Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[050]
(Toleo La 1.0
20030411-20030411)
Kwenye Injili fupi ya Yohana tuna hadithi moja
iliyoandikwa inayoonyesha jinsi maji yalivyogeuzwa kuwa divai kwenye arusi ya
Kana ya Galilaya. Tutaona kwamba hakuna sio tukio moja tu peke yake bali ni
mawili ambayo yameelezewa kufanyika hivyo. Tukio la pili ni agano ambalo
Ibrahimu na uzao wake waliloingia walifuate na kumti yeye Mungu wa Pekee na wa
Kweli.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati
Miliki © 2003 Peter Donis, ed. Wade Cox)
(tr.
2015)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Arusi iliyofantika na kuandikwa (Injili ya Yohana) ina maana katika
kuashiria wito wa kuitwa taifa la kimwili la Israeli, sadaka ya Masihi, na
kuwakusanya watu ambao waliwezesha kufanyika mwili au kundi la Kanisa.
Arusi hii iliyoandikwa inaashiria mfano wa ukombozi wa mwanadamu. Inaonyesha
kwamba Kristo ndiye msingi wa mpango wa wokovu. Arusi hii ni taswira ya ya
agano la Mungu linaloendelea. Tunaona jinsi linavyoendelea bado na limetolewa
Kanisani, watumishi wake, yeye Mungu Aliye Juu Sana. Mvinyo uliotolewa kwanza na
ukaisha ulioandikwa ni taswira ya dhabihu ya mnyama iliyokuwa inafikia kikomo,
na mvinyo mpya uliotolewa ni ishara ya agano jipya ambalo Kanisa linakwenda
kujumuisha nalo.
Hadithi inaanzia kwenye Yohana 2:1 kama hivi.
Yohana 2:1-10 Na
siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu
alikuwapo. 2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini
pamoja na wanafunzi wake. 3 Hata divai
ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. 4 Yesu
akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. 5
Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni. 6 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa
huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio
mbili tatu. 7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji.
Nao wakayajaliza hata juu. 8 Akawaambia, Sasa tekeni,
mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka. 9 Naye mkuu wa
meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka,
lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza
alimwita bwana arusi, 10 akamwambia, Kila mtu kwanza
huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo
dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.
Tunaangalia kwenye kila aya moja moja, kwa mpangilio wa ufafanuzi,
tukianzia aya ya kwanza ya Yohana sura ya 2.
Yohana 2:1 Na siku ya tatu
palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya;
Kuna mifano mingi kwenye Biblia inayotaja matukio yaliyotokea katika siku
ya tatu. Mojawapo na linalojulikana sana ni lile la Ufufuko wa Kristo kutoka
kwa wafu siku ya tatu. Tungeweza kufundisha somo la ukombozi, wokovu au uhai,
vinavyohusiana na matukio yaliyotukia siku ya tatu.
Mkusanyiko uliokuja kwenye arusi hii ulitokea siku ya tatu. Shughuli za
Arusi na ndoa siku za kale mara nyingi zilichukua siku nyingi sana na hapa tunaona
mfano uliotumika mara nyingi kwenye mpangilio wa mzunguko wa mwaka wa saba,
ambao vitu vingi vilianzia kwenye mwaka wa tatu ulio kwenye mzunguko mtakatifu.
Kuna mlingano mkubwa zaidi unaofanana na
Israeli wa zamani, ambao walikuwa wakikusanyika pamoja na kufika kwenye jangwa
la Sinai katika mwaezi wa tatu baada ya kuondoka Misri na kuingia kwenye agano na
Mungu (Kutoka 19:1). Matukio yalilo kwenye Kutoka sura ya 19 yanafanana na hili
la arusi liiyohudhuriwa na Kristo na wanafunzi wake. Makutano waliambiwa
wazifue nguo zao, jambo ambalo linafanana na vazi la mhusika wa arusi na kanzu nyeupe
la kuushinda ulimwengu huu (Ufunuo 6:11; 3:5) kuuvaa unyenyekevu (1Petro 5:5).
Mkutano uliambiwa kuwa tayari siku ya tatu (Kutoka 19:11,15). Kwa kuwa ilikuwa ni siku hii
ndipo Mungu, kwa kupitia Malaika wake, ambaye alikuwa ni Kristo, alijitokeza
machoni mwa watu wote (Kutoka 19:11) kuingiza kwenye agano.
Kutoka 19:10 Bwana akamwambia Musa, Enenda kwa watu hawa, ukawatakase
leo na kesho, wakazifue nguo zao, wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu Bwana atashuka katika mlima wa
Sinai machoni pa watu hawa wote.
Ndivyo ilivyo pia, kwamba Kristo alishirikiana na
wanafunzi wake, alikuja arusini, ambako agano kati ya bibi arusi (ambaye ni sawa
na Kanisa) na bwana arusi (anayefananishwa na Kristo) lilifanyika. Kristo
alipasa kujidhihirisha mwenyewe kwa kupitia ishara yake ya kwanza kwa
watumishi, ikiwaashiria wale walioitwa.
Tunaweza kuhitimisha pia kwamba hii siku
ya tatu iliyotajwa inamwambatano wa maana kwenye hadithi ya Yoshua 9:1-27. Kwa
jambo hili, wenyeji wa Gibeoni, wajulikanao kama Wahiti, walijua kwamba Bwana
Mungu alikuwa pamoja na Yoshua. Walijua kwamba wasipojitoa wenyewe kwenye
mikono ya Yoshua wasingeweza kuishi. Utoaji wao “viriba vikukuu na vyenye ngozi
iliyopasuka na kushonwa tena” kuliweka taswira ya hali yao ya kiroho wakati
walipolikaribia kundi la Israeli likiwa chini ya Yoshua.
Katika siku ya tatu Yoshua alifika kwenye miji yao. Tunaona la kujifunza
likiendelea. Yoshua mwana wa Nuni (maana yake ni Wokovuthe unapatikana kwa
kuvumilia) linaonekana kufanana na la Kristo (soma jarida la Yoshua, Masihi, Mwana wa
Mungu (Na. 134)). Wale waliokuwa ni wamataifa walipewa fursa ya
kupandikizwa kwenye mwili au kundi la Israeli/ Yoshua aliwauliza, “Ninyi ni
kina nani na mnatoka wapi?” Wahiti walimjibu kwa udanganyifu. Walimjongelea
Yoshua, na ingawa walikuwa ni majirani, walisema, “Sisi watumishi wako twatoka
nchi iliyo mbali sana”. Jambo hili lilionyesha au kuashiria hali ya kiroho
waliyokuwanayo.
Matukio haya yanakumbushia wakati Yesu alipokuwa na wanafunzi wawili zaidi,
yaani Filipo na Nathanieli (Yohana 1:43, 47), katika siku ya tatu baaya ya
kubatizwa kwake na Yohana Mbatizaji, Yesu alimuona Nathanieli anakuja kwake.
Kristo alisema, “Basi Yesu
akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli
kweli, hamna hila ndani yake.”, sio kama Wahiti waliomjia Yoshua kiudanganyifu. Kristo alimjua Nathanieli
kuwa ni mtu wa aina gani mara tu alipomfikia na kule alikotoka. Hii imeonekana
kwa ukweli kwamba Masihi ajimuona Nathanieli alipokuwa ameketi chini ya mti wa
mtini (Yohana 1:48). Alikuwa na tunda la roho. (Rejea kwenye jarida la Kuulaani Mtini (Na. 90)). Nathanieli alimjia Masihi bila hila wala
udanganyifu wowote, nia yake ilikuwa ni kuutafuta ukweli kwa moyo wake wote.
Hili linapasa kuwa ndilo lengo letu pia. Hakuna jinsi ya kumdanganya wala kumpumbaza
Mungu.
Mji wa Galilaya unatumika na kutajwa kwa namna hii, kwamba unaweza kufanana
na sisi, kama mtu mmoja mmoja au kama bodi ya kanisa. Galilaya inaweza kuwa na
maana zaidi kama ni sehemu mojawapo ya Israeli. Kusifiwa kwake kwa mema
kunaweza kutuelezea sisi kama mtu mmoja mmoja na kanisa. Tunaweza kuichukulia
Galilaya ili kumaanisha hilo:
Kristo alikuja kama nuru ing’aayo huko Galilaya ya Wamataifa, wale ambao
waliwahi kuishi gizani (Isaya 9:1). Kristo alikuja kuwaponya hata wenye magonjwa
na waliosumbuka ma maumivu miongoni mwetu (Mathayo 4:23). Tulimkaribisha Kristo
mioyoni mwetu (Yohana 4:45) na anatutumia sisi kuwafikia wengine (Yohana
4:3,4). Tumekuwa tukipewa roho ili kuyafundisha mataifa yote (Matendo 2:7).wale
wanaotusikia watajua kuwa sisi ni wake, katika Kristo kwa kuwa tunaongea kwa
lafudhi ya kipekee (Mathayo 26:73; Marko 14:70), ambayo ni tofauti na wengine.
Dunia hii haikanushiki kuwa inatutupa sisi nje, kwa kuwa sisi tunazishika amri
za Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo (Mathayo 26:69). Kristo anaonekana ndani
yetu, baada ya ufufuko wake (Mathayo 26:32) sasa, Kristo huyu anaishi ndani
yetu, sisi ni Kanisa linalomfuata yeye na ni kumtumikia yeye. Ili tuwe tumekuja
pamoja naye kwenye Yerusalemu ya Kiroho (Marko 15:41), mama wa sisi sote (Wagaatia 4:26).
Mawazo haya yameakisiwa kwa wanafunzi wake Kristo. Wanafunzi wote wa Masihi walikuwa ni Wagalilaya, na isipokuwa mmoja wao—Yuda Iskarioti (Mathayo 4:18; Yohana 1:43–44; Matendo 1:11; 2:7). Rejea kwenye vitabu vya hawa wafuatao Youngblood, R. F. (1995). Nelson's new illustrated Bible dictionary. Rev. ed. ya: Nelson's illustrated Bible dictionary; Includes index. Nashville: T. Nelson.
“na mama yake Yesu alikuwepo”
Maria (ambalo limetafsiriwa kimakosa, kwa kweli ni Mariamu) alikuwa
inayonekana kabisa kuwa alikuwa na uhusiano wa karibu na wa kidamu wa upande wa
bwana arusi. Kwa hiyo, hawakuhitaji kualikwa. Wajbu wake wa kwanza ulipasa kuwa
ni kusaidia kuandaa shughuli ya arusi, kwa kupangilia shughuli na kazi zote za
upande wa bwana arusi. Aliwajibika pia kuwaelekeza watumishi mambo ya kufanya.
Injili ya Yohana haitaji kabisa mama wa Yesu kuwa ni Maria. Hii ni kuonyesha tofauti, kama tutakavyoona baadae. Kama tujuavyo, mwanamke anawakilisha haiba ya kanisa au taifa (Ufunuo 12:4-6). Kwenye jambo hili, twaweza kutafsiri kuwa mama yake Yesu analiwakilisha taifa la kimwili la Israeli ya kale na ukuhani wa Walawi kwa kupitia uzao wa Ibrahimu.
Kuonekana kwake kama yuko hapo tayari, kunaonyesha jambo la kwamba anafanya taswira ya ukuhani wa Kilawi ambao walikuwa wanashiriki kwenye Agano na Mungu. Tunapaswa kutilia maanani pia ukweli wa kwamba mama wa Kristo alikuwa kwa sehemu ni Mlawi. Kwa kuhitaji msaada kunaweza kuashiria kwa jambo hili utaratibu wa kutoa sadaka ambao kwamba makuhani walihudumu kaka kitu cha kwanza kwenye agano.
Aya ya 2: Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja
na wanafunzi wake.
Ili kuwa sehemu ya wanaoshiriki sherehe za arusi, inabidi mtu aalikwe. Ni Mungu ndiye anayefanya uchaguzi. Kristo hahusiki na mchakato huu wa kukaribisha ndipo kusema kuwa Mungu ndiye anayemchagua mtu na kumpa Kristo (Yohana 6:39).
Kristo alikuja ili kufanya mfano wa bwana
arusi wa Kanisa (Mathayo 9:15; Marko 2:20). Wanafunzi waki watano waliokuja
pamoja naye wanaweza kuyawakilisha makanisa matano ya kwenye Ufunuo ambayo
yanamfanya bwana arusi ayafanye yaweze kuingia kwenye ufalme (pamoja na kila
mmoja anayefanyaiwezesha
kwa kupitia tangu kwa Makanisa ya Walaodikia na Wasardi). Kwa kina zaidi kuhusu somo hili, soma
jarida la Davudi na Goliathi (Na. 126).
Wakati
tunapolitazama hili kama agano kwenye mchakato, tunaona kwamba mwaliko wa
Kristo unakuwa wa makusudi ya namna mbili. Mwaliko wake ulitumwa maelfu ya miaka
huko nyuma kupitia Ibrahimu (Mwanzo 12:3, 22:18). Tazama pia jarida la Agano la Mungu (Na. 152).
Mwanzo 26:4 Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia. Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.
Ili kuupokea
mwaliko inahitaji kufanya kitu fulani kwa upande wetu. Ibrahimu aliupata
mwaliko wake wa kuingia kwenye agano na Mungu, kwa kuzishika amri na maagizo
yote ya Mungu, miongozo yake na sheria zake. Alizichukulia sheria za Mungu kuwa
ni kitu cha thamani kinachotakiwa kutamaniwa. Tunapaswa nasi pia kufanya
hivyohivyo, kama tunaukubali mwaliko huu. Yatupasa pia kulitii neno la Mungu na
amri zake, kama tutamkubali Roho Mtakatifu na kuingia kwenye sherehe ya arusi.
Mfano wa wanawali wapumbavu watano na werevu watano unaonyesha kwamba wale
walio na mafuta bado kwenye taa zao zikiwaka, waliweza kuingia kwenye karamu ya
arusi. Kwa mwonekano wan je, wote walionekana kufanana. Bali walikuwa ni wale
waliolithamini neno la Mungu na kuwa na Roho Mtakatifu, ambao waliweza kuingia
wakati bwana arusi aliporejea.
Mithali 21:20 Kuna
hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima; Bali mwanadamu
aliye mpumbavu huyameza.
Watu wote, wa
mataifa yote walihakikishiwa kuupata wokovu kwa kupitia Kristo.
Wagalatia 3:8 Na
andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa
kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe
Mataifa yote watabarikiwa.
Mungu, baba yetu alituchagua sisi kabla ya kuwekwa
misingi ya dunia na ametuweka kwenye mwili wa.
Waefeso 1:4 kama vile alivyotuchagua
katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu
wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Yatupasa tujue kwamba baada ya ubatizo Mkristo aliyeongoka anaambiwa awe
mtakatifu na asiwe na dawaa kwa wenzake na katka kumpenda kwake Mungu kwa
utakatifu (Walawi 19:2). Sheria zake zinatokana na asili yake au jinsi alivyo
yeye mwenyewe, kama tunavyoona; Sheria yake ni takatifu (Warumi 7:12). Sheria
zake zinadhihirisha upendo, kwakuwi pendo (1Yohana 4:16). Kwahiyo yatupasa kufikia
kwenye hi=atima hiyohiyo kama Ibrahimu, na Sulemani, walivyofanya, ambavyo ni
kumcha Mungu na kuzishika amri zake (Kutoka 12:13).
Tumepewa mwaliko mkuu (Isaya 55:1-13) pasipo kulipa gharama yoyote (Ufunuo
22:17) wa kuwa wana wa Mungu (soma jarida la Roho ya Kufanyika Wana (Na.
34)). Filipo kwa mfano alipewa mwaliko wa kumfuata Kristo
(Yohana 1:43). Ni mwaliko wa kuubeba msalaba (Marko 10:21). Ni wito wa kufanika
sadaka iliyohai (Warumi 12:1). Wengi wameipuuzia fursa hii (Luka 14:15-24).
Lakini hatujachelewa bado (Yoeli 2:12-13); kwa wale wanaoukubali mwaliko watabarikiwa
(Mathayo 25:34).
Aya ya 3: Hata divai
ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.
Hii ni kuonesha kwamba sadaka zote za wanyama walizozitoa makuhani
zingekoma na zilimlenga Kristo. Tungedhania kuwa ule mvinyo ulioisha wakati
sherehe hii ya arusi ingali ikiendele bado ilikuwa ni tawira ya mchakato wa
ukombozi ambao ulitafutwa kwa kupitis sadaka za wanyama zilizotumiwa na
Makuhani Walawi. Uandaaji wa arusi unapunguza nguvu utaratibu na mchakato wa
ukombozi wa mwanadamu. Utaratibu wa kutoa dhabihu ulikuwa ni budi ufikie mwisho
au ukome ili kuuwezesha utaratibu mpya uchukue mkondo wake. Damu wa mafahali ya
ng’ombe na ndama ilipasa imilike katika Kristo, ambaye afipangiwa afe mara moja
na kwa ajili ya wote (Waebrania 7:27, 9:24-28, 10:10,12,14; 1Petro 3:18). Mungu
alifungua njia ya wokovu kwa kupitia Kristo. Hii ndiyo sababu mama yake Yesu
alimwendea. Inatupasa kujua na kuzingatia dhana ya kwamba Mariamu hapa ni mfano
wa taifa lililo chini ya ukuhani wa kimwili. Namna ambayo Mariamu alimaanisha
nia na wajibu wake kwa mvinyo, inaonyesha na kumaanisha ukweli kwamba makuhani
walijua kwamba sadaka ya damu ya ilitakiwa na ilikuwa muhimu.
Hebu na tusahau sasa habari za wageni waliohudhuria arusi na kunywa mvinyo.
Neno yayin (SHD 3196) linatokana na shina la neno
lisilotumika la yayan – kuchachusha au kughoshiwa. Ilikuwa ni
mvinyo huu kama mvinyo ulioghoshiwa na kwa hiyo, inaweza kumaanisha pia kama
kulevya. Kuna mwingine ambazo zinamaanisha mvinyo huu ili usiweze kunywewa, na
kule kutajwa kwake mvinyo huu kwenye Biblia unatajwa juisi ya zabibu
zisizochacha. Mtazamo huu unachukuliwa kimakosa kwenye uelewa wake wa Maandiko Matakatifu.
(Rejea kwenye jarida la Mvinyo Kwenye Biblia (Na. 188)).
Kwene Maandiko Matakatifu mvinyo kwa kawaida unafananishwa na habari njema
na zene furaha. Wakati Mariamu aliposema, “Wameishiwa na mvinyo”, anaweza kuwa
alikuwa anamaanisha ukweli wa kwamba hawakuweza kuwa na furaha ya kipawa cha
Roho Mtakatifu (1Wathesalonike 1:6). Hata wanafunzi wa Kristo walipata ugumu
kuelea kile Masihi alichokuwa anajaribu kuwafundisha. Walikuwa wanaanza tu kwa
kweli kuelewa neno la Mungu wakati Roho Mtakatifu alipowashukia siku ya Pentekoste.
Mariamu alikuwa
na imini kubwa kwa mwanawe. Kungekuwa na idadi ya watu pale ambao wangemwonea
mashaka Kristo ukweli wa kwamba mimba yake ilitungwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Huenda mama yake angempasa akaguliwe ili kumthibitisha mbele y wote waliokuwepo. Mafarisayo kwa
mfano uliofuatia, walipokuwa wanaitetea haki yao, walitangaza walimpazia sauti zao kwa nguvu wakimwambia Yesu, “Sisi
sio watoto wa zinaa,” (Yohana 8:41), ikiashiria vile alivyokuwa Kristo.
Inayewekana kuwa huenda Mariamu alidhaniwa kuw wa namna hii kwenye fursa ya kueneza uvumi wa namna
yoyote aliyeweza kuwa amezungukwa.
Aya ya 4: Yesu
akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.
Kristo anaelekeza majibu yake kwa mama yake. Kristo anatumia neno ‘mama’
akimaanisha kimfano kulitaja taifa la kimwili ya Israeli na akionyesha ukuhani
wa kimwili.
Wagalatia 4:4 Hata
ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na
mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,
Tunaweza kudhani kwamba Kristo alikuwa anawaambia makuhani kwamba hawajui
anachokwenda kukifanya na kukianzisha kwenye agano lilolopo sasa na kwamba
utaratibu wa utoaji wa dhabihu walionao unakwenda kukamilika katika yeye.
Kristo anaonyesha tofauti kati ya utaratibu wa kimwili wa kidini wa siku zile
na kile alichokuwa anakwenda kukihitisha ambacho ni kuzaliwa tena kwa mwili wa
kiroho (Yohana 3:5).
Ndiyo, kipindi cha kutolewa kwa dhabihu ya Kristo ulikuwa umekaribia. Lakini
mchakato wote mzima unaoendelea yapasa uwe sawasawa,na mapenzi ya Mungu. Hatuwezi
kubadili ni nani, ni wakati gani, au jinsi ya yule,tunayemwabudu ambaye ni
Mungu wa Pekee wa Kweli.
Ukristo mamboleo uliopo sasa umepotoka kwa kutoelewa kile ambacho upande wa
pili wa agano hilihili inachohitaji na kwa ajili hii wanajikwaa (Waebrania 10:1-31).
(Rejea kwenye jarida la Tofauti Kwenye Torati (Na. 96)). Kusudi la Kristo limeshindwa kueleweka
na mashirika mengi ya kidini. Ili kuelewa vizuri zaidi jambo hili rejea majarida
ya: Lengo la Uumbaji na Sadaka ya
Kristo (Na. 160) na Kazi ya Mwasihi (Na. 226).
Aya ya 5: Mamaye akawaambia watumishi, Lo
lote atakalowaambia, fanyeni.
Maneno haya ya mama yake Yesu yanahusiana na maneno yaliyonenwa na Musa kuwaambia
Israeli wa kimwili kuhusu Masihi.
Kumbukumbu la Torati
18:15 Bwana, Mungu wako,
atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni
yeye.
Mama yake aliyewakilisha Israeli
ya kale, alielewa kwamba amri zilipaswa kushikwa (Kumbukumbu la Torati 26:17-19).
Sheria ya utoaji dhabihu ilikuwa inakubalika kwenye sheria zote (Kutoka 20 to
34). Sheria ya utoaji dhabihu ilimlenga \masihi na ilitimilika kwa yeye. Sheria
hii haikuondolewa kwa tendo hili. Mfuatano wa matukio ya utaratibu huu wa ibada
haukubadilishwa. Mfano shirio
wake ulikuwa na maana nyingine tu (soma jarida la Agano la Mungu (Na. 152)). Kristo alisema:
Mathayo 5:17-19 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au
manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa maana, amin,
nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya
torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. 19 Basi
mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha
watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu
atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
Tumeamriwa kuendelea kwenye sheria kamilifu na yenye uhuru (Yakobo 1:25).
Haya ni maneno ya mwisho yaliyoandikwa ya mama yake Yesu Kristo. Tunaona
kwamba walikuwa ni hawa wenyewe tu ndio walioambiwa wamtii Kristo. Hakuwaelekeza
watumishi wamwendee mtu mwingine yeyote. Kwa kuwa ni kwa huyo Kristo
tunaokolewa (Matendo 15:11). Tunaona kwamba Kristo anamsikiliza mama yake kulitenda
jambo hili. Hii inapotosha pia ukweli kwamba mwitikio wa maonyo ya unabii umekuwa
ukichukuliwa kuoka kwa makuhani wa kimwili wa Israeli ya zamani na limepewa
Kanisa, watumishi wa Mungu. Zipo kwenye uangalizi wa Kanisa sasa Maonyo ya Mungu (Na. 184)).
Tungedhania kwamba fundisho hili lingeweza kuonekana kuwa limechukuliwa na
wakati Kristo alipomuweka mama yake chini ya uangalizi wa Yule “mwanafunzi
aliyempenda””.
Yatupasa kuwa makini kwamba neno mwanafunzi
aliyempenda kwa maana kubwa kwamba aliwapenda wale aliopewa na Mungu.
Aliutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake (Yohana 15:13). Mwanafunzi aliyempenda laweza kuwa hi neno la mfano lililotumika
kulielezea Kanisa.
Yohana 19:26 Basi Yesu alipomwona mama
yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake,
Mama, tazama, mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na
tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake
Tunapoliangalia andiko hili kwa mwangaza wa yeye ambaye watu hawa wawili
wanaweza kujifunza kutoka kwake, tunaona kuwa Kristo alikuwa anaonyesha kuwa
Makuhani Walawi ambao Kanisa limeanzisha ulikuwa ni wa mwana wake. Alikuwa ni
kwa huyu mwanae kwamba urithi unakuwa. Kristo analiambia pia Kanisa kuwa
linapaswa kulijua na kuliheshimu agano walilopewa na kulishika Israeli wa
zamani. Tutakwenda kuiona hii imewekwa kwenye taratibu za kikanuni kwenye amri
ya tano isemayo Mheshimu Baba yako na
Mama yako (Kutoka 20:12). Tangu kifo cha Kristo, Kanisa linawajibika
kushika maagizo yaliyo kwenye Agano, pamoja na sheria zote na kanuni zake Mungu.
Katika siku moja, kama Maandiko Matakatifu yalivyonena kabla, kuna dhabihu
moja ambayo itakuja kuikomesha na kuundoa utaratibu wa utoaji dhabihu wa Walawi
(Malaki 2:3), kwa hiyo utaratibu mpya wa makuhani, ulio mfano wa ukuhani wa
Melkizedeki utaanzishwa. Ilikuwa ni kwa sababu hii ndio maana alipoambiwa kuwa
mama yake na ndugu zake wapo nje wanahitaji kuongea naye kwa mazingira
aliyokuwanayo ya kuongea na Mafarisayo aliwanyooshea kidole wanafunzi wake na
kusema: “Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!.” Alisema kuwa mama yake na ndugu
zake walikuwa ni wale waliokuwa wanayatenda mapenzi ya Baba yake aliye mbinguni
(Mathayo 12:46-50).
Wale wanaosadikika kuwa ni wafuasi wa Kristo leo na huku wakizipuuzia amri
na sheria za Mungu wapo kwenye kundi la waivunjao amri ya tano isemayo; mheshimu Mama yako na Baba yako. Kwa
kutozingatia na kuzikubali amri za Mungu na sheria zake mioyoni mwao, basi
walikuwa wanasema moja kwa moja kwamba walikuwa hawamchukui mama yake Kristo
majumbani mwao. Wangekuwa wamelikataa kulishika na agizo la Kristo la kuwataka
wamchukue na kumtunza huyo mama yake, kwa kuwa wangeona kuwa sheria za Agano la
Kale hazina ulazima wowote tena, na kwamba hazihitajiki kuzishika tena. Kwa
hiyo wangeivunja sheria kwa kutompenda na kumheshimu mama yake Kristo na
kumuona kama wa kwao.
Kumbuka kuwa Mariamu alikuwa na watoto wake wengine wa kiume
aliyewazaamwenyewe ambao angeweza kuondoka na kwenda kuishi nao. Lakini wakati
tunapomtathimini kila mmoja kwa kuchukulia mfano sehemu mbili la Agano la Mungu,
tunaona kwamba walipasa kuwekwa wawiliwawili na kuishi pamoja. Agano la kwanza
halikuwa limeondolewa na kukoma, bali liliendelea hadi kwenye hili la pili.
Mama yake Kristo hakumuomba msaada kila mtu pale arusini. Hamuombi kila mtu
kumwendea na kumpa mkono. Ni wale tu waliokuwa pale wamehudhuria ndio
walichaguliwa kwa kazi ile. Wale wanaomtii Mungu na Mwanae Yesu Kristo
walioelezwa kwenye Maandiko Matakatifu kuwa ni watumishi. (2Nyakati
24:9; Tito 1:1; Yuda 1:1; Yakobo 1:1; 2Petro 1:1). Kwa kuwa hilo ndilo lengo letu,
kutumika na si kutumikiwa.
1Wakorintho 4:1 Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za
Mungu.
Anawatumia watu dhaifu na wanyonge wa dunia hii ili kuwaaibisha wenye nguvu
(1Wakorintho 1:27).
Sisi, Kanisa, tunsaendea kumwabudu na kumii Mungu wa Pekee na wa Kweli,
Eloa, kuzishika Sabato zake, Miandamo ya Mwezi Mpya, Sikukuu zake na Siku zake
nyingine takatifu (soma jarida la Siku Takatifu za Mungu (Na. 97)). Hatujapewa mamlaka ya kuzivunja au kuziondoa sheria
za Mungu na kumuweka Eloa, Mwenyezi Mungu kwenye muundo wa Uungu wa kiutatu (soma
majarida ya Mungu Tunayemwabudu (Na. 2) na Amri Iliyokuu ya Kwanza (Na. 252)).
Aya ya 6: Basi
kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya
Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.
Mapokeo ya Kiyahudi yalihitaji kufanyika kwa uoshaji wa namna mbalimbali wa
kukamilisha maagizo na taratibu za kidini. Wayahudi walisisitiza sana kuosha
mikono yao kabla kula chakula, katikati yam lo na baada ya kumaliza kula. Aina
hii ya utakaso iliendelea sio kwa kuosha mikono yake mtu peke yake, bali pia ni
kwa mtu kuosha vikombe vyake na sahani zake (Marko 7:3, 4).
Vyungu vyenye maji vilitumika kwa kuhifadhia maji. Watu wamefananishwa na
vyombo kama hivi kwenye Biblia (Isaya
66:20). Vyungu hivi sita vya
kuhifadhia maji vinaweza kuwa vinawakilisha mwanadamu, kwa kuwa sita
inaaminika kuwa ni tarakimu mwanadamu. Vikiwa vimetokana na moto vingefananishwa
na ukweli kwamba kwa kuyaamini na kubobea kwenye mapokeo yaliyotungwa na
wanadamu, mioyo yetu ilifanyika kuwa migumu kama jiwe.
Kristo analiendeleza wazo hili wakati alipowakataa Mafarisayo. Kristo
alifundisha kwamba yatupasa tusafishe kwanza kile kilicho “ndani ya kikombe” na
ndipo hata kile kilicho nje kitakapokuwa kisafi pia (Mathayo 23:26). Kikombe kilitumika
kwa kuwa kilikuwa ni chombo kinachoweza kushikilia maji na kwa hiyo ni mfano wa
kifaa au chombo.
Nabii Ezekieli aliongelea juu ya kubadilishwa kwa vyombo hivi kutoka kwenye
moyo wa jiwe, na kufanyika kuwa ni vyombo vilivyojazwa Roho wa Mungu, vikiwa na
hamu ya kweli nay a kumaanisha ya kukaa kwenye neno la Mungu.
Ezekieli 36:25-27 Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na
uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. 26 Nami
nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo
wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na
kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.
Ezekieli
anaongelea usafi wa kunyunyiziwa na Roho Mtakatifu. Tutapewa moyo mpya na kwa hiyo
tutazitii sheria za Mungu. Sheria za Mngu ambazo zilikuwa zimeandikwa kwenye
mbao za mawe, zitaandikwa kwenye vibao vya mwili mioyoni (2Wakorintho 3:3).
Yatupasa
kusafisha mioyo yetu ya uovu na kutakasa mioyo yetu.
Yakobo 4:8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia
ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi
wenye nia mbili.
Vyombo hivi vya
utakaso bado vinatumika hata leo. Yatupasa tuweze kuona kwamba sisi vyombo vya
Mungu Aliye Juu Sana. Na kama tunazishika sikukuu za dini za kipagani,
zilizoanzishwa na wanadamu, kama vile sikukuu za Kristmas na Easter, ndipo kwa
kweli tunakuwa kama Mafarisayo. Tunachotakiwa kufanya ni kujisafisha sisi wenyewe
kwa nje, kwa muonekano peke yake, tukishuhudiwa na wote kuwa tunazishika sheria
zake ‘tukiziacha amri za Mungu na kuyashikilia kufuata mapokeo ya’ (Marko 7:8).
Yatupasa kutilia
maanani zaidi kutakasa mioyo yetu kwa kuzitii sheria za Mungu kwenye kweli yote.
1Petro 1:22 Mkiisha kujitakasa
roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki,
basi jitahidini kupendana kwa moyo.
Yatupasa tujiulize wenyewe swali hili, “Je, sisi bado tunajiosha kwa nje na
tukiwa hatuzishiki amri za Mungu? Je, bado tunaziadhimisha sikukuu zilizoamriwa
na siku nyingine zote za ibada kwa ajili ya mapokeo yaliyoanzishwa na wanadamu,
na hasahasa yakiwa chini ya mwavuli wa Mungu au dini? Je, tunamtii Mungu
kikweli? Je, tunao upendo wa dhati kwa wapendwa wenzetu wa imani moja? Je, mioyo yetu iko safi?”
Dunia hii ipo ili kutuonda sisi mbali kabisa na Mungu. Yatupasa tufikirie
juu ya toba yetu kuzitubia dhambi tulizozifanya kwa kuzishika sikukuu za
kipagani na kuamua kubazitwa kabisa ili kuziosha na kuziondolea mbali dhambi
tulizozitenda huko nyuma (Matendo 22:16). Wale waliobatizwa yawapasa kuendelea
kujitakasa mioyo yao kwa kumtii Mungu na sheria zake. Tukimkaribia Mungu naye
atatukaribia sisi (Yakobo 4:8).
Aya ya 7: Yesu akawaambia,
Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.
Sasa ni Kristo peke yake anayewaambia wanafunzi wake, kwa kuwa
wanaliwakilisha Kanisa. Anatuamuru sisi kuijaza mitungi ya maji. Twaweza
kudhania kwamba Kristo anatuambia sisi kuwajaza watu walio kwenye mataifa kwa
maji ambavyo tunaweza kuchukulia tendo sawa na neno la Mungu. Kwa hiyo mitungi
ya maji tuliyoijaza ili kuwaosha mataifa mikono na vikombe vilivyojazwa maji
ili kuashiria kuoshwa kwa mataifa kwa njia ya neno la Mungu (Waefeso 5:26).
Waebrania 10:22 na tukaribie wenye moyo wa kweli,
kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya,
tumeoshwa miili kwa maji safi.
Ni wajibu wetu kuihubiri injili kwa mataifa yote, ambayo ni ishara ya
kuvijaza vile vyombo hadi juu. Hakuna taifa au watu walioachwa nje ya wale wasionufaika
na sadaka au dhabihu ya Kristo isipokuwa ni Wanefili peke yao (soma jarida la Wanefili (Na. 154)).
Wote tunakazi ya kufanya, na
yatupasa kuifanya kwa uaminifu mkubwa. tll have a job to do, and we una Mungu
muaminifu, ambaye kila wakati yupo hapa. Tunaongozwa hatua kwa hatua. Miujiza
isingeweza kutokea kama watumishi wake wasingetii, au kufanya walichoambiwa
kukifanya. Wanaweza kuwa hawakuyaamini yatakayotokea, au waliendelea kuwa na
mashaka mioyoni mwao. Sisi ni muujiza unaoendelea, hivyo ni kusema, Tumejazwa na Roho wa Mungu.
Mara tu tukiacha kumwabudu Mungu wa Pekee wa Kweli, na tukaacha kumwamini mwanae,
ni wakati ambao muujiza wetu unaacha kutokea.
Aya ya 8: Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee
mkuu wa meza. Wakapeleka.
Kristo aliyageuza maji kuwa divai. Sasa tunajua kwamba Kristo ni divai na
sisi tulio watu wake, ni matawi (Yohana 15:1-11). Kuwa mawazo fulani kwenye aya
hizi yanahusiana na sherehe hii ya arusi. Kristo aliyageuza maji yaliyokuwa
kwenye vyungu na kuwa divai. Tunaona kutokana na aya za hapo juu kwamba Kristo
ndye mvinyo wa kweli. Kila tawi ndani yake linapasa lizae matunda. Kwenye
Yohana 15:3 tunasoma kwamba tumekuwa safi kwa neno. Tumeambiwa kuwa ndani ya
Kristo. Sisi tulio matawi “Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake,
lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.” (aya ya 4).
Kwa jinsi hiyohiyo, watumishi hawakuweza kuwa na mvinyo bila kuwa ndani ya
Kristo.
Na karidi arusi ilipokuwa inakaribia, ikiashiria taswira ya zama hizi zetu,
ni sehemu ndogo tu walikuwa wanaondoka kwa Mshereheshaji. Bwana Mungu ni “Bwana
wetu” (Yeremia 3:14). Watumishi
wanawakilisha wale wene ushuhuda na imani ya Yesu Kristo. Watumishi waliambiwa
kuwa sasa wanaweza kuchota kwenye vyungu vya maji. Hii inaonyesha mbele kwenye
uhai wa Kristo uliotolewa na damu yake ilimwagika kwa ondoleo la dhambi.
Warumi
6:22 Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na
dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na
mwisho wake ni uzima wa milele.
Tumepewa fursa ya kuchota mvinyo. Sisi kama watumishi tumepewa fursa ya
kuja kwenye ushirikiano mwema na Mungu na Mwana wake. Hatupaswi kuikataa fursa
hii, bali na tuitumie na tuende mbele za Mungu tukiwa kama watumishi wa Kristo (Wagalatia
1:10; Wakolosai 4:12; Warumi.1:1) ambaye yeye mwenyewe anamtumikia Mungu (Wafilipi.
2:5-8).
Aya ya 9: Naye mkuu
wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka,
lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza
alimwita bwana arusi,
Mungu ameiandaa arusi na amemwandaa bibi arusi. Anautumia mfano huu ili
kulinganisha na wokovu wa mwanadamu. Kikombe kinachotumika kuchotea maji
kinafananishwa na mwanadamu, anayeonekana kumuwakilisha Kristo aliye limbuko la
malimbuko yote na kinaweza pia kufananishwa na wale wanaounda mkusanyiko au
mwili wa wateule. Hawa ni wale waliochukuliwa kutoka hapa ulimwenguni, kutokana
na dhabihu ya Kristo, na wamemwagwa kama sadaka ya kinywaji kwa Mungu Aliye Juu
Sana.
Twaweza kujifunza somo kutokana nah ii. Roho wa Mungu hapaswi kuachwa
kwenye vyombo. Alilazimu kuletwa mbele za Mungu, afungiwe kama ilivyokuwa.
Tunapaswa kujitoa kwa Mungu, kama sadaka zilizohai. Tumekirimiwa vipawa kwa
kupitia Roho Mtakatifu ambazo hazifai zipotezwe tu kirahizi (Mathayo 25:14-30).
Mungu anaujua mwisho tangu mwanzo wake (Isaya 46:10; Ufunuo 1:8). Twaweza
kujionea hapa kuwa Mungu, Baba yetu hana upendeleo. Kila amchaye na kuishi
sawasawa na neno lake anakubalika machoni pake.
Watumishi walijua ulikotoka mvinyo. Kama watumishi hawa ni sisi tunaojua,
ndipo yatupasa wote tujue kuwa tu sehemu ya mwili wa Yesu Kristo, na kwamba
tumeokolewa kwa kupitia uingiliaji kati wa Yesu Kristo na karama ya Roho
Mtakatifu. Tumepewa kujua kwamba kuna miujiza iliyohusika na kwamba Roho wa
Bwana ndiye mwili ule. Huyo ni Roho wa Bwana, Roho wa kweli, aliyemtia mhuri
Kristo na ndiye anayetutia mhuri na sisi sote pia, na ndiye anayetuwezesha sisi
kuwa ni sehemu ya mwili huo. Tunafanyika kuwa sehemu ya Mungu, kama Kristo alivyofanyika
kuwa sehemu ya Mungu. Tunaishi ndani ya Kristo, na Kristo na Mungu Baba
wanaishi ndani ya kila mmoja wao. Sote tunauhusiano unaoingiliana. (Rejea
kwenye jarida la Maana ya Mkate na Divai (Na. 100)).
Aya ya 10: akamwambia,
Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo
huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.
Mungu, Baba yetu
anafanya tofauti kati yake yeye mwenyewe na jinsi wanavyowaza wanadamu na jinsi
wanavyotenda. Baba yetu wa mbinguni anafikiri, anatenda na anatilia maanani kwa
kiwango kikubwa sana kiasi kwamba hakuna hata mmoja wetu angaliyeweza kudhani
kabisa. Uelewa wa Mungu ni mkubwa sana na mawazo yake yapo juu sana (Zaburi
147:5). Baba yetu wa mbinguni hakosei na anajua kila jambo (Ayubu 37:16).
Kitendo cha kuwapa mvinyo bora zaidi baadae kwenye sherehe hii ya arusi
kunahusishwa kwenye Maandiko Matakatifu. Mungu alishasema hapo mwanzoni kuhusu
utukufu wa hekalu utakavyokuwa katika siku za mwisho.
Hagai 2:9 Utukufu wa mwisho wa
nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi;
na katika mahali hapa nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi.
Arusi iliyo kwenye injili ya Yohana inaenda sambamba na agano ambalo Mungu
aliliweka na Ibrahimu na sasa linaendelea na Kanisa la Mungu.wyatupasa sasa
kuitakasa mioyo yetu ya jiwe na kuwa na mioyo ambayo ameiandika sheria zake.
Sisi sasa ni washirika wa mwili wa Kristo. Kama utasoma kile anachokisema
Kristo kwenye Yohana 15:1-11 tunaona kwamba aya hizi zinahusiana na matukio ya
kwenye arusi ya Galilaya na kwenye Kanisa linaloshiriki agano na Mungu.
Yohana 15:1-11 Mimi ndimi mzabibu wa
kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Kila tawi ndani
yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno
nililowaambia. 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu.
Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu;
kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni
mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana;
maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 6 Mtu
asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na
kuyatupa motoni yakateketea. 7 Ninyi mkikaa ndani
yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi
mtatendewa. 8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile
mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. 9 Kama
vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo
langu. 10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo
langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo
lake. 11 Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani
yenu, na furaha yenu itimizwe.
Matendo au harakati za Yesu Kristo katika kuja na kuzaliwa kwake katika
mwili hazikulihalifu au kutangua agano aliloliweka Mungu na Waisraeli. Kristo
alilifanya upya agano hilo na kufanya au kuweka utaratibu mpya na wa hali ya
juu wa mwingiliano uliopo na wanadamu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Sisi kwa
kulishika agano la Mungu, tunajifanya wenyewe kuwa tayari ni mabibi arusi kwa
ajili ya arusi ya mwanakondoo (Ufunuo 19:7).
q