetu, Yesu Kristo.

                                                            q