Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[108]

 

 

 

Maana ya Maono ya Nabii Ezekieli

(Toleo La 3.0 19950421-19990703-20071114-20080310)

 

Maono ya nabii Ezekieli yameonekana kuwa ni kama chombo au viumbe wa angani wenye matairi na mabawa na viumbe wengine wa aina ya wanyama. Biblia inawataja kwa wazi sana viumbe hawa kuwa ni Makerubi. Je, maono yake yana maana gani? Ni mafundisho gani basi tunayojifunza kutkana na maono haya? Hapa tunaona maana yake

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hatimiliki © 1995, 1998, 1999, 2007, 2008  Wade Cox)

(tr. 2015)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 


Maana ya Maono ya Nabii Ezekieli

 


Ezekiel 1:1-28 Ikawa katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa pamoja na watu waliohamishwa, karibu na mto Kebari, mbingu zilifunuka, nikaona maono ya Mungu. 2 Siku ya tano ya mwezi, nao ulikuwa ni mwaka wa tano wa kuhamishwa kwake mfalme Yehoyakini, 3 neno la Bwana lilimjia Ezekielii, kuhani, mwana wa Buzi, kwa dhahiri, katika nchi ya Wakaldayo, karibu na mto Kebari; na mkono wa Bwana ulikuwa hapo juu yake. 4 Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo. 5 Kukatokea katikati yake mfano wa viumbe hai vinne. Kuonekana kwao kulikuwa hivi; walikuwa na sura ya mwanadamu. 6 Na kila mmoja alikuwa na nyuso nne, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne. 7 Na miguu yao ilikuwa miguu iliyonyoka; na nyayo za miguu yao zilikuwa kama nyayo za miguu ya ndama; zikimetameta kama rangi ya shaba iliyosuguliwa sana. 8 Nao walikuwa na mikono ya mwanadamu chini ya mabawa yao, pande zote nne; na wote wanne walikuwa na nyuso zao na mabawa yao hivi; 9 mabawa yao yaliungana, hili na hili; nao hawakugeuka walipokwenda, walikwenda kila mmoja kuelekea mbele. 10 Kwa habari za mfano wa nyuso zao; walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kuume; na hao wanne walikuwa na uso wa ng'ombe upande wa kushoto; na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia. 11 Na nyuso zao na mabawa yao yalikuwa yametengana kwa juu; mabawa mawili ya kila mmoja yaliungana, hili na hili, na mawili yalifunika miili yao. 12 Nao walikwenda kuelekea mbele, kila mmoja wao; roho ilikotaka kwenda ndiko walikokwenda; hawakugeuka walipokwenda. 13 Kwa habari za kuonekana kwao vile viumbe hai; kuonekana kwao kulikuwa kama makaa ya moto yawakayo, kama kuonekana kwa vinga vya moto; moto ule ulikuwa ukienda juu na kushuka chini, katikati ya vile viumbe hai; na ule moto ulikuwa na mwangaza mwingi, na katika ule moto ulitoka umeme. 14 Na vile viumbe hai walipiga mbio, kwenda na kurudi, kama kuonekana kwa kumulika kwa umeme. 15 Basi, nilipokuwa nikivitazama vile viumbe hai, tazama, gurudumu moja juu ya nchi, karibu na kila kimoja cha vile viumbe hai, pande zake zote nne. 16 Kuonekana kwake magurudumu hayo na kazi yake kulikuwa kama rangi ya zabarajadi; nayo yote manne yalikuwa na mfano mmoja; na kuonekana kwake na kazi yake kulikuwa kana kwamba ni gurudumu ndani ya gurudumu lingine. 17 Yalipokwenda yalikwenda pande zote nne; hayakugeuka yalipokwenda. 18 Katika habari za vivimbe vyake; vilikuwa virefu, vya kutisha; nayo yote manne, vivimbe vyake vimejaa macho pande zote. 19 Na viumbe hao walipokwenda, magurudumu yalikwenda kandokando yao, na viumbe hao walipoinuliwa, magurudumu nayo yaliinuliwa. 20 Kila mahali ambako roho hiyo ilitaka kwenda, walikwenda; walikuwa na roho ya kwenda huko; nayo magurudumu yaliinuliwa karibu nao; kwa maana roho ya viumbe hai ilikuwa ndani ya magurudumu. 21 Walipokwenda hao, yalikwenda hayo nayo; na waliposimama hao, yalisimama hayo nayo; na walipoinuliwa hao juu ya nchi, magurudumu yaliinuliwa karibu nao; maana roho ya viumbe hai ilikuwa ndani ya magurudumu. 22 Tena juu ya vichwa vya viumbe hai palikuwa na kitu mfano wa anga, kama rangi ya bilauri, lenye kutisha, limetandwa juu ya vichwa vyao. 23 Na chini ya anga mabawa yao yamenyoshwa, moja kulielekea la pili; kila mmoja alikuwa na mawili yaliyowafunika miili yao upande mmoja, na kila mmoja alikuwa na mawili yaliyowafunika miili yao upande wa pili. 24 Nao walipokwenda nalisikia mshindo wa mabawa yao, kama mshindo wa maji makuu, kama sauti yake Mwenyezi, mshindo wa mvumo, kama mshindo wa jeshi; hapo waliposimama walishusha mabawa yao. 25 Tena palikuwa na sauti juu ya anga lile, lililokuwa juu ya vichwa vyao; hapo waliposimama walishusha mabawa yao. 26 Na juu ya anga, lililokuwa juu ya vichwa vyao, palikuwa na mfano wa kiti cha enzi, kuonekana kwake kama yakuti samawi; na juu ya mfano huo wa kiti cha enzi, ulikuwako mfano kama kuonekana kwa mfano wa mwanadamu juu yake. 27 Nikaona kana kwamba ni rangi ya kaharabu, kama kuonekana kwa moto ndani yake pande zote, tangu kuonekana kwa viuno vyake na juu; na tangu kuonekana kwa viuno vyake na chini, naliona kana kwamba ni kuonekana kwa moto; tena palikuwa na mwangaza pande zake zote. 28 Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa Bwana. Nami nilipoona nalianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja anenaye.

 

Katika siku ya Tano ya mwezi wa Nne ambao wengine wanauita mwezi wa Tammuz (sawa na Julai) wa mwaka 594 KK, mwaka wa tano wa wa Yehoyakini kuwa utumwani, katika mwaka wa Kumi na Tatu wa Kalenda Takatifu, nabii Ezekieli alionyeshwa maono kwenye kingo za mto Kebari (Ezekieli 1:1ff.). alikuwa pamoja na watumwa wengine wa kabila la Yuda aliokuwa wameletwa huko kwenye utawala wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli.

 

Alionyshwa maono kwenye mto Kebari na akapelekwa kwenye mto mwingine wenye jina sawa, ambao ulikuwa ni unapeleka maji kwenye mto mkuu wa Frati.

 

Manabii Ezekiel na Danieli walikuwa kwene kipindi kimoja. Hata hivyo, Mungu aliwatumia na alinena na watu kwa kupitia wao kwa nyakati tofauti.

 

Ezekieli alionyeshwa maono ya Makerubi wanne waliokifunika Kiti cha Enzi cha Mungu, na kwa ishara alionyeshwa Mpango wote mzima wa Wokovu na wajibu wa taifa la Israeli (unaowajumuisha wateule Wamataifa) kwenye mpango huo kama kuhani wa ulimwengu.

 

Hata hivyo, ukweli muhimu wa kwanza unaoweza kuhitimika kutokana na maono haya ni ile ya kufikia kwenye miaka ya Yubile na kwenye miaka ya Sabato. Hii inafanya iwezekane kufanya marejesho ya Sabato za mapumziko ya ardhi kwenye nyakati za mwisho, kwa kuwa marejesho ni ya muhimu kwa mafanikio endelevu ya watu wetu. Marejesho ya mfumo wote mzima wa utawala au serikali ya Mungu yanawezekana tu kwa kuzirejesha Yubile. Uhesabuji wa Yubile umefanyika tu kwa maneno haya ya nabii Ezekieli: unatupa sisi tarehe iliyothibita ya kihistoria pamoja na usemi wa ni mwaka gani wa Kalenda Takatifu nah ii ilikuwa, yaani Thirtieth.

 

Mwaka wa tano wa Yehoyakini kuwa utumwani umeanza kwa maana ifuatayo. Tunajua kwamba Yerusalemu ulianguka na Yehoyakini alichukuliwa mateka na kuwa mfungwa katika siku ya pili ya mwezi wa Adari, au siku ya 15/16 Marchi, ya mwaka wa 597 KK (kwa mujibu wa Encyclopedia Judaica). Kwakuwa Adari ni mwezi wa mwisho wa mwaka (na mwaka huu ulikuwa ni ule unaojulikana kawa WeAdar au Adar 2: soma maelezo yaliyo mwishoni mwa jarida hili), mwaka wake wa pili ulianza mwezi mmoja uliofuatia, yaani wa Abibu au ni wa Aprili mwaka 597 KK, mwanzoni mwa Mwaka Mtakatifu. Mwaka wa tano kwa hiyo ulikuwa mwaka wa 594 KK, ambao umeanzisha mwaka wa Kumi na tatu wa Kalenda Takatifu wa mwaka 594 KK. Miaka ya Yubile kwa hiyo uliangukia kwenye miaka ya 574 KK na 524 KK kwenye karne na kadhalika mwaka 1 BK, na kuanza kwa zama tulizonazo sasa iliyotuama kwenye mwaka wa Yubile wa zama hizi ambao ni mwaka 27.

 

Kristo alianza huduma yake kwenye Pasaka ya mwaka wa 28 BK mwishoni mwa mwaka wa Yubile. Alibatizwa siku 50 kabla ya siku hiyo na alifanya muujiza wake wa kwanza wa kugeuza maji kuwa divai kabla ya muda wake haujafika (Yohana 2:4) mwishoni mwa mwaka wa Yubile, siku kadhaa kabla ya maadhimisho ya Pasaka, wakati akiwa bado Galilaya baada ya mfungo wa saumu wa siku 40  (Mathayo 4:2). Hii ilikuwa ni kabla hajashuka kwenda Kapernaumu kwa siku chache kabla ya Pasaka (Yohana 2:12) (soma jarida la Usomaji wa Torati Ulivyofanywa na Kina Ezra na Nehemia (Na. 250)).

 

Mwaka uliofuatia wa Yubile ulikuwa ni wa 77 BK. Tarehe au siku za miaka iliyotangulia Yubile hii zina maana na umuhimu mkubwa sana. Sabato tatu za miaka zilizotangulia kabla ya Yubile ya mwaka wa 77 BK zilikuwa ni za miaka ya 62 BK, 69 BK na 76 BK.

 

Mwaka wa 62 BK ulihitimisha mwisho wa majuma 62 ya unabii wa Danieli 9:25, kukomeshwa kwa utoaji wa zaka kwenye Hekalu la kimwili, na kifo cha mtiwa mafuta wa pili. Tangu kipindi cha miaka ya 62 BK hadi wa 70 BK, Hekalu la kimwili lilivunjwa na kuangamizwa na utaratibu wa kutoa zaka ulihamishiwa kwenye Hekalu la kiroho ambalo ni Kanisa lilipokuwa jangwani (sawa na yasemavyo majarida ya Utoaji wa Zaka (Na. 161); Totari au Sheria ya Mungu (Na. L1) na majarida mengine yanayohusiana na Torati (Nambari 252-263)). Mtiwa mafuta wa kwanza wa mwishoni mwa majuma saba ya kwanza ya miaka alikuwa Nehemia. Mwaka huu ulikuwa ni wa thelathini na mbili wa utawala wa Artashasta II (Arsakes) mwaka wa 372 KK, wakati aliporudi numbani Nehemia (Nehemia 13:10-18) na kulitakasa Hekalu pamoja na Sabato zake.

 

Mtiwa mafuta wa pili alikuwa Yakobo, ndugu yake Yesu Kristo na mzee wa kanisa na askofu wa Yerusalemu, aliyetiwa mafuta ya wakfu mwaka 62 BK. Tangu mwaka 63 BK, juma la mwisho la miaka lilianza kwa mateso ya Nero na kwa kuuawa kwa Mitume Paulo na Petro, na kuanza kwa zama ya dhiki na matatizo yaliyopelekea kuzuka kwa Vita ya Wayahudi. Mwaka wa 69 BK ulikuwa ni mwaka wa Sabato uliotangulia mwisho wa miaka 40 iliyotolewa na unabii wa Yona kwa kulinganisha na huduma ya Kristo. Yuda walipewa kipindi kilicholinganishwa siku moja sawa na mwaka mmoja kwa kulinganishwa na kipindi kilichoruhusiwa na walichopewa watu wa Ninawi kutubu kufuatiwa na mahubiri ya nabii Yona.

 

Kristo aliwatabiria Yuda kwa kipindi cha miaka mitatu (Yona alitabiri kwa muda wa siku tatu) na i kwa muda wa siku tatu) na Yuda waliruhusiwa au walipewa miaka 40 ambayo ilikuwa ni sawa na siku 40 walizopewa watu wa Ninawi. Watu wa Ninawi walitubu lakini Yuda hawakutubu. Kipindi cha mwisho cha miaka saba cha mzunguko wa Yubile tangu kipindi cha huduma ya Kristo kilishuhudia kubomolewa na kuangamizwa kwa Hekalu kulikofanyika mwaka wa 70 BK, kulikohitimisha majuma 70 ya miaka tangu kutolewa kwa Amri au Tangazo la mfalme Dario mwaka wa 421 KK, na kuondolewa  kwa mamlaka ya kiroho kutoka Yerusalemu na kuhamishiwa kwenye Kanisa lene zama au vipindi maalumu saba.

 

Mnamo mwaka wa 73 BK, Masada ulianguka na Yuda wakachukuliwa na kupelekwa utumwani, ili kwamba kwenye mwaka wa Sabato wa mwaka wa 76 BK na Yubile ya mwaka 77 BK mchakato ulikamilika kwa kiasi kwamba mwaka wa mavuno makuu au mengi ya mwaka wa 75 BK hakukwendana au kufanana na kwa hiyo kuliruhusiwa kuiadhimisha Sabato ya miaka kwenye miaka ya 76 BK na 77 BK. Kwa maneno mengine, Mungu alihitimisha na kuruhusu kuangamizwa kwa Yudea kwenye mpangilio wake aliouweka ili waaminifu waendelee bado kuzishika amri na hukumu zake ili awaandae tangu mwaka 74 BK kuiadhimisha miaka ya Sabato na Yubile ambayo ni sehemu muhimu kwa Sabato na ili ziadhimishwe bila kukoma. Yuda walipelekwa utumwani kwa kuwa roho ya kuzishika sheria na Torati ilikuwa imeharibika na kunajisika na utaratibu wa kuzishika Yubile ulikuwa umepotea kwa kiasi kwamba Wayahudi walifikia hata kiasi cha kuuza ardhi katika mwaka wa Saba ambao ni mwaka wa Sabato, ardhi aliyokuwa anaimiliki mtu binafsi kumuuzia hata mtu wa tatu na kuidai amrdhi hiyo mwaka unaofuatia; na kadhalika, walifanya biashara au kukodisha wakati wa Sikukuu, nk. matendo haya yalimchukiza sana Mungu na yalimkasirisha.

 

Ushikaji wa Sabato hautakiwi na ni mgumu kwa mtazamo wa ustawi au maendeleo endelevu ya kitaifa. Hukumu iliyowekwa kwa kuyavunja maagizo ya Torati na ya kuvunja amri ya Sabato za mapumziko ya ardhi na Yubile ni taifa zima kwenda utumwani captivity (Lev. 26:33-35).

 

Kutokana na 2Nyakati 36:20-21, tunajua lengo la unabii uliotolewa na nabii Yeremia, wakati Yuda walipochukuliwa kwenda utumwani na mji wa Yerusalemu na nchi ya Yudea kuangamizwa na kusalia kuwa maganjo kwa muda wa miaka 70, ili nchi istarehe au izifurahie Sabato zake – kwa kuwa Yuda hawakuzishika Sabato na Torati kikamilifu kwa kipindi cha majuma 70 ya miaka iliyotangulia nyuma yake: yaani tangu kujengwa kwa Hekalu la Sulemani, ambacho ndicho kilikuwa kipindi cha historia ya Israeli kilichoonyeshwa kimfano na Kerubi wa pili aliyeonekana kwenye maono ya Ezekieli. Yapasa ikumbukwe pia kwamba taifa lililotumiwa kuiangamiza Yuda na lenyewe liliangamizwa baada ya muda na Yuda ilifanywa upya.

 

Hata hivyo, kipindi kilichofuatia, yaani cha baada ya kuangamizwa kwa Hekalu, cha majuma 70 ya miaka ba baada ya sheria za Torati kufundishwa na kurejeshwa tena na Nehemia, Kerubi wa tatu wa maono ya Ezekieli aliendelea kwa kipindi kirefu na, baada ya Yuda kuiacha na kuinajisi Torati na kumkataa Kristo, taifa lilipelekwa utumwani; na halikuweza kurejea tena hadi siku zilizofuatia baadae za mwisho. Matunda waliyostahili wao walipewa watu wengine, yaani, Kerubi wa nne au kipindi cha Makanisa saba ambacho kwa mujibu wa Mhubiri 6:6 kinaonekana kuwa kilianza kuishia miaka 2,000, na wakatawanywa na kuteswa. Kanisa hili lililindwa kwa hali hii ya kutawanyishwa (Ufunuo 12:15-16).

 

Ufunuo 12:15-16  Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. 16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.

 

Kwa maneno mengine, kulikuwa na usalama kwenye nchi walizotawanyikia tu na walikokimbilia. Kipindi hiki cha kukimbia huku na huko kitaendelea hadi pale kama Kristo alivyosema:

Mathayo 10:23 Lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.

 

Mazingira yanaandaliwa kwa uwezekano wa kuwepo kwa mateso mengine kwa maandalizi na ukomesho au mateso ya kidini. Israeli hatahivyo, watashughulikiwa pia kama taifa.

 

Sabato hizi za mapumziko ya ardhi bado zinatakiwa kuadhimishwa kwenye taifa. Baada ya marejesho ya taifa la Israeli tangu miaka ya 1800, kama umoja wa Jumuia ya Madola na taifa la Marekani, miaka hii ilifanyika kuwa na mlundikano wa madeni au yenye madeni makubwa, kwakuwa kilikuwa ni kipindi cha kuanzishwa tena kwa taifa la Yuda katika Israel tangu kwenye mwaka wa Sabato wa 1948. Kipindi cha kuwekwa tena kwa agano kilikuwa ni cha miaka 200 cha takriban vipindi vinne vya Yubile za miaka ya 1777/8 hadi Yubile ya mwaka 1977/8, na kuendelea hadi mwaka 2027/8. Yubile ya mwisho ilikuwa ni ya mwaka 1977, na mwaka 1976 ulikuwa ni mwaka uliotangulia wa Sabato. Miaka ya 1975 na 1978 ilikumbukwa au kuchukuliwa kuwa ni miaka bora sana, mwaka wa 1978 kwa kweli ulikuwa ni mwaka wa miaka 100 ya mafuriko. Sabato iliyofuatia ya mwaka 1984 ilitanguliwa na mwaka mzuri sana, na ulifuatiwa na mwaka mzuri sana mwingine. Haijalishi chochote kwamba Mwaka Mtakatifu kuanzia mwishoni mwa Marchi 1983 ulioishia kwa ukame uliodumu kwa muda mrefu kwa miaka kadhaa nchini Australia. Rainfall anamnukuu mwandishi aliyeamini bila mashaka kwamba Sabato na miaka ya mavuno mengi ni ukweli uliopo.

 

Kushindwa kuyatii maagizo ya Torati na, hasahasa, Sabato za juma na za miaka na Yubile, ndivyo viliwapelekea Yuda (na Israeli) kulaumiwa na kuingia hukumuni. Ishara ya Yona walipewa Yuda kwa mlinganisho wa siku moja kuwa sawa na mwaka mmoja, sawa na kipindi alichokitabiri Ninawi. Kwa kuwa siku 40 wazolipewa Waninawi, Yuda walipena miaka 40, lakini, kama Yuda walivyopewa miaka 40, ulimwengu ulipewa Yubile 40 za kutubu na za kuanzishwa kwa mfumo wa Sabato. Hii haijafanyika bado na kwahiyo, kwenye Yubile ya 40, mfumo ulioko sasa ulimwenguni utaangushwa na kutokomezwa kabisa.

 

Ingekuwa ni dhahiri sana kulima kwa kujiendeleza kiuchumi kwamba gharama au faida ya kulima katika miaka ya Yubile nay a Sabato kwenye mazingira ya ardhi yenye ukame huotesha kiasi fulani cha mazao majira ya kutolimwa ya Simwa ya miaka ya Sabato yanapunguza hali ya shamba kutokuwa na rutuba, na inafanya marudisho au marejesho stahiki kuongezeka sana. Urutubisho wa ardhi unahitaji unahitaji mbolea nyingi na yenye gharama, sio tu kwa mwaka ule tu, bali pia kwa miaka mingine sita inayofuatia. Mazao yanaondoa vimeng’enyo ambavyo mbolea haiwezi kuvirudishia, ikipunguza uzalishaji wa muda mrefu na kiwango endelevu cha uzalishaji wa mazao. Mmomonko wa udongo na gharama nyinginezo vinaongeza uzito wa kigharama wa kuendesha shughuli za kilimo na sekta za umma, na kadhalika. Faida ya muda mfupi ina hasara ya muda mrefu, ambazo taifa na wataalamu wanaikolojia hawawezi kuimudu kuigharamia. Sabato hizi za Bwana yapasa zishikwe au kutunzwa na mataifa yote. Watu wa Mungu wanapaswa kuwa mfano. Adhabu iliyowapata kwa kutofanya hivyo ilikuwa ni kuchukuliwa utumwani.

 

Australia inapoteza uwezo wake wa kiuzalishaji wa chakula chake yenewe. Asilimia 70 ya mahitaji yake ya chakula inalimwa na kuingizwa kutoka nje na kiwango hiki kinazidi kuongezeka. Chakula kinachozalishwa hapa kinasafirishwa pia nchi za ng’ambo bila ya kuwa na fasafirishwa pia nchi za ng’ambo bila ya kuwa na faida ya moja kwa moja kwa taifa hilo. Utaratibu huu ni mbaya na yapasa ukomeshwe. Sisi tu mfano na yatupasa kutoa maelekezo kwa jambo hili.

 

Ardhi imeendelea kushuka thamani tena na tena. Siku za zamani mtu aliweza kumpanda farasi wake na kumwendesha pembeni mwa pwani ya Afrika Kaskazini na asiweze kuiona vizuri nuru ya jua kwa sababu ya uwezo wake wa kusafiri ingawa kuna misitu mikubwa endelevu huko.

 

Katika Siku hizi za Mwisho, utumwa utakuwa ni wa kipindi cha millennia, chini ya utawala wa Yesu Kristo. Masihi “atawachukua wafungwa utumwani” ili kurejesha na kufanya upya mfumo ulioharibiwa kwa kukusudiwa na taratibutaratibu kwa zaidi ya miaka 6,000. Hadi ufikapo mwaka wa 2027 dunia yote itakuwa imefanywa upya kwa kanda zake za kitaifa. Mpangilio huu mpya yapasa uchukue mkondo wake baada ya mavuno ya kabla ya miaka ya Sabato na Yubile yatakayohitajika kwa umuhimu mkubwa kwa mwaka 2025 (kama lisemavyo jarida la Torati ya Mungu (Na. L1) na majarida meingine ya mlolongo wa Sheria au Torati (Na. 252-263)).

 

Maana ya aina ya Makerubi

Ili kuelewa mlolongo wa matukio kwenye Yubile hii ya mwisho, ni muhimu kwanza kuelezea maana ya Makerubi wanne au Makerubi wa nabii Ezekieli. Maono ya Ezekieli yalitokea upande wa kaskazini na mwonekano au maelekezo yake ni ya muhimu ili kulinganisha na mwonekano wake. Hekalu la Mungu lilikuwa upande wa kaskazini (Zaburi 48:2 KJV).

Zaburi 48:2 Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu.

 

Kimapokeo, pande za kaskazini ulikuwa ni mwelekeo wa kilipokuwa Kiti cha Enzi cha Mungu (Isaya 14:13).

Isaya 14:13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.

 

Lusifa alichagua kujiinua na kuwa kama Yeye Aliye Juu Sana.

 

Mawingu haya na moto vilifanana  na vile vya kwenye kitabu cha Kutoka ambapo Roho wa Bwana alipowaongoza na kuwawezesha Israeli wawe ni watu wa tofauti na watu wengine na kuwafanya wawe watu watakatifu. Moto ulikuwa wa rangi ya rangi kaharabu au shaba, iliyotokana na mwili wa Roho Mtakatifu. Moto unaojisokota wenyewe uliashiria kuimarika na kumaanisha kwa Roho kwenye maagano yake na utaratibu wake. Kujisokota huku kulionesha maana ya Sheria au Torati ya Mungu ambayo kwayo Makerubi waliruhusiwa, hata kwa Roho mwenyewe alitokea au kuruhusiwa na kufichwa kwa kuwa Torati ilitokea kwenye asili na tabia hii hii ya Mungu ambayo tunairithi (2Petro 1:4).

 

Kitendo cha kujisokota kwa moto kinamaanisha pia mlolongo wa wakati wa Makerubi wanne waliojifunika mbawa zao ili waweze kuonyesha uwepo wao kwa pamoja. Kiti kilichokuwa juu ya Makerubi kilimaanisha Kiti cha Enzi cha Mungu ambacho ndicho kutoka hapo ndipo hakimu wao, Elohimu na Eli anatawala. Anafunikwa juu ya Makerubi ili kuwalinda, na kama kitovu cha Maskani. Kiti hiki cha Enzi pia ni “kiti cha rehema” na kiliwekwa ndani ya Maskani yenyewe ya kidunia, ili kuonyesha uumbaji wote wa kiroho wa Hekalu la milele la Kiroho. Yahova anamwambia Yahova wa Majeshi kwa mfumo na muundo huu. Wamesimama kwenye lango la upande wa mashariki na utukufu wa Mungu ukashuka juu yao (Ezekieli 10:18-19).

Ezekieli 10:18-19 Kisha huo utukufu wa Bwana ukatoka pale juu ya kizingiti cha nyumba, ukasimama juu ya makerubi. 19 Nao makerubi wakainua mabawa yao, wakapaa juu kutoka katika dunia machoni pangu, hapo walipotoka nje, nayo magurudumu yakawa kando yao; wakasimama mahali pa kuingilia pa mlango wa upande wa mashariki wa nyumba ya Bwana; na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.

 

Kwenye Hesabu sura ya 9 tunaona kwamba ushikaji wa Pasaka ni jambo linaloonyesha tofauti iliyopo kati ya watu watakatifu wa Mungu na wageni wamataifa mengine katikati yao. Kwenye Kutoka 13:6-9, tunakuta kwamba, Pasaka (na Idi ya Mikate Isiyotiwa Chachu) kuwa ni mhuri wa Mungu kama ishara kwenye mikono yetu na ni kama ukumbusho au ishara katikati ya macho yetu (yaani kwene vipaji vya nyuso zetu). Hii ni alama au mhuri wa Bwana, inayowatenganisha watakatifu wake "ili kwamba sheria ya Bwana ipate kuwa kinywani mwako" (Kutoka 13:9). Kwa maneno mengine ni kwamba, mhuri wa Mungu kuwa mioyoni mwetu na kwenye nia zetu kunafanyika kwa alama au ishara au kwenye paji la uso katikati ya macho, na alama ya mikononi mwetu inaonyesha na kumaanisha kwamba matendo yetu yanaendana sawa na maneno yetu. Ushikaji wa Pasaka na Mikate isiyo na Chachu, pamoja na Sabato za kila juma, ni alama maalumu ya mkutano wa kusanyiko la Bwana. Ushikaji wa Sabato nyingine zilizoorodheshwa kwenye Mambo ya Walawi 23 kunafuatia kwenewe tu kutokana na alama ya Pasaka. Upatanisho wenyewe inafanyika kuwa ishara na alama ya watu wa Bwana (sawa na lisemavyo jarida la Kazi ya Amri ya Nne Kwene Historia ya Makanisa ya Mungu ya Washika Sabato (Na. 170)).

 

Dhana ya Alama ya Mnyama imetokana pia kutokana na dhana hii kwa sheria yake na sikukuu zake. Hizi zilikuwepo kutoka kipindi cha tukio la Kutoka kama zilivyokuwa zipo ibada za Easter na Jumapili, na sikukuu za tarehe 25 Desemba zilizotokana na sikukuu hizi za kishetani na za alama ya mnyama (sawa na yasemavyo majarida ya Chanzo cha Krismas na Easter (Na. 235); Kalenda ya Mungu (Na. 156); Hoja za Wakuartodesiman (Na. 277); na la Alama ya Mnyama (Na. 25)).

 

Nguzo ya wingu na moto ililifunika Jeshi la Watakatifu, kwa kara ya kwanza kabisa kwenye Kutoka 14:19, na kwenye Hesabu 9:15 tunaona kwamba wingu liliifunika Maskani katika siku ambayo ilisimamishwa. Maskani ya Bwana ilifunikwa wakati wote kama wingu majira ya mchana na kwa moto usiku, kama ishara inayoonyesha kwamba Roho wa Mungu alikuwa kwenye Hema ya Ushuhuda na kwamba alikuwa pamoja na Jeshi la watakatifu wake Mungu kwa kuwa walikuwa wamechaguliwa kuwa ni makuhani. Wakati huu moto na wingu viliponyanyuka juu kisha ndipo Maskani iliinuliwa pia na kuondolewa (Hesabu 9:21-23).

 

Viumbe waliohai wanawakilisha mfano wa awamu nne ya historia ya makuhani wa Israeli. Awamu ya kwanza ilikuwa ni ya Maskani ya jangwani na ya Waamuzi. Awamu ya pili au ya Kerubi wa pili ilikuwa ni ya Hekalu la kwanza kuanzia Sulemani hadi kipindi cha utumwa. Awamu ya tatu ilikuwa ni ya tangu kuanzishwa tena ya baada ya kurudi utumwani hadi kipindi cha kuangamizwa au kubomolewa kwa hekalu mwaka 70 BK, na awamu ya nne ilikuwa ni kama zama ya kurudi kwa Masihi (sawa na yasemavyo majarida ya Sanduku la Agano (Na. 196); na Pentekoste ya Sinai (Na. 115)).

 

Kila awamu iko kama Kerubi wa Agano aliyekilinda Kiti cha Enzi cha Mungu, mikono ya mwanadamu (chini ya mbawa) akitimiliza makusudio yake hapa Duniani. Viumbe Waliohai wamekuwa wakielezewa au kutajwa sehemu nginginezo kwenye Biblia, ila alama wanazoziwakilisha za muonekano wao zina maana ya kiundani sana zaidi ya zile za upekee wa kimaumbile wenye sura nne tofauti. Kwenye Ufunuo 4:6-8 tunaziona sura zilezile, ila zilizo mbali na Viumbe hawa Waliohai pamoja na mmoja mwenye sura nyingi lakini mwene mabawa sita.

Ufunuo 4:6-8 Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma. 7 Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye. 8 Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.

 

Maana ya sura hizi nne yanaweza kuwa yanatokana na uwepo wake na viwango vya kivita vya Israelli kutoka muundo au utaratibu wake wa kwanza asilia wa kupanga marago. ‘Amri ya mutembea’ ya Waisraeli ilianza kwanza tangia siku ya 20 ya mwezi wa Pili wa Zivu, wa mwaka wa pili baada ya tukio la Kutoka, na imechukuliwa kutokana na ilivyotolewa kwenye Hesabu 10 na vipengele vikundi vingine vilifuatia.

 

Jeshi la ziada liliundwa na makabila ya Yuda, Isakari na Zabuloni, waliotembea kwa viwango vya kivita vya watu wa Yuda, ambaye alipewa jina la mbaraka la samba. Maskani ikiwa imelindwa kikamilifu, ilifuatiwa na askari hodari wenye weledi wa kimafunzo. Kundi la tatu liliundwa na kabila la Reuben na makabila mengine yaliyosaidia ya Simeon na Gadi yaliyotembea kwa viwango vya kivita vya kabila la Reuben ambao walikuwa ni wanaume.

 

Kundi la nne na kikosi cha mwisho cha watu wengi kilifuatiwa na Ubunifu au Kazi Takatifu ya kupangilia Maskani. Mara zote Maskani ilisimamishwa kabla hawajafika kwenye marago au kambi jipya. Kundi hili la nne liliundwa na kabila la Efraimu pamoja na nusu ya makabila ya Manase na Benyamini. Hawa waliondoka na kutembea kwa mintaarafu ya Efraimu, ambaye jina lake la mbaraka lilikuwa ng’ombe dume, bali ilikuwa hatimaye pia pengine alikuwa ni taswira ya nguvu za umoja wao wa kama mnyama.

 

Kundi dogo liliundwa na watu wa kabila la Dani wakifuatiwa na kabila la Asheri na kisha kabila la Naftali. Makabila haya walitembea nyuma ya viwango vya kivita vya Dani, ambaye jina lake la mbaraka aliitwa tai (ingawaje joka lenye sumu kali litambaalo ni taswira pia ya kabila hili – walikuwa ni ‘wauma mkiani’). Sehemu ya Sanduku la Agano iliwatangulia watu wa Mungu kama eneo la uwekaji hakika ya safari yao.

 

Wakati Keshi la watu wa Mungu lilipofanya kambi kwa kuizunguka Maskani na makabila yalipanga marago nje yao, sawasawa na makundi yao. Kutokana na Hesabu 2 kunafikia kunaona kuwa walijipanga hivi: upande wa mashariki yalikuwapo makabila ya Yuda, wakifuatiwa na Isakari na Zabuloni, upande wa kusini walikuwepo kabila za Reuben, wakifuatiwa na kabila la Simeoni likifuatiwa na kabila la Gadi, upande wa magharibi kulikuwa na makabila ya Efraimu, wakifuatiwa na Manase na Benyamini; upande ma kaskazini kulikuwa na makabila ya Dani na Asheri na Naftali i.

 

Mpangilio huu wa kuweka marago haukubadilika kabisa, na ni kwa sababu hii ndipo Ezekieli aliona maono yakitokea upande wa kaskazini yenye sura ya mwanadamu upande wa mbele (Ezekieli 1:10), yaani kabila la Reuben upande wa kusini. Sura ya samba upande wa kuume lilikuwa kabila la Yuda upande wa mashariki. Sura ya ng’ombe dume maksai upande wa kushoto walikuwa Efraimu upande wa magharibi, na sura ya tai nyuma yake walikuwa ni Dani upande wa kaskazini wakitazama mbele kwenye mwelekeo waliotoke.

 

Mpangilio wa kimakazi ya taifa kuizunguka Maskani haukubadilika, na kwa sababu hii Ezekieli alisema kwamba kila mmoja wao alikwenda moja kwa moja akitazama mbele bila kugeuka. "Nao walikwenda kuelekea mbele, kila mmoja wao; roho ilikotaka kwenda ndiko walikokwenda; hawakugeuka walipokwenda" (Ezekieli 1:12).

 

Mpangilio huu wa kimakazi pia unaonyesha taswira ya utaratibu wa kiibada wa kukizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu, ulioonekana kwene Ufunuo 4:1 hadi 5:14. Kuna Wazee ishirini na nne au manabii waliogawanywa kwenye makundi kumi na mawili, wanaowakilisha makabila yaliyo na migawanyo mikuu minne.

 

Katikati ya Kundi hili la watu wa Mungu kulikuwa na Maskani na Roho wa Mungu "kama makaa yawakayo kama mienge imulikavyo huku na kule katikati ya viumbe wenye uhai". Makaa haya yanayoungua ni utakaso wa Watakatifu kwa namna ambayo ndivyo alivyotakaswa nabii Isaya kwa makaa ya moto, nah ii ilikuwa pia ni taswira ya sadaka Roho aliyekuja baadae siku ya Pentekoste.

 

Kila mmoja wao alikuwa na mabawa manne na mawili kati ya mabawa haya yaliguusana kila kerubi moja kwa mwenzake, wakifanya kazi ya kujikinga kwa mzunguko wa upangaji marago na wakiashiria umoja na ulinzi wa kimwili wa taifa na wa Maskani. Mabawa mawili yanayofunika miili yanafanya taswira ya ulinzi wa kiroho wa kila mtu aliyetakaswa na kukamilika kama mtumishi wa Mungu.

 

Makerubi wanne wanaonekana kuwa na magurudumu yakitembea juu ya Dunia, kila moja wapo, na jinsi yalivyotenyenezwa na yanavyoonekana kuwa kama yalikuwa gurudumu ndani ya gurudumu linguine. Mbavu zake na spoko zake na macho ya magurudumu ni matendo ya watu watakatifu yaliyo muhimu na kuhitajika kwenye Mpango wa Wokovu, unaoendelea mbele kwa kila gurudumu moja likaribialo kwenye kwenye uwepo wa Bwana. Spoko zinawakilisha umoja wa watu wa Mungu. Yapasa ikumbukwe kwamba Makanisa Saba, yaliyowakilishwa na Kerubi wa nne, ndiyo kwa kweli matofali yanayojenga jingo la kiroho ambalo ni Hekalu la Mungu. Na ni kwa sababu hii ndipo Ezekieli anasema mara mbili kwamba Roho ya wale Viumbe Hai ipo kwenye yale magurudumu. Roho Mtakatifu ndiye alikuwa kifaa ambacho Wateule walihitimisha usemi huu.

 

Ukombozi wa kiroho wa Wateule ulionyeshwa kwa mfano wa mikate ya siku ya Pentekoste. Baada ya Pasaka kuifanya dhambi isamehewe au kuondolewa na Sikukuu ya Mikate Isiyo na Chachu ikiwa imetumika kama alama ya msamaha wa dhambi na utakaso (kama mwili uliozingwa na mabawa ya Makerubi), ndipo chachu mpya iliwekwa kwenye mikate miwili ya maadhimisho ya Pentekoste, ikiashiria chachu mpya ya chachu ya kweli na haki – ya Roho Mtakatifu. Mikate miwili inaashiria kimfano uwokovu wa undumila kuwili na kutangatanga wa Waisraeli na Yuda, yaani kati ya Waisraeli na Wamataifa, chini ya Masihi wa Haruni na wa Israeli.

 

Wokovu huu alionyeshwa nabii Zekaria kwa taswira ya mizeituni miwili iliyosimama upande wa kuume na wakushoto wa kinara cha taa (wa zama saba za Makerubi wa mwisho) – Masihi wa Haruni mwanzoni na Masihi wa Israeli mwishoni akimwaga uwepo wa Roho wa Mungu wa Milele Duniani kwa kupitia mifereji miwili ya dhahabu. Maana za aina mbili za ishara hizi zinarudiwa pia na manabii wanaowafuatia.

 

Makerubi wanne au awamu za watakatifu wake Mungu zina michongoko ishirini na nne iliyoonyeshwa kwa mfano wa Wazee Ishirini na nne wa kwenye Ufunuo 4:9. Hawa wazee ishirini na wanne ni ishara au mfano wa makundi ishirini na manne ya makuhani watumikao waliotajwa kwenye 1Mambo ya Nyakati 24:1-6, na kwenye mpangilio au utaratibu ulioelezewa kwenye aya za 7-18.

 

Mwelekeo au mahali au utaratibu wa makuhani vinaendana na msingi wa watu wawili kwa kila kabila moja. Pia kuna elohim wawili wanaopangwa kwenye kila kabila au kundi. Tuaweza kukadiria kwamba hii inataswirishwa pia na idadi ya Waamuzi na Mitume kwa msingi wa kila mmoja sawa na kabila moja, wakawa kumi na mbili kwenye kila mpangilio.

 

Kwa kuongezea kuhusu migawanyo hii ishirini na nne ya Hekalu, yaani, ya Kerubi wa pili au wa tatu, kulikuwepo pia na Waamuzi ishirini na nne, Waamuzi kumi na mbili wakitumika kwenye Maskani ya kwanza au Kerubi kama ilivyokuwa kipindi cha Waamuzi na Mitume kumi na mbili watakaofanywa kuwa wahukumu kwenye kipindi cha marejesho cha Milenia, ambao wanafanya taswira ya Wazee wa migawanyo ishirini na nne wanaozitupa taji zao mbele za Bwana wa Majeshi, kwa kuwa kipindi cha utumishi wao kitamjumuisha Bwana. Wakati huu, Makerubi wanne, au Viumbe wenye mabawa sita, watapewa mabawa mengine mawili yasiyoharibika wala kufa ya kiroho, watakayopewa na Bwana wa Majeshi. Kiwango au daraja hili la kimaumbile linafanana na lile lya Maserafi au malaika wa daraja la juu zaidi. Kwa hiyo, wateule watafanyika kuwa na daraja la elohim au theoi watakaloruzukiwa.

 

Zekaria 12:8 Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.

 

Kwa hiyo, mnenyekevu na mnyonge atakuwa kama Daudi na nyumba ya Daudi itakuwa Elohimu kama Malaika wa Yahova mbele yao. Andiko hili linaanzisha mlolongo wa kiawamu. Malaika wa Yahova alikuwa ndiye Elohimu wa Israeli, aliyeandikwa kwenye Zaburi 45:6-7. Elohimu huyu ni Kristo, kama isemavyo Waebrania 1:8-9. Nyumba ya Daudi au wateule watafanyika kuwa elohimu kama alivyokuwa Kristo mwenyewe. Watawatia nguvu waliodhaifu wakati wa marejesho ya Masihi katika siku za mwisho (soma majarida ya Wateule Kama Elohimu (Na. 1); Malaika wa YHVH (Na. 24); na Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa Kwake Rasmi (Na. 243)).

 

Kipindi cha mwisho cha Watakatifu kinaoenekana Viumbe hawa wenye Uhai wakikizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu, lakini utaratibu wa Wateule kwenye kipindi hiki cha tano imebadilika. Upangiliaji wa jinzi ya kujipanga makabila inahusiana na jinsi ya uondokaji wa makabila ya Yuda, Reuben, Efraimu na Dani kulitegemea haki yao. Ukaaji wa makabila na mpangilio wake kwenye Ezekieli 48:31ff. Kwenye malango yanatofautiana pia mwelekeo wa malango yote mawili kwa malango na nchi au ardhi (Ezekieli 48:1-29).

 

Mgawanyo wa makabila kwa makundi ya idadi sawa ya watu 144,000 kumewekwa pia kwenye dhana hii. Dani walijitenga na kabila la Efraimu kama kabila la Yusufu, na Manase likafanyika kuwa kabila lenye haki yake lenyewe kwenye mgawanyo huu, kama linavyoonekana kabila la Lawi. Mgawanyo huu ulifanyika kwa lengo la kuwajumuisha makuhani wapya na utaratibu wake mpya (Ufunuo 7:4-8) (pia soma jarida la Mji wa Mungu (Na. 180)).

Ufunuo 7:4-8 Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu. 5 Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu. 6 Wa kabila ya Asheri kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Naftali kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Manase kumi na mbili elfu. 7 Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu. 8 Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Yusufu kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Benyamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri.

 

Kwenye mpangilo huu kabila la Dani linaunganishwa na Efraimu kama kabila moja na Yusufu ili kwamba kabila la Lawi lichukue nafasi yake ya ukuhani wa Melkizedeki katika Nyakati za Mwisho – lakini Dani ataendelea kuchukua haki yake ya uzaliwa wa kwanza kwa jinsi ya kimwili kama Mwamuzi atakaye wahukumu Israeli.

 

Kerubi ni kiumbe mmoja na Masihi kwenye awamu ya mwisho pia. Dhana hii ya utawala wa millennia inachambuliwa kwa kina mahali pengine.

 

Kumbuka:

Maamuzi ya kutangaza kuonekana kwa mwezi wa Adari na (We)Adar mwaka wa 597 KK kulifanywa kwa mwonekano wa mwezi mwandamo. Kitabu cha Uchambuzi wa Neno na Maana zake cha The Encyclopaedia Judaica kinaonesha kipindi maalumu kilichofanyika tukio la watu kwenda utumwani na kinaonysha kuwa tukio hili lilitukia kwenye 2 Adari ambayo ni sawa na tarehe15/16 Marchi ya mwaka wa 597 KK. Makala ya ‘Ezekieli’ kwenye Toleo la 6 ukurasa wa 1082, bango kitita ya 1 inasema hivi:

Uhesabuji wa mwaka kwenye tarehe zinazoanzia tangu tukio la chukuchukuliwa utumwa ni kwa Mfalme Yehoyakini (1:2; 33:21; 40:1), kunajadiliwa sana na matukio ya kihistoaria ya Wababeloni kwamba kama ilikuwa ni 2 Adari (matikati ya mwezi Marchi) mwaka wa 597. Hata hivyo, II Nyakati 36:10 inaonesha kuwa tukio hili la utumwa ulianza kipindi cha “mwishoni kabisa mwa mwaka”  -- yaani mwezi uliofuatia, wa Abibu au Nisan, mwanzoni mwa mwaka wa 8 wa utawala wa Nebukadneza (II Wafalme 24:12). Zama za utumwa ndipo ilianza katika mwezi wa Abibu au Nisan (Aprili) mwaka 597, na mwaka wake ni kama mwaka wa mkubwa kwa Wababelonia, ulioanza tangu mwezi wa Abibu au Nisan hadi Adari.

 

Hii sio sahihi. Wayahudi wanaweka rejea kwenye Adari 1 kama ni Adari na Adari 2 kama na Adari au WeAdari. Andiko hili halitumii maneno ya Adari 1 na 2; linasema tu kuwa ni Adari na Adari.

 

Mahali panapoonyesha kuwa ni mwishoni mwa mwaka ni kwenye 2Nyakati 36:10 panapoonyesha kuwa siku ya ikwinoksi ilikuwa mwezi March. Haitaji kuwa ni mwezi wa Abibu au Nisan. Biblia inataja kuwa ni mwishoni mwa mwaka kwenye maadhimisho ya Vibanda pia ikimaanisha kuwa ni kipindi cha ikwinoksi ya mwezi Septemba. Ikwinoksi ya majira ya joto huwa iaangukia kwenye mwezi huu wa WeAdari mara saba kila baada ya mwaka wa saba wa mzunguko wa miaka. Kitabu cha Matukio ya Wababeloni na 2Nyakati vinaelezea kwa kina kuhusu tukio hili la utumwa.

 

Anavyotaja nabii Ezekieli kuwa ni mwaka wa Kumi na Tatu. Utajaji kama huu sio wa mwaka wowote wa kumi na tatu wa mfalme yeyote anayejulikana au mfumo wowote. Usemi rahisi umechukuliwa mana inayoeleweka kwenye maandiko ya Agano la Kale.

 

Pia kuna matengenezo mengine yanayofundishwa na Whiston, ambayo sio sahihi, yanayotuama kwenye mfumo mpotofu wa miaka ya nyuma. Mkanganyo mwingine unajitokeza kutokana nah ii wakati mwingine.

 

Kipimo cha kuamua Mwezi Mpya matika mwaka wa 597 inatuonyesha kuwa kulikuwa na kutilia maanani utaratibu huu wa WeAdar kwenye mwaka ule.

 

Mwezi Mpya uliangukia tarehe 12 Marchi saa 9:00 alasiri kwa majira ya Yerusalemu ya LMT. Mwezi Mpya uliofuatia uliangukia tarehe 11 Aprili saa 1:.33 asubuhi. Siku ya ikwinoksi iliangukia tarehe 27 Marchi saa 7:33 mchana kwa majira ya Yerusalemu ya LMT.

 

Ni zaidi ya siku 14 kamili tangu tarehe 12 Marchi 597 hadi tarehe 27 Marchi 597 alasiri hadi alasiri nyingine ambapo tuna siku kumi na sita. Kwa hiyo, Marchi hauwezi kuwa Mwezi Mpya ulio karibu sana na siku ya ikwinoksi, na tarehe 11 Aprili saa 1:33 asubuhi iwe ni siku ya Mwezi Mpya wa Nisan. Kwa hiyo ni lazima tuwe na WeAdar na siku ya 2 ya WeAdar ni tarehe 14/15 Marchi, hata kwa kudhania kwamba tarehe 13 Marchi kuwa huenda ni mwanzo wa mwezi na sio tarehe 15/16 Marchi kama Judaica inavyoshikilia kuamini.

 

Tukio la watu hawa kwenda utumwani lilitokea mwishoni mwa mwaka, yaani kwenye kipindi cha ikwinoksi, ambayo ilikuwa katika mwezi wa WeAdari na katika siku ya 2 WeAdari au tarehe 14/15 Marchi au tarehe 15/16 Marchi kwa hesabu na kumbukumbu za Wayahudi.

 

Kwa hiyo mwaka ulihesabiwa tangu mwanzo wa mwaka uliopita mnamo Aprili 598 KK.

 

Aprili ya mwaka 597 KK ni mwanzo wa mwaka wa pili; mwaka 596 KK ni mwanzo wa mwka wa tatu; mwaka wa; 595 KK ni mwanzo wa mwaka wa nne; na mwaka 594 KK ni mwanzo wa mwaka wa tano wa Yehoyakini kuwa utumwani (sawa na yasemavyo majarida ya Jinsi Usomaji wa Torati Ulivyofanywa na Kina Ezra na Nehemia (Na. 250); na Kuanguka kwa Yerusalemu na Wababeloni (Na. 250B)).

q

 


 


NYONGEZA A:

 

 

Page I = Ukrasa wa I

Jinsi ya Kuipangilia Miaka ya Yubile kwa Kutumia Nyakati Zilizo Kwenye Ezekieli 1:1

Onyo: Jedwali hili litumie kama kitu cha kusaidia tu

 

LEGEND

A ...........=.....Abibu au mwezi wa 1 wa kalenda ya Mungu

40, 50,7 = ...Miaka ya Sabato au ya Yubile

N 1 = ..........Mwaka wa kwanza wa utawala wa Nebukadneza

N2 = ...........Mwaka wa pili wa utawala wa Nebkadneza

N3 = ...........nk.

J1 = ...........Mwaka wa kwanza wa utawala wa Yehoyakini

J2 = ...........Mwaka wa pili wa utawala wa Yehoyakini

J3 = ...........nk.

 

KUMBUKA:

Ikwinoks ya majira ya baridi ilitukia yapata mwezi Marchi Tarehe za 17/18 za siku za nabii Ezekieli, mara nyingi ni nyakati zilizo Mwezi wa kwanza wa kalenda ya Mungu [Abibu] Huwa karibu na mwezi Aprili.

 

**************************

 

 

 

Page II = Ukurasa wa II

 

Page III = Ukurasa wa III

 

Na Yekonia, mfalme wa Yuda, akatoka akamwendea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake, na watumishi wake, na wakuu wa watu wake, na maakida wake; mfalme wa Babeli akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake. 2Wafalme 24:12

 

Start of Nebuchadnezzar’s Reign = Kuanza kwa Utawala wa Nebukadneza

September 605 BCE = Septemba 605 KK

 

9. Ni kwa miaka ishirini na moja, Nebukadneza alikuwa mfalme wa Babeli

 

10. ilipofika siku ya 8 ya mwezi wa Abu [15 Agust 605] alikwenda alikokusudia; katika mwezi wa Ulolu Nebkadneza alirudi Babeli.

 

11. na siku ya 1 ya mwezi wa Ulolu [tarehe 17 Septemba] alisimika kiti cha enzi cha ufalme huko Babeli.

Tazama kwenye wavuti, makala ya ‘Nebukadneza II’ chini ya ‘rejea’ chini ya kiunganishi cha KK.

 

 

 

 

 

 

Page IV = Ukurasa wa IV

 

Mwaka ulipokwisha, Nebukadreza akatuma wajumbe, akamchukua mpaka Babeli; pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya Bwana; akamtawaza Sedekia nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu. [Nyakati 36:10]

 

Note: Return of the year...Kumbuka:

 

Utumwa wa Yehoyakin. Mwezi Marchi mwaka 597 KK.

 

Utumwa wa Yehoyakin. Mwezi Marchi mwaka 597 KK.

 

* kwa hiyo tukio la utumwa lilitokea mwishoni mwa mwaka, yaani wakati wa ikwinoks ambayo ilikuwa kwenye WeAdari au siku ya 2 ya WeAdai au tarehe 14/15 Marchi au tarehe 15/16 Marchi kwa kumbukumbu za Wayahudi.

 

 

 

 

 

 

 

Page V = Ukurasa wa V.

 

1. Ikawa katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa pamoja na watu waliohamishwa, karibu na mto Kebari, mbingu zilifunuka, nikaona maono ya Mungu. [EZEKIELI 1:1]

 

Nukuu muhimu zilizochukuliwa kutoka kwenye jarida Na. 108 “Maono ya Nabii Ezekieli”

 

Kwa kuwa Adari ni mwezi wa mwisho wa mwaka (na mwaka huu ulikuwa ni wa WeAdari au wa Adari 2; tazama notisi mwishoni mwa jarida), mwaka wake wa pili ulianzia mwezi mmoja baadae kwenye Nisan au Aprili ya mwaka 597 KK mwanzoni mwa mwaka mtakatifu.

 

(See paper No. 108) = (Tazama jarida Na. 108).

 

Kwa hiyo mwaka ulihesabiwa kuanzia mwanzo wa mwaka ulitangulia kwenye Aprili ya mwaka 599 KK.

Aprili ya mwaka 597 KK kwa hiyo ulikuwa ni mwanzo wa mwaka wa pili. Mwaka wa 596 KK ni mwanzo wa mwaka wa tatu. Mwaka 595KK ni mwanzo wa mwaka wa nne na mwaka wa 594 KK ulikuwa ni mwanzo wa mwaka wa tano wa utumwa wa Yehoyakini.

 

(See paper No. 108) = (Tazama jarida Na.108).