Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[087]

 

 

 

 

 

 

 Zaburi Kutoka Kwenye Ibada za Hekaluni

(Chapisho La 2.0 20040523-20041122-20070731)

 

 

Ibada za Hekaluni zilitumia Zaburi au Tenzi maalumu aakati walipokuwa wanatoa dhabihu zao za kila siku. Hapa tunazionyesha na kuzitathmini Zaburi hizo.

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki ©  2004, 2007 Wade Cox)

(tr. 2014)

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 

 


Zaburi Kutoka Kwenye Ibada za Hekaluni

 


Kanisa linaabudu kila siku kwa maombi na kufunga saumu kwa siku hizohizo. Kulingana na utaratibu wa mambo ya Hekaluni, kulikuwa na utolewaji wa dhabihu kila siku. Dhabihu za kila siku ziligawanywa kwnye makundi yaliyojulikana kama sadaka za asubuhi na za jioni.

 

Kanisa lilifuata linaenndelea bado kufuata, utaratibu wa Hekaluni wa ibada na kalenda yake yenye jumla ya miezi kumi na miwili, pamoja na mwezi mwingine wa pili unaofuatana na ule wa kumi na mbili unaotokea kwa baadhi ya miaka unaotokea mara saba katika kipindi cha miaka kumi na tisa (soma jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 156) [God’s Calendar (No. 156)]. Inafanya kazi kwa mujibu wa kipindi mpito na ibadi ya siku iloyo kwenye kipindi hiki cha mpito wa kufikia mwandamo wa mwezi mpya. Kuna jumla ya takriban siku 59 katika kila miezi miwili. Sabato inaangukia katika kila siku ya saba, ambayo ni, na mara zote huangukia siku ya Jumamosi au kwa Kiingereza inaitwa Saturday iliyo katika mfumo wa jina la kipagani lililoitwa kutokana na mungu wa kipagani aitwaye Saturn.

 

Kanisa pia linakusanyika kufanya ibada siku ya Mwandamo wa Mwezi na katika Siku Takatifu za Sikukuu, na linakusanyika kufanya ibada kwenye Sikukuu ambazo kwa ujumla wake zinafanyika kwa majira matatu kwa mwaka kama zilivyoamriwa na Mungu kupitia manabii wake (soma jarida la Siku Saba za Sikukuu (Na. 49) [Seven Days of the Feasts (No. 49)]. Kwenye vipindi hivi vitatu vya Sikukuu migawanyo yote ishirini na nne ya makuhani yalijumuika pamoja (kwa mujibu wa kitabu cha Schürer, Historia ya Wayahudi katika Zama za Yesu Kristo au Kwa Kiingereza ni History of the Jewish People in the Age of Jesus Christ, Vol. II, p. 292). Sadaka za kila siku zilitolewa asubuhi na jioni. Jopo la makuhani lilifanya huduma zake kwa kupeana zamu za juma hadi juma na makuhani walibadilishwa kwa kuhudumu siku ya Sabato. Wale waliostaafu walihudumu kwenye utoaji wa sadaka za jioni (Schürer, ibid.).

 

Makuhani waligawanyika kwenye makundi ishirini na nne kama walivyokuwa Walawi pia, na taifa au kutaniko la Israeli pia liligawanywa kwa migawanyo au vikundi ishirini na nne, “kila kundi moja lilitumika kuhudumia kwa mzunguko wa juma hadi juma, wakiwa kama wawakilishi wa watu kwa Mungu, na ndipo sadaka za kila siku zilitolewa” (Schürer, ibid., pp. 292-293). Sawa na kama makuhani na Walawi, mkutano, hata hivyo, hawakulazimika kwenda Yerusalemu kila wiki, bali walikutanika kwenge sinagogi kufa nya ibada na maombi na kujisomea au kujifunza Biblia, na huenda kulikuwa na wawakilishi tu waliokwenda na kuwawakilisha huko Yerusalemu (ibid., p. 293).

 

Kipindi cha utoaji wa dhabihu kilikuwa ni saa 3 ya asubuhi au saa la tatu na ndipo walipomtolea dhabihu ya asubuhi, na saa 9 alasiri au saa la tisa la siku ndipo walimtolea dhabihu ya jioni. Ilikuwa ni dhabihu hii ya jioni iliyotolewa saa tisa alasiri ndipo walipoanza kuwachinja wanakondoo wa Pasaka. Na hii ndiyo maana tunaadhimisha Kifo cha Mwanakondoo kwenye ibada tunayoifanya kila mwaka siku ya 14 ya Mwezi wa Kwanza (Abibu), ambayo ndipo tunafanya ukumbusho wa Ml wa Meza ya Bwana jioni iliyo kabla. Wanakondoo walichinjwa tangu saa tisa hadi saa kumi na moja, yaani saa 9 alasiri hadi 11 jioni, siku ya 14 mwezi wa Abibu (sawa na kitabu cha Josephus, cha Wars of the Jews, VI, ix, 3). Kipindi au muda huu ulikuwa ni kwa mujibu wa kiwango hitajika cha utoaji wa sadaka za kilasiku au za daima za jioni.

 

Kwenye chumba maalumu cha Hekalu (chumba cha upande wa mashariki) kilikuwa na vyetezo au vyombo vitatu vitakatifu. Katikati kulisimamishwa madhabahu ya dhahabu ya kufukuzia uvumba, ambapo pia iliitwa au kujulikana kama  madhabahu ya upande wa ndani ambayo kwayo uvumba ulifukiziwa kila siku – vipindi vyote viwili, yaani asubuhi na jioni. Kusini yake kulikuwa na kinara kimoja kikuu chenye matawi ya vinara saba juu yake iliyosimamishwa na chenye mafuta ndani yake na kilichokuwa kinawaka bila kuzimika masaa yote (Schürer, pp. 296-297; fn. 17, p. 297). Kaskazini mwa madhabahu kulisomamishwa meza ya dhahabu ya mikate ya wonyesho, ambayo ilikuwa na mikate kumi na mbili iliyowekwa kila siku ya Sabato.

 

Maandiko a Biblia yanatuambia kwamba taa za Menora ziliwashwa saa za jioni ili kuwawezesha watoe sadaka za kuteketezwa wakati wa jioni. Shughuli kwenye Hekalu zilikuwa ni kwamba waliwasha vinara ay taa tatu saa za mchana na saba zote ziliwashwa saa za usiku, kwa mujibu wa Josephus (AntiqJews, III, viii, 3), lakini kwa mujibu wa Mishnah anasema kuliwashwa moja mchana moja saa za mchana na jioni ziliwashwa saba zote (m.Tam. 3:9); 64:1; sawa na Sifra kwenye Mambo ya Walawi 24:1-4; sawa na Schürer, ft. 17 p. 297).

 

Tunajua kwamba Kanisa lilishika na kutilia maanani vipindi vya kutoa sadaka za daima za kila siku kwenye ibada zake, kipindi walichokusanyika pamoja ibadani siku ya Pentekoste saa tatu asubuhi au kitarakimu ni saa 3 asubuhi. Wakati huu, Roho Mtakatifu aliwashukia na akatolewa kwenye Kanisa. Hii ilikuwa ni siku ya hamsini kamili tangu siku ilipotolewa Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa, iliyotolewa na kutikiswa kwenye dhabihu ya asubuhi ya Siku ya Kwanza ya Juma au Jumapili watati wa Mikate Isiyo na Chachu (kama ilivyoandika kwenye Mambo ya Walawi sura ya 23). Kanisa lilizishika Sabato zote, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu – utaratibu na mfumo mzima wa Sikukuu, kama tunavyosoma kutoka kwenye Injili, Matendo ya Mitume na Nyaraka—na liliendelea kufanya hivyo wakati wote lilipodumu kabla ya kukumbwa na zama za mateso. Tunajua pia kwamba Kanisa lilishika Miandamo ya Mwezi, Sikukuu zilizoamriwa na Siku nyingine zote Takatifu zilizoorodheshwa kwenye Kalenda ya Hekalu, na kwamba dhana ya maahirisho haikuwepo wala kufundishwa hadi ilipofikia karne ya tatu BK.

 

Inadaiwa kwamba katika siku za Ahazi, sadaka za asubuhi zilikuwa ni sadaka za kuteketezwa na sadaka za jioni kwa kawaida zilikuwa ni za nafaka (2Wafalme 16:15) (sawa na Schürer, ibid., p. 300). Kwa hiyo, ilimaanisha kwamba sadaka za kuteketezwa zilitolewa jinoni (lWafalme 18:29-36). Hata hivyo, tunajia pia kwamba sadaka za kuteketezwa zilikuwa zinatolewa jioni (Ezra 9:4,5; Danieli 9:21). Schürer anaweka hoja hii ili kufanya madai kwamba kulikuwa na mabadiliko katika utoaji wa sadaka hizi. Nabii Ezekieli anatuonyesha kwamba sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka zilitolewa jioni (Ezekieli 46:13-15). Hata hivyo, Schürer anadai kuwa hii inaashiria mabadiliko ya utaratibu wa utoaji wa sadaka (ibid.). katika kusaidia madai haya ndipo anasema kwamba maandiko yanakinzana, na kile kinachoitwa “nakala za maelekezo ya makuhani” yanayosema kwamba sadaka za kuteketezwa na za nafaka zilitolewa katika nyakati zote mbili za asubuhi na jioni, na sadaka za vinywaji kila moja (Kutoka 29:38-42; Hesabu 28:3-8). Utoaji wa sadaka ya kuteketezwa mara mbili kwa siku ulidumu kwa siku nyingi, kama tunavyoona kwenye vitabu vya Mambo ya Nyakati (lNyakati 15:40; 2Nyakati 8:11, 31:3).

 

Ukweli wa mambo ni kwamba sadaka zote mbili za daima au za kila siku za asubuhi na za jioni zilikuwa kwenye utaratibu wake mkamilifu wa kiibada, na zilihitaji utaratibu mkamilifu, juhudi au bidii na kuzijali kwene maeneo yote matatu ya taifa, yaani kutoka kwa Makuhani, Walawi hadi kwenye Migawanyo ya Kitaifa kwenye maeneo yao ya makazi yao. Sadaka za asubuhi ziliona mchakato ukiwekwa kutoka mapema sana asubuhi wakati siku ikiwa imeanza, na wahudumu waliohitajika sana wakianza kusafisha majivu madhabahuni ya sadaka ya kuteketezwa. Wale waliopangiwa na kutakikana kuhudumu walikuwa wamekwisha oga tayari kabla ya kuwasili kwa maafisa au wakuu wa watu. Wanapiga kura ili kumpata atakayehudumu kazi hizi. Katika kuuwasha moto wa madhabahun,imtu aliyechaguliwa alinawa kwanza mikono yake na miguu yake kwene beseni la shaba na kusimama kati ya Hekalu na madhabahu, anashuka kupitia kwenye ngazi na kuyasafisha majivu kwa bakuli ya fedha. Wakati mambo haya yakifanyika, makuhani wanaandaa sadaka ya nafaka zilizosagwa za Kuhani Mkuu aliyekuja na kushiriki kazi zao.

 

Kuni nzuri zililetwa madhabahuni. Wakati zilipokuwa zinawashwa makuhani waliosha mikono yao na miguu yao na hatimaye walikwenda kulikokuwa kunaitwa lishkath ha-gazith, ambapo palikuwa ni mahala ma kukutania pa baraza la Sanhedrin tangu kipindi kile hadi lilipobomolewa Hekalu. Wakiwa huko wanapiga kura nyingine zaidi. Mkutano wao huu kwene nukuu za Agano Jipya ulifanyika kwenye nyumba ya Kuhani Mkuu kama ilivyoelezewa kwenye mchakato wa usio wa kawaida kujadili jambo majira ya usiku (sawa na alivyosema Schürer, ibid., pp. 224-225).

 

Wakuu hawa walipiga kura ili kuamua mambo yafuatayo: 1) wachinjaji; 2) wapakaji dhamu kwenye madhabahu; 3) ni nani atakayesafisha majivu kwenye madhabahu ya ndani; 4) ni nani atasafisha taa, na kumpata mtu atakayeleta kila kipande cha mnyama atakayetolewa sadaka kwenye ngazi za madhabahu, ambazo ni: 5) kichwa na paja moja; 6) miguu miwili; 7) mkia na paja jingine la mguu; 8) kidari na shingo; 9) vipade viwili; 10) matumbo; 11) mtu atakayebeba unga mzuri; 12) sadaka za nafaka zilizookwa (za Kuhani Mkuu); 13) mvinyo (sawa na alivyosema Schürer, ibid., p. 304).

 

Utoaji wa sadaka huu haukufanyika kipindi cha jua kuwaka mchana. Wakati kondoo alipokuwa anachaguliwa au kuteuliwa majira ya alasiri, basi makuhani wawili waliochaguliwa kusafisha madhabahu yenye uvumba na kinara cha taa walikwenda Hekaluni – ya zamani ilikuwa ya bakuli la dhahabu na hatimaye lililofuatia lilikuwa la guduli. Walilifungua lango kuu la Hekalu na kuingia ndani. Kuhusu kinara hiki cha taa cha dhahabu, ikiwa vinara viwili vikielekea upande wa mashariki vikiwaka, basi viliachwa bila kuguswa na ni vile vinara vilivyobakia tu ndizo zilikuwa zinasafishwa. Iwapo kama hivi vinara vilivyo upande wa mashariki vikienda nje, ndipo vilisafishwa na kuwashwa tena kwanza, kabla ya mkumbushaji vilisafishwa na kujazwa.

 

Makuhani wawili waliachilia mbali ala walizokuwa wakizitumia Hekaluni walipoondoka.

 

Wakati walipokuwa wanashughulikia usafishaji, makuhani wengine waliopangiwa walimchagua mwanakondoo na kumchinja. Ndipo hatimaye alichunwa na kukatwakatwa vipande na kila kuhani aliyechaguliwa alipokea kipande alichostahili. Mnyama aligawanwa kwa makuhani sita kwa ujumla. Matumbo yalioshwa kwenye kwenye meza za malumalu iliyoko machinjioni. Kuhani wa saba alikuwa na sadaka ya unga, wa nane alikuwa na sadaka ya nafaka zilizokandwa za Kuhani Mkuu, na wa tisa alikuwa na sadaka ya kinywaji cha mvinyo. Hizo zote ziliwekwa upande wa mashariki ya ngazi za kupandia kuelekea madhabahuni na ilienezwa chumvi. Ndipo hatimaye kuhani aliiondoa hadi kwenye lishkath ha-gazith ambako waliomba dua maalumu zilizojulikana kama Shema. Kwa kufanya hivi wanapiga kura tena Kwanza, kura hii ilipigwa kwa utoaji wa Sadaka ya ya Uvumba kwa ajili ya wale ambao hawajawahi kuifanya kazi hii. Kwa hiyo kura zilipigwa ili kumpata atakayebeba mambo ya mtu yahusuyo sadaka ya kujitoa madhabahuni. (Kwa mujibu wa R. Eliezar bin Jacob, kuhani yuleyule aliyefanya hivi kwa kawaida ndiye anayeifanya kazi hii na ndiye anayewachukua hadi kwenye ngazi za madhabahuni.) Wale ambao kura haikuwaangukia walikuwa huru kuondoka, na walivua mavazi yao matakatifu na kuondoka.

 

Makuhani waliochaguliwa ili kuleta sadaka ya uvumba sasa walichukua kifuniko cha dhahabu likiwa na bakuli ndogo yene uvumba ndani yake. Kuhani wapili alitafuta na kuchukua mkaa wa madhabahuni wa sadaka ya kuteketezwa kwenye mkuki au bakuli ya fedha na kuumwagia kwenye umma au bakuli ya dhahabu. Kisha wote wawili watakwenda Hekaluni. Mmoja wao atamwaga ule mkaa kwenye madhabahu yenye uvumba, akiingia kwenye hali ya ibada na kisha ataishia hapo. Makuhani wengine walichukua bakuli dogo lenye ubumba ndani kutoka kwene bakuli kubwa, akimkabidhi waraka kuhani wa tatu na kisha kumwaga uvumba kutoka kwenye bakuli na kuumwaga mkaa kwenye madhabahuni ili kuuruhusu moshi upae juu. Yeye alijifanyia ibada pia na kisha aliishia hapo. Wawili waliofanya kazi ya kusafisha madhabahu na vile vinara vya taa, waliingia tena Hekaluni kabla hawa wengine hawajatafuta vifaa vingine kama vilivyotajwa hapo juu. Msafishaji wa vinara vya taa ndipo alisafisha kwa urahisi zaidi hizi taa zilivyokuwa bado vichafu. Nyingine ziliachwa zikiwaka ili nyingine ziwashwe kutoka na hizi ifikapo jioni. Kama zingekuwa zimeondolewa basi zingesafishwa na kuwashwa tena kwa moto wa madhabahuni wa sadaka za kuteketezwa.

 

Makuhani watano wanaoshughulika kwa kazi nyingi Hekaluni ndpo wanapanda ngazi wakielekea mbele ya patakatifu au maskani huku wakiwa na ala tano za dhabahu na kutangaza Baraka za kikuhani kwao (Hesabu 6:22-23) kwa watu. Kwa kufanya hivyo wanakuwa wamelitangaza Jina Takatifu kama ilivyoandikwa. Walisema Yahova. Hawakusema Adonai (sawa na Schürer, ibid., p. 306). Kwa hiyo wazo la kusema kwamba kuhani hakulitaja jina la Mungu ni la uwongo. Sio tu kwamba walilitaja tu, bali pia walilitangaza kwenye maombi ya hadharani yakiwa kama sehemu ya huduma zao Hekaluni huko Yerusalemu na kwingineko kote.

 

Pili, utoaji wa sadaka ya kuteketezwa uliendelea. Kuhani aliyechaguliwa aliweka mikono yake juu vipande vilivyotenganishwa vya mnyama aliyetolewa sadaka aliyelazwa kwenye ngazi za madhabahu na walimchukua madhabahuni na kumuweka na kumuacha hapo (alitupwa, anavyosema Schürer) hapo madhabahuni. Wakati Kuhani Mkuu alipotaka kujihusisha, alidaiwa kwamba alikuwa na mikono ya makuhani kumpa vipande hivi mkononi mwake (sawa na Mhubiri 1:12) na alivitupa juu ya madhabahu. Mwisho ni sadaka mbili linguine za nafaka—ya watu na Kuhani Mkuu—ambayo ilitolewa pamoja na sadaka ya vinwaji. Wakati makuhani waliponama kuimwaga sadaka ya vinywaji, ishara ilionyeshwa kwa Walawi ili waanze kuimba. Ndipo walianza kuimba kwa namna zao aote na kila walipopumzika kuimba, mekuhani wawili walizipiga baragumu za fedha. “Na kila mlio wa baragumu ulipopigwa, watu walijiinamisha na kusujudu” (Schürer, ibid.). “Ibada ya jioni ilikuwa sawa tu na ile ya asubuhi. Kipindi cha zamani, hata hivyo, sadaka ya uvumba ilitolewa mwishoni kuliko kuitoa baada ya sadaka ya kuteketezwa, na taa zilizo kwene kinara zikwa hazijasafishwa bado tayari kwa kuziwasha jioni” (sawa na alivyosema pia Schürer, p. 303).

 

Watu walikuwa wanajikusanya wenyewe Hekaluni wakati wa kuendelea kwa mcakato huu wa maandalizi ya asubuhi kwa ajili ya dhabihu za mwisho. Walijinyenyekesha na kuina kusujudu, wakati baragumu zilipopigwa wakati uimbaji ulipopumzishwa. Kulikuwa na Zaburi za namna mbalimbali zilizopangiliwa kwa kila juma. Nyimbo au Zaburi zilizoimbwa siku ya Kwanza ya Juma, Jumapili ilikuwa Zaburi ya 24; siku ya pili ya juma, Jumatatu, ilikuwa ni Zaburi 48; Jumanne ilikuwa ni Zaburi 82; Jumatano ilikuwa Zaburi 94; Alahamisi ilikuwa Zaburi 81; Ijumaa Zaburi 93; na siku ya Sabato ilikuwa Zaburi 92.

 

Maana ya kiroho ya harakati hizi inavutia sana. Sadaka hii ya asubuhi haikutolewa saa za alfajiri na kuendelea hadi asubuhi. Bali watu walikuweo na walishiriki harakati hizi ambazo zilifikia kilele chake yapata saa tatu ya asubuhi.

 

Utoaji wa sadaka unawakilisha au kuonyesha maendeleo mema ya Imani. Pasaka inayomtaja Masihi kuwa ni kama Mwanakondoo na malimbuko na Mganda wa Kutikiswa. Dhabihu ya jioni ilimaanisha Mkutano Mkubwa wa Kanisa. Sabato, Miandamo ya Mwezi na Siku Takatifu zinawakilisha wateule 144,000. Kila adhimisho moja la Sabato, na kadhalika zina utoaji wa sadaka za asubuhi na jioni, ambazo ni muhimu kwa wateule katika kuendelea vizuri katika Roho Mtakatifu kupitia uhusiano wao na Mungu. Kanisa lote la Mungu linatakiwa kuwa na tabia hii ya kutoa dhabihu za jioni, ingawa hazikutajwa kama dhabihu za jioni kwenye utaratibu wa Hekalu lijalo.

 

Ingekuwa wazi kwetu sote kwamba ibada za Kanisa kuwa ni saa 3 asubuhi na saa 9 alasiri katika kila siku ya kusanyiko. Kanisa lilikusanyika saa 4 asubuhi na saa 8 mchana kwa kila Siku hizohizo Takatifu lakini kila mara walikutana saa 3 asubuhi kwa maadhimisho ya Mganda wa Kutikiswa na Pentekoste. Hii imekuwa ni kwa kuwa ndugu wengi wanasafiri umbali mrefu hadi kufika kwenye ibada watafuata nywkati za kawaida wa dhabihu za asubuhi na za jioni.

 

Kristo aliishika pia Sabato kwa bidii na uaminifu, na katika siku hizi hakuna biashara iliyokuwa inaruhusiwa kufanyika sawa na alivyosema nabii Amosi 8:5. Kwenye Mathayo 14:14-15, tunaona kwamba watu walimuendea Kristo wakati wa utoaji dhabihu ya jioni, ambayo iliuwa ama ya siku ya Mwandamo wa Mwezi au Sabato. Wakati Sabato ilipokuwa imeisha, na ilikuwa jioni na watu walikuwa bado wamekusanyika pamoja, wanafunzi wake walimwambia kama wangeruhusiwa kuondoka na kwenda kununua chakula.

 

Mathayo 14:14-15  Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao. 15 Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.

 

Kanisa kama bodi ya wafalme na makuhani linawajibika kufanya maombi ya kila siku, kwa mara zote mbili yaani asubuhi na jioni (Kutoka 30:7-8). Maandalizi na maombi ya asubuhi yanatangulia kipindi cha utoaji dhabihu za jioni. Kwa hiyo maombi yetu yanafanya kazi mbadala ya sadaka ya uvumba na uwashaji wa kinara cha taa ya dhahabu kinachosimamishwa mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, na kuuombea ulimwengu kwa Mungu. Na ndiyo maana wale Wazee ishirini na nne wamepangiwa kuratibu maombi yetu na wanatusaidia sisi (Ufunuo 5:8-10).

 

Kuna umuhimu wa kuwa imara kwenye Imani kwa masuala ya Kalenda. Yule tunayemuabudu hajulikani kwa uelewa wetu au ujuzi wetu tu kuhusu asili ya Mungu peke yake. Ukweli wa kwamba kuna Mungu mmoja tu wapekee na wa Kweli, ambaye ndiye Baba yetu sisi sote, aliyemtuma Yesu Kristo – na anayeweka msingi wa ibada zetu – inaweza kushushwa umuhimu wake kwa ajili ya kukosea kuifanyia kazi Kalenda na mchakato wa ibada. Kama tutaishika kalenda ya uwongo, basi tujue kwamba tutakuwa tunamuabudu mungu aliyeiweka na kuimuru kalenda hiyo. Kama tutaziahirisha siku za kufanyia ibada, ndipo tujue kwamba tunamuweka mungu mwingine badala ya Mungu wa Pekee na wa Kweli. Basi na usipotoshwe. Ishikilie Imani iliyotolewa kwa watakatifu.

Zaburi

Kama tulivyojionea, utaratibu wa ibada Hekaluni uliotumia Zaburi maalumu kila siku kwa kutolea dhabihu za kila siku. Tangu Siku ya Kwanza ya juma, tunayoiita Jumapili kwenye utaratibu wa kalenda ya kipagani, tunaona kwamba Zaburi 24 inaanza kwa kulitaja tukio la uumbaji wa Mungu. Kwenye Zaburi hii tunaona uendelezaji wa mwanadamu kwa Roho Mtakatifu, na mtu anayetembea na Mungu kwenye mlima wa Yahova.

 

Kinyume na ngano au hadithi mashuhuri, uandishi wa jina la Mungu ulitajwa kwa wazi kwenye ibada za Hekaluni, na jina hilo lilikuwa ni Yahova (YHVH) na Adonai. Halikuwa linatamkwa na makuhani peke yao kila siku, bali lilikuwa linaimbwa na mkutano wote na makuhani wote kwa ujumla wao kama baraza la Israeli kwenye Zaburi.

 

Zaburi au Tenzi hizi zilichaguliwa ili kulionyesha taifa kuwa limechaguliwa na Mungu. Zinawatambulisha Israeli kuwa ni wateule wa Mungu, na kwamba wokovu wa Issraeli wote unakuja na utasababisha mwanzo wa kuwepo kwa ibada ya Israeli kwenye mlima wa Yahova, Aliye Tukuka Sana.

 

Zaburi za kila siku zinaonyesha maendeleo ya uumbaji wa kipindi chote cha miaka elfu sita yaliyoruhusiwa na Mungu hadi itakapofika Sabato ya Milenia, ambayo inawakilisha au kivuli cha utawala wa Haki utakaokuwa chini ya mamlaka ya Masihi na wateule wake Wtakatifu.

 

Siku ya Kwanza ya Juma (Jumapili): Zaburi 24 (Mfalme wa Utukufu) – Zaburi ya Daudi

 

Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu. Sela

 

Hapa tunaona kwamba elohim wa wokovu wa Israeli na wa kila mmoja alikuwa ni huyu Yahova wa Majeshi, na ni Mungu wa Mababa wa imani. Hapa mwanzoni mwa juma, mkutano wa Mungu unaelezewa kwamba viufmbe wote ni mali ya Yahova. Makutano wanaambiwa wamekubaliwa na Mungu kwa kumfanyia ibada na wale wataomwendea Mungu na kumjongelea karibu.

 

Siku ya Pili ya Juma (Jumatatu): Zaburi 48 (Sayuni Inasifiwa) – Zaburi ya wana wa Kora

 

Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu. Mungu katika majumba yake Amejijulisha kuwa ngome.


Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walipita wote pamoja. Waliona, mara wakashangaa; Wakafadhaika na kukimbia. Papo hapo tetemeko liliwashika, Utungu kama wa mwanamke azaaye. Kwa upepo wa mashariki Wavunja jahazi za Tarshishi

.
Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Katika mji wa Bwana wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu ataufanya imara hata milele. Sela


Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu, Katikati ya hekalu lako. Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu, Ndivyo na sifa yako hata miisho ya dunia. Mkono wako wa kuume umejaa haki; Na ufurahi mlima Sayuni. Binti za Yuda na washangilie Kwa sababu ya hukumu zako.


Tembeeni katika Sayuni, Uzungukeni mji, Ihesabuni minara yake, Tieni moyoni boma zake, Yafikirini majumba yake, Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja. Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza.

 

 Katiku ya pili ya juma Mji wa Sayuni unatajwa kuwa ni Mji wa Yahova. Hekalu hili linatajwa kuwepo kule. Mgongano na Yahova unamfanya alilinde kikamilifu kutaniko kwa ujumbe wa Zaburi. Meli za Tarshishi zilitia nanga huko Ulaya pande za kusini mwa Iberia, au kusini mwa Hispania. Walisaidia kuweka taratibu imara za kibiashara ulimwenguhni kote.

 

Yahova ni Yahova wa Majeshi na kwa hiyo Yahova ni Mkuu na Aliye Juu Sana.

 

Siku ya Tatu ya Juma (Jumanne): Zaburi 82 (Ombi la Hukumu ya Haki) – Zaburi ya Asafu

 

Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu. Hata lini mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya? Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara; Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.

 

Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika.

 

Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia. Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.

 

Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana Wewe utawarithi mataifa yote.

 

 Tunaona kutoka kwenye Zaburi hii kwamba elohim wanatajwa kwa majina ya uwingi ya wana wa Mungu, na elohim anayeulizwa swali hapa kwenye kutaniko la mkutano wa mbinguni wa Baraza la Elohim. Anaanza kuihukumu dunia kwa kuwa mataifa yote yameletwa hukumuni mwake.

 

Kitu cha kwanza kufanyika kwenye uumbaji ni Malaika wa mbinguni ambao ni elohim. Wanadamu walioongoka pia wanafanyika kuwa wana wa Mungu kama elohim, na ni hapa kwenye siku hii ya tatu ya juma, ambayo kwa sasa inaitwa Jumanne, ndipo Zaburi hii ilikuwa inaimbwa. Hii ni siku iliyotangulia ile ya maandalizi iliyokuwa siku ya 14 Abibu mwaka 30 BK.

 

Kwa hiyo, wakati Kristo alipoyatamka maneno haya, yeye mwenyewe na kila aliyekuwepo pale alijua kuwa yalikuwa yanaimbwa siku ile na hadi kabla ya kuchwa kwa jua siku ile, wastani wa takriban masaa sita yaliyotangulia.

 

Kuhani Mkuu aliona kwamba siku iliyotangulia siku ile kuliimbwa Zaburi hii, kusudi la andiko hili liliwekwa wazi, na Kristo alitangaza hatima ya kimbinguni ya wateule. Imeandikwa kwamba kuhani Mkuu alitabiri mapema kabisa kabla ya matukio kwamba yapasa mtu mmoja afe kwa faida ya wengi.

 

Andiko lililofuatia nukuu ya Kristo linaonyeha elohim atakayekuja atauhukumu Ulimwengu, na kwamba elohim huyo ni Masihi.

 

Kwa hiyo Kuhani Mkuu alimuona Kristo kuwa amejitangaza mwenyewe kuwa ni Masihi, Mwana wa Mungu. Zaburi ya siku ya nne, au ya Jumatano, inathibitisha ukweli huu na Kuhani Mkuu alijua hivyo, kama ilivyokuwa kwa kila mtu.

 

Siku ya Tano ya Juma (Jumatano): Zaburi 94 (Mhukumu wa Haki)

 

Ee Bwana, Mungu wa kisasi, Mungu wa kisasi, uangaze, Mwenye kuihukumu nchi, ujitukuze, Uwape wenye kiburi stahili zao.


Bwana, hata lini wasio haki, Hata lini wasio haki watashangilia? Je! Wote watendao uovu watatoa maneno, Na kusema majivuno, na kufanya kiburi? Ee Bwana, wanawaseta watu wako; Wanautesa urithi wako; Wanamwua mjane na mgeni; Wanawafisha yatima. Nao husema, Bwana haoni; Mungu wa Yakobo hafikiri.

 

Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini; Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili? Aliyelitia sikio mahali pake asisikie? Aliyelifanya jicho asione? Awaadibuye mataifa asikemee? Amfundishaye mwanadamu asijue? Bwana anajua mawazo ya mwanadamu, Ya kuwa ni ubatili.

 

Ee Bwana, heri mtu yule umwadibuye, Na kumfundisha kwa sheria yako; Upate kumstarehesha siku za mabaya, Hata asiye haki atakapochimbiwa shimo. Kwa kuwa Bwana hatawatupa watu wake, Wala hutauacha urithi wake, Maana hukumu itairejea haki, Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata.

 

Ni nani atakayesimama Kwa ajili yangu juu ya wabaya? Ni nani atakayenisaidia Juu yao wafanyao maovu? Kama Bwana asingalikuwa msaada wangu, Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya. Niliposema, Mguu wangu unateleza; Ee Bwana, fadhili zako zilinitegemeza. Katika wingi wa mawazo ya moyoni mwangu, Faraja zako zaifurahisha roho yangu.

 

Je! Kiti cha udhalimu kishirikiane nawe, Kitungacho madhara kwa njia ya sheria? Huishambulia nafsi yake mwenye haki, Na kuihukumu damu isiyo na hatia. Lakini Bwana amekuwa ngome kwangu, Na Mungu wangu mwamba wangu wa kukimbilia. Naye atawarudishia uovu wao, Atawaangamiza katika ubaya wao, Naam, Bwana, Mungu wetu, atawaangamiza.

 

Ikumbukwe hapa kwamba huyu Elohim mwenye kisasi na haki anayeetajwa hapa ni Yahova aliyewapa Israeli urithi wake. Kwa hiyo, dhana iliyopo hapa ni Yahova wa Majeshi aliyempa mamlaka Yahova wa Israeli. Kiumbe au mtu huyu ni Yahova aliyeandikwa kwenye Kumbukumbu la Torati 32:8, ambaye alikuwa mmoja wa wana wa Mungu. Tafsiri ya Masoretic text (MT) ilibadilishwa baada ya tukio hili na kifo cha Masihi na kusomeka: sawa na idadi ya wana wa Israeli. Bila shaka ilifanyika ili kuficha wazo hili. Hata hivyo, andiko linasema, sawa na idadi ya wana wa Mungu, kama tunavyojua kutoka kwenye tafsiri ya Septuagint (LXX), na sasa kutoka kwenye gombo lijulikanalo kama “the Dead Sea Scrolls (DSS)”. Tafsiri ya RSV inaonyesha kuandikwa kiusahihi.

 

Shutuma dhidi ya majivuno na kiburi zinazoonyeshwa hapa ziliwalenga moja kwa moja makuhani ambao kwa kweli walikuwa wanawahukumu watu wasio na hatia na hapa wanamuua Masihi. Andko hili lote lililenga moja kwa moja kwa wenye kupenda dhuluma na matendo ya dhuluma, na Kuhani Mkuu alijua kwamba ndicho walichokuwa wanamfanyia Kristo kwa kupitia unabii na ushuhuda wake Kristo mwenyewe kwenye kipindi chenyewe na muafaka kwenye mchakato huu. “Mimi”anayejiita kwenye andiko hili ni Masihi.

 

Siku ya Tano ya Juma (Alhamisi): Zaburi 81 (Wito wa Kutii) – wa Waasafu Wagiti

 

Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha, Mshangilieni Mungu wa Yakobo. Pazeni zaburi, pigeni matari, Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda. Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu. Kwa maana ni sheria kwa Israeli, Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo. Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu, Alipoondoka juu ya nchi ya Misri;

 

Maneno yake nisiyemjua naliyasikia. Nimelitenga bega lake na mzigo, Mikono yake ikaachana na kikapu. Katika shida uliniita nikakuokoa; Nalikuitikia katika sitara ya radi; Nalikujaribu penye maji ya Meriba.

Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya, Ee Israeli, kama ukitaka kunisikiliza; Usiwe na mungu mgeni ndani yako; Wala usimsujudie mungu mwingine. Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.

 

Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu, Wala Israeli hawakunitaka. Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao, Waenende katika mashauri yao. Laiti watu wangu wangenisikiliza, Na Israeli angeenenda katika njia zangu; Ningewadhili adui zao kwa upesi, Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu;


Wamchukiao Bwana wangenyenyekea mbele zake, Bali wakati wao ungedumu milele. Naam, ningewalisha kwa unono wa ngano, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani.

 

Zaburi hii ilikuwa ni ya kuwaonya Israeli baada ya wao kumuacha Yahova aliyewatoa Utumwani. Kwa ukweli walimuua na ni siku iliyotangulia katika mwaka ule wa 30 BK. Israeli walichukuliwa kutoka jangwani na kujaribiwa kwenye maji ya Meriba – na kwamba huyu Elohim aliyekuwa na wao akiwaongoza alikuwa ni Kristo. Hawakumsikiliza na Yahova aliwalipa sawasawa na ugumu wa shingo zao na matendo yao.

 

Zaburi zinautaja Mwandamo wa Mwezi wa Abibu kuwa ni Siku takatifu ya Sikukuu kwa Israeli. Huu ni Mwaka Mpya ulioamriwa. Wayahudi walioishi kipindi zama cha kale kabla ya utawanyiko waliibadili hii ili isomeke "katika Mwandamo wa Mwezi na Mwezi Mkamilifu", na kisha waliitumia ili kuifananisha siku ya 1 Tishri kuwa ni Mwezi wao Mpya kwa mafundisho yao mapotofu. Lakini maandiko ya asili yanasema siku ya Mwandamo wa Mwezi, na andiko linaonyesha wazi kwamba inahusiana na Kutoka mwezi wa Abibu na kwa hiyo haliwezi kumaanisha mwezi wa Tishri.

 

Siku ya Sita ya Juma (Ijumaa): Zaburi 93 (Utawala wa Milele wa Mungu)

 

Bwana ametamalaki, amejivika adhama, Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike; Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani; Wewe ndiwe uliye tangu milele.

 

Ee Bwana, mito imepaza, Mito imepaza sauti zake, Mito imepaza uvumi wake. Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana Aliye juu ndiye mwenye ukuu.

 

Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee Bwana, milele na milele.

 

 Kwa hiyo, tunaona hapa kwamba Yahova aliye Juu anasifiwa kuwa ni Mkuu. Katika siku hii iliyo kwenye mchakato wa Pasaka ya mwaka 30 BK, Masihi alikuwa bado yuko kaburini.

 

Siku ya Saba ya Juma (Jumamosi): Zaburi 92 (Upendo wa Mungu na Uaminifu wake) – Wimbo wa siku ya Sabato

 

Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu. Kuzitangaza rehema zako asubuhi, Na uaminifu wako wakati wa usiku. Kwa chombo chenye nyuzi kumi, Na kwa kinanda, Na kwa mlio wa kinubi.

 

Kwa kuwa umenifurahisha, Bwana, Kwa kazi yako; nitashangilia Kwa ajili ya matendo ya mikono yako. Ee Bwana, jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa. Mtu mjinga hayatambui hayo, Wala mpumbavu hayafahamu. Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele;

 

Bali Wewe, Bwana, U Mtukufu hata milele. Maana hao adui zako, Ee Bwana, Hao adui zako watapotea, Na watendao maovu watatawanyika wote pia. Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati, Nimepakwa mafuta mabichi. Na jicho langu limewatazama walioniotea, Sikio langu limesikia habari za waovu walionishambulia.

 

Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni. Waliopandwa katika nyumba ya Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu wetu. Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. Watangaze ya kuwa Bwana ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu.

 

Zaburi hii inamsifu Yeye aliye Juu Sana na Mwenyezi aliye mwaminifu katika upendo na anayestahili kuabudiwa na kupewa sifa, kwa nyakati zote mbili, asubuhi na jioni.

 

Siku ya Sabato tunajionea ujumbe unaokanganya wa aina mbili. Ilikuwa ni mwishoni mwa siku hii ndipo Masihi alifufuliwa na Mungu na akajihudhurisha kwenye baraza ya elohim. Ahadi ya Zaburi hii inaendelea hadi kipindi cha Milenia na Utawala wa Masihi. Sabato ni kivuli cha utawala huu unaokuja kwenye kipindi cha jumla ya miaka elfu saba tangu kuumbwa kwa Adamu.

 

Ufufuko wa Kristo mwishoni mwa Sabato ni alama au kivuli ashirio cha Ufufuo wa watu Wote waliokufa utakaofanyika mwishoni mwa kipindi cha millennia. Toka kipindi hiki na tukio hili tutakuwa tunajiandaa kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wote na kukabidhiwa mamlaka yote Mwenyezi Mungu.

 

Siku ya Jumapili asubuhi, majira ya saa 3 asubuhi, Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa ilitolewa kwa kuutikisa mganda mbele za Mungu. Jumapili asubuhi baada ya kufufuka kwake jioni iliyotangulia, Kristo alipaa hadi kwenye Mlima wa Mungu huko Mbinguni. Hapa alikuwa amekwisha kubalika kuwa ni sadaka ya haki na takatifu ya ulimwengu wote. Zaburi hii pia inaonyesha ukweli wa kukubalika kwa utakatifu kwenye kipindi au zama mpya. Kukubalika kwa wanadamu wote waliotubu kunaashariwa kwenye Mganda huu wa Kutikiswa ukianzia kwa Kristo na kuendelea hadi kwetu sisi sote.

 

Kwa hiyo, mchakato wa matukio katika Pasaka ya juma la kusulibiwa ulionekana kwa miaka elfu moja kabla yake. Uwongo kuhusu kwamba dhabihu hii ilitolewa siku ya Ijumaa inapingana na ukweli wa dhana iliyo kwenye Zaburi hii ya ibada za Hekaluni na maana zake kwa wanadamu.

 

******

Zaburi hizi kwenye jarida la Kiingereza zimenukuliwa kutoka kwenye tafsiri ijulikanayo kama the Holman Christian Standard Bible, Holman Bible Publishers, 2003, pamoja na majina yote yaliyobadilishwa kutoka kwenye matumizi yake ya asili ya Kiebrania. Wakati ambapo aya zote kwene jarida hili la Kiswahili zimenukuliwa kutoka kwenye Biblia ya Union Version.

 

Tafsiri ya Holman kwa kifupi HCSB mara nyingi imetafsiri Kiebrabia majina ya Mungu kama ifuatavyo:          

 

Tafsiri ya Kiingereza ya HCSB

Kiebrania Asilia

God - Mungu   

Elohim

LORD - BWANA

YHVH (Yahovah)

Lord    - Bwana

Adonai

Lord GOD-Bwana Mungu

Adonai Yahovah

LORD of Hosts-Bwana wa Majeshi

Yahovah Sabaoth

God Almighty-Mungu Mwenyezi

El Shaddai

 

q