Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[116]
Majina ya Mungu
(Toleo La 2.0 19950306-20000705)
Majina ya Mungu
yametolewa na kufafanuliwa. Mazingira ambayo yametumika ni ya muhimu kwenye kuelewa
jinsi Mungu anavyotenda na ni kwa nani anayeongea naye.
Email: secretary@ccg.org
(Hatimiliki © 1995,
2000 Wade Cox)
(tr. 2016)
Masomo
haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na
tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa
mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza
kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka
maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia
yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Majina ya Mungu
Moja kati ya
dhana au nadharia inayokosewa kueleweka vyema kwenye Biblia ni jina la Mungu.
Imekuwa ikipotoshwa kwa upande mmoja na makosa ya kuwaaminisha au kuwafundisha
waamini Utatu au Watrinitariani ikifuatiwa na karne ya nne, na kwa upande
mwingine, kwa kukithi shauku ya imani ya Kiyahudi ili kuilinda imani yao ya
Mungu mmoja au Umonotheism dhidi ya mafundisho potofu ya Kitrinitarian pamoja
na mamlaka au nguvu kuwili za kiuzushi. Shauku ya kulinda ukuu wa kipekee wa
Mungu na kuitetea imani ya Kimonotheism iliyo kwenye mfumo na mafundisho ya Biblia
kutokana na makosa na upotoshaji yanayoendelezwa kwenye mafundisho ya
Kibinitariani na Watrinitarian kwa uzushi mkubwa na wa nguvu, ulioshuhudia
hatimaye imani ya Kiyahudi ikiachana kwa taratibu sana ukweli kuhusu uhalisia
na muundo mdogo wa jinsi Mungu alivyowafanyia Israeli. Malaika Mkuu ambaye
Elohimu amemhusisha kwenye maandiko. Matokeo mabaya ya jambo hili ni upotoshaji
wa baadhi ya maandiko muhimu na kuificha kweli umuhimu wa kiumbe huyu
mwakilishi aliyeshughulika na kuwaongoza Israeli kwenye kipindi cho chote cha historia
yao. Viumbe hawa wana majina, na majina yao yanaashiria uhusiano wao. Justin
Martyr kwenye waraka wake wa First Apology au Utetezi wa Kwanza kwa niaba ya
Kanisa aliompelekea mfalme wa Roma anasema kwamba Kristo alikuwa ndiye Malaika
wa Mungu kwenye Agano la Kale aliyempa Torati nabii Musa.
Kulijua jina la
Mungu ni ishara na dalili tosha ya kuielewa vyema Biblia. Makosa makubwa na
yaliyozoeleka ya mafundisho potofu kuhusu jina la Mungu yanatokana na kuielewa
vibaya Zaburi 83:18.
Zaburi 83:18 Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.
Jina hili
lilikuwa linatamkwa Yahova (halikuwa na herufi J kwenye lugha ya Kiebrania). Viumbe
wengi wanachukua jina hili kwa niaba ya yeye Mungu wa Kweli.
Andiko hili lenye
rejea ya karibu na Kutoka 6:3 na Isaya 26:4. Maandiko haya matatu yalikuwa
ndiyo sehemu tatu kwenye tafsiri ya biblia ya Authorised Version ambamo andiko
hili lilitafsiriwa na kuchapishwa kwa herufi kubwa na zilizokolea. Andiko la
Zaburi 83:18 linaonyesha cheo kingine chenye jina la Yehova aitwaye Elyon au
Mungu Aliye Juu Sana. Hiki ni cheo kinachotofautisha kama tutakavyokwenda
kujionea. Ni Yehova yuleyule ndiye afanyaye kazi na kuonekana akiwa sawasawa tu
pasipo kutofautika. Anayeonekana wazi mwingine ni Yahwe. Huyu pia anakuwa
hafanani. Maandiko mawili mengine yanasomeka:
Kutoka 6:3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na
Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
Isaya 26:4 Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.
Jina la Mungu
ambalo lilikuwa halijulikani na Mababa wa zamani yalikuwa na maana halisi na
ndivyo ilivyokuwa pia na madhumuni yake.
Jina Yehova (au
kwa usahihi wake sana linaitwa Yahova) ni mjumuisho wa jina Elohim nan linamaanisha
Elohim na El kwenye Zaburi 83:1. Elohim ni jina la uwingi, ambalo linategemea
na jissi linavyotumiwa. Linamaana zote mbili, yaani Mungu mmoja na miungu.
Linamaanisha au kumtaka kiumbe mmoja asilia na asiye wa kawaida. Linawataja
viumbe wengi wasiojulikana walio kwene Mwanzo 1:26.
Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Wabinitariani
wanajaribu kuhusisha au kuumaanisha usemi huu na viumbe wawili, wajulikanao
kama Mungu Baba na Kristo, lakini hata hivyo, jambo hili haliwezekani kupewa
maana kubwa ya kuwepo kwa Elohimu wengi na andiko lililo kwenye Ayubu
linalowataja wana wengi waliokuwepo wakati wa uumbaji (Ayubu 1:6; 2:1; 38:4-7).
Ayubu 1:6 Ilikuwa, siku moja
ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye
akaenda kati yao.
Ayubu 2:1 Tena
kulikuwa na siku hao wana wa Mungu walipokwenda kujihudhurisha mbele za Bwana,
Shetani naye akaenda kati yao, ili kujihudhurisha mbele za Bwana.
Hawa ni Wana wa Mungu (haElohim). Neno Bwana
lililopo hapa linamaana ya Yehova
(yaani Yahova). Tafsiri ya biblia ya The Companion Bible lina makala inayofafanua
kuhusu jina hili la Yehova kwenye
Jarida lake la Nyongeza au Appendix 4, II. Yehova inachukuliwa kumaanisha wa Milele au Mwenye Kusikika. Tafsiri yake ipo kwenye Mwanzo 21:33.
Mwanzo 21:33 Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la Bwana Mungu wa milele.
Umilele
unaoelezewa hapa unatokana na neno la Kiebrania la ‘olam lenye maana ya kipindi endelevu au bila ukomo. Chimbuko
la neno Yehova maana yake inaaminiwa
kuwa ni Yeye aliyekuwepo na Anayekuja. Kuna
tatizo katika kulichukulia jina lililotolewa pale Sinai kulichukulia kuwa lina
maanisha Yehova tu, peke yake.
Kutoka 3:14 Mungu
akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa
Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu.
Neno Mimi niko lililoko hapa linamaana ya hayah (%*% SHD 1961) ambalo maana yake ni kuwepo,
kuwa au kufanyika kuwa. Tafsiri
ya biblia ya the Companion Bible inaonyesha andiko hili kuwa ‘ehyeh ‘asher ‘ehyeh, na imelitafsiri neno
hili kuwa Nitakuwa jinsi nitakavyokuwa (au
nitakuwa) (soma maandiko yake kwenye ukurasa wa Nyongeza wa 48), hakuna pia
kinachomaanisha neno Yehova kuwa ni Yeye
atakuwa anaongelewa kwa pamoja na wenginewowote. Wanazuoni wa chuoni Oxford
wameonyesha kwenye tafsiri yao ya biblia ijulikanayo kama Oxford Annotated RSV kwamba
Yahwe kwa kweli ni muundo wa nafsi ya
tatu ya vebu ambayo kwa kweli inamaanisha Yeye
anayesababisha kuwa.
Kwa hiyo Mungu
anajidhihirisha kuwa ni kama Nitakuwa
kama nitakavyokuwa kwa kupitia Malaika pale Sinai. Anajulikana na kutajwa
kama Yehova (Yahova) ambayo inamaanisha kwa mtindo au umbo la nafsi ya tatu: Anayesababisha kuwa. Wakati mtu yeyote
anapotajwa kuwa ni kama Yehova kwa kweli utakuwa unasema kwamba Aliyesababisha kuwa. Na kwa hiyo utakuwa
unaunga mkono au kuitabua asili ya usaidizi wa kiumbe yeyote anayenena na wewe.
Wayahudi walielewa hilo na Mungu hakuongea nao kabisa na wao; bali walipewa
maelekezo yao yote na malaika ambao walikuwa ni wajumbe wake. Wajumbe hao
waliitwa Yehova na jina hilo linamaanisha ni
Yeye anayesababisha kuwepo, kwa kuwa yeye anayesababisha mambo kuwa
hakuwepo kabuisa huko. Unapolielewa neno Yehova unakuwa kila mara unajua kuwa
unamtaja mjumbe ambaye ni mtu fulani ambaye hujawahi kumuona au kuongea naye. Neno Yehova lina maana ya moja kwa moja ya
Sijawahi kumuona kabisa yeye.
Kwa hiyo, jina
alililotolewa la kuwa ni MIMI NIKO
pale Sinai lilikuwa ni Mimi niko na
ambaye nitakuwepo ambao ndiyo ujumbe ambao Mungu aliyempa Malaika huko
Sinai. Neno la Mungu lililotafsiriwa kama MIMI
NIKO haliku limetumika kabisa tena. Lilitumiwa mara moja tu kwenye Biblia. Neno
la Mungu ambalo neno hili limetoholewa kwalo limeandikwa kwa namna au mtindo wa
nafsi ya tatu la vebu. Tunajua kutokana na Yohana 1:18: Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu
Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua. Hivyo, walilitafsiri tu kuwa ni Mwana
pekee ili kuifikia nadharia au wazo la kwamba kulikuwa na mmoja tu aliyezaliwa
na Mungu.
Ni Mungu pekee
ndiye aliyenena na huyo ndiye monogenes theos, yaani Mwana pekee wa Mungu. Kwa
maneno mengine ni kwamba Yesu Kristo ndiye pekee aliyenena au kuongea na Mungu.
Baba Mungu hajaongea kamwe. Unapoyaona majina haya kwa lugha zote mbili, yaani
Kiebrania na Kiyunani ndipo unapata kujua au kuelewa. Tunapata matumizi mamoja
tu ya neno moja kumtaja Mungu na kisha tunalitumia jina Bwana na mambo mengine
ili kufikiliza. Kuwa na neno moja la Mungu kunatosha sana kwa kuwa hatutaweza
kujua kinachofanyika kwa kupitia majina ya Mungu.
Andiko
linalofuatia kwenye Ayubu ambali linahusika na Jeshi la Malaika ni kwenye Ayubu
38:4-7.
Ayubu 38:4-7 Ulikuwa
wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu. 5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani
aliyenyosha kamba juu yake? 6 Misingi yake ilikazwa
juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, 7 Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa
Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
Kutokana na andiko
hili tunajua kwamba andiko lililo kwenye Mwanzo 1:26 …… Na tumfanye mtu kwa
mfano wetu, kwa sura yetu; linataja kundi la viumbe ambao walikuwepo tangu
mwanzo wa kuumbwa kwa dunia; na kwamba kulikuwa na nyota wengi wa asubuhi; na
nyota ya asubuhi ni daraja au cheo na sio kiumbe. Kwenye suala hili la
mwanzoni mwa kuumbwa kwa dunia kuna nyota wengi wa asubuhi. Kulikuwa na mifumo
mingi ya makamanda waliokuwepo wakati wa kuumbwa kwa dunia hii. Hivyo
kunajitokeza hoja nyingi hizi zote kwamba kuna nafsi mbili Elohimu na kwamba kuna
Mwana mmoja tu wa Mungu. Maandiko hayo yanaonyesha kwamba imani ya Kibinitariani
ina uwongo mkubwa sana kama
ilivyo ya Kiutatu au Utrinitariani tu na inakwaza uelewa wa hatika yetu na
inajaribu kututenganisha na urithi wetu, ambao ni kufanyika kuwa warithi tulio
sawa na Kristo na kutawala kama wana wa Mungu na tutatawala tukiwa kama elohimu
na eli.
Nyota za asubuhi
wanazotajwa hapa ni wengi na wakati bado Kristo hajachukua wadhifa wake wa kuwa
nyota wa asubuhi wa sayari yetu hii na Shetani alikuwa ni Lusifa bado au mpeleka
nuru kama mwana wa asubuhi, nyota ya asubuhi au nyota ya mchana. Yeye ni mungu wa
dunia hii na mfalme wa nguvu za anga (2Wakorintho 4:4; Waefeso 2:2).
2Wakorintho 4:4 haisemi
kwamba Shetani ni theos wa dunia hii pasipo sababu. Waamini Utatu wanajaribu na
kusema kwamba tangua Thomas aliposema kuwa ninyi ni kurios na theos wangu kwa
Kristo, kwa hiyo basi yeye ni Mungu Babba kwenye mjumuiko wa Utatu. Kwa kweli,
Paulo anasema wazi kabisa kwamba Shetani ni theos wa dunia hii. Wote wawili ni
theoi: wote wawili ni miungu. Biblia inasema wazi sana kuhusu jambo hilo. Paulo
anasema kwenye 1Wakorintho 8:5 kuwa kuna theoi wengi na Mabwana wengi.
Kile tunachokiona
kuhusu Shetani kimeendelezwa kutoka kwenye Isaya 14:12-17 kunakomtaja kama
Lusifa au Mleta Nuru.
Isaya 14:12-17 Jinsi
ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi
ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! 13 Nawe
ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu
kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za
mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya
mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. 15 Lakini
utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.
Hawa nyota wa
Mungu wanaotajwa hapa ni wana wa Mungu. Nyota ni cheo au daraja. Yeye ni
kaburi. Tunakwenda kuwa naye nyota wa asubuhi anayekwenda kuzikwa kaburini.
16
Wao wakuonao
watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha
dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme;
Tuna
mabadiliko kwenye mazingira ya kicheo hapa kwa mwanadamu.
17
Aliyeufanya ulimwengu
ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?
Hapa tunaona
kwamba Lusifa, au mleta nuru, alikuwa mwana wa asubuhi au nyota ya
asubuhi au nyota ya mchana. Wadhifa
huu wa kicheo amepewa Kristo na aliwashirikisha wateule wake (2Petro 1:19; Ufunuo
2:28; 22:16):
Ezekieli 28:14-19 Wewe
ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu
ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. 15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa,
hata uovu ulipoonekana ndani yako. 16 Kwa wingi wa
uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa
sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho
najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya
moto. 17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako;
umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini,
nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama. 18 Kwa
wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu
pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami
nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao. 19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia;
umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.
Maandiko haya
yapo wazi. Vifaa vitakavyotumiwa kumwangamiza Shetani vinakuja kutokana na
nguvu za kiroho zilizoko ndani yake, yaani nguvu hizi zinakwenda kuwa ni vifaa
vitakavyomwangamiza au vya kuangamizwa kwake. Roho hii haitakwenda kuwepo tena
kabisa. Lusifa, nyota wa Asubuhi anakwenda kukoma kuwepo kwake. Anakwenda
kufanyika kuwa mwanadamu, akiwekwa kwenye mchakato na kupewa fursa ya kutubu na
kisha anakwenda kubadilishwa hulka yake na kuwa kiumbe wa namna nyingine. Njia
pekee ya kumtiisha Shetani pamoja na malaika zake waovu ni kwa kuwatoa nje ya
hulka au maumbile yao waliyonayo sasa, na kuwapa fursa ya kutubu na kwa suala
la Shetani kumfana aingie kwenye mchakato ambao kwao anaweza kutiishwa. Kwa
hiyo ndipo anapoweza kufanyika tena kuwa ni nguvu na uweza na ndipo anaweza
kutiishwa na kufikia utii kamili na maovu yake yanaweza kuondoka na kisha
akarejeshwa kwenye kundi la malaika.
Propaganda nyingi
zimekuwa zikienezwa kusema kwamba Mungu hatendi haki na kwa kweli ndiye
aliyemuumba Shetani awe kama hivi alivyo tangu mwanzo na Shetani hajapewa fursa.
Kwa jinsi hiyohiyo, Kristo naye aliumbwa mkamilifu tangu mwanzo na asingeweza
kufanya lolote kwa kuwa alikuwa na tabia na asili ya Mungu na Shetani hakuwa
nayo na wote ni mchezo uliokusudiwa. Hii ni propaganda ya Kishetani na kama
utaangukia kwenye uwongo huo wa kwamba Kristo asingeweza kutenda dhambi na
kwamba Shetani asingeweza kufanya jambo lolote jema, basi utakuwa unaifanya
kazi ya Shetani kwa niaba yake na kuutendea kazi mfumo wote wa imani ya Utatu
unaoendelezwa kusema kwamba kanuni zake ziliimarika, na kwamba Mungu hatendi
haki. Mungu hana upendeleo kama tutakavyokwenda kuona.
Shetani anakwenda
kuangamizwa kabisa na hataweza kuishi, kwa mujibu wa andiko hili. Atakwenda
kupunguzwa na kushughulikiwa wakati wa Marejesho mapya na siku ya Hukum (soma
majarida ya Hukumu ya Mapepo (Na. 80) na Lusifa, Mbebeba Nuru na Nyota ya Asubuhi
(Na. 223)). Vyeo hivi
hata hivyo vilikuwepo hata kabla ya kuumbwa kwa dunia na walikuwa wengi. Wana
wa Mungu (haElohim) walijihudhurisha mbele za Yehova kama tulivyojionea kwenye kitabu cha Ayubu.
Jina au neno Yehova liko kwenye aina mbili zenye maana
iliyo tofauti. Ni neno ambalo linaendana pia na majina mengine. Aina mbili
zilizo tofauti zipo kwenye jina hili la Yehova (SHD 3068) na jina Yehovi lililo
kwenye kamusi (SHD 3069). Kwa kweli yanatofautiana kwa kuonyesha watu wawili wenye
kubeba jina hili la kiwdhifa la mwingine na mwingine ni mdogo.
Kamusi ya Strong inasema kwamba Yehova ni jina la Kiyahudi la Mungu wa taifa.
Utofauti wa Yehovi (au kiuhalisia na sahihi huitwa Yehovi) linatumiwa badala ya
kutaja Adonai au Bwana. Huyu ndiye Bwana, Yehovi au ni mkuu kwa Yehova. Nie Yehova elyoni au Yehova wa Majeshi. Jina Yehova linatumika kama neno la
kutofautisha. Yehova anayeitwa kuwa Yehova wa Majeshi kama Yehova, ndiye Yehova
aliyetajwa kwenye Ezekieli 16:36, 31:10,15; 38:10,14; 39:8. Anayejulikana kama Yehova dabari
au neno la Mungu linalojitokezwa
kwenye Ezekieli. Adonai Yehovi linatumia
kwenye unabii wa Ezekieli 29:8 ambalo linaashiria kutofautisha kati ya neno la
Mungu na Yehovi Adonai.
Zekaria inaonyesha
kwamba kuna tofauti kwenye majina na watu wenyewe (Zekaria 2:3-12).
Zekaria 2:3-12 Na tazama, yule malaika
aliyesema nami akasimama karibu, na malaika mwingine akatoka ili kuonana naye; 4 naye akamwambia, Piga mbio, kamwambie kijana huyu, na
kusema, Yerusalemu utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na kuta, kwa sababu
ya wingi wa watu na mifugo iliyomo ndani yake. 5 Kwa
maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami
nitakuwa huo utukufu ndani yake. 6 Haya! Haya! Ikimbieni
nchi ya kaskazini, asema Bwana; kwa maana mimi nimewatawanya ninyi kama pepo
nne za mbinguni, asema Bwana. 7 Haya! Ee Sayuni,
jiponye, wewe ukaaye pamoja na binti Babeli. 8 Kwa
maana Bwana wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa
wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake. 9 Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao, nao
watakuwa mateka ya hao waliowatumikia; nanyi mtajua ya kuwa Bwana wa majeshi
amenituma. 10 Imba, ufurahi, Ee binti Sayuni; maana,
tazama, ninakuja, nami nitakaa kati yako, asema Bwana. 11 Na
mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu wangu;
nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako. 12 Na Bwana atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi
takatifu, naye atachagua Yerusalemu tena.
Ni wazi sana kutokana
na andiko hili kwamba kuna malaika wawili wanaohusika hapa. Mmoja ni bora na
mkuu kwa mwingine na huyu aliyebora zaidi na mkuu ni Masihi kwa kipindi chake cha
kabla ya kuzaliwa kwake rasmi hapa duniani. Ananena kwa niaba ya Yehova wa
Majeshi aliyemtuma. Aya ya 5 inamtaja kama kwa
maana Mimi nasema Bwana lakini kwa kweli inasema kwa kuwa Mimi ni mjumbe wa Yehova (soma kwenye Companion Bible fn.
to v. 5). Malaika huyu ambaye no mjumbe wa Yehova ndiye atawaokoa Israeli
kutoka kwenye mataifa (aya ya 9) na, kwa hiyo, mataifa mengi yatajua kwamba
Yehova wa Majeshi amemtuma kiumbe huyu kwao. Neno mboni ya jicho lake kwa kweli linamaanisha mboni ya jicho langu. Neno “langu”
limebadilishwa na kusomeka “lake” na
Sopherim kwa likitiliwa maanani neno lililo kama ni kumpunguzia heshima au
udhalilishaji kwa Yehova (soma kwenye tafsiri ya Companion Bible fn. Hadi aya
ya 8). Mabadiliko haya huenda yalitokana na kwamba neno mboni ya jicho langu limesababisha kufanya lionekane
kuwa ni mboni ya jicho la kiumbe mdogo. Mataifa mengi yataunganishwa kwa Bwana (Yehova)
katika siku ile. Ataketi katikati yao na watajua kwamba Yehova wa Majeshi amemtuma
kwao.kwa maneno mengine ni kwamba huyu Yehova anayetajwa hapa ni malaika
aliyetumwa kwa Waisraeli na Yehova wa Majeshi. Malaika huyu au mjumbe wa Yehova
wa Majeshi alikuwa ni elohim wa Israeli. Zekaria 12:8 inaonyesha wazi kwamba
Malaika wa Yehova alikuwa ndiye elohim na kwamba watakatifu watakuwa pia elohim
kama alivyo yeye.
Zekaria 12:8 Katika siku hiyo Bwana atawalinda
wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi
siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele
yao.
Neno “Mungu” lionekanalo
hapa linamaanisha elohim na malaika wa Bwana ni Malaika wa Yehova. Lengo lake
liko wazi. Wote wawili, yaani malaika na watu wa nyumbani mwake Daudi (yaani
watakatifu) watakuwa kama elohim.
Elohim kama
ilivyoelezewa hapo nyuma ni jina la uwingi la Mungu. Neno linalosimama kuhusu Mungu
kwa umoja ni Eloah. Jina hili linathibitisha haiba ya umoja ya Mungu. Mithali 30:4-5
inaonyesha kwamba ana mwana pamoja na kulitoa jina lake Eloah baada ya kuuliza
swali.
Mithali 30:4-5 Ni
nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa
makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya
imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama
wajua? 5 Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni
ngao yao wamwaminio.
Neno linalosimama
kuhusu Mungu kwenye aya ya 5 ni Eloah. Dhana na nadharia kuhusu mwana wa Mungu
ni kwamba linaweka wazi kwenye Agano la Kale. Nabii Ezekieli anaonyesha pia dhana
hii kwenye andiko lake la sura ya aya ya 21:8-13:
Ezekieli 21:8-13 Neno la Bwana likanijia, kusema, 9 Mwanadamu, tabiri, useme, Bwana asema hivi; Nena,
Upanga, upanga, umenolewa na kusuguliwa, 10 umenolewa
ili kufanya machinjo; umesuguliwa ili uwe kama umeme; basi je! Tufanye furaha?
Upanga unadharau fimbo ya mwanangu, kama unavyodharau kila mti. 11 Nao umenolewa usuguliwe, upate kushikwa mkononi;
upanga umenolewa, naam, umesuguliwa, ili kutiwa katika mkono wake auaye. 12 Piga kelele, utoe sauti ya uchungu, Ee mwanadamu,
kwa maana upanga u juu ya watu wangu, u juu ya wakuu wote wa Israeli;
wametolewa wauawe na upanga pamoja na watu wangu, basi, jipige pajani. 13 Kwa maana kuna kujaribiwa; itakuwaje, basi, ikiwa
upanga unaidharau hiyo fimbo? Haitakuwapo tena; asema Bwana MUNGU.
Usemi ulio
kwenye aya ya 9 unatokana na jina Yehova, hata hivyo baadhi ya viambatanisho vyenye
matoleo mengine matatu yaliyochapishwa mwanzoni zamani (mijawapo lenye bango
kitita za Marabi chini yake) zinasomeka Adonai. Kwene aya ya 13 tunasoma kwamba ni mjumbe wa
Yehova Adonai. Hivyo, tunashughulikia kuhusu Yehovi au Yehova mkubwa wa Majeshi
na tunaamini kuwa huyu ndiye mwanae ambaye alikuwa ni Masihi. Alipewa fimbo.
Upanga unaotajwa kwenye aya ya 11 ilikwenda kwa mfalme wa Babeli akiwa kama
mchinjaji lakini bado huu ulikuwa ni upanga uliowekwa kwenye bustani ya Edeni.
Hivyo Kristo aliuitimiliza unabii huu. Upanga wa mwanawe ulidharauliwa kwa kusulibiwa.
Upanga uliilaumu fimbo na kwa hiyo hata huo upanga hautaweza kuwepo tena. Kwa
hiyo kuhusu mwana na kifo chake ni mambo yaliyo wazi sana kwenye maandiko ya
Agano la Kale. Masihi ni mdogo kwa Yehova wa Israeli ambaye alitumwa na Yehova
wa Majeshi.
Andiko hili
linahusu kuchinjwa na maangamizo ya Israeli, na kukomshwa kwa ufalme, ambao
kwamba siku yake inakujaa ambapo uovu utakoma (aya ya 25). Kwa hiyo ndipo ufalme
utakoma hadi atakaporudi Masihi, ambaye
haki ni yake (aya ya 27).
Muundo wa
shina la Jah (au Yaho)
Yehova ni jina
moja tu linalomtambulisha Mungu na pia kwa wasaidizi wake wanaolitumia jina
lake. Muundo msingi wa kiini cha jina hili ni Jah ambalo pia ni jina
linalomhusu na kumtaja Mungu. Yehova wa Israeli hakuwa ndiye mlengwa kwenye maombi
au ibada. Mlengwa kwenye maombi ni Yehova wa Majeshi. Jina la Hekalu lilitokana
na chimbuko la jina hili likiandikwa na kutamkwa Yaho ambayo ndiyo neno la kale
lililomaanisha kuwa ni Jah au Jahh. Hili pia limeorodheshwa kuwa ni kama jina
la Mungu kwenye Zaburi.
Zaburi 68:4 Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,
Mtengenezeeni njia ya barabara, Apitaye majangwani kama mpanda farasi; Jina
lake ni YAHU; shangilieni mbele zake.
Mahala pa kwanza
kujitokeza jina Jah ni kwenye Kutoka 15:2. Hivyo, ni sahihi sana kusema kwamba
mfano huu upo kwenye sehemu ya pili au kwenye kitabu cha Kutoka cha Zaburi.
Huyu Jah anatajwa
hapa kama ni Bwana. Dhana ya kuwepo
kwa kiumbe anayemiliki au kutamalaki inaonekana. Inatumika kwa mara ya kwanza
kwenye Biblia kunahusianishwa hapa na ukombozi. Yeye ni El na ni baba wa hawa elohi.
Kisha aya ya 3 inaendlea
kusema kwamba Yehova ni ish au mtu wa vita.
Kutoka 15:3 Bwana ni
mtu wa vita, Bwana ndilo jina lake
Hapa Yehova anaitwa Bwana.
Kwa hiyo Sifa
zinatolewa kwa jina la Jah, kwenye Zaburi 68:4. Andiko lililo kwenye aya ya 8 linautaja
uwepo wa Mungu kwenye Kutoka.
Zaburi 68:8 Nchi ilitetemeka Naam, mbingu zilidondoka
usoni pa Mungu; Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli.
Huyu Mungu wa
uwepo wake alikuwa ni Malaika wa Yehova. Alikuwa hapa kama pani au uwepo wa elohim au peni-el,
Uso wa Mungu. Uwepo ulikuwa pamoja
nao jangwani. Andiko hili linamtaja elohim,
elohi wa Israeli, Mungu, Mungu wa Israeli.
Zaburi 68:17 inaonyesha
maana nyingine kwenye ustadi wa kuumba.
Zaburi 68:17 Magari ya Mungu ni ishirini elfu, maelfu
maelfu; Bwana yumo kati yao kama katika Sinai, Katika patakatifu.
Andiko hili lina
maana ile ile na nyingine. Tafsiri ya The Companion Bible inalibaini andiko
lisemalo kwamba idadi ya magari ya Mungu aliyoandikwa kwa lugha ya Kiebrania ni
mara mbili ya maelfu kumi na makumi elfu mengine, ambayo ni idadi ya milioni
ishirini. Andiko hili ni kwa mujibu sawa na elimu ya kame ya ki-tahajia kwenye
mgawanyo wa neno (Companion Bible fn.), ambayo ingesomeka Yehova ameshuka kutoka Sinai na kuja kwenye Maskani (Ginsburg, Intr., pp. 161,162). Au kwa kiudondoo au
kwa kutupia maneno ingesomeka kuwa ni Yehova
aliye katikati yao (yaani ni malaika na magari) [wamekuja kutoka Sinai] na
kuingia kwenye Maskani. (Linanisha na isemavyo Biblia.).
Tafsiri ya andiko
hili imeendelezwa kwenye aya nyingine inayofuatia ya 18.
Zaburi 68:18 Wewe umepaa juu, umeteka mateka, Umepewa
vipawa katikati ya wanadamu; Naam, hata na wakaidi, Bwana Mungu akae nao.
Yehova anayetajwa
hapa kuwa ameshuka mahala pa juu na kuwapa vipawa wanadamu na hata kwa wale
malaika waasi ili kwamba huyu Bwana Mungu au Jah Elohim aweze kuwa pamoja nao. Hii ni rejea ya moja kwa moja ya
tukio lililofanyika siku ya kuutoa Mganda wa Kutikiswa utowao siku ya Kwanza ya
juma au Jumapili asubuhi saa 3 kamili. Kristo alitolewa kuwa ni sadaka ya Mganda
wa Kutikiswa na akapokea vipawa ili awape wanadamu, kipawa kijulikanacho kama
Roho Mtakatifu. Kutokana na andiko la Yohana 20:17 Kristo alimhakikishia Mariamu
kuwa Anapanda kwenda kwa Mungu na Baba yetu wote. Kwenye Yohana 20:19-22 tunaona
kwamba hatimaye alirejea siku hiyohiyo na kuwapulizia pumzi ya Roho Mtakatifu
kwa Wanafunzi, akiashiria kukubalika kwake na kuwapa vipawa vilivyoahidiwa
kwenye Zaburi 68:18 na kwamba sasa zinatolewa rasmi na Baba kwa Kanisa ili kuanza
mchakato wa kuwatuma waende. Siku hii ilianzisha kipindi maalumu cha Hesabu ya
kuelekea kwenye Pentekoste ambako ndiko vipawa au karama za Roho Mtakatifu
vitatolewa kwa kanisa zima lote. (Soma pia jarida la Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa (Na. 106b)).
Jah au kwa
usahihi zaidi inaandikwa Yaho ni neno shina ya jina linalomtaja Mungu kwendana na
uwakilishi na namna zake. Jah [wa] Elohim ni sawa tu na Yehova wa Majeshi. Yehowa
mdogo anatajwa hapa kuwa amewatoa watumwa kutoka utumwani ili kwamba viumbe
wote wa namna mbili zote, yaani watiifu na waasi waweze kupatanishwa na Mungu. Kiumbe
huyu anayewaokoa au kuwatoa watumwa kutoka utumwani anaonekana kwenye andiko hili
na kutajwa kuwa ni Kristo kwa rejea iliyo kwenye Waefeso 4:8 na Ufunuo 13:10. Alipokea
vipawa kutoka kwa Mungu na alivitoa kuwapa wanadamu.
Waefeso 4:7-8 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa
kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. 8 Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka
mateka, Akawapa wanadamu vipawa.
Andiko hii
linamlenga Kristo na kumtaja kuwa ni malaika aliyetumwa kuwasaidia Israeli.
Hapa Paulo anataja tukio la kupaa kama kulivyoelezewa kwenye Zaburi 68:17 lakini
hakuondoi somo lenyewe kamili la maana yake kwenye andiko hili.
Sambamba nayo,
kwenye Ufunuo kunazitafsiri aya hizi kuhusu kuwatoa
watumwa au wafungwa utumwani hivi:
Ufunuo 13:10 Mtu
akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa
upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.
Ni wazi kabisa
kwamba Yehova hapa ni Kristo ambaye pia ni Malaika wa Yehova. Kwa hiyo, Yehova
ni jina la uwakilishi tu. Yehova hastahili kuabudiwa. Ni kwa pale
anapodhihirishwa tu kuwa ni Yehova elohim au Yehova wa Majeshi anaweza kujulikana
au kuchukuliwa kuwa anastahili kuabudiwa. Ni jina la Mungu tu peke yake ambalo linamtaja na
kumdhihirisha Baba kwa neno moja ni Eloah. Inampasa Yehova aambatane na maneno
mengine au achukuliwe kwenye mstakabala wa kuonyesha mhusika. Kwa hiyo, Mungu
Baba anaweza kujulikana tu kama hivyo kwa neno Eloah. Linapotumiwa kwa mtindo
wa shina la neno lenyewe la Jah, ndipo lazima iwe kuwa anayetajwa hapo awe ni
Mungu.
Matumizi ya neno Jah
yanawezesha utendaji kazi kwene maandiko. Linatokea kwa takriban mara arobaini
na tisa, jambo linaloonekana kuwa ni hitimisho la mizunguko saba. Lina maana
yake Fulani na maalumu kama Yehova
amefanyika kuwa wokovu wetu. Linakamilisha mara 49 au mizunguko ya
kuingilia kwenye Patakatifu pa Patakatifu kwenye mzunguko wa Hamsini ambao ni
ishara kamili ya Hekalu la Mungu ambalo sisi ndilo Hekalu lake.
Hekalu limeitwa
kuwa ni Hekalu la Yaho kutokana na herufi na uandishi wa lugha ya Kiaramu la
Hekalu lililoko huko Elephantine (soma kitabu cha Pritchard, cha The Ancient Near East etc., vol I, pp.
278-280). Kwa hiyo Jah linalitaja jina la kale la Yaho lililotumika tangu
takriban mwaka 407 KK. Kwa hiyo, namna sahihi ya kimuundo la kiuandishi la Yehova
ni Yahova au Yahovih kutegemea kisarufi kilichotumika anapotajwa kiumbe
mwenyewe. Linatamkwa Yahowe au Yahowih. Neno Yahweh kwa hiyo ni sahihi sana (soma
jarida la Abracadabra: Maana ya Majina (Na. 240)).
Umakini ni lazima
uchukuliwe katika kumuonyesha au kumwelezea Yahowe kuwa ndiye anayestahili peke
kuabudiwa. Vinginevyo kama hataonyeshwa na kueleweka kuwa ni kama Mungu mkuu, Yahovah
wa Majeshi ambaye ni Eloah, na hapa ndipo imani juu ya Mungu mmoja inakanganywa
na ndipo imani ya Kibinitariani inapoanzia.
Jina Yehova au
Yahova linajumuishwa na majina mengine kumi. Yamepangiliwa kwa mpangilio sawia na
yanatokea kwenye maandiko ya Kiebrania yafuatayo kama hivi:
1. Yehova-Yire Yehovah ataona
au atatupatia mahitaji yetu (Mwanzo 22:14).
2. Yehova-Ropheka Yehova
awaponyaye ninyi (Kutoka 15:26).
3. Yehova-Nissi Yehova
bendera yangu (Kutoka 17:15).
4. Yehova-Mekaddishkem Yehova awatakasaye ninyi (Kutoka 31:13; Walawi
20:8; 21:8; 22:32; Ezekieli 20:12).
5. Yehova-Shalom Yehovah [aletaye]
atumaye amani (Waamuzi 6:24).
6. Yehova-Zeba’oth Yehova wa
Majeshi (1Samweli 1:3 na sehemu nyingine nyingi tu).
7. Yehova-Zidkenu Yehova ni haki
yetu (Yeremia 23:6; 33:16).
8. Yehova-Shamma Yehova yupo
hapa (Ezekieli 48:35).
9. Yehova-’Elyon Yehova
Aliyejuu Sana (Zaburi 7:17; 47:2; 97:9).
10. Yehova-Ro’I Yehova mchungaji
wangu (Zaburi 23:1).
Zaburi ya Ishirini
na Tatu inatumia tabia saba zilizotajwa kwenye majina haya ya Mungu:
Aya ya 1; inaendeleza
dhana 1 (Yehova-Yire).
Aya ya 2; inaendeleza
dhana 5 (Yehova-Shalom).
Aya ya 3; inaendeleza
dhana 2 na 7 (Yehova-Ropheka na Yehova-Zidkenu).
Aya ya 4; inaendeleza
dhana 8 (Yehova-Shamma).
Aya ya 5; inaendeleza
dhana 3 na 4 (Yehova-Nissi na Yehova Mekaddishkem).
Tafsiri ya the
Companion Bible ina mkururo wa hoja (Nyongeza 4) kuhusu El kuwa ni muhimu sana na
ndiye mwenyezi ingawaje neno lenyewe halijaashiria kuwa hivyo kabisa. Dhana hii
kwa kweli ni kama El Shaddai. Matumizi ya neno El yanatumiwa ni kumaanisha kuwa
Mungu ana uweza wa kipekee wa Kuelewa kila jambo. Elohim linatumika kwa maana
ya kwamba Mungu ni Muumbaji kwa kuwa Mungu anaumba na ameziweka kanuni au sheria
na torati mikononi mwa waombezi au wapatanishi. Elohim ni uwingi. El linatumika
kama shina kwa maelekezo muhimu ya kumuelezea Mungu. Ni Eloa tu peke yake
ambaye ndiye Mung anayependa na ni mmoja peke yake anayestahili kuabudiwa na
watu wake (soma pia tafsiri ya Companion Bible. Jalada ya Nyongeza 4). El inadhaniwa
kuwa ni Mungu ajuaye mambo yote au kila jambo (limejitokeza kwa mara ya kwanza
kwenye Mwanzo 14:18-22) na aonaye mambo yote (Mwanzo 16:13) na anawafanyia kila
jambo watu wake (Zaburi 57:2) na ni ambaye kwa yeye mambo yote ya mbinguni nay
a kimungu yanahusika (Comp. Bible ibid.). Hata hivyo kuna ukweli kwamba neno El
ni shina linalojitokeza kwenye majina na vyeo vinavyoashiria au kuonekana kwamba
ni shina tu ambalo kwamba linafanya tofauti ya viwango inayoonekana kwenye vitu
ambavyo vinatenda kazi kwa kuwakilisha. Kwa mfano, Malaika wa Yehova pia ni El
Bethel au Mungu wa Nyumba ya Mungu. Kwa maneno mengine, inaonesha mamlaka au
uweza kwenye muunganiko huo. Ni Eloah t uni namna moja ya uenezi wa kiibada.
Eloah ni Elohim
wa Elohim; Yeye atiaye mafuta (Zaburi
45:6-7; Waebrania 1:8-9). Eloah ni Mungu Apendaye. Mungu huyu nuyu ndiye anayestahili
kuabudiwa na ni kini na mlengwa mkubwa wa Elohim. Huyu ndiye aliyependa na nye
aliyependa na ni katika yeye vitu vyote vimekuwapo na viliumbwa (Ufunuo 4:11).
Ufunuo 4:11 Umestahili wewe,
Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe
ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo
vikaumbwa.
Huyu ndiye
mlengwa na anayestahili kuabudiwa na wazee ishirini na nne na mwana kondoo
ambaye ni Masihi (Ufunuo 4:1-5:14). Masihi ndiye mwana na mzaliwa pekee na Eloah ni Baba kutokana na Mithali 30:4-5.
Kujitokeza kwake kwa kwanza kwa jina hili kunahusiana na stahili yake ya
kuabudiwa (Kumbukumbu la Torati 32:15,17). Linatumika kwa namna tofauti na sanamu
naye ndiye Mungu aishiye na aliyehai. Huyu ndiye Mungu ambaye hapatwi na
madhara wala hafi (1Timotheo 6:16). Wengine wote wanapata uzima wa milele kutoka
kwake kwa mapenzi na maelekezo.
El Elyon ni jina
linalommaanisha Eloah kuwa ndiye El Aliye Juu Sana. Yeye ni Mungu wa peke na
Aliye Juu Sana na ni Baba kama tunavyojua kutokana na lugha ya Kiyunani
inayomtaja hivyo kwenye Luka 1:35. El Elyon ni kiumbe aliyeyagawanya mataifa (Kumbukumbu
la Torati 32:8). Aliwapa Israeli kama sehemu ya Yehova. Kwa hiyo, Yehova hapa ni
Yehova wa Israeli na ni mdogo kwa Eloa au El Elyon. Ni huyu Eloah au Elyon ndiye
mlengwa na anayestahili kuabudiwa. Israeli hawabumuabudu huyu elohim mdogo. Tilia
maanani kwamba andiko la Kumbukumbu la Torati 32:8 limepotoshwa kwenye maandiko
yaliyo kwenye tafsiri ya Masoretic ili isomeke sawasawa na idadi ya Wana wa
Israeli zaidi kuliko kama ilivyoandikwa kwenye maandiko yake asilia yasemayo wana wa Mungu au idadi ya malaika (LXX) au eliym
au miungu (DSS).
Mwanzo 14:18-22 inaonyesha
kwamba Mungu Aliye Juu Sana ndiye amiliki wa mbingu na nchi na kwamba
Melkizedeki ni kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana nay eye mwenyewe hawezi kuwa
ndiye huyo Mungu. Mtu hawezi kuwa kuhani anayejitolea dhabihu mwenyewe.
Maandiko haya yapasa kulinganishwa na Zekara 6:13 na 14:9.
Zekaria 6:13 Naam, yeye atalijenga hekalu la Bwana; naye atauchukua
huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na
kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao
wawili.
Kwa hiyo tunaelewa
kwamba kiti cha enzi cha Mungu Aliye Juu Sana anatawala na Masihi kwa kuelekezwa.
Muungano wa ufalme mfumo wake unatokana viumbe walio chini ya mapenzi ya Eloah.
Zekaria 14:9 Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi
yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.
Yehova (iliyotafsiriwa
Bwana) atakuwa mfalme juu ya dunia na ulimwenguni kote. Kisha Yehova atakuwa ni
mmoja (ehad) na jina lake litakuwa moja (ehad). Huu umoja unaoainishwa wa
utawala wa Yehva ni kwamba Mungu anafanika kuwa yote katika yote na ndani ya
yote (1Wakorintho 15:28; Waefeso 4:6).
Waefeso 4:6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na
ndani ya yote.
Kwa hiyo Mungu ni
Baba tu na yupo juu ya mambo yote na kila jambo. Kristo amejumuishwa kwenye
mahudhui haya.
1Wakorintho 15:28 Basi,
vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa
chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika
wote.
1Wakorintho 15:28 Basi,
vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa
chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika
wote.
Wakati vitu vyote
vinapotiishwa chini yake, ndipo hapo mwana mwenyewe atajinyenyekeza kwa Mungu
na kukabidhi vitu vyote aliyemkabidhi mambo yote na kuviweka chini yake ili kwamba
Mungu afanyike kuwa yote katika yote. Tafsiri ya RSV haiko sahihi ikionekana kutokana
na shauku yake ya kukusudia kuyashinda mahitimisho yote na hoja zinazotolewa na
wale wasioamini Utatu yaliyochukuliwa kutoka kwenye andiko hili. Mungu atakuwa
ndani ya yote kama alivyo ndani ya Kristo.
Kwa hiyo, Elyon yupo
ulimwenguni kote (Zaburi 83:18). Jina hili la kicheo linakutikana mara 36 au 6
x 6 ambayo inamaana yake fulani inayohusiana na uumbaji wa mambo yote.
Shaddai inamaanisha Mwenyezi kwa maana ya kuwapatia watu vitu na mahitaji yao.
Limetumika wakati Ibrahimu alipoitwa atoke ili aenende pamoja naye kwenye
Mwanzo 17:1. Mtazamo wa kuitwa atoke uliitikiwa na Ibrahimu na unakubalika pia
na Kanisa 2Wakorintho 6:18.
2Wakorintho 6:17-18 Kwa hiyo, Tokeni kati yao,
Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa
kiume na wa kike,
Kwa mara nyingine
tena tunamtaja Mungu Baba. Neno lililotumika ni El Shaddai.
Adon. Ni moja kati ya majina matatu ya kicheo, (ambayo ni Adon, Adonai, Adonim). Kwa ujumla yanaitwa na kutamkwa kama Bwana. Kwa ujumla, yanamaana ya Bwana
kama mtawala wa dunia. Inatofautiana
na neno Adonai ambalo linatumika kama
linachukua mapenzi ya Mungu hapa duniani. (Bwana katika uhusiano wake na dunia
Companion Bible ibid.). Vokali inaoonyesha uhusiano wake na Yehova wakati inapotumika
na Adon inasikika au kufanya ionekane na kusomeka Adonai. Hii ilifanyika kwa makusudi kabisa kwenye vifungu vya 134 ambavyo
vimegeuzwa kwa kupotoshwa na kutolewa kwenye tafsiri ya Massorah (§§ 107-115)
(soma poa kwenye tafsiri ya Companion Bible App. 32 ili kupata orodha yake).
Adonim ni uwingi
wa Adon na haijatumiwa kabisa kwa mwanadamu (Comp. Bible ibid.). Imerahisishwa
kwamba huenda Adon anaweza kuwatawala wengine ambao hawapo upande wake. Kwa hiyo,
pasipo na kijimakala hicho ingeweza kutumiwa na watu. Bullinger haelezei kwa
kina sana na uwingi na umoja kwenye matumizi ya maneno yanayohusiana na viumbe
wa mbinguni. Hakuna mashaka kwamba matumizi ya neno Adonai na elohim yalitumika
ili kuweka tofauti fulani na maalumu kati ya majina haya mawili ya Yehova na
Yehova wa Majeshi. Yehova kama lenyewe lilivyo tu (SHD 3068) ni elohi wa taifa
wa Israeli (soma kamusi ya Strongs) na hapaswi wala sio mlengwa wa kuabudiwa. Yehovih
(SHD 3069) ni ni mkuu kwa Yehova, ni elohi wa Israeli ambaye pia anaitwa Malaika
wa Yehova.
Yehova kwa maneno
mengine na kama Adonai Yehova anaitwa Bwana Mungu na kwa hiyo ni tofauti na
matumizi ya umoja. Kuna maneno mawili yanayoitwa na kumaanisha Bwana Mungu nayo
ni Adonai Yehova na Yehova Elohim. Neno moja au jina elohim mara nyingi
linatumika kwa malaika na hasahasa Malaika wa Yehova ambaye ni elohim aliyetiwa
mafuta kwenye Zaburi 45:6-7 na ambaye ndiye Kristo (Waebrania 1:8-9).
Kwa hiyo, Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita
wenzio.
Kwa jinsi hiyohiyo
ndipo sisi sote tutakapofanyika kuwa elohim chini ya jina lake na uweza au
nguvu zake (Zekaria 12:8) kwenye imani ya Mungu mmoja iliyoko kwenye nadharia
ya Biblia. Imeandikwa Mimi nimesema, Ndinyi Miungu; Wana wa Aliyejuu Sana
ndinyi nyote na Maandiko Matakatifu hayawezi kutanguka (Yohana 10:34-35). Imani
za Kibinitariani/Kitrinitariani zinaknza kuelewa dhana na nadharia kwamba
tutatawala pamoja na Mungu.
q