Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[058]
Mwaswali Yaulizwayo Mara
kwa Mara Kwenye Masomo ya Biblia ya Agano Jipya
(Toleo La 2.0 20000630-20011206-20091125)
Mwaswali
Yaulizwayo Mara kwa Mara Kwenye kwenye maandiko ya Agano Jipya yameorodheshwa
hapo chini, ndiyo haya.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati
Miliki © 2000, 2001, 2009 Wade
Cox)
(tr. 2015)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
YALIYOMO KWA MUHUTASARI
Masihi…Mwana wa
mtu-mtoto Pekee-Mwana wa Pekee, mwana aitwaye Yesu, Nabii wa Mungu-sadaka ya
Dhambi-Imani kwa Kristo-Ubatizo wa Kristo-Njia pekee kwa
Baba-Kuhani-Yoshua-Wengine walimuita Yesu-Barua ya Pilato-mwaka wa
Kusulibiwa-Msalaba-Ufufuko-wa Kimwili au wa Kiroho-Mwili wa Yesu-Israeli
walioolewa na Kristo-Dhabihu-Kundi dogo la wanafunzi-Yesu
Mwokozi-Mafundisho-Asiyekula nyama-Neno la Yesu au la Mungu-Mkuu-Malaika wa
Ufunuo-Yesu/Biblia.
Roho Mtakatifu…huyu
Roho Mtakatifu-Mungu humtoa Roho Mtakatifu-Roho/Roho wake-Ufalme wa
Mungu-Maji/miamba.
Mathayo…Mathayo
2:2;-2:13;-2:17-18;-6:5-15;-12:50;-17:21;-20:13;-28:19
Marko…Marko 5:21-43;-7:15;-10:18
Luka…Luka
12:36;-17:11;-19:12;-23:43
Yohana…Yohana/Mwanzo-Yohana
5:1-24;-5:18;-7:52;-Sura ya 10;-12:12-13;-19:31
Matendo…Hakuna
neno amen-Matendo 1:15;-15:24-29;-15:28:29
Warumi…Warumi
sura ya 1-Warumi 3:20;-10:4;-Sura ya 14;-16:16
1Wakorintho…1Wakorintho
5:5-6;-11:10-15
Wagalatia…Wagalatia
4:9-11;-4:10
Waefeso…Waefeso
3:15
Wafilipi…Wafilipi 2:10
Wakolosai…2:14;-2:16;-2:18;-4:3
2Wathesalonike…2Wathesalonike 2:3-4,6
1Timotheo…1Timotheo 4:1-3
Waebrania…Waebrania 7:3
Yakobo…Mwanzo wa Yakobo-Yakobo 1:17
1Yohana…1Yohana 5:7
Ufunuo…Mafunuo ya Mtakatifu Yohana-Ufunuo 1:4;-5:6;-2:17;-2:20;-2:28;-3:7;-3:12;-4:2-6;-5:12-17;-6:2;-6:4;-6:5;-6:8;-7:14;-8:10;-sura
ya 9;-sura za 10;-13:18;-sura za 14;-17:5;-20:10;-20:15;-21:18;-21:1;-hali
Ngumu ya Yakobo ya dunia-Kile knachotokea kwenye ufufuo wa Watoto wa kwanza
wawajuao wazazi walio chini ya mamlaka ya mlo wa Arusi ya
Yesu-Watakaohudhuria-Mji wa Mungu -
Kalenda…Wakati inapotimi saa la 3 la
Ikwinoksi-Mwandamo wa Mwezi Mpya-Mwezi Mchanga-Kalenda ya uwongo-Mwaka wa
Zaka-Ushahidi wa kipindi cha kiza cha mwezi-Mwandamo wa Mwezi Mpya wakati wa
Kristo-kalenda ya Karaite-Tarehe lengwa-Pasaka: Usikuwa wa Kuuangaliwa sana-Hesabu
ya Omeri-Mkate & Mvinyo-Kuoshana Miguu-Meza ya Bwana
Kanisa…Siku Takatifu za Wakristo-Ufalme wa
Mungu-Mamlaka\ya Kubadili mafundisho-Masharti ya kuwa Mkristo-fursa ya Pili-Mteule-Mahali
alipo Mungu-Ni S-Ni Sabato au Jumapili:Kuna ushahidi wowote katika kuishika na
kuabudu siku ya Jumapili-kuna msaada wowote kwa upande asi wa Sabato-Wengi
huabudu siku ya Jumapili-Ibadaa ya Kipagani ya Wapagani ya Jua-Dhana isemayo
Kila siku ni Sabato-Kwa nini ni Jumapili sasa-Kanisa la Kwanza lilifanyaje-Mabaraza
Manne ya Mitaguso-Mababa wa Kanisa na mpango wa Mungu kwetu -
Ibada za Kipagani: Easter-Utrinitari
Mpingakristo…Mpingakristo & Torati ya Musa-Mafundisho-Yesu
akishukiwa kuwa mpingakristo.
************************************
MASWALI
YAULIZWAYO MARA KWA MARA KWENYE AGANO JIPYA FAQ NEW TESTAMENT
Masihi
Ni nani Mwana wa adamu? Kwa nini aliitwa Mwana wa
Adamu?
Jibu: Kulikuwa na wana wa Mungu wengi ambao Kristo alikuwa mmoja wao tu (Ayubu
1:6; 2:1; 38:4-7). Ni wale tu waliozaliwa wanadamu. Hii ndiyo maana lengwa ya
neno monogenes theos au aliyezaliwa na mamlaka ya kiuungu ya Yohana 1:18 na
Mithali 30:4-5.
Hii ndiyo dhana
iliyoko nyuma ya andiko la Waebrania 1:8-9 iliyochukuliwa kutoka kwenye Zaburi
45:6-7. Kwenye Waebrania inazidi kwenda mbele kwa kuonyesha kwamba elohimu
hakuwa tena kama sawa na malaika walioitwa wana wa Mungu. Bali alikuwa ni
kuhani mkuu mpya kama mwana wa adamu.
Soma majarida ya Zaburi 8 (Na. 14); Uwepo wa Yesu Kristo wa Kabla ya Kuzaliwa Kwake
(Na. 243); Jinsi Mungu Alivyofanyika kuwa Familia (Na. 187); na Kusudi la Uumbaji na Dhabihu ya Kristo (Na. 160).
Kwa nini Biblia inasema " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,
hata akamtoa Mwanawe pekee, (monogene)"? Angewezaje basi kuwa wa
pekee kama kusingekuwa na wana wengi wengine?
Jibu: Kuna wana wengi wa Mungu kama Maandiko Matakatifu yanavyosema. Hata hivyo,
yeye alikuwa ni wa kwanza kuzaliwa. Wengine walikuwa ni wale walioumbwa wakiwa
kama wana wa namna ya Kimalaika. Alikuwa ni Prototokos au Mwanzo wa Uumbaji wa
Mungu na ni Stadi wa Uumbaji wa Mungu. Yeye pia ni Limbuko au Prototokos la
waliokufa. Hata hivyo, yeye ni mzaliwa wa pekee wa Mungu au monogenes theos
aliyetajwa kwenye Yohana 1:18.
Mambo haya
yameelezwa kwa kina kwenye majarida ya Stadi wa Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na
Omega (Na. 229); na Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa Kwake Rasmi Duniani (Na. 243).
Kwenye Zaburi 2:7, Matendo 13:33, na Waebrania 1:5
tunasoma: “Wewe ndiwe Mwanangu,
mimi leo nimekuzaa. na Yohana 1:14 “utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba.” Ni nini maana ya neno “mzaliwa wa pekee”? Wakati Kristo alipozaliwa na
kwa nini hasa ameitwa Mwana mzaliwa “PEKEE” wakati malaika wakiwa pia ni wana
wa Mungu? Je, usemi huu wa kuwa amefanyika kutokana na roho na kuwa mwanadamu
mwenye roho?
Jibu: Ilitokeza kwa makusudi kabisa kwa Watrinitariani. Kuna majina mawili: moja
ni la “Prototokos” lenye maana ya “mzaliwa wa kwanza” na linguine ni
“monogenes” ambalo maana yake ni “mzaliwa wa pekee.” Jina linalofanana na
Kristo kuwa ni kama mzaliwa wa kwanza na aliyezaliwa kwanza aliyefufuka kutoka
kwa wafu ni “Prototokos.”
Anatajwa kuwa ni
kama “mzaliwa wa kwanza wa Mungu” kwenye Yohana 1:18 kutokana na neno
“Monogenes Theos.” Andiko hili lilibadilishwa kwenye Receptus ili lisomeke
“mtoto pekee kuzaliwa” au “muunganiko wa monogenes” na kisha ikatafsiriwa kama
“mwana mzaliwa wa pekee.” Hii ilifanyika ili kugeuza au kupotosha tofauti kati
ya ukweli kwamba kulikuwa na wana wengine wengi wa Mungu wakiwa malaika, ambao
kwamba Kristo ndiye “prototokos”, bali ni ndiye aliyezaliwa na kwa hiyo,
alikuwa ni mzaliwa wa pekee “mungu” au “theos.”
Majina haya
yamechambuliwa kwa kina kwenye majarida ya Mteule Kama Elohimu (Na.1) na Malaika wa YHVH (Na. 24); Ustadi wa Uumbaji wa Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na
Omega (Na. 229) na Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa Kwake
Duniani (Na. 243).
Kuna mahali popote kwenye Biblia ambapo Yesu
anajiita Mwenyewe kuwa yeye ni Mungu?
Jibu: Anaitwa Mungu kwenye maandiko mengi ya Biblia. Hajitaji mwenyewe kuwa ni
Mungu, bali maandiko yanafanya hivyo na inamtaja kuwa ni mungu mdogo. Kwa
mfano, andiko lililo kwenye Zaburi 45:6-7 linaonyesha wazi sana kuwa ni Kristo
ndiye aliyetiwa mafuta kuwa Mungu na Mungu wake kwa mafuta ya furaha awe juu ya
washirika wake kwenye Waebrania 1:8-9. Uhusiano uliopo kati ya Malaika Mkuu wa
Agano la Kale kama elohim ni jambo la muhimu sana kwenye Teolojia ya Biblia.
Muundo wa
uhusiano huu umeelezwa kwa kina kwenye majarida yafuatayo: Mteule Kama Elohim (Na. 1); Malaika wa YHVH (Na. 24); na Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa
Kweke Duniani (Na. 243). Tangazo la ukiri wa imani la Ulfilas, askofu wa Wagoths, limeainishwa
kwenye jarida hili, pia linaainisha uhusiano huo. Jarida la Teolojia ya Mwanzoni ya Uungu (Na. 127) litakuonyesha kwamba Kanisa la Mwanzo
lilifundisha na kueleweka kuhusu jambo hili.
Je, Yesu alikuwa nabii?
Jibu: Musa alisema kwamba ndivyo alivyokuwa. Alisema kuwa Mungu atawainulia
nabii kama alivyo yeye, Musa na kwamba iliwapasa wamsikilize yeye. Kwa hiyo,
yeye alikuwa Kuhani, Mfalme na Nabii. Soma jarida la Yesu Kristo, Mfalme, Kuhani na Nabii (Na. 280). Maneno haya, kama yalivyoandikwa,
yanaonyesha kuwa ni unabii, na yalotimilika kama alivyosema. Alinena kwa mujibu
sawa na Torati na Ushuhuda (Isaya 8:20). Hiki ndicho kipimo cha nabii.
Mwanzo 4:7 inasomeka hivi: “Kama ukitenda vyema, hutapata kibali?
Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni. Na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.” Tafsiri ya The Companion Bible inaonyesha dhambi –
kama sadaka ya dhambi. Je, kinachoatajwa hapa kwa njia ya mfano na isiyo moja
kwa moja kuwa Masihi kuwa ndiye sadaka hii ya dhambi iliyotajwa kwenye Zaburi
22 na mlango ulioandikwa kwenye Ufunuo 3:20 na damu ya kwenye miimo ya milango
ya kwenye Kutoka 12:7?
Jibu: Ndiyo, ni andiko muhimu sana. Waaka kwa
Waebrania unatilia mkazo kwa kusema “kweli” na pili “iwapo kama”. Bullinger
anasema kwenye tafsiri ya the Companion
Bible akitilia maanani andiko linalofana kuwe na uwezekano kamili na
mtakatifu. Kwa Kiebrania ni “chat'a” na maana yake ni sadaka ya dhambi kama
ilivyoongezwa kwenye Kutoka 30:10; Walawi 4:3; 6:25; 8:2; Zaburi 40:6 (sawa na
2Wakorintho 5:21; Waefeso 5:2).
Neno “lieth” ni la kiume na sadaka ya dhambi ni la kike. Kwa Kiebrania
linasomeka: “kwenye lango la kuingilia [mwanaume] ipo, au sadaka ya dhambi.”
Pia tazama kwenye Mwanzo 3:16 isemapo “tawala.” Masihi, kama tujuavyo ni sadaka
ya dhambi. Tazama kwenye majarida ya: Fundisho la Dhambi ya Asili Sehemu ya I Bustani ya Edeni (Na. 246); na Fundisho la Dhambi ya Asili Sehemu ya 2 Kizazi cha
Adamu (Na. 248).
Wakristo wote wanaonekana kuamini kuwa
wanahitajika kuwa na imani, lakini ni kuamini nini? Je, inamaana gani dhana hii
ya kumwamini Kristo?
Jibu: Imani ni tumaini liendanalo na kumuamini Mungu na kuamini kuwa anaweza
kuuleta wokovu wa kila mmoja, kwa mpango aliokusudia, ambao utafanya kazi kwa
manufaa ya wata kazi kwa manufaa ya watu wote. Mungu ataufanyia kazi wokovu wa
viumbe wake wote ili asiwepo mwene mwili yeyote atakayepotea.
Imani hii
imeelezwa kwenye matendo ya Kanisa kwa kupitia historia yote tangu Adamu hadi
sasa. Waebrania sura ya 11 inakupa orodha ya watu muhimu wanaojulikana kama
mashujaa wa imani, na matarajio yao ya kila wakati na matendo yao. Wokovu
haupatikani kwa kupitia imani iliyotajwa katika Kristo. Wokovu, kama watakatifu
wa Kanisa, unapatikana kwa kuzishika Amri za Mungu na Ushuhuda au Imani katika
Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12). Kristo mwenyewe alikuwa na imani kwa Mungu
aliemuokoa.
Ni imani kwa
Mungu ndiyo inayookoa kwa kupitia matendo ya Yesu Kristo aliyemtuma (Yohana
17:3). Wengi wamemuita yeye “Bwana, Bwana” na atawaambia “Tokeani kwangu, maana
siwajui ninyi.” Kama unampenda Kristo, basi zishike amri.
Wakristo wamebatizwa kwa jina la Baba, Mwana na
Roho Mtakatifu, bali unadhani ni maneno gani aliyatumia Yohana Mbatizaji
alipokuwa anambatiza Kristo?
Jibu: Ubatizo wa Yohana ulikuwa kwa ajili ya toba ya dhambi na kwa ajili ya
maelekezo ya kuitayarisha njia kwa Yahova na kutengeneza mapito yanooke,
kutokana Isaya 40:3 ambayo imenukuliwa kwenye Mathayo 3:3. Ubatizo wake
haukufanwa kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Kristo alibatizwa ili ampokee Roho
Mtakatifu, ambaye alimpokea, kama walivyompokea pia manabii wa zamani nyuma
yake. Maneno yake yanaonekana kuwa: “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba;
bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata
kuvichukua viatu vyake;.”
Amri na maagizo
yake kwa Kristo yalikuwa: “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya
ulimwengu!” (Yohana 1:29)) na alisema ninahitaji
kubatizwa na wewe nawe waja kwangu.
Maneno yaloyo
sehemu ya kwanza ndiyo yanayooekana kwanza kabisa kuwa kama yanatamkwa na yeye.
Ambayo ni kwamba: “Kweli mimi
nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba;.” Luka anaandika kuwa Kristo alikuwa anaomba pia huko (Luka 3:21). Mbingu
zilifunguka na Roho Mtakatifu alishuka juu yake kama hua, na Mungu akasema, “Huyu ni
Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” Marko anamengi au machache ya kuandika
kuhusiana na jambo hilohilo kama Mathayo. Hatujapewa maneno yenyewe halisi.
Je, ni kweli kuwa Yesu
Kristo ndiye njia ya pekee ya kwenda kwa Baba?
Jibu: Kwenye Yohana 14:1-6 Kristo alisema kuwa
yeye alikuwa ndiye njia pekee kwa Baba. Kuna vipingamizi vingi kwene tamko lake
hili, lakini vipingamizi vyote vina msingi wa teolojia potofu nay a uwongo na
kutoyaelewa maandiko ya Biblia.
Hoja ya kwanza: Mungu alinena na Musa na Mababa wa imani wa kale na manabii
nab ado hawakumhitaji Kristo. Jibu ni kwamba hakuna mtu aliyewahi kumuona
Mungu. Wamezaliwa tu katika Mungu, wakawa kifuani mwa Baba, aliyenena (Yohana
1:18). Kanisa la Kwanza lilifundisha kuwa Kristo ndiye alikuwa Malaika wa Agano
la Kale aliyempa Torati nabii Musa na aliyenena kwa manabii. Justin Martyr
anasema wazi kabisa kuhusu jambo hili kwenye kitabu chake cha “First Apology au
Utetezi wa Imani wa Kwanza.” Pia soma jarida la Teolojia ya Mwanzo ya Uungu (Na. 127).
Mchakato wa ufufuo wa wafu unahakikisha kwamba hakuna atakayeweza uzima
usioharibika au uzima wa milele isipokuwa ni kwa kusimama mbele za Kristo
kwenye hukumu kama kiumbe aliyefufuka toka kwa wafu. Tazama majarida ya Roho (Na. 92); na Ufufuo wa Wafu (Na. 143). Na ndiyo maana mafundisho ya Roho Isiyokufa na
Mbinguni na Motoni ni yasiyo ya kimungu na ni mafundisho yenye kukufuru.
Lilikuwa ni jaribio la kweli kwa Mkristo kwenye karne ya kwanza nay a pili.
Yeyote aliyesema kuwa ni Mkristo na kwamba akifariki anakwenda mbinguni,
hawakuwa wanamuamini. Walimhesabia kuwa hakuwa Mkristo. Kwa kupitia ufufuo wa
miili wa wafu, kila goti sasa litapigwa kwa Kristo na hakuna mtu atakayekuja
kwa Baba isipokuwa ni kwa kupitia yeye.
Mbali tu na Yesu Kristo kuwa Masihi au mwokozi
wetu, yatupasa pia kumchukulia yeye kuwa kuhani, au huenda ni nabii au hata
kuwa mfalme? Au basi yawezekasa kumuita kuwa alikuwa ni Mungu yeye mwenyewe?
Jibu: Ndiyo, yeye ni yote ya haya mambo yote. Yeye ni kuhani na ni kuhani mkuu
wa mfano wa Melkizeeki. Yeye ni nabii, kama alivyosema Musa. Yeye ni Mfalme wa
Wafalme na Bwana wa Mabwana kwa kuruzukiwa na Baba.
Mungu wa Pekee wa
Kweli pia alimchagua yeye kuwa ni mungu mdogo kwa kumtia mafuta ya furaha juu
zaidi ya ndugu zake (Zaburi 45:6-7 na Waebrania 1:8-9). Hii ilionyeshwa pia
kwenye Zekaria 12:8 wakati Malaika wa YHVH kichwani mwetu alikuwa ni elohim
kama sisi wenyewe tutakavyokuwa elohim na Maandiko hayawezi kutanguka (Yohana
10:34-35). Tazama majarida ya: Mteule Kama Elohim (Na. 1); Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa Kwake Duniani (Na. 243); Malaika wa YHVH (Na. 24).
Ni kwa nini kwamba neno la Kiyunani la Yoshua
limetafsiriwa kwenye lugha ya Kiingereza kuwa Joshua isipokuwa wakati
anapotajwa Yesu Kristo linatafsriwa kuwa Jesus ambaye ni Yesu? Kwani
isingewezekana jina hilohilo lilivyo kwenye Kiyunani likatafsiriwa kama jina
hilohilo moja kwenye lugha ya Kiingereza?
Jibu: Ndiyo, lilipaswa kutafsiriwa kwa namna
moja hiyohiyo. Tofauti hii ilifanywa na Wayunani wenye mchanganyiko na Warumi
alionuia kulitenganisha Agano la Kale na Agano Jipya ili wafanikishe azma yao
ya kuziondoa Sheria au Torati ya Mungu. Habari hii imechambuliwa kwa kina
kwenye jarida la Yoshua, Masihi, Mwana wa Mungu (Na. 134) (soma toleo la 2). Mabailiko yalifanywa
pia kwenye majina ya familia yote ya Kristo kwenye Biblia pia. Soma jarida la Bikira Mariamu na Fa,ilia ya Yesu Kristo (Na. 232).
Wako wapi watu wengine wenye majina ya Yesu mbali
na huyu Yesu wa Nazareti?
Jibu: Niyo, kwa kweli walikuwepo. Jina Iesous kwa kweli linatokana na uandishi
wa Kiyunani wa jina Yoshua Yahoshua. Kulikuwa na namna mbalimbali ya kuliandika
jina hili. Lilikuwa ni jina kuu na lenye heshima katika Israeli na kwa hiyo
Yoshua lilikuwa jina linalijulikana sana katika Yuda pia
Kwa hiyo, Yesu
halikuwa ni jina la Kristo. Bali hili ni jina lenye hisia ya Kiingereza la
tafsiri ya Kiyunani. Josephus, na sasa Schurer, anayaandika majina mengine.
Mfano ni kama Yesu, mwana wa Damnai; Yesu, mwana wa Gamaliel; Yesu, mwana wa
Phiabi Kuhani Mkuu aliyemtiwa mafuta au kusimikwa na Herode; Yesu, mwana wa
Sapphias, adui wa Tiberias kwenye uasi wa kwanza; Yesu, mwana wa See, Kuhani
Mkuu aliyetiwa mafuta na kusimikwa na Archelaus; na Yesu, mpinzani wa Josephus
(sawa na kisemavyo kitabu cha The History of the Jewish people in the age of
Jesus Christ [Historia ya Wayahudi Wakati wa Yesu Kristo] (Vols. 1. 419, 431,
469, 489, 497; II, 180-181, 229, 232, 234).
Majina yaliyo
kwenye Biblia za Kiingereza ni tafisiri ya Kiyunani na mara nyingi hayafanani
na yalivyo kwenye Kiyunani, mbali na hata kuyafananisha na Kiebrania. Kwa
mfano, jina James lilikuwa ni Yakob, Jude ni Yudah au Judah, Joses ni Yosef au
Josef. Tazama pia majarida ya Bikira Mariamu na Familia ya Yesu Kristo (Na. 232) na Yoshua, Masihi, Mwana wa Mungu (Na. 134).
Inasemekana kuwa kuna waraka
kutoka kwa Pilato aliomwandikia Mfalme Claudio unaoashiria kama alimtaja Yesu.
Je, waraka huu bado upo? Na kama ni hivyo unasemaje kuhusu Yesu?
Jibu:
Barua ya Pilato
aliyomwandikia Claudio imejumuishwa au inapatikana kwenye Injili ya kiapokrifa
ya Nicodemus iliyoko mwishoni mwa toleo la kwanza. Toleo la Kiyunani la barua
hii linaonekana kuandikwa pia kwenye injili za kiapokrifa za Petro na Paulo.
Utajionea matoleo kadhaa ya barua zilizoandikwa na kupelekewa wafalme Augustus,
Claudius na hatimaye Tiberius kwenye kitabu cha the ANF vol viii, pp, 353, 454,
459 et seq.
Je, Kristo alisulibiwa kwenye mwaka ahirisho? Kama
sivyo, nawezaje kuthibitisha hilo?
Jibu: Hapana, hakusulibiwa kwenye mwaka ahirisho na ni rahisi kuthibitisha.
Kwanza kabisa, katika mwaka huu wa 30 BK siku ya 14 iliangukia siku ya Jumatano
na ilikuwa ni namna hiyo isingejalisha ni utaratibu au mfumo gani ulitumika.
Hata hivyo, sababu kubwa ni kwamba utaratibu wa kuahirisha haukuwa ukitumika
wakati huo. Kimsingi, utaratibu wa Kuahirisha ulikuwa ni “barza maalumu”
ulioingizwa baadae baada ya kipindi cha kuangamizwa kwa Hekalu mwaka 70 BK.
Baraza la wazee lililojulikana kama Mishnah lililoundwa mwanzoni mwa karne ya
tatu takriban zaidi ya mwaka 200 BK inaonyesha kuwa utaratibu huu wa uahirisho
ulikuwa bado haujaanza hata kipindi hicho.
Utaratibu wa
kuhesabu ndiyo unapelekea hali hii ya uahirisho na hata hivyo ilikuwa haujafanyika
wala kuanza hadi ulipoletwa na kuingizwa na Marabi wawili wa Kibabeloni mwaka
344 na kisha ukabatilika na kuanzishwa rasmi chini ya Rabi Hilleli II mwaka
358. Hauikuwa umekamilika hadi kwenye karne ya kumi na moja. Kwa hiyo, Kristo
alisulibiwa yapata zaidi ya miaka mia tatu kabla ya utaratibu huu wa uahirisho
kuanza.
Kalenda ya sasa
ya Kiyahudi haikuwa ikitumika kabisa kwenye shughuli za Hekaluni. Utajisomea na
kujifunza zaidi kwenye majarida ya Kalenda ya Mungu (Na. 156) na jarida la Mwezi Mwandamo na Mwaka Mpya (Na. 213) na pia Kalenda na Mwezi Mwandamo: Ni Uahirisho au
Sikukuu? (Na. 195).
Ni kwanini basi kwamba kwenye maandiko ya Kiyunani
neno msalaba halitumiki kabisa wakati yanapoelezea kuhusu pale aliposulibiwa
Kristo? Neno la Kiyunani lililotumika ni “stauros,”
ambalo halimaanishi msalaba, bali ni mti tu wa kawaida. Je, kwani alisulibiwa
msalabani au kwenye mti?
Jibu: Neno hili msalaba halikutumika kabisa kwenye zama zote za Ukristo wa
kwanza. Alama iliyokuwa karibu sana ilikuwa ni ya “kiutata.” Ilieleweka kwamba
“stauros” ilikuwa ni mti. Mkakati wa kuufanya msalaba kuwa nembo ulifuatia
baadae, na hatimaye wakajichongea sanamu juu yake baadae. Hakuna hata mojawapo
ya mambo haya yaliyokuwa yanatumika na kuwekwa kwenye madhabahu za Kikristo za
pande za Magharibi hadi millennia hii. Mwendelezo wa uhalalishaji wa nembo ya
msalaba, habari zake zimechambuliwa kwa kina kwenye jarida la Msalabas: Chanzo Chake na Maana Yake (Na. 39). Makanisa mengi ya Mungu, hadi sasa, bado
hayakubaliani kuweka alama yoyoyote ya msalaba kwenye ibada zao na hawauamini.
Je, unaweza kuelezea basi ni kwa jinsi gani huu
msalaba ulionekana na ni kwa jinsi ipi Yesu alipigiliwa misumari juu yake?
Jibu: Neno lililotumiwa kuelezea “stauros” ambalo ni neno la Kiyunani ambalo
linamaanisha “fimbo” na hasahasa ni “mti uliosimama kwenda juu” (sawa na
inavyosema Thayers New Greek English Lexicon p. 586) na chanzo chake ni mti au
mlingoti uliosimama wima, hususan uliosimikwa hivyo kwa kazi maalumu. Haya
ndiyo matumizi yake kwa maandiko ya Kiyunani.
Wayunani na
Warumi walikuwa na neno lao kuhusu kifo iki kwa kuongeza maana yake ya
kusulibiwa mtini kutokana na lugha ya Kifoeniki (ibid). Neno “msalaba”
linatokana na neno la Kirumi “crux.” Mwendelezo wa mkakati wa kuufanya msalaba
kuwa nembo unaelezwa kwa kina kwenye jarida la Msalaba: Chanzo Chake na Maana Yake (Na.
39).
Kristo
alisulibiwa kwenye hii “stauros” kwa kupigiliwa misumari mikononi na miguuni.
Lengo lao lilikuwa ni kuufanya mwili uanguke chini kwa ajili ya uzito wake,
ukishindwa kumudu kujishikilia wenyewe. Dhana ya msalaba ililetwa baadae
ikifanywa kuwa ziada ya kuendeleza habari ya kifo. Kasi ya kifo cha Kristo na
siku au tarehe vinaashiria kuwa hii “stauros” ilikuwa ndiyo mti wa kijadi wa
Wafoenike na Wayunani, zaidi kuliko msalaba ulioingizwa baadae na kuendelezwa
dhana yake. Historia yake, ya matumizi yake katika kipindi cha kabla ya zama za
\Ukristo na siri au fmbo lake imeelezwa kwa kina kwenye jarida la Na. 39.
Biblia yangu ya NKJV inaema hivi: “Naye alipofufuka alfajiri siku ya
kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu...”(Mark 16:9). “Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya
kwanza ya juma, Mariamu...” (Mat 28:1). Je, Yesu aliamka au
kufufuka asubuhi ya siku ya Jumamosi au Jumapili asubuhi? Na kwa kuwa siku ya
Mungu huanzia baada ya kuchwa jua, basi ikiwa kama alifufuka wakato wowote
baada ya machweo ya siku ya Jumamosi basi ingekuwa imechukuliwa kuwa ni siku ya
kwanza ya juma. Je, haikuwa hivyo?
Jibu: alitumia kushinda siku tatu mchana na usiku kaburini alifanya hivyo
kuanzia siku inayoitwa leo Jumatano jioni wakati wa jua kuzama na alifufuka
siku ya Jumamosi jioni majira ya jua kuzama.
Ilimpasa
kuyatimiliza matukio matatu kwenye Pasaka yake. Ilimpasa afe au auawe kama
Mwanakondoo kwa wakati wake muafaka wa kuuawa kondoo kwa kuchinjwa. Vinginevyo,
basi asingekuweza kuwa kindoo wa Pasaka; bali angekuwa ni mtu mwingine tu
aliyeuawa. Ilimpasa pia kuitimiliza Ishara ya nabii Yona, kwa kuwa hii ilikuwa
ndiyo ishara pekee iliyopewa huduma yake. Hiyo ilikuwa muhimu kwa kuwahukumu
Yuda kwa miaka mingine arobaini iliyofuatia, mwaka 70 BK.
Kitu cha pili
alichopasa kukifanya kilikuwa ni kuhitimisha Sadaka ya Mganda wa Kutikisa.
Alikuwa ni limbuko na hivyo alipaswa kukubaliwa na Mungu akiwa anafanya huduma
yake kwa ajili hiyo. Kwa hiyo ilimlazimu kupaa juu kwa Mungu siku ya Kwanza ya
Juma Asubuhi saa 3:00 asubuhi ili kuanzisha mchakato wa Kuhesabu Kipindi cha
Mpito kuelekea Pentekoste ili mavuno yetu yaanze. Alikuwa ni Mavuno ya Shayiri
na ilimpasa kukubaliwa ili kumuwezesha Roho Mtakatifu atolewe atakaporudi.
Fundisho la
Easter la miungu migeni nay a uwongo lilianzishwa kwa makusudi mazima ya
kutatiza au kuposha muujiza huu na uweza wa Mungu. Mungu wa Utatu aliingizwa au
kubuniwa pia kwa kusudi hilihili. Na ndiyo maana imani ya Kiutatu haina
maadhimisho ya Mganda wa Kutikiswa na unapinga upaaji wa siku ya Jumapili,
wakauweka siku arobaini baadae kwa kuumujuisha kimakosa na ule upaaji wa
mwisho. Ndiyo maana kwamba Shetani amefanikiwa kuwaleta ua kuwaweka Makristo
wengi bandia—ili wafundishe watu kudharau utimilifu wa Sheria au Torati ya
Mungu kwenye imani ya kweli ya maadhimisho ya sikukuu.
Na hii ndiyo
sababu pia inayopelekea imani zilizo kwenye muungano wa Baali-Easter kuw na
migogoro mikubwa na kupingana sana kwa kuitupilia mbali imani ya kweli na
kalenda ya Mungu inayoendana kwa mujibu wa Amri za Mungu. Na hii ndiyo sababu
pia ni muhimu sana.
Je, Kristo alikuwanao (wa kiroho au wa kimwili)
alipofufuka?
Jibu: Maandiko ya Agano Jipya (hususan Yohana 20) yanaonyesha kuwa Kristo
alifufuka kimwili, jioni iliyopita na alipaa juu kwa Baba wakati wa Mganda wa
Kutikiswa, ambayo ilikuwa Jumapili asubuhi. Akarudi siku hiyohiyo na akamwambia
Thomaso amsike. Anaonekana kuwa alikuwa amekwisha mudu kujibadilisha kutoka mwili
wake wa kibinadamu na kuwa na wa kiroho. Tazama majarida ya Mganda wa Kutikiswa (Na. 106b) na Majira ya Kusulibiwa na ya Kufufuka (Na. 159).
Nafasi yake kwenye Korani
inaelezwa pia kwenye jarida la Kristo na Korani (Na. 163) kwenye tovuti ya www.ccg.org na www.logon.org ambako inapatikana pia kwa Kiarabu,
Kirusi na lugha nyingi nyinginezo.
Kupewa huku kwa mwili wa Yesu hakuonekani kabisa,
basi je, mwili wake wa kibinadamu utapaa mbinguni pamoja na roho yake? Nadhani
kwamba ni roho yake tu ndiyo ilifufuka, na mwili ni kama gamba tu la kimwili
lililovulika na kuachwa nyuma yake. Kama ni hivyo, kuna fursa yoyote ya kudhani
kwamba mifupa au skeleton ya Yesu yawezekana upo mahali fulani popote, huenda
ilifichwa na mmoja wa wanafunzi wake? Najua kuwa aliweza kuonekana siku kadhaa
baadae, ila hii haikuwa ni kivuli tu, au alikuwa
na mwili wa kibinadamu pia?
Jibu: Yesu alifufuka toka kwa wafu na mwili wake wa kibinadamu ulifufuka na
kubadilika kama Mganda wa Kutikiswa wa juma majira ya saa tatu asubuhi, ambayo
ni saa 9 asubuhi, na ambao ndio ulikuwa muda au kipindi ambacho ulikuwa
unatolewa kila mara.
Kubadilika kwa
mwili kunaaminika kulifanyika baada ya kufufuka toka kifoni. Nabii Ezekieli
anaonyesha kuwa ilikuwa ni kimwili. Fundisho la roho kutokufa si la kibiblia
kabisa. Jinsi ya kumgundua Mkristo wa uwongo kwenye karne ya 2 ilikuwa ni
kwamba, kama atasema kwamba anapokufa atakwenda mbinguni, basi alihesabiwa kuwa
sio Mkristo. Wanostiki aliingiza mafundisho haya ya watu kwenda mbinguni na
motoni kwenye Ukristo tangu wakati huo.
Jambo hili
limechambuliwa kwa kina kwenye majaria ya Roho (Na. 92) na Ufufuo wa Wafu (Na. 143). Watu wengi leo wanaodai kuwa Wakristo na
wakiamini au kuhubiri mafundisho haya ya kwenda mbinguni na motoni hawajui
wanachokiongea. Nyingi ya hizo zinatokana tu na mpagao wa kimsisimko wa
kipagani, na mapokeo yao wapagani.
Dhehebu nililokuwa mshirika
wao zamani lilikuwa likifundisha kuwa Israeli wa kale waliolewa na Kristo. Je,
kuna Andiko Takatifu lolote linalounga mkono dhana hii?
Jibu: Yeye Aliye Juu Sana na Mwenyezi
aliwakabidhi Israeli kwa Yahova awe urithi wake (Kumbukumbu la Torati 32:8)
wakati alipoyagawa na kuyaanzisha mataifa sawasawa na wana wa Mungu. Jambo hili
la andiko la Agano la Kale limepotoshwana baraza la Sopherim, baada ya kuanguka
kwa Hekalu ili lisomeke “sawasawa na idadi ya wana wa Israeli.” Kwa hiyo,
Yahova wa Majeshi Aliye Juu Sana aliwakabidhi Israeli kwa Yahova kama urithi
wake. Tunamuona Yahova akihusishwa, akiwa kama msaidizi wa Yahova aliyefanyika
kuwa elohimu wa Israeli.
Zaburi 45:6-7 inasema: “Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekupaka mafuta,
Mafuta ya furaha kuliko wenzako.” Kwa hiyo, Yahova au elohim wa Israeli ana Mungu. Tunajua kwamba huyu
elohim wa Israeli ni Kristo, kwa mujibu wa Waebrania 1:8-9. Tunajua pia
kutokana na andiko la Waebrania, kwamba malaika wengine ni washirika wazuri wa
Kristo. Wao ni elohim pia kutokana na isemavyo Zaburi 8, ambayo kwenye
tafsiriri ya Kiingereza, wanaonekana pia kuitwa “Malaika” ikifiatiwa na tafsiri
ya Septuagint. Kwenye Kiebrania pia ni
“aggelos” na kwenye Kiyunani na inafuatia kwenye Kiingereza ikiandikwa “angels”
kuliko kuitwa “miungu” (sawa na jarida la Zaburi 8 (Na. 14)).
Kiumbe huyu ndiye kwenye Agano la Kale aliyempa Torati Musa, na kumtokea
kichakani, na ndiye aliyeshindana mieleka na mababa zetu wa imani, alikuwa ni
Kristo kama elohim wa Israeli. Mungu Mmoja wa Kweli, Eloah aliyewatoa Israeli
kwake kama wachumba wake na taifa zima lilikusudiwa kuwa ni wafalme na makuhani
wa Mungu kupitia Kanisa. Wote kwenye Agano lote la Kale uhusiano na Yahova
ulikuwa ni wa mume na mke. Ibada za sanamu zilichukuliwa kuwa ni uzinzi. Ndiyo
maana Israeli walikwenda utumwani kama waliotalikiwa, na walipojirudi kutoka
kwenye ibada zao za sanamu walifanywa upya. Taifa la Israeli liliendelea na
likaenda utumwani. Yuda walitengwa na pia wakaandama ukahaba kwa kuzini na
miungu wa uwongo (Yeremia 3:8-18).
Kwenye andiko la Yeremia Mungu anasema amewaoa Israeli na anasema kwamba
atatuchukulia au kutupa, mji mmoja na familia mbili, na kutupeleka Sayuni.
Atatawala kutoka Yerusalemu na Sanduku la Agano halitaletwa mioyoni tena.
Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itatembea mkono kwa mkono na Nyuma ya Israeli
kutoka upande wa Kaskazini hadi kwenye nchi waliyopewa baba zetu kuirithi.
Kwenye Yeremia 3:14 Bwana anasema kuwa anafanya hivyo kwa kuwa amefanyika kuwa
mume wetu.
Andiko lenyewe kwa kweli linasema hivi: “Rudini, enyi
watoto wenye kuasi, asema Bwana; maana mimi ni mume wenu;...”. Huyu ndiye Yahova, aliyetolewa kwa Israeli
kama urithi wake, na tunayemjua kuwa kama Malaika Mkuu wa Agano la Kale
aliyempa Torati Musa, na alikuwa ni mwamba wa roho jangwani ambao kwao, Israeli
walikula na kunywa chakula cha kiroho (cha 1Wakorintho 10:4). Tunamjua mtu huyu
kwenye Agano Jipya kuwa ni Yesu Kristo. Huu ulikuwa ni mtazamo wa Kanisa zima
lote la Kikristo, likiwemo kanisa la Roma, kwa kipindi cha karne moja hadi
mbili za kwanza (sawa na alivyosema Justin Martyr kwenye kitabu chake cha First
Apology LXIII). Tazama majarida mengine ya: Teolojia ya Mwanzo ya Uungu (Na. 127); Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa Kwake
Duniani (Na. 243); Wateule Kama Elohim (Na. 1); Zaburi 8 (Na. 14); na Torati na Amri ya Tano (Na. 258).
Itakuwaje basi kuwe na
sababu ya utoaji dhabihu kipindi cha Milenia kama kifo cha Kristo kilihitimisha
dhabihu & kukomesha utoaji wa dhabihu siku hizi? (Zekaria 14:16-19;
Ezekieli 46:3).
Jibu: Umwagaji wa damu umekoma na kuthibitiwa.
Uanzishwaji wa utaratibu wa kuchinja wanyama wakati wa sikukuu huko Yerusalemu
hauna mashaka yoyote kabisa. Sababu ya kufanya hivyo ni kuthibiti vifaa zana
vya machinjioni na utakatifu wa mchakato wenyewe kwenye mpango wa Mungu. Imani
ya kula mbogamboga peke yake na kutokula nyama ijulikanayo kama Uvujiteriani ni
fundisho la mapepo na ndiyo maana vikundi vya watu hawa wasiokula nyama
wanapenda kufundisha kuwa kipindi hiki cha millennia kitakuwa mbinguni kama
wanavyofanya wafuasi wa Waadventista Wasabato wakiwa chini ya mafundisho ya
nabii mke wa uwongo Ellen G White. Tazama na kulisoma jarida la Milenia na Unyakuo (Na. 95). Kristo alikuwa ni dhabihu kamilifu bali
sheria na kanuni au utaratibu ya kusimamia sikukuu na ulaji wa nyama unazidi
kawaida kwa kiasi fulani kwenye imani ya mrengo wa milenia ya kimwili.
Kwa nini wakati mwingine Kristo aliwagawa “makundi
madogomadogo” wanafunzi watatu watatu? Nagundua kuwa kuna wakati ambapo
wanafunzi walitumwa wakiwa na vikundi vya wawili wawili nk, lakini watatu hawa
wanaonekana kuunganishwa pamoja kwa wakati wake muafaka.
Jibu: Utaratibu chini ya ufalme ulikuwa ni wa mfalme, akifuatiwa na watatu
wengine na kisha thelathini. Mashujaa hawa watatu waliokuwa chini ya Daudi walikuwa
chini ya Abishai, ndugu yake Yoabu na mwana wa Seruya (2Samweli 23:13, 18).
Utaratibu au muundo huu unaonekana pia kwenye 2Nyakati 27:1. Jeshi la Israeli
liligawanyika kwa vikosi 12 vya watu 24,000. Hawa walikuwa chini ya usimamizi
wa watu kumi na mbili miongoni mwa thelathini. Hawa thelathini walikuwa ni
baraza la ndani la wazee sabini.
Waliliwakilisha
baraza la Elohim kwenye maskani ya mbinguni. Kwa hiyo, hawa watatu walikuwa ni
mashujaa wa watu kumi na mbili na walikuwa ni makamanda wa jeshi zima la
Israeli. Petro, Yohana na Yakobo wanawakilisha uwepo wa watu hawa watatu kwenye
Jeshi la Israeli chini ya Masihi. Jeshi la askari 600 la Daudi (1Samweli 23:13)
liligawanywa kwa vikosi vitatu vya askari 200 kila kimoja na lenye vikosi
vidogovidogo kumi kumi. Kila kimoja kiliongozwa na mmoja wa wale thelathini.
Kamanda wa wale thelathini hakuw mmoja wa wale watatu. Bullinger ameandika
habari za watu hawa kwenye ura na aya za 27:1 na sura ya 11 na pia kwenye
2Samweli 23.
Kristo alikuwa na
watatu pamoja na wale kumi na mbili, lakini kwa jambo hili, hawa watatu
walikuwa ni sehemu ya kumi na mbili kwa kuwa hawa watatu kwenye kipindi cha
milenia waliwakilishwa na mitume hawa waliokuja kipindi na zama nyingine. Na
bado kwamba sehemu yao ilijulikana kama si ya muhimu kwenye mchakato na
utendaji kazi wa huduma ya Kristo akiwa kama mfalme wa Israeli. Hawa watatu kwa
kweli ni Ibrahimu, Musa na Eliya. Wote hawakuwepo hai kipindi hiki.
Kuna maandiko meingine mengi kwenye Biblia
yanayosema kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi wetu. Pia kuna maandiko mengi kuwa
Mungu ni Mwokozi wetu. Tunaweza kudhani na kufikiri kutokana na andiko hili
kwamba Mungu na Kristo ni mtu mmoja? Au huenda kwamba Mungu ana sehemu mbili au
tatu za Utrinitariani au Ubinitariani tunaotakiwa kuuamini? Tafadhali, nisaidie
kupata ufumbuzi wa fumbo hili. Je, Mwokozi wetu ni yupi hasa?
Jibu: Swali hili ni chanzo cha mkanganyiko uliowakumba waru wengi. Ndiyo, Biblia
inasema kuwa Kristo ni Mwokozi wetu, na pia inasema kuwa Mungu ni Mwokozi wetu
pia, na inatupa maandiko pia ambayo kwayo yanawataja watu wote wawili kwa uzito
mmoja uliosawa. Ni kwa kutokana na maandiko mengi kwenye Biblia ambako maneno
haya yanatumika na tunafikia kuelewa maana na utendaji kazi wa maneno haya.
Swali hili
limejibiwa kwa kina kwenye jarida lenye kichwa cha maneno Mungu Mwokozi Wetu (Na. 198). Ni kama yalivyo majina yote ya vyeo vya Kristo,
ni cheo alichopewa kama cheo alichoruzukiwa na Mungu. Kwa kutathmini kwa kina
zaidi kuhusu kazi au huduma ya Masihi, kama tutaililia maanani kanuni hiyo basi
tutaona mgongano wote ulioko kwenye mwonekano wake halisi. Majarida
yanayosaidia kujua zaidi jambo hili ni haya hapa chini Kazi ya Masihi (Na. 226) na Stadi wa Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na Omega (Na. 229).
Ni mtindo gani wa ufundishaji alioutumia Yesu ili
kutimiliza unabii wa Zaburi? Wengine wanasema kuwa ni kwa Mifano. Nadhani aliutimiliza
unabii kwa jinsi alivyoishi maisha yake na hadi kifo chake mtini na
alivyofufuka. Je, nakosea?
Jibu: Waweza kufundisha kwa mifano pamoja na kwa kuelekeza. Biblia inasema kuwa alifundisha kwa
mifano, na iltabiriwa kuwa atafundisha kwa mifano. Utaratibu alioufanya wa
kufundisha kwa maelekezo ulikuwa sahihi pia. Kwa kweli, alifanya yote mawili,
lakini mpango na jibu rahisi ni kwamba alifundisha kwa mifano, na hivyo ndivyo
alivyofanya. Hakuna shaka kuhusu mfano wa maisha yake, kifo chake na kufufuka kwake
vilikuwa ni mwonekano wa nguvu sana wa Mpango wa Mungu, jambo ambalo alikuja
hapa kufundisha.
Kristo alisema
kwa mifano ili wasiweze kuelewa kabla ya wakati wao na wasije wakageuka na
kuokolewa: Zaburi 49:4; 78:2; Ezekieli 17:2; 20:49; 24:3; Mathayo 13:3-35;
21:45; 22:1 na kadhalika. Na ndiyo maana ni wachache sana wanaoielewa Biblia
leo – kwakuwa walikuwa ni nyumba ya uasi.
Nimelitafuta jibu hili kwene
Biblia na sijaliona. Utafiti wangu unaonekana kuwalenga kuonyesha kuwa watu
wanaweza uwa walaji wa mbogamboga tu na wasiokula nyama kama watachagua kuwa
hivyo. Hivi karibuni nilisikia kuwa
Kristo alikuwa mtu wa kundi hili la wasiokula nyama. Je, ni kweli?
Jibu: Yesu Kristo kwa kweli hakuna wa imani hii
ya wasiokula nyma na wala mbogamboga. Yeye pamoja na mitume walimla Pasaka na
walizishika sheria za ulaji wa vyakula na walisika maadhimisho ya sikukuu kama
ilivyoamriwa na Mungu. Fundisho hili potofu la ulaji wa mbogamboga tu na
kutokula nyama ni la uwongo, ambalo liliingia kwenye Ukristo kutoka kwenye
Unostiki katika karne za mwanzoni na liliupotosha Ukristo tangu wakati huo kwa
kiwango kukibwa na cha wastani.
Historia yote nzima ya fundisho hili imefafanuliwa kwa kina kwenye jarida
la Uvijitariani na Biblia (Na. 183). Likiwa ni fundisho la kizushi, kwa
kawaida linaendelea mbali sambamba na fundisho linguine la kyjinyima anasa
lihusulo kuwa na kiasi na unywaji wa juisi ya zabibu. Hii imeelezewa kwa kina
pia kwenye jarida la Mvinyo Kwenye Biblia (Na. 188). Fundisho la ulaji mbogamboga tupu au Uvijiteriani ni upotoshaji wa makusudi
juu ya asili ya Mungu.
Ni imani yangu kabisa
kuamini kuwa Mungu, Yesu na Roho Mtakatifu wako mbalimbali kila mmoja na
mwenzake. Wakati Yesu alipokuwa pale mtini na akasema “Baba wasamehe kwa kuwa
hawajui watendalo” hakuwa anamwambia Mungu? Iwapo kama unaambia watu kwamba
wanasema kile kinachominiwa na dini potofu za uwongo au kalti. Wanaamini kuwa
Mungu ni neno aliyekuwepo mwanzoni na kwamba ndiye huyu diye huyu Yesu na
kwamba yeye ni (Mungu) aliyekuja duniani. Je, kuna majarida au maandiko
matakatifu yanayothibitisha hilo?
Jibu: Kwenye karne mbili za kwanza za Kanisa,
yeyote aliyesema kuwa Kristo alikuwa sawa na wa milele kama Mungu ambaye ni
Baba, angetengwa na ushirka kwa kuchukuliwa kama mfundisha uzushi na
angeondolewa mbali kutoka Kanisani. Tazama jarida la Teolojia ya Mwanzoni ya Uungu (Na. 127). Imani ya Utrinitariani haikuwepo hadi
mwaka 381 BK kwa maazimio ya mtaguso wa Constantinople.
Imani ya Kiinitarian ilianzishwa kwenye mtaguso wa Nicaea mwaka 325.
Umodalism uliingizwa Kanisani kwenye karne ya tatu. Kwenye karne ya pili, kila
mahali hata Wamontana, waliamini kuwa Kristo alikuwa ni Mwana wa Mungu na sio
Mungu wa Pekee wa Kweli, na kwamba Roho Mtakatifu alikuwa ni nguvu au uweza tu
wa Mungu. Kanisa huko Roma lilimwandikia mfalme wa Roma mnamo miaka ya 150-154
likisema kwamba Kristo alikuwa ndiye Yule Malaika wa Agano la Kale aliyempa
Musa Torati (sawa na kitabu cha Justin Martyr: cha First Apology). Justin kwa niaba ya Kanisa la Roma alimwambia
mfalme kuwa, kama wangeuja watu wanaodai kuwa wao ni Wakristo na wakasema kuwa
kama watakufa watakwenda mbinguni, asiwaamini kabisa kwa kuwa hawakuwa Wakristo
(kitabu chake cha Second Apology).
Walikuwa ni wafalme wa Kinostiki kabisa walioingia Kanisani na huk wakiwa
na mafundisho yao ya uwongo. Lakini kinyeume na hali hiyo, siku hizi kama
utaongea na Wabaptisti wa Kusini watakuambia: Hakika wanakwenda mbinguni na
wakosefu wengine wote wanakwenda kuungua motoni milele.” Makanisa ya Kristo
yatakupa dondoo za kina ya mahubiri ya jinsi unavyokwenda kuungua kwenye moto.”
Kisha hao wote, Kanisa Katoliki la Roma kwa ujumla litakuambia kuwa ni uzushi
mkubwa sana kutoamini Utatu, Fundisho kuhusu Roho na uwepo wa mbinguni na
motoni na watachukuliwa na Maria kwenda mbinguni pia. Kama wangesema hivyo,
basi maaskofu wa Roma wa kipindi cha mwishoni mwa karne ya kwanza vichwa vyao
vingepasuka kwa mbio wangalizokuwanazo kukimbilia mlangoni ili kumkimbia mtu
huyo.
Ukristo wa Makanisa Kongwe wa leo ni wa mchanganyiko wa imani za Kinostiki
na Kipagani na ambao hauhusiani chochote na Ukristo wa kale wenyewe na wa ile
Imani waliyopewa watakatifu mara moja tu. Ndiyo maana Kristo aliiliza swali
kwamba “Nitakaporudi nitaikuta imani duniani?” kulia na kusaga meno kunawakumba
watu waliohai leo wanaodhani kuwa wangekuwa huko ya Kristo leo, lakini
wakijikuta wakikataliwa tu na wazee wake na manabii wake. Hawakuzishika sheria
na Amri za Mungu wao wenyewe na waliwaua au kuwatesa wale walioamua kuzishika,
wakati wowote walipofanya hivyo. Waalimu wa uwongo waliokufa, watabakia kuwa
hivyo hadi kwenye Ufufuo wa Pili wa wafu. Wengi hawatashangaa kuhusu ni ufufuo
gani watakaojikuta wenyewe wakiwemo. Wengine watashangaa sana. Kama unalijua
hlo basi huenda Mungu anashughulika na wewe. Roho Mtakatifu atashughulika nawe
kwa kukutia wenye kweli yote. Hebu mkabidhi njia zako Mungu, naye atakuongoza
mawazo yako. Hakuna njia nyingine mbadala wake. Yakupasa kutenda sawasawa na
ulivyopewa kuelewa, na utakapozidishiwa ufahamu zaidi. Yakupasa kumtafuta mmoja
kati ya wazee wamtumikiao Mungu ili akuwekee mikono ili umpokee Roho Mtakatifu,
kama umshabatizwa tayari ukiwa mtu mzima na sio kwenye dini yoyote ya imani
kongwe hizi au kuwa mwanadini tu. Na ndipo yakupasa kuwa mtii kwenye ushikaji
wa sheria na amri za Mungu. Usiwaruhusu vipofu hawa waendlee kukuongoza na
ambao wanakuondolea fursa yako ya kuungia ufalme wa Mbinguni pia yasome
majarida yafuatayo: Toba na Ubatizo (Na. 52); Msalaba: Chanzo Chake na Maana Yake (Na. 39); Torati ya Mungu (Na. L1); Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa Kwake Rasmi
Duniani (Na. 243).
Ni nini maana ya neno “stdi?”
Jibu: Neno “Stadi” (kwenye SHD 746) linamaanisha manzo au chanzo na kwa hiyo, ni
mwanzo. Kwa mtazamo huu, linaweza pia kumaanisha “mwanzo” na wakati mwingine
linatumika kwa kumaanisha “mtemi au kuu” akiwa wa kwanza katika kuwekwa kwenye
utaratibu. Kwa hiyo linatumika kwa kumaanisha “utawala au sheria” kama ilivyo
kwene Yohana 20:20 ambapo imetafsiriwa kama “nguvu.” Hii ni mara chache sana
kama linavyotuiwa kwa kawaida kama “mwanzo,” nah ii ndiyo hasa kusudi lake.
Matumzi ya “mtemi” au “mtawala” mara zote linamaanisha kuwa ni moja ya jozi kwa
linavyojitokeza. Kwa hiyo, ni mamlaka au mfalme kwa jinsi ya kwamba mtu huyu ni
wa kwanza kwenye jozi.
Inatumika mara 43
kwenye Agano Jipya ambako imetafsiriwa kama “mwanzo.” Matumizi ya neno “Stadi”
ikimhusisha Kristo kuna maana maalumu ya kiteolojia, ambayo yamepingwa na waamini
Utatu na imepelekea kwenye nyongeza ya kwenye tafsiri ya KJV kwenye Ufunuo 1,
kusomeka Alfa na Omega. Jambo hili limechambuliwa kwa kina kwenye jarida la Stadi wa Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na Omega (Na: 229).
Tafsiri ya NIV
inatajwa “stadi au mwanzo wa uumbaji” kwenye Ufunuo 3:14 kama “mtawala wa
uumbaji wa Mungu” ili kupata dalili halisi ya matumizi ya neno hili kwene
andiko hilo. Hata hivyo, tafsiri ya Thayers Greek English Lexicon pia inatoa ufafanuzi
wa jambo hili na wakati wote kwenye muono huu inaonyesha kama ni mtu wa kwanza
au kitu kwenye mwandamano wa matukio (pp. 76-77).
Ni nani basi huyu malaika aliye kwene Ufunuo
anayesema: “Liambie Kanisa la Laodikia kuwa Mimi ni mwanzo wa uumbaji wa
Mungu”?
Jibu: Mwanzo wa Uumbaji wa Mungu ni Yesu Kristo. Mazingira yameelezewa kwa kina
kwenye majarida ya Stadi wa Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na Omega (Na.
229) na Uwepo wa Yesu Kristo Kipindi cha Kabla ya Kuzaliwa Kwake Rasi Duniani (Na.
243).
Imekuwaje kwamba Yesu hakuandika kitabu chochote
cha kwenye Biblia yeye mwenyewe? Nafikiri kwamba kitabu hicho kingekuwa bora
zaidi kwenye Biblia yote.
Jibu: Kristo alinena kwa manabii, nao waliyanena aliyoyasema. Yeye ndiye
aliyenena na Musa na kumpa Torati. Alinena na manabii wa Agano la Kale, na alinena kwa mitume wa kanisa la
Agano Jipya, na aliwapa maelekezo na mifano, ambayo walinukuu na kuandika. Kwa
hiyo, ndipo tuna Biblia ambayo ni kazi yenye uvuvio wa Mungu iliytolewa na Yesu
Kristo aliyewapa manabii. Soma majarida ya Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa Kwake Rasmi Duniani (Na. 243); na Biblia (Na. 164).
Roho
Mtakatifu
Je, kwani Roho Mtakatifu ni mtu, au ni nguvu tu ya
Mungu, au ni kitu kingine chochote?
Jibu: Roho Mtakatifu ni Nguvu au Uweza wa Mungu, iliyomwezesha Kristo naa
Malaika wote kuwa wana wa Mungu. Suala la mwonekano wa kimwili wa Roho
Mtakatifu lilijadiliwa sana kwenye Halmashauri Kuu ya Mtaguso wa Constantinople
mwaka 381, ambapo walimtangaza rasmi kuwa ni nafsi ya tatu ya Uungu. Tatizo
lililo kwenye lugha ya Kiingereza ni kuelewa kuwa yeye si nafsi ya kibinadamu,
inatokana na utamaduni wa kutendanisha au kuipa jinsia kwenye kanuni ya lugha
ya Kiingereza, jambo lisilo hivyo wala lazima kwenye lugha ya Kiyunani na hata
kwenye lugha nyingine nyingi nyinginezo. Tazama majarida ya Roho Mtakatifu (Na. 117); Kuwa Sawa na Baba (Na. 81); Jinsia ya Roho Mtakatifu (Na. 155); na Mwendelezo wa Mtindo wa Uplatoni Mamboleo
(Na. 17).
Je, unaamini kwamba kama ukiomba kwa Roho
Mtakatifu, ndipo Mungu atakupa tu?
Jibu: Ndiyo, atakuzidishia mno na atakuleta kwenye ubatizo. Tatizo ni kwamba
inakupasa kuwa mtii ili umpokee. Anatenda kazi pamoja nawe hadi ubatizwe na
kisha anakaa ndani yako unapobatizwa, lakini kama ukiasi na kutotii ndipo
huwezi kumpokea au kumpata. Mara tu unapofikia hatua ya kuelewa, utaweza
kumtafuta na kumuomba mmoja wa wazee wa Kanisa na ubatizwe kwenye mwili wa
Kristo ( na sio kwenye dini au dhehebu).
Kama hupendi
kufanya hivyo, basi usiombe kufanyiwa hivyo, na hatabakia ndani yako. Tazama
majarida ya Roho Mtakatifu (Na. 117) na Kuwa Sawa na Baba (Na. 81).
Je, kuna tofauti yoyote ya kibiblia kati ya nafsi
na roho? Au ni kitu kimoja tu? Ni wapi basi kila kimoja
kinakwenda baada ya kifo? Je, zinakwenda zote mbingun?
Jibu. Biblia inaongelea kuhusu nephesh
(Kiebrania) na pneuma (Kiyunani).
Wanyama wote wana hii nephesh. Nephesh ya mwanadamu imetajwa kuwa inamrudia
Mungu aliyeitoa na mwili unangojea Ufufuo wa Wafu. Kwenye karne za kwanza kama
mtuyeyote akisema kuwa yeye ni Mkristo na akasema kuwa wanapokufa au wakifa
watakwenda mbinguni, ndipo ulijua kuwa walikuwa ni Wakristo wa jina tu lakini
ni waumini wa imani potofu ya Kinostiki.
Justin Martyr
alisema hivyo kwa Mfalme kwa niaba ya Kanisa huko Roma mwaka 150-4 BK. Tazama
majarida ya Nafsi Hai (Na. 92) na Ufufuo wa Wafu (Na. 143).
Ni upi basi Ufalme wa Mungu? Unawezaje kuwa ndani
yetu kama alivyosema Yesu?
Jibu. Ufalme wa Mungu u ndani yetu kama punje ya haradali. No Roho Mtakatifu
tuliyepewa, na anayekua ili kwamba Mungu awe yote katika yote na ndani ya yote.
Tunakuwa elohim kama Malaika wa Yahova vichwani mwetu.
Habari hii
imeelezewa kwa kina kwenye majarida yafuatayo Ufalme wa Milele wa Mungu (Na. 144); na mengine ya Roho Mtakatifu (Na. 117); Kuwa Sawa na Baba (Na. 81); na Wateule Kama Elohim (Na. 1).
Kuna maeneo mengi kadhaa yanayotaja kuhusu maji na
miamba, na maji yaliyotoka kwenye miamba, kwenye maandiko matakatifu. Ni nini maana
ya haya yote?
Jibu: Miamba na maji ni ishara ya Roho Mtakatifu, anayetoka kwenye mwamba ambao
ni Kristo, na ambaye ni mwamba usioweza kuchongwwa kwa mikono ya mwanadamu
kutoka kwenye mlima wa Mwamba ambaye ni Mungu na ambaye juu yake Kristo
atalijenga kanisa lake.
Kristo alikuwa
ndiye mwamba uliokuwa katika Israeli jangwani na kutoka kwa huo, Israeli
walikunywa maji. Kazi na huduma ya Kristo imeandikwa kwa kina kwenye majarida
yafuatayo Kazi ya Masihi (Na. 226); Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa Kwake Rasmi
Duniani (Na. 243); Malaika wa YHVH (Na. 24); na Lengo la Uumbaji na Dhabihu ya Kristo (Na.
160).
Mathayo
Inaonekana kuwa watu huamini kwamba kulikuwa na
nyota iliyokuwa ikiwaka na kung’aa upande wa mashariki wakari Kristo alipokuwa
anazaliwa. Je, hivi ndivyo? Ni nini maana ya kuitaja nyota kwenye Mathayo 2 na
maelezo mengine mengi ya kuzaliwa kwa Masihi?
Jibu: Andiko lililo kwenye Mathayo 2:2 inasema: maana tumeiona nyota yake upande
wa “anatole” na huko ni “mashariki,” ila ni neno pia lililopewa Anatolia au
Asia Ndogo. Inaweza kumaanisha kuwa ‘tuliiona nyota yake kutoka….’, yaani,
wakati wakiwa upande wa mashariki au Anatolia. Kwa kweli, kuenda walikuwa
upande wa kaskazini-mashariki mwa Yudea. Hesabu 24:15-19 inataja kuwa “Nyota”
itatoka “kutoka kwa Yakobo,” ambaye ni Masihi.
Lengo lilikuwa ni
kuifananisha hii kama nyota ya asubuhi Venus, ambayo ilikuwa ni alama au ishara
ya utawala wa kisayari kama mleta nuru. Shetani ana cheo hiki ambacho kinamtaja
pia Kristo kuwanacho atakaporudi. Ni kama anavyosema Bullinger, maswali yote
yamefumbuliwa kama yatachukuliwa kama ni ya kimiujiza.
Inaonekana kuwa ni ngeni
kwangu kwamba wakati Mfalme Herode alipojaribu kumuua Masihi angali bado mtoto
mchanga (Mathayo 2:13), na Mfalme Herode Mwingine aliyekuwa na Yakobo, ndugu wa
Yohana, alimuua (Matendo 12:1). Je, kuna kitu fulani ndani ya jina la Herode
ambacho kina maana fulani ambavyo ndiyo sababu wanakuwa kinyume kabisa na
Masihi na wafuasi wake?
Jibu: Chuki inarudi nyuma kwa namna kubwa.
Herode alikuwa ni Idumean. Kwa maneno mengine alikuwa Muedomu. Kizazi chao
chote cha utawala katika Yuda kilitokana na wongofu wa shuruti chini ya
Hyrcanus na Wamakabayo. Walienea maeneo yote ya Midiani, lakini waliingia pia
pande za kusini mwa Yudea kwa kuongoka kwao na wakaweka makazi maeneo ya
Hebron. Eneo la mashariki mwa Yudea kwa hiyo lilikuwa ni la watu
waliochanganika na Waedomu na Yuda, Lawi na Wasamaria.
Ndiyo maana Kristo alituhumiwa kuwa ni Msamaria na Mafarisayo – sio kwa
sababu yeye alikuwa hivyo, bali kwa kuwa walikuwa na tahadhari kuhusu wakzi w
eneo hilo wasiokuwa Israeli halisi waliokuwa chini ya utawala wa kizazi cha
utawala cha Hasmonean tangu wakati wa Hyrcanus. Uchungu na kisasi unaelekea
nyuma hadi kwenye zama za Esau na Yakobo. Haki ya uzaliwa wa kwanza ilikuja kwa
kupitia Yusufu bali fimbo ya enzi ya ufalme ilikuja kupitia kwa Yuda, na
Hasmoneans walijua sana kuwa hawakuwa kwenye mstari wa uzao wa kifalme wa Yuda.
Familia ya Kristo ilikuwa ni ya uzao wa kifalme pia kama tunavyoona kwenye
maandiko ya Agano Jipya na walikuwepon sana na wakiwa vizuri kama Desposyni
walioliongoza au kulitawala kanisa. Kwa hiyo, Waherodi, na ambao baadae
walijulikana kama askofu wa Kirumi, wote walijaribu kuwakomesha kwa sababu
hizohizo. Tangu mwaka 318, askofu wa Roma alijaribu kuwaua na kukomesha imani yao
kwa kipindi cha zaidi karne mbili, na hakkuweza kufanikiwa japo kidogo.
Kwenye Mathayo 2:17-18,
Yeremia 31:15-20 kunanukuliwa kimakosa mno kama unabii ilitimia. Ni nini
kilitokea kwa Herode ambaye hakuwa hata amekaribia kwenye unabii huo ulio
kwenye Yeremia. Je, Mathayo alikuwa ni nabii wa uwongo?
Jibu: Hapana, watoto wa Raheli walikuwa na haki
ya uzaliwa wa kwanza. Kwa jambo hili, iliwajumuisha makabila yote pamoja na
Yuda. Mauaji ya Herode hayakufanyika kwa mtindo kama mauaji ya kuangamiza jamii
nzima ya Wayahudi yajulikanayo kama Holocaust, bali wote walikuwa na ahadi moja
hiyohiyo. Imeandikwa: “Manase atamlisha Efraimu na Efraimu watamlisha Manase na
wote wawili watamlisha Yuda.” Sasa, Yuda ni mtoto wa Lea, na sio wa Raheli.
Umefafanua kuwa toba ya kweli inatikana na maombi
na kufung; nimegundua kuwa Mungu maombi ya kupayukapayuka nay a kurudiarudia.
Je, unaweza kuelezea njia bora ya maombi mazuri? (Mathayo 6:5-15)
Jibu: Mungu ameweka utaratibu wa kuomba kwenye Biblia. Kristo alitupatia
madondoo ya jinsi ya kuomba kwenye Mathayo 6. Bali wewe usalipo, ingia
katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za
Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Nanyi mkiwa
katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya
kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao;
maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. Roho Mtakatifu atakupa jinsi ya kuomba na
kutamka na kusihi.
Utaratibu wa
kuomba na dondoo zake ni:
1) Baba yetu uliye
mbinguni. Msifu yeye na
mshukuru kwa kila jambo.
2) Jina lako
litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko
mbinguni. Omba aje Masihi na
kuanzishwa kwa utawala wa millennia na ufalme wa Mungu uje hapa duniani.
3) Utupe leo riziki
yetu. Ombea mahitaji yetu ya
kila siku na umshukuru kwa kutupatia.
4) Utusamehe deni
zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Hii inatukumbuksha kanuni ya sheria nay a
msamaha wa dhambi na madeni ilivyo kwenye kanuni za Biblia.
5) Na usitutie
majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Utajaribiwa lakini hakuna jaribu ambalo hutapewa
njia au mlango wa kutokea. Hata kwenye majaribu ya maishani mwetu tutatiwa
nguvu kitabia.
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe
ninyi. Hivyo, Maombi ya Bwana yanaweza kuonekana
kuwa kama ni dondoo au kiashirio cha maombi ya watakatifu. Hayapo kwenye
mpayukopayuko kwenye mpangilio wake. Tazama jarida la Tufundishe Kuomba (Na. 111).
Mathayo 12:50: “Kwa
maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye
ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.” Napenda kujua mawazo yako
yalikuwa wapi kwa hili?
Jibu: Tukiweka msingi wetu kwenye andiko hili, tunachukua majukumu na wajibu wa
kuwafundisha wengine kama washirika katika mwili wa Kristo kwa kiwango kingine
cha juu sana. Kwa mfano, tunapokuwa kwenye majukumu au wajibu wa kuhakikisha
kwamba masikini wanapaswa kusaidiwa wamudu kuhudhuria sikukuu, inafuatia kuwa
inawapasa waishike sikukuu na wewe ili uwasaidie.
Yatupasa kufanya
maamuzi haya kila siku. Kwa mfano, tunapokea maombi ya kuomba kusaidiwa kutoka
kwa idadi kubwa ya Makanisa ya India, Afika na kwingineko. Wengine ni kutoka
makanisa ya Kipentekoste na wengine ni kutoka kwa watu wetu wenyewe. Mara
nyingi, wale wanaotokana na makusanyiko yetu wanapewa zaidi au wanawekewa
kipaumbele kikubwa. Iwapo kama hatutafaletea madhara yoyote watu hawa,
hatutaweza kuwasaidia kwa kuwapa vitu vyetu.
Akili za kuzaliwa
nazo zinakuambia kuwa mtu anayeyafanya mapenzi ya baba yako wa mbinguni
anastahili kupewa kipaumbele. Hili ni jaribio rahisi na lililosawa. Kama
hawaneni wala kuenenda sawasawa na sheria na ushuhuda, hakuna nuru ndani yao
(Isaya 8:20). Kama utaona tukio la mara moja linalohitaji msaada, ndipo unatoa
msaada wako kama Msamaria Mwema. Inapojitokeza jambo linalostahili kusaidia
sawasawa na hitaji ndipo itabidi uijali familia kwanza. Familia hiyo ni Kanisa.
Tazama majarida ya Torati na Amri ya Tano (Na. 258) na Mlolongo wote wa majarida ya Torati
likiwemo la Amri Iliyokuu ya Pili (Na. 257).
Nimekutana na maandio mengi yahusuyo ufungaji
saumu kwenye Biblia, lakini sina uhakika yote haya yana maana gani. Je, unaweza
kunifafanulia? (Mathayo 17:21)
Jibu. Andiko hili linaonyesha mapepo ya namna mbalimbali na aina hii ilihitaji
maombi na kufunga saumu kwa wateule. Kwa hiyo, utaratibu wa kuabudu unaweza
kuonekana kama mchezo au mzaha tu kama ukifanywa bila utii wa kuyatii tu
mapepo.
Andiko hili
linatokana na lugha ya Kisyria na maandiko mengine yameliruka. Bullinger
ameandika vizuri sana kuhusu jambo hili na analinukuu andiko hili lililoachwa
kuandikwa kwene ukurasa wa 21 kwenye tafsiri ya Companion Bible. Tazama pia kwenye jarida la Upatanisho (Na. 138).
Kwenye mfano wa Mathayo 20:13 tunasoma habari za
mtu anayeitwa Rafiki aliyekata tamaa kutokana na wengine kulipwa ujira sawa na
yeye ingawaje yeye alikuwa kazini kwa kuda mrefu zaidi ya wote. Kisha kwenye
Mathayo 22 tunasoma habari za ‘mtu’ aliyeingia arusini bila kuvaa vazi la
arusi. Kwenye aya ya 12 mtu huyu anaitwa pia ‘Rafiki’ na hatimaye kwenye aya ya
13 anafungwa na kutupwa nje gizani. Kisha kwenye Mathayo 26 tunasoma Kristo
akimwita Yuda ‘Rafiki’. Swali langu ni kwamba je, Maandiko haya yanamaanisha
kumtaja Shetani?
Jibu: Neno lililo kwenye Mathayo ni “hetairos” au ndugu, ambalo ni tofauti
kabisa maana yake na neno “philos.” ‘Mtu’ aliyetajwa kwenye nje ya kundi, kwa
namna hiyohiyo mtume Petro alikuwa ‘ndiye’ aliyetajwa kwenye Mathayo 19:27.
Yeye hana vazi la arusi na haina maana yoyote kwa kuwa hawezi kujibu uachwaji
huo. Kuna mlolongo wa makundi hapa. Yule aliyeficha hakuja. Hii inammaanisha
Yuda. Anaweza pia kupunguza kwamba inaweza kuonekana kufunika watakatifu, na
wote walikataa kuingia kwenye ufalme wa mileniamu.
Kitendo cha kulia
na kusaga meno sio cha malaika walioasi. Wanajua walichokifanya na kilichobakia
kwao sasa. Lakini bado wangali na fursa ya kuokoka, bali wakiwa kama viumbe
wenye kuonekana, na kisha watabadilishwa kuwa viumbe wapya kwenye ufalme huo.
Wao pia watapewa fursa ya kuzaliwa mara ya pili.
Wengi wa hawa watakaosaga
meno watakuoja kutoka kwa wale wanaojiita wenyewe kuwa Wakristo lakini wakiwa
hawazishiki amri zake Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12).
Wanamwita “Bwana, Bwana” na huku wakiacha kutenda aliyoyatenda yeye au
aliyoyaamuru, na wakiuhalalisha uasi wao kwa uwongo. Wapo wengi sana watu kama
hawa na kwa kweli, wengi wao watakataliwa kwa kuwa mwenendo wao uliwaondoa
kwenye atahiki ya kuuingia ufalme na hawajitawali kutokanao iwe kama wewe
umebadilishwa na kuingizwa mjini Yerusalemu na Kristo au la, hakuna mjadala.
Iwe kama umetii au la.
Wafu hawajui
lolote, bali waliohai watasaga meno kwa kuwa wanakwenda kwenye dhiki kuu na
hawatalindwa watoke katika saa ya kujaribiwa iliyoayari kuujaribu ulimwengu
wote. Kwenye mfano wa tatu, Yuda alikuwa anawawakilisha Yuda iliyouza sehemu
yao kwenye ufalme. Ndivyo pia alivyofana Shetani, na ndivyo adui anawakilishwa
na atapasa kukabiliwa ufufuo wa pili wa wafu pia. Majarida haya ya Ufufuo wa Wafu (Na. 143); Hukumu ya Mapepo (Na. 80); Kondoo Aliyepotea na Mwana Mpotevu (Na. 199); na Dondoo la Majira ya Nyakati (Na. 272) yanaonyesha mpango huu.
Je, Jina la Baba ni lipi na la Roho Mtakatifu
kwenye Mathayo 28:19?
Jibu: Ni swali zuri.
Biblia inajijibu yenyewe. Swali linatokana na Mithali 30:4: “Na ni nani jina la
mwanawe, kama wajua”. Limejibiwa kwenye aya inayofuatia: “Kila neno la Mungu
limehakikishwa”. Jina la Mngu wa Pekee na wa Kweli ni “Eloah.” Ni Torati yake. Makuhani walimwabudu yeye
na Hekalu lake. Alisababisha jina lake liwekwe huko Yerusalemu (sawa na Ezra
4:24-7:26).
Eloah ni jina
linaloonyesha umoja na amejiongeza mwenyewe ili awe Elohim. Yeye ni “Ha Elohim”
au “Mungu.” Huyu alikuwa “Elahh” kwa Wakaldayo na alijiongeza kuwa “Elahhin”
kwa wana wa Mungu. Elahh ndiye hatimaye aliitwa “Allah’ ” kwa Kiarabu. Yeye ni
Elyon au Mungu Aliye Juu sana. Yeye ndiye Yahovah wa Majeshi aliyewawatoa
Israeli na kuwapa Yahovah kama mali na warithi wake maalumu (Kumbukumbu la
Torati 32:8 RSV). Yeye ni Yahovih (SHD 3069) ambaye ni Mungu wa Yahovah (SHD
3068).
Mambo haya
yameelezwa kwa kina kwenye majarida ya Majina ya Mungu (Na. 116); Malaika wa YHVH (Na. 24) na pia
Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa Kwake Hapa Duniani (Na. 243).
Kuna matatizo makubwa
sana kwenye teolojia ya Majina Matakatifu. Tazama jarida la Abracadabra: Maana ya Majina (Na. 240).
Marko
Unaweza kuniambia jinsi
Yohana batizaji alivyokuwa anavaa vazi lililotengenezwa kwa singa ya ngamia na
huku ngamia akiwa ni mnyama najisi na ambaye hatupaswi kugusa mizoga ya wanama
najisi? Nadhani kuwa alikuwa anajivika mwili wake wote na sio nywele
zisizokatwa peke yake. (Marko 1:6)
Jibu: Vazi lake halikuwa la ngozi bali ni la
manyoya yaliyosokotwa ya ngamia. Hakuna katazo kufana hivyo. Katazo la kutogusa
mizoga kwa kawaida linahusu vitu vilivyojifia vyenyewe kibudu. Kuna maandiko ya
ziada kwene Campanion Bible kwenye Marko 1:6 kuhusu manoya ya ngamia.
Je, waweza kufafanua tafadhali maana iliyokusudiwa
kwene Marko 5:21-43? Vitu ninavyovigundua ni mwanamke ugonjwa wa kutokwa damu
kwa miaka 12 mwenye imani ya kugusa tu pindo la Kristo na akapona, na pia binti
mwenye umri wa miaka 12 aliyekuwa hali ya kufa pamoja na baba, ofisa au
mtumishi wa sinagogi, aliyekuwa na imani ya kwamba Kristo angewea kumpona.
Ingawa aliambiwa kuwa mtoto wake alikuwa amekwisha fariki, Kristo akatangulia
kwenye chumba cha mtoto na kumponya binti huyo na kumwambia apokee chakula. Ni
vifungu vinavyovutia sana lakini maana yake ni nini?
Jibu: Maeleo ya maandiko yenewe ni haya.
Marko 5:21-43 Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia
ng'ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya
bahari [Yairo akaja]. 22 Akaja mtu mmoja katika wakuu
wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake, 23 akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa;
nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi. 24 Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata,
wakimsonga-songa. 25 Na mwanamke mmoja mwenye kutoka
damu muda wa miaka kumi na miwili, 26 na kuteswa mengi
kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae
hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya 27 aliposikia
habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; 28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. 29 Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu
mwilini mwake kwamba amepona msiba ule. 30 Mara Yesu,
hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano,
akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu? 31 Wanafunzi
wake wakamwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusonga-songa, nawe wasema, Ni
nani aliyenigusa? 32 Akatazama pande zote ili amwone
yule aliyelitenda neno hilo. 33 Na yule mwanamke
akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia,
akamweleza kweli yote. 34 Akamwambia, Binti, imani
yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena. 35 Hata alipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa yule
mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kumsumbua
mwalimu? 36 Lakini Yesu, alipolisikia lile neno
likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu. 37
Wala hakumruhusu mtu afuatane naye, ila Petro, na Yakobo, na Yohana
nduguye Yakobo. 38 Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa
sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu. 39 Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na
kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu. 40 Wakamcheka
sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamaye,
na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana. 41 Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi;
tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka. 42 Mara
akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na
miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu. 43 Akawaonya
sana, mtu asijue habari ile; akaamuru apewe chakula.
Kwenye Marko
7:15 Yesu alisema yafuatayo: “Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho
kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo
unajisi yule mtu.” Watu wengine huyatumia Maandiko haya kuonyesha kuwa hakuna
chakula kilicho najisi na kwamba vitu vyote vinawea kuliwa. Kwani Yesu
anasemaje hasa hapa?
Jibu: Mafarisayo walikuwa wanahusika na shuguli a kusimamia sheria na tarfatibu
na taratibu a kutawadha aidi ya ilivyoagiwa kwenye Maandiko Matakatifu, na
walikuwa wanawalaumu wanafuni. Lengo kamili la andiko hili lawea kuonekana
kwenye jarida la Maandiko ya Mtendo ya Sheria - au MMT (Na. 104).
Andiko hili lililopotea
lilikutikana kwenye Gombo zilizochimbuliwa kwenye Bahari ya Chumvi, mashuhuri
kama Dead Sea Scrolls kwenye karne hii. Mtume Paulo pia aliandika kupinga hali
hii kwenye nyaraka zake kwa Wagalatia na Wakolosai. Luther hakuelewa kabisa
alichokuwa anakisema na kumaanisha Mtume Paulo kwa sababu ya mtazamo wake wa
kupinga Usemitiki.
Kristo alikuwa
anasema kuwa Mafarisayo wanapaswa kuyaangalie au kuyatakari sana yale
waliyokuwa wakiyasema, ambayo yalikuwa yanapotosha mahudhui ya sheria au torati
zaidi kuliko vile walivyokuwa wakiogopa ambayo yaliingia vinywani wakati
walipokuwa wanakula. Kristo na Mitume wakewote walishika Sheria ya Vyakula na
Kanisa limekuwa likizishika kwa kipindi cha takriban miaka 2000. Tazama kwenye jarida la Sheria ya Vyakula (Na. 15).
Swali langu linatokana
na Mark 10:18, linalosema: “Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna
aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.” Nilitaka kujua, kama Yesu alikuwa Bwana,
basi ni kwa nini hakutaka kuitwa mwema, na ni yupi basi huyu Mungu
mwingine anayemuita Mwema?
Jibu: Yohana 17:3 inajibu swali hili, kama inavyofanya Yohana 1:18 kwenye
tafsiri ya Marshall’s Interlinear RSV na 1Timotheo 6:16. Yohana inasema: “ambaye yeye
peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala
hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye
hata milele. Amina.” Na tena “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu
wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”
Kwa hiyo, huyu
Mungu wa pekee wa Kweli ndiye alimtuma Yesu Kristo. Ili kuujua ukweli huu na
ili kuwajua wao ndiyo kuupata uzima wa milele. Yohana sura ya 1, inaelezea
jinsi alivyotumwa Kristo, na huyu Mungu wa Pekee wa Kweli na kusudi lake.
Yohana 1:18 inasema: “Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee
aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua. Neno “monogenes theos” au “yeye aliyezaliwa na Mungu
lilibadilishwa ili lisomeke “monogenes uios” au “mwana aliyezaliwa wa pekee”
kwenye Receptus.
Pia Paul
anafafanua kuwa hakuna mtu aliyewahi kumuona Mungu, au atakayeweza kumuona
Mungu. Anaketi kwene makao yasiyofikika na yeye peke yake ndiye hawezi kufa
(1Timotheo 6:16). Tazama kwene majarida ya Kwa Hali ya Kutokufa (Na. 165) na Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa Kwake Duniani (Na. 243). Kristo pia alifafanua kuwa hakuna mtu
aliyewahi kumuona Mungu. Inamaana kwamba hakuna hata aliyewahi “hata kuisikia
sauti yake wakati wowote wala kuliona umbo lake” (Yohana 5:37).
Kwa hiyo jinsi
Kristo alivyo imeelezwa kwa kina kwenye Zaburi 45:6-7 na ambaye anajulikana
kama Kristo kwenye Waebrania 1:8-9. Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha
enzi,(ni kiti cha enzi cha) Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme
wako ni fimbo ya adili. Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu
wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.” Kwa hiyo, mwana ni elohim. Anatajwa kwenye
Zekariah 12:8 kama “Malaika wa Bwana” ambaye alikuwa ni kichwa cha numba ya
Daudi, ambao ni wateule na ambao vilevile watakuwa elohim. Imeandikwa: “Mimi nimesema,
Ndinyi miungu. Wana wa Alie Juu, ninyo wote pia, na maandiko hayawezi kutanguka” (sawa na Yohana 10:34-35).
Luka
Ni watu gani hawa wanaotajwa kwenye Biblia kuwa ni
ndugu zake? Je, ni wale tu walio na imani sahihi na wanaozishika amri za Mungu,
au ni wengine wote waliobatizwa kwa jina la Yesu lakini wakawa wanaabudu kwenye
mapokeo ya wanadamu na sio kwa Mungu? Tunawezaje kuwafanyia vema wengine ambao
hawajiiti wao wenyewe ndugu, bali ni wa dunia hii? (Luka 10:25-37)
Jibu: Swali aliloulizwa Kristo na Mwanasheria lilikuwa, “Jirani yangu ni nani”
sawa na, “Ndugu yangu ni nani?” Ndipo Kristo akawapa mfano wa Msamaria Mwema
ili kuonyesha kwamba dhana hii inawahusu watu wote. Torati au Sheria za Mungu
zi mioyoni mwetu na kwa hiyo hakuna upendeleo unaowezekana. Tazama jarida la Kupendelea Watu (Na. 221) na Upendo na Utaratibu wa Torati (Na. 200). Tunatumwa na kupelekwa katikati ya mbwa
mwitu. Wapende watu wote. Hata hivyo, wakati mwingine ni vizuri kumpenda mtu wa
mbali.
Watu wengi duniani wanaamini kuhusu unyakuo wa
kanisa. Mimi sipingi dhana hii, kwa kuwa name nimeipenda dhana hii, lakini
siioni kwenye Biblia. Na ninapojitahidi kwa bidii kubwa kutafuta uthibitisho,
ndipo kwenye Luka 12:36 najaribu kuona kama panafanana na fundisho hili
lisemapo: “nanyi iweni kama watu
wanaomngojea bwana wao, ATAKAPORUDI KUTOKA ARUSINI, ili atakapokuja na kubisha,
wamfungulie mara.” Hii inaonekana kana kwamba alikuwa
arusini, kashaa akarudi “kubisha hodi” kwa wale ambao hawakwenda arusini, kama
ilivyo kwenye mfano wa wanawali 10. Je, ni wakati gani itakavyofanyika arusi
hii na wa karamu ya arusi?
Jibu: Ndiyo, Luka 12:36 ni andiko linaloeleweka sana. 1Wathesalonike 4:17 ni
andiko mashuhuri wanalolitumia waamini unyakuo. Andiko hili hata hivyo
linaelezea kuhusu kuchukuliwa kwa wateule hadi mawinguni ili kumlaki Bwana
atakaporudi hapa chini duniani na watakutanika nay eye huko Yerusalemu kama
tuonavyo kwenye maandiko mengine mengi yanayohusiana na tukio hili. Jambo hili limefafanuliwa kwa kina kwene
jarida la Tarumbeta (Na. 136). Dhana yote nzima kuhusu kunyakuliwa
imetathiminiwa kwa kina kwenye jarida la Milenia na Unyakuo (Na. 95). Neno hili jinsi lilivyoandikwa kwenye
injili ya Luka 12:36 ni “kurudi.”
Neno lililotumika
ni “analuo.” Linajitokeza hapa peke yake na kwenye Wafilipi 1:23 kwenye Agano
Jipya. Lilitumika kwenye tafsiri ya Septuagint (LXX) peke yake kwenye vitabu
vya Apokrifa, na kilamara likimaanisha “kurudi tena.” Bullinger anasema kuwa
lina mrengo wa “ana-kampti” (Waebrania 11:15). Mahali inapotajwa pengine ni
kwenye vitabu vya Tobiti 2:9; Yudithi 13:1; 1Esdras 3:3; Hekima 2:1; 5:12;
16:14; Ecclesiasticus 3:15; 2Wamakabayo 8:25; 9:1; 12:7; 15:28. Nauni ya
“analusis” kama “mwili kuyarudia mavubi”, kama kwenye Mwanzo 3:19, inaonekana
mara moja tu kwenye 2Timotheo 4:6.
Utaratibu wa
karamu ya arusi waonekana kuwa ulitabiriwa na walengwa wa kwanza ni waliokwisha
kufa au kulala mauti katika Kristo ndio watakuwa wa kwanza kwenye utaratibu
huu, na hatimaye waliohai watahusishwa kwenye awamu ya pili kwenda kumlaki
hewani ili kuwa pamoja na Bwana milele. Biblia inasema kuwa wale watakaokutwa
wakiwa hai hawatawatangulia (kuwazuia) wale waliokwisha kulala mauti. Bali
watafufuliwa ili kuhudhuria kikamilifu karamu ya arusi kwanza. Hii ndiyo sababu
na umuhimu wa kurudi kwake Masihi kwa wale wanaomngojea. kisha ndipo
tutakapokuwa kwenye mchakato wa kuifanya upya dunia na kuitawala mwa kufuata
mujibu wa Sheria za Mungu kwa kipindi cha miaka elfu cha Milenia. Tazama jarida
la Uchambuzi wa Ratiba ya Nyakati (Na. 272).
Je, unaweza tafadhali kufafanua maana ya mfano wa
wakoma 10 waliotakaswa na ni kwa nini ni Msamaria peke yake ndiye alirudi ili
kushukuru na kumpa Mungu utukufu? Hadithi iliyoandikwa kwenye Luka 17:11.
Jibu: Andiko linasema kuwa Kristo alikuwa anapita katikati ya Samaria na
Galilaya na wakoma kumi walimwendea wakasimama kwa mbali. Hii ilikuwa ni kwa
mujibu wa sheria zilizoagizwa kwenye Mambo ya Walawi 13:45-46. Tafsiri ya Talmud hatimaye iliandika
makadirio ya umbali huu kuwa ni takriban mita 100.
Makabila Kumi
yalikuwa ni wa asili ya Samaria. Wasamaria walikuwa ni mchanganyiko wa
Wakutheans na Wamedi waliochanganya damu zao na masalia wachache wa makabila
kumi yaliyokuwa yamesalia katika Israeli baada ya kuhamishwa kwao utumwani na
Mfalme Shalmaneser mwaka 722 KK.
Wayahudi
waliwachukia na waliwapinga kwa kipindi cha karne kadhaa na kukataa kuyakubali
mapokeo yao. Upande wa Kaskazini mwa Galilaya ulikuwa ni nchi iliyojitenga
kabisa Yudea. Ulikuwa pia umejumuisha Wayahudi, Wasamaria na wengineo. Wayudea
walikuwa ni mkusanyiko wa aina zote mbili, yaani Yuda na Lawi, na pia Waidumean
au Waedomu walioongokea imani ya Kiyahudi chini ya Wamakabayo ambao Mfalme
Herode alikuwa ni mmoja wao.
Mmoja wa hawa
waliotakasika, Msamaria, alirudi kumpa Mungu utukufu kwa kutakasika kwake.
Kristo akamuuliza, “Je, hamkutakaswa kumi? Wakowapi kenda wengine?” hii
inaonyesha ukweli kwamba makabila mengi hayajamrudia yeye.
Mfano huu
unatupeleka pia nyuma kwenye tukio lililo kwenye 2Wafalme 17:29-35 na
kuondolewa kwa Israeli nchini mwao na nafasi yao kuchukuliwa na Wakutha na
Waavi na Wahamathi. Jinsi Mungu alivyowapelekea simba ili wawaue hadi
walipowaomba wapelekewe makuhani hadi Israeli ili wawaonyeshe na kuwafundisha
jinsi ya kumwabudu Mungu. Lakini pamoja na hayo watu wa kila taifa wakajifanyia
miungu yao wenyewe, wakaiweka katika nyumba za mahali pa juu, walipopafanya
Wasamaria, kila taifa katika miji yao walimokaa. Watu wa Babeli wakafanya Sukoth-benothi
kuwa mungu wao, watu wa Kutha wakafanya Nergali, watu wa Hamathi wakafanya
Ashima, Waavi wakafanya Nibhazi na Tartaki; nao Wasefarvi wakawaunguza wana wao
katika moto kwa Adrameleki na Anameleki, miungu ya Sefarvaimu.
Kulikuwa na waume
watano wa Kisamaria waliobudu na kulikuwa na miungu ya mataifa matano
iliyoingizwa kutoka kwenye ufamle wa kaskazini na kutoka kwa Waisraeli
waliotawanyika. Ndipo hatimaye walimwabudu Yahova pamoja na miungu wengine. Na
hii ndiyo sababu iliyompelekea Kristo kumwambia yule mwanamke aliyekutananaye
kisimani, ambaye alikuwa ameolewa na wanaume watano na yule aliyekuwanaye
wakati ule sio wa kwake “Unaabudu usichokijua” (Yohana 4:18, 22).
Alitumiwa kama
mfano na Mungu kwa maisha yake ya kikahaba na ndoa ya nchi za Kaskazini
iliyofananishwa na wanaume watano, na wasiomjua Mungu wanaoishi dhambini kwenye
amri au makatazo haramu katika Samaria. Mwanamke aliyekuwa kisimani ni
mlinganisho wenyenguvu na pia ni fundisho kuhusu ndoa.
Tunaweza
kulinganisha kifungu hik cha maandiko na Isaya 54:5; 23:17; Yeremia 22:20;
Hosea. 2:10-12. Kutumia mfano wa wakoma kumi yalilenga kuhusianisha na makabila
ya kaskazini nay a Wamataifa, na kuwaleta mataifa katika Israeli na kuwatakasa.
Msamaria alikuwa ndiyo peke yake aliyerudi na kuja kushukuru kuonyesha kuwa ni
sehemu ya hawa walioponywa ambao wametubu kihalisia na kumpa Mungu utukufu.
Neno lililotumika kumtaja “mgeni” hapa ni “asiye mwenyeji.”
Hivyo, kuna
mashahidi wawili pia kwa kila mataifa matano walioletwa upande wa kaskazini na
walio kinyume na miungu mitano iliyoiletea madhara imani yao ya kiibada na
inayowachukulia wao kuwa wako najisi na wakoma.
Rafiki yupo kwenye darasa la Biblia la Agano Jipya
na aliuliza mahali ambapo mfano wa talanta ulikusudia, msikilizaji wake alikuwa
nani na maana yake ilikuwa ni ipi. Je, unaweza kuniapa mtazamo wako kuhusu
kifungu hiki? Je, unaielewaje maana yake Luka 19:12 na wa paundi
10?
Jibu: Mifano huu uliyofuatiwa unabii wa Mzabibu. Wanafunzi walimfuata Kristo
kutoka Hekaluni hadi kwenye Mlima wa Mizeituni na wakamuuliza kwa siri awaambie
ni lini mambo haya yote yatakapotokea. Ndipo akawapa mfano wa Mzeituni na
kashaa akaendelea kuwapa mifano mingine. Maana ya andiko hili ni kwamba kila
mmoja amepewa kiwango fulani cha nguvu za kiroho na uelewa, mwingine zaidi yaw
engine. Kanisa linapaswa kuungana pamoja naa wengine wote wenye talanta au
karama, bila kujali kwa wingi au uchache kiasi gani, bal wanatakiwa kuchangia
ili kusaidia kazi ili kwamba iweze kukua.
Wale walo na
msingi tu wa Roho hawasamehewi kufanya kazi. Wanatakiwa kujipambanua kama mwili
na kuweka mali zao kwenye mahitaji ya wengine. Na kama hawatafanyahivyo basi
Kristo atawakataa kuingia kwenye ufalme wake. Na ndiyo sababu hakuna yeyote
kati yetu anayeweza kukaa nyumbani bila kujishughulisha na kitu chochote.
Paundi zilizoelezwa kwenye mfano wa Injili ya Luka unamaana moja iliyochukuliwa
kwa mujibu wa juhudi binafsi kwa niaba ya kazi. Utendaji wa kimakini na wa
mafanikio ya kazi unaijara sawasawa na juhudi alizoonyesha mtu.
Wakati Kristo alipokuwa pale
mtini akisulibiwa pamoja na wezi wawili, mmoja wao alimpokea Yesu. Na Yesu
alimjiu kuwa ‘Yesu akamwambia, Amin,
nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami Paradiso. (Luka 23:43). Je, Peponi au Paradiso ni “mahali pa kushikiliwa wafu” au ni
mbinguni? Sielewi. Kwenye kitabu cha Mwanzo kuasema kuwa aliziumba “mbingu na
nchi” mbingu nyingi na nchi moja. Tafadhali fafanua.
Jibu: Wakati Kristo alipokuwa pale mtini
alimwambia mtu yule: “Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja
nami peponi.” Ni sawa tu na
kusema kwamba, “Nakuambia sasa hivi, utakuwa pamoja nami” nk. Imetafsiriwa
vibaya na Wanostiki ili kuhalalisha mafundisho yao. Kristo alikuwa mautini kwa
kipindi cha siku tatu mchana na usiku, kwa hiyo, kama alimaanisha hivyo, mtu
yule angekuwa mbinguni pamoja naye siku ile, basi angekuwa ni mwongo na
kumfanya asiwe Masihi. Maelezo kuhusu mchakato wa uumbaji ni mapana sana kwa
dunia na hali yake asilia na kutoka kwenye mkazo wa huko nyuma.
Yohana
Natafuta mlinganisho kati ya
kitabu cha Mwanzo na kitabu cha Yuhana. Nimekwisha fananisha tayari neno la
Mungu na nuru na sijawa na kitu kingine chochote. Je, unaweza kunisaidia?
Jibu: Hili ni jambo linalopendeza. Injili ya
Yohana iliandikwa baada ya injili nyingine zinazofanana, na inatosheleza
mafungufu yaliyomo kwenye injili hizo ya kumtaja Kristo kwenye mfuatano wa
matukio ya nyakati zake na kipindi kamili cha kuhudumu kwake. Yuhana
anahusishwa, kama unavyoonekana kuashiria, kwa kudhihirisha nafasi na uwepo wa
Kristo kipindi cha kabl ya kuzaliwa kwake rasmi duniani akihusiana kiukaribu na
Mungu. Kanisa la Agano Jipya lilifanya kazi ya kufundisha kwa kipindi cha marne
mbili kuwa Kristo alikuwa ndiye yule Malaika wa Agano la Kale aliyempa Torati
nabii Musa. Hili lilikuwa ni jambo la muhimu ili kujua na kuelewa jukumu na
wajibu wa Kristo na nafasi yake kwa Mungu, na mafundisho ya Agano la Kale kama
yalivyotafsiriwa kwenye Agano Jipya. Mambo haya yamechambuliwa kwa kina kwenye
majarida ya: Uwepo wa Yesu Kristo Kipindi cha Kabla ya
Kuzaliwa Kwake Rasmi Duniani (Na. 243); Malaika wa YHVH (Na. 24); Stadi wa Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na Omega (Na.
229); na Yoshua, Masihi, Mwana wa Mungu (Na. 134).
Utakutana na idadi kubwa
ya majarida kwenye tovuti yetu yanayoelezea asili ya Mungu na nafasi ya Kristo.
Uhusiano wa Injili ya Yohana na vitabu vya Torati unaonekana wazi kwenye majarida.
Je, unaweza kunifafanulia kuhusu Yohana 5:1-24?
Je, Yesu aliivunja Sabato au ni je, Mungu alimruhusu kufanya hivyo?
Jibu. Hapana, Yesu hakuivunja Sabato. Mafarisayo walisema kuwa alivunja. Kile
alichotangua kilikuwa ni tafsiri yao ya uwongo ya naneno yaliyo kwenye Yeremia
17:21-22. Mafarisayo alikitumia kifungu hiki walifanya ubebaji wa kitu chochote
kutoka sehemu moja ya wazi hadi nyingine, na kingine kutoka sehemu moja ya siri
hadi nyingine, siku ya Sabato kuwa ni halali (soma Talmud Sabb. 6a).
Nabii Yeremia
anaongelea kuhusu ubebaji wa mizigo kuingia Yerusalemu, au kutoka nyumbani, na
kwenda kufanya kazi siku ya Sabato. Kuchua mkeka mmoja tu wa kulalia nyumbani
kungekuwa ni uvunjaji mkubwa sana wa Sabato, lakini walikuwa wanataka kufanya
ionekane hivyo. Hatimaye Baraza la Mishnah (mwaka 200) lilifafanua kwa kina
kilichopasa kutolewa, kuhusu suala hili la vifaa vya kulalia, iwapo kama kwa
mfano, Siku ya Upatanisho ikiangukia siku iliyofuatia baada ya Sabato, ambayo
kwa wakati mwingine walifanya kabla ya mafundisho ya uahirisho hayajashika
kasi. Kristo alishika Sheria, ila mara nyingi alikosoa kitendo cha kutafsiri
vibaya au kimakosa sheria, kama ilivyo kwenye suala hili.
Yohana 5:18: Basi kwa
sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu,
bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Kwa
nini Wayahudi walimwelewa Yesu kuwa alikuwa anasema
kuwa alikuwa sawa na Baba, wakati inaonekana wazi sana kwamba alichokuwa anadai
ya kuwa yeye ni Mwana wa Mungu? Wale wanaoamini Utatu wanalichukulia andiko
hili kama ushahidi kwamba Mwana alikuwa na hadhi sawa ya kiuungu na Baba kama
sehemu ya muungano wao wa Utatu.
Jibu: Kuelewa kuwa Elohim aliyetajwa kwenye Agano la Kale, ambaye ndiye alimpa
Musa Torati, kuwa alikuwa Malaika Mkuu ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wana wa
Mungu. Wanalielewa andiko la Zaburi 45:6-7: “Kwa hiyo MUNGU, Mungu
wako, amekupaka mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.” kuwa ni kama linamtaja Masihi ambaye ndiye
alikuwa Mwana wa Mungu.
Mithali 30:4-5
inauliza swali kama ilivyo kwenye jina la Mungu ni lipi na la Mwanae ni lipi
pia, na kisha inalitaja jina lake Mungu wa Pekee wa Kweli kwa umoja wake kwenye
aya ya 5, ilimuita kuwa ni Eloah. Kwa Kikaldayo, aliitwa “Elahh.” Uwingi wake
ulikuwa ni “Elohim” na “Elahhin” kwa Kikaldayo. Toleo la kimashariki la lugha
ambayo ilifanyika kuwa ni Kiaramu cha Kimashariki ambayo hatimaye kilikuja
kufanyika kuwa ni Kiarabu, na ndiyo maana Waislamu wanasema kuwa jina la Mungu
kuwa ni “Allah’”; likiwa na h mbili kuwa ni msisitizo.
Wakati Kiyunani
kinapolitumia neon “aggelos” lililotafsiriwa kama “malaika” au “angel” kwa
Kiingereza. Limetumika kuwataja “wana wa Mungu” au “elohim” kwenye Kiebrania.
Limetumika hivyo pia kwenye tafsiri ya Kiyunani ya Septuagint (LXX) na pia
kwenye Agano Jipya. Zaburi 8:4,5,6, iliyonakiliwa ikisema: “Mtu ni kitu
gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko
Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; Umemtawaza juu ya kazi za mikono
yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.”
Sasa neno hili
ni, kama tunavyoliona kwenye Kiebrania, “elohim” ambalo maana yake ni “miungu.”
Lilitafsiriwa kama “malaika” wengi kwenye tafsiri ya Septuagint na pia kutoka
hapo hadi kwene maandiko ya Kiyunani kwenye Kiebrabia. Inabeba maana hiyohiyo
kwenye tafsiri za Vulgate, Kisyria na Kiarabu kwa kuwa iliwapendeza waamini
Utatu kuwa nayo hii kama “malaika” na kuruka maneno yasemayo “kwa kitambo
kidogo.” Sababu iliuwa ni kwamba hakuna hata mmoja wao aliyependa kujua kuwa
“elohim” walikuwa ni ongezeko tu la utaratibu wa viumbe.
Hata hivyo,
andiko hili ni wazi kabisa linasema “elohim” kwenye Kiebrania asilia, na
makuhani walijua kuwa mwana wa adamu alikuwa ni elohim aliyefanyika hatimaye
kuwa ni Mwana wa Mungu akiwa ni “monogenes theos” au “mzaliwa pekee wa Mungu”
aliyetajwa kwenye Yohana 1:18 (sawa na tafsiri ya Marshall’s Greek English
Interlinear RSV). Maandiko yaliyo kwenye tafsiri ya Companion Bible kuhusu
andiko hili yanafafanua kwa kina mambo haya.
Walikuwa
wanamtaja yeye walimfanya kuwa sawa na elohim na, kwa kuwa hii haikuongelewa
kwenye Kiyunani ila kwenye Kiaramu, tunapata andiko hili kuwa “elohi” kisha
linaonekana kuwa ni “malaika.” Wana wa Mungu wote walikuwa ni elohim kama
maandiko ya Agano la Kale yanavyoonyesha kwenye matumizi yake. Elohim hawa
walijulikana kama “aggelos” {ang’-el-os} au
“wajumbe” na walitafsiriwa kama malaika au “angel” kwa Kiingereza na kwenye
maandiko mengine. Hata hivyo, makuhani wa Hekaluni hawakuyumbishwa na mapokeo
ya kipagani ya Kirumi wakiigiza kujifanya kama Wakristo kwa karne chache za
wakati huu, na kwa hiyo walijua maana yake kikamilifu na vizuri sana.
Kwenye Yohana 7:53 Mafarisayo wanamkemea Nikodemo wakisema: “Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya
hakutokea nabii.” Usemi huu si sahihi, ikikumbukwa pia kwamba Yona
alitokea Galilaya. Hata hivyo, Isaya 9:1 inasema: “...hatimaye yeye (Mungu)
ataiondolea aibu na kudharauliwa Galilaya...” ambayo inafuatiwa na aya ya 6
inayosema “Maana kwa ajili yetu
mtoto amezaliwa, … Naye ataitwa jina lake … Mfalme wa amani.” Aliwezaje Isaya
kupata uhakika wa wazi sana kiasi hiki? Je, Mafarisayo walifanya makosa ya
kiuana zuoni, au walikuwa wanafanya makosa ya makusudi kuusema uweli, yaani
waliamua kuongopa, ili kutumikia mwisho wao mbaya na usiofaa?
Jibu: Ndiyo, walikuwa wanaongopa ili kuzitumikia tama zao zisizokoma, kama
mtazamo wa shughuli za kidini ulivyo hata leo, kuongopa ili kujipatia faida zao
wenyewe. Ukristo wa imani za dini Kongwe ni vurimai ya ibada za kipagani,
miungo ya uwongo na imani potofu kwa kuwa makasisi wake wanafundisha au
kutumika kwa malipo au mshahara na wamejitungia au kijitengenezea imani zao za
uwongo ili kukidhi au kuchanganya na mapokeo na imani za kipagani za watawala
na Dola ya Warumi walizozipenda na kuziamini.
Yona na Hosea
wote wawili walitokea Galilaya, Eliya alikuwa Mtishbi na Wagileadi walikuwa
wanatoka mashariki, Bullinger anasema kuwa yeye na Elisha, na huenda hata Amos,
wanaonekana kuwa walikuwa na uhusiano wa kinasaba na Galilaya.
Sababu hasa nay a
kweli pia ilikuwa ni kwamba Wagalilaya walikuwa pia ni wana wa kweli wa Yuda,
lakini wenyeji wa Yudea wengi walikuwa na idadi kubwa ya Waedomu. Hii huenda
ndiyo sababu ya kwamba misingi halisi ya uliokuwa nyuma ya juhudi ya Mafarisayo
ya kupotosha au kutafsiri vibaya Maandiko Matakatifu. Chini ya sheria, Galilaya
ilichukuliwa kama ni sehemu nyingine iliyotengwa na nchi. Jambo mhimu na la
kweli ni kwamba Yona alitokea Galilaya, na Ishara ya Yona ndiyo pekee
iliyoitolwa ili kuithibitisha huduma ya Kristo na ambayo kwayo Yuda
waliangamizwa kwayo. Soma kwene jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Tena
wa Hekalu (Na. 13); na Uchambuzi wa Ratiba ya Nyakati (Na. 272).
Kwenye Yohana sura ya 10 Yesu Kristo anaongelea
kuhusu Mchungaji Mwema na kuwajua kondoo wake, kuutoa uhai wake kwa ajili ya
kondoo zake hao, nk. Kisha aya ya 16 inaongelea kuhusu ‘kondoo wengine’, ambao sio
wa zizi lake. (1) Kina nani hawa Kristo anaowaelezea kuwa ni kondoo wa ‘zizi
hili’ na (2) kina nani hawa wanaotajwa kuwa ni ‘kondoo wengine?’
Jibu: Kondoo hawa ni wale wanaowafuata na kuwasikiliza wachungaji wa uwongo.
Alisema pia kwamba wengi watamwita “Bwana, Bwana,” wa wasiyatende mapenzi yake.
Atawaambia “Tokeni apa kwangu.” Hawa pia ni wale walioitwa lakini wasiwe
wateule na kuingia kwenye zizi la wateule. Maelezo ya kitabu cha Ufunuo
huonyesha kuwa kuna imani yaa dini za uwongo, ambazo zitaangamizwa katika siku
za mwisho. Hivi ndivyo alivyoelezea na ufafanuzi alioufanya.
Dini za uwongo
zilikuwa kazini katika kujaribu kuingiza imani potofu ya Baal-Easter mapema
sana katika wakati wa Yohana, aliyeziandika kwa kina mafundisho na habari za
Mpingakristo, mafun disho yanayotenganisha ubinadamu wa Kristo na hali ya
uungu. Haya yalikuwa ni mafundisho ya imani ya waabudu mungu Attis, ambayo
yalimuweka mungu Attis kwenye cheo cha namna zote mbili, yaani baba na mwana
kuwa ni mungu mmoja huyohuyo.
Mafundisho haya
na mtazamo huu ukaingizwa kwenye imani ya Kikristo kama Ubinitariani na
hatimaye ukazaliwa Utrinitariani. Imani ya Unostiki ilipata nguvu na ushawishi
mkubwa pamoja na kukubalika na kuingizwa kwa imani na mafundisho yao ya
mbinguni na motoni, makatazo au kujinyima vinywaji, useja na ulaji wa
mbogamboga tupu, yaani imani ya kutokula nyama. Soma majarida ya Uvijiteriani Kwene Biblia (Na. 183); na Mvinyo Kwenye Biblia (Na. 188).
Yohana 12:12-13 inaonyesha kuwa watu walibeba
matawi a mitende na wakaenda kumlaki. Je, matawi ya mitende yana maana yoyote
kiimani pamoja na miti yennewe ya mitende au kuna uhusiano na ile ya kwenye
Kutoka 15:27, Hesabu 33:9 au ile ya kwenye mahekalu ya 1Wafalme 6:29,32,35,
2Nyakati 3:5, Ezekieli 40:16, 29, 32,35,41:18-20?
Jibu: Salamu iliyo kwenye andiko hili inatokana na Zaburi 118:25,26. Uingiaji
wake Bwana Hekaluni na jinsi walivyomsifu kundi la watu kwa Kiaramu inamaaisha:
“saidia sasa” (Hoshi' an-na). miti ya mitende ina maana yake kwa kuwa inafanana
pia na ukweli wa Masihi. Kwenye hekalu aliloonyeshwa nabii Ezekieli utauona
umewekwa katikati ya makerubi wawili, makerubi yenye vichwa vya binadamu na
samba. Mti wa mzeituni unaashiria Malaika wa Uwepo na mti uliofanya maji ya
Meriba yakubalike na Israeli.
Kama Yesu alisulibiwa siku ya Jumatano, ni nini
basi kinachomaanisha kwenye Yohana 19:31?
Jibu: Siku hii ilikuwa ni ya 14 ya mwezi wa Abibu, ambayo ilikuwa ni Siku ya
Maandalizi makubwa ya Pasaka ambayo mwanakondoo wake aliuawa alasiri wakati
alipouawa Kristo. Na mwanakondoo huyo aliliwa usiku ule ule wa Siku ya Kwanza
ya Miate Isiyotiwa Chachu. Kumbuka isemavyo Yohana 19:31:
“Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili
isikae juu ya misalaba [stauros] siku ya sabato, (maana sabato ile ilikuwa siku
kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe, wakaondolewe. ”
Katika mwaka
aliosulibiwa Kristo, ambao ni mwaka wa 30 BK, siku ya 14 Abibu iliangukia siku
ya Jumatano. Kwa hiyo, Siku ya Takatifu ya Kwanza ya Mikate Isiyotiwa Chachu ya
15 Abibu iliangukia siku ya Alhamisi tangu join ya siku iliyotangulia (yaani
usiku wa Jumatano). Kwa hiyo alishinda kaburini siku za Alhamisi, Ijumaa na
siku ya Sabato. Alifufuka mwishoni mwa Sabato kukiwa ni siku tatu kamili za
mchana na usiku kuwa kaburini, sawaswa na ulivyosema unabii.
Taarifa za
mwanzoni zinasema walikuwa wanafundisha kuwa tukio hili la kusulibiwa
lilifanyika siku ya Jumatano. Imani na maadhimisho ya Easter na Usulibiwaji wa
Ijumaa vinatokana na imani potofu za miungu ya Attis na Adonis. Tazama majarida
ya Chanzo cha Krismas na Easter (Na. 235); Mabishano ya Wakuartodeciman (Na. 277). Pia tazama jarida la Majira ya Kusulibiwa na Kufufuka (Na. 159).
Itajibu maswali yako
kuhusu nyakati na maandiko.
Matendo
Kwa nini baadhi ya vitabu
kama cha Matendo haviishii na neno Amina
na vitabu vingine vingi vinafanya hivyo?
Jibu: Neno hili “Amen” linatokna na lugha ya
Kiebrania SHD 543 “'amina” maana yake ni “hakika.” Linapotumika kama kijivebu,
linatumika kama “kweli” na kimsisitizo linamaanisha “uaminifu”. Kwa hiyo
linamaanisha, “na iwe hivyo” au “ni kweli”. Neno “Amina” linatumika kwa kuwa ni
agizo la moja kwa moja la Mungu chini ya sheria. Neno la Kiyunani SGD 281 amen ni tafsiri ya kiuandishi ya moja
kwa moja kutoka kwenye lugha ya Kiebrania lenye maana hiyohiyo moja. Ilichukuliwa
kutoka kwenye Kiingereza kwa karne nyingi lenye maana hiyohiyo. Kwa hiyo, watu
wetu wanaendelea kulitumia hadi siku hizi kwa agizo walilopewa na Mungu pale
Sinai. Makundi yote mawili, yaani wanawake na wanaume wanabudi kulitumia neno
hili (sawa na Hesabu 5:22; Kumbukumbu la Torati 27:15-26). Ni msisitizo wa
kuonyesha au kumaanisha ushindi au kukubaliana yaliyoombwa kwenye maombi na
watu wote. Lilitamkwa hivyo kwenye kipindi chote cha marejesho mapya (Nehemia
5:13; 8:6). Linatokea kwenye Zaburi pia. Lilinenwa na manabii (Yeremia 28:6).
Kristo aliagiza litumike kama sehemu ya Sala ya Bwana.
Limerukwa kwenye maandiko hayohayo kwa kuwa yalikuwa ni historia tu. Kwa
wengine, lilitumika kama msisitizo wa kusema “na iwe hivyo” kwa kuwa Kanisa
lilikuwa likishutumiwa lilikuwa kwenye anga la Mamlaka ya Mungu, wakati kwamba
kitabu cha Matendo hakikuwa waraka uliohitaji kuonyesha ushindi au kutenda
kutoka Kanisani. Kuna nadharia iliyozidishwa inayoendelewaa na baadhi ya
Makanisa ya Marekani kuwa linauhusiano fulani na imani za kale za Wamisri na
kwa namna fulani linatokana au limechukuliwa kwenye mitindi ya ibada za mungu
Amun Ra. Huu ni uwongo wa wazi kabisa na waanzilishi wa uvumi huu au mafundisho
haya wanajaribu tu kuishusha hadhi na kuipotosha sheria moja wapo iliyo kwenye
Torati ya Mungu inayosisitiza kutamka neno hili, jambo ambalo Israeli na Kanisa
wamekuwa wakilifanya kwa uaminifu mkubwa tangu pale Sinai hadi siku za leo.
Kwenye Pentekoste ya kwanza, baada ya kifo cha
Measihi, wanafunzi 12 walikusanyika pamoja saa 3 asubuhi na wakampokea Roho
Mtakatifu. Je, hii inaweza kuwa ni dalili ya wateule kuwa mahali pa kusaidia
kusimamia sheria ya Mungu? Yawezekana kuwa kwamba wale makutano 120 wa kwenye
Matendo 1:15 ni ishara au imanaanisha Yubile 120 iliyotimia kikamilifu, ambayo
kwamba Shetani na malaika wake waasi watafungwa kwa kipindi cha miaka “1000” na
Roho Mtakatifu wa Mungu atakuwepo ulimwenguni mwote wakati huu wa millennia na
kufuatia?
Jibu: Ndiyo. Hili ni jambo lenye kupendeza sana. Tunajifunza kuona kwamba
vipindi vitatu vya miaka arobaini arobaini vinafanya jumla ya miaka 120,
ambavyo ni zama tatu na hivi vinaonekana kimuashirio kwenye maisha ya nabii
Musa na vya Utawala wa Wafalme. Jaiida litatolewa hivi karibuni kuelezea kwa
kina. Mtazamo wa kwamba hawa 120 walikuwa muhimu kama taswira ya kuhitimisha
mavuno ya Mungu unavutia sana na huenda ni sahihi.
Matendo 15:24-29 inaonekana kusema kuwa wamataifa
hawapaswi kuzishika sheria zote, bali wanapaswa tu kujiepusha na ulaji wa nyama
zilizotolewa sadaka kwa sanamu na ulaji wa damu na uasherati? Wakati kwamba
vitu vya “lazima vimekwisha orodheshewa?
Matendo 15:24-29 states: Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu
waliotoka kwetu wamewasumbua kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, ambao sisi
hatukuwaagiza; 25 sisi tumeona vema, hali tumepatana
kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwapeleka kwenu pamoja na wapendwa wetu
Barnaba na Paulo, 26 watu waliohatirisha maisha yao
kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo. 27 Basi
tumewatuma Yuda na Sila, watakaowaambia wenyewe maneno yayo hayo kwa vinywa
vyao. 28 Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi,
tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima, 29 yaani,
mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama
zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.
Jibu: Kwenye tafsiri, mtu hazuiwi wala kufungwa na chochote. Ndiyo, Agano Jipya
linaonyesha wazi sana kuwa waliishika sheria ya vyakula, na waliishika Kalenda
Takatifu, na waliishika Pasaka. Kwa kweli, Mabishano ya Waquortodeciman
yalipelekea kufarakana kwa kanisa mwaka 192 na Makanisa ya Washika Sabato
yamejitenga mbali kutoka kwenye Kanisa la Roma tangu wakati huo. Soma jarida la
Mabishano ya Waquartodeciman (Na. 277).
Pia kuna makundi
mengine yaliyotengwa mahali pengine ambayo hayajajuluishwa hapa. Kwa hiyo,
andiko hili linapasa lishughulikiwe na mambo fulani yakinifu kwa malengo fulani
kusudiwa. Hili limeongelewa kwa kina kwenye jarida la Sheria ya Vyakula (Na. 15) na Imani ya Kutokula Nyama ya Ulaji
Mbogamboga Tupu na Biblia (Na. 183).
Andiko hili
waliandikiwa watu waliokuwa kwenye mazingira ya numba ya wapagani, kama vile
watumwa wa mabwana wapagani. Hii ilifanya mazingirfa kuwa ni vigumu sana kwa
waongofu. Maandiko haya hatimaye yaliwahusu watu dhaifu aa imani wanaokula
mbogamboga eke yake kwa tatizo kama hilohilo. Iwapo kama tutalitathimini andiko
hili, na kulichukulia kama linavyosomeka kwamba hii ndiyo imayohitajika pekee
kwenye imani, kisha ndipo amri mbili zikaorodheshwa na ni kipande saidizi cha
sheria au kanuni kuhusu ulaji wa damu.
Amri ya sita hata
haionekani kutajwa hapa, pamoja na ile ya pili moja kwa moja, nay a tatu, ya
nne, ya hamsini na nane, ya tisa na kumi na sio vyovyote. Kwa hiyo, kwa tafsiri
kama hiyo, si vibaya kuua, kudanganya, kuongopa, kuiba, kutamani, na kumkufuru
Mungu. Hakuna anayeamini hivyo, na kuna aliyelitafsiri andiko hilo kwa namna
hiyo au kwa mapokeo yoyote ya kidini, isipokuwa waantinomia siku hizi. Soma
jarida la Sheria ya Mungu (Na. L1) na mwandamano wa majarid mengine ya Torati.
Naelewa kuwa inatupasa kuishika Torati au sheria
za Mungu kutokana na maandiko mbalimbali kadhaa yaliyo kwenye Biblia. Nilikuwa
nasoma kitabu cha Matendo na inasema hatulazimiki kutahiriwa au kuzishika
sheria (Matendo 15:24).
Matendo 15:28-29: "Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na
sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima, 29 yaani,
mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama
zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.”
Naona mahali panapoonyesha kuwa walizishika Sabato, Siku Takatifu, Miandamo ya Mwezi Mpya, nk.
Hii ni sehemu ya maagizo ya Torati. Je ayah ii inaongelea kuhusu sheria
nyingine yoyote; je, ni inakosea au ni makosa ya kitafsiri; au kuna namna
nyingine zaidi ya kuitafsiri kwamba ni kwa nini walisema kwamba Wamataifa
hawalazimiki kufuata na kushika sheria?
Jibu: Andiko lililo kwenye Matendo 15:24 ni la kughushi na limeingizwa makusudi
kwa nia ya kupotosha kwenye tafsiri ya Receptus likiwa na lengo la makusudi
kabisa ya kupotosha mahudhui na umuhimu wa waaminifu wake wasiishike Torati ya
Mungu. Tafsiri ya the Companion Bible KJV inamaelezo yanayoelezea vizuri maneno
haya kwamba: “Kusema kwamba yawapasa mtahiriwe na kuzishika sheria” ambayo
hayapo kwenye maandiko ya zamani, na yahapo kwenye tafsiri nyingine za Biblia na
ikisomeka hivyo au ikituama kwenye maandiko ya zama kale.
Suala lililopo
hapa kuhusu watu wa Mataifa kuingia kwenye imani ndani ya nyumba za wapagani na
ambao walikuwa wanaonyeshwa kwenye imani hizo za kipagani. Utoaji wa moja kwa
moja wa sadaka kwa sanamu uliepukwa, kama ilivyokuwa umeonekana mara nyingi
kuwa ni matendo kutoa sadaka za wanyama zilizosongolewa au kibudu.
Kinachotakiwa kuepukwa pia ni desturi ya uasherati au kufanya ngono, ambayo
ilikuwa ni ya kawaida kufanyika kwenye ibada za Hekaluni ambako damu ilikuwa
inaliwa pia. Kile kiitwacho “Utumbo wa Nguruwe” ni masalia ya siku hizi
yatokanayo na matendo haya. Andiko
hili linashughulika na matendo na halitenganishwi. Soma majarida ya Uvegetariani na Biblia (Na. 183) na Mafundisho ya Mapepo ya Siku za Mwisho (Na. 48).
Warumi
Yeyote anayeijua vyema Warumi sura ya 1 anajua
kwamba Mtume Paulo anaendelea mbele zaidi kwa kulielezea tendo hili na
analitaja kama tendo la ufiraji. Paulo anachagua kutumia neno ‘la kike’
kuelezea tabia takatifu ya kimbinguni. Mambo muhimu na ya juu kiasili yako
kijozi, yaani mwanaume na mwanamke; mwanaume aliongozana na mwanamke, na
mwanamke na mwanaume. Wakati mwanadamu anaposahau hili, walianza kuishi maisha
ya jinsia moja, yaani mwanaume kwa mwanaume, na mwanamke kwa mwanamke. Kifungu
kisemacho “Hekima ya Mungu iliyotajwa” (Luka 11:49) ni sahihi. Kwa imani ya
Kiyahudi, neno Hekima lilikuwa la
nasaba ya kike kwa Mungu. Neno lenyewe lilikuwa linaonyesha nasaba ya kike ya Mungu. Hekima ni kwa Mungu
ambavyo Logos ni Mungu. Kwa mara nyingine tena tunaletwa kwenye mawasiliano na
tabia asilia ya kike ya Mungu. Je, jambo hili linaashiria nini kwenye Ukristo?
Jibu: Dhana iliyopo ya Sophia, kuwa kama hekima, ni ya kike kwa kuwa Logos ni
Bwana arusi, na Kanisa ni Bibi arusi. Hii imetokana pia na mgangano wa kijinsia
wa Roho Mtakatifu (soma jarida la Jinsia ya Roho Mtakatifu (Na. 155)).
Mlingano huu mpya
ulibidi uanguke chini tunaposema kuwa Kristo alipewa roho na kupaa juu kama
Mwana wa Mungu kwa nguvu kwa Kufufuka kwake kutoka kwa wafu. Sio sahihi sana
kumuweka roho wa Kristo kwenye jinsia ya kike kama ilivyo kwenye nasaba ya
kiume kwa kanisa. Wanaume hawana ugumu wa kuelewa dhana ya ubwana arusi wa
Kristo na wakuwa kwa wakati mmoja Mwana wa Mungu.
Tunajua dhana ya
siri za Mungu kwenye Maandiko ya familia. Uandishi wa waraka wa Warumi
umekusidiwa ili kuonyesha mwendelezo wa kupunguza watu wenye asili ya imani
wakati ibada ya sanamu ikiwa imepuguzwa. Wakati mtu anapomchukua mungu wa
uwongo, ndipo mtu huyo anaanza mwendelezo wa kupungua katika Roho Mtakatifu na
kwa taifa. Ukweli unabakia kwenye ufisadi na ndipo hasira ya Mungu
inawaangukia. Wanageukiana kwa tama zao za mwili.
Mtu hawezi
kurikiria kuelezea vizuri kuhusu mwendelezo wa mzoroto au kuzorota na kupungua
kwa Kanisa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 2000. Baada ya kuingizwa kwa imani ya
Mungu wa Utatu, kipindi cha karne ya pili, Kanisa lililoungana likafanyika kuwa
ni shirika au kiungi kisichoongezeka klichobobea kwenye matendo ya kisodoma na
ukengeufu; likiwaua wale wanaozishika amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo,
likiyakumbatia mafundisho ya mapepo, na kuwaamuru wale wanaojizuia kuoa na
kutokula nyama, ambazo zilitolewa ili zipokelewe kwa shukrani.
Matatizo
mbalimbali yameelezewa kwenye majarida ya Uvegetariani na Biblia (Na. 183) na Wanikolai (Na. 202).
Ni nini “Matendo ya Sheria” (Warumi 3:20)
anayoyataja Paulo kwenye maandiko yake?
Jibu: Matendo ya Sheria ni kitabu. Kilijulikana kama Miqsat Ma'ase
ha Torah. Kwa Kiyunani, kilijulikana kama “ergon nomou” na kwa Kiingereza
ndicho kinachoitwa “Works of the Law”, yaani Matendo ya Sheria.” Kitabu hiki
kilipotezwa kwa makusudi miaka takriban 1900 iliyopita. Gombo mashuhuri la The
Dead Sea Scrolls lina nakala yake. Nakala hii ilitafsiriwa na maprofesa Qimron
na Strugnell. Waraka huu uliandikwa kwa maana yake kwenye fasiri za ufafanuzi
za Agano Jipya. Jarida la Maandiko ya Matendo ya Sheria - au MMT (Na. 104). Maandiko asilia na tafsiri zake
zinapatikana pia kwenye majarida na vitabu vya CCG.
Warumi 10:4 inassma:
‘Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.’
Je Torati iliishia kwa Kristo? Ni nini kilichogongomelewa mtini, maarufu kama msalabani? Na kama ni hivyo,
ni kwa kitu gani gani basi tulichopatanishwa nacho sisi?
Jibu: Torati yote ilimhusu Kristo na mpango wa Mungu kwa kuwa sheria au torati
ilianza kutokana na Asili au Tabia ya Mungu. Na ndiyo maana kwamba Kristo ndiye
mwisho wa Sheria. Hakuitangua torati. Alichokigongomelea pale mtini kama
inavyosema Wakolosai ni mashitaka ya deni au kwa lugha nyingine inaitwa Hati ya
Mashitaka au Chierogriphon. Tuko huru kwa kuwa alilipa gharama ya madeni yetu
kwa kila mmoja wetu na pia kwa kundi kama wateule.
Yeye ajitakasaye na wale wanaotakaswa wote wana asili moja kama inavyosema
Waebrania. Tumepatana na Mungu kwa njia ya Kristo aliyestahili kuwa kiongozi
wetu. Tazama jarida la Uhusiano Uliopo Kati ya Wokovu kwa Neema na Sheria
(Na. 82). Mlolongo wa majarida ya Sheria ni muhimu ukasoma. Tazama pia kwene jarida
la Sheria ya Mungu (Na. L1).
Unaweza kufafanua jambo alilokuwa anajaribu
kulisema Mtume Paulo kwenye Warumi 14.
Jibu: Kwenye Jamii ya Warumi wengi waliokuwa waumini Kanisani walikuwa watumwa.
Kwenye nyumba za Warumi walitenga milo au chakula kwa kulinganisha sawasawa na
siku za utoaji dhabihu. Kwa hiyo, dhana ilikuwa ni kwamba mtu aliye kwenye
milki ya nyumba ya wapagani alichukuliwa kama anakula nyama iliyotolewa sadaka
kwa sanamu.
Samaki walikuwa
watakatifu kwa Atargatis, au Dercato au Cato, na samaki alililiwa kwenye siku
yake, na hivyo Ijumaa ilikuwa ni siku maalumu ya samaki. Kitendo hiki
kinakutikana hata leo kwenye imani ya Wakatoliki Warumi. Wanapoulizwa wanasema
kuwa walifanya uamuzi wa kusaidia kiwanda cha samaki, lakini ukweli ni kwamba
ilianzia kwa samaki mtakatifu aliyejulikana kama mungu Atargatis. Pinata au
kofia ya kiaskofu ilitokana na kumuenzi samaki huyu pia.
Nguva jike
aliyopo ndani yake ni mbegu mpya za uzima au uhai na inatakiwa ivunjwe ili
mbegu zitolewe: Ambayo ni sadaka ya damu ya mwanadamu. Mungu Attis, na makuhani
wake matowashi, walishirikishwa na dini hii potofu ya Easter. Kanisa lilikuwa
linashughulikia na ukweli ambao ndugu wapendwa hawakuujua kwamba ni wapi nyama
hizo zilikokuwa zinatokea. Kwa hiyo, walikuwa wanahukumiana kila mmoja na
mwenzake na wengine waliamua kula mbogamboga tupu, peke yake ili kujiepusha na
uwezekano wa kula nama zilizotolewa sadaka kwa sanamu.
Mtume Paulo
alikuwa anawaambia wajihadhari sana. Sanamu zenyewe hazikuwa ktu kwao, na kama
mtu hakujua, ndipo wale waliokuwa na imani kuu mipngoni mwao walikula nyama
bila kudhurika na chochote. Kwa jambo hili, kuua lilikuwa ni jambo sahihi na
hivyo, damu haikuliwa. Kwa mujibu wa Bullinger, kipindi cha nabii Danieli,
waliacha kula nyama kwa kuwa wanyama walikuwa hawakuchinjwa vyema (tazama
tafsiri ya Companion Bible kwenye
Daniel 1).
Kitendo cha
kufuatilia siku kilifanyika kwa lengo la kuamua ni siku zipi ambazo pia ni aina
gani ya nyama zinapaswa kutolewa sadaka. Halikuwa ni suala la kutozishika
Sabato peke yake, kwa kuwa hilo lilikuwa wazi imeamriwa na kujulikana wakati
ule. Kwenye suala hili, waliamua aina ya dhabihu kwa lengo la kuzila nyama
zake. Jambo hili limeelezwa
kwa kina kwenye jarida la Uvegetariani na Biblia (Na. 183).
Wakati mume anapomchukua au kumuoa mke,
analazimika kumpa jina lake. Kwa hiyo inaweza kusemekana kwamba Kanisa likiwa
kama bibi arusi wa Kristo yapasa liiwe kwa jina lake. Hivyo basi, mtu aliye
kwenye Kanisa la Kristo anaweza kudai kuwa wao ni kanisa sahihi kwa kuwa
wamelichukua jina hili kama lilivyo kwenye Warumi 16:16. Je, hii ni kweli na
sahihi?
Jibu: Hapana. Hiyo si sahihi. Biblia inasema wazi kabisa kuhusu hilo kwamba
Kanisa lina maneno machache. Na majina hayo ni kama yafuatavyo: “Kanisa la
Mungu” (kwenye Wakorintho na kwingineko) kwa makanisa ya mahali pamoja, na
“Makanisa ya Mungu” kwa jina la ujumla kwa mataifa yote. Pia waliitwa
“Wakristo” na kama shirika waliitwa “Njia” au “Watu wa Njia Ile.” Warumi 16:16 inasema kwenye maandiko ya
zamani kwamba “Makanisa yote ya Kristo yanawasalimu.” Hii kwa namna yoyote
inapunguza uzito wa kusudi au lengo la Mungu la kuwa Kichwa cha Kanisa. Kichwa
cha kila mwanaume ni Kristo, na Kichwa cha Kristo ni Mungu. Kristo ni mwili kwa
maana ya kwamba yeye ni Kanisa, na hivi ndivyo ilivyotumika kwenye Warumi.
Jambo hili limefafanuliwa kwa kina kwenye jarida la Muundo wa Makanisa ya Kikristo ya Mungu
(Na. 68).
1Wakorintho
Je, kwani Paulo anaizungumzia Sikukuu ya Miate
Isiyotiwa Chachu hapa?
IWakorintho 5:6-8 Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba
chachu kidogo hulichachusha donge zima? 7 Basi,
jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile
mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka,
yaani, Kristo; 8 basi na tuifanye karamu, si kwa
chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio
weupe wa moyo na kweli.
Na kama ni hivyo, hii inajumuisha pia kuishika
Pasaka kama alivyosema pia kuwa Kristo alitolewa sadaka kama Pasaka wetu? Je,
hii ndiyo sababu iliyopelekea Pasaka kutolewa kwa Waisraeli kwa kipaumbele cha
kwanza ili dhabihu hii ikamilike katika Kristo?
Jibu: Ndiyo, alikuwa anaiongelea Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, ambayo ni
sehemu ya sikukuu hii, inayofanyika mwanzoni mwa Siku 14 ya mwezi wa Abibu
ambayo ni ya Maandalio. Pia alianzisha utaratibu wa kuadhimisha Mlo wa Meza ya
Bwana kwenye mlo wa kwanza wa siku ya 14 Abibu kwenye karamu ya kwanza
ijulikanayo kama Chagigah, ulioanzia siku ya Maandalio ya Pasaka jioni
inayofuatia, ambayo ndiyo ilikuwa Pasaka ya Kristo.
Kama mtu haishiki Sikukuu ya Mikate Isiyo na Chachu, basi halielewi lengo
na dhumuni la kuondolewa kwa dhambi kupitia kwa dhabihu ya Kristo. Mtume Paulo
mitume wengine na kanisa lote la kwanza walizishika sikukuu zote. Mkanganyo
ulianzia mnamo mwaka 192 wakati askofu wa Roma alipojaribu kushurutisha
kuingiza mafundisho ya kizushi ya maadhimisho ya Easter kitendo kilichopelekea
kugawanyika kwa kanisa. Soma jarida la Malumbano na Hoja za Wakuartodeciman (Na. 277). Pia kuna majarida mengine ya Pasaka na
Sikukuu ya Mikate Isiyo na Chachu. Soma pia majarida ya Pasaka (Na. 98); Chachu ya Kale na Mpya (Na. 106a); na Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa (Na. 106b).
Wengine wamefikia kuhitimisha kwamba wanawake
wanapaswa kujifunika ushungi vichwa vyao wanapokuwa wanamuomba Mungu Baba yetu.
Nadhani hii ilikuwa ndiyo sababu kwa wanawake kuvaa nywele ndefu, ambazo ni kwa
ajili ya kuwafunika na kuwalinda. Je, unaweza kunisaidia hili? Je, ni lazima
wanawake wajifunike vichwa vyao wanapoomba?
Jibu: Mwanamke yampasa kufunika tu kichwa chake anapoomba, iwapo kama ana nywele
fupi tu, kwa kuwa nywele zake ni utukufu wake. Yampasa kufunika kichwa chake
kwa kuwa yeye ni mtiifu kwa mumewe kwa ajili ya Malaika (1Wakorintho 11:10-15).
Nywele zake ni kifuniko chake. Na ndiyo maana ni aibu kwa mwanaume kuwa na nywele ndefu. Mwanamke anapaswa awe na nywele ndefu ili kujifunika, kwa hiyo, urefu wa nywele za mwanamke wapasa uwe ni zaidi ya nywele za mwanaume. Ni mwanaume tu ndiye anaruhusiwa kukata nywele zake. Kama mwanamke akkata nywele zake, basi itamlazimu afunike kichwa chake. Ndiyo maana kwamba ni aibu kwa mwanamke kuwa na nywele fupi au zilizonyolewa kipara, kama tulivyoshuhudia, kwa mfano, yaliyotukia mwishoni mwa vita ya Ufaransa.
Wagalatia
Ni nini maana ya andiko lililo kwenye Wagalatia
4:9-11?
Jibu: Ni mafundisho ya kizushi yalijitokeza kwenye makanisa ya Galatia na
Kolosai, na habari zake zimeelezwa kwa kina kwenye jarida la Mafundisho ya Kizushi Kwenye Kanisa la Mitume (Na. 89). Ilikuwa ni aina ya teolojia ya Kinostiki
iliyokuwa inashughulika na mambo kadhaa fulani na kufanya mambo sawasawa na
nyakati za mwanzo wa upagani. Waweza pia kusoka jarida la Uvegetariani na Biblia (Na. 183) na kwa mambo mengine
soma jarida la Nafsi Hai (Na 92) ili kujua tatizo lilitokana na nini.
Waabudu
Mashetatani na Wapigaramli au Wanajimu wanaoitumia kama kipimo cha kutabiri
maafa, na kumuinua mtu juu kuliko Mungu na kumfanya kama ni mungu wa nadharia
hii. Mafundisho ya Biblia yanakataza kufanya hivyo. Hatima yetu ni kufanyika
kuwa wana wa Mungu, na tunangojea ufufuo wa kwanza wa wafu ili tufanyike kuwa
wana wa Mungu wenye nguvu za Roho Mtakatifu, ili Mungu afanyike kuwa ni yote katika
yote na ndani ya yote (Waefeso 4:6). Tazama majarida ya Nafsi Hai (Na. 92); na Ufufuo wa Wafu (Na. 143).
Ni siku, miezi, nyakati na miaka gani ambayo
Wagalatia alikuwa wanaiadhimisha ambayo Mtume Paulo alikuwa anawaonya
wasiiadhimishe?
Jibu: Wagalatia 4:10 haiwezi kusomwa na kueleweka pasipo kwanza kujua kilichojiri
kwenye andiko lililotangulia ambalo ni Wagalatia 4:9 na aya nyinginezo. Desturi
za kutenda dhambi au udhaifu na kuombaomba zilikuwa ni kawaida kwenye imani ya
Wakostiki. Mafundisho ya kizushi ya Wakolosai yalitofautiana. Huko Galatia,
walikuwa wanalinganisha mambo ya ulimwengu. Maandiko yaliyo kwenye Wagalatia
hayana uhusiano wowote na mabishano au hoja zilizo kwenye Wakolosai 2:16 kuhusu
ushikaji wa sikukuu na Miandamo ya Mwezi Mpya na Sabato.
Kwa maneno
mengine, watu hawa walikuwa wanaamini elimu ya unajimu ili kujua la kufanya
kwenye siku na nyakati za mwaka na zilituama kwenye ishara. Walikuwa wanarudi
tena kuziamini ishara hizi. Hali hii iliwakumba waumini wa kanisa la Galatia.
Pazia la Hekalu la Herode lilikuwa na ishara zilizoshonewa kwalo (kwa kujibu wa
Josephus). Ushawishi wa imani ya Kinostiki kwenye Kanisa, umeelezewa kwenye
majarida ya Uvegetariani na Biblia (Na. 183); Wanikolai (Na. 202); na majarida mengine mengi yanayoelezea
Uungu, na pia jarida la Nafsi Hai (Na. 92).
Waefeso
Waefeso 3:15 inasema: "kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia
katika Kristo Yesu Bwana wetu." Kuna familia ngapi zilizoko
Mbinguni? Unaweza kunijulisha na kunifafanulia?
Jibu: Mungu aliiweka familia tangu mwanzo na waliitwa wana wa Mungu (soma Ayubu
1:6 na 2:1) na hata Shetani alikuwa ni mwana wa Mungu na kerubi mwenye mabawa
yafunikayo mtiwa mafuta.
Kwa kweli, Familia ni "ubaba". Huu ni mtazamo ambao kwao,
Kristo anauitwa “Baba wa milele” kwenye Isaya 9:6. Soma jarida la Isaya 9:6 (Na. 224) kwa maelezo zaidi. Muundo wa Familia ya Mungu umeandikwa kwenye jarida la Jinsi Mungu Alivyofanyika Kuwa Familia (Na. 187). Jarida la Stadi wa Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na
Omega (Na. 229) itakuonyesha vyeo vya Kristo kutokana na matendo yaliyo kwenye mapenzi ya
Mungu.
Wafilipi
Nimewasikia watu wakiitumia Wafilipi 2:10
“kuthibitisha” mtu anayepigamagoti “kanisani.” Je, andiko hili lina maana gani
hasa?
Jibu: Wafilipi 2:10 ni ahadi inayohusiana na kumuinua Kristo kutokana na utii
wake na kifo chake pale mtini. Hakupenda kujifanya kuwa sawa na Mungu bali
alijifanya kuwa si kitu na akauchukua mwili na hali ya kibinadamu kama
alivyoamriwa kufanya.
Kitendo cha
kupiga magoti wakati wa kuomba maombi kilitokana na imani ya ibada za
Baal-Easter, ambayo bado inafanyika. Kwa ajili hii, Mungu alijisazia watu
wasiopiga goti kwa Baali. Katika siku za Eliya, kulikuwa na watu takriban 7000
wakati nabii Eliya alipokuwa anadhani kuwa yuko peke yake.
Andiko hili
linaonyesha kuwa dini na imani yote ya ibada za Baali-Easter, ambayo inatuama
kwenye imani hii ya unyenyekevu, italetwa kwa Kristo na kufanywa iwezekane
kumjua yeye kuwa ni Bwana. Muundo wa uandishi umetuama kwenye neno “inama” kama
“kampto” (Warumi 11:4 sawa na Isaya 45:23; Warumi 14:11).
Vitu vya kuinama
kwa heshima: mbinguni (yaani jeshi la malaika, tazama Waefeso 3:10); vitu vya
duniani (yaani vya kidunia kama kwenye 1Wakorintho 15:40); vitu vilivyo chini
ya dunia (yaani wafu kwenye ufufuo wao, yaani aina zote mbili za Ufufuo (Ufunuo
20) sawa na Ufunuo 5:13 na malaika na mapepo (1Wakorintho 6:3 Luka 8:31; Ufunuo
9:11 na pia Zaburi 148.)
Badala ya kiumbe
huyu kuongezewa unyenyekevu, kumeahidiwa kwamba yeyote atakayetenda hivyo na
kutia uwezo wa Kishetani wa imani ya Baali-Easter ya waabudu jua na imani ya
waabudu mungu mke, watafanyika watubie dhambi na matendo yao kwenye ufufuowa
wafu.
Tazama majarida
ya Ufufuo wa Wafu (Na. 143); Nafsi Hai (Na. 92); Hukumu ya Mapepo (Na. 80); na Kondoo Aliyepotea na Mwana Mpotevu (Na. 199).
Suala la wajihi wa Kristo
limeandikwa kwa kina kwenye majarida ya Sheria na Amri ya Kwanza (Na. 253); Sheria na Amri ya Pili (Na.. 254); Sheria na Amri ya Tatu
(Na. 255); na Amri Iliyokuu ya Kwanza (Na. 252). Tazama pia jarida la Uwepo wa Yesu Kristo Kipindi cha Kabla ya Kuzaliwa Kwake Rasmi Duniani (Na.
243) na Stadi wa Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na Omega (Na. 229).
Wakolosai
Nadhani kuwa Wakolosai 2.14
imeweka hatua ya somo kwenye aya zinazofuatia … ‘akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya
kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena,
akaigongomea msalabani. Kwenye Wakolosai 2.13 Paulo anaongelea
kuhusu ubatizo badala ya tohara. Kisha kwenye 1Wakorintho 5:7… ‘Basi,
jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya’. Wakolosai 2.16 ‘Basi,
mtu asiwahukumu ninyi….’ Haipasi watu kunihukumu na wala Kristo hakufanya hivyo. Kwa hiyo, hakuna
mtu anayestahili kunihumu mimi kwa kile ninachokula au ninachokunywa, au kwa
ajili ya Siku Takatifu ninazozichagua kuziadhimisha. Namaanisha kwa kweli, zile
zinazomfanya mtu kama Mkristo hata hivyo?
Jibu: Kinachoelezewa kuwa kiligongomelewa pale
mtini kwenye Wakolosai 2:14 klikuwa ni “cheirographon” au hati ya mashitaka
unayopewa wakati unapokwenda mkahawani na kupewa bili ya chakula ulichokula.
Aligongomelea hiyo bili ya madeni yetu tuliyokosa kwa mujibu wa sheria kwenye
mti huu wa mateso, akatulipia kikamilifu madeni ya dhambi zetu mara moja kwa
wakati wote.
Siku Takatifu hazikufutwa kama tunavyoona kwenye maisha ya imani ya
Wanafunzi kwenye kitabu cha Matendo. Matendo 20:6 inaonyesha kuwa waliishika
sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. baads that thy a Idi ya Mikate Isiyotiwa
Chachu waliabiri kutoka Filipi. Kwa hiyo tunaona kwamba Paulo na Kanisa la
Filipi walizishika Sikukuu. Wkolosai 2:16 inaonyesha kuwa Wakolosai walizishika
pia. Matendo 20:7 inasema kuwa baada ya Sya Sabato au “mia ton Sabbaton” ambayo
kwa maana nyingine ni “Sabato ya Kwanza kati ya nyingi nyinginezo” na Bullinger
anasema hii kuwa ni Sabato kamili ya Kwanza ya Hesabu ya kuelekea idi ya
majuma, na sio Jumapili. Kwa hiyo tunaona pia kuwa waliishika Pentekoste,
ambayo tunathibitisha kuwa waliishika kutokana na inavyosema Matendo 2:1. Usemi
wa kwamba “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste,” kunamaanisha kuwa walikuwa wanazishika Sabato
iliyotangulia pia kama sehemu ya sikukuu hizi mbili. Tunajua kuwa waliishika
Siku ya Upatanisho na Sikukuu zingine zote za Mwezi wa Saba, kutokana na andiko
la Matendo 27:9, linaloonyesha ukweli kuhusu Siku ya Upatanisho.
Kwa hiyo, unasema, licha ya sisi kupewa Kalenda na Yesu Kristo, aliye
mwombezi na mtetezi wetu kwa Mungu, na licha ya kwamba yeye pamoja na Kanisa la
Agano Jipya kuwa lilishika; na licha ya Kanisa kuwa liliteswa kipindi chote cha
historia kwa sababu ya kuzishika sikukuu hizi; bali wewe bado utaamua
kutozishika idi hizo, na wala hutozishika Sheria za Mungu na wala
hutawafundisha watu kuzishika. Kwa kweli, Kristo aliweka wazi kabisa kwa
kinachotokea na kuwapata watu wanaofanya hivyo. Watahesabiwa kuwa si kitu
kwenye ufalme wa Mungu.
Je, Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kwa
kuwa hakuna namna au jinsi ya mimi kuzishika sheria, hivyo basi, iwapo kama
namwamini yeye yanipasaje kuzishika sheria? Kwani hakuzishika kwa ajili yangu
na kwa ajili ya mwingine yeyote amwaminiye?
Jibu: Hiyo ni ngano au hadithi ambayo waantinomia au wasiopenda kuzishika amri
wangependa uamini hivyo. Hilo ni fumbo kubwa na hadithi dunia zinazosema kuwa
sheria zimegongomelewa msalabani wanavyotumia kuitafsiri vibaya Wakolosai 2:14.
Kilichogongomelewa pale mtini ni Chierographon, ambayo ilikuwa ni hati ya
mashitaka chini ya sheria ambayo Kristo alitulipia na kwa njia ya neema
tunaweza kuishi kwa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu.
Hakuna nukta wala
kijoti chochote cha torati kitakachoondoka hadi mbingu na nchi itapita. Bado
iko na inadumu na itakuwa hivyo kwa kipindi kingine cha miaka mia elfu moja na
moja na ishirini na saba angalau, kama tulijuavyo neno la Mungu.
Wateule na
watakatifu ni “wale wazishikao amri za Mungu na ushuhuda (au imani) ya Wateule
na watakatifu ni “wale wazishikao amri za Mungu na ushuhuda (au imani) ya Yesu
Kristo" na ndiyo maana Yule joka anatukasirikia na anataka kutuangamiza
(Ufunuo 12:17; 14:12). Mlolongo wa majarida yafundishayo Torati yatakuhekimisha
zaidi. Soma jarida la Sheria za Mungu (Na. L1) na majarida mengine yote yanayofuatana
nalo yaliyoandikwa na yanapatikana.
Wakolosai 2:16: inasema
‘Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika… Siku; lakini Mwili ni wa Kristo.’ Na
Sabato zetu naongezea; ni vigumu sana kuyapuuzia mafundisho afundishayo mtu?
Jibu: Wakolosai 2:16 inaonyesha kuwa Kanisa lilikuwa linazishika Sabato,
Miandamo ya Mwezi Mpya na Siku Takatifu. Usemi wake wa kwamba basi mtu na
asiwahukumu unaonyesha kumaanisha kuwa unazishika basi. Kitabu cha Matendo
kinaonyesha wazi kuwa Kanisa lote lilikuwa linazishika sikukuu na Sabato na
hata Miandamo ya Mwezi Mpya. Tumekuwa tukzishika na kuadhimisha kwa kipindi cha
zaidi ya miaka 1,971. Waliishika Pentekoste, hinginevyo wasingeweza kumpokea
Roho Mtakatifu (Matendo 2:1). Injili imejaa maandiko yanayotaja ushikaji wa
sikukuu uliofanywa na Kristo na mitume wake. Hakuna hata andiko moja linalosema
kuwa waliacha kuzishika–hakuna hata moja. Mtume Paulo alizishika nah ii inaweza
kutafsiriwa kutoka kwenye maandiko yake mwenyewe (Matendo 12:3; 20:6).
1Wakorintho 5:7-8 inaelezea jinsi tunavyotakiwa kuishika Sikukuu ya Mikate
Isiyotiwa Chachu.
Kanisa lilishika
na kuiadhimisha Siku ya Upatanisho (Matendo 27:9). Huwezi kuuelewa mpango wa
Mungu pasipo kuzijua Siku Takatifu za Mungu. Kristo alikuwa ni Pasaka na Mganda
wa Kutikiswa. Alituamuru tuadhimishe ushirika wa Meza ya Bwana jioni ya siku
aliyosalitiwa, ambayo ni siku ya 14 Abibu.
Hakuna mahali
popote hata pamoja panapotaja kuwa Sabatp ilibadilishwa, au panapoliambia
Kanisa lisizishike Sabato, Miandamo ya Mwezi Mpya na Sikukuu zilizoamriwa
ikiwepo Wakolosai 2:16. Mtume Paulo anafanya masahihisho ya sadaka kwenye Siku
ya Kwanza ya juma kwa kuwa ingeweza kufanywa siku ya Sabato. Hapa ndipo mahala
pekee panapoonekana waliusanyika siku ya kwanza ya juma. Hata siku zenyewe
zimeitwa kuwa “Siku ya Kwanza ya juma” kwa kweli inamaanisha “Sabato ya kwanza”
kwa Kiyunani.
Tafadhali kinachosemwa
kwenye Wakolosai 2:18 kuhusu kitendo cha kuwaabudu malaika?
Jibu: Neno “kuabudu” linamaanisha “dini” kwenye
Matendo 26:5 na linajitokeza tu kwenye maeneo haya mawili tu. Ili kuelewa
mafundisho ya kizushi yaliyokuwa huko Galatia na Kolosai, mtu anahitaji kujua
au kuielewa dhana ya kidini kuhusu siku. Nadharia hizi zimeeleweshwa kwa kina
kwenye jarida la Mafundisho ya Kizushi Kwenye Kanisa la
Mitume (Na. 89). Upangiliaji wa utaratibu wa muda mrefu na mambo yanayoonekana kuwa ni
sehemu yake. Maneno na maana zake yapo kwenye maandiko yanayotajwa. Mumbe
hastahili kuabudiwa. Mtindo huu wa kuwaabudu malaika umeingia kwenye Ukristo
kwa kupitia mtindo au mbinu nyingine na watu hawafikirii kuabudu kitu kingine
zaidi kuliko ibada hizi za kuwaabudu malaika na watakatifu.
Je, unaweza kufafanua tafadhali kuhusu hii siri ya
Kristo inayotajwa kwenye Wakolosai 4:3?
Jibu: Siri ya Kristo iliyotajwa hapa ni ukombozi kwa Wamataifa na kufanyika kuwa
wana wa Mungu. Wale wasiokuwemo wanajumuisha moja kwa moja kwenye mchakato wa
kununuliwa nje ya harakati za kanisa linalotenda kazi likitumikia siri za
Kristo. Maandiko haya yanapatikana kwenye waraka kwa Wagalatia. wagalatia 3
inaonyesha kwamba kwa kupitia Ibrahimu mataifa yote yatabarikiwa na wamataifa
wanahesabiwa haki kwa njia ya imani na Maandiko yanasema kwamba wale walio na
imani ndiyo wana wa Ibrahimu (Wagalatia. 3:6-7).
Roho alimhubiria
injili Ibrahimu akisema kwa yeye mataifa yote watabarikiwa (Wagalatia 3:8-9).
Mtume Paulo anaichukulia “ergon nomou” au Miqsat Ma'ase ha Torah (MMT) (soma
jarida la Maandiko ya Matendo ya Sheria - au MMT (Na. 104)). Anawakumbushia andiko hili Wagalatia kuhusu suala la laana ya torati.
Hakuna anayehesabiwa haki kwa sheria, kama mwenyehaki anavyoishi kwa imani (Wagalatia
3: 11-12; Habakuki 2:4; sawa na Warumi 1:17; Waebrania 10:38).
Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa
ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti (Wagalatia 3:13; sawa na Kumukumbu la
Torati 21:23). Hii ilifantika ili kwamba Baraka za Ibrahimu ziwafikie Wamataifa
kwa njia ya Yesu Kristo na ili tumpokee Roho Mtakatifu kwa imani (Wagalatia
3:14).
Mtume Paulo
anaiendeleza hoja hii ili kukabiliana na mafundisho ya kizushi huko Galatia na pia
Kolosai. Soma jarida la Mafundisho ya Kizushi Kwenye Kanisa la Mitume (Na.
89). Kwenye Wagalatia 4:3 anaelezea kuhusu utumwa wetu tulionao kwa mambo ya
dunia. Anashughulikia mafundisho ya kizushi yaliyojipenyeza huko
Galatia. Anasema kuwa “Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma
Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi
awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa
wana. Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni
mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.” (Wagalatia 4:4-6).
Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u
mrithi kwa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. (Wagalatia 4:7). Kwenye Waefeso 5:14 Paulo
anaiainisha kwa kuifafanua Isaya 60:1-2 na anaongelea kuhusu nuru ilitolewa na
Kristo kwa kuwaamsha wale waliokufa. Anatumia maneno hayohayo yaliyo kwenye
Waefeso 5:16 kuhusu kuukomboa wakati kama tunavyoona kwenye Wagalatia 3:13 na Wakolosai
4:5. Akituonya tuenende kwa hekima kwa walio nje, na tukiukomboa wakati kwa
kuwa ni nyakati za uovu.
Anaongelea pia
kuhusu umuhimu wa kushukuru kwa kila jambo na kunyenyekeana na tukimcha Mungu.
Kwa hiyo, siri ya Kristo ni ukombozi kwa Mataifa kama wana wa Ibrahimu kwa njia
ya imani kwa Kanisa, na uwana wa Mungu kwa kupitia Kristo ambako ndiko kuvunjwa
kwa laana ya torati lakni ni kuwezesha kuanzishwa kwa vitu vyote kwa imani.
Yatupasa tuenende
kwa busara kwa njia ya imani tukishukuru kwa kila jambo na kunyenyekeana kwa
imani tukimcha Mungu. Kwa namna hiyo, kwa njia ya siri za Kristo, tunafania
kuwa wana wa Mungu aliyehai. Kwa kuwa imeandikwa: “Mimi nimesema, Ndinyi
miungu, Na wana wa Aliye juu...” na maandiko hayawezi kutanguka (Zaburi 82:6; Yohaa. 10:34-35).
II Wathesalonike
Kutokana na hali ya mtawangiko wa Kanisa,
unayaonaje Maandiko Matakatifu yaliyo kwenye IIWathessalonike 2:3-4, 6 kuhusu
huyu mtu wa kuasi “aketiye juu ya Hekalu la Mungu?” kwenye aya ya 6 ni kitu
gani hasa anachoambiwa kuwa “akijifanya yeye mwenyewe?”
Jibu: Ukengeufu Mkuu umekwishatokea kwa karne nyingi sana zilizopoita. Ulianzia
huko Roma na ukaendelea kuenea kwenye Makanisa yote ya Kikristo tangia karne ya
4. Ukengeufu huu unaoendana na kuiasi kweli umezidi kuendelea na kudumu.
Matokeo yake yakawa ni kutangazwa kwa amri ya kuwatesa watu wa Mungu waliokuwa
wanajaribu kuitii Torati ya Mungu kwa kipindi cha karne kadhaa.
Nyakaati za
mwisho zimetolewa rasmi kwenye dini na imani ya uwongo, mfumo utakaopelekea
kuwakomesheleambali Watakatifu wake Yeye Aliye juu. Ili kutimiliza hilo, karne
iliyopita walimtangaza Papa kuwa ni Mwakilishi au Mbadala (Vicar) wa Kristo na
Mungu hapa duniani. Yeye akiwa kama kiongozi wa dini na imani hii na mchakato
huu unaomtoa huyu mtu wa kuasi na mwana wa uharibifu, tunatarajia kuwa
ukengeufu ni budi uendelee na kuchukua mahali pake na kuwa ni mwisho wa zama ya
Washika Sabato, ambapo watakomeshelewa mbali na kukomesha nguvu yao.
Hii imeshuhudiwa
kufanyika kwenye miongo mitatu ya mwisho iliyopita kwa tukio lililojitokeza la
Kanisa lote zima la Mungu na matawi yake madogomadogo kujikuta wanakuwa
mawakala na watetezi wazuri wa imani zenye nasaba ya kipagani za Utatu na
Ubinitariani zilizo kwenye mchako wa kumuabudu Mungu wa Utati. Ni Makanisa na
vikundi vichache sana vilivyobakia vikiendelea kushikilia kwenye mafundisho
asilia ya Kanisa lililoanzishwa na Mitume. Ni machache sana pia yanayoendelea
kuzishika na kuzifundisha Sheria au Totati yake Mungu na kumfuata Kristo kwa
kumchukulia kama Malaika Mkuu wa Agano la Kale aliyempa Torati nabii Musa, kama
ilivyokuwa ikifundishwa kwenye Makanisa ya kipindi cha karne ya kwanza nay a
pili.
Mtume Paulo
anasema kwenye aya ya 7: “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi”. Mungu anaiachia hali hii itokee “hata
atakapoondolewa.” Kuna
aliyekuwako wakati huo na aliruhusiwa aendelee hadi mwisho na “ili aondolewe?”
Jibu lake laweza kuwa ni mmoja tu, ambaye ni mshitaki na adui Shetani. Siri ya
kuasi ni mkakati mkuu wa imani hii na hivyo kwamba kwa njia ya Dini potofu za
Imani Siri na fumbo, Shetani hutenda kazi ya ukengeufu na kuwadanganya
ikiwezekana hata wateule.
Kwa hiyo, Shetani
ndiye huyu anayeketi kwenye Hekalu la Mungu akijifanya yeye mwenyewe kuwa ni
“Mungu,” na kina mtumishi anayemfuata na kufundisha mafundisho ya kuadhimisha
sikukuu ya kipagani ya Easter ni “mtu wa kuasi” ambaye ni mwakilishi wa Shetani
ulimwenguni akiwa ni sehemu ya imani ya waabudu Jua. Ni watu wachache tu ndiyo
watakaomudu kubaki Kanisani katika siku za mwisho, wakimudu kufanya kazi na kueneza
kwa kuyagawa machapisho mbalimbali yenye mafundisho yenye uzima na injili ya
Ufalme wa Mungu.
Wakati wa
mchakato huu, ndipo marejesho mapya yatafanyika na kuongoka kwa watu wa Yuda na
wito wa watu waende Yerusalemu utaanza. Hadi wakati huo, itatupasa kujaribiwa
kama kwenye moto. Soma majarida ya Kuitwa Kwa Watu Kwenda Yerusalemu (Na. 238); Ujumbe wa Ufunuo 14 (Na. 270).
Kuna mambo mawili ambayo
yanauathiri pia mchakato huu nayo yameainishwa kwenye majarida ya: Maonyo ya Siku za Mwisho (Na. 44) na Jeshi la Gideoni na Siku za Mwisho (Na. 22).
1Timotheo
Andiko la 1Timotheo 4:1-3 linamaanisha nini
linapoongelea kuhusu mafundisho ya mashetani?
Jibu: mafundisho ya Mashetani yalichukuliwa kama Unostiki wakati ule wa kanisa
la kwanza. Walifundisha
uasetiki au maisha ya kujienga na anasa na useja. Mafundisho haya yameaishwa
kwenye majarida ya Uvegetariani na Biblia (Na. 183); Wanikolai (Na. 202); Mvinyo Kwenye Biblia (Na. 188); Nafsi Hai (Na. 92) na Mafundisho ya Mashetani ya Siku za Mwisho
(Na. 48).
Waebrania
Napenda kuelewa vizuri zaidi maana ya andiko la
Waebrania 7:3 lisemalo “hana
baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai
wake.” Mfalme huyu wa Salemu kwa hakika anaonekana
Mfalme wangu wa Yerusalemu!
Jibu: Ukuhani wa Melkizedeki ni ukuhani mpya na wa tofauti kwenye Kanisa uliojiri
baada ya ule wa Melkizedeki, uliohudumu tangu kipindi cha gharika kuu.
Umefunuliwa kwa Wamataifa na hivyo kwamba wanawekwa wakati wanapoongoka na
hivyo kuwafanya wawe washiriki/ “sanaa” na “ustadi” au “asiye na baba” wala
“mama.” Hivyo basi, si mrengo wa uzao wa kiumeni wala wa kikeni.
Mwanzo wake wa
siku na mwisho wa miaka ulikuwa unahitajika kwa kuhani. Sharti la kuingia
Hekaluni na kuanza kuhudumu akiwa na umri wa miaka 25 na kuacha kuhudumu akiwa
na umri wa miaka 50 ilikuwa ni sheria ya makuhani wa uzao wa Haruni, na
kufundisha tangu umri wa miaka 30 na kuendelea hadi kipindi cha kushindwa
kuendelea kuhudumu Hekaluni kwa kawaida kilikuwa ni umri wa miaka 65-70 au
zaidi kidogo ya hapo. Hata hivyo, hakuna kuhani aliyehudumu Hekaluni baaba ya
umri wa miaka 50.
Ukuhani wa
Melkizedeki ni tofauti na, isitoshe unawaweza kuwajumuisha wana wa Haruni
pamoja na Wamataifa. Ndiyo maana Ibrahimu alimwendea Melkizedeki huko
Yerusalemu. Huu ulikuwa ni mji wa Wayebusi na ulikuwa ni wa Wamataifa. Kwa
hiyo, Melkizedeki alikuwa na makuhani Wamataifa kwenye huduma yake. Tazama
jarida la Melkizedeki (Na. 128) for more information.
Yakobo
Unaweza kunifafanulia tafadhali chanzo na maana ya
waraka wa Yakobo.
Jibu: Mwandishi alikuwa yakobo, ndugu wa kimwili na Yesu Kristo na Mwenekiti wa
Baraza la Mitume. Hoja na malumbano kuhusu uandishi kuondoa kwa Luther kwa
Waraka (“wa”) ni kwa sababu ya ukali wa itikadi ya maadui wa Usemitiki na
kutangazwa kwa Sheria au Torati kuwa ni Sheria Kamilifu ya Uhuru.
Wote hujaribu
kuiondoa wanaposhikilia imani ya wapinga sheria za torati au uantinomia na
wapinga Usemitiki. Fundisho hili linafuatilia kwa ukaribu sana sauti au mdundo
wa kimafundisho wa Hotuba au Mafundisho ya Mlimani. Yakobo alikuwa ni ndugu
yake Bwana (Wagalatia 1:19), na ni mmoja wa nguzo muhimu kama inavyosema
Wagalatia 2:9. Alikuwa mwenyekiti na alitoa maamuzi kwenye Baraza ka Mitume
(kama ilivyo kwenye Matendo 15:13,19).
Wayahudi walikuwa
bado wanakusanyika kwa ibada zao kwenye masinagogi (2:2). “Maskini” (sawa na
Yohana 12:8) walikuwa warithi wa ufalme (kama kwenye 2:5). Walithibitika kwa
mujibu wa Torati na kumfanya Ibrahimu kama baba yao (2:8 ff., 21). Iuatiwa na
Matendo 3:19-21, kuhusu ujio au “parousia” ya Bwana ambao ulikuwa imekaribia
(5:7,8).
Umewalenga
makabila kumi na mbili yaliyokuwa kwenye utawanyko. Unadhaniwa sana kuwa
uliandikwa kutoka Yerusalemu si muda mrefu baada ya yaliyofanyika kwenye kitabu
cha Matendo, na huenda hata kabla ya kipindi cha Matendo ya Mitume. Yawezekana
sana kuwa ni mapema kabla ya kuuawa kwake mtume Yakobo mwaka 63 KK, ambako
kumeainishwa kwenye jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Tena wa
Hekalu (Na. 13).
Tunaweza kuona
kwamba matokeo ya ujumbe huu yananguvu sana kuhusiana na mambo yahusuyo imani
na matendo. Ni sawa tu na leo kama watu wanavyokuja kujikuta wakiangukia kwenye
ulaghai wa Uantinomia wa Kiprotestant na kujikuta wamekamatwa na mapokeo ya
Ukatoliki wa Kirumi, na kuanzia hapo tena kuangalia kwa kumaanisha Sheria za
Mungu.
Yakobo 1:17:
“Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu,
hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha
kugeuka-geuka..”
Ni kwa namna au jinsi gani inaposema kuwa wote
wenye mwili wataokolewa kwenye Maandiko kadhaa tofauti tofauti yanasema kwamba
wazinzi, wauaji na waabudu sanamu hawataurithi ufalme wa Mungu?
Jibu: Kwenye ufufuo wa pili wa wafu, watu wote watahukumiwa na watatubu.
Hakutakuwa na kuoa wala kuolewa kwenye ufufuo wa pili wa wafu. Watakatifu
wafanyao hivyo kwenye ufufuo wa kwanza watakuwa hawajafanya hivyo, vinginevyo
itawapasa watubu na kuacha kufanya hivyo.
Watu wote wengine watakuwa kwenye ufufuo wa
pili wa wafu. Huko watakuwa wamepewa kuelewa na kutubu au toba. Tazama majarida
ya: Ufufuo wa Wafu (Na. 143) na Hukumu ya Mapepo (Na. 80).
1Yohana
Kwa maana wako watatu
washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni
umoja. (1Yohana 5:7) andiko hili lina maana gani?
Jibu: Unanukuu maandiko yaliyokosewa na yanayopotosha kwenye 1Yohana 5:7 kwenye Receptus yaliyoingizwa kwenye tafsiri ya KJV. Hayapo kwenye Biblia yoyote nyingine. Ni mwingizo wa andiko la 1Yohana ili kutafuta msaada mwingine wa kbiblia kuhalalisha fundisho la Utatu. Waprotestanti wanadai kuwa misingi ya “Sola Scriptura” au kuamini “Maandiko Peke yake” na hivyo ukosefu au kutokuwepo kwa Utatu kwenye Biblia kulipasa kuwe na hali ya unafuu kiuhalalisho na Biblia na mapokeo ya kimaandiko.
Kwenye teolojia ya Kanisa Katoliki
ijulikanayo kama C. M. LaCugna (Mungu Kwa
Ajili Yetu) inafafanua jinsi imani hii ya Utatu wa Mungu ilivyoingizwa kwenye
teolojia ya kanisa tangu kwenye vikao vya Mabaraza ya Karne ya Nne huko Constantinople
mwaka 381. Augustine ndipo alipoutafakari uhusiano kwa kiwango cha mwingiliano
wa kimungu. Kanisa Katoliki la Roma linategemea maamuzi yanayotokana na vikao vya
Mabaraza ya kanisa nah ii haihitaji kuingizwa mambo ya kughushi yaliyoingizwa
kwenye Receptus ili kukithi haja ya kaulimbiu yao ya Sola Scriptura. Mchakato
huu umeainishwa kwenye jarida la Teolojia ya Mwanzoni ya Uungu (Na.
127).
Ufunuo
Najua
kwamba kitabu cha Ufunuo alipewa Mtakatifu Yohana Ufunuo, lakini huyu alikuwa
ni nani hasa kwa kweli?
Jibu: Kitabu cha Ufunuo ni Ufunuo hasa wa Mungu aliopewa Yesu Kristo. Yohana anasema kwamba aliuandika alipokuwa Patmo ukimbizini. Kristo alimpa alipoupokea kutoka kwa Mungu. Hili ni jambo la muhimu sana kuhusiana na suala la tabia ya Kujua kila jambo ya Mungu na utayari wa kujidhihirisha wa Mungu Baba yetu.
Inaonekana kuwa Yohana alikuwa ametupwa au kufungwa mwaka wa 96 wa kuinuka kwa mtawala au mfalme mpya. Eusebius anasema kuwa Yohana alirudi Efeso na kuishi hadi kipindi cha Trajan (H. E. III, 18.1; 20:9; 23:4). Appollonius anasema alimfufua mfu huko Efeso (Eusebius V, 18, 14).
Clement wa Alexandria anaeleza jinsi alivyomshuhudia na kumuongoa mnyang’anyi na kumleta kwa Kristo (Ni tajiri gani anayewezao ya kizushi Kuokolewa? 42). Irenaeus anaeleza jinsi alivyopingana na mafundisho ya kizushi ya Cerinthus (Her. III, 3, 4). Inasemekana kuwa alichukuliwa au kubebwa alipokuwa mzee, alirudia tena na tena kuwasihi watu akiwaambia kuwa: “Watoto wagodo pendaneni!”
Irenaeus alikuwa mwanafunzi wa moja kwa moja wa Polycarp na Papius, na walimpa taarifa za moja kwa moja akiwepo na kazi za Yohana huko Efeso na dini yake. Eusebius anasema kuwa Papius anasema kuwa yeye mwenyewe hakuwashuhudia mitume hawa kwa macho yake, bali alipata taarifa zao kutoka kwa marafiki zao (III, 39, 2). Kwa hiyo, Irenaeus alifundishwa na watu hawa pamoja na Polycarp akimpa habari za mkono wa kwanza za wanafunzi wengine. Hakuna mgongano kwenye taarifa hizi za Irenaeus.
Tertullian anasema kuwa Yohana alikwenda Roma na “alishindikana kuungua kwenye mafuta yaliyochemshwa moto na ndipo alihamishiwa Kisiwani.” (Patmo) (sawa na Kitabu cha Her, 36). Polycrates wa Efeso anasema kuwa Yohana alikuwa ni “kasisi alyekuwa anavaa joho lenye kimduara kama cha sahani” (Eusebius, Hist. V, 24, 3; cf. Interp. Dictionary of the Bible, John the Apostle, vol. 2, p. 954). Hii ilimfanya kuonekana kuwa Yohana ni mwana wa Lawi na ni Mkoheni.
Masalia yajulikanayo kama Muratorian Fragment (II, 9-23) yalisema kwamba Yohana alikuwa na mitume wengine waliobakia wakati Yohana alipopewa kuandika injili yake. Hii inamaanisha kwamba ilikuwa ni mapema sana kabla ya kuuawa kina Yakobo wa wenzake (yapata mwaka 63 BK) na huenda huko Palestina. Huenda ilikuwa hata kwenye Baraza la Mitume.
Desturi iliyotumiwa kujaribu kumuua Yohana inatikana na maandiko ya George Mdhambi (kwenye karne ya tisa) na nakala ya kwenye karne ya nane ya Historia ya Matukio ya kwenye karne ya tano yaliyoandikwa na Philip wa Side (Interp Dict. ibid). Hata hivyo, hii ni kinyume na jopo la mashahidi wengi wa zama za kwanza na Biblia inaashiria hakupasa kuuawa. Yohana aliandika vitabu vitano (Injili ya Yohana, Waaraka wa 1 hadi 3 wa Yohana na Ufunuo wa Yohana) kama zilivyo kwene mapokeo na desturi zilizokubaliwa.
Ignatius hamtaji yeye huko Efeso kama ilivyo kutokana na maandiko yake, kuna upotoshaji kiimani huko Roma kutoka kwenye teolojia ya kwanza ya mitume uliotuama na kumtafsiri vibaya Mtume Paulo. he Paulo. Hii ilikuwa ni kupotosha na hatimaye kuliharibu kabisa kanisa kwa ukengeufu.
Eusebius anashikilia kuamini kwamba Injili ya Yohana ni ya kwanza ingawaje zinaonekana kuwepo na zingine. Wanasema kuwa iliandikwa baada ya vitabu hivi vingine vitatu, na inasahihisha makosa ya kuruka ruka yaliyokuwa kwenye hizi tatu nyingine kuhusu miaka ya kwanza ya huduma ya Masihi. Ni Mathayo tu na Yohana ndio walikuw mitume wa mwanzoni.
Ni kwa
nini basi asili ya kibinadamu INATAKA kuamini kuwa tunaongoza migogoro iliyoko
ulimwenguni kote? Ni kwa nini kuna watu hapa duniani wanaonekana KUPENDA
kuamini kuwa uovu utakuja kushindwa na kusababisha matatizo na jehanamu, kwa
ujumla na kwa moja kwa moja? Kuna mtu alielezea ukweli kwamba kitabu cha Ufunuo
kiliandikwa kwa lengo la kumpinga kisiasa ya Nero na ukweli huo unabaki kuwa
ujuzi uliojikita mawazoni. Kwa nini wengine bado wanataka kuamini kuwa ni
unabii?
Jibu: Wazo la kwamba kitabu cha Ufunuo kiliandikwa u wanaojaribu kuupotosha ujumbe ulio kwenye kitabu hiki cha Ufunuo. Kwa kweli sio sahihi kabisa kama wanavyodai wengine. Yohana mwenyewe anasema kuwa alikiandika wakati akipokuwa kifungoni kwenye Kisiwa cha Patmo. Alifungwa huko mnamo mwaka 95 BK na alirudi kipindi cha utawala mwingine wa mfalme mwingine Nerva mwaka 96 BK.
Kanisa Lote zima lilikubali kuhusu kuinuka kwa utawala huo kuwa ni kweli. Nero alikuwa akwishakufa kwa miongo kadhaa. Harakati zilizo kwenye Ufunuo zinaelezea kinagaubaga utawala wa Kristo na watakatifu wake utakaodumu kwa kipindi cha miaka elfu moja. Kudai kwamba huu si unabii ni utotofu tu.
Mtu anaweza kujiuliza kwamba huenda si kitabu chenye unabii uliovuviwa au la, kama walivyofanya wengine. Hata hivyo, kudai kuwa hiki sio kitabu cha unabii inamaana kwamba mtu kama huyo hajayaisoma maandiko au anajaribu tu kuyaondoa idadi kubwa ya mahudhui yaliyomo ndani yake. Historia ya mahali pake kwenye kanoni imeainishwa kwenye jarida la Biblia (Na. 164). Unabii wake mwingi umekwisha timilika na dondoo zake. Sehemu kubwa nyingine ya unabii wake haijatimia. Kwa kweli andiko hili linahusu mambo yatakavyokuwa atakaporudi Masihi na kwamba jambo hilo halijatimia bado. Madai ya kwamba kinachukuliwa kama unabii na watu wanaoonekana kutaka kuona migogoro ikienea ulimwenguni kote hayafai kabisa.
Uandishi wenyewe unaelezea dhamira isiyotafsirika ya ulimwengu kwa zaidi ya kipindi kizima cha kuangamia kwake kabisa. Kazi hii ni ya muhimu kiunabii ya Biblia na ambayo haijafunuliwa bado kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu mbili. Kunakaribia sana tutajionea jinsi kazi ilivyo ya kweli. Ni Ufunuo ambao Mungu alimpa Yesu Kristo ambaye naye aliamini kuwapa watumishi wake kupitia kwa Yohana. Hakuna kiongozi wa Kanisa la Mungu kwenye karne ya pili aliyekichukulia kitabu hiki kama ni cha habari za kihistoria tu, na hakuna kiongozi wa Kanisa hata aliyejaribu kudai kudhania hivyo. Na wala hakuna aliyediriki kudai kuwa kilikuwa ni waraka kwa Nero. Katika miaka kumi ya mateso ya Kanisa kati ya miaka ya 303 na 313 ilijulikana wazi sana kwamba waraka kwa Wasymirna ulikuwa na maana.
Mungu anasema: “Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno
ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa
uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu
hiki.” Na hivyo ilivyoandikwa ndivyo itakavyokuwa.
Nimesoma
kwenye Ufunuo kuhusu roho saba za Mungu. Kutokana na hizo nadhania kwamba
pamoja na Mungu Mwenyezi, kwa sasa kunaweza kuwa na washirika sita wengine
kwenye baraza la elohim wanaoweza kuwa na vyeo va chini zaidi ya Mwenyezi
Mungu. Je, hii ni sahihi? (Ufunuo 1:4; 5:6)
Jibu: Roho saba za Mungu zimetajwa kwenye Ufunuo 1:4 na Ufunuo 5:6. Mtu anaweza
kudhania kwamba kuna viumbe saba kutokana na isemavyo Ufunuo 1:4, lakini andio
la kwenye 5:6 linaonyesha kuwa Mwanakondoo ana pembe saba na roho saba za
Mungu. Kwa hiyo hizi ni alama
au ishara za uweza na tabia ya Mungu.
Yapasa kuwe na misingi imara ya Roho Mtakatifu, inayofanya fursa ya
kuonyesha uweza wa kujua kila jambo kwa mpokeaji, kwa kadiri anavyotenda kwenye
Mapenzi ya Mungu kwa maongozi ya Roho Mtakatifu. Yapasaa kuwe na matendo ya
Roho Mtakatifu kwenye mnyumbuisho wa kazi ya Mungu hadi kwa jeshi la elohim.
Unaweza kuelezea hii “mana iliyofichwa” ni nini na
ni lini tutakapoyapokea majina mapya? (Ufunuo 2:17)
Jibu: Israeli walilishwa hii mana kwa kipindi cha miaka arobaini jangwani,
ambayo iliitwa ni chakula cha malaika. Neno Mana maana yake ni “ni kitu gani
hiki?” Neno hili lenyewe tu lilikuwa na maana yake fulani kama nieuwakilisho wa
kitu fulani kilichokuwa hakijajulikana kwa Waisraeli wakati wa tukio lao la
Kutoka.
“Mana liyofichwa”
ilimaanisha Roho Mtakatifu, ambaye alikuwa ni kifaa muhimu ambaye kwaye
tulifanyika kuwa wana wa Mungu na elohim. Walipewa wale wanaoshinda tu, peke
yao. Tulipewa malipo ya awali kwa tulipobatizwa, na tunapokea uweza kamili wa
Roho Mtakatifu kama wana wa Mungu wenye nguvu tutakapofufuka kwenye ufufuo wa
wafu (Warumi1:4).
Kanisa lilipewa
yubile arobaini kuwa kwenye jangwa la Kutoka. Lilikuwa ni jangwa la dhambi na
walilishwa mana walipokuwa wanatangatanga jangwani.
Jiwe jeupe lenye
jina jipya linaashiria mambo mawili. Mawe meupe yalitumiwa pia kwenye ujenzi wa
Hekalu kutoka kwenye misingi wyake. Jina lililoandikwa kwenye jiwe linamaanisha
uwenyewe kwenye Mji wa Mungu.
Hivyo basi
misingi ya ujenzi ni wale walioshinda wanaotokea kwenye makanisa hayo saba.
Watapokea uraia wao na watafanyika kuwa sehemu ya Hekalu la Mungu. Wataipokea
mana kutokana na ubatizo wao na kisha kwa uweza kwa kufufuka kwao toka kwa wafu
na wenyeji wao kamili kwenye Mji wa Mungu mwishoni mwa Ufufuo wa Pili wa wafu
baada ya kazi zao kufanika kwa kipindi chote cha utawala wa milenia wa Kristo.
Soma majarida ya: Ufufuo wa Wafu (Na. 143); Hukumu ya Mapepo (Na. 80); Milenia na Dhana ya Unyakuo (Na. 95); Mji wa Mungu (Na. 180); na Siku ya Bwana na Nyakati za Mwisho (Na. 192).
Je, jiwe jipya na jina jipya vina maana gani?
Jibu: Jiwe kama alama ya jina kwa maana ya
wenyeji au uraia kwenye ulimwengu wa kale. Lilitumika kutia alama raia na
liliashiria msimamo wao. Bullinger anasema kuwa jiwe jeupe lilikulikana siku za
kale kama jiwe la “ushindi” (lisemwalo kwenye Ufunuo 2:17). Mwendelezo wa kutenganisha ulikuwa ni kwa kuweka
chapa nyingi sana nyeusi dhini ya jina lililoorodheshwa. Alama nyingi sana
nyeusi na zilimaanisha utumwa. Majina ya watu yote yana msingi wa miungu ya
kipagani na ni vigumu kuyakwepa kwene jamii zetu. Wakati atakapokuja Masihi
dunia itapewa lugha mpya na nzuri na wateule watakuwa na majina mapya. Hii
itatimiliza unabii wa Isaya 62:2 na penginepo. Mawe mapya pia yanaunda sehemu
ya utaratibu wa ujezi wa Hekalu la Mungu.
Ni nani huyu mwanamke Yezebeli aliyetajwa kwenye
Ufunuo 2:20.
Jibu: Yezebeli alikuwa binti wa Ethbaali aliyekuwa mfalme wa Sidoni iliyokuwa
chini ya dola ya Watiro. Ethbaali alikuwa ndiye aliyemuua mfalme na mkatili
(Josephus A. Apion 1.18; A of J viii. 3. 1). Ethbaali alikuwa
kuhani wa mungu Astarte au Easter, mungumke wa dini ya Wafoinike. Jina lake
maana yake ya moja kwa moja ni “aliye pamoja na Baali.”
Yezebeli
(‘Iyzebel’ maana ya kihamasa) alikuwa kuhani mke wa Baali-Easter. Kwa hiyo
dhana ya “adhabu” hapa ni kumweka wakfu mungumke. Hakuwa vinginevyo bali ni
adhibu yenye utaratibu wa hekaluni. Israeli walikuwa kwenye ushirikiano au
ushirika na dini za Watiro na Wafoenike kutokana na urafiki wao na Daudi na
Hiramu. Imani na dini hii ya Easter ilijipenyeza katika Israeli kutoka kwa
Wafoenike, na ilifikia kilele chake chini ya Yezebeli ambapo Sheria na Torati
ya Mungu ilipuuzwa kabisa. Watu walijikita kwenye imani ya mungu Easter na
kumuabudu Baali na maashera. Manabii wa Mungu walitishwa kwa dharau.
Easter ni sehemu
ya imani ya zamani za kale ya ibada za mungu Baali na haitofautiani na imani za
Siri na fumbo. Tazama pia kwenye jarida la Ndama wa Dhahabu (Na. 222). Wafoinike waliichukulia hii ulimwenguni
kote kwenye taratibu zao za kibiashara.
Kwa mujibu wa
Maandiko Matakatifu, Biblia inamashiko, lakini uelewa wetu unakikomo, na
mapenzi halisi yatatupeleka mbali. Kristo anatuita tuishi kwa imani na kumuamini yeye na kupendana.
Hakutuamuru kabisa kuyafanya Maandiko yote Matakatifu kuwa sawa. Kwa kweli,
aliwakemea watu waliokuwa wanadini sana wanaojifunza Maandiko Matakatifu ya
siku zake ya kutokuwa sahihi kwenye tafsiri zao.
Kwa upande
mwingine, Mungu aliivuvia Biblia, inajumuisha kweli yote. Wale wanaomwamini
watapenda kulielewa Neno lake, na kuyafuata mafundisho yake ili wawe wazuri
iwezekanavyo. Yatupasa tu kujua ukomo wa uwezo wetu, haitupasi, kwa namna
yoyote ile, kutazama chini tukwaangalia wale wasioonekana kuyaelewa Maandiko
Matakatifu pamoja na yale tunayoyadbania kuwa tunayafanya. Hebu na tuishi kwa
imani na tuonyeshe pendo kila mmoja wetu.
Liana maana gani neno hili la kwamba "Nitampa
nyota ya asubuhi"? (Kwenye Ufunuo 2:28)
Jibu: Nyota ndogo ya Asubuhi ni daraj la cheo. Kulikuwapo na nyota wengi wa
Asubuhi waliokuwepo wakati wa uumbaji wa Dunia kama tuonavyo kwenye Ayubu
38:4-7. Jina la Lusifeli linahusiana na cheo hiki. Neno ndogo linachukuliwa
kuwa la mungu wa ulimwengu hu. Siku hizi Shetani ni Lusifeli na Nyota ya
Asubuhi.
Huyu mdogo
anaweza kuchukuliwa kutoka kwake na akapewa Kristo atakaporudi. Yeye kama mteule
atapewa cheo cha kutawala na Kristo. Kwa maneno mengine, wateule
watashirikishwa kwenye Utawala wa Mungu hapa duniani kipindi cha Milenia na
hata baad ya hapo. Jambo hili limeainishwa kwa kina kwenye majarida ya: Lusifa: Mpeleka Nuru na Nyota ya Asubuhi (Na. 223); na Utawala wa Mungu (Na. 174). Pia soma jarida la Jinsi Mungu Alivyofanyika kuwa Familia (Na. 187).
Ni kiumbe gani basi anayetajwa kwenye Ufunuo 3:7
kuhusu ufunguo wa Daudi? Je, inahusiana na Isaya 22:22?
Jibu: Ndiyo, uko sahihi. Ufunguo wa mwongozo wa ufalme wa Israeli ulifikia
kilele chake chini ya Daudi na kufikia upeo wake kamili. Tendo lenyewe lilikuwa
pia ni kuingia kwenye maskani lilijumuishwa kwenye mamlaka haya ya mfalme.
Sulemani, kwa
mujibu wa mapokeo ya Kiyahudi, alikuwa na unfunguo wa Hekalu. Soma kwenye
jarida la Wimbo Uliobora (Na. 145). Andiko lililo kwenye Isaya 22:22
linaonyesha kuwa uweza wote wa kifalme alipewa Masihi. Andiko lililo kwenye
Ufunuo linaonyesha kuwa alikuwa na uweza huu na alitumia mamlaka yake
kuliwezesha liwepo kanisa la Wafiladefia, kwenye Ufunuo, nguzo za Hekalu.
Anawapa mlango uliofunguliwa wazi ili kuimaliza kazi kwenye siku au nyakati za
mwisho. Andiko hili linaonyesha pia kuwa Wafiladefia ni Nguzo zinazolisimamisha
Hekalu, tulimo sisi sote leo. Zimesimama kwenye mawe ya msingi ya Mitume na
Yesu Kristo akiwa ni Jiwe Kuu la Pembeni lililo kwenye mwamba ambao ni Mungu.
Tazama pia kwenye jarida la Mji wa Mungu (Na. 180).
Ina maana gani kwa kusema kwamba "Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika
hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake
jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya,
ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu (Yesu) mwenyewe, lile
jipya."? (Ufunuo 3:12)
Jibu: Andiko la Ufunuo 3:12 halisemi jina jipya la Mungu. Bali andiko linasema:
"Nitaandika juu yake jina la Mungu wangu." Munbu ana majina, matumizi ya kila
jina moja yanaendana na hali halisi ya kimamlaka. Akiwa Eloah, anaonyesha kuwa
yeye ni wapekee na ni Mungu wa Kweli. Anapolitumia jina la Ha Elohim anaonesha
kuwa ni muumbaji, yaani Mungu muumbaji, aliyeanza na elohim.
Kwa hiyo, wana wa Mungu wote ni alohim ai
theoi. Yeye ni Yahova wa Majeshi na wote watumikao pamoja naye wanaliitia jina
la Yahova. Na ndiyo maana kla mmoja wa malaika kwenye Agano la Kale wakati wote
aliitwa Yahova. Yeye ni Yehovih au Elyon, Liye Juu Sana na “Anayesababisha
Kuwepo kwake” wa Kutoka 3:14. Mji huu ni Yerusalemu Mpya, ulio juu na ni mama yetu sisi sote. Ushukao toka mbinguni kwa Mungu. Soma
jarida la Mji wa Mungu (Na. 180).
Eloah hana jina
jipya. Ni Kristi ndiye mwenye jina jip-ya. Sisi tu elohimu kama Malaika wa
Yahova atutanguliaye (Zekaria 12:8). Sisi ni miungu (elohim na theoi) na
Maandiko hayatanguki. Kristo amepewa jina jipya nasi tutakuwa na jina hilo
jipya limeandikwa kwenye vipaji vya nyuso zetu na tutamtumikia Kristo na Mungu
kwa uweza. Soma pia jarida la Uwepo wa Yesu Kristo Hata Kabla ya Kuzaliwa Kwake
Hapa Duniani (Na. 243).
Ni nani huhu anayeketi
kwenye kiti cha enzi cheupe na hiki ni kipindi gani? (Ufunuo 6:2)
Jibu: Kiti cha Enzi Kikubwa Cheupe kinaonekana
kwenye Ufunuo 4:2-6. Utawala wa mwisho wa Milenia sasa utakuwa umefikia kikomo
kwenye Ufufuo wa Pili wa Wafu ambapo Kristo atashirikiana utawala na mamlaka
yake na Mungu naye atapewa mamlaka ya Kuukumu ulimwengu wote kwenye kipindi
chote cha miaka 100. Hiki ni kipindi cha Ufufuo wa Pili wa Wafu, wa baada ya
kupindi cha utawala wa Milenia wa Kristo na Watakatifu. Roho Mtakatifu ametumwa
kutoka kwa Mungu na kwa uweza huo ndipo Ufufuo unafanyika na Hukumu ya watu
itafanyika. Sayari nzima yote itatengamaa kipindi hiki.
Mwishoni mwa miaka 100, watakatifu watakuwa kwenye umoja na mwelekeo wa
pamoja na kuwa kama Mji wa Mungu. Soma majarida ya Ufufuo wa Wafu (Na. 143); Milenia na Dhana ya Unyakuo (Na. 95) na Mji wa Mungu (Na. 180). Isaya 65:25 inasema: “‘Mbwa-mwitu na
mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng'ombe; na mavumbi
yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu
mtakatifu wote, asema Bwana.”
Ufunuo 6:12-17 inasema:
Nami nikaona,
alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi
kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, na nyota zikaanguka juu ya nchi
kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. Mbingu
zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa
kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri,
na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini
ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini,
mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye
kusimama?
Unadhani huu kuwa ni unabii?
Inaweza hii kuwa ndiyo iliyosababisha au chanzo cha kundi la vilimia hapa
duniani?
Jibu: Ndiyo, huu mhuri wa sita unaashiria
mlolongo wa matukio ya ishara za mbinguni zilizosababishwa na muingiliano wa
hali ya halisi ya hwa ulimwenguni, ina inawezekana kusababishwa na silaha
zinazotoka kwenye vituo mbalimbali vya angani. Kile kinachokitangaza ni ujio wa
Masihi. Wafalme wa duniani wanamashaka kwa kilichosemwa na manabii katika siku
za mwisho kama ni kweli kwamba: Masihi amekuja na kwamba watakabiliwa na
ghadhabu yake.
Mfano wa kondoo na mbuzi unakuambia unachopaswa kutegemea.kama
walivyowahukumu watakatifu ndivyo watakavyohukumiwa na wao. Jambo hili limepembuliwa kwa kina kwene
majarida ya Mihuri Saba (Na. 140); Baragumu Saba (Na. 141); Kuanguka Kwa Yeriko (Na. 142) na Baragumu (Na. 136).
Hawa farasi weupe na uta vinawakilisha nini?
Jibu: Ufunuo 6:2 inataja farasi
mweupe na uta. Farasi mweupe anaonekana kuwa ni mmoja anayefanana na
mwanakondoo lakini ni dini au imani au utawala unaoshinda ambao ni uta (toxon).
Kiumbe huyu si Masihi na huyu farasi mweupe na anayempanda kwenye Ufunuo 19:11.
Huyu anayempanda
ni taswira au anawakilisha dini ya uwongo inayotenda kazi kwa kibali na jina la
huyu ampandaye lakini ni mwongo na washindaji walio sambamba na imani au dini
ya uwongo. Kutokana na mpandaji huyu, kunatokea vita, na kisha magonjwa mabaya
kama tauni na ukame, na hatimaye kufa kwa mpanda farasi mwingine. Huu ulikuwa
ni mfumo au dini iliyokuwa imeandaliwa na kuwekwa wakati dini ya uwongo
ilipowekwa hada duniani na Shetani nab ado inatawala hapa duniani. Soma
majarida ya Upembuzi Kuhusu Ratiba ya Nyakati (Na. 272) na pia linguine la Mihuri Saba (Na. 140) na Baragumu Saba (Na. 141).
Huyu farasi mkali mwekundu mwenye upanga mkubwa
vinawakilisha nini na vina umuhimu gani? (Ufunuo 6:4)
Jibu: Farasi Mwekundu anamaanisha vita. Huu ni mgogoro uliowahi kuipata dunia
kama matokeo ya migawanyiko yake iliyosababishwa na dini ya uwongo. Upanga huu
ni upanga wa vita na wenye kugawanya. Yakwanza inataingulia ya pili nay a pili
inafuatiwa na ya tatu nayo inafuatiwa na ya nne. Tazama jarida la Mihuri Saba (Na. 140).
Je, huyu farasi mweusi anawakilisha nini na jozi
ya mizani inamaana gani na vina maana gani? (Ufunuo 6:5)
Jibu: Farasi mweusi ni ukame, tauni na magonjwa. Mizani au uwiano vinamaanisha
hukumu na uhaba wa vitu farasi wawili na
gharama au thamani ya wapanda farasi wa kwanza. Kipimo kimetolewa sawasawa na
jinsi wanavyopimwa. Mafuta na mvinyo vinawakilisha watakatifu wenye Roho
Mtakatifu waliotawanyika kwenye mataifa mbalimbali. Wanaweza kuuawa kama
mashahidi wa imani lakini msingi muhimu wa kudumu na uadilifu wa kanisa
vitalindwa na dunia yenyewe haitaweza kukumbwa na madhara hadi wale 144,000
watakapokuwa wamekwishatiwa mhuri na kundi kubwa likiwa limemalizika tayari.
Je, huyu farasi wa kijivujivu na jina la mauti
vina maana gani? (Ufunuo 6:8)
Jibu: Farasi wa kijivu aliye kwenye Ufunuo 6:8 ni mauti na kuzimuni
vinavyofuatiwa na machafuko yatakayojitokeza na kufanywa na Mpanda farasi
aliyepita wa Dini ya Uwongo, Vita, na Magonjwa au Tauni isiyokoma na baa kuu la
Njaa vilivyosababishwa na huyu Farasi Mweusi.
Haya mauti na
vifo ni hukumu dhidi ya wakazi wa duniani wanaoifuata dini hii ya uwongo na
wakaenda kwenye ufufuo wa pili na kisha kukabiliwa na mauti ya pili. Tazama majarida ya Mihuri Saba (Na. 140); Baragumu Saba (Na. 141); Ufufuo wa Wafu (Na. 143); na Milenia na Dhana ya Unyakuo (Na. 95).
Unaweza kunielewesha maana ya dhiki kuu
itakayowakumba watakatifu iliyoandikwa kwenye kitabu cha Ufunuo na watatoka
wapi? (Ufunuo 7:14) Pia nilisikia ikisemwa kwamba kutakujakuwa na miaka 7 ya
dhiki kuu katika siku za mwisho. Itatokea wapi?
Jibu: Biblia inataja aina tatu za dhiki kuu. Moja wapo ni ile ya siku 1,260
iliyotajwa kuwa ni ya mwanamke kuwa jangwani, ambapo joka atakuwa anamfuatilia
na nchi itamsaidia na kummeza huyo joka. Hii ni miaka 1,260 au siku za kinabii
za kudumu kwa iliyojiita kuwa Dola Takatifu ya Roma iliyodumu tangu mwaka 590
hadi 1850. Katika kipindi hiki, mamilioni ya Watakatifu wengi waliuawa na
Kanisa la Ukristo unaoshadidia imani na maadhimisho ya Easter na washika
Jumapili wa Ulaya. Tazama
jarida la Kazi ya Amri ya Nne ya Mungu Kwenye Historia ya Makanisa ya Mungu ya
Washika Sabato (Na. 170).
Biblia pia
inaitaja shiki kuu nyingine ya wakati wa kufunguliwa kwa Mmhuri wa Tano ambapo
watakatifu waliambiwa wasubiri hadi itimie idadi ya ndugu zao waliouawa kama
walivyouawa hao wenyewe. Mateso ya dhiki hii yameanza rasmi tangu kipindi cha
Vita Kuu ya I ya Dunia na yaliendelea hadi kifo cha Stalin mwaka 1956. Watu
wengi waliuawa na makanisa ya Kilutheri na Roma kwa kuwatumia Manazi wa Ulaya.
Inakisiwa kuwa walikuwa takriban waumini milioni 18 miongoni mwao. Hatutaweza
kuijua idadi kamili, ila waliuwa kwenye makambi ya mateso yapatayo takriban
15,000 na kwenye kambi za mauaji zilizoandaliwa sehemu zote za Ulaya.
Tuna tarifa rasmi
ya idadi ya kambi hizi kuwa zilikuwa ni zaidi ya elfu kumi kumi na idadi
tuliyonayo inaashiria kuwa ni zaidi ya kambi 15,000. Katika siku za mwisho,
kutakuwa na Dhiki Kuu baada ya kurudi kwake Masihi atakayekuja kuliokoa Kanisa.
Dhiki hii Kuu ya mwisho ni maafa yatakayofanywa na mwanadamu, ambayo yanaweza
kuzuiwa au kuepushwa kwa njia ya toba. Habari hii imeelezewa kwa kina kwenye
majarida ya Mihuri Saba (Na. 140); Baragumu Saba (Na. 141); pia na
Kuanguka kwa Yeriko (Na. 142).
Je, kuna uhusiano wowote ule kati ya Ufunuo 8:10
ambapo nyota inaitwa kuwa ni pakanga iliyosababisha 1/3 ya viumbe walioko
majini kufa (kwa uchungu), na Kutoka 15:25, wakati Israeli walipofika Mara
(ambayo maana yake ni uchungu pia) na maji ya huko yalikuwa machungu hadi
ulipotiwa mti ndani yake yakawa matamu? Je, andiko hili la Ufunuo 8:10
livhukuliwe kwa tafsiri ya moja kwa moja kama lilivyo, au kama kimafumbo, au
kama kinadharia tu inayoweza kutafsiriwa kwa namna zote mbili. Najua kwamba,
mara nyingi, matukio ya kimwili yanapelekea utimilifu wa matukio au maana ya
kiroho. Je, hiki ndicho tunachojionea hapa kuhusu maji machungu?
Jibu: Ni mtazamo wetu kwamba tafsiri na mtazamo huu ni sahihi. Maji ya huko Mara
yalikuwa machungu. Mti ambao ulikuwa ni Kristo, ulitiwa ndani yake ili kuyafana
yaondokane na uchungu. Huku ni kuzaliwa ambako ukweli wake ni kwamba Yesu
Kristo anachukuliwa kitaswira kama mtende ulio katikati ya mtu mpya mwenye
kichwa cha mwanadamu na Yule mwenye kichwa cha simba ambaye ni Kerubi wa kwenye
Hekalu la Mungu lililo kwenye kitabu cha nabii Ezekieli.
Dunia itakujakuwa
haifai na Kristo atarudi ili kuja kuikoa. Maji mapya yatakuwa yakitoka kwenye
Mlima wa Hekalu na kuwafanya samaki na viumbe wengine waishio. Tazama jarida la Pentekoste ya Sinai (Na. 115).
Ole hizi ni za nini na ni
lini hawa Mashahidi watakapo kuja?
Jibu: Ufunuo sura ya 9 inaelezea kuhusu Baragumu ya Tano nay a
Sita, ambazo ni Ole ya Kwanza nay a Pili. Ole ya Pili inaendelea mbele kwenye
kipindi chote kilicho kwenye Sura za 10 na 11.
Ufunuo sura ya 10 inaelezea kipindi cha mpito kati ya
baragumu ya Sita nay a Saba. Huyu ni Malaika mwenye Gombo dogo au Injili. Huu
ni ujumbe wa Baragumu ya Saba. Ni kwenye kipindi hiki ndipo siri za Mungu
zitakamilika au zitafunuliwa kikamilifu. Tukio hili na kurejeshwa kwa maongozi
ya Torati ni budi litawatangulia watakatifu. Baragumu ya Sita na vita vya
Baragumu ya Tano nay a Sita zimepita. Ni kwa mwingiliano huu ndipo tunachukua
awamu ya mwisho ya Kupimwa kwa Hekalu na ndipo siku 1260 za Mashahidi na
kipindi chake cha miaka mitatu na nusu mitaani. Kitendo cha kuzirejesha Sheria
za Mungu na Upimaji wa Hekalu vitafanyika pamoja sambamba (soma jarida la Upimaji wa Hekalu (Na. 137).
Mwishoni mwa kipindi hiki ambacho Malaika wa Saba atapiga baragumu na ndipo
ufufu wa wafu utafanyika. Baragumu la Saba kwenye vitasa Saba vya Ghadhabu ya
Mungu. Kwenye Baragumu hii anaanza kutawala. Kristo hapa kwenye hatua hii
kwenye wasaa maalumu wa Ufufuo wa wafu. Hii inaanzia kwenye mashahidi wawili.
Mhuri ulifunguliwa wazi muda mrefu uliopita na unaendelea.
Kwenye Ufunuo 13:18, kunasema kwamba tarakimu ya
Mnyama ni ya kibinadamu, na jumla yake ni 666. Nimejitahidi kusoma majarida na maandiko
mbalimbali ya kanisa la SDA na yanasema kwamba tarakimu ya mtu huyu ni ya papa,
ambayo ni Vicarius=112 Fil II=53 Dei=501 = 666. Unaichukuliaje tafsiri hii?
Ulisema kwamba ni wa kidini, lakini kitabu cha Ufunuo hakisemi kuwa ni namba ya
mwanadamu. Hii inafanya mashiko kwangu kujua kwamba huenda papa ni kiongozi wa
dini na mfumo huu unaompinga Mungu.
Jibu: Kiongozi wa mfumo wa kidini wa ulimwengu, ulio kwenye mbobeo wa kuabudu
jua na dini nyingThe head of tne za uwongo, ndiye mtu huyu. Dini yote na mfumo wake una nembo au alama
yake. Wanaabudu siku ya jua, na ina fundisho la Mpinga Kristo. Inaamini mungu
wa Utatu wa dini ya Baal-Easter na Ndama wa Dhahabu ilikuwa ndiyo dini yake ya
mwanzoni. Soma majarida ya Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235); Ndama wa Dhahabu (Na. 222); Fundisho la Dhambi ya Asili Sehemu ya I Bustani ya Edeni (Na. 246).
Hakuna watarajiwa
wengi wenye heshima ya namna kuwili wa kuwa ni viongozi wa imani na dini hii.
Ukweli kwamba wadhifa ay cheo unachokiongelea cha kipekee hadi kufikia tarakimu
hii ya 666 tu unashinikiza tatizo au hitimii ule wa sheria za Mungu ulio kwenye
mioyo na mikononi kwa matendo. Mambo haya yameainishwa kwenye jarida la lililo
kwenye mlolongo wa majarida ya Torati au Sheria za Mungu (Na. L1).
Imani ya SDA
inajaribu kuitafsiri alama hii ya kidini kwa kuifananisha na kitendo cha
kuipinga Sabato na huku wakiipuuzia Kalenda yote ya Mungu, ambayo
hawakuruhusiwa kuishika. Soma
pia kwenye majarida ya Torati na Amri ya Nne (Na. 256).
Pia soma jarida la Alama ya Mnyama (Na. 25).
Familia yangu na mimi tumefanya utafiti kuhusu hawa 144,000 waliotajwa kwenye kitabu hiki cha Ufunuo. Tumekuta vyanzo kadhaa vinavyofundisha kwamba hawa 144,000 watakuwa ni wale kipindi cha Kristo na hadi kwenye nyakati za mwisho, wakati vyanzo vingine vimesema kuwa hawa 144,000 ni wa kutoka wakati wa uumbaji hadi nyakati za mwisho. Je, unaweza kutoa maonre from the time yako kuhusu jambo hili? (Ufunuo sura ya 14)
Jibu: Mafundisho kuhusu watu hawa 144,000 limeainishwa kwenye jarida la Mavuno ya Mungu, Dhabihu ya Mwezi
Mpya na Wale 144,000 (Na. 120). Hawa 144,000 wantokana na vipindi vya
Mababa, Manabii, Waamuzi, Daudi na huenda Sulemani na viongozi wengine wakuu wa
Israeli hadi karibu na mwanzo wa Agano Jipya. Kwa hiyo, Kanisa lilitumika kama
chanzo cha kwanza kutoka kwa Kristo, na alama wazilizozitumia zimeelezewa kwa
kina zote kwenye majarida. Hutaweza kuzijua kikamilifu hadi utakapolielewa
jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 156).
Tatakimu hii imejumuishwa na baraza au halmashauri ya Mungu, au Sanhedrin lene wajumbe 72, ambalo lilihamishiwa kanisani (Luka 10:1,17). Sabato Miandamo ya Mwezi Mpya, na Makusanyiko ya Mungu, yote yanajumuishaa wajumbe 72, na kwa zaidi ya miaka 2000 vinafanya kuwe na jumla ya watu 144,000. Kipindi kifupi na tata ni kile cha Shetani na cha Ujio wa Masihi kilichofanywa na Mababa pamoja na Manabii, na kufanya jumla ya hawa 144,000. Mkutano huu makubwa ni masalia ya kanisa, wanaoiwakilisha sadaka au dhabihu ya jioni. Dhabihu ya Asubuhi iliyo kwenye Hekalu la Ezekieli, inawakilisha kipindi na utawala wa milenia.
Tunavijuaje
vigezo vya kukubaliwa kwa hawa 144,000?
Jibu: Ni Mungu tu ndiye anayewajua hawa ni kina nani na ndiye anayempa Kristo watu hawa, lakini hawajajulikana wala kutambulishwa na hata wenyewe hawajijui hadi kwenye kipindi cha marejesho mapya ma mwisho na ufufuo wa kwanza wa wafu. Dunia haitadhurika hadi atakapokuwa ametiwa mhuri mtu wa mwisho kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu kwenye mwili wa Kristo, kwa jina la Mungu.
Ni
nani anayetajwa au kukusudiwa kwenye Biblia inapomtaja kwenye Ufunuo kinapotaja
kuhusu Babeli Mkuu, Mama wa Makahaba na machukizo ya nchi? (Ufunuo 17:5) Nineshangazwa
kila mara kuhusu aliyekuwa anakusudiwa kuongelewa hapa.
Jibu: Inaongelea kuhusu imani na mfumo wa dini kubwa uliojifunganisha kwenye mfumo wa dini ya Kibabeloni inayofungamana na waabudu mungu Sin ambaye ni mungu Mwezi na walio kwenye dini ya mungu Istar au Easter pia kama anavyojulikana kwenye kugha ya Kiingereza. Kwa Waisraeli wa zamani alijulikana kama mwenzi wa Ashtoreth na wa Baali na kwenye dini siri alijulikana kama Isis kwa Wamisri na Venus kwa Warumi.
Mungu mfu alikuwa ndiye mlengwa kwenye dini
hii potofu kama ilivyokuwa kwene maadhimisho yake ya sikukuu ya Easter. Alikuwa
pia ni mama wa mungumke na dini yake imeenea ulimwenguni kote. Na ndiyo maana
anaitwa mama wa makahaba kwa kuwa ana dini yake inayoshughulika na kujitia
unajisi yenyewe kwa kutumia nguvu za dola na za kisiasa na makuhani wake
wanazini na wafalme wa dunia. Imani na dini hii imechambuliwa kwa kina kwenye
majarida ya Ndama wa Dhahabu (Na. 222) na
pia kwenye Chimbuko la Krismas na Easter (Na.
235).
Nina maswali 3: 1. Ufunuo 20:10 inasema: “Nao watateswa mchana na usiku hata milele na
milele”. Ni nani huyu anayetajwa hapa? 2. Je, Ufunuo 20:15 inamtaja mwanadamu pia? Unawezaje
usionekane kwenye kitabu cha uzima? 3. Andiko la Ufunuo 21:8 lina maana gani?
Jibu: Soma majarida ya Hukumu ya Mapepo (Na. 80), Ufufuo wa Wafu (Na. 143); na pia Mji wa Mungu (Na. 180). Jibu la swali hilo linakutikana kwenye sehemu ya
mwisho ya swali lako. Ufunuo 21:8 inasema kuwa, “Bali waoga, na
wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo
sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na
kiberiti. Hii ndiyo Mauti ya Pili.”
Kwahiyo, ni mauti ya pili, na sio hukumu ya milele. Waovu na watenda dhambi
wanatakiwa watubu na hukumu ya pili ya kurekebishwa inahusika na watu hawa.
Kila atakayebakia kuwa mtenda dhambi atakufa na kuteketezwa kwa moto. Neno
lililotumika kwenye Ufunuo 20:10 linamaanisha kuwa “watateswa,”
(basanisthesontai) limetuama kwenye neno linalomaanisha “kuipinga kweli kwa
uovu” na “kuondolewa mbali”. Na “kwenye ukamilifu wa dahari” inamaana ya
“milele na milele.” Mnyama ni nadharia na mfumo wa utawala, na sio kiumbe
binafsi.
Shetani ni roho. Ni “nabii mke wa uwongo au bandia” ni unabii wa uwongo na
ni mfumo kwa ujumla, na sio ni nabii fulani binafsi wa uwongo. Ziwa la Moto ni
“Puros” na “Theiou.” Huu sio moto wa kibiriti tuujuao. Puros ni kitu
“kinachong’aa kama moto.” Neno “kibiriti” lililotumiwa hapa ni “Theiou.” Neno
lwenyewe linaashiria “umbinguni.” Kwa hiyo, ni kama Ziwa kali na la hukumu
(soma Thayers Lexicon). Tafsiri hii ya kiroho ni ukumbusho war oho ipotoayo au
ya upotevu iliyoondolewa kwa uumbaji wa kimwili. Inamaanisha wanadamu wote.
Wale ambao hawataonekana wameandikwa kwenye Kitabu cha Uzima ni Mnefili na
Mrefaimu (Isaya 26:13). Soma jarida la Wanefili (Na. 154). Mauti ya pili ina nguvu kwa wale walio kwenye Ufufuo wa Pili. Kama mtu
hatatubu ndipo atakumbwa na mauti hii. Ni kazi ya Kristo na wateule wake kuweka
mikakati ya kuwaokoa ili wasife.
Magundua kwamba Ufunuo 21:1 inasema “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana
mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.” Je, kutakuwa na bahari kipindi cha milenia?
Jibu: Ndiyo, kutakuwa bado na bahari kipindi hiki cha Milenia. Marejesho haya
mapya ya Masihi yanashuhudia kuwepo kwa mito itakayotokea kwenye Mlima wa
Sayuni itakayoelekea kwenye bahari ya upande wa magharibi na hadi Araba na
itatumiwa na samaki na kuokota au kuzoa chumvi kwenye kingo za Araba.
Andiko lililo
kwenye Ufunuo linaelezea mazingira au hali inayoanzia mwishoni mwa Ufufuo wa
Pili na ujio wa Mji wa Mungu. Soma jarida la Mji wa Mungu (Na. 180).
Jarida la Milenia na Dhana ya Unyakuo (Na. 95) linashughulika na
dhana potofu kuhusu Milenia na hali yake sahihi.
Kuna rejea nyingi sana zinazotaja “bahari” kwenye
Maandiko Matakatifu; je, kuna ishara maalumu na muhimu ya kuitilia maanani
ninapokuwa nasoma kuhusu bahari zilizotajwa hapo juu? Kuna dhana yoyote ya kwa
nini isemwe kutokuwapo tena kwenye Ufunuo 21:1?
Jibu: Bahari ina maana zaidi ya mbili kwenye tafsiri ya Biblia. Maana ya kwanza
ni ya moja kwa moja kama bahari tuionayo ya kimwili. Na maana ya pili ni ya
kimfano na inamaanisha uwingi wa watu au mataifa meingi. Kwa hiyo lile neon la
“wanyama kutoka baharini” wanamaanisha umati wa watu walio kama mfumo wa
kimaongozi au serikali. Kwa hiyo, mnyama ni mfumo wa utawala wa kidemokrasia
unaojiweka na kujihesabia haki wenyewe. Nyakati za mwisho, bahari hii itakuwa
ya kiroho. Ka hiyo, umati utatoweka kwa maana ya kwamba utayeyuka na kuwa kitu
kubadilikabadilika kama ulivyofanyika kuwa mji mmoja kama wana wa Mungu. Soma
jarida la Mji wa Mungu (Na. 180).
Dunia itatakaswa kwa moto na bahari zilizopo zinaweza kuwa ama zimeondolewa
au kufanywa upya kimuundo mwingine. Hiyo itatokea baada ya Ufufuo wa pili na
hakutakuwa na mtu aishiye atakayebakia kama tujuavyo hivi sasa. Soma majarida
ya Ufufuo wa Wafu (Na. 143).
Unamaana gani usemi huu “Wakati wa dhiki ya Yakobo?”
Jibu: Yakobo ni taifa la Israeli. “Wakati wa dhiki ya Yakobo” unamaanisha
kuitaja hali ya taifa hili itakavyokuwa katika Siku za Mwisho. Mwishoni kabisa,
karibu na ujio wa Masihi, taifa la Israeli litapita kwenye kipindi cha dhiki
kuu itakayosababishwa na viongozi wake lenyewe pamoja na watu waovu
watakaokujakuwa ndani yake. Taifa la Israel lililo kwenye hii Nchi ya Ahadi
tuijuayo leo lina makabila mawili tu wanaoliunda, ambao ni kabila la Yuda na
sehemu ya kabila la Lawi.
What does the Bible indicate the planet will be like at the beginning of the Millennium?
Jibu: Dunia inaonekana kuwa kwenye hali mbaya kwa sababu ya mwenendo wa
watu wa nyakati hizi. Biblia inasema kwamba ulimwengu utakuwa karibu na
kangamia kabisa. Mchakato unaendelea mbele kwa kupitia awamu mbalimbali
tuzijuazo leo kama Mihuri Saba, na kufuatiwa na Baragumu Saba, Vitasa Saba vya
Ghadhabu ya Mungu. Mihuri hii
Saba ni Baragumu Saba, na hivi Vitasa Saba ni Baragumu ya Saba. Soma majarida mengine ya Mihuri Saba (Na. 140) na Baragumu Saba (Na. 141). Ulimwengu unaweza kutubu na kuachana na
uwendawazimu wake, lakini hautaweza kutubu kihivyo. Wakati wa Baragumu hii ya
Saba kutashuhudiwa theluthi ya miti yote na nyasi vikikauka, na theluthi ya
maji yote duniani yatabadilika kuwa damu, theluthi moja ya bahari zote itakufa
kiasi cha kusababisha samaki wote walio maeneo hayo kufa pia, na yapata zaidi
ya theluthi moja ya wanadamu watauawa kwenye vita ya baragumu ya sita na ya
sita. Lakini bado hawatatubu.
Masihi atakuja
kusimamisha mauaji haya, lakini toba haitafanyika, na dunia itaendelea mbele
kwa kuiangamiza miti yote na nasi zake zote, samaki wote wa baharini, karibu
wanadamu wote, na wanyama watakufa pia. Kisha ndipo tutauunganisha ulimwengu
uliokufa pamoja na kuanza tena kwa Sheria au Torati ya Mungu. Tutapaswa
kuukomesha na kuanza kuzishika sheria au Torati ya Mungu sasa, lakini
hatutaweza kufanya hivyo sasa. Tungeweza kuyalinda mazingira kwa kuzishika
sheria za vyakula lakini hatutaweza kumudu kufanya hivyo kabisa. Soma jarida la
Sheria ya Vyakula (Na. 15).
Tuna mfano wa
kuufuata kutoka kwa Kristo na kwa Mitume na wa Kanisa la Kwanza. Hata hivyo,
dunia iliwaua Mitume wote na watakatifu na wakaisimamisha dini na imani ya
uwongo waliyoiita “Ukristo.” Umemuua kila mtu aliyejaribu kuzitii na kuishika
Torati au amri za Mungu na Ushuhuda wa Yesu Kristo, wakiwaua kwa kutumia mkakati
maalumu na uliopangiliwa vizuri tangu mwaka 590 BK. Wengi wa waliozishika Amri
na Torati waliokuwa wasika Sabato wamekuwa wakiuawa kwenye karne hii zaidi,
yawezekana hata kuliko hata wakati mwingine wowote wa kihistoria. Wamekuwa
wakiuawa na “Wakristo wazuri wa imani ya Kikatoliki” na “Wakristo wengine
wazuri wa imani ya Kiprotestanti” makundi haya yote mawili yakilitumia jina la
Mungu wao wa Utatu, wanayemwabudu siku ya Jumapili, wakiwaua na kuwatesa wale
wanaozifuata na kuzishika amri za Mungu wa kweli na imani au ushuhuda wa Kristo
na Mitume. Haihitaji kuwa ya namna hiyo, lakini watu watafanya hivyo kuliko
mumtii na mumcha Mungu.
Ufufuo
Tafadhali nifafanulie kitakachotokea wakati mtu
atakapofufuka.
Jibu: Mchakato wote kamili umeainishwa kwenye jarida la Ufufuo wa Wafu (Na. 143). Tazama pia kwenye jarida la Nafsi Hai (Na. 92). Mchakato huu kama ulivyokuwa kwa Kristo alifufuka
na kisha kubadilika kimwili. Alipaa kwenda mbinguni akiwa kama Mganda wa
Kutikiswa siku ya Kwanza ya Juma asubuhi, akitolewa mbele ya kiti cha enzi cha
Mungu kama Mganda wa Kutikiswa. Aliingia Patakatifu pa Patakatifu na akarudi
kwa uweza wa Roho Mtakatifu, aliowapulizia wanafunzi wake (sawa na ilivyo
kwenye Yohana 20:22).
Ezekieli
anaonyesha kuwa ufufuko ni wa miili. Wale wafu waliolala-wakiwa
watakatifu-watafufuliwa kwenye Ufufuo wa Kwanza. Kisha ndipo na sisi
tutakaobakia hai, wote tutabadilishwa na kwenda Yerusalemu kuwa pamoja na
Masihi. Ndipo dhiki kuu itaanza. Majeshi ya mataifa yataletwa huko Armagedoni
au kwenye bonde la Yezreeli. Watakuja kupigana na Masihi na yataangamizwa (soma
jarida la Baragumu (Na. 136)).
Kisha dunia
itaongozwa kutoka Yerusalemu kwa kipindi cha miaka 1000 (soma jarida la Milenia na Dhana ya Unyakuo (Na. 95).
Mwishoni mwa miaka hii
1000, Shetani atafunguliwa tena na vita ya mwisho itatokea. Mataifa
yatajikusanya na kuja tena Yerusalemu na kisha majeshi hayo yataangamizwa. Watu
watakaobakia kuwa watiifu na wasiasi ni wale waliobadilishwa na kufufuka kwenye
ufufuo wa kwanza.
Wale waliokuwepo
na wengine wote waliowahi kuishi watafufuliwa kwa kipindi cha miaka 100. Ndipo
dunia yote itapatana na Mungu na kuongoka. Kila pepo aliyeasi atafanyika kuwa
mwanadamu kama alivyokuwa Kristo, na utambulisho wao wa hali ya zamani
vitakoma. Watapewa pia fursa ya kutubia dhambi na makosa yao (soma jarida la Hukumu ya Mapepo (Na. 80)).
Kila mtu kwenye
ufufuo wa pili atakabiliwa na madhara ya mauti ya pili kama hawatatubu. Walio
kwenye Ufufuo wa Kwanza hautakumbwa na mauti haya ya pili, kwa kuwa muda wa kuhukumiwa
kwao ni sasa. Hii ni dhana iliyo kwenye waraka wa Waebrania unaposema kuwa
Ufufuko wa Kwanza ni ni wa heri na bora zaidi.
Mwishoni mwa
Ufufuo wa Pili na Hukumu huenda ni takriban mwaka 3127, dunia itafanywa upya
kwa moto. Mji wa Mungu utashuka kutoka mbinguni na ndpo Kristo atakabidhi
mamlaka yote kwa Baba, na vitu vyote vitakuwa kwenye mamlaka ya Baba, naye
atakuwa ni yote katika yote na ndani ya yote. Soma jarida la Mji wa Mungu (Na. 180).
Wakati wa ufufuo, je, watotoo watawajua au
kuwakumbuka wazazi wao? Na watu wengine wataweza kujuana kipindi hiki kwa namna
waliyojuana kabla ya wakati huu?
Jibu: Ndiyo, kwenye Ufufu wa Pili watu wote watafufuliwa na watapatanishwa wote.
Viumbe wote pamoja na mimba zote zilizotungwa na ambazo ziliwahi kutungwa
zinajlikana na ziko salama kwenye mawazo ya Mungu. Zitafufuliwa zote na
watajulikana wote na kukumbukana.
Na hii ndiyo
sababu kwamba watu wengi hawapendi kusikia jambo hili. Zaidi sana watu wanapenda
kufundishwa uzushi wa kuwa wataishi motoni na kuunguzwa humo milele. Pia
itakuwa vigumu sana kwetu kuhusika nao, kwa mfano, wanawake waliowashuhudia
watoto wao wakiuawa kwa kupigwa risasi kwenye mauaji ya kuangamiza Wayahudi na
Washika Sabato wa Ulaya yajulikanayo kama Holocaust, ndipo hawatakuwa na la
kujitetea askari wa vikosi waliofanya hivyo.
Itakuwa ni rahisi
zaidi kwa wao kutubu, kuliko kuwasamehe waliowakosea. Yote mawili ni muhimu kwa
kuupata wokovu. Ndiyo maana kumefanywa uwongo mwingi wa namna mbalimbali kwenye
dini za dunia. Kwa mfano, dhana au fundisho la kuzaliwa tena na tena kwa
kubadilika badilika lilianzishwa ili kuwafanya watena na tena kwa kubadilika
badilika lilianzishwa ili kuwafanya watu walichukulie fundisho la kweli la
Ufufuo wa Pili kuwa ni kama aina tu nyingine ya mtindo huu wa kuzaliwa kwa
kubadilika badilika waujuao itatupasa kushughulika kulielezea jambo hili pia.
Wanakwenda kuwa
na makasisi wapotofu sana na wataabisaji kutokea watakaowafundisha aina nyingi
ya ole na makatazo ya uwongo kwa ajili ya fedha na mamlaka. Tunapoyaona
yaliyokwisha kufanywa huko nyuma kwa jina la dini, na hata kwenye karne hii,
basi itawakumba watu wengi.
Nasoma mahali fulani kwamba
kwenye Ufufuo wa Kwanza watu wataishi na kufa kama ilivyo sasa. Je, hii ina
maana kwamba wakati atakaporudi Yesu, yeyote atakayekuwa anaishi hai kipindi
hicho hataweza kufufuka? Je, watu wanaokufa kipindi hiki ch ufufuo wa kwanza
watafufuliwa kwenye ufufuo wa pili?
Jibu: Ndiyo, watu wataendela kuishi, na sio
kila mtu atafufuka wakati atakaporudi Kristo. Kwa kweli, watli, watu wengi
hawatafufuliwa kwenye ule ufufuo wa kwanza. Ni watakatifu tu peke yao ndio
watafufuliwa, waliozishika Amri za Mungu na Ushuhuda au Imani ya Yesu Kristoo
(Ufunuo 12:17; 14:12) na aliopewa Kristo na Mungu watakuwa kwenye Ufufuo wa
Kwanza.
Fufuo utakuwa wa makundi mawili. Kundi la kwanza ni la wale 144,000 na la pili ni la Mkutano Mkubwa kama
linavyoonyeshwa kwenye Ufunuo 7. Watatawala duniani hapa pamoja na Kristo kwa
kipindi cha miaka 1,000 kama alivyofanya Shetani pamoja na malaika zake kwa
kipindi cha miaka 6,000 sasa. Mwishoni mwa kipindi hiki cha Milenia, Shetani
atafunguliwa tena kwa muda mfupi ili awadanganye mataifa na ndipo vita ya
mwisho itatokea. watu wataendelea kwa kiasi cha kuzidi au kupungua kiwango cha
umri wao tukilinganisha na ilivyo sasa, lakini wote wataishi na kufuata
maongozi ya amri na maongozi ya Torati ya Mungu. Kimeelezewa na manabii wa
zamani kuwa ni kipindi cha Utawala wa Haki. Ufufuo wa Pili utahusu mfumo mzima
wote wa Uumbaji na viumbe vyake vyote wakiwemo malaika waasi, na baada ya hapo
tutaunganishwa wote na Mungu pamoja kwenye Mji wa Mungu. Soma majarida ya: Ainisho la Ratiba ya Matukio ya Nyakati (Na. 272); Milenia na Dhana ya Unyakuo (Na. 95); Baragumu (Na. 136); Ufufuo wa Wafu (Na. 143); Nafsi Hai (Na. 92); na Hukumu ya Mapepo (Na. 80).
Je, naelewa vyema kuamini
kwamba wale walio kwenye ufufuo wa kwanza watakuwa kweenye utawala wa Yesu na
kila kitu kitakuwa kama kilivyo leo? Je, watajihisi kuhuzunishwa wakati mtu
anapokufa, au zitakuwepo nyumba na makazi, watu kufunga ndoa, kazi na
mishughuliko, shule na masomo, na dunia itakuwa inafagiliwa ili kuifanya iwe
safi?
Jibu: Dunia itaendelea kudumu kwa kipindi cha
miaka mingine 1000 baada ya kurudi kwake Kristo. Itakuwa kwenye hali ya
kuharibika na itapasa kutengenezwa au kukarabatiwa upya. Dhumuni la Ufufuo wa
Kwanza ni kufanya wawepo na kundi la viumbe wa kiroho watakao tawala na Kristo
watakaozifanya kazi walizokusudiwa kuzifanya mapepo kama wasingeasi hapa
duniani kwa kipindi hiki cha miaka 6000. Wakati huu mambo yote yatafanyika
sawasawa na sheria ya Torati ya Mungu. Dunia bado itakuwa na viumbe wa kimwili
kipindi hiki na kutakuwa na mpangilio wa kifamilia na watu wataenenda kwa
mujibu wa maagizo ya Torati. Kutakuwa na tukio kubwa la Kutoka kwa wana wote wa
Israeli wanaohitajika kuunganishwa ili kuhitimisha idadi katika Israeli,
sawasawa na maelekezo ya Kristo, wakiwa kama makuhani na Walawi. Hii imeelezwa
wazi kwenye Isaya 66.
Tukio hili la Kutoka litakuwa Kubwa kuliko lile la kwanza lililoandikwa
kwenye kitabu cha Kutoka na litafanyika baada ya vita ya Armagedoni na
kuangamizwa kwa majeshi ya ushirika wa mataifa. Kama mtu alichukuliwa kwenye Ufufuo
wa Kwanza na akabatizwa, na mtoto akaachwa kwa kuwa hajafikisha umri
unaostahili abatizwe, ndivyo sasa kwamba mzazi akiwa mtu wa ulimwengu wa roha
atamuwezesha kufana hivyo kwa ajili ya matunzo ya mtoto kuliko hata
angalivyoweza kumtendea wakati akiwa mwanadamu. Kwahiyo ndipo watafanyika kuwa
elohim moja kwa moja. Watoto watakuwa wamebarikiwa sana kipindi hiki. Soma
majarida ya: Ufufuo wa Wafu (Na. 143); Milenia na Dhana ya Unyakuo (Na. 95); nad Ainisho la Ratiba ya Zama na Nyakati (Na. 272).
Karamu ya Arusi
Unaweza kunifafanulia kwa hakika ni nini maana ya
karamu ya arusi ya mwanakondoo?
Jibu: Kwenye jarida la Baragumu (Na. 136) mambo mawili ya Siku ya Baragumu
yameelezewa kwa kina. Sehemu ya kwanza ni ya Kurudi kwa Masihi nay a ili ni
Karamu ya Arusi ya Mwanakondoo. Masihi baada ya mashahidi wawili watakapotoa
ujumbe au watakapokuwa wamehubiri ujumbe wao na kuwezesha kurudisha kukubalika
kwa maongozi ya Torati ulimwenguni. Watauawa na kisha watafufuka baada ya siku
tatu na nusu.
Mhuri wa Sita wa
Ishara kutoka Mbinguni zitakazotangulia Ujio wa Masihi. (soma jarida la Mihuri Saba (Na. 140).) Ni Baragumu Saba tunazoziona kwenye vita vya mwisho na Ujio wa Masihi.
Soma jarida la Baragumu Saba (Na. 141).
Wakati
atakapokuja Masihi, waliokufa katika Kristo ambao ni wale waliolala mautini
watafufuliwa kwanza. Kisha wale walio hai ambao ni watakatifu watabadilishwa
miili yao na kuvikwa miili ya kimbinguni au ya kiroho pamoja na wale waliokufa
katika Kristo na ndipo watakwenda wote Yerusalemu ili kuwa na Kristo.
Ataugawanya Mlima wa Mizeituni pande mbili na wateule pia watakuwa pamoja naye.
Karamu ya
Mwanakondoo ni mojawapo ya mifano ya Wanawali Wenye Busara. Hawa ni wateule
waliozishika amri za Mungu na ushuhuda au imani ya Yesu Kristo na watakuwa
kwenye Ufufuo wa Kwanza. Soma
pia kwenye jarida la Ufufuo wa Wafu (Na. 143); Nafsi Hai (Na. 92) na Milenia na Dhana ya Unyakuo (Na. 95).
Kusaga meno
kutakako yakumba Makanisa ya ulimwengu huu wanaomita Kristo “Bwana, Bwana”
lakini wakiwa hawazishiki Amri za Mungu na Ushuhuda wa Krist. Hawa ni wale
wanajaribu kwenda kwenye Karamu ya Arusi na kukuta walikuwa hawaruhusu wala
kukifikia kigezo cha kiwango cha kiroho. Hawakuwa na mavazi meupe na hawakuwa
viumbe walio katika ylimwengu wa kiroho. Hii ni hatua ya kukataliwa na kutupwa
nje. Wanasaga meno kwa kuwa wanagundua kuwa waliyapotosha maandiko na
kufundisha uwongo na hawakuyatii bali waliyaasi maana na malengo yaliyokusidiwa
na Maandiko Matakatifu.
Kwa Mungu hakuna
upendeleo wala msimamo wa njia mbili. Ni ama kutii au kuasi. Kama utazitii na kuzishika amri na imani ya Kristo,
utaruhusiwa kuingia kama sehemu ya waliokusudiwa tangu mwanzo, waliochaguliwa
na wateule walioitwa waliohesabiwa haki na kutakaswa wakati huu wa Karamu ya
Mwanakondoo.
Wengine
waliosalia ulimwenguni ndipo watajaribu kufanya vita na Kristo, na majeshi ya
muungano wa ulimwengu yatapelekwa huko Megido, au bonde jipya la Yezreeli, hadi
Armagedoni. Ulimwengu utatiishwa na Shetani pamoja na mapepo yake watafungwa
kwa kipindi cha miaka elfu ya Milenia.
Maandiko Matakatifu
ya Torati ya Mungu yatakuwa yanafundishwa na kila mmoja kati ya wateule kwenye
Karamu hii ya Mwanakondoo. Wale ambao hawatazishika Sikukuu zilizoamriwa na
Mungu, pamoja na Sabato zake, na Miandamo ya Mwezi Mpya zilizo kwenye Kalenda ya Mungu (Na. 156), na kutuma wawakilishi wao kwenda Yerusalemu, mvua
haitanyesha kwa wakati wake muafaka na watakumbwa na magonjwa ya tauni ya Misri
(Zekaria 14:16-19).
Soma pia jarida
la Torati na Amri ya Nne (Na. 256). Kristo anakuja kuwaokoa wale wanaomngoja kwa hamu
na makini. Dini potofu za uwongo za imani zilizotungwa na kukubalika hapa
ulimwenguni zitakomeshwa na kuangamizwa. Mfumo na imani potofu na mbovu ya Ukristo
bandia na wa uwongo ambayo ndiyo yule kahaba Mkuu wa Babeli aliye kwenye kitabu
cha Ufunuo itaangamizwa na mnyama mwenyewe.
Wateule wa
Kanisani watakuwa ni viumbe katika ulimwengu wa roho, baada ya kufufuka kwao,
watakuwa wajumbe watakaokwenda ulimwenguni kote kuwahudumia makabila yote ya
kidunia na koo zao. Kisha tukio Kuu la Kutoka litatokea na taifa la Israeli
litapangiliwa vizuri na kurejeshwa upya kikamilifu huko Mashhariki ya Kati.
Tukio la kwanza la Kutoka litafanyika kwa hali isiyo na maana ndani ya tukio
hili la Kutoka (Isaya 66:18-24).
Soma pia jarida
la Kuwaita Watu Kwenda Yerusalemu (Na. 238).
Wanawali wapumbavu
wangali bado wamechumbiwa na Masihi na wataolewa naye, lakinii wataolewa kwenye
Ufufuo wa Pili mwishoni mwa kipindi cha Milenia. Soma jarida la Ainisho la Ratiba ya Zama na Nyakati (Na. 272).
Ufufuo wa Kwanza ndio
ulio bora kuliko, na mauti ya pili haina nguvu kwa wateule kwenye Ufufuo ule.
Unaweza kufafanua tafadhali ni nani
atakayehudhuria kwenye arusi ya mwanakondoo na itafanyika lini?
Jibu: Karamu ya Harusi ya Mwanakondoo imeelezewa kwa kina kwenye sehemu ya II ya
jarida la Baragumu (Na. 136). Watakaohudhuria Karamu ya Arusi ni walio Kanisani
waliofufuliwa kwenye Ufufuo wa Kwanza.
Kuna wale 144,000
na Mktano Mkubwa walioandikwa kwenye Ufunuo 7. Hawa ni wale waliozishika Amri
za Mungu na Ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufunuo 12:17: 14:12). Wamefufuka, kama
walikuwa wamekwisha kufa tayari, pamoja na wale walio hai watabadilishwa kuwa
viumbe katika ulimwengu wa roho na watachukuliwa kwenda Yerusalemu kuwa pamoja
na Kristo. Watatawala duniani hapa kwa kipindi cha miaka elfu na kuianda tayari
kwa Ufufuo wa Pili.
Kwenye Ufufuo huu
wa Pili, wale wote waliowahi kuishi watafufuliwa wakwa na miili halisi na
watafundishwa kikamilifu na kupewa fursa ya kutubu nay a wokovu. Mwishoni mwa
miaka 100, wale watu waliokataa kuzipokea na kutii Torati au sheria za Mungu
ndipo wataachyears, those people who have not accepted the Laws of God will
simply be alloweiliwa wafe, na watachomwa kwenye Jehanamu, jina ambalo chimbuko
lake linatokana na jalala la takataka lililokuwa nje ya mji wa Yerusalemu. Kwa
maneno mengine hili linajulikana kama Ziwa la Moto likimaanisha kuwa ni mahala
pa kuteketeza mizoga au miili iliyokufa ya wale waliokataa kuukubali mpango wa
Mungu kwenye kipindi hiki maalumu cha mwishoni mwa Ufufuo wa Pili na cha Kiti
cha Enzi Kikubwa Cheupe cha Hukumu.
Kama wale
walioalikwa kwenye karamu ya arusi wanafanya kazi zao kisahihi, hakutakuwa na
yeyote atakayepotea. Ni yule mpumbavy na mjinga ndiye atakayeukataa uzima wa
milele kwa Sheria za Mungu baada ya kuona kwamba njia nyingine zote zimefanywa
kuwa za kilimwengu. Wataponywa wote na kila mmoja atakuwa kwene nia sahihi.
Awamu inayofuatia
ni ya kuuunganisha Mji wa Mungu. Hii inapelekea Malaika wote wa mbinguni
kuwekwa chini ya Kristo kwenye sayari hii, na kisha Kristo atashika hatamu ya
kuuongoza ulimwengu wote, akiwamiliki Malaika wote milele. Soma jarida la Mji wa Mungu (Na. 180).
Kwa hiyo,
kimtazamo, karamu ya arusi itaishia hapo kwa kitambo. Wanawali hawa wenye
busara waliolewa kwanza lakini Kristo amechumbia wanawali wapumbavu na wote
walitarajia kuingia karamuni pamoja naye, kwa kuwa uchumba ule ukiwa ni arusi
kubwa sana. Mtu aliyeingia karamuni au arusini akiwa hakuvaa vazi la arusi
alipaswa kutoka nje na kurudi alikotoka na akavae ili awe na fursa kwenye
sherehe inayofuatia ya karamu ya arusi. Na ndiyo maana waliitwa “wanawali
wapumbavu.”
Mchakato huu wa
kuyatengeneza mambo yote upya utajiri pia wale malaika walioasi ambao watapewa
pia fursa ya kuvikwa vazi jipya na kupewa jina jipya. Itawapasa kwenda kwa
kupitia mchakato huo huo alioupitia Kristo. Itawapasa kuwa wanadamu, ili waweze
kufufuliwa, kisha ndipo waishi kwa miaka 100 wakiwa kama wanadamu wakiwasaidia
wale wote waliowazuia kwenye kipindi chote cha kudumu kwa uumbaji.
Soma kwenye
majarida ya Ufufuo wa Wafu (Na. 143); Nafsi Hai (Na. 92); Hukumu ya Mapepo (Na. 80); Kondoo Aliyepotea na Mwana Mpotevu (Na. 199); na Ainisho la Ratiba ya Zama na Nyakati (Na. 272).
Mji wa Mungu
Nimesikia kukijadiliwa kuwa Mji wa Mungu utakuwepo
baada ya miaka 40,000. Naamini kuwa umeandaliwa kutokana na msingi wa maandiko
yafuatayo: Kumbukumbu la Torati 7:9; Zaburi 105:8; 1Wafalme 3:4; Luka 1:50.
Dhana iliyopelekea kufundishwa hivyo ni kutokana na imani iliyopo kwamba rehema
za Mungu zinadumu kwa vizazi 1000 vya wampendao, hivyo basi kuwa sawa wa miaka
hii 40,000. Nilidhani kuwa rehema za Mungu zinadumu hata milele na milele.
Unaonaje kuhusu hilo?
Jibu: Mji wa Mungu utaletwa mara tu baada ya tukio la Ufufuo wa Pili na cha
Hukumu. Kwa nini Mungu asubirie kwa miaka 33,000 kabla ya kuja kwake duniani
kuanzisha utaratibu wote mzima wa Mji wa Mungu (soma jarida la Mji wa Mungu (Na. 180). Neno lipasalo kuuita ni la kinadharia tu.
Hata hivyo, kama
tukiangalia nyuma kwenye historia kwenye matendo na harakati za malaika,
walianza uumbaji kwa kipindi cha takriban miaka 40,000 iliyopita na Cro-Magnon
inaihesabu tangia wakati hhuu. Inawezekana kabisa utajwaji wa rehema ulienea
kwa malaika kwa matendo na harakati zao za wakati wa mwanzoni sana pia.
Inahusiana pia na rehema inayoweza kuenezwa hadi kwao kwenye Hukumu, kama
tutakavyowahukumu wao (1Wakorho 6:3). Soma majarida ya Hukumu ya Mapepo (Na. 80); Kondoo Aliyepotea na Mwana Mpotevu (Na. 199); Ainisho la Ratiba ya Zama na Nyakati (Na. 272); Ufufuo wa Wafu (Na. 143) na Wanefili (Na. 154).
Kalenda
Kwenye kijitabu kidogo cha Tamko la Msingi wa
Imani, kipengele cha 4.2, ukurasa wa 28, kuna palipotaja saa tatu kuwa ni saa 3
asubuhi na saa tisa kuwa ni 9 alasiri. Sielewi iko hivyo kwa nini. Nijuavyo mii
ni kwamba siku inaanzia jua linapozama na inaishia pia jua linapozama. Kama ni
hivyo, basi saa tatu ingebidikuwa ni saa 3 ya usiku au zaidi yake. Kama kuna inapotaja kwenye saa ya sasa ya ukutani kwamba ni saa 3 ya usiku.
Unaweza kunifafanulia jambo hili tafadhali, ni wapi hali hi inakotokea japo kwa
ufupi?
Jibu: Kuna namna mbili inayotajwa kuhusu siku. Aina ya kwanza ni ile ya saa
ishirini na nne kama unavyosema, lakini Kristo pia alisema “kwani Siku moja
haina masaa kumi na mawili?” kwa jinsi hii inamaanisha kuwa ni masaa ya mchana.
Saa la kui na
mbili kwa kawaida linaanzia saa 6 usiku hadi saa 6 ya mchana, kama
tunavyohesabu kwa mujibu wa masaa ya dini ya Kanisa la Roma wanavyohesabu tangu
karne ya 19. Usiku pia uligawanywa kwa masaa, lakini mara nyingi yalitajwa kama
masaa ya “zamu.” Zamu ya katikati ilijiri kuanzia saa 4 usiku hadi saa 8
alfajiri kwa saa za siku hizi.
Saa la kawaida la
kwanza la siku ni lile tunalolijua sasa kuwa saa 12 asubuhi, na saa la kwanza
la usiku lilikuwa ni saa 12 ya jioni. Kwa hiyo, hesabu ya dhabihu za asubuh na
za jioi zilifanyika saa tatu, na ndiyo maana Kanisa lilikusanyika wakati huo
siku ya Pentekoste. Roho Mtakatifu aliwashukia majira ya utoaji wa Dhabihu ya
Asubuhi. Hii ilikuwa na maana kubwa sana kwa wote waliokuwepo.
Utaratibu huo
uliendele kutumika hadi hata siku za hivi karibuni. Utaratibu wa kuishika
kalenda na nyakati zake vimeainishwa kwenye majarida ya Kalenda ya Mungu (Na. 156). Mwezi Mwandamo na Mwaka Mpya (Na. 213) linafurahisha sana
jambo hili pia.
Unasema kwamba siku ya usiku na mchana masaa kuwa
sawasawa maarufu kama ikwinoksi ya majira ya baridi na yalituwa kwenye kuamua
kuupata mwezi wa kwanza. Kwani ikwinoksi hii ya majira ya mapukutiko mara zote
inaangukia kwenye mwezi fulani tu maalumu au kipindi fulani maalumu kila mwaka?
Jibu: Kuna vipindi viwili tu vya majira kwa mwaka kwenye Biblia. Navyo
vinajulikana au kuanza kwa kufuata kutukia kwa hizi siku za Ikwinoksi. Kwa wale
walio kama wewe wanaoishi kwenye ncha ya Kaskazini mwa dunia (Sayansi inadaiwa
sasa kukubaliana kwamba ncha ya kusini ipo juu, kwa maana ya ulimwengu),
yakupasa useme kuwa ni ikwinoksi za majira ya mapukutiko, lakini kwa upande wa
Ncha ya Kusini mwa dunia, kuna namna nyingine iliyopo. Siku ya 14 ya mwezi
ambayo ni mwanzo wa maadhimisho ya idi ya Pasaka inaangukia kwenye ikwinoksi ya
mwezi Machi, na haiwezekani kabisa kutokea siku nyingine yoyote mbali na mwezi
huu. Kwa utaratibu huu wa kikanuni, kwa kawaida inafuatia kwamba Siku ya Mwisho
ya Mkutano wa Makini ya Sikukuu ya Vibanda inaangukia kabla yake na wakati
mwingine baadae kidogo, lakini sio baada ya Ikwiniksi ya mwezi Septemba. Kwa
hiyo, majira matatu ya mavuno ya Mungu mara zote yanaangukia kwenye majira ya
joto ya upande wa Kaskazini katikati ya hizi Ikwinoksi.
Unazihesabuje siku za “Mwezi Mpya?” nimejisomea
vitabu vingi sana kuhusu jambo hili. Sikuti chochote kwenye Maandiko Matakatifu
kinachoniongoza kujua jinsi ya kuhesabu, ingawaje Sauli, Daudi na Manabii
wengine waliijua siku hii. Nauliza swali hili kwa kuwa siku zako zinaonekana
kutofautiana siku moja zaidi kuliko kipindi cha mpito wa kuandama mwezi cha
kinajimu, nadhani.
Jibu: Hapana. Siku zetu zinatokana na kipimo hicho hicho cha siku ya mpito ya
kuandama mwezi cha wataalamu wa Elimu ya Anga na imewekwa sawasawa na kama
zinavyoanza siku huko Yerusalemu, jioni hadi jioni inayofuatia. Hivi ndivyo
Wasamaria walivyofanya hadi siku za leo, na ndivyo ilivyofanyika kwenye
utaratibu wa hesabu za Hekaluni kipindi cha Masadukayo.
Ndiyo maana
ilijuliana wakati wote kabla. Mwezi Mpya kila mara uliwweza kuhesabiwa kwa
kufuata Kanuni zake au Phasis, kama zilivyokuwa jedwali za maji kujaa na kupwa
ulimwenguni kote. Hesabu ya wakati wa kupwa maji iliamua siku, sawa na kama
yanapokuwa yanajaa. Iliwapendeza Marabi wa Kiyahudi kudhania kwamba tulikuwa
wote hatujui ilivyokuwa ikifanyika siku hizo kwa kuwa hawakupenda kushika
sheria za Torati ya Mungu bila kuchanganya na mapokeo yao. Katika siku za
zamani au za kale zilizokuwa zinafanyika biashara kabla ya kipindi cha Hekalu,
vipimo vya nyuzi ulalo za za wima za dunia zilipimwa na ambazo tumezipoteza
wakati wa Zama ya Giza iliyoingizwa na iliyojiita kuwa ni Dla Takatifu ya Rumi.
Alama ya mwezi
mchanga mwandamo ni Kidole cha mungu Ashirat. Alama hii ya mwezi mchanga
unaoandama unafanyiza kucha ya kidoleni mwa mungumke anaykusudiwa. Pia ni ishara
ya pembe za mungu Sini, au za mungu Hathori akiwa kama mungumke wa urutubisho.
Isis pia ni mama wa mungumke na anafuatiwa kwa mbele yake na Horus. Easter au
Istar pia ni mama wa mungumke na anafuatiwa kwa mbele yake na kina Attis na
Adonis na wengine kadhalika. Ulitumika kama kiashirio cha nyakati na dini
mchanganyiko za Kibabeli na Kiashuru na Wamisri waliokuwa wanamuabudu mungu
mwezi, Sini na mungumke Easter au Ashirat na Wamisri wote wa zama kati ya
Milenia ya pili KK.
Ndiyo ilikuwa
ibada ya waamini Utatu na mungu mwezi, Sini na habari zake zinachambuliwa kwa
kina kwenye jarida la Ndama wa Dhahabu (Na. 222).
Habari za kalenda
zimeandikwa kwa kina kwenye majarida ya Kalenda ya Mungu (Na. 156) na Torati na Amri ya Nne (Na. 256).
Israeli na Kanisa
wamekatazwa kuindama imani ya mungu Sini na Dini au Imani za Mafumbo.
Sikukuu, Miandamo ya Mwezi Mpya na Siku Takatifu
zilizoagizwa kwenye Biblia na habari zake zinaonekana mara zote kujitokeza
kwenye tarehe zinazohesabiwa kutokana na matukio ya idara za wataalamu wa mambo
ya nyota. Kalenda zingine zimehesabiwa kwa matukio ya kidini, na huku bado mashirika
ya kidini yanayofika kwenye maadhimisho ya Siku Takatifu za namna hii bado
yanadai kuwa hizi ni Sikuku Takatifu za Mungu. Ni kwa namna gani au kwa kufuata
kanuni zipi tunapata mashiko ya kuamua siku hizi katika siku hizi?
Jibu: Kalenda ya Hekaluni ilihesabiwa kwa kuanzia siku ya mpito ya kutoonekana
mwezi na Wasamaria waliuhesabu kwa kuanzia siku ya mpito ya kutoonekana mwezi
hata sasa, kama tufanyavyo sisi. Nakala zilizokutikana Uchina zinaashiria
kwamba vonyesha kuwa vipindi hivi vya mpito pamoja na matukio ya kupatwa kwa
jua na mwezi na matukio mengine ya elimu ya kinyota au unajimu vilihesabiwa
tangu milenia ya tatu KK; kwa maneno mengine ni tangu wakati wa Nuhu kwa kweli.
Sheree au sikukuu
ya Rosh Hashanah ni ya Kibabeli iliyokuwa ikisherehekewa huko Babeli na
kuingizw kwenye sikukuu za Kiyahudi zilizoanzishwa au kuingizwa na marabi wa
Kiyahudi mnamo karne ya tatu ya siku zetu. Kalenda ya Biblia imeeleweshwa kwa
kina kwene jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 156) na pia Mwaka Mpya umeainishwa kwa kina kwenye
jarida la Mwezi Mwandamo na Mwaka Mpya (Na. 213).
Pahala na umuhimu wake
kwenye sheria na Torati umeelekezwa kwa kina kwenhe jarida la Torati na Amri ya Nne (Na. 256).
Msingi wa kufanya
uahirisho wa Kalenda ya Rabi Hilleli, na ambayo imetuama kwenye kuanza kwake
kufuatia na sikukuu hii ya Rosh Hashanah, vyote hivyo vimeelezewa kwa kina
kwenye jarida la Kalenda na Mwezi Mwandamo: Ni Uahirisho, au Sikukuus? (Na. 195).
Je, ushahidi gani tulionao
unaotuhakkishia kuwa kalenda ilianzia siku ya mpito wa kutoonekana mwezi?
Jibu: Mchakati rahisi wenye mashiko ndio huu.
Mwezi Mpya kwenye mataifa yote mara zote umekuwa ni kipindi kile cha mpito cha
wakati wa kutokuonekana mwezi. Imejulikana hadi sasa kuwa ni kipindi hiki cha
mpito cha kutoonekana mwezi na mataifa yote na wataalamu wao wa elimu-anga.
Dunia na mfumo wake wote unashuhudia kuwa ni kipindi hiki cha mpito cha
kutoonekana mwezi na kwa kutumia ali ujazo na kupwa kwa bahari na mwenendo
wake.
Utaratibu uliokuwa kwenye Hekalu na Zamani ulikuwa ni huu wa kuhesabu tangu
kipindi cha giza cha kutoonekana mwezi. Wasamaria walitumia pia utaratibu huu
wa kipindi cha kutoonekana mwezi na wangali bado wanatumia hivyo hadi sasa (pia
soma jarida la Mwezi Mwandamo na Mwaka Mpya (Na. 213) na majarida ya Mwezi Mpya kwa ujumla
pamoja na lile la Kalenda ya Mungu (Na. 156) Mambo haya yamefafanuliwa kwa kina kwenye
majarida yenye kichwa hiki cha maneno.
Kanisa la Mungu huko Ulaya lilitumia kipindi hiki cha mpito wa kutoonekana
mwezi kwa karne nyingi (soma pia jarida la
Wajibu wa Amri ya Nne Kwenye Historia ya
Makanisa ya Mungu ya Washika Sabato (Na. 170) na la Wasabato
wa Transylvania) matatizo yaliyoinuka kwenye imani ya Kiyahudi yalitukea
huko Jamnia wakati Mafarisayo waliposhika hatamu na kuanza kuwasha nguzo siku
za mwandamo wa mwezi mchanga kwa mintaarafu ya kuadhimisha kulikotokana na hamu
na tama zao ya kufanya uahirisho wa kurudi hadi nyuma kwenye Sabato. Matokeo
yake, kwa mara ya kwanza Wasamaria walianza kuwasha nguzo siku sahihi ya mpito
wa mwezi kutoonekana kutokana na maposhaji mpya ya Mafarisayo. Kuna kinachoitwa
misingi mipotofu inayotajwa kwenye imani ya Kiyahudi. Hata hivyo, Wasamaria
mara zote walikubali utaratibu wa Hekaluni wa mwezi mpya kuanzia siku ya mpito
ya kutoonekana mwezi na kamwe hawaziwashi taa zao kipindi ambacho utaratibu wa
hekaluni ulipokuwa unaendeshwa vizuri. Hawakubadilisha kamwe kabisa.
Alama ya mwezi mchanga mwandamo imechukuliwa kutoka kwenye ibada za
kipagani na iliingia kwenye imani zote mbili, za Kiyahudi na Uislamu kutoka
kwenye imani za kipagani pia (soma jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa ya Washika Sabato (Na. 122). Chanzo chake inatokana na kidole cha
mungu Easter au Ashirat au Astarte iliyotumika kama kiashirio cha majira au
wakati na imani ya Wamisri na Wababeloni walipokuwa kwenye ushawishi wa ibada
za mungu Ishtar kwa muonekano na madhihirisho mbalimbali. Kipindi hiki cha
mpito cha kutoonekana mwezi kilikuwa ni mwanzo wa Miezi Mipya kwa kipindi
kirefu hata huko Uchina katika millennia ya pili KK. Iwapo kama wataalamu wa
elimu ya anga walishindwa kuihesabu na matukio ya kupatwa kwa jua na kwa mwezi,
basi waliadhibiwa tangu nyakati za zamani sana (sawa na yasemavyo majarida ya ERE
kuhusu Kalenda kuhusu ya China nk).
Mafundisho ya kizushi ya Karaite yalianza kuenea kipindi cha Zama za Kati
kutokana na kutoelewa na ni utaratibu huu ndiyo ulinaozidi kuenea kama
maadhimisho a kijinga na yasiyo na maana hadi sasa. Mtu anaweza kujiuliza swali
rahisi tu kwamba: Kama siyo propaganda tu nini basi kwamba Marababi waliitumia
kufanikisha mkakatti wa kufanya uahirisho ukubalike ambao Masihi alionyesha
haukuwa ukitumika kipindi cha kuanzishwa kwake na ilikuwa ni sababu ya
kuingizwa kwa mchezo wa maadhimisho yake na kanuni ilishindwa kufanikiwa
kuwakumba watu wengi wa jamii ya Yudea kama mashahidi na kuzidisha shikaji
hatamu wao, nu wao, ni ushahidi upi uliopo hapo wa kuhalalisha utaratibu huu wa
ahirisho kuadhimisha mwandamo wa mwezi mchanga siyo kuwa unatokana na upagani
na imani za Ndama wa Dhahabu?
Mitindo ya Kialmanaks (kwa Kirababu inamaanisha kuhesabu) ililetwa na
Waanglo Saxons kutoka Mashariki ya Kati walipokuja huko Ulaya wakati wa
kuanguka kwa Dola ya Parthian (mnamo karne ya 2 KK), na ambayo ingali inadumu
bado ikionyesha kwamba kuna siku hamsini na tisa kwa kila mwezi sawa na mfumo
wa Kiarabu, tangu Mwezi Mpya unaokaribiana zaidi na siku ya ikwinoks ya mwezi
Machi na ikabakia hivyo hadi katika karne ya kumi na saba huko Uingereza. Mungu
aliziumba mbingu ili kufanya majira na nyakati. Hakuhitajiki kutafakari makundi
madogo madogo yaliyopotoshwa ya Wayahudi wa kipindi cha Zama Kati ili kuamua
mwelekeo wa Kalenda. Imekuwa ni ushuhuda wa watu wote na kwa nyakati zote.
Kwa mbinu au mtindo wa
kutofautisha maoni kama kwa kadiri ya inavyohusika kuanza kwa siku za miezi
mipya, Ningependezwa sana kukijua kile kinachochukuliwa kama msingi wa kuamua
siku ya kuanza kwa miezi mipya jinsi ilivyofanywa wakati wa Kristo?
Jibu: "[sikukuu] ya tat uni mwanzo wa
mwezi mpya pamoja na jua”. "Philo wa Alexandria [kwenye kitabu chake cha F H Colson (Harvard
University Press, Loeb Classical Library, Cambridge, MA, 1937); The Special
Laws, II, XI,41]. And in II, XXVI,140 kinasemaa: "Huu ni Mwezi Mpya, au
mwanzo wa mwezi mwandamo, ujulikanao kaama kipindi cha katikati ya siku moja ya
mpito ya mwezi kutoonekana hadi ya pili, na urefu wa kitu kilichohesabiwa
kikamilifu kwa mwelekeo wa kiuanazuoni wa elimu ya anga". (Soma jarida la Kalenda na Mwezi Mwandamo: Ni Uahirisho au
Sikukuu? (Na. 195).
Mambo mengine ya kuyatilia maanani ni: Kutokana na usomaji wa Injili tunaweza
kuona kwamba Kristo alikufa siku ya Jumatano, na alifufuka mwishoni mwa siku ya
Jumamosi kuelekea siku ya Jumapili. Tunajua kwamba alikufa saa 9 (saa 9
alasiri) na alikufa kwa siku 3 mchana na siku 3 usiku (Mathayo 12:40). Tunajua
pia kwamba Mariamu alikuja kaburini kwake siku ya Jumapili asubuhi (Mathayo
28:1). Kwa hiyo, ukirudi nyuma hadi siku ya 3 za chana na siku 3 za usiku, ni
wazi sana kwamba aliuawa siku ya Jumatano tu. Ikitiliwa maanani kwamba Jumatano
inaanzia kwanza usiku, na Alhamisi ikawa siku ya kwanza, na angeweza tu kuwekwa
kwenye kaburi lake baada ya saa 9 alasiri siku ya Jumatano. Hakuna mashaka pia
kwa namna yoyote ile kwamba alikufa siku ya maandalio ya 14 ya mwezi wa Abibu,
akiwa kama mwanakondoo wa Pasaka.
Kwa vipengele hivyo 2 (yaani kwamba alikufa siku ya 14 ya mwezi wa Abibu,
na mwaka ule, siku ya 14 Abibu iliangukia siu ya Jumatano), na tukihesabu kwa
kwenda nyuma tunaweza kutarajia kuwa siku ya 1 ya mwezi wa Abibu kuangukia siku
ya Alhamisi, ikianzia siku ya Jumatano wakati wa kuzama jua. Kutokana na mwanzo
huo, linajitokeza swali kwamba: je, siku ya 1 ya mwezi wa Abibu ilikuwa ni ya
mwezi mpya au ya kuandama kwa mwezi mchanga? Kwenye jarida la Nyakati na Majira ya Kusulibiwa na Kufufuka (Na.
159) siku zote
zilipewa majira ya mwezi mpya zilikuwa ni mwezi Machi na Aprili tangu mwaka wa
28 BK hadi 33 BK. (Imetolewa na Idara ya Mambo ya Anga iitwayo Her Majesty's
Nautical Almanac Office). Jumatano ya yarehe 22 Machi mwaka wa 30 BK saa 20:59
ilikuwa ni mwezi mpya, kuonyesha kwamba Abibu i ilianza wakati wa kuzama jua
kwa Jumatano. Hii iikuwa ni siku ya mwezi mpya, na sio ya mwandamo wa mwezi
mchanga. Inakuwa na mashiko kwa mwaka wa 30 BK kuwa ni mwaka wa aliosulibiwa
Kristo kwa ajili ya Ishara ya nabii Yona (ambayo ilianzia tangu mwaka wa 30 BK
na kuishia Abibu 1 ya mwaka 70 BK).
Wayahudi wa jamii ya Karaite wamasema kuwa mwezi
mpya ni wakati ule wa kuandama kwa mwezi mchanga. Najua kwamba kipindi cha
mpito cha kutoonekana mwezi cha wataalamu wa elimu ya anga kuwa ni sahihi sana.
Tunawezaje kujua kutokana na Biblia, ni ipi inayokubaliana na maagizo ya YHVH?
Tunajua kuwa siku inaanzia wakati wa jua kuzama, lakini kwa kusudi la kila siku
ya 1 ya kila mwezi kutumia upigaji wa Baragumu kama mfano, inakuwa ni sahihi
kurudi nyuma hadi kwenye uzamaji wa jua uliopita baada ya mwezi mpya? Nadhani
kwa mujibu wa jinsi nilivyoambiwa mimi kuhusu ushuhuda wa kuitangaza siku hii
na nashangaa waliwezaje kuuona na hata waseme kuwa ilianza tangu siku iliyopita
wakati wa kuzama jua. Siku hii yote hadi kuzama kwa jua ni kipindi kitakatifu
cha Sabato, kwa hiyo nataka kuwa na uhakika siku tunayoabudu kwa siku hizi.
Jibu: Wayahudi hawa wa jamii ya Karaite ni dini iliyokuwepo katika siku za zama
za kati ya Kiyahudi iliyotokana na hazingira ya kutoelewa historia na utaratibu
wa Biblia wa Kipindi cha Hekalu. Mataifa yote huanza kuhesabu siku ya Mwezi
Mpya kuanzia siku ya Mpito ya kutoonekana mwezi, na walifana hivyo katika
kipindi cha Hekalu.
Wasamaria bado wanaanza
mzunguko wa kalenda yao kwa kuweka kigezo chao siku hii ya mpito ya kutoonekana
mwezi, ingawaje walifungamaniba kalenda na ikwinoks ya tarehe 25 Machi katika
karne ya tatu KK. Watangulizi wetu kwenye Kanisa la Mungu waliweka kalenda kwa
kigezo hiki hii cha kipindi cha mpito kwa miaka elfu. Malumbano yaliyoibuka
katika karne ya 20 yalitokana na jaribio la kulikasumbisha itikadi za Kizayoni
kanisa na makosa yaliyotokana na imani na mafundisho ya Armstrong.
Kama mtu
atakwenda kwenye duka la wanasesere na akanunua kijewali cha mviringo, ndipo
ataona kuwa mara zote mwezi mpya utaangukia siku hii ya mpito, haijalishi ni
nchi gani uliyopo. Neno la
“miale ya Mwezi” linatokana na neno “Phasis” ambayo ni Mwezi Mpya. Alama ya
mwezi mchanga unaoandama inahusiana na ibada za mungu Mwezi, Sini aliyekuwa
maarufu huko Mashariki ya Kati na ambaye alikuwa pia anaabudiwa kwa kumchongea
sanamu ya Ndama wa Dhahabu. Soma
jarida la Ndama wa Dhahabu (Na. 222). Pia soma majarida mengine ya Mwezi na Mwaka Mpya (Na. 213); Kalenda ya Mungu (Na. 156); na Kalenda na Mwezi Mwandamo: Uahirisho au Sikukuu? (Na. 195).
Je, unajua kwamba historia hii ni kabla ya
kuanzishwa kwa mfumo wa tarehe. Naamini kuwa ilikuwa ni matumizi ambayo
yatapaswa kurekebishwa. Watu wengi sana wamekuwa na maono yao yanayoungwa mkono
na mwanadamu mwenye chupa ya maziwa tu katiyao na Baba zaidi kuliko Kristo kuwa
ni mwombezi wa pekee.
Jibu: Tunajaribu kuyafanya mapenzi ya Mungu na historia ya mwenendo wa majira
sio matokeo halisi tunapotilia maanani ukweli wa kwamba kuamua mwanzo wa Mwezi
Mpya yanatokana na siku hii ya mpito ya baada au kabla ya utusitusi na kwa hiyo
siku imaamuliwa kwa uhusiano wake na Kipindi cha mpito kinachohusiana na
utusitusi huko Yerusalemu, na hivyo, siku ile inaamuliwa na kipindi.kwa hiyo,
utaratibu wa Muainisho wa Siku wa Kimataifa kwa hakika ni aina ya pili ya
kuhesabu. Kuzama kwa jua hadi kuzama tena kwa jua na kipindi cha masaa ishirini
na nne kinafanya jumla ya siku moja yenye masaa ishirini na manne ndani na
mfumo mmoja wa nyakati iliyopimwa kama siku halisi.
Katika kujaribu kuifutilia mbali kalenda ya
uwongo, kuna utaratibu mwingine wowote wa kuupata mwezi mpya (wa Abibu)
ulionenwa mwaka 1930 na kugawanya mara 100 ya mizunguko (miaka 19) ili kupata
“uwezekano” wa kusulibiwa siku ya Jumatano? Kinatokea nini kwenye saa ambayo
mzunguko wa Meton unapokoma? Sijaribu kuiweka siku nyingine ya kusulibiwa (au
mwaka), bali ni kukitafuta kile ambacho kalenda zingeweza kuashiria kuwa huenda
ni katika miaka ya...26-31AD.
Jibu: Uko sahihi kwa hilo kwamba mzunguko wa miaka 19 umekwisha kwa takriban
masaa mawili. La msingi ni kujaribu kutumia mizunguko ya mara 100 kufikia siku
ya kusulibiwa (tangu mwaka 1931) ilitumiwa na ushirika wa Worldwide Church of
God. Walikuta kwamba haikuwa siku ya Jumatano isipokuwa kwenye utaratibu wa mwezi
Aprili, na hivyo kuamua siku ya maadhimisho ya Pasaka kulikofanywa tarehe 25
Aprili mwaka 31 BK. Haikuwa kipindi kama hiki cha kabla tangu karne nyingi
Kabla ya Kuzaliwa Kristo na kabla ya kipindi cha Hekalu.
Sababu
iliyowapelekea kufanya hivyo ilikuwa ni kwa sababu waliamua kuwa huduma ya
Kristo ilidumu kwa miaka mitatu na nusu ili kujikita na kipande kingine cha
unabii wa uwongo. Hii kinyume chake ilisababishwa na kushindwa kwao kupangilia
ujenzi wa Hekalu kisahihi, kutokana na makosa ya kitafsiri ya Danieli 9:25
kwenye tafsiri ya biblia ya KJV. Kwa hiyo waliliweka tukio hili mwaka wa 31 na
sio mwaka 30 BK, kama maelezo au hadithi ya Biblia inavyoonyesha.
Vipindi halisi
vya nyakati za Kusulibiwa na kalenda kwenye miaka ya 27-33 BK vimeelezwa kwenye
jarida la Majira Kusulibiwa na Kufufuka (Na. 159). Wakati sahihi wa utaratibu na shughuli za
Hekalu unakutikana kwenye jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Tena wa Hekalu (Na. 13).
Najua kuwa siku ya 1 Abibu ni Mwaka Mpya wa
Kibiblia, lakini tunapouchukulia mwaka wa Yubile unahesabiwa kuanzia siku ya
Upatanisho ya mwaka mmoja hadi siku nyingine ya Upatanisho ya mwaka unaofuatia,
je tunapaswa kuhesabia mwaka wa utoaji zaka zetu tangua mwezi wa 7? Kwa miaka
mingi, wengi wetu tulio kwenye Makanisa ya Mungu tumekuwa tukiyaacha mashamba
na bustani zetu zipumzike katika mwaka wa 7, ila tumekuwa hatufanyi hivi kwa
wakati huohuo mmoja kama inavyotuagiza Biblia. Je, tunapaswa kuanza kuhesabu
mwaka wa 1 baada ya kubatizwa kwetu, au ni kwenye Sikukuu gani ya Vibanda
tunayopaswa kuihesabia?
Jibu: Mwaka wa kutoa zaka ni wa namna ileile kama mwaka wa kawaida tu unaoanzia
siku ya 1 Abibu. Licha ya maelezo na ufafanuzi kwenye Mishnah, Sabato kwa
mujibu wa mzunguko wa Yubile na mwaka wa mwisho wa Sabato uliofanyika mwaka
1998 tangu mwezi wa Abibu (1/1/21/40) hadi mwezi wa Abibu wa mwaka 1999 au
1/1/22/40. Mwaka wa tatu ni mwaka wa utoaji zaka ambao kwao zaka ya pili
inatolewa kwenye kanisa ili kuwasaidia maskini na wa kuadhimisha sikukuu
malangoni mwetu.
Mchakato huu wa
mzunguko utaendelea hadi mwaka 2026 katika mwezi wa Saba itakapopigwa baragumu
ya kutangazwa kwa siku ya Upatanisho, na mwaka huo utaendelea hadi siku ya
Upatanisho ya mwaka 2027, ambao ni mwaka wa Yubile. Tangu siku ya 21 ya mwezi
wa Saba wa mwaka wa Yubile ardhi yote itarejeshwa kwa wenyewe, na ndipo
harakati za kilimo na kupanda zitaanza kwa ajili ya mavuno ya mwaka wa Kwanza
wa Yubile Mpya ya wakati wa Pasaka ya mwaka wa 2028. Habari zii imeandikwa kwa
kina kwenye majarida ya Utoaji Zaka (Na. 161);
Torati na Amri ya Nne (Na. 256) na lile la Kalenda ya Mungu (Na. 156).
Naamini na kuelewa
unayofundisha kwenye majarida ya CCG kuhusu Kalenda, bali sielewi jinsi
unavyokitumia kipindi cha kutoonekana mwezi. Siku hii ya kutoonekana mwezi
inaweza kuishia tangu siku 1.5-3.5 katika Mashariki ya Kati? Pia, ni nini
kuhusu uivaji wa shayiri au shayiri mbivu (masuke mabichi) inayoashiria mwanzo
wa mwaka, yaani mwezi wa Abibu? Napenda kama ugeitumia Kalenda ya Karaite.
Jibu: Kipindi na utaratibu huu wa siku
isiyoonekana mwezi ni mtingo unaotokana na tukio la elimu ya ya kuhesabu miaka
mapema na ilihesabiwa hivyo hata kipindi au wakati wa Nuhu. Siku za kila mwaka
za Wachina zinaichukulia hii kuwa ilianzishwa kwenye millennia ya tatu KK na
mtu aitwaye Hwang Ti, mtu wanayemuita mfalme wa Manjano. Utaratibu wa kuhesabu
vipindi hivi vya kutoonekama mwezi na kupatwa kwa jua au mwezi kuwa ni lazima
kushindwa kwake kufanya hivyo kuliadhibiwa. Hakuna shaka kuwa taratibu hizo
zilitumika na kuhesabiwa kipindi chote cha zama za Hekalu, kama utaratibu
huohuo ulitumiwa huko na huko Uchina pia na ulianzishwa na Nuhu. Yaonekana kuwa
inawezekana Shemu alitawala akiwa kama kuhani wa Melkizedeki huko Yerusalemu.
Ulimwengu wote ulitawaliwa kwa kalenda hii hadi kuanzishwa kwa dini za waabudu
jua. Pia tazama kwenye jarida la Melkizedeki (Na. 128).
Wasamaria walihesabu kwa kukichukulia kipindi hiki cha kutoonekana mwezi
hadi leo, kama tufanyavyo sisi na walivyofanya Masadukayo kipindi cha Hekalu.
Walishika huduma za Hekalu kila mara isipokuwa katika miaka tisa chini ya
Malkia Alexandra wakati Mafarisayo waliposhika shughuli za Hekalu, lakini
hawakuingilia kati suala la kalenda, kama utaratibu wao wa kuanzia siku hii ya
kutoonekana mwezi ulikuwa haujaanza. Kanisa limekuwa likichukulia kipindi hiki
cha kutoonekana mwezi kwa kipindi cha miaka 2000 sasa. Liliipuuzia na kuikataa
kalenda ya Hilleli mwaka 358 na kuichukulia kuwa ni uzushi mpotovu wa Wayahudi.
Uzushi wa Karaite ulioibuka kipindi cha zama za kati haukukubalika kabisa na
kanisa na mafunmdisho yake yalikuwa kinyume sana nay ale ya kanisa, ni kama
ilivyo sasa.
Wapagani badi wanalazimishwa kuanzisha majedwali au michoro yao ya mduara
yanayolingana na mzunguko wa siku hizi za kutoonekana mwezi na mienzi mwandamo
mbali na kalenda ya jua, na Karaites hawakuyachukulia pamoja na wavuzi
wasioelewa. Masuke ya kijani ya shayiri, yalikuwa ni masuke yasiyoiva, na
yanakatwa yanapokuwa ya kijani na kuhiniwa. Na ndiyo maana yanaitwa “masuke ya
kijani.” Ikiwa hujawahi punje hii isiyovunwa basi ungeelewa. Mganda wa
Kutikiswa unawakilisha mwanzo wa Malimbuko, ambaye ni Yesu Kristo,
aliyekatiliwa mbali akiwa mbichi na wakijani kupungwa kuashiria mwanzo wa
Kipindi Maalumu cha kuhesabu Kuelekea kwenye Pentekoste. Tazama jarida la Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa (Na. 106b).
Mafundiho mapotofu na ya uwongo ya Karaite yanatokana na hamu au nia ya
kukataa mafundisho ya ukenyeufu ya kalenda ya Hilleli, lakini pia kunatokana na
hali mbaya ya kutojua historia ya Hekalu na kwa dhahiri kabisa kuwa ni hali ya
kutojua kabisa historia ya Kanisa. Nasi pia tumekuwa tukiishika kalenda hii hii
kwa kipindi cha takriban miaka 2000 pamoja na kipidi chote cha Hekalu. Tunaijua
aina ya kalenda gani ilikuwa inatumiwa Kanisani kipindi cha Matengenezo kama
ilivyoandikwa na Rabbi Samuel Kohn kwenye kitabu chake cha Wasabato wa Transylvania (CCG Publishing, USA, 1998). Ushawishi wa
Wayahudi ulipelekea kuanzishwa kwa kalenda ya Hilleli baadaye. Kalenda ya
Hilleli, pamoja na utaratibu wake wa uahirisho, iliingizwa kanisani karne hii.
Mafundisho haya ya kizushi ya Karaite hayakukubaliwa kabisa wala kufuatwa na
Kanisa la kweli la Mungu, wala haijawahi kufanyika hivyo. Majarida yafuatayo
yana mrengo mmoja wa kufanana: Kalenda ya Mungu (Na. 156); Mwezi Mwandamo na Mwaka Mpya (Na. 213); na Kalenda na Mwezi Mwandamo: Ni Uahirisho au Sikukuu (Na. 195).
Pasaka
Unaweza tafadhali kuelezea kwa kina kuhusu kipindi
cha wakati muafaka cha Usiku wa Kuuangalia sana na ni mambo gani yunayopasa
kuyatenda?
Jibu: Wakati wa kusulibiwa unaelezea ni wa namna gani. Siku ya 14 Abibu, Kristo
na mitume aliingia kwenye mahali pa muda kama ilivyohitajika kwenye Kumbukumbu
la Torati 16:5-6. Waliuandaa mlo wa maandalizi kwa pamoja na kuanzisha Ushirika
wa Meza ya Bwana jioni ile, ambayo kanisa linawajibika kuendeleza kuula usiku
ule kila mwaka, na ndivyo lilivyoweza kufanya kwa muda wote wa takriban miaka
elfu mbili.
Kristo alikamatwa
na kuteswa na kusulibiwa. Aliuawa kwenye kipindi kilekile halisi ambacho
Mwanakondoo aliuawa kwa ajili ya Pasaka mwishoni mwa siku ya 14 Abibu. Jioni
ile ulianza mlo wa Pasaka ambayo kwamba alifanyika kuwa kondoo mbadala. Usiku
wa Kuuangalia sana unaanza kwa kula mlo maalumu siku ya 15 Abibu na kanisa
linatarajia kuitumia jioni ile kwa kukusanyika na kujifunza au kusoma.
Asubuhi
waliruhusiwa kurudi makaoni mwao na kuhudhuria ibada ya Siku Takatifu ya Kwanza
ya Mikate Isiyoliwa na Chachu. Watu wengine wanaichukulia siku hii kuwa ni
usiku unaotumika wa kuangalia sana hadi mapambazuko yake. Matokeo ya kawaida ni
kwamba kama mtu akikaa hadi mapambazuko, basi ibada za Siku Takatifu hazitaweza
kupangiliwa siku kwa mkoromo wenye mlio mdogo.
Hata hivyo, ni
vizuri na sahihi sana kwenda kulala mapema ama kuwa ni sehemu tu. Inapasa
kutumika kwa matarajio na kwa kumsifu Masihi. Wasamaria wangali bado
wanayashika mapokeo haya kila mwaka, na walipoweza waliweza kuadhimisha kwenye
Mlima wa Gerizim.
Nahitaji kusoma zaidi kuhusu Kanuni ya Kuhesabu
siku za kuelekea Idi ya Majuma nay a Mganda wa Kutikiswa. Sielewi kiusahihi
hivi ni vitu gani. Nitajisomea wapi kwenye Maandiko Matakatifu kuhusu kipindi
sahihi cha kumla Mwanakondoo wa Pasaka? Pia kwa kufanya mdhanio, aya zilizo
kwene tafsiri zangu za KJV na NKJV ni za kughushiwa?
Jibu: Hapana, aya hizo zinaelezea mambo kwa mitazamo tofauti na Marko hajaliweka
wazi jambo hili. Yohana ameainisha vizuri. Majarida muhimu ni: Kalenda ya Mungu (Na. 156); Siku Takatifu za Mungu (Na. 97); Sadaka ya Mganda wa Kutikisa (Na. 106b); Kanuni ya Kuhesabu Kuelekea Sikukuu ya Pentekoste
(Na. 173); Roho Mtakatifu (Na. 117); na Torati na Amri ya Nne (Na. 256).
Mimi ni mwanamke mtu mzima ambaye hawezi
kuhudhuria kwenye sikukuu ya Pasaka na wengine. Kwa kuwa siwezi kuhudhuria
kwenye Sikukuu na kuoshwa miguu yangu, nitakuwa naoshwa kutokana na dhambi zote
nizitendazo kila siku kwa njia ya toba? Ni nini basi maana ya alama ya mkate na
divai?
Jibu: Torati inawataka wanaume wote kujihudhurisha kwenye sikukuu mara tatu kila
mwaka. Wanawake wanaruhusiwa kuiadhimisha Pasaka majumbani mwao, kama watakuwa
wanaumwa au wakiwa wazee. Hata hivyo, siku za 14 na 15 Abibu hazitakiwi kulala
majumbani au malangoni mwetu kwa mujibu wa Torati (Kumbukumbu la Torati
16:5-7). Yakupasa kuondoka kuoka makaoni mwako na waweza kurudi asubuhi yake,
ambayo ni Siku Takatifu ya Kwanza ya Mikate Isiyotiwa Chachu.
Ulaji wa Mez ya
Bwana unafanyika sambamba na ibada na inaweza kufanyia peke yake. Hata hivyo,
inapendekezwa kujihudhurisha kwenye Pasaka ili kwamba mwili wa Kristo uwe
pamoja na uweze kukua katika roho. Kama utakuwa umelindwa kwa shuruti ya
kimazingira ndipo unaweza pia kushiriki Pasaka mwezi unaofuatia ambao ni Mwezi
wa Pili.
Katika mwaka wa
tatu, sikukuu zinaweza kuadhimishwa majumbani ambao ni mwaka unaotolewa zaka ya
tatu, ambayo inatolewa maalumu kwa wasiojiweza au kuwasaidia ndugu walio kwenye
uhitaji mwaka huo. Mwaka 2001 utakuwa ni wa utoaji wa zaka hii ya tatu. Soma
majarida ya: Torati na Amri ya Nne (Na. 256); Pasaka (Na. 98); Mchakato wa Mlo wa Meza ya Bwana (Na. 103B); Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa (Na. 106b). Kuna mlolongo mwingine wa majarida
yanayohusu Pasaka na Mkate Usiotiwa Chachu.
Kama tunaishika Pasaka kama Kristo alivyofanya
itatupasa kuoshana miguu? Kama ni hivyo, hii inamaana gani?
Jibu. Ndiyo, inatupasa na tunapaswa kuoshana miguu kwenye maadhimisho haya ya
Pasaka. Neno lililotumika lilikuwa ni titheni
ambalo linamaana ya kujinyenyekesha na kujitoa mtu ili kuwatumikia wenzake
ambayo ndiyo tabia na mwenendo unaotupasa kuuendeleza. Soma jarida la Maana ya Kuoshana Miguu (Na. 99). Hii ni sehemu ya mlolongo wa majarida ya Pasaka.
Nakumbuka kuwa ushirika wa watakatifu kutoka utoto
wangu; lakini ni nini hasa jambo hili na ni vipi na lini limeanza jambo hili?
Jibu: Dhana ya kwamba Ushirika wa Watakatifu ulianzishwa kwa Mlo wa Meza ya
Bwana siku ya 14 Abibu, wakati kanisa la Agano Jipya lilikutanika kila mwaka
ili kuamsha hali yao katika Roho Mtakatifu. Dhana hii ilienea kwa kufanya
utaratibu wa kushiriki ushirika wa meza ya Bwana kila juma kulikofanywa katika
karne ya pili, na maji yaliajumuishwa sambamba na mvinyo, jambo linaloonekana
kuwa linatokana na imani au dini ya Mithras, kama ilivyokuwa jina la Baba.
Wakati huo, mvinyo haukujumuishwa pamoja na makasisi wa Kanisa la Kirumi. Soma
jarida la Malumbano na Hoja ya Wakuartodesiman (Na. 277) ili kujisomea kwa kina zaidi kkuhusu
malumbano yaliyojiri kwenye karne ya pili na kuendelea.
Kanisa
Iwapo kama siu takatifu zote, maadhimisho na
mapokeo ya ulimwengu yanatokana na vyanzo vya kipagani, ni siku zipi basi
Wakristo wanapaswa kuzitakatifuza na/au kuziadhimsha?
Jibu: Biblia iko wazi sana kwamba ni siku zipi tunazotakiwa kuzishika, nazo ni
Sabato, Mwezi Mpya na Sikukuu. Sabato ni Siku ya Saba ya Sabato na sio Siku ya
Kwanza ya juma au Jumapili, ambayo imefungamanishwa na utaratibu huohuo wa
ibada, kama ilivyo Krismas, inayotokana na dini za waabudu Jua.
Kristo na Kanisa
walishika maadhimisho yote ya Sabato, Mwezi Mpya na Sikukuu (kama isemavyo
Wakolosai 2:16). Sikukuu zenyewe ni: Mwaka Mpya (1 Abibu); Mfungo wa Saumu kwa
ajili ya dhambi au Makosa ya Kupotoshwa (7 Abibu); Ushirika wa Meza ya
Bwana/Pasaka (14 Abibu); Usiku wa Kuuangalia Sana (15 Abibu); Siku ya Kwanza ya
Mikate Isiyotiwa Chachu (15 Abibu); Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa (Jumapili
iliyo ndani ya kipindi hiki cha Pasaka na Mkate Usiotiwa Chachu); Siku ya
Mwisho ya Mikate Isiyotiwa Chachu (21 Abibu); Idi ya Majuma au Pentekoste (Siku
ya Sabato na Jumapili ya siku ya Hamsini yangu siku ya Mganda wa Kutikiswa);
Siku ya Upigaji wa Baragumu (Mwezi Mpya wa Mwezi wa Saba)); Siku ya Upatanisho
(Siku ya Kumi ya Mwezi wa Saba); Sikukuu ya Vibanda (Inaanzia Siku ya Kumi na
Tano ya Mwezi wa Saba); Siku Iliyokuu ya Mwisho au Siku ya Mkutano wa Makini
(Siku ya 21 ya Mwezi wa Saba).
Hizi ndizo
Sikukuu za Bwana. Tutafaidika kwa kusoma majarida ya Kalenda ya Mungu (Na.156); Siku Takatifu za Mungu (Na. 97); Mwezi Mwandamo na Mwaka Mpya (Na. 213); Sikukuu za Mungu Jinsi Zinavyohusiana na Uumbaji
(Na. 227); na Chanzo cha Krismas na Easter (Na. 235). Kuna majarida pia yaliyoandikwa kwenye
kila Sikukuu zilizotajwa hapo juu.
Unamaana gani usemi huu kwamba “hakuna mtu
atakayeurithi ufalme wa Mungu” iwapo kama hakuna mtu atakayekwenda mbinguni na
kila mtu atafufuliwa na kupewa fursa ya pili? Je, kutakuwa na hukumu nyingine
yoyote zaidi ya ile ya kufngwa gerezani katika ulimwengu huu wanayopewa
wabakaji na wauaji? Najua kwamba ni mapenzi ya Mungu kuwa asiwepo mwenye mwili
atakayepotea, lakini watu wengine ni waovu kupitiliza.
Jibu: Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wa sura yake. Waliumbwa kwa namna hiyo
na kupewa uhuru wa kuchagua au kufanya maamuzi. Shetani alikuwa ni kerubi
mkamilifu aliyetiwa mafuta. Alichagua kutenda dhambi. Hakuna aliyemuovu kiasi
cha kutoweza kuokolewa. Na hii ndiyo sababu iliyomfanya Kristo afe. Hata
Shetani atapewa fursa ya kutubu.
Kipindi cha
ufufuo wa pili kimewekwa kwa ajili ya ukarabati wa hali nzima yote ya
mwanadamu. Ni watu wale tu wanaoweza kuona na kusamehe na kuwaelekeza kwa
kuwaonya au kuwarudi wengine wanastahili kuingia kwenye Ufufuo wa Kwanza wa
wafu. Na ndiyo maana Kristo
alisema “Baba wasamehe, maana hawajui watendalo.” Stefano aliomba kwamba
wasihesabiwe makosa. Kama kungewezekana, watesaji wakubwa hapo wangeweza
kuukataa Wokovu na nusu ya Agano Jipya lisingeweza kuandikwa. Mhemko mkuu wa
kitendo cha kumpiga mawe Stefano na shuhuda maalumu alikuwa ni Sauli wa Taso.
Tunamjua sasa kama Mtume Paulo.
Kanisa lilidhani
kuwa alikuwa muovu asiyeweza kubadilika. Ni kweli kwamba Paulo aliwauua au
kuwatesa wengi wao ili kuhalalisha nadharia yake. Watu wanaodhani kuwa wengine
wanakwenda kuungua motoni jehanamu au wanaotaka iwe hivyo hawafai kuuingia
Ufalme wa Mungu. Soma majarida ya: Kondoo Aliyepotea na Mwana Mpotevu (Na. 199); Hukumu ya Mapepo (Na. 80); Nafsi Hai (Na. 92); Ufufuo wa Wafu (Na. 143); Mji wa Mungu (Na. 180).
Je, Kanisa lina mamlaka yoyote lililopewa kwa
namna yoyote ile na Mungu au Yesu Kristo ya kubadilisha mafundisho? Kama ni
hivyo, imeandikwa wapi? Pia ni je, Biblia ni mamlaka kamili, au ni mafundisho
ya kanisa, maandiko, na mafundisho ndiyo mamlaka kamili?
Jibu: Hapana, kanisa halina mamlaka yoyote ya kuzibadilisha Amri za Mungu.
Kristo alisema Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi
zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa
mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika
ufalme wa mbinguni. (Mathayo
5:19).
Kristo alianzisha
Kanisa lake na kuna aina nyingi za uongozi na utendaji kazi, lakini Bwana ni
mmoja. Wamepewa mamlaka ya kuliongoza Kanisa kwa kufunga na kufungua lakini
hawana mamlaka ya kubadilisha Sheria au Torati ya Mungu au kupotosha kwa namna
yoyote ile.
Unaweza kusema kuwa kuna michakato mingi ya
kufanyika Mkristo na inaanza kwa kuamini kwamba Kristo alizaliwa na mwanamke
bikira na alikufa mtini kwa ukombozi na ondoleo la dhambi?
Jibu: Kama Mkristo, mtakatifu ametajwa kwenye Ufunuo 12:17 na 14:12. Hawa ni wale
wazishikao Amri za Mungu na Ushuhuda au Imani ya Yesu Kristo. Mchakato wa
kufanyika kuwa Mkristo umeandikwa kwenye Warumi 8:29-30. Wakristo wameitwa na
Mungu.
Wamakusudiwa na
kujulikana tangu mwanzo kwa uweza wake wa Usioshindwa na kitu chochote ili
afanane na sura ya Mwaa wake. Wamechaguliwa na kisha kuitwa. Mara tu wanapoitwa
na Roho Mtakatifu kwa mujibu wa Uweza usioshindikana wa Mungu, ndipo wanaletwa
kwa Kristo na kuandaliwa kwa ajili ya ubatizo. Kisha mara tu baada ya kubatizwa
kwenye mwili wa Kristo, Roho Mtakatifu anakuja juu yake akiwa kama malipo
stahili yake kwa kupewa roho ya kufanyika mwana.
Watafanyika kuwa
wana wa Mungu waliozaliwa mara ya pili. Wanahesabiwa haki kwa imani na kuupata
wokovu wao, ambao umetolwa bure kabisa kwa neema, kwa kuitii Sheria au Torati
ya Mungu kwa matendo. Imani bila matendo imekufa. Wamebadilishwa kwa kupitia
Ufufuo wa Wafu wakiwa kama wana wa Mungu na hivyo kutukuzwa. Mchakato huu
umeainishwa kwa kina kwenye majarida ya Kuzaliwa Mara ya Pili (Na. 172); Roho ya Kufanywa Wana (Na. 34); Toba na Ubatizo (Na. 52) na Ufufuo wa Wafu (Na. 143).
Je, watu walioonyeshwa
ukweli na kuukubali wanahukumiwa sasa? Kama watu walioweka mikono yao ili
kulima, wanaamua kutembea au kwenda mbali zaidi na kwenda ulimwenguni tena, (na
kufa nafsi yake), je hii haisababishi kutenda dhambi isiyosameheka? Je, Mungu
anatoa fursa hii ya pili?
Jibu: Biblia inatuambia kuwa tumepewa fursa
mbili za kuamua. Tatizo pia lipo kwenye mamuzi na wito. Daudi alitenda dhambi
na bado akawa mfalme wa Israeli kwenye Ufufuo wa Kwanza. Dhambi isiyosameheka
ni ile ya kumkataa au kumkufuru Roho Mtakatifu. Wale walioteuliwa wako hukumuni
sasa. Kama watashindwa watarudi kwenye Ufufuo wa pili au ufufuo wa jumla wa
wote wa Wafu. Wale waliojulikana na kukusudiwa na Mungu na kuwachagua anawaita
na kuwahesabia haki na kuwatukuza (Warumi 8:29-30). Kwahiyo hawawezi kushindwa
kwa kuwa wamechaguliwa akijua hawatashindwa. Walioitwa ni wengi bali wateule ni
wachache. Hilo ndilo lengo na
hatima yake. Umepewa uhuru wa kuamua. Kama unasikia wito na kuja, bali
kushindwa kufanya hivyo sio Mungu anayekusababisha wewe ushindwe au amtoe Roho
kutoka kwako. Mapenzi yako mwenyewe au maamuzi yako yanafanya hayo. Baadae
chini ya utaratibu mkamilifu zaidi tumepewa sote fursa ya wokovu.
Kuitwa au kuchaguliwa, je, hii
ni tofauti kati ya wateule na wateule walewale?
Jibu: Hapana. Mteule ni yeye aliyechaguliwa na
Mungu. Neno “mteule yuleyule” maana yake ni “mteule halisi”. Neno “mteule” lina
maana ya “kuchaguliwa”" au “kuteuliwa.” Mungu huchagua na tumeitwa kwa
msingi wa kujulikana kwetu tangu mwanzo. Kuna wengi wanaosikia wito lakini
hawajachaguliwa. Wanaangukilia mbali kama ulivyo mfano wa mpanzi. Mungu anajua
kuwa watashindwa lakini anawapa Roho Mtakatifu wamuombapo kwa namna yoyote kama
alivyoahidi kwa kupitia watumishi wake manabii. Mungu hana upendeleo. Hili
ndilo lengo lake zima kwa uhuru wa kuamua na uamuzi kwenye wito wa Mungu.
Inaonekana kwamba mapokeo ya
Kanisa la Mungu ya kushika Siku Takatifu yanaugeuza Ukristo kwenye uzoefu wa
kiakili. Hapo kunatakiwa kuwa na imani, ndoto za kinabii, umoja, furaha, na
ushindi na sio suala tu la kutafsiri Maandiko. Nasikia kuhusu dini za siri za
Kibabeloni na nasikia kwamba mapepo yanaweza utenda mambo na hata kuponya.
Sijawahi kabisa kuponywa na Mungu wala na mapepo bali nimeshagawahi kuumia. Zio
wapi ishara hizi za miujiza Kanisani? Yuko wapi Mungu? Hajajidhihirisha kabisa
kwangu na simuoni.
Jibu: Inaweza kuwa ni uzoefu tu wa kiakili
ukijaribu kuunda ukweli utokanao na viinimacho au ulaghai na maneno ya uwongo
ya waamini Utatu. Walishindwa. Wengi hawakujua kile walichokiamini na
walijipenyeza na kudharauliwa au kupuuzwa na mawakala wa dini za waamini Utatu.
Kanisa letu linaundwa kwa muungano wa bodi ya watu, waliotawanika
ulimwenguni kote na kwenye nchi nyingi, waliojitoa kikamilifu na waadilifu
wanaojitahidi kumtii Mungu kama alivyoyadhihirisha mapenzi yake kwa kupitia
Manabii. Wengi wetu wamekuwa wameumizwa. Wengi wetu tumeponywa, na wengi wetu
hawajaponywa pia. Kuna wale walioponywa zaidi kwa kutakaswa zaidi ya wale ambao
hawajaponywa bado? Ni Mungu tu ndiye ajuaye jibu lake. Inaonekana kuwa wengi
wameiacha njia waliyopo kama kipimo cha kujihesabia kwao haki wakijilinganisha
na wengine.
Makanisa ya wasika Sabato yamekuwa yakiendendelea kwa kipindi cha miaka
elfu kadhaa kupita kwenye kambi za mateso yajulikanayo kama Holocaust kwa kuwa
walikuwa wanaishika Sabato, Sikukuu za Mungu na Sheria za Uiajl Vyakula na
waliwekwa kwenye daraja la Wayahudi. Kuna kundi na vitengo maalumu
vilivyotengwa kwa ajili yao kwenye kambi hizi za mateso. Kulikuwa na mateso ya
kuwaning’iniza vichwa chini na kuwanyonga au vyumba vya kuwanyima hewa kwa kile
kilichoitwa “Bibelforscher.” “Watafiti” hawa wa Biblia walikomeshwa na
kuondolewa. Haukuwa uzoefu tu wa kiakili. Ni wale waliojitoa tu ndio waliishika
imani na kufa. Soma jarida la Kazi ya Amri ya Nne Kwenye Historia
ya Makanisa ya Mungu ya Washika Sabato (Na. 170).
Washika Sabato wa huko Bektashi waliotokomezwa tu. Mamilioni ya Waarmenia
walitolewa nje na kuuawa kwa kuiigwa risasi. Washika Sabato wa Transylvania
waliteswa kwa kipindi cha karne nyingi na hata hawakuruhusiwa kumiliki mitambo
ya kuchapishia wala chombo cha habari. Waliandia nyaraka zao mara kumi kwa
mokono na kuzipeleka nakala hizo kwa kwenye maeneo kusudiwa kumi. Wote
walifanya hivyo kwa kuwa walimpenda Mungu na walipenda kumtii na kumheshimu
yeye. Unapotendea kazi kile ulichopewa kukielewa, Mungu atakupa mambo zaidi ya
kuyajua.
Mungu kwa sasa hashughuliki na kuuhukumu ulimwengu huu. Bali bado upo chini
ya mungu wa ulimwengu huu, Shetani. Unauona ulimwengu huu karibu ujiangamize
kabisa wenyewe kabla ya miaka mingine ishirini ijayo, na itapasa ijengwe tena.
Hilo halitakuwa kosa la Mungu. Ataruhusu hili ili kutuonyesha kinachotokea
tunapokuwa hatuzitii na tunaziasi Sheria zake. Biblia inasema wazi kitu kimoja:
Mkabidhi Mungu njia zako, naye atazithibitisha, hakuna njia nyingine yoyote
karibu. Tii kile ulichopewa kwanza na kisha utapata uelewa mwingi zaidi. Kuifia
imani si kitu kingine bali zoezi la kiujuzi.
Sabato au Jumapili
Ni ushuhuda gani hapo, zaidi ya ukusanyaji wa
ujumla uliomchukua Paulo mbali na Yerusalemu kwenye Agano Jipya na
kinachoonekana kuwa alikuwa Roma mwaka 150 BK, kwa ibada yoyote ya Jumapili
kwenye Kanisa la Karne ya Kwanza?
Je, ushahidi huu unawezaje kukanushwa kama ni
upotoshaji au uvunjaji wa Sabato na kupelekea kuanza kwa ibada za Jumapili?
Ni ushahidi gani ulioko hapa kwenye Agano Jipya na
mahala pengine popote kukanusha mtazamo kinyume na kwa Sabato, Mwezi Mpya na
Sikukuu za Biblia?
Jibu: Watrinitarian waabudu Jumapili kwa kawaida wanadai kwamba Agano Jipya
linaashiria kwamba Wakristo wa jamii ya Kiyahudi walishika siku zote mbili,
yaani siku ya saba na siku ya kwanza ya juma na kuzichukulia kama siku takatifu.
Hakuna mashaka kwamba Krsto mwenyewe aliishika Sabato na Sikukuu zote, Mwezi
Mpya na Siku nyingine zote Takatifu zilizoadhimishwa kipindi cha Hekalu na
ndivyo walivyofanya mitume wote wengine. Paulo alihubiri kwenye sinagogi siku
ya Sabato. Ilikwa ni kwa ajili hii ndipo aliagiza changizo la kuwasaidia
wapendwa wa kanisa la Yerusalemu lifanyike siku ya kwanza ya juma, jambo
linalodaiwa na wapotoshaji kwamba Wakristo Wamataifa walikuwa wanakusanyika
kufanya ibada siku hii ya kwanza ya juma. Hii inatokana na kulitafsiri vibaya
andiko la Matendo 20:7. Hii ilidaiwa kuwa ni kama siku ya pili takatifu na
iliitwa siku ya Bwana ili kuitofautisha na Sabato. Wengine hata wanajaribu
kudai kwamba huenda ilikuwa ni siku moja tu ya pekee iliyokuwa inatumiwa kuiadhimisha
na waongofu Wamataifa. Madai haya ni ya ueongo kabisa. Andiko la Matendo 20
linaitaja inayojulikana kama the mia ton
Sabbaton ambayo kama asemavyo Bullinger kuwa ni siku “Sabato ya kwanza kati
ya nyinginezo” na inamaanisha kuwa ni juma la kwanza la Mchakato wa Kuhesabu
kuelekea Pentekoste tangu siku ya Mganda wa Kutikiswa. Inadhaniwa na kuaminika
kuwa ni Siku ya Kwanza ya Juma kwa kuwa inaendana na masomo ya siku ya Jumapili
kuifanya iwe namna hiyo. Ni maelezo hayohayo yapo kwenye Yohana kwamba ni siku
ya Mganda wa Kutikiswa baada ya kufufuka kwake.
Ibada ya Jumapili
haikuingia wala kuwepo kanisani hadi mwaka 111 BK kutoka Roma. Wakolosai 2:16
inaonyesha walikuwa wanazishika Sabato na Miezi Mipya na Siku Takatifu na Paulo
anasema kwamba mtu na asiwahukumu kwa ajili ya wao kuzishika siku hizi. Kwa
hiyo inaweza kuonekana kwamba kanisa la Kolosai lilikuwa linazishika siku hizi
na maagizo yote ya Biblia.
Uhakika
unaotakiwa mara zote kama kigezo ni “Mafundisho ya Mltume Kumi na Mbili” na
madai yanayosisitizwa sana yamefanywa kutokana na tarehe zao za mwanzo katika
kuanzisha mchakato wa kwenye karne ya kwanza ya kuinganisha na ibada za
Jumapili kama inavyosemwa kuhusu Siku ya Bwana na kuendelea kuitaja hivyo hadi
siku hizi na kuiona kama kutaniko takatifu na la kuumega mkate (sura ya 14).
“Mitume Kumi na Mbili” wanaunganishwa kwenye Katiba ya Mitume na na hueanda wana asili ya kisyria. Tafsiri ya
ANF inaiweka hii kwenye Toleo au Gombo la Saba pamoja nao na hata jopo la
kitivo cha waabudu Jumapili wanaojadili umahiri na weledi wa kuhesabu na
mishikamano. Iwapo kama ingechukuliwa kiuweledi na kiumakini sana kuwa ni
kwenye karne ya kwanza, basi ingekuwa kwenye toleo la 1. Sio ni kwa sababu
imekuwa ni upotoshaji wa hivi karibuni kusaidia dhana ya ibada za Jumapili
pamoja na mafundisho mengine ya kizushi yaliyoingizwa kanisani.
Kile kinaoitwa
kuwa ni Waraka wa Ignatius kwa Wamagnesians (ANF, vol. 1, p. 63) ni mfano wa
kwanza wa rejea hiyo na weledi wa kiusemi wa muundo mrefu zaidi unaoashiria
kuwa uliandikwa kwa weledi sana ili kuanzisha matendo ya uko nyuma. Inaonyesha
kwamba Sabato ilikuwa inatunzwa pia bali aina ndefu zaidi ni jaribio la
kuanzisha dhana ya kuifana Siku ya Nane kuwa Siku ya Bwana, ambayo haipo kabisa
kwenye majisifu makubwa ya aina fupi.
Rejea inafanywa
kwa Pliny kusaidia ibada za Jumapili; hata hivyo, mamlaka ya kanisa yenyewe
yanaonyesha kwamba Sabato ilishikwa ulimwenguni kote. Ni katika Roma na
Alexandria peke yake kitendo hiki cha undumila kuwili kilifanywa.
Justin Martyr
(yapata kama 150-154 BK) anaelezea ibada ya kidini ya Wakristo wa kwanza,
maadhimisho yao ya sakramenti, nk, katika :siku ya kwanza.” Ni kweli kwamba
Justin Martyr anaitaja ibada ya Siku ya Bwana kwenye kitabu chake kijulikanacho
kama Utetezi wa Kwanza, yaani First Apology (ANF I, 186) lakini anasema wazi pia kwamba walikuwa wanakusanyika
siku za Sabato pamoja na kwenye Mdahalo
wake alioufanya na Trypho. Anasema kwamba sheria mpya inakutaka kuzishika
Sabato za milele kwa kuzitubia dhambi zote na hivyo kuifanya kila siku kama
Sabato (Sura ya 12 ANF I 200). Kwenye
Mdahalo wake na Trypho anaonyesha kwamba wanajadili dhana ya Seabato na Sikukuu
na inaonekana kwamba malumbano dhidi ya Sikukuu yalitokea Roma katikati ya
karne ya pili walipokuwa wanaiigiza sikukuu ya kipagani ya Easter (sura ya
XVIII ibid. p. 203). Jumapili iliingizwa pamoja nayo na kwanza iliiondoa au
kupotosha maadhimisho ya Pasaka na kuipa nafasi kubwa Easter na kisha ikaiondoa
Sabato yenyewe.
Justin
anashughulikia mapokeo ya Trypho kama vile unywaji wa maji ya moto siku za
Sabato. Anasema kuwa anafanya hivyo wakati Trypho alikuwa hafanyi. Malumbano
kuhusu mapokeo ya Kifarisayo dhidi ya roho ya sheria katika Kristo. Anaongelea
kuhusu ujio wa Masihi huko Yerusalemu na ufungaji wa saumu (Siku ya Upatanisho)
kama ulivyoelekezwa na nabii Isaya (58). Hoja ni mtazamo wa watu wa Yuda kuhusu
haki ipatikanayo kwa sheria zaidi kuliko kwa njia ya neema katika Roho
Mtakatifu.
Mdahalo au
malumbano yanajiri ktokana na kushindwa kukubwa na hivi ndivyo ilivyokuwa
kwamba Justin alikuwa ameachana na ukweli kwamba Anicetus aliyachukua au
kuyaingiza mafundisho mapotofu na yakizushi ya kipagani ya Easter huko Roma na
yalienea na kuliharibu kanisa zima. Ili kuyachukulia maandiko haya kuwa yana
nguvu zaidi ilimbidi amkemee kwa maneno makali zaidi Anicetus alishutumiwa na
Polycarp kwenye Mdahalo wa kwanza kati ya Migahalo ya Wakuartodeciman.
Ni Victor tu
(takriban mwaka 190-192) tunayemuona kuwa aliishurutisha imani hii huko Roma na
malumbano ya Wakuartodeciman yalitokea, na kuligawa kanisa (soma jarida la Malumbano ya Wakuartodeciman (Na. 277)). Polcrates hakuwa na nguvu ya kuisimamisha au
kuikataza wakati Polycarp aliyekuwa kabla yake alimudu kuzuia hila hiyo.
Irenaeus alikuwa
pia kwenye nafasi ya hatari alipokuwa anateuliwa na Smyrna askofu na
aliyefundishwa na Polycarp aliyeishika Sabato na Sikukuu zilizoamriwa kama
alivyofanya Yohana na mitume wote waliomtangulia hadi kufikia kipindi cha kufa
kwake na kuendelea, alijaribu kutunza amani na kina Victor na Polycrates na hii
ilishindikana mwaka 192.
Ni kwa waandishi
wa kipindi cha karibia karne ya pili ambao tunawaona wakiiunga mkono ibada hii
ya Jumapili na ikiendelezwa kutokana na shinikizo walililoshinikizwa kutoka
Roma. Dionysius wa Korintho aliita kuwa ni “Siku ya Bwana.” Irenaeus wa Lyons
ndiye wakati mwingine anayechukuliwa kuwa alidai kuwa Sabato ilikuwa imekoma.
Hakuna mahala panapomtaja Irenaeus aliinenea vibaya ay kuitangua Sabato.
Anaielezea Sabato kwenye kitabu chake sura ya XXIII. Ni ushahidi gani uliopo wa
kumuona kuwa hakuwa anaishika? Anafanya mtofautisho kati ya makanisa mawili ya
Yerusalemu kwenye maandiko yake. Moja ni sahihi na nyingine si sahihi.
Anaelezea jinsi
Kristo alivyoishika kiusahihi na kikamilifu na mitume na wazao wa imani ya
Ibrahimu. Anampinga Marcion
na kueleza kuwa Kristo aliitimiliza na wala hakuitangua wala kuihalifu sheria (Adv. Haer. VIII, ANF, Vol. 1, pp.
470-471). Anaendelea mbele kwa kuelezea kuwa ilikuwepo lakini mwandishi mmoja na mmoja aliishia kwenye maagano (ibid.
ch IX, p. 472). Hata hivyo, maandiko mengi yaliandikwa baada ya Mtaguso wa
baraza la Nicaea yakilenga kuipa kipaumbele Jumapili. Maandiko au kitabu
kilichoandikwa na Justin Martyr, kinamtaja Irenaeus akisihi kutopiga magoti kuabudu
siku ya Jumapili lakini wakuu wanakubaliana na utajwaji huu wa Jumapili siku ya
Pasaka. Siku hiyo ilikuwa ni ya maadhimisho ya Mganda wa Kutikiswa ambayo kwa
makosa kabisa waliiiita Easter kama inavyitwa kwa lugha ya Kiingereza (sawa na
isemavyo ANF, vol. I, p. 569 and note
9).
Injili ya Barnabus inatumika kuonyesha kwa kanisa la kwanza liliabudu siku ya Jumapili (Ep. Of Barn., ANF Vol. 1, pp. 146-147). Hii ilitumika ili kushadidia tabia na mwenendo waliokuwanao mitume na matendo yao. Hata hivyo, Injili ya Barnabus ilidaiwa kuwa iliandikwa na Myahudi wa Alexandria kipindi cha utawala wa Trajan na Hadrian (yapata mwaka 100 BK na kuendelea). Ukweli wa kwamba nia ya Hadrian ya kuujenga mji inaonekana kuwa iliainishwa kwa kina kwenye sura ya 5 (ANF inaunukuu waraka) ikiaashiria kuwa tunaongelea siku za zamani sana za kabla ya mwaka wa 100 BK na kuenda baada ya matatizo yaliyotokea mwaka 135 BK. Ukweli wa kwamba mara nyingi anaonekana au kusikika kama Mmataifa akisalimiwa kwa mshangao na wafafanuzi kwenye ANF. Sababu yake si vigumu sana kuiona. kama Wakristo walikuwa hawathaminiwi kwa kiasi kikubwa sawa na kama ilivyokuwa Sabato na Torati, basi wangefukuzwa na kuchukuliwa kama vuguvugu lililokuwepo la kidini kama wangekuwa hawaneni sawasawa na sheria na ushuhuda (Isaya 8:20). Alexandria kulikuwa ni kitovu cha mhimili wa sera ya uchumi jamii wa Kinostiki na hilo halipaswi kusahauliwa. Pia Sabato ilishikwa kwa uaminifu sana huko Afrika Kaskazini kwa kipindi cha miaka mia nne. Ndiyo maana tunamuona Clement wa Alexandria akiitaja (Strom., ii, 6, ii, 7 etc) na inadhaniwa kuwa ni kutoka kwa Barnabus, Mlawi wa Cyprus. Na ndivyo hata tunavyojionea hata sisi Mnostiki Origen akiielezea kama Waraka wa Kikatoliki (Cont. Cels, i, 63), akiupa heshima yake stahiki (Comm., in Rom., I, 24).
Peter wa Alexandria (300 BK) ananukuliwa kama anayesema: "Tunaishika Siku ya Bwana kuwa ni siku ya furaha kwa kuwa yeye alifufuka siku hiyo."
Ni kwa sababu hii tunaiona imani ya Kirumi ikigeukia kuwatesa Wakristo ili kufanikisha kuishamirisha ili iweze kufanyika kuwa kama chombo au kifaa cha kutumiwa kufanikisha mikakati ya utawala wa wafalme wa dunia. Constantine alitangaza amri iliyojulikana kama Tangazo la Kuhuvumiliana mwaka 314. Mwaka 318 aliamuru kukaliwe kongamano la mtaguso wa Desposyni. Ndugu wa damu wa Yesu Kristo walidai kwamba Sheria ua Torati ya Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo virejeshwe. Constantine kwa kuombwa na mtume Sylvester, askofu wa Roma, alimpa mamlaka Sylvester kuamuru au aagize kuuawa kwao. Kwenye agizo lililotolewa mwaka 321, Constantine aliitukuza na kuienzi siku hiyo, iitwayo Siku ya Bwana, na kuitambua kuwa ni mojawapo ya siu takatifu kwa Wakristo, na kuamuru kuwa biashara na shughuli zote zifungwe siku hii. Hatimaye, Baraza la Mtaguso wa Nicaea (325 BK) kwenye mchakato wake rasmi ulitoa maelekezo kuhusu aina moya ya ibada ya Kikristo ifanyike siu hii peke yake, na Baraza la Mtaguso wa Laodicea (366) lilikazia kuwa siku hii inayoitwa Siku ya Bwana iwe na maana sawa na Sabato. Kwa hiyo, kwa tangazo na amri ya mfalme na mitaguso iliyoitishwa na kupitishwa katika karne ya nne vililiingiza kwenye Kanisa la Kikristo kwenye Kasumba ya upagani wa Kirumi, mabadiliko yaliyopokelewa na kukubaliwa na kuthibika.
Waabudu Jumapili wa Siku hizi wanahoji tofauti iliyopo kati ya siku mbili hizi, yaani Sabato na Siku ya Bwana: Neno “Sabato" limetoholewa kwenye lugha ya Kiebrania liitwalo "Shabua," maana yake "saba," au ni hatima ya mzunguko wa siku saba. Lilichukuliwa ili kumaanisha siku ya saba za juma la Biblia, ambalo wanalitaja kama “Juma la Kiyahudi” (inayoanzia tangu kuchwa kwa jua Ijumaa hadi kuchwa kwa jua Jumamosi). Ndipo kisha wanahoji au kupinga licha ya ukweli wa kwamba Kristo na Mitume walizishika Sabato hizi za kwenye Biblia na Mwezi Mpya na Sikukuu na kwamba ni kwenye kipindi tu cha mtawanyiko wa Wakristo ndipo siku ya mapumziko ilibadilishwa kutoka siku ya saba na kuwa siku ya kwanza ya juma, ili kuifanyia ukumbusho siku aliyofufuka Kristo, na kuipa heshima yake stahiki na kwa hiyo haijawahi kuwa Sabato (ambayo ilimaanisha kwa “usemi wa Wayahudi wa zamani”) na wala Jumapili (ambalo ni neno lenye maana na tafsiri ya kipagani, yaani, "siku ya jua"), bali wao wangali bado wakibisha na kudai hii kuwa ni “Siku ya Bwana.” Haipo kwao na hadhi na maadhimisho sawa nay ale ya Sabato ya Biblia, kama siku ya mapumziko na kuacha kabisa kuzifanya kazi zote ya utumishi au ya kuajiriwa, bali na kuifanya kuwa siku ya kujikuza kiroho na kutafakari na kufanya mambo yaliyo ya harakati za kidini na ni kipindi cha kujiepusha kuyafanya na kuyafuatilia mambo ya kidunia. Madai meingine yanafanywa kutokana na mapokeo potofu ya Mafarisayo ili kuonyesha jinsi ushikaji huu hauwezekani. Ukweli wa kama Kristo aliishika Sabato na siyo Jumapili imepotea kabisa kwao.
Makanisa ya Waethiopia na Waabyssinia yalikuwa ya washika Sabato kwa karne nyingi na ushahidi wake unaweza kujadiliwa. Waabudu Jumapili hawazishiki siku Takatifu za Mungu licha ya kuamriwa na kwao zinaonekana kama sheria zisizofaa wala kuutazishika amri zake.u ni kumcha Mungu na kuzishika amri (Mhubiri 12:13). Uzao wa mwanamke ni wale wazishikao amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12).
Firsa ipasayo ni rahisi tu.
Mungu ni habadiliki na hana kigeugeu. Kristo ni yeye yule, jana, leo na kesho. Wala habadiliki. Kristo alimpa Musa Torati akiwa kama Malaika wa Uwepo wake. Kristo alizishika Sheria za Mungu maisha yake yote. Alizishika Sabato, Mwezi Mpya na Sikukuu zilizoamriwa sambamba na kuzishika katika roho na kuihubiri injili ya ufalme wa Mungu.
Mitume na kanisa la kwanza walishika amri hizi zote na sikukuu za Mungu. Na ndivyo lilivyofanya kanisa kwa kipindi chote cha miaka 2000 bila kushindwa. Limepitia kwenye mateso na kuuawa mamilioni ya waumini wake udhalimu ulofanywa na wale walio kwenye imani potofu za waabudu jua. Kristo anakaribia kurudi na anakwenda kuhimiza umuhimu wa kuzishika Sabato na Mwezi Mpya (Isaya 66:23) na Sikukuu zote zilizoamriwa (Zekaria 14:16-19). Wale watakaopuuzia kuzishika sikukuu watakufa.
Sababu zenye mashiko ziko wazi:
Kama Kristo alizianzisha kwa amri ya Mungu; Kama Kristo aliwatuma manabii kwa kipindi cha miaka elfu ili kuwaonya Israeli ili wazishike (soma Amosi 8:5); na kama Kristo na kanisa la kwanza walizishika, na ukweli walizishika; na kama kuna kanisa linalozishika kwa maumivu na vifo kwa takriban zaidi ya miaka 1970, na ambalo bado lipo; na, kama Kristo anakwenda kuhuisha upya umuhimu wake kwa adhabu ya kifo atakaporudi, na kwamba haya ni Maandiko Matakatifu na Maandiko hayatanguki (Yohana 10:34-35): Ndipo sasa kinachofuatia ni kwa sisi wateule kufanya hivyo, na yatupasa pia kuzishika sasa. Ukweli haupingiki.
Ni
nini basi kuhusu hali iliyopo kwamba Wakristo wengi wanashikilia kuabudu siku
ya Jumapili?
Jibu: Ukweli ni kwamba waalimu wa uwongo wanawaambia watu kuwa hawalazimiki wala hakuna sababu kwa wao kuzishika amri za Mungu na hakuna udhuru. Kichwa cha kila mwanaume ni Kristo na kichwa cha Kristo ni Mungu. Wateule ni wale wazishikao amri za Mungu na Ushuhuda au Imani ya Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12).
Mungu alitupatia amri ya nne kwa kupitia
kwa watumishi wake manabii na kuwafundisha Israeli kwa kipindi cha miaka
arobaini ili kuianikiza mioyontumishi w mwao. Ni kwa nini dunia ilimficha
mwanamke jangwani kwa miaka 1260 ya dhiki kuu iliyoandikwa kwenye kitabu cha
Ufunuo? Ni nani basi aliyekuwa akilitesa kanisa? Majibu yake yanapatikana
kwenye majarida ya Mgawanyo Mkuu wa Makanisa ya
Mungu ya Washika Sabato (Na. 122) na Jukumu la Amri ya Nne
na Historia ya Makanisa ya Mungu ya Washika Sabato (Na. 170).
Kristo alisema kuwa walioitwa ni wengi lakini wateule ni wachache. Wateule wamejulikana tangu mwanzo kwa uweza wa milele wa Mungu wa kuelewa kila jambo. Wamejulikana tangu mwanzo, kisha wachaguliwa na kuitwa na kasha wametakaswa na kisha wakatukuzwa. Na ndiyo maana Biblia inasema kwa mifano. Inafanya hivyi ili watu wasiielewe na wakageuka kabla hawajakusudiwa kuitwa. Na ndiyo maana Kristo atakaporudi watamuita Bwana, Bwana, na atawaambia Siwajui ninyi kamwe.... Ndiyo maana alisema: Ukinipenda utazishika amri zangu.
Je
waabudu siku ya Jumapili hawatakwenda mbinguni?
Jibu: Hakuna hata mmoja wa watu hawa wanaotangatanga visiwani katika “roho” kwenye Jumapili aliyeitwa. Hakuna hata mmoja wao atakayekuwa na sehemu kwenye ufufuo wa kwanza. Iwapo kama unataka kuwepo kwenye ufufuo wa kwanza, basi zishike amri za Mungu na imani ya Yesu Kristo kwa upendo kama ulivyonenwa kwenye 1Wakorintho 13. Pia soma jarida la Ufufuo wa Wafu (Na. 143).
Kama kanisa lilivyomwambia mfalme huko Rumi katikati ya karne ya pili: “Unapowasogelea wale wanaosema kuwa ni Wakristo na kwamba wanapokufa wanakwenda mbinguni basi hao ni Wakristo.” Ni lipi fundisho la kutenganishwa kwa nafsi ya ubinadamu na umbinguni ya Kristo ni kama fundisho la Mpingakristo ilikuwa ni jaribio la kuashiria au kumjua Mkristo wa kweli katia karne ya kwanza na ya ili lingali linaendelea bado kutumiwa kama jaribio la kumuelewa mfuasi wa kweli. Mshika Sabato hii ya Siku ya Saba wa kweli ndiye ishara au alama za kweli za Kanisa hilo.
Kwa
kusema kweli, Yesu alisema kuwa yeye alikuwa Bwana hata wa Sabato na Paulo aliwaambia
kanisa fulani kwamba wanapaswa kuwa waalimu baada ya kwenda kanisani mara nyingi
na kuhubiri habari za wokovu na mafundisho kama hayo. Sasa kwangu mimi naona
kama ukiisoma Biblia utaijua na kuielewa sawa tu na kama alivyo mhubiri
mwingine yeyote. Na kama unasema kuwa sisi, ndiyo tulioitwa, basi tunakuwa
wateule kwa kuwa tu Wakristo kwenye Kanisa la Sabato, ambalo hatimaye linatuita
sisi kuwa mara zote tuwe tayari kuyafanya mapenzi ya Mungu kama tunavyotakiwa,
kama vile kulisha kondoo wake. Je, huwezi kumtoa shimoni mmoja wa kondoo zake
hata siku ya Sabato? Je, ni vibaya au dhambi kutenda mema siku ya Sabato? Je,
hutakuwa unafanya kazi nguvu siku ya mapumziko? Hata hivyo, hawakuwa makuhani
kipindi cha kabla ya Kristo walishughulika kwa kazi ya kuchinja wanyama
waliohitajika kwa ondoleo la dhambi na walijua kuwa Kristo atafanyika kuwa
mwanakondoo wa sadaka? Kwangu mimi naona kuwa siku zote ni Sabato tu.
Jibu: Kristo alisema: Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala
nukta moja ya torati haitaoondoka, hata yote yatimie. Basi mtu ye yote
atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo,
ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na
kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
Kama Kristo
aliivunja Amri ya Nne, basi sio Masihi. Alikuwa anatuonyesha jinsi tunavyopaswa
kuishika kwa mujibu wa Torati ya Mungu kwa kuwa iliwekwa kwa ajili ya
mwanadamu. Mari Kumi ni Amri Kumi
tu, na siyo mapendekezo kumi. Inatupasa kupandisha kiwango cha mwenendo na
matendo yetu kana kwamba kila siku ni Sabato. Hata hivyo, amri ya Sabato
inasimama, na ndani yake kunakamilika Torati yote na Manabii pamoja na Siku
Takatifu na kumwabudu Mungu. Soma jarida la (Torati na Amri ya Nne (Na. 256)).
Mdahalo wetu na
Wakatoliki si kama IWAPO kama inapasa kuzishia amri, bali ni kama wana haki na
mamlaka ya KUIBADILISHA Sabato na kuwa Jumapili. Kristo aliishika Sabato, na Mwezi Mpya na Sikukuu
zilizoamriwa na Mungu. Hizi
zinapatikana kwenye Kalenda ya Mungu. Sabato iliwekwa tangu uumbaji. Mitume na
kanisa la kwanza wote walizishika. Kanisa la Mungu limezishika kwa kpindi cha
miaka 2000 na waumini wake wameuawa kwa ajili ya ukweli huu. Hebu soma kwenye
majarida ya Jukumu la Amri ya Nne Kwenye Historia ya Makanisa ya Mungu ya Washika
Sabato (Na. 170); Malumbano na Hoja za Wakuartodeciman (Na. 277); Mgawanyo Mkuu wa Makanisa ya Washika
Sabato (Na. 122); Kalenda ya Mungu (Na. 156); Siku Takatifu za Mungu (Na. 97).
Mtazamo
wanaouibua wapinga ushikaji wa sheria ulitumiwa kwa mara ya kwanza ili
kuipotezea Sabato kutoka Roma, wakati ibada ya Jumapili ilipoingiwa ikitokana
na dini potofu za waabudu Jua za huko. Mpango na mtazamo huu haukukubaliwa
kabisa na Kanisa la Mungu. Kihistoria, wakati wote inaletwa kama shambulio kwa
Kanisa na Torati ya Mungu. Ni mafundisho yaliyoanzishwa na kufundishwa na
Mashahidi wa Yehova baada ya baadhi ya waanzilishi wao waliokuwa chini ya
kiongozi wao mwanzilishi Russell kujiengua na kutoka kwenye Kanisa la Mungu na
kuchukua fundisho hili na kujaribu kulikarabati ili lieleweke na kupendeka
zaidi kwa waongofu. Ni uzushi na watahukumiwa kwa kuwafanya wale
wanaolifundisha kuwa watakwenda kwenye Ufufuo wa pili wa wafu.
Kwa kweli,
Shetani hakuwaambia watu hawa uwongo, kwa hilo amewaambia kuwa wataingia kwenye
kipindi cha millennia wakiwa kama viumbe walio katika mwili. Hilo ndilo
fundisho lao na hivyo ndivyo itakavyotokea kwa wale watakaobalia hai. Hata
hivyo, watu hawa watakuwa wanazishika Sabato na Mwezi Mpya (Isaya 66:23), na
pia watakuwa wanashika sikukuu za Mungu na kuwapeleka wawakilishi wao huko Yerusalemu.
Vinginevyo mvua haitanyesha kwa muda muafaka na hatimaye watakumbwa na baa la
njaa au watakumbwa na magonjwa ya tauni (Zekaria 14:16-19). Haya ni Maandiko
Matakatifu na Maandiko hayawezi kutanguka.
Kwa ukweli hoja
hii ni za uwongo sana na za kishetani, kama watu hawa wasiozishika siku zote
kama Sabato. Wanafanya kazi siku za Sabato na wanakwenda kuabudu siku za
Jumapili, ambavyo ni kinyume kabisa na jinsi Mungu alivyokuamuru ufanye.
Hawazishiki wala
kuziadhimisha Siku Takatifu licha kuamriwa hivyo na hawaipendi kabisa kweli.
Mungu hashughuliki na dunia kwa sasa na ni wazi sana kwamba hashughuliki nao
hata wao bado kama unampenda Mungu basi utazishika amri zake. Kiilichobakia ni
kumcha Mungu, na kuzishika Amri zake (Mhubiri 12:13). Uzao wa mwanamke ni wale wazishikao amri za Mungu na
ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12).
Kama Wakristo walianza kuabudu kwa kuiadhimisha
Sabato ya siku ya saba ya juma, kwa nini makanisa mengi wanakutanika siku za
Jumapili sasa?
Jibu: Katika karne ya pili ya zama tulizonazo dini za waadhimisha Easter
ziliingizwa kutoka kwenye dini na imani za kipagani huko Roma. Haya ndiyo
yalikuwa Mabishano ya Wakuartodeciman. Soma jarida la Malumbano ya Wakuartodeciman (Na. 277). Dini ya waabudu Jua ilikuwa ndiyo mhimili
mkubwa wa imani hii. Krismas chanzo chake hasa kilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa
mungu jua anayehudumu kwenye majira ya baridi kali ya ncha ya kaskazini. Easter
ni jina la mungumke Easter na ni mshirika au kimada wa Baali aliyejulikana kama
Easter, au Istar, au Astarte. Mungu mfu alikuwa ama Attis kwa upande wa
maskazini huko Roma, au Adonis kwa upande wa Mashariki huko Ugiriki na
ushawishi wao.
Wamisri
walimuombolezea Osiris. Hii iliitwa Ijumaa ya kusulibiwa au ya mateso na
walisherehekea Kufufuka kwake siku ya Jumapili. Maadhimisho ya kufufuka kwa
siku ya mungu Jua kulikuwa ni sehemu ya imani ya dini hii ya mungu wa Utatu. Soma kwenye jarida la Chanzo cha Krismas na Easter (Na. 235).
Sabato ilipingwa
na kushambuliwa na kupingwa vibaya kwanza huko Roma kwa ibada za pamoja na
utaratibu wa kutoa komunio siku ya Jumapili, ni kama ilivyokuwa kwenye imani za
waabudu jua. Na hii ndiyo sababu inayopelekea kila mwaka Pasaka inaambatana
sambamba na maadhimisho ya Easter. Mnamo mwaka 300, baraza la mtaguso wa Elvira
liliyanenea vibaya maadhimisho haya, na mwaka 325 imani na maadhimisho ya
Easter yalialalishwa na kurasimishwa kwenye Dola yote na imani ya Kibinitarian
ya mungu Attis ndipo iliingizwa rasmii kwenye Ukristo. Mwaka 366 baraza la
mtaguso wa Laodicea uliipiga marufuku Sabato.
Historia ya
kipindi cha mpito inakutikana kwenye kitabu kilichoandikwa na Sam Bacchiocchi
(cha Kutoka Sabato Hadi Jumapili [From
Sabbath to Sunday], Pontifical Gregorian University Press Rome, 1975).
Mwaka 381 imani ya Utatu ilibuniwa kwenye Baraza la Mtaguso wa Constantinople
na mwaka 451 huko Chalcedon muundo wa imani hii ulikamilika. Wayunitariani,
hasahasa wenye asili ya Parthian, waliukataa uzushi huu mpotovu na ndipo vita
vikaanza.
Wakati wa
kuzinduliwa kwa iliyokuwa ikijulikana kama Dola Takatifu ya Rumi, Sabato
ilipigwa marufuku na waliokiuka marufuku hii na kuishika waliteswa pasi huruma
popote walipoonekana kufanya hivyo (soma jarida la Vita vya Wayunitariani na Watrinitariani
(Na. 268)). Dini nyingi zilizoko leo ni matokeo ya
kukengeuka huku kutoka kwenye kweli kutokana na mateso au kuteswa kwa makanisa
yanayoishika Sabato. Historia yake inakutikana kwenye majarida ya Mgawanyo Mkuu wa Makanisa ya Mungu Yanayoshika Sabato (Na. 122) na Jukumu la Amri ya Nne Kwenye Historia ya
Makanisa ya Mungu ya Washika Sabato (Na. 170).
Makanisa mengi ya waabudu
Jumapili wameipotezea Pasaka, na kisha kuikataa asili na tabia ya Mungu.
Wamefungiwa kwenye mfumo mzima. Na sio ni kuabudu siku ya Jumapili peke yake.
Bali ni pamoja na Krismas na Easter, ni pamoja na kumuabudu mungu Utatu.
Jisomee hayo zaidi kwenye majarida ya Fundisho la Dhambi ya Asili Sehemu ya I
Bustani ya Edeni (Na. 246); Imani za Kuwa Sawa za Kiariani na Uyunitariani (Na. 185); Ubinitariani na Utrinitariani (Na. 76); Kuwa na Hadhi Sawa na Baba (Na. 81); Mteule Kama Elohim (Na. 1) na Teolojia ya Mwanzoni ya Uungu (Na. 127).
Kanisa la kwanza lilifanyaje kuhusu ibada?
Jibu: Wakolosai 2:16 inaonyesha kuwa kanisa lilikuwa
linazishika Sabato zote na Miandamo ya Mwezi na Siku zote Takatifu. Inasema
kuwa mtu na asiwahukumu kwa kuzishika siku hizo, bila kuzipuuzia. Kitabu cha
Matendo kinaonyesha wazi kuwa kanisa zima lilikuwa linazishika sikukuu na Sabato
na hapa Miandamo wa Mwezi. Sisi tumedumu kuzishika pia kwa takriban miaka 1971.
Waliishika Pentekoste au vinginevyo wasingempokea Roho Mtakatifu (Matendo 2:1).
Injili zimechafuliwa kwa kubadilishwa maeneo yanayosema utunzaji huu wa
sikukuu, jinsi alivyokuwa anazishika zote Kristo na mitume. Mtume Paulo
alizishika nah ii inayatafsiri maandiko yake (Matendo 12:3; 20:6). 1Wakorintho
5:7-8 inaeleza jinsi inavyotupasa kuishika Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu.
Kanisa
liliiadhimisha Siku ya Upatanisho (Matendo 27:9). Huwezi kujua mpango wa wokovu
bila kuzijua siku takatifu za Mungu. Kristo alikuwa ndio Pasaka na Mganda wa
Kutikiswa. Alituamuru kuiadhimisha Meza ya Bwana kwenye usiku aliosalitiwa
ambayo ni siku ya 14 Abibu. Hakuna andiko hata moja lililoibadilisha Sabato na
lililoliambia kanisa lisishike Sabato, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu, likiwemo
andiko la Wakolosai 2:16. Mtume Paulo aliwapangia utaratibu wa kukusanya
changizo kuwa ufanyike Siku ya Kwanza ya juma kwa kuwa ilikuwa haikufanyika
siku ya Sabato na hili ndilo andiko pekee lililopo na linaloonyesha
walikutanika siku ya kwanza ya juma au Jumapili. Na hata siku yenyewe inayoitwa
kuwa kuwa ni Siku ya Kwanza ya Juma kwa
kweli ni Sabato ya kwanza ya hesabu ya
kuelekea kwenye idi ya majuma kwa Kiyunani.
Krist alisema
usipoula mwili na kuinywa damu yake, huna ushirika naye. Kwenye usiku
aliosalitiwa alisema: Huu ndio mwili
wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
Vivyohivyo akakitaa
kikombe kwenye mlo huo na kusema: Kikombe hiki ni
agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu. (Luka 22:19-20)
Ni kwa wazi kiasi
gani inafanyika? Tunaadhimisha Meza ya Bwana pamoja na Pasaka na Idi ya Mikate
Isiyotiwa Chachu kwa kuwa imeamriwa. Tunaadhimisha kumbukumbu ya mwanakondoo saa
9 jioni, siku ya 14 Abibu kwa kuwa tumeambiwa tuishike Pasaka nje ya malango
yetu kama alivyofanya Kristo na tunakumbuka kuwa katika kipindi hiki ndipo
pazia la Hekalu lilipasuka katikati na kufanya iwezekane sisi kuingia
Patakatifu pa Patakatifu. Tunakutanika kuadhimisha ukumbusho wa Mganda wa
Kutikiswa majira ya saa 3 asubuhi, siku ya Jumapili asubuhi kwa kuwa Kristo
ndye alikuwa limbuko na aliingia kwenye Kiti cha enzi cha Mungu wakati huo na
akarudi kwa uweza wa Roho Mtakatifu na kufanya iwezekane kwetu sisi kuwa wana
wa Mungu. Tangu hapo ndipo tunaanza kuhesabu muda wa kuelekea kwenye Pentekoste
na kwenye mavuno yetu. Tunangojea uamsho na urejesho wa Roho Mtakatifu siku ya
Pentekoste saa 3 asubuhi wakati tunapotakiwa kufanya hivyo. Tunamngojea kwa hamu
kubwa Masihi tangu kwenye ibada zetu hadi siku ya ukumbusho wa kuzipiga
Baragumu.
Mungu anatutaka
tujitese kwa kufunga saumu ili kuzitesa nafsi zetu pasipo kuwakwaza na
kuwataabisha wengine, na kushindana na maadui zetu. Amesema hataisikia saumu
kama hiyo wala maombi ya mtu kama huyo. Bali yatupasa kufunga saumu kwa ajili
ya kuvunja nira za uovu na kutuweka huru kutokana na matendo ya dhambi, uongo
na maovu. Yatupasa kupendana na kusema kweli pasipo hila.
Saumu hii ni ya
tangu jioni ya siku ya kwanza hadi jioni ya siku ya ili, na inamaanisha
kutokula chakula chochote wala kunywa maji kipindi chote cha mfungo huu. Kwa
habari ya siku hii ya Upatanisho, ni mfungo wa masaa 24 tangu jioni ya kwanza
hadi inayofuatia na kama mtu hatafunga saumu hii, basi ataondolewa mbali kutoka
taifa la Israeli, ambalo ni Kanisa lililo chini ya Kristo. Huwezi kuwa Mkristo
na ukawa hushiriki mfungo huu wa saumu siku hii (isipokuwa kama itakuwa
imethibitika kuwa ni hatari kwake akifanya hivyo).
Mitume waliushika
mfungo huu na imeandikwa kwenye Matendo 27:9. Saumu unatakiwa kufanywa ukiwa
umeosha sura yako na uwe safi, na uvae vizuri na umuombe Mungu na kujisomea
maandiko. Kama utawapa chakula wenye njaa na kuwainua na kuwasaidia wanaoonewa
basi atakusikia umuombapo.
Ikiwa tutaenenda
mbele zake kwa unyenyekevu na kujinyima au kuachana na ubatili na kuyanena
maovu ya wengine, ndipo atasikia na kutuongezea uwezo wa kuelewa kushughulika
nasi kwa wema. Afya yetu itaboreka sana na atatulinda wakati wa ukame. Watu
wetu watapajenga mahali palipobomoka, na kisha tutaijenga misingi ya vizazi
vingi na tutaitwa wajenzi wa mahali palipovunjika. Mfanya marejesho mapya wa
njia za kuishi ndani yake. Safari ya miaka elfu moja inaanzia hapa kwa hatua
hii ya kwanza. Soma jarida la Tufundishe Jinsi ya Kuomba (Na. 111).
Ninavyojua mimi ni kwamba kulikuwa na mabaraza 4
kwenye historia ya mwanzoni. Kama sikosei, ilikuwa ni mitaguso ya Nicaea,
Laodicea, Constantinople, na Chalcedon. Nijuavyo mimi pia ni kwamba kulifanyika
mabadiliko mengi sana ambayo yalianzishwa kinyume na imani ya kweli ya kanisa
la kwanza kwenye mitaguso hii. Unaweza tafadhali kuelezea japo kwa kifupi
kuhusu mabadiliko gani yaliyofanywa kwenye kila mmoja wa mitaguso hii, na ni kwa
kiasi au namna gani mabadiliko haya yameiathiri imani halisi nay a kwanza ya
kanisa?
Jibu: Kuna mitaguso minne ambayo ni:
Nicaea mwaka 325:
Mtaguso huu ulianzisha imani ya Muundo wa Kibinitariani na walimuinua Kristo
kuwa ni kama Mungu wa kweli. Mtaguso huu pia ulirasimisha maadhimisho ya
Easter, sikukuu iliyoingizwa ikitokea kwenye dini za kipagani za miungu Attis
na Adonis na pia ilikuwa ikiabudiwa kwenye dini za Wamisri. Tarehe za
kuadhimisha zilitofautiana upande wa Mashariki na Magharibi kwa wafuasi wa
miungu hii ya Attis na Adonis. Hii ilibadilika.
Kanuni na
maazimio ya mtaguso huu zilipotea na kile kilichojulikana kama Tangazo la Ukiri
wa Imani la Nicaea kwa kweli ni tangazo la ukiri wa imani la Mtaguso wa
Constantinople mwaka 381. Mtaguso wa Laodicea ulianzisha kanoni au sheria 29
zilizotumika kupiga marufuku kuiadhimisha siku ya Sabato na badala yake
ikaingizwa Jumapili. Hali hii iliendelezwa na baraza la mtaguso wa Elvira mwaka
300, ambapo walijaribu kuihalilisha Jumapili ichukue rasi mahala pa Sabato, ila
ilishindikana baada ya kuanzishwa tena kanisa la mrengo wa Kiyunitariani baada
ya mwaka 327 na kutudishwa tena kwa maaskofu wa Kiyunitariani, kulikofanwa na
Constantine.
Mwaka 358,
Wayahudi walianzisha Kalenda mpya ya Hillel na mfumo wa uahirisho. Mwaka 381,
baada ya uahirisho wa mzaliwa wa Hispania aitwaye Theodosius na Gratian,
Mtaguso wa Constantinople uliitishwa. Imani ya Utatu ilianzishwa na
Wakapadokian na waliikubali kwa sehemu.
Mwaka 375,
Krismas iliingizwa kanisani kutoka Syria na mnamo mwaka 386 imanii hii ilifika
hadi Yerusalemu na mungu wa Utatu aliingizwa rasmi na kuanza kuabudiwa kwenye
imai ya Kikristo. Mwaka 450-451 huko Chalcedon, imani ya Utrinitari na muundo
wake wa imani mpya vilikubalika. Mgawanyiko huu ulipelekea kuanzishwa kwa
Kanisa la Coptic, lakini sikukuu za kipagani za Easter na Kristmas ziliingizwa,
na katika karne iliyofuatia kulishuhudiwa kuingizwa kwa imani nyingine ya
kipagani ya kumuabudu mungumke aliyeingizwa kwa jina la Maria na ibada zake za
kusali kwa kutumia shanga, viliingizwa kwa uvamizi huu.
Soma majarida ya Cheanzo cha Krismas na Easter (Na. 235); Teolojia ya Mwanzoni ya Uungu (Na. 127); Kuendelea kwa Mtindo wa Uplatoni Mamboleo (Na. 17); Kuwa Sawa na Baba (Na. 81); Roho Mtakatifu (Na. 117) na Ubinitariani na Utrinitariani (Na. 76).
Ni kina nani walikuwa Mababa wa Kanisa? Niwajuao
mimi ni kina Clement, Augustine, Athanasus, Eusebius, nk. Niliiona orodha yao
kwenye tovuti ya Wakatoliukuliwa kama mababa wa Kanisa “Katoliki la Roma.”
Jibu: Watu hao walioorodheshwa waliitwa mababa wa Kanisa, kwa maana kwamba
walikuwa waalim na wanateolojia wa kanisa waliofundisha imani ya kweli ya
kanisa kwenye matawi yake mbalimbali. Kanisa Katoliki la Roma kama tujuavyo
sote halikuwepo huko nyuma hadi mwaka 381.
Kanisa liliitwa
Kanisa Katoliki kwa maana kwamba lilikuwa la ulimwenguni kote, na hawa “mababa”
hawakuwa wanakubaliana wote na Roma, na wengine hawakuwa hata na ushirikiano
nalo. Tertullian, kwa mfano, mwanzoni alikuwa anashirikiana na Roma, lakini
akawa ni wa mrengo wa Wamontana na alipingwa na kuthibitiwa sana na Roma.
Irenaeus, askofu
wa Lyon, alifundishwa kwenye Shule ya Mtume Yohana chini ya Polycarp wa Smyrna,
na hakuwa hata amepangiwa na Roma. Athanasius na Augustine walikuwa kwenye
mstari wa walioyashadidia na kuendeleza mawazo mapotofu ya Warumi. Fundiso la
Wapinga maazimio ya Mababa wa Nicaea kuhusu asili ya Mungu waweza kuyasoma
kwenye jarida la Teolojia ya Mwanzoni Kuhusu Uungu (Na. 127). Hili litakuonysha mtiririko wa kimawazo.
Ibada za Kipagani
Hatuini Easter ikitajwa mahali popote kwenye
maandiko ya Agano la Kale na kwa hiyo tunapenda kujua chimbuko la sikukuu hii
ni nini na neno hili linatokana na nini?
Jibu: Neno Easter ni la Kianglo-Saxon la munumke (soma kamusi ya Oxford
Universal Dictionary). Mungumke huyu anaitwa pia Istar au Ostar. Kwenye Biblia
anaonyeshwa kuwa ni mwenzi au mke wa Baali kama “Ashtaroth” (SHD 6252). Wakati
mwingine, anaitwa pia “Ashteroti.” Sulemani alishiriki ibada za sanamu kwa
kuadhimisha sikukuu hizi na kuabudu, yaani sikukuu ya Easter.
“Ashtar” ni shina
la kina lililopelekea kuitwa kwa jina hili la Easter. Lugha za muungano wa
Anglo Saxon ndizo ziliunda kwa pamoja jina hili Ashtar kutoka kwea Israeli wa
kale. Watu wa Austria walikuwa na jina waliloiita nchi yao lililoitwa kwa ajili
yake mnamo mwaka 996, ambalo lilianzishwa na Ostarrichhi au ufalme wa Ostar. Soma kwenye jarida la Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235).
Hatuioni Easter kwenye maandiko ya Agano la Kale
ikiwa kama miongoni mwa sikukuu za Mungu, tungependa kujua ni wapi wazo la
kuabudu na kuiadhimisha siku hii lilitokea?
Jibu: Sikukuu au maadhisho ya mungu mfu ilikuwa ni sehemu ya imani na
maadhimisho ya Easter ya Wababeloni. Sikukuu hii ilikuwa inaadhimishwa na
waumini wa mungu Attis upande wa Magharibi, na Adonis kwenye ulimwengu wote
ulioathiriwa na mafundisho ya Kihellen upande wa Mashariki, na Osiris, na mungu
mfu wa Wamisri. Dhana iliyoko ya Kusulibiwa kwa Kristo siku ya Ijumaa na
kufufuka kwake Jumapili inatokana na itikadi ilikuwa inafanywa kwenye dini hii
potofu. Mti wa msonobari ulikuwa ni mti mtakatifu kwenye dini ya Attis ambao
ndio alisulibiwa juu yake.
Wakati Ukristo ulipoanza kuwa maarufu na
kushamiri huko Roma, wafuasi watiifu wa dini zenye maana za Kisirisiri,a
hasahasa dini ya Attis, waliingia kwenye Ukristo na wakaiingiza imani Easter na
maadhimisho yake. Maaskofu wa Roma walijaribu kuipinga na kuipiga marufuku mwaka
152 BK chini ya Anicetus bila mafanikio. Bali waliiadhimisha huko na kwenye
miaka ya 190-192, Victor aliingiza a kuiruhusu na akaligawa Kanisa. Haya yaliitwa Mambishano ya
Wakuartodeciman. Soma kwene jarida la Mabishano ya Wakuartodeciman (Na. 277).
Yawezekana kuwa kwamba imani ya Utatu ni aina
nyingine ya ibada za sanamu, wakati kwamba tofauti pekee ni kwamba sanamu
haziabudiwi ila ni nabii wa Mungu? Inawezakuwa kwamba bado watu ni wajing au
hawajui? Ni maana, Wakristo wanasema kuwa Mungu ni mmoja, lakini hudhani kwamba
wanamgawanya?
Jibu: Imani ya Utatu inatokana na fundisho la mungu wa Utatu. Kuna watu wengi
wasiojua kuwa ni waumini wa Utrinitarian ambao ni waumini wa Kanisa la Utatu,
lakini hawayaamini maneno haya. Wangali wakimuabudu bado Mungu mmoja wa Pekee
na wa Kweli, ambaye ni Baba, kwa jina la Mwanae Yesu Kristo, na hawamchukulii
Kristo kuwa ni Mungu.
Wao kwa kweli ni
Wayunitarian. Kwenye Kanisa la Kipresbyterian miaka elfu mbili iliyopita,
ingekufanya kuwa vigumu sana kutofautisha na Watrinitarian wa kweli. Viongozi
wengi wan chi ya Marekani walikuwa wa Yunitarian. Jefferson alidhani na
kutamani kuwa angeona nchi yote ya Marekani wakiwa Wayunitarian. La kusikitisha
sana ni kwamba tangu siku hizo za imani iliyopendwa yenye kuonewa mashaka,
ndipi ilirudi nyuma kwenye nchi iliyopupumbazika. Mababa Wahamiaji walikuwa
Wayunitarian, na waliteswa kwa sababu ya kuamini hivi na kwa kuishika kwao
Sabato mara tu baada ya kuanzisha kwao koloni. Fundisho la kwamba Mungu na
Kristo ni sehemu ya Mungu mmoja huyohuyo, ni fundisho la mungu Attis, na yeyote
anayemtenganisha Kristo na ubinadamu au asiyekiri kuwa ni mwanadamu na kwamba
si Mungu ana mafundisho ya Mpingakristo. Soma majarida ya Asili ya Mungu ambayo
ni Programu ya Kujifunza Biblia (Na. B1); Torati na Amri ya Kwanza (Na. 253) na Amri Iliyokuu na ya Kwanza (Na. 252).
Wazo la kuwaomba
miungu mingine, au watakatifu na masalia ya wafu, ni ibada ya sanamu kabisa na
isingeweza kuvumiliwa kwenye Kanisa la kwanza. Mungu anaichuza mioyo ya watu na
anawajua wasiopiga magoti yao kwa Baali. Taifa linalindwa na hali yake ya kawaida ya watu waaminifu. Watakatifu
walio kwenye nchi hiyo hulitakasa. (Soma majarida ya Utakaso wa Hekalu la Mungu (Na. 241) na Utakasi Kwa Ajili ya Dhambi Zilizofanywa Pasi Kukusudia (Na. 291).)
Mpingakristo
Biblia ilipasa kusema kuwa mpingakristo atakuja na
kujaribu kuanzisha mkakati wa kurejesha ushikaji tena wa Torati ya Musa.
Unaweza kunipa rejea ya Maandiko Matakatifu yanayosema hivyo?
Jibu: Hakuna andiko kama hilo popote. Wahubiri wa Kiprotestant nchini Marekani
wanasema kuwa Mpinhakristo ataanzisha tena mchakato wa kuzishika Amri na Torati
ya Musa. Lakini hilo ndilo hakika tunalopasa kulitarajia kufanywa na Kristo kwa
mujibu wa maandiko ya Biblia.
Kwa mfano, Kristo
atarejesha tena ushikaji wa Sabato, na Miandamo ya Mwezi, na sikukuu (Isaya
66:23). Watu wote watawapeleka wawakilishi wao huko Yerusalemu kila mwaka
kwenda kuishika sikukuu ya Vibanda, vinginevyo hawatapata mvua kwa wakati wake
(Zekaria 14:16-19). Hii inamaana kuwa utazishika Sheria za Mungu na na Sabato
zake, vinginevyo utakufa kwa njaa.
Unaweza kuniambia mafundisho ya Mpingakristo ni
yepi? Pia, je, unadhani kuwa Mpingakristo yungali hai bado?
Jibu: Mafndisho ya Mpingakristo yaleelezewa kwenye 1Yohana 4:1-2. Andiko lililo
kwenye Biblia sasa limebadilishwa kulinganisha na lilivyoandikwa kwenye
maandiko yake asilia. Andiko sahihi la zamani linapatikana kwenye kitabu cha
Irenaeus, Sura ya 16:8 (soma jarida la ANF, Vol. 1, fn. Hadi ukurasa wa 443).
“Katika
hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika
mwili yatokana na Mungu. 3 Na kila roho isiyomkiri Yesu
haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo.”
Socrates Mwanahistoria
anasema (VII, 32, p. 381) kwamba kifungu hiki kimepotoshwa na wale walionuia
kutenganisha hali ya ubinadamu wa Yesu Kristo kuoka kwenye hali yake ya
kimungu. (Soma pia jarida la Msingi wa
Imani wa Imani ya Kikristo, Machapisho ya CCG publishing, fourth edition,
p. 7 pia kama jarida la Msingi wa Imani (Na. A1).)
Tofauti ilikuja
kutoka kwenye mafundisho ya imani na ushikaji wa Easter na ya mungu Attis
yaliyojipenyeza kwenye Ukristo. Ni ya imani ya mungu Attis aliyeaminika na
kufundishwa kuwa baba na mwana walikuwa ni mungu mmoja, na kwamba huyu mtoto
aliuawa lakini uungu wake ulidumu na kubakia. Imani na fundisho hili
lilikubalika na kuingizwa kwenye imani ya Kikristo kwa Muundo wa Kibinitaiani
kwenye Baraza la Mtaguso wa Niacea, na hatimaye ikapitishwa kuwa Utatu kwenye
Baraza la Mtaguso wa Constantinople mwaka 381 kwa juhudi za Wakappadocians.
Soma jarida la Teolojia ya Mwanzo ya Uungu (Na. 127) na pia majarida mbalimbali kadhaa yanayofundisha
Asili ya Mungu nay a Masihi yanayopatikana kwenye jarida la Utaratibu wa Kujisomea Biiblia (Na. B1).
Mpingakristo amekuwa
pamoja nasi tangu mwanzo, na fundisho hili liliendelea kanisani na sasa kwa
watu wengi wanaojiita Wakristo waamini Utatu.
Je, Yesu atakuja kama
mwanadamu kiasi cha watu kumdhania kuwa yeye ni Mpingakristo? Watu watakaobaki
wanaishi baada ya theluthi moja ya wakazi ulimwenguni wameangamia, je
watabahatika kufufuliwa au hata kuwa hai tu na kuwa na miili kama ilivyo sasa
na kurudi kwenye mchakato wa ufufuo wa kwanza na wa pili?
Jibu: Malaika wanaweza kuwa na umbo la
kibinadamu wakipenda. Viongozi wa utawala wa millennia bado watakuwa wanadamu,
watakaokuwa wanawaongoza wanadamu. Israeli watawachagua viongozi wao kama
isemavyo Biblia na makuhani wao watakuwepo. Wakati Keisto atakapokuja hapa
watamuona na hakuna atakayeona mashaka kama wakati alipokuwa kwanza hapa
duniani. Kama watawaambia kuwa yuko jangwani, nk, msiwasadiki. Kila jicho
litamuona kama ilivyoandikwa atawatela mataifa yote mahali paitwapo
“Armagedoni,” na kuwaangamiza wote. Kutakuwa na matenki ya kutosha na masalia
yatakayoachwa kuwakimbia Israeli na mafuta ya kutuia kwa miaka mingi. Chuma
kitakuwa ni chanzo cha masalia kwa karne nyingi. Watu wengi watakao pigana naye
watakuwa ni wale walio kwenye Ukristo bandia au wa kipagani wa leo, na wafalme
wa Mashariki. Kwa hiyo,
utakuwa ni mchakato endelevu. Majarida ya Mihuri Saba (Na. 140) na Baragumu Saba (Na. 141) ni ya muhimu sana. Soma pia jarida la Baragagumu (Na. 136) na Mapitio ya Nyakati ya Zama (Na. 272).
q