Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[227]
Sikukuu za Mungu na
Jinsi Zinavyohusiana na Uumbaji
(Toleo La 3.0
19980101-19980424-20070718)
Jarida hili linaokusudia kuonyesha kuhusu Sikukuu zilizoamriwa
na Mungu na Sabato na Miandamo ya Mwezi na jinsi zinavyohusiana, kipindi au
mahali zinapotakiwa kufanyika muafaka, kwenye “juma la uumbaji” kwenye Kitabu
cha Mwanzo. Jarida hili pia linatathmini uhusiano wake wa ndani kati ya Sikukuu
na vipindi vyake vinavyotakiwa kuadhimishwa.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1998, 2007 Wade Cox,
based on a 1997 paper by Alan Williams)
(Tr.
2014)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Sikukuu za
Mungu Jinsi Zinavyohusiana na Uumbaji
Uumbaji wa Dunia ni jambo la kuanzia na la msingi katika
mpangilio wa Sikukuu za Mungu. Kwa mujibu wa muundo wa uumbaji, juma la uumbaji
linaanzia siku ya kwanza ya juma (Jumapili) na linaenda hadi siku ya saba au
siku ya Sabato (Jumamosi). Juma hili linaonyesha kuweka taswira ya miaka elfu
saba (2Petro 3:8), ambako kwamba, Jumapili inawakilisha taswira ya miaka elfu
moja.
Mwanzo 1:2-3 Nayo
nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya
maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru
Ni muhimu kujua kwamba kwenye muundo huu juma
linalotangulia linaonekana pia kuwa kama ni siku ya Kwanza ya mwezi wa Kwanza
kwa mtazamo wa kimapokeo wa kawaida. Siku ya Kwanza iliyo muhimu ilipaswa kuwa
ni ile siku ya Kwanza ya mwezi wa Kwanza na hivi ndivyo ilivyokubalika kwa
ujumla. Kuna idadi ya mambo yanayokihusu kipindi hiki maalumu yenye maana ya
moja kwa moja na uumbaji na lengo lake la kwanza halisia, ambalo ni uumbaji wa
mwanadamu. Kwa hiyo hii hatimaye inahusiana na mwelekeo wa kwenda kwenye
Sikukuu za kwanza na utakaso wa wanadamu.
Siku ya Kwanza ya mwezi wa Kwanza ilitumiwa pia na Mungu
kuiukarabati tena dunia kipindi cha Nuhu, Musa na katika marejesho mapya
yaliyotabiriwa kwenye Biblia (Mwanzo 8:13). Maangamizo ya Dunia yalitangulia
kutoka mwaka uliotangulia siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili baada ya Safina
kufungwa siku ya kumi. (sawa na Mwanzo 7:9-11). Tendo hili la kuwatenga na kuwaweka kando mbali wateule kwa namna inayoonyesha kiuashirio kwa
Pasaka ya pili, kama tutakavyoona baadae.
Siku ya Kwanza ya Mwandamo wa Mwezi wa Kwanza wa Abibu tangu
kuanza kwa mhakato wa kulitakasa Hekalu la Mungu. Ni ushuhuda unaaonekana pia
kwenye imani na dini ya Kiyahudi kwa wazi kabisa kimwili. Ni kama ilivyosemwa
na Kristo, na kwenye Ukristo, jambo hili lina taswira ashirifu ya Hekalu la
Mungu ambalo limejengwa kwa mawe yaliyo hai na Hekalu hilo ndilo sisi (1Petro
2:5; 1Wakorintho 3:16; 6:19 sawa na jarida la Utakaso wa Hekalu la Mungu (Na. 241) [Sanctification of
the Temple of God (No. 241)].
Kuelekea chini hadi aya ya 31:
Mwanzo 1:31 Mungu akaona kila
kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku
ya sita.
Mwanzo 2:1-3 Basi
mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. 2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku
ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. 3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo
Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Neno lililotafsiriwa akapumzika (SHD 7673) lililotumiwa kwene Mwanzo
2:3 linamaanisha kusimama au kuacha [kuto
exertion] au kusimama baada ya kumaliza; kupumzika.
Sabato ya Juma
Siku ya saba ya mwezi wa Kwanza ina maana mbalimbali
zinazoiashiria, zinazohusiana na wokovu wa mwanadamu. Tunaona kwamba kwenye juma
hili la kwanza, siku ya Saba ya mwezi wa Kwanza ilikuwa pia ni Sabato.
Juma (na Sabato) imeoorotheshwa na Sikukuu za Mungu
kwenye Mambao ya Walawi 23:1-3. Hii inaonyesha uhusiano wa moja kwa moja
ilionao na hizi Sikukuu.
Mambo ya
Walawi 23:1-3 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Nena na wana wa Israeli, na
kuwaambia, Sikukuu za Bwana, ambazo mtazipigia mbiu kuwa ni makusanyiko
matakatifu; hizi ni sikukuu zangu. 3
Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya
kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yo yote; ni Sabato
kwa Bwana katika makao yenu yote.
Mungu anasema kwamba siku ya Sabato ni ya mapuziko.
Tunapaswa kufanya kazi kwa siku sita kama Mungu alivyofanya alipokuwa anaumba,
na akapumzika siku ya saba.
Sabato, kama tunavyoambiwa, inatukumbusha mapumziko ya
Mungu na mwisho wa juma la uumbaji. Andiko linaonyehwa kwamba Sabato inaonyesha
taswira ya mapumziko ya Mungu na utimilifu wa mambo aliyoyaumba na kuyafanya.
Mwanzo 2:3 Mungu akaibarikia siku ya
saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya
kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Kwenye Injili ya Yohana 5:17, Kristo anasema kwamba ueue
na Baba bado wangali wanafanya kazi. Mapumziko haya ya Mungu ni ashirio ya mapumziko
yajayo, kama yanavyoonyeshwa kwenye waraka kwa Waebrania.
Waebrania 4:1-4 Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha
yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. 2 Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile
vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu
halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia. 3 Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha ile; kama vile alivyosema, Kama
nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu: 4 Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu
alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote;
Kwa muhibu wa tulivyoona hapa tunagundua kwamba Israeli
wa kimwili hawakuingia kwenye raha au pumziko la Mungu Aliye Hai na ndio ulikuwa
Mpango wa Mungu kuwa na Israeli wa kiroho na kuwafanya waingie kwene raha
iliyotajwa kwenye aya ya 8:
Waebrania 4:8-9 Maana kama Yoshua
angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye. 9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.
Katika Waebrania sura ya 3 na 4, tunaona kwamba Sabato
ilikuwa inaashiria ahadi iliyotolewa ya raha au mapumziko kwa Israeli kutokana
na maadui zake wakati walipokuwa kwenye Nchi ya Ahadi. Hatahivyo, hawakuipata
kamwe hiyo raha au mapumziko kwa ajili ya kuasi kwao (Israeli hawakuzitii amri
za Mungu). Historia ya Biblia ya Waisraeli hawa wa kimwili tunapaswa kuitumia
ili kujifunza masomo, na pia kwa ajili ya unabii wa Siku za Mwisho.
Warumi
15:4 Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi;
ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.
1Wakorintho
10:11 Basi mambo hayo
yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi,
tuliofikiliwa na miisho ya zamani
Sabato ni ishara pia ya kutolewa kwa watu wa Mungu kutoka
utumwani hhuko Misri.
Kumbukumbu la
Torati 5:12-15 Ishike siku ya Sabato uitakase, kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru. 13 Siku sita fanya
kazi, utende mambo yako yote; 14 lakini
siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote,
wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala
ng'ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako ye yote, wala mgeni aliye ndani
ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe.
15 Nawe utakumbuka
ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa Bwana, Mungu wako,
alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo
Bwana, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.
Kwa hiyo, kuna muunganiko kati ya siku ya kwanza ya Mikate
Isiyo na Chachu na Sabato ya siku ya saba ya juma la uumbaji, kama siku ya
kwanza ya mikate Isiyo na Chachu ambayo inaashiria pia kutoka kwao utumwani
Misri.
Kutoka 12:47-51 Na wafanye jambo hili
mkutano wa Israeli wote. 48
Na
mgeni atakapoketi pamoja nawe, na kupenda kumfanyia Bwana pasaka, waume wake
wote na watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya pasaka; naye atakuwa mfano
mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi; lakini mtu ye yote asiyetahiriwa asimle. 49 Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu, na kwa
mgeni akaaye kati yenu ugenini. 50
Ndivyo
walivyofanya wana wa Israeli wote; kama Bwana alivyowaagiza Musa na Haruni,
ndivyo walivyofanya. 51 Ilikuwa siku ile ile
moja, Bwana akawatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri kwa majeshi yao.
Kutoka na kuondoka Utumwani kulikoandikwa kwenye Kutoka
13:3-10:
Kutoka 13:3-10
Musa
akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba
ya utumwa; kwa kuwa Bwana aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na
usiliwe mkate uliochachwa. 4
Ninyi
mwatoka leo katika mwezi wa Abibu. 5
Itakuwa
hapo Bwana atakapowaleta mpaka nchi ya Wakanaani, na Wahiti, na Waamori, na
Wahivi, na Wayebusi, nchi hiyo aliyowaapia baba zako kwamba atakupa wewe, ni
nchi imiminikayo maziwa na asali, ndipo mtakapoushika utumishi huu katika mwezi
huu. 6 Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba,
nayo siku ya saba itakuwa ni sikukuu ya Bwana. 7 Mikate isiyochachwa italiwa katika hizo siku saba; mkate uliotiwa chachu
usionekane kwako, wala chachu isionekane kwako, ndani ya mipaka yako yote. 8 Nawe utamwambia mwanao siku hiyo, ukisema, Ni kwa sababu
ya hayo Bwana aliyonifanyia hapo nilipotoka Misri. 9 Nayo itakuwa ishara kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya macho
yako, ili kwamba sheria ya Bwana ipate kuwa kinywani mwako; kwani Bwana
alikutoa utoke Misri kwa mkono wenye uwezo. 10 Kwa hiyo utaitunza amri hii kwa wakati wake mwaka baada ya mwaka.
Uhusiano
kati ya Sabato na Pasaka hata hivyo, uko kwenye juma la pili la juma la mwezi
wa Kwanza. Kabla hatujauangalia uhusiano uliopo kati ya Sabaso na Pasaka na Idi
ya Mikate Isiyo na Chachu, tunapaswa kuliangalia juma la kwanza la mwezi wa
Kwanza. Siku ya Kwanza ya mwezi wa
Kwanza ilikuwa ni ya Utakaso wa Hekalu, na utaratibu wa huduma za Hekalu
lilitayarishwa kwa ajili ya Mpango wa wokovu kama ilivyoonyeshwa kwenye Pasaka.
Siku ya Saba ya mwezi wa Kwanza ni siku ya Utakaso kwa ajili ya dhambi
zilizofanywa kwa Kupotoshwa na ni ya muhimu sana kwenye muundo wa mwisho wa
Hekalu ambako siku hii imeamriwa kuadhimishwa kwa ajili ya Utakaso (Ezekilei
45:18-20).
Ezekieli
45:18-20 Bwana
MUNGU asema hivi; Mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, utatwaa ng'ombe
mchanga mume mkamilifu; nawe utapatakasa mahali patakatifu. 19 Na kuhani atatwaa baadhi ya damu
ya sadaka ya dhambi, na kuitia juu ya miimo ya milango ya nyumba, na juu ya
pembe nne za daraja ya madhabahu, na juu ya miimo ya lango la ua wa ndani. 20 Nawe utafanya
vivyo hivyo katika mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi kwa ajili ya kila mtu
akosaye, na kwa ajili ya mtu aliye mjinga, ndivyo mtakavyoifanyia nyumba
upatanisho.
Ndipo
tunapoona hapa kuwa kuna dhabihu ya muhimu sana ya kulitakasa Hekalu au Nyumba
ya Mungu, ili kuliwezesha lifanye kazi zake kwa huduma za kulitakasa taifa
kwenye Pasaka. Kwa hiyo Pasaka inakuwa kwenye mchakato au awamu ya pili au wiki
ya pili ya uumbaji. Kwa hiyo, kitendo cha kuutakasa Ulimwengu ulikoandikwa
kwenye kitabu cha Mwanzo ulielekea kwenye tendo la kujitakasa kwa ajili ya
dhambi zilizofanywa kwa kupotoshwa ili wawe na sehemu na kuhesabiwa kwenye
mchakato uliopo kwenye Mpango wa Mungu. Soma jarida la Utakaso kwa Ajili ya Dhambi
za Kupotoshwa (Na. 291) [Sanctification of the Simple and Erroneous (No. 291)].
Juma la kwanza la utakaso linaonyesha kwamba siku ya Saba
ya Mwezi wa Kwanza la shughuli za Uumbaji ilikuwa ni siku ya Sabato. Kwa hiyo
wazo au dhana utakaso sio la kulifanyia haraka, bali ni njia pekee muhimu ya
kulitakasa kusanyiko ni kwa njia ya haraka. Kwa hiyo, matendo ya Mungu kwa
wateule yanawezesha kwenye uumbaji wote kamili kuchukua sehemu yake kwenye
Pasaka. Sabato kwa kawaida ni kipindi cha sikukuu
lakini kitendo cha kufunga saumu kwa kuzitubia dhambi zilizofanywa kwa
kupotoshwa na kutokujua ni ukweli uliotiliwa chumvi.
Ni
suala la kimzunguko wa kila mmoja aweze kuletwa kwenye Imani kutoka kwenye
harakati za wateule wakiwa kama kundi la kiroho linaloonekana kwenye Pasaka.
Ingekuwa haiwezekani kwa mtu kuingizwa Hekaluni la Mungu akiwa kama Jiwe lililo
Hai kutoka kwenye maadhimisho ya Pasaka kama haikuwa rahisi kutokana na
mchakato wa utakaso wa wana wa kiroho wa Mungu. Mchakato huu unaashiriwa kwa
utakaso wa juma la kwanza la mwezi wa Kwanza katika siku za Kwanza na Saba za
mwezi. Ishara hii inaonyeshwa kwa kutoa dhabihu ya kondoo mke kwa ajili ya dhambi zilizofanywa kwa kutoshwa na
imeelezewa vizuri kwenye Hesabu 15:27-29. Dhambi hii iliyofanywa pasipo kujua
au kwa kupo hwa na uthibitisho kwamba zinafanywa kwa utoaji wa dhabihu unafanyika
ulimwenguni kote.
Hesabu 15:27-29 Tena kama mtu mmoja akifanya
dhambi pasipo kujua, ndipo atasongeza mbuzi mmoja mke wa mwaka wa kwanza kuwa
sadaka ya dhambi. 28 Naye
kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya huyo mtu akosaye, atakapofanya dhambi
pasipo kujua, mbele za Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye
atasemehewa. 29 Mtakuwa na
sheria moja kwa huyo afanyaye neno lo lote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa
kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao.
Dhabihu
hii ya kondoo jike imetimizwa katika
Kristo akiwa kama kichwa cha Kanisa. Dhabihu ambayo ni Kanisa iliwakilishwa na kondoo jike (ambaye ni Mtamba Mwekundu)
ni mmoja ya dhabihu chache za wanyama wakike zilizowahi kutolewa. Kwa hiyo,
utoaji wa dhabihu ulifanyika uwezekane na Kristo na Wana wa Mungu wakiwa ni
Malaika na wateule katika siku ya kwanza ya juma la mwezi wa Kwanza.
Dhabihu
ya Pasaka ilimaanisha na uumbaji wa vitu, ambaye hatimaye aliruhusiwa mteule
aletwe Kanisani wachukue mahala pao kwenye mchakato endelevu wa dhabihu ulio
kwenye Mpango wa Mungu.
Pasaka
ilikuwa kwene juma la pili la mwezi wa Kwanza. Kabla hatujaangalia maana yake tutatathmini
Mpango mzima.
Juma la
uumbaji kama Mpango wa Wokovu
Tunaweza kuona kutokana na utaratibu huu utekelezaji
kwetu katika siku za mwisho. Sabato ya juma inatokana na juma la uumbaji. Kwa
hiyo tunaweza kutendea kazi muundo huu wote na kuona kwamba Mpango wa Mungu
umeonyeshwa kwenye mchakato wa juma la uumbaji.
2Petro 3:8 inasema kwamba siku moja ni sawa na miaka
elfu, na vivyohivyo miaka elfu ni sawa na siku moja.
2Petro 3:8 8 Lakini, wapenzi,
msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka
elfu ni kama siku moja.
Miaka elfu sita imewekwa kwa mwanadamu chini ya Malaika
walioasi.
2Wakorintho
4:3-4 Lakini
ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; 4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao
wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake
Mungu.
Waefeso 6:12 Kwa maana kushindana
kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya
wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Miaka elfu moja imewekwa kwa ajili ya Siku ya Bwana chini ya Kristo na wateule
wake (Ufunuo 20:4).
Ufunuo 20:4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake,
nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya
ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule
mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso
zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka
elfu.
Kwa hiyo,
juma lenye siku saba linaonyesha Mpango wa Mungu wa wokovu. hata kuna
mwingiliano wa kimahusiano na mwezi na sikukuu kama zikiangukia kila mwezi, ambao
unaonyesha marudio wa harakati au sughuli za Mungu, zilizoonyeshwa pia kwenye matumizi
ya wiki kama zinavyoonekana kwenye kila sikukuu kwenye mwezi husika.
Tungeweza kuliona juma la uumbaji kama kipindi cha miaka
elfu saba, lakini kimatendo ni Pasaka tunapenda kuijua mchakato wa harakati
zilizotangulia. Juma lenyewe linalitangulia juma ambalo linaloangukia Pasaka,
inayoashiria uumbaji wa Malaika au Viumbe wa mbinguni, ambao kimsigi ni uumbaji
wa vitu vinavyoonekana na ni muhimu kwa utakaso wa viumbe tunavyoviona. Siku ya
Saba ya mwezi wa Kwanza ni siku maalumu kwa utakaso wa |Viumbe wote na ndiyo
maana hasa inayoongelewa kwenye Waebrania 2:11. Masihi alikusudiwa ama kulengwa
kwa matendo yake kwenye juma la pili la kuutakasa ulimwengu wote, kwa namna zote
mbili, yaani kimwili na kiroho. Utakaso wa siku ya Saba ni ishara ya utaratibu
wa kiroho wa Malaika na wateule katika harakati kama zinavyohusiana na mambo ya
kimwili.
Waebrania 2:11 Maana yeye atakasaye na
hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita
ndugu zake;
Kaliuawa siku ya Jumatano alasiri la juma tulijualo la uumbaji. Siku ya 14 ya
mwezi wa Kwanza ni mwisho wa juma la pili la mwezi Nisani lililoanzia siku ya
nane ya mwezi. Kwa hiyo, siku ya tisa ilikuwa ni siku ya kwanza ya juma la pili
la mchakato wa uumbaji. Kwa hiyo, dhabihu ya Pasaka inafanyika kwenye juma la pili,
na kwa kweli inawakilisha mapumziko ya Sabato ya juma la pili, ambaye ni Kristo.
Mwaka
halisia wa Pasaka, hata hivyo, ulikuwa siku ya Jumatano na ashirio hapa lina
maana nyingine, ambao unaweza pia kumaanisha na juma la uumbaji. (Kwenye jambo
hili tunaweza kuhitaji siku ya kwanza ya mwezi kuwa iliangukia siku ya
Alhamisi. Tungeweza kujionea hilo kwa maana ya mfano ulioachwa.)
Siku ya kutolewa sadaka Kristo kwa hiyo inaweza kuwa
ilitajwa kwamba ilikuwa mwishoni mwa siku ya kmilenia ya 4. Kama tutaichuklia
hii kuwa ni siku ya 14 ya Nisan, basi alichaguliwa kabla ya siku ya kwanza ya
juma (ambayo ni siku ya 10 ya Nisan) – kwa kuhesabu kuanzia nyuma tangu
Jumatano ya siku ya 14, ndipo tunaipata siku ya 10, ambayo ilikuwa ni Sabato na
siku iliyotangulia kuanza kwa juma la pili la uumbaji. Kwa hiyo Masihi
alitangulia juma lililokuwepo, akachaguliwa na kuwekwa kando kiroho na kuwa pia
kwenye uumbaji wa kiroho.
Kutoka 12:3-6
Semeni na
mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa
mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba
moja;
4 na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa
mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae
mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila
mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo.
5 Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja;
mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.
6 Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule;
na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni.
1Petro 1:20 inaongelea mwonekano wa Masihi kwetu katikA Siku
za Mwisho.
1Petro
1:20 Naye
amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini
alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu;
Siku ya kumi ya mwezi Nisan kwenye maelezo haya inatokea
kuwa tu kwenye juma la pili kwenye mchakato wenyewe ulivyokuwa katika mwaka 30
BK ambao unaashiria kuwa ulipangwa au kukusudiwa mapema kabla ya Imani na
wateule kabla hawajajitoa kwenye ulimwengu huu unaoonekana.
Kristo ndiye mwanzilishi na mwendelezaji, mlengwa wa
wokovu wetu (Waebrania 5:9; 6:20; 12:2).
Waebrania 5:9
naye alipokwisha
kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;
Waebrania 6:20 alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu,
amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.
Waebrania 12:2
tukimtazama
Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya
furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye
ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu
Tunajua pia kwamba ufufuko wa wote kutoka kwa wafu
utatokea katika Siku ya Mwisho.
Yohana 6:40 Kwa kuwa mapenzi yake
Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na
uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Yohana 6:44 Hakuna mtu awezaye kuja
kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Yohana 6:54 Aulaye mwili wangu na
kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho
Yohana 11:21-26
Basi Martha
akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. 22 Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba
Mungu, Mungu atakupa. 23 Yesu akamwambia, Ndugu
yako atafufuka. 24 Martha akamwambia, Najua
ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. 25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa,
atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na
kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
Kutokana na Maandiko haya Matakatifu tunauona ufufuko utafanyika
Siku ya Mwisho ambao una maana lengwa yake na Sikukuu ya mwezi wa Saba.
Juma lililotokea kifo cha Kristo katika mwaka wa 30 BK – ambalo
kusulibiwa kwake kulifanyika siku ya Jumatano – linaonyesha mfano kivuli huu
muhimu kama tunavyoutendea kazi kwenye juma la uumbaji.
Tunaona kwamba Hekalu linasafishwa siku ya Kwanza na
utakaso unafanywa siku ya Saba yake. Katika juma la kusulibiwa kwake ndipo Kristo
alisafisha Hekalu yeye mwenyewe kutoka siku ya kwanza ya juma au Jumapili,
kuliko kufanya hivyo siku ya Kwanza ya mwezi kama ilivyotakiwa ifanyike kwenye
Hekalu kwa mujibu wa Torati.
Kwa hiyo tunaona shinikizo kubwa kufanyika kwenye juma la
kusulibiwa kwake likionyesha kuwa ni ishara ya Mpango wa Wokovu wa wanadamu na
utaratibu uliodhahiri. Harakati hizi tena zinatanguliwa na kitendo chake cha usafishaji
wa Hekalu katika siku ya Kwanza ya juma (Jumapili) kama Mungu alivyoifanya upya
tena Dunia kwene milenia ya kwanza.
Mathayo
21:10-14 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani
huyu? 11 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya. 12
Yesu akaingia ndani ya hekalu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua
hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza
njiwa; 13 akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali
ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi. 14 Na vipofu na viwete wakamwendea
mle hekaluni, akawaponya
Kristo alikufa siku ya Jumatano, kama ilivyoelezewa kwa
kina kwenye jarida la Majira ya Kusulibiwa na Kufufuka (Na. 159) [Timing of the Crucifixion and the
Resurrection (No. 159)]:
Ili afanane na Ishara ya nabii Yona, alishinda siku tatu
usiku na mchana kwenye tumbo la Nchi (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya
Ujenzi Upya wa Hekalu (Na. 13) [The Sign of Jonah and the History of the
Reconstruction of the Temple (No. 13)]. Ufufuko wake ilifanyika Siku ya Mwisho,
Sabato ya juma.
Mathayo 28:1 Hata sabato ilipokwisha,
ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa
pili, walikwenda kulitazama kaburi.
Mathayo
28:5-6 Malaika
akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa
mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa. 6
Hayupo
hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.
(Angalia Sehemu ya Nyongeza ili upate kuelewa kikamilifu
kuhusu mlolongo wa matukio yaliyotokea juma hili.)
Pia kumbuka kwamba uingiaji huu wa shangwe mjini
Yerusalemu ulifanyika katika Sabato iliyopita au Jumamosi ya siku ya 10
(Mwanakondoo aliyechaguliwa hata kabla ya kuekwa kwa misingi ya dunia!).
Kulichukua hili kwenye mtazamo halisi wa juma la uumbaji
ya siku kuwa ni taswira ya miaka elfu, tunaona kwamba Jumatano, Alhamisi,
Ijumaa na Jumamosi ni Siku za Mwisho.
Sabato ya Jumamosi ni taswira au kivuli cha “pumziko la millennia”. Siku hii ya
Mwisho pia ni siku ya ufufuo, ambao pia umefanyika mwishoni mwa siku hii ya
mapumziko.
Milolongo ya
siku Saba katika Mpango wa Wokovu
Tunona kuwa kuna idadi ya milolongo ya siku ya saba
kutoka kwenye tukio la kusafisha lililofanyika katika siku ya kwanza ya juma
hadi kufikia Pasaka ya juma linalofuatia. Hii kwa hiyo ilifuatiwa na Idi ya
Mikate Isiyo na Chachu, ambayo iansiku saba.
Sikukuu ya Mjuma au Pentekoste (hesabu ya siku hamsini)
inafikia baada ya Sabato saba. Kuna aina tatu ya mavuno ambayo tunatakiwa au
kuamriwa tukajihudhurishe mbele za Bwana.
Vipindi
vihi vitatu vya mavuno ya Mungu tumeamriwa kukusanyika pamoja mbele za Mungu.
Kila vuno moja linawakilisha mavuno ya kiroho ya Mungu kwenye Mpango wa Wokovu
(soma Kumbukumbu la Torati 16:16-17).
Kumbukumbu la
Torati 16:16-17 Mara tatu kwa mwaka na
watokee wanawaume wako wote mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua;
katika sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, na katika sikukuu ya majuma, na
katika sikukuu ya vibanda; wala wasitokee mbele za Bwana mikono mitupu. 17 Kila mtu na atoe
kama awezavyo, kwa kadiri ya baraka ya Bwana, Mungu wako, alivyokupa.
Pasaka/Mikate
Isiyo na Chachu: majira ya kwanza ya mavuno
Sasa tutajoea kuhusu Idi ya Mikae Isiyo na Chachu kwa
mtazamo au mlinganisho wa mavuno makuu matatu ya Mungu. Mavuno haya
yanashabihiana na Krisro, Kanisa na ufufuo wa pumziko la wanadamu litakalofanyika
mwishoni.
1Wakorintho
15:22-25 Kwa
kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote
watahuishwa. 23 Lakini kila mmoja mahali
pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. 24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake;
atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote
chini ya miguu yake.
Maadhimiso ya Mikate isiyo na Chachu ni majira ya mavuno
ya kwanza au malimbuko kati ya matatu. Pentekoste ni ya Pili na Vibanda ni ya
tatu (Kutoka 34:18-23). Kwa hiyo, inafuatiwa kwamba majira haya ya mavuno ya
kwanza yanaashiria taswira ya majira ya kwanza ya Kristo – ambaye ni wa kwanza
katik ya malimbuko ya mavuno ya shayiri.
Tutaiangalia idi ya Mikate Isiyo na Chachu kwa mtazamo wa
taswira yake kwa majukumu au kazi za Kristo katika wokovu wa wanadamu.
Juma la Mikate Isiyo na Chachu kadhalika linamuonyesha
Kristo aliyeuachinjwa kabla ya
kuanza kwa siku ya kwanza.
Kutoka 12:6 Nanyi mtamweka hata siku
ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli
watamchinja jioni.
Kuna matukio muhimu nay a maana matatu yanayoonyeshwa au
kuilengwa kwenye siku za Mikate Isiyo na Chachu. Siku ya kwanza inaonyesha
utimilifu wa kazi ya Kristo akiwa kama dhabihu safi isiyo na dhambi na ni
Kuhani Mkuu aliyekuwa anajiandaa kuingia katika Patgakatifu pa Patakatifu mara
moja tu kwa ajili ya wote na kwa damu yake mwe nyewe na sio ya mafahali ya
ng’omba. Mganda wa Kutikiswa unaonyesha ukubalifu wa Mungu wa dhabihu ya Kristo
na Kristo anapokea mamlaka yake ya kutawala amoja na ukuhani mpya.
Danieli
7:13-14 Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye
mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa
siku, wakamleta karibu naye. 14 Naye akapewa mamlaka, na
utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote,
wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na
ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Ufunuo 1:6 na kutufanya kuwa ufalme,
na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele
na milele. Amina.
Siku ya mwisho ya Mikate Isiyo na Chachu inaashiria kazi
ya Kristo katika Siku za Mwisho akiwa kama Mfalme.
Kama tutalilinganisha juma la Mikate Isiyo na Chachu na
juma lenyewe lilivyokuwa mwaka 30 BK, siku ya kwanza inaionyesha kazi ya
Kristo kwenye juma la uumbaji (Waebrania 1:2). Mganda wa Kutikiswa unaonyesha
jukumu la Kristo kama mwokozi aliyekubaliwa na Kuhani Mkuu aliyechaguliwa na
Mungu katika siku ya nne (Jumapili ya Mganda wa Kutikiswa), inayotokea kwenye
Jumatano ya juma la uumbaji, na kwa hiyo ni siku ya mwisho ya Mikate Isiyo na
Chachu ambayo pia ni mapumziko.
Siku ya mwisho ni Sabato kwa kuwa kazi ya Kristo katika
kipindi cha Milenia (au mwaka wa elfu moja wa “juma la uumbaji”, Sabato). Hii
ni kazi yake itakavyokuwa katika Siku ya Bwana. Anakuja kama Mfalme katika Ujio
wake wa pili wakati dunia itakapopata pumziko.
Siku hizi saba zinajulikana kwa tendo la kuondoa chachu
ambayo inaonysha uondoaji wa dhambi maishani mwetu. Kristo aliishi maisha
yasiyo na dhambi. Akiwa ni dhabihu isiyo na dhambi aliweza kupigilia tangazo la
msamaha wa madeni au chierographon kwenye stauros au mtini.
Kutokana na tukio hili, basi tumeokolewa.
Mkate Usio na Chachu unaonyesha ukombozi wetu kutoka
dhambini, kama inavyoonyesha Kutoka 13:3-9, na tendo hili la kuiondoa dhambi ni
endelevu kutoka maishani mwetu. Sikukuu ya Mikate Isiyo na Chachu ina kiwango
kingine cha kwanza cha maana ikiwa kama mavuno
ya kwanza ya Mungu. Mkate Usio na Chachu ni majira ya mavuno ya ya Kristo.
Haimaanishi mavuno ya Kanisa bali zaidi sana inaonyesha harakati za Kristo kwa
kipindi chote na matayarisho ya Kanisa kwa mavuno yake. Na kwa hiyo kimuundo
inatofautiana na Sikukuu ya Vibanda ambayo kwamba siku ya nane na siyo ya saba
inakuwa ni Siku Takatifu, ambavyo siku hii ya mwisho inaonyesha au inalenga
hitimisho la mpango aliouweka Mungu baada ya Milenia. Kwa hiyo, siku ya mwisho
ya siku hizi saba za Vibanda sio Siku Takatifu.
Kuna
mzunguko ndani ya wateule kuanzia utakaso wa Watakatifu hadi kipindi cha
maadhimisho ya Pasaka na Mikate Isiyo na Chachu, ambacho kinatumiwa kwa kuongoa
chachu na hamira kwa wale walioitwa na kuchagulia tangu mwanzo ili kuwaandaa
kumpokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Siku hamsini zinaashiria maisha yao
tangia ukubwa wao tangu wakiwa na umri wa miaka ishirini. Wanapoongoka,
wanachukua mahala pao kwenye Utakaso wa kiroho wakiwa kama Wana wa Mungu ili
wafundishe na kulitakasa kundi linguine la wale walioitwa watoke kwa Mpango wa
Mungu.
Pentekoste au
Idi ya Majuma: majira ya mavuno ya pili
Kuna Sabato saba za juma kuhesabiwa tangu siku ya Mganda
wa Kutikiswa, na siku moja baada ya Sre are seven weekly Sabbathabato ya saba
ambapo kunaadhimishwa Pentekoste. Mauma saba kyelekea Pentekoste yana idadi
kadhaa ya matukio na mambo ya kuyatenda.
Yanaweza kuonekana kama ni zama ya saba ya Kanisa
inayoelekea kwenye pumziko lijalo kwa mtindo endelevu.
Waebrania 4:3
Maana sisi
tulioamini tunaingia katika raha ile; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa
hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu:
Waebrania 4:10 Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake
amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi
zake
Inaweza pia kuonekana kuhusiana na kipindi cha Yubile,
kama tuonavyo hapo chini.
Tendo la kuhesabu linaanzia tangu siku ya Mganda wa
Kutikiswa. Kuelekea hadi P entekoste ni moja ya uchaguzi na kuachana na ukuhani
mpya ulio chini ya Kuhani Mkuu aliye mfano wa Melkizedeki (sawa na Waebrania
5:6 to 7:21).
Waebrania 6:20
…mtangulizi
wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki
Mganda wa Kutikiswa unaashiria kupaa kwa Kristo na ndenda
kwenye chumba chenye Kiti cha Enzi cha Mungu ili akubalike baada ya kufufuka
kwake toka kwa wafu, kama inavyoonekana kwenye Danieli 7:13-14 na Yohana 20:17.
Yohana 20:17 Yesu akamwambia.
Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu
ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu
naye ni Mungu wenu.
Kuna miaka saba ya Sabato, na hatimaye, mwaka unaofuatia
baada ya huu wa saba wa Sabato, unakuwa ni mwaka wa Yubile. Kwa hiyo, kuna
uhusiano kati ya Pentekoste na mwaka wa Yubile na huku miundo yote miwili ikiwa
ni sawa. Muundo wa Yubile pia unaakisi maisha ya mtu mkamilifu aliye na miaka
hamsini tangia utuuzima wake hadi kwenye umri wa miaka sabini na “mapumziko” yale
yanatokutikana kwa Mungu. Waisraeli walizishika Pentekoste arobaini jangwani,
ambayo pia inaonyesha upana wa matukio ya Mungu kwa Masihi. Kuna mambo ya
kujifunza sisi. Sisi nasi tupo “jangwani” kwa kipindi cha Yubile arobaini
(miaka 2,000) au Siku za Mwisho (Alhamisi na Ijumaa ya juma la uumbaji).
Pentekoste inaakisi kuwa kwetu sisi malimbuko au matunda yavunwayo kwanza na
kuwa kwetu “tuliomwagiliwa na kurutubishwa kwa maji” au kuongozwa na Roho
Mtakatifu.
Yeremia 5:24 Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche Bwana,
Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na
kutuwekea juma za mavuno zilizoamriwa.
Majuma
yaliyowekwa ya mavuno kama yalivyoelezewa hapa ni
majuma saba ya Pentekoste. Kwahiyo, kipindi cha Mganda wa Kutikiswa hadi Pentekoste
kimetengwa na watu wa Mungu.
Pentekoste ni mavuno
ya pili ya Mungu na wakati mwingine inatajwa kama ni Sikukuu ya Mavuno kama
kwenye Kutoka 23:16 inavyoonyeshwa.
Kutoka 23:16 tena, sikukuu ya mavuno,
hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani; tena, sikukuu ya kukusanya,
mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani.
Inaonyesha mavuno endelevu ya kiroho na kuhukumiwa kwetu kwa
kiwango endelevu pia (mikate ya kutikiswa). Inaitwa mavuno ya malimuko, kwa hiyo kuonyesha kuwa ni mavuno ya mwisho. Mikate
ya kutikiswa siku ya Pentekoste inatiwa chachu.
Chachu ya kale ya uovu na dhambi inawekwa kwenye chachu
mpya ya Roho Mtakatifu anayefanya kazi kwenye mambo mawili ya Kristo na kwenye
Agano la Mungu. Maisha yetu yanamchanganyiko wa dhambi, lakini hatupo kwenye
utumwa tena. Sadaka inayotolewa siku ya Pentekoste inaonyesha hitaji kwa ajili
ya dhabihu ya dhambi ambayo ilitolewa kwa ajili yetu kupitia kwa Yesu Kristo
ambaye aliitoa dhabihu ile mara moja tu na kwa ajili ya wote kwenye Pasaka. Kwa
hiyo, tunatarajia mavuno yetu kwenye Pentekoste iwezekane kwa mavuno ya Kristo
kwenye Pasaka. Sadaka ya dhambi inaashiria ondoleo la dhambi katika maisha yetu
kwa kiwango endelevu (sawa na jarida la Chachu
ya Kale na Mpya (NA. 106a) [The Old and the New Leaven (No. 106a)].
Mambo ya
Walawi 23:15-21 Nanyi mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya Sabato, tangu siku hiyo
mliyouleta mganda wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia Sabato saba; 16 hata siku ya
pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea Bwana
sadaka ya unga mpya. 17 Mtatoa
katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili
za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa Bwana. 18 Nanyi, pamoja na
hiyo mikate, mtasongeza wana-kondoo saba, walio wakamilifu, wa mwaka wa kwanza,
na ng'ombe mume mmoja, na kondoo waume wawili; watakuwa sadaka ya kuteketezwa
kwa Bwana, pamoja na sadaka yao ya unga, na sadaka zao za kinywaji, sadaka ya
harufu ya kupendeza iliyosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. 19 Nanyi mtasongeza
mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wana-kondoo wawili waume wa mwaka wa
kwanza kuwa dhabihu ya sadaka za amani. 20 Kisha kuhani atawatikisa pamoja na
hiyo mikate ya malimbuko kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana, pamoja na
wale wana-kondoo wawili; watakuwa watakatifu kwa Bwana, wawe wa huyo kuhani. 21 Nanyi mtapiga
mbiu siku iyo hiyo; kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; msifanye kazi yo yote
ya utumishi; ni amri ya milele katika makao yenu yote, katika vizazi vyenu'
Kumbuka kuwa kuna mbuzi wa dhabihu ya dhambi anayeonyeshwa
kwenye aya ya 19. Pia kumbuka kwamba Mganda wa Kutikiswa hauhusiani na matoleo
ya sadaka ya dhambi, kwa kuwa unaashiria taswira ya Kristo aliyeishi maisha
yasiyo na dhambi.
Mambo ya
Walawi 23:9-14 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 10 Nena
na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi
niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa
malimbuko ya mavuno yenu; 11 naye atautikisa
mganda mbele za Bwana ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada
ya Sabato kuhani atautikisa. 12 Na siku hiyo
mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa
kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana. 13 Na
sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba
uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto kuwa
harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini.
14 Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata
siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni
amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote
Tukiwa kama waumini tuliobatizwa katika mwili wa Yesu Kristo,
tunahukumiwa kwa yale tunayoyatenda.
Ayubu 34:21-23
Kwani macho
yake ya juu ya njia za mtu, Naye huiona miendo yake yote. 22 Hapana weusi, wala hilo giza tupu, Wawezapo kujificha
watendao udhalimu. 23 Kwani yeye hana haja ya
kumfikiria mtu zaidi, ili aende mbele za Mungu ahukumiwe.
Pentekoste inaashiria hii kuwa ni mikate ya kutikiswa,
ambayo kwa matendo Israeli waliishika mata arobaini walipokuwa wakitangatanga
jangwani. Kwa kuiunganisha hii kwenye Yubile kama ilivyosemwa kabla inaonyesha
hukumu yetu kwa Mungu kwa msingi endelevu kwa kipindi cha miaka elfu mbili. Na
mtume Petro alikuwa na la kusema kama hivi.
1Petro 4:17 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika
nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu
utakuwaje?
Pentekoste ya kwanza ya Waisraeli ilikuwa wakati
walipoipokea Torati pale Sinai. Pentekoste ya kwanza ya Kanisa la Agano Jipya
ilikuwa wakati walipopokea Sheris iliyoandikwa ndani ya mioyo yao, kumwagiwa
kwao na Roho wa Mungu.
Waebrania 8:10 10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli
Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na
katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu
wangu.
Matendo 2:17-21 Itakuwa siku
za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na
binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota
ndoto. 18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi
wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri. 19 Nami
nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na
mvuke wa moshi. 20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa
damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri. 21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.
Kwenye Matendo 2:18 inasama “siku” (katika uwingi) na kwenye
aya ya 17 inataja kuwa Siku za Bwana. Aya ya 20 inaweka siku hizi kabla ya siku ya mwisho: “...
siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana”. Kwa hiyo, tunaziona siku mbili
(Alhamisi na Ijumaa ya juma la uumbaji) au miaka elfu mbili hadi kufikia Milenia.
Dhana nzima kuhusu Siku za Bwana imefafanuliwa kwa kina kwenye jarida la Siku ya Bwana na Siku za Mwisho (Na. 192) [The Day of the
Lord and the Last Days (No. 192)].
Kuna Sabato saba kamili tangu Mganda wa Kutikiswa
(Kristo) hadi kwenye mavuno (Pentekoste) ya wateule. Pia inaeleweka kwamba
kuwepo kwa zama ya Makanisa la saba kuliashiriwa na Makanisa saba ya Ufunuo
sura za 2 na 3, na yanapaswa kukamilika kabla ya mavuno.
Maana ya
baragumu
Baragumu au Tarumbeta zilitumika katika kuwaonya Israeli
wakati wa vita. Zilipigwa pia kwenye Sikukuu, Miandamo ya Mwezi na wakati wa
kutoa sadaka ya kuteketezwa na walipokuwa wanatoza sadaka za amani. Zilitumika
kwa kupigwa ili kuwakusanya viongozi au watu pamoja na kuwapa maelekezo ya
jinsi watakavyoondoka na kusafiri Israeli walipokuwa jangwani.
Hesabu 10:2-10
Jifanyie
tarumbeta mbili za fedha; utazifanya za kazi ya ufuzi; nawe utazitumia kwa
kuwaita mkutano wakutane, na kwa kusafiri kwao yale makambi. 3 Na hapo watakapozipiga hizo tarumbeta, mkutano wote
utakukutanikia wewe, hapo mlangoni pa hema ya kukutania. 4 Nao wakipiga tarumbeta moja tu ndipo wakuu, walio vichwa
vya maelfu ya Israeli, watakukutanikia wewe 5 Tena hapo mtakapopiga sauti ya kugutusha sana, marago yaliyoko upande wa
mashariki yatasafiri. Tena hapo mtakapopiga sauti ya kugutusha ya pili, marago
yaliyoko upande wa kusini watasafiri; 6
watapiga
sauti ya kugutusha kwa ajili ya safari zao. 7 Lakini mkutano utakapokutanishwa pamoja mtapiga, lakini hamtapiga sauti ya
kugutusha. 8 Wana wa Haruni, makuhani,
ndio watakaopiga hizo tarumbeta; nazo zitakuwa kwenu ni amri ya milele katika
vizazi vyenu vyote. 9 Tena hapo mtakapokwenda
kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo
mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za Bwana,
Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu. 10 Tena katika siku ya furaha yenu, na katika sikukuu zenu zilizoamriwa, na
katika kuandama miezi kwenu, mtapiga hizo tarumbeta juu ya sadaka zenu za
kuteketezwa, na juu ya dhabihu za sadaka zenu za amani; nazo zitakuwa kwenu ni
ukumbusho mbele za Mungu wenu; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Hapa kulikuwa na baragumu mbili. Baragumu iliyopigwa kwa
mlio mtulivu ilipigwa kuwaita na kukusanya viongozi. Ya pili ilitumika kuwaita
na kuwakusanya wote. Baragumu zikipigwa kwa milio ya uwingi zinahusiana na
kuwaita wateule na kwa taifa.
Kitabu cha Ufunuo kinatuambia kuna baragumu saba.
Baragumu saba zina mihuri wa saba. Mhuri
unahusiana na sehemu ya gombo la maandiko, kwenye baragumu hizi ni ufunuo.
Baragumu ya saba inafanya kurudi kwa Kristo akiwa kama Mfalme na kusanyiko la
wateule. Baragumu
ya saba inafunuka na kuwa kitasa cha saba cha ghadhabu ya Mungu. Kwa hiyo, Siku
ya Baragumu inaashiria kipindi fulani na sio ni tukio tu. Tunapotazama kuhusu
kutwaliwa kwa Yeriko, Kitabu cha Yoshua kinaonyesha ashirio la jambo hili pia.
Waliuzunguka mji mara moja na kupiga baragumu kila siku kwa siku sita na katika
siku ya saba walitembea wakiuzunguka mji mara saba na wakapiga baragumu kila
mzunguko mmoja. Kisha, wakati walipokuwa wanazipiga baragumu mara ya saba na
huku wakuzunguka, watu walipiga kelele kwa nguvu.
Yoshua 6:1-20
Basi Yeriko
ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka
wala hapana mtu aliyeingia. 2
Bwana
akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake,
na mashujaa wake. 3 Nanyi mtauzunguka mji
huu, watu wote wa vita, mkiuzunguka mji mara moja. Fanya hivi siku sita. 4 Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za
kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba,
nao makuhani watapiga tarumbeta zao. 5
Kisha
itakuwa watakapopiga hizo pembe za kondoo waume kwa nguvu, nanyi mtakaposikia
sauti ya tarumbeta, watu wote watapiga kelele kwa sauti kuu; na ukuta wa mji utaanguka
chini pale pale, na hao watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele kukabili. 6 Bali Yoshua, mwana wa Nuni, akawaita makuhani,
akawaambia, Lichukueni sanduku la agano, tena makuhani saba na wachukue
tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Bwana. 7 Naye akawaambia watu, Piteni mbele, mkauzunguke mji, na
hao watu wenye silaha na watangulie mbele ya sanduku la Bwana. 8 Basi ikawa Yoshua alipokwisha kusema na watu, wale
makuhani saba, wenye kuzichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele
za Bwana, wakatangulia, wakazipiga hizo tarumbeta; nalo sanduku la agano la
Bwana likawafuata. 9 Wale watu wenye silaha
walikwenda mbele ya hao makuhani waliozipiga tarumbeta, na wale waliokuwa nyuma
wakalifuata hilo sanduku; makuhani wakizipiga tarumbeta walipokuwa wakienda. 10 Yoshua akawaamuru watu, akasema Msipige kelele, wala
sauti zenu zisisikiwe, wala neno lo lote lisitoke kinywani mwenu, hata siku ile
nitakapowaamuru kupiga kelele, ndipo mtakapopiga kelele. 11 Basi akalipeleka sanduku la Bwana liuzunguke huo mji,
likauzunguka mara moja, kisha wakaenda kambini wakakaa kambini. 12 Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao makuhani
wakalichukua sanduku la Bwana.13
Na
wale makuhani saba wakazichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele
ya sanduku la Bwana, wakaendelea wakazipiga tarumbeta; nao watu wenye silaha
wakawatangulia, na hao waliokuwa nyuma wakalifuata sanduku la Bwana; makuhani
wakizipiga tarumbeta walipokuwa wakienda. 14 Siku ya pili wakauzunguka mji mara moja, wakarejea kambini; ndivyo
walivyofanya siku sita. 15
Ikawa
siku ya saba wakaondoka asubuhi na mapema wakati wa mapambazuko, wakauzunguka
mji vivyo hivyo mara saba; ila siku hiyo waliuzunguka huo mji mara saba. 16 Hata mara ya saba makuhani walipozipiga tarumbeta, Yoshua
akawaambia watu, Pigeni kelele; kwa maana Bwana amewapeni mji huu. 17 Na mji huu utakuwa wakfu kwa Bwana, mji wenyewe na vitu
vyote vilivyomo; isipokuwa Rahabu, yule kahaba, ataishi, yeye na watu wote
walio pamoja naye nyumbani, kwa sababu aliwaficha hao wapelelezi tuliowatuma. 18 Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu;
msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo
mtayafanya matuo ya Israeli kuwa yamelaaniwa na kuyafadhaisha.19 Lakini fedha yote, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na
chuma, ni vitakatifu kwa Bwana; vitaletwa katika hazina ya Bwana. 20 Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga
tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia sauti ya tarumbeta hao watu
wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka nchi kabisa,
hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea kukabili
mbele; wakautwaa huo mji.
Kuna uhusiano wa wazi hapa kwenye upigaji wa baragumu ya
saba ya Ufunuo 11:15,18 na katika baragumu au parapanda ya mwisho na upigaji wa
Malaika Mkuu.
1Wathesalonike
4:16 Kwa
sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya
malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa
kwanza.
1Wakorintho
15:51-52 Angalieni,
nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda
ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu,
nasi tutabadilika.
Baragumu zilipigwa kwa siku saba zote za kipindi cha
kuizunguka Yeriko. Tena tunaweza kuhusianisha hii hadi nyuma kwenye juma la
uumbaji. Katika kutumia mlinganisho huu, ndipo tunauona mzingito wa Yeriko ukionyesha
Mpango wa Mungu wa ukombozi ya sayari hii na maonyo kupitia kipindi cha miaka
elfu. Sikm ya saba ni ashirio la kuja au kurudi kwa Masihi na kukomeshwa au
kuangamizwa kwa Dunia hii na mifumo yhake yote. Masihi atafanya hivi kipindi
atakapokuja mwanzoni mwa Milenia. Hii inahusianishwa na ujio wa Kiumbe wa aina
ya malaika mtakatifu mapema katika siku ya saba ya mzingiro wa mji wa Yeriko.
Ikumbukwe kwamba Kristo anaonekana kuwa alikuwepo akiwa kama Jemadari wa jeshi
la BWANA”.
Yoshua
5:13-14 13 Ikawa hapo Yoshua
alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama,
mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi
mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa
adui zetu? 14 Akasema, La, lakini
nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshua akapomoka kiusouso hata
nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?
Kumbuka na kujua kwamba Kristo amekwisha kuja (aya
ya 14). Pia kumbuka kuwa kitendo cha kumuokoa na kumlinda Rahabu wakati huu, alilindwa
na kunusurika kwa ajili ya kamba nyukundu aliyoiweka dirishani kwake.
Yoshua
2:14-18 Wale
wanaume wakamwambia, Uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari
ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati Bwana atakapotupa nchi hii,
tutakutendea kwa ihisani na uaminifu. 15
Ndipo
akawashusha kwa kamba dirishani, maana nyumba yake ilikuwa katika ukuta wa mji;
naye alikaa ukutani. 16 Akawaambia, Enendeni zenu
mlimani, wale wanaowafuatia wasije wakawapata; mkajifiche huko siku tatu hata
wao wanaowafuatia watakaporudi; kisha enendeni zenu. 17 Wale wanaume wakamwambia, Sisi tunataka tusiwe na hatia kwa ajili ya kiapo
hiki ulichotuapisha. 18 Angalia, tutakapoingia
katika nchi hii, funga kamba hii nyekundu katika dirisha hili ulilotutelemshia;
nawe uwakusanye kwako nyumbani mwako, baba yako, na mama yako, na ndugu zako,
na watu wote wa nyumba ya baba yako.
Yoshua
6:23-25 Basi
wale vijana wapelelezi wakaingia, wakamtoa Rahabu, na baba yake, na mama yake,
na ndugu zake, na vitu vyote walivyokuwa navyo, wakawatoa na jamaa zake wote
pia; wakawaweka nje ya matuo ya Israeli.
24 Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote
vilivyokuwa ndani yake; bali fedha, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na vya
chuma, wakavitia katika hazina ya nyumba ya Bwana. 25 Lakini Yoshua akamhifadhi Rahabu, yule kahaba, na watu wa nyumba ya baba
yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo; naye akakaa kati ya Israeli hata leo; kwa
sababu aliwaficha wale wajumbe aliowatuma Yoshua ili kuupeleleza mji wa Yeriko.
Hadithi hii inamuonyesha kama Kanisa katika siku za
mwisho. Kanisa litalindwa kwa sababu ya dhabihu iliyotolewa ya Mwanakondoo –
Kristo. Kamba nyekundu inawakilisha damu yake kama ilivyotumika huko Misri
kwenye milango na miimo ya milango. Hapa sio mahali salama, akama Rahabu
alivyokuwa mahala pabaya sana alivyokaa – ukutani. Pia inaashiria ukweli kwamba
emelindwa na kuwaokoa wale waliokuwa karibu naye wakati wa kuangamizwa na
kupinduliwa kwa mataifa, kwa ajili ya uhusiano wake na Jeshi la Bwana kwa imani
aliyokuwa nayo. Habari hii yote imeelezewa kwa kina kwenye jarida la Kuanguka kwa Yeriko (Na. 145) [The Fall of Jericho (No.
142)].
Mchakato
huu wote ilifanyika kipindi chote cha Pasaka. Tangu siku ya kwanza ya Sikukuu
hii walikula mazao ya nchi mpya ambayo ui kuhifadhi nafaka za mavuno ya zamani.
Mana ilikoma na hawakuendelea tena kuitegemea hii mana huko jangwani na
waliweza kuingilia kati mambo yao wenyewe kwenye Torati ya Mungu na imani.
Kama ilivyoelezwa hapo juu, baragumu zililazimu kupigwa
kwenye Siku za Sikuu, Miandamo ya Mwezi, juu ya sadaka na kwenye sadaka za
kuteketezwa ikionysha hii kuwa ni sehemu ya huu utaratibu wa maonyo ya Mungu.
Zilitumika katika kuita na kuelekeza namna
ya kuenenda katika kambi ya watu wa Mungu (Hesabu 10:2). Uhusiano wa wazi na
wateule una kuonekana.
Kwa hiyo, baragumu zilivyotumika kwenye hadithi hii ya
biblia, zinaashiria Mpango wa Mungu kutoka kwenye mtazamo mwelekezo wa maonyo
ya Mungu yaliyotolewa kipindi cha zaidi ya miaka elfu sita. Mlolongo huu wa
mambo unakuwepo kwenye kipindi cha ujio wa Kristo pamoja na mkusanyiko wa
wateule wake atakapokuja. Hii itafuatiwa na kuangamizwa kwa mfumo wa dunia hii
ulioonyeshwa kama hasira ya Mungu kwenye vitasa saba au majipu saba makuu na
vita ya Siku Kubwa ya Mungu.
Ufunuo 11:15-19 Malaika wa saba akapiga
baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia
umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata
milele na milele. 16 Na wale wazee ishirini na
wanne waketio mbele za Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifulifuli,
wakamsujudia Mungu 17 wakisema, Tunakushukuru
wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza
wako ulio mkuu, na kumiliki. 18
Na
mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa
waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, na hao
walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi. 19 Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na
sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na
radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.
Kwa
hiyo, Siku ya Kwanza Takatifu ya mwezi wa saba inaitwa Siku ya Baragumu na
inawakilisha Kurudi kwa Masihi akiwa kama Mfalme Mshindi kuja kuyatiisha mataifa.
Kuna
uhusiano na Sikukuu za miezi ya Kwanza na Saba kama tutakavyoendlea kuelezea
hapo chini. Siku Takatifu inayofuatia kunayoielezea kwenye mlolongo huu ni Siku
ya Upatanisho.
Siku ya
Upatanisho
Mambo ya
Walawi 16:1-31 Bwana akasema na Musa, baada ya kufa kwa hao wana wawili wa Haruni,
walipokaribia mbele za Bwana, wakafa; 2
Bwana
akamwambia Musa, Sema na Haruni ndugu yako, kwamba asiingie wakati wo wote
katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu
ya sanduku, asije akafa; maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti
cha rehema. 3 Haruni ataingia katika
patakatifu na vitu hivi; ng'ombe mume mchanga kwa sadaka ya dhambi, na kondoo
mume kwa sadaka ya kuteketezwa. 4
Ataivaa
ile kanzu takatifu ya kitani, atakuwa na zile suruali za kitani mwilini mwake,
atafungwa ule mshipi wa kitani, naye atavaa ile kofia ya kitani; hayo ndiyo
mavazi matakatifu, naye ataoga mwili wake majini, na kuyavaa. 5 Kisha atatwaa mikononi mwa mkutano wa Waisraeli mbuzi
waume wawili, kwa sadaka ya dhambi; na kondoo mume kwa sadaka ya kuteketezwa.6 Na Haruni atamtoa yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye
kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake
mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake. 7
Kisha
atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za Bwana mlangoni pa hema ya
kukutania. 8 Na Haruni atapiga kura
juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya Bwana; na kura ya pili kwa
ajili ya Azazeli. 9 Na Haruni atamleta yule
mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Bwana, na kumtoa awe sadaka ya dhambi.
10 Bali yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya
Azazeli atawekwa hai mbele za Bwana ili kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka
jangwani kwa ajili ya Azazeli. 11
Na
Haruni atamsongeza ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake,
na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba
yake; naye atamchinja yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya
nafsi yake. 12 Kisha atatwaa chetezo
kilichojaa makaa ya moto yatokayo katika madhabahu iliyo mbele za Bwana, na
konzi mbili za uvumba mzuri uliopondwa sana, mikononi mwake, naye atauleta
ndani ya pazia. 13 Kisha atatia ule uvumba
juu ya moto mbele za Bwana, ili moshi wa ule uvumba ukisitiri kiti cha rehema
kilicho juu ya ushuhuda, asije akafa. 14
Kisha
atatwaa baadhi ya damu ya yule ng'ombe, na kuinyunyiza kwa kidole chake juu ya
kiti cha rehema upande wa mashariki; na mbele ya kiti cha rehema atainyunyiza
ile damu kwa kidole chake mara saba. 15
Kisha
atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta
damu yake ndani ya pazia, na kwa damu hiyo atafanya vile vile kama alivyofanya
kwa damu ya ng'ombe, na kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema, na mbele ya kiti
cha rehema, 16 naye atafanya upatanisho
kwa ajili ya mahali patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli,
na kwa sababu ya makosa yao, naam, kwa ajili ya dhambi zao zote; naye atafanya
vile vile kwa ajili ya hema ya kukutania, ikaayo pamoja nao katikati ya machafu
yao. 17 Wala hapatakuwa na mtu katika hema ya kukutania,
wakati aingiapo ili kufanya upatanisho katika patakatifu, hata atakapotoka nje,
baada ya kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya
nyumba yake, na kwa ajili ya mkutano wote wa Israeli. 18 Kisha atatoka na kuiendea madhabahu iliyo mbele za Bwana na kufanya
upatanisho kwa ajili yake; atatwaa baadhi ya damu ya yule ng'ombe, na ya damu
ya yule mbuzi, na kuitia juu ya pembe za madhabahu pande zote. 19 Tena atanyunyiza baadhi ya damu juu ya madhabahu kwa
kidole chake mara saba, na kuitakasa, ili machafu yote ya wana wa Israeli
yaitoke. 20 Naye akiisha kufanya
upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na madhabahu,
atamleta yule mbuzi aliye hai. 21
Na
Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na
kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao
zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani
kwa mkono wa mtu aliye tayari. 22
Na
yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye
atamwacha mbuzi jangwani. 23
Na
Haruni ataingia katika hema ya kukutania, naye atavua mavazi yake ya kitani,
aliyoyavaa alipoingia katika patakatifu, atayaacha humo; 24 naye ataosha mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na
kuvaa nguo zake, na kutoka, na kusongeza sadaka ya kuteketezwa yake mwenyewe,
na sadaka ya kuteketezwa ya watu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya nafsi
yake, na kwa ajili ya watu. 25
Na
mafuta ya sadaka ya dhambi atayateketeza juu ya madhabahu. 26 Na mtu yule amwachaye mbuzi wa Azazeli aende zake,
ataosha nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia katika
marago. 27 Na yule ng'ombe wa sadaka
ya dhambi, na yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, ambao damu yao ililetwa ndani
ifanye ukumbusho katika patakatifu, watachukuliwa nje ya marago; nao watachoma
moto ngozi zao, na nyama yao, na mavi yao. 28 Na yeye awachomaye moto atafua nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na
baadaye ataingia maragoni. 29
Amri
hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi,
mtajitaabisha roho zenu, msifanye kazi ya namna yo yote, mzalia na mgeni akaaye
kati yenu. 30 Kwa maana siku hiyo
upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi
zenu zote mbele za Bwana. 31
Ni
Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajitaabisha roho zenu; ni amri ya milele.
Taratibu
zote na maadhimosho ya Siku ya Upatanisho vimeelezewa kwa kina kwenye majarida
ya Upatanisho (Na. 138) na Azazeli na Upatanisho (Na. 214) [Atonement (No. 138) and Azazel and Atonement (No. 214)].
Katika Siku ya Upatanisho kulikuwa na mbuzi wawili wa
sadaka ya dhambi kwa ajili ya watu. Kuhani Mkuu ndiye eke yake aliruhusiwa
kuingia Patakatifu pa Patakatifu na aliruhusiwa kuingia hapo mara moja tu kwa
mwaka katika hii Siku ya Upatanisho. Alioaswa aingie huko na sadaka ya dhambi
kwa ajili yake mwenyewe – ng’ombe dume – na alichukua damu ya mafahali na damu
ya mmoja ya mbuzi katika Patakatifu pa Patakatifu. Tunajua kwamba hii ilikuwa
inamlenga Kristo.
Weebrania
9:11-14 Lakini
Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema
iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya
ulimwengu huu, 12 wala si kwa damu ya mbuzi
na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu,
akiisha kupata ukombozi wa milele. 13
Kwa
maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe
waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; 14 basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa
milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha
dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?
Kuhani Mkuu, akiwa anafanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe,
watu na Patakatifu pa Patakatifu, nk, kisha alikiri na kuungama dhambi za watu
juu ya kichwa cha mbuzi wa Azazeli. Kisha
mbuzi aliondolewa mahali pale palipofurika watu na mwanaume mahiri su anayestahili.
Tunajionea mchakato wa namna hii hii wa upatanisho
tunaouona katika mwezi wa Kwanza kwenye Utakaso wa Hekalu na kisha upatanisho
na makuhani na watu kama ni wateule. Hapa mchakato ni upatanisho wa kuhani na
hatimaye watu, kukafuatiwa na kuondolewa kwa Shetani. Kuhani alipatanishwa na
Kristo, kwa mfano wa Yule dume wa ng’ombe, kuonyesha mabadiliko ya ukuhani.
Kuondolewa kwa mbuzi wa Azazeli kunaasiria kitendo cha kufungwa kwa Shetani
mwanzoni mwa kipindi cha Milenia. Watu wanapaswa kufunga saumu na “kuziteza
nafsi zao” – inaonyesha utakaso na upatanisho. Kondoo waliotolewa kwa ajili ya
sadaka ya kuteketezwa kwa kuhani na watu wanaashiria majaribu na mateso ambayo
tunapaswa kuyapitia. Tunajua kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya watu wote.
1Yohana 2:2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu;
wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
Upatanisho huu unaendelea ili kuijumuisha sayari yote. Ni
lazima ishike mkondo wake mapema kabla ya utawala wa Kristo. Kwa hiyo, Shetani
lazima afungwe ili kuzuia ushawishi wake, kama ilivyoonyeshwa kwenye Ufunuo 20:1-3.
Kristo alichaguliwa na kutengwa kando siku ya 10 ya mwezi wa Kwanza. Anautenga
mbali ulimwengu kwa upatanisho na wongofu wa siku ya 10 ya mwezi wa Saba.
Idi ya Vibanda:
majira ya mavuno ta tatu
Sikukuu ya Vibanda inafanyika kwa kipindi cha siku saba
tu, ya kwanza ikiwa ni Sabato. Baada ya siku saba kukamilika au kwisha, siku
inayofuatia ni Sabato. Siku hizi saba zinaashiria hitimisho, bali hizi sio
Sabato ya siku ya saba ya juma. Ufanyaji wa kazi za kawaida wa siku ya saba ni
ishara kufunguliwa kwa Shetani na harakati endelevu za Mungu kwenye mchakato. Siku
Takatifu kwa hakika ni ile siku ya nane au Siku Iliyo Kuu nay a Mwisho ya
Sikukuu au Siku ya Mkutano wa Makini. Kipindi cha siku saba inawakilisha
kipindi cha miaka elfu saba. Sabato ya siku ya kwanza inaonyesha kufufuliwa kwa
wateule wakati wa kurudi kwake Kristo. Sabato katika siku ya nane inaonyesha
ufufuo wa mwisho utakaotokea baada ya kipindi hiki cha miaka elfu kikiisha na
ujio wa Mji wa Mungu (tazama majarida ya Ufufuo wa Wafu (Na. 143) na Mji wa Mungu (Na. 180) [The Resurrection of the Dead
(No. 143) and The City of God (No. 180)].
Ufunuo 20:4-5
Kisha
nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona
roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno
la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea
ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai,
wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. 5
Hao
wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa
kwanza
Kutoka aya ya 5 tunaona kwamba siku ya nane ni Ufufuo wa
Pili wa wafu; ufunuo 20:4-5 inaonyesha Ufufuo wa Kwanza utakaotokea moja kwa
moja baada ya miaka elfu. Siku ya Bwana ni
kipindi chote kizima cha miaka elfu na kinaendela mbele kuhitimisha Siku ya
Mwisho Iliyo Kuu ambayo ni kivuli au taswira ya Siku ya Mwisho Iliyo Kuu ya
Sikukuu ya Vibanda ambayo kwayo watu wote watafufuliwa.
Yohana
6:39-40 Na
mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze
hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho. 40 Kwa
kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na
kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Yohana 7:37-38
Hata siku ya
mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema,
Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 38 Aniaminiye mimi,
kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
Yohana
11:24-26 Martha
akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. 25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye
aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki
hayo?
Yohana 12:48 Yeye anikataaye mimi,
asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo
litakalomhukumu siku ya mwisho.
Yohana 12:48 inaonyesha wale ambao hawajaitwa sasa (Yeye alikataae mimi na hayapokei maneno
yangu) watakuwa na fursa nyingine katika Siku ya Mwisho – siku yao ya
hukumu.
Kwahiyo, siku ya nane ni sehemu ya Sikukuu ya Vibanda na
ni siku ya ufufuo wa watu wote. Siku
ya nane pia ni Sabato kuu ya saba ya mwaka, kwa hiyo ni hitimisho na pumziko la
Mungu kutoka kwenye utendaji wa kazi yake ya wokovu.
Majira haya ni Sabato ya juma la uumbaji, mavuno ya tatu ya Mungu.
Ufufuo wa Kwanza menenwa na Maandiko Matakatifu kuwa ndio
ulio “bora”. Ni bora kwa sababu wale walio ndani ya ufufo huu watafufuliwa kwa
uzima wa milele. Watakuwa wamekwisha hukumiwa tayari kabla ya ufufuo na kwa
hiyo mauti ya pili hawana sababu ya kuiogopa. Wamefufuliwa milele na sio kwa hukumu au kwa maamuzi, kama wale walio kwenye
Ufufuo wa Pili.
Yohana
5:29 Nao watatoka; wale waliofanya
mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Hawahitaji kufanya maamuzi wala kuhukumu kwa kuwa haya
yamekwisha pita kwao. Ufufuo wa pili ni ufufuo wa hukumu na kufanya maamuzi au
kukata shauri. Watu hawa hawajui wakati wa kufufuka kwao, ila wapende
wasipende, wata watakumbwa na mauti ya pili. Wataishi kwa kitambo na kisha
kuhukumiwa sawasawa na waliyoyafanya kipindi kile – maamuzi waliyoyafanya na
maamuzi yaliyofanywa juu yao.
Hosea
5:14-15 Maana mimi nitakuwa kama
simba kwa Efraimu, na kama mwana-simba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi
nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukulia mbali, wala hapatakuwa na mtu
wa kupokonya. 15 Nitakwenda zangu
niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu;
katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.
Hosea 6:1-2 Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye
amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu. 2 Baada ya siku mbili atatufufua; siku
ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake.
Aya hizi zinamahusiano ya Luka 13:32-33. Kwa hiyo zina
maana kwenye huduma ya miaka mitatu ya Kristo. Pia ina uhusiano na mavuno ya Israeli,
ambayo tumeyaona kwa suala la miaka mitatu ya mateso, sawa na kama Yuda
walivyopitia mateso na mauaji makuu ya kimbari yanayojulikana kama Holocaust. Hata
hivyo, hii ina maana ana zaidi ndani yake yanayohusiana na kipindi cha miaka
elfu tatu ya mwisho (soma Hosea 6:2). Kipindi hiki kinafanya mabadiliko ya
mfumo ukuhani mkuu kutoka ule wa Walawi kwenda kwa wa Melkizedeki (pia soma
Hosea 5:14).
Kwa hiyo tunapaswa kuisoma Hosea 6:2, pale inaposema
“baada ya siku mbili”, akimaanisha baada
ya Alhamisi na Ijumaa, Jumamosi au Sabato. Hapa inahusiana na kufanyiwa
“kuamshwa” na “kufufuliwa” katika siku hii. Kwa hiyo tunaweza kupunguza
mlolongo nyakati za utoaji dhabihu na mateso kuwa ni kama siku tatu tangu kufa
kwa Masihi na juma la Pasaka kama lilivyohusiana na mchakato wa miaka mitatu na
wa miaka elfu tatu. Kipindi hiki kimehusishwa na kujumuishwa kwa miaka elfu
mbili cha jangwani na miaka elfu moja ya utawala wa millennia na Yesu Kristo.
Hii inaendana na Pentekoste ya arobaini (Yubile) kama kipindi chetu kirefu
kabla ya mavuno makuu ya Mungu chini ya Masihi (Yeremia 5:24).
Kama ilivyoandikwa kwenye Mambo ya Walawi 23:42-43, Sikukuu
ya Vibanda pia ilikuwa inafanya taswira kipindi cha Waisraeli walichotoka
utumwani Misri na wakakaa kwenye Vibanda. Tutaweza kusema kwa ufupi tu kwamba
sikukuu hii inahusiana na utokaji mpya kutoka utumwani wa tgaifa zima lote Isaya
66:20.
Isaya 66:20 Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa
yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika
machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu
mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka
yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.
Kwa hiyo tunaweza kusema kwa
ufupi tu kwamba maana yah ii ilikuwa inawahusu Israeli wa kimwili katika
Milenia, kipindi hiki watakuwa kwenye maeelekezo au sheria za haki na watakuwa
na Roho Mtakatifu mioyoni mwao na ndipo watamtii Mungu na Torati yake ambazo
zitakuwa ndiyo sheria na kanuzi za kuliongoza taifa na ni kipimo cha hukumu
katika ufufuo wa mwisho wa wanadamu waliobakia.
Kwa
hiyo kuna mahusiano mkubwa kati ya Sikukuu ya mwezi wa Kwanza na Sikukuu za
mwezi wa Saba. Zinamaana kwa kila moja kwa nyingine kwa muundo unaotegemeana.
Tangu mwezi
wa Kwanza hadi wa Saba
Mchakato
huu wa marejesho ya kwanza umekusudiwa kufanywa na Masihi. Mlolongo wa mambo wa
zama hizi umeelekezwa na mchakato uliopo kwenye mwezi wa Kwanza.
Katika
siku ya kwanza ya mwezi, Utakaso wa Hekalu la Mungu unafanyika – Hekalu ambalo
ni sisi (1Wakorintho 3:16; 6:19).
Aiku
ya saba ya mwezi ni ya utakaso kwa ajili ya dhambi zilizofanywa kwa kupotoshwa
au bila kukusudia. Kufanya hivyo ni mumihu kwa ajili ya uumbaji wa viumbe
vionekanavyo kwa sasa na kwenye Milenia na ni moja ya tofauti iliyopo kati ya
miezi ya Nisan na Tishri, ambazo vinginevyo zinafanya taswira mpango huohuo na
matendo yake.
Siku
ya kumi ya mwezi wa Kwanza tunaona uchaguzi na kumtenga kando mwanakondoo
ambaye anatangulia mchakato wa ukombozi na harakati kwa ajili ya malimbuko
yanatolewa na yanakubalika na Mungu.
Siku
ya 14 ya mwezi wa Kwanza ni Sikukuu ya Pasaka. Marejesho yote kwenye zama hii
yanaanzia tangu na yanahusiana na mwezi wa Kwanza yakiendelea hadi katika
utoaji na ushiriki wa mlo wa mwili na damu ya Kristo ikiwa ni sakramenti ya
pili ya wateule. Sakramenti ya kwanza ya wateule ni ubatizo, ambao ni awamu ya
kwanza ya utakaso wa Hekalu. Kimsingi, hii inachukua nafasi yhake baada ya
majira ya Sikukuu na baadae kidogo na kati ya siku ya 1 na ya 7 ya mwezi Nisani
na kabla ya siku ya 14 ya mwezi wa Kwanza.
Sikukuu
ya Pasaka na Mikate Isiyo na Chachu inakuwa ya siku moja na inafuatiwa na siku
saba nyingine. Siku ya Kwanza Takatifu kenye sikukuu zote mbili inakuwa ni siku
ya 15 ambayo kwa kawaida iakuwa ya mwezi kamili. Mchakato huu unaashiria
dhabihu na maandalizi ya wateule kwa kuondoa dhambi na kisha kujijenga tayari
kwa Pentekoste na Mavuno ya wateule Katika Yubile ya arobaini jangwani.
Kuna
Siku Takatifu mwanzoni na mwishoni mwa Idi ya Mikate isiyo na Chachu, ambazo ni
siku ya kwanza au Siku ya Pasaka siku ya 14 Nisani ikiwa ni siku ya maandalizo.
Wateule wasipokuwa safi hawaruhusiwi kuula mkate usio na chachu wa Pasaka,
ambao tumeuona kwenye Marejesho mapya (soma jarida la Marejesho ya Yosia (Na. 245)
[Josiah's Restoration (No. 245)] wakati makuhani wa Mahali pa
Juu hawakuruhusiwa kwenda Hekaluni kuila Pasaka. Kwa hiyo, ibada za sanamu
ziliwatenga makuhani na kuwafanya wasistahili kuila Pasaka Hekaluni.
Tofauti
iliyoko kati ya miezi hi yaw a Kwanza na wa Saba ni kwamba kusanyiko la
Baragumu, na tena Miandamo ya Mwezi au siku ya Kwanza ya mwezi, inatangaza ujio
wa Masihi kwenye harakati ya mambo ya dunia. Ataingia na kuzifupisha siku hizi
kwa ajili ya wateule na uwepo wao na kuendelea wakiishika imani kama watu wa
Mungu. Wanajulikana kwa matendo na kazi zao, zinaoendana na kuashiriwa na
Sabato, iandamo ya Mwezi, Sikukuu na harakati zao tangu mwezi wa Kwanza na
kuendelea na pamoja na kumpokea kwao Roho siku ya Pentekoste na Torati ya Mungu
kwa ujumla.
Hakuna
kufunga saumu katika siku ya saba ya mwezi wa Saba. Hakuna kile mtu
anachokifanya leo kinacho fanana. Mwanakondoo amekwisha chinjwa tayari na kutolewa
sadaka na kwa hiyo ufungaji saumu unafanyika siku ya kumi ya mwezi wa Saba
wakati kwamba katika mwezi wa Kwanza umekuwa ukitengwa tu kwa ajili ya dhabihu
inayotolewa siku ya 14. Katika mwezi wa
Saba, Yule Mwanakondoo aliyewekwa kando kule Mbinguni anarudi akiwa kama Mfalme
Mshindi akitanguliwa na Baragumu au Tarumbeta, siku ya Kwanza ya mwezi wa Saba.
Inapofika Siku ya Kumi ya Upatanisho, dunia inapatanishwa na kuandaliwa kwa
utawala wa milenia.
Mataifa
yanahukumiwa kwa mpangilio endelevu. Ni kama Yosia alipofanya marejesho ya
Hekalu na Torati kutoka kwenye Pasaka na akaendelea zaidi kwa kipindi kisicho
cha kawaida cha miaka kumi na mitatu baada ya mwaka 623/2 KK hadi alipokwenda
Megido mwaka 609 KK kuyakabili mataifa na kufa, ndivyo vivyo hivyo ufalme
utapita kutoka mikononi mwa wafalme hadi mikononi mwa Masihi, anayestahili.
Sikukuu
ya \Mkusanyiko inatakiwa iende sambamba na utoaji wa sadaka jioni ya siku ya
kwanza ya Sikukuu. Siku ya kwanza ya idi ya Vibanda ni Takatifu, kwa hiyo
hakuruhusiwi kufanya kazi yoyote na wanadamu zaidi ya kutoa sadaka ya kusanyiko,
ambayo haitakiwi ibakie hadi asubuhi.
Siku
saba za Vibanda zinafananishwa na millennia nazo zinakuwa saba sawa na siku za
Mikate Isiyo na Chachu. Kwenye mfano wa kwanza, Masihi alikufa ili kuiwezesha
Sikukuu ya Pasaka. Matendo ya wanadamu yanapaswa kuondoka duniani.
Katika
mwezi wa Saba, Sikukuu inaashiria utawala wa Masihi kwenye hii sayari ambako
hakuna ulazima wa kutoka na kuiacha dunia, kwa kuwa ulimwengu wote utakuwa
kwenye jutawala wa haki na maongozi ya Torati ya Mungu.
Kwa
hiyo, siku ya saba ya Idi ya Vibanda sio siku takatifu, kwa kuwa inaashiria
dunia kurudi kwenye Ibilisi Msitaki wetu na kipindi cha vita.
Kwa
upande mwingine, Siku ya Mwisho Ilikyokuu ni siku ya nane, ambayo ni tofauti
kabisa na siku za Mkate Usio na Chachu, iko mwishoni na siyo mwanzoni na ni
Siku Takatifu. Paska kwa namna nyingine sio Siku Takatifu kwa sababu kwa kuwa
inaziwakilisha kazi za Masihi kwa wokovu wa mwanadamu.
Siku
ya MWisho Iliyo kuun ni Takatifu kwa kuwa inawakilisha hukumu ya haki kwa ulimwengu
na kuondolewa dhambi mara ya mwisho katika historia. Inawakilisha ujio wa Mungu
Ulimnwenguni na kushuka kwa |Mji wa Mungu vikiungana kwa marejesho ya mwisho.
Haya
marejesho ya mwisho ni hitimisho ya mwisho ya Mpango wa Mungu.
Marejesho
mapya ya dunia katika Mpango wa Mungu kama yalivyoashiriwa na maadhimisho ya
Sikukuu na Siku Takatifu na utaratibu wake, yameelezewa kwa kina kwenye
majarida ya Utakaso wa Hekalu la Mungu
(Na. 241), Utakaso Kwa Ajili ya Dhambi za Kupotoshwa (Na. 291) na Sabato Kuu Saba
(Na. 107 [Sanctification of the Temple of God (No. 241); Sanctification of the Simple and Erroneous (No. 291); Josiah's Restoration (No. 245) and The Seven Great Passovers of the Bible (No. 107)]. Sikukuu hizi na Siku Takatifu hizi zote zina maana yake kwa harakati zake kwenye
mchakato wa Mpango wa Mungu.
Ukurasa wa Nyongeza kwenye jarida hili Namba 227
Alhamisi, siku ya 1 Nisani: Mwandamo wa Mwezi na Siku ya Kwanza ya Mwaka
Mtakatifu. Utakaso wa Hekalu ulifuatia
baada ya siku hii (Ezekieli 45:18; sawa na jarida la Utakaso wa Hekalu la Mungu
(Na. 241) [Sanctification of the Temple of God (No. 241)]. Mwandamo wa Mwezi uliadhimishwa
wakati wa kipindi chote cha huduma ya Kikuhani Hekaluni, pamoja na utoaji wa
sadaka za siku za Sabato na Siku Takatifu (kwa mujibu wa Josephus, Wars of the Jews, Bk. V, ch. V,
7). Katika siku za Miandamo ya Mwezi, hususan siku hii, na Sabato na Sikukuu,
Kuhani Mkuu alipanda kwenda Hekaluni pamoja na makuhani wengine.
Jumatano, siku ya 7 Nisani: (siku 8 kuifikia Pasaka na mwisho wa juma la kwanza na la Utakaso la mwaka0).
Utakaso kwa ajili ya Dhami zilizofanywa kwa ujinga na kupotoshwa (Ezekieli
45:20; sawa na jarida la Utakaso Kwa Dhambi za Kupotoshwa (Na. 291) pSanctification
of the Simple and Erroneous (No. 291)]. Kristo anaandaliwa. Anautakaso kwa ajili ya wote kwenye Pasaka hii.
Alhamisi, siku ya 8 Nisani: (siku 7 kuifikia Pasaka) Kristo
anaingia mjini Yerusalemu alitokea Yeriko. Anashinda usiku nyumbani kwa Zakayo
(Luka 19:1-10).
Ijumaa, siku ya 9 Nisani: (siku 6 kuifikia Pasaka) (vitu vyote kueoka hapa vimeelezewa kwa kina
kwenye jarida la Wakati wa Kusulibiwa na
Kufufuka (Na. 159( [Timing of the Crucifixion and the Resurrection (No. 159)].
Kristo anaingia kwa mara ya kwanza akitokea Bethfage (sio
Bethania; sawa na Mathayo 21:8-9). Hakutarajiwa. Analisafisha Hekalu sawasawa
na maagizo ya Torati (sawa na Mathayo 21:12-16). Anaondoka kwenya Bethania na anaadhimisha
Sabato huko. Mariamu anampangusa miguu yake Bwana Yesu kwa manukato (Mathayo
21:1-9; Yohana 12:1).
Jumamosi, siku ya 10 Nisani: (siku 5 kuelekea Pasaka)
Kristo anaishika Sabato huko Bethania. Anateuliwa na
kutengwa kama Mwanakondoo (Yohana 12:2-11).
Jumapili, siku ya 11 Nisani: (siku 4 kufikia Pasaka)
Anaingia kwa shangwe mjini Yerusalemu akitokea Bethania. Yesu
anaingia na kulikagua Hekalu kissa anarudi Bethania (Marko 11:1-11; Luka
19:29-44; Yohana 12:12-19).
Jumatatu, siku ya 12 Nisani: (siku 3 kufikia Pasaka)
Kristo
anarudi asubuhi anatokea tena Hekaluni na analisafisha.
Anarundi Hekaluni (Mathayo 21:18-22; Marko 11:12-19; Luka
19:45-48).
Jumanne, siku ya 13 Nisani: (siku ya 2 kufikia Pasaka)
Kristo anakuwa tena mjini Yerusalemu. Anafundisha kwa
njia ya maswali na mafumbo. Unabii juu ya Hekalu na mafuta ya Mzeituni yanatolewa.
Ilipofika kuzama kwa jua Kristo anawaambia wanafunzi wake waende Yerusalemu
wakatafute mahali na kuiandaa Pasaka (Mathayo 21:23-39; 24:1-51; 25:1-46; 26:17-20;
Marko 11:20-33; 12:1-44; 13:1-37; Luka 20:1-21:38).
Jumatano, siku 14 Nisani: (siku 1 kuelekea Pasaka; siku ya/1 ya
Mikate Isiyo na Chachu)
Mlo wa usiku wa Jumatano halafu Ushirika wa Meza ya Bwana
au Pasaka, Kuoshana miguu, kusalitiwa, nk.
Majira ya mchana – kusalitiwa, nk, halafu Kusulibiwa.
Kristo anapelekwa chini mtini na anazikwa kaburini kabla
ya jua kuzama (kuanza kwa Sabato ya Pasaka) (Mathayo 26:20-27:66; Marko
14:17-15:47; Luka 22:14-23:55; Yohana 13:1-19:42).
Alahamisi, siku ya 15 Nisani
PASAKA/SIKU YA 1 ya MIKATE
ISIYO NA CHACHU
Majira ya usiku – Siku ya 1 usiku kaburini. Majira ya mchana – siku
ya 1 kaburini.
Ijumaa, siku ya 16 Nisani
Majira ya usiku – usiku wa 2
kaburini. Majira ya mchana – siku ya 2 ksburini.
Jumamosi, siku ya 17 Nisani
Majira ya usiku – usiku wa 3
kaburini. Majira ya mchana – siku ya 3 kaburini.
Majira ya alasiri, Kristo
Mungu anamfufua Kristo kutoka kwa wafu.
Jumapili, siku ya 18 Nisani
SADAKA YA MGANDA WA KUTIKISWA
INATOLEWA
Kristo anapaa kwenda mbinguni kwa Baba yake ambaye ni
Mungu wake ili akubalike kama sadaka kwa ajili ya dhambi zetu (Mathayo 28:1-7;
Marko 16:1-7; Luka 24:1-9; Yohana 20:1-9; 20:16-17).
q