Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[242]

 

 

 

Kifo Cha Mwana Kondoo

(Toleo 1.0 19980314-199803114)

 

 

 

 

Wakristo waliowengi hawatilii maanani kwa kile kinachotokea wakati wa Pasaka na majira na maana ya kifo cha Masihi kama Mwana Kondoo wa Mungu.

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Copyright © 1998 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 


Kifo Cha Mwana Kondoo [242]

 


Tumeisha elewa wakati wa kusulibiwa na kufufuka (tazamajarida la Nyakati za Kusulibiwa na Kufufuka [159].

 

Pasaka imefafanuliwa sana katika jarida lisemalo Pasaka [098] na imevunjika katika maeneo thabiti katika kufafanua kuhusu Ushirika wa Meza ya Bwana kama ilivyoandikwa katika jarida lisemalo Ishara ya Uoshaji Miguu [099], Ishara ya Mkate na Divai [100], na Ushirika wa Meza ya Bwana [103].

 

Tunajua kuwa Pasaka ni sheria iliyoamriwa na Bwana na ya kwamba iliadhimishwa na Israeli kama ilivyoamriwa kwenye Biblia hadi kufikia kipindi cha mwisho wa Hekalu yapata mwaka 70 BK.

 

Tunajua ninini kilitokea wakati wa Ushirika wa Meza ya Bwana na tunafahamu kuwa matukio haya yalifanyika usiku wa siku ya 14 ya mwezi wa Nisani mapema kabisa kabla Masihi hajakamatwa na majaribu na baadae kusulibiwa kwake.

 

Kila tendo katika mwandamano wa matukio ya wakati wa Pasaka yalikuwa ni kwa kufuatana na mujibu wa mpango mkamilifu wa na kwa mujibu wa sheria zake na majira yake. Kristo hakusulibiwa katika siku ya Ijumaa na hakufufuka siku ya Jumapili kama inavyofikiriwa na na kuaminika na Wkristo walio wengi. Mwanzo wa sikukuu ya wapagani ya Easter na tafsiri yake ya kuifanya Pasaka ionekane na kuaminika kuwa ni sikukuu ile ile ya Easter imefafanukliwa kwa kina sana katika jarida liitwalo Mwanzo wa Christmas na Easter [235].

 

Vile vile Wayahudi hawakuwa na majira yaliyokosewa na Kristo hakufa katika majira yaliyo kosewa. Alikufa katika majira makamilifu kama Mwana kondoo wa Pasaka alivyokuwa anauawa Hekalu la Mlimani na kwa mujibu wa maelekezo ya sheria kama zilivyoamriwa na Mungu.

 

Tunafahamu toka mioyoni mwetu kuwa matendo na huduma ya karamu ya mwisho kuwa Bwana aliatoa Ushirika wa Meza ya Bwana. Tunajua kwamba hii ni ojawapo ya sacramenti mbili za Kanisa (tazama jarida la Sakrament za Kanisa [150]. Sakramenti nyingine ni ya Ubatizo (tazama jarida lisemalo Toba na Ubatizo).

 

Kile ambacho kimeshindwa kueleweka vilevile ni majira na sababu gani zilizopelekea kifo cha Masihi kama Mwana Kondoo wa Mungu.

 

Sheria ya Pasaka

Mambo ya Walawi 23:4-14 inasema: 4Sikukuu za BWANA ni hizi, ni makusanyiko matakatifu, ambayo mtayapigia mbiu kwa nyakati zake. 5Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya ya mwezi wakati wa jioni, ni pasaka ya BWANA. 6Na siku ya kumi na tano ya mwezi uleule ni sikukuu kwa BWANA ya mikate isiyotiwa chachu; mtaila mikate isiyotiwa chachu muda wa siku saba. 7Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu msifanye kazi yoyote ya utumishi. 8Lakini mtasongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto siku saba; siku ya saba ni kusanyiko takatifu mfifanye kazi yoyote ya utumishi. 9Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia. 10Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; 11naye atautikisa mganda mbele za BWANA ili kwamba akumaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa. 12Na siku hiyo matakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. 13Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini. 14Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote.

 

Tunaona kuwa sheria hii imegawanyika katika mchanganuo wa maeneo yafuatayo:

 

 

 

 

Kuna idadi ya sheria ndogondogo ambazo zinasimamia Pasaka na ambazo zimetoa mwanga wa matendo ya Masihi na mitume kwa ajili ya Pasaka katika mwaka wa 30 BK mwaka ambao alikufa.

 

Pasaka ilikuwa inaadhimishwa kwa ajili ya sababu kuu mbuli. Sheria ya kwanza kabisa asilia ilitolewa kwa ajili ya chakula kilicholiwa majira ya jioni kufuatiwa dhabihu iliyotolewa majira ya alasiri ya siku ya 14 ya mwezi wa Nisani, mfano ni katika jioni ya siku ya 15 ya mwezi wa Nisani. Kwa ule mwanzo wake asilia ilikuwa ni mwana kondoo aliyeliwa kwa pamoja na mchanganiko wa mboga zenye uchungu; aliyeuawa kule Misri na damu yake ilipakwa kwenye miimo ya milango au kwenye kizingiti cha mlango ili kwamba malaika wa mauti aweze kupitaa juu ya nyumba za wana wa Israeli. Kwa ajili hii, wazaliwa wa kwanza Misri waliuawa na wana wa Israeli walipitwa juu – kwa hiyo, neno Pasaka. Kwa njia hii, Mungu alionyesha kitu ambacho angefanya na dunia na kwamba wokovu ungekuja kwa kupitia kifo cha Masihi kama Mwana kondoo wa Mungu kwa kuruhusiwa kuingia katika familia ta Mungu tukiwa kama sehemu ya taifa la Israeli.

 

Dhabihu hii imeamriwa katika kitabu cha Kutoka.

 

Kutoka 12:1-14 inasema: BWANA akanena na Musa, na Haruni katika nchi ya Misri akawaambia, 2Mezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. 3Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkmwammbie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana koondoo kwa watu wa nyumba moja; 4na ikwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na atwae mwana kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yulr mwana kondoo. 5Mwana kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi. 6Nanyi mtamweka katika siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni. 7Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla. 8Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chacu; tena pamoja na mboga zenye uchungu. 9Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani. 10Wala msisaze kitu kitu chake cho chote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto. 11Te.mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya BWANA. 12Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA. 13Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoingia nchi ya Misri. 14Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyot, kwa amri ya milele.

 

Mwana Kondoo wa Pasaka au mbuzi alitakiwa auawe na makutano wote wa mkutaniko wa Israeli. Alikuwa anachaguliwa katika siku ya kumi ya mwezi na kuuawa katika siku ya kumi na nne ya mwezi. Aliliwa katika usiku wa siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza na alitakiwa atunzwe hata katika Usiku wa Kuuabgalia Sana milele. Wakati malaika wa mauti alipokuwa anapita juu katika usiku wa manane wa siku ya 15 mwezi Nisani aliwaua wazaliwa wa kwanza wa Misri kuanzia mtoto wa Farao hadi yule aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa.

 

Kutoka 12:29-36 inasema: 29Hata ikawa, usiku wa manane BWANA akawapiga wazaliwa wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama. 30Farao akaondoka usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu. 31Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; enendeni, mkamtumikie BWANA kama mlivyosema. 32Twaeni kondoo zenu na ng’ombe zenu kama mlivyosema, enendeni zenu, mkanibariki mimi pia. 33Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote. 34Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabagani. 35Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi. 36BWANA akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara.

 

Jioni hii iliamriwa waiadhimishe kama ukumbusho wa kuachiliwa huru kwa Israeli. Tendo hili pia linatazama mbele kwenye wokovu wa ulimwengu kwa kupitia dhabihu ya Masihi.

 

Kutoka 12:42 inasema: 42Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za BWANA, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao.

 

Sheria hii ilibadilishwa baada ya Pasaka ya kwanza kwa maana ifuatayo.

Kumbukumbu la Torati 16:1-8 inasema: Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA, Mungu wako. 2Nawe umchinjie pasaka BWANA , Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng’ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake. 3Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku saba utakula naye mikate isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya mateso; kwa maana ulitoka nchi ya Misri kwa haraka; ili upate kukumbuka siku uliyotoka nchi ya Misri kwa haraka; ili upate kukumbuka siku uliyotoka nchi ya Misri, siku zote za maisha yako. 4Wala isionekane kwako chachu muda wa siku saba katika mipaka yako yote; wala katika hiyo nyama uchinjayo siku ya kwanza jioni, kisilale cho chote usiku kucha hata asubuhi. 5Usimchinje pasaka ndani ya malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako; 6ila mahali atakapopachagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, ndipo mtakapomchinja pasaka jioni, katika machweo ya jua, kwa wakati kama uliotoka Misri. 7Nawe umwoke na kumla mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako; kisha asubuhi yake ugeuke uende hemani mwako. 8Siku sita utakula mikate isiyotiwa chachu; na siku ya saba na uwe mkutano mtukufu kwa BWANA, Mungu wako, usifanye kazi yo yote.

 

Hapa, tunaona kuwa sheria ilirudishwa kutoka kwenye ile ya asilia. Katika Pasaka ya kwanza, ilifanyika katika katika nyumba za Misri na hakuna mtu aliyeruhusiwa kuondoka. kisha pia nyumba zililindwa na damu iliyopakwa juu ya miimo ya milango au kwenye kizingiti.

 

Kwa njia hii, watakatifu walionyeshwa kulindwa wakiwa kwenye nchi ya ng’ambo kutokana na harakati za malaika wa mauti ambaye alikuwa ni Masihi mwenyewe katika kazi hii kama muhukumu wa ulimwengu. Ili kufikia kiwango cha kukubalika katika kazi hii, alipaswa kuonyesha utashi wake kuyatoa maisha yake mwenyewe kwa ajili ya ulimwengu wote na alipaswa kuuhukumu.

 

Ishara hii ilichukuliwa kama jukumu katika makazi ya Israeli wakati Yoshua walipoanza kukaa katika nchi ya ahadi. Kamba nyekundo iliyoning’inizwa katika kizingiti cha nyumba ya Ahabu kwenye ukuta wa Yeriko ilikuwa ni mfano wa Pasaka hii ya malaika wa mauti kama alivyomtokea Yoshua kama Amiri wa Jeshi la Bwana (soma jarida lisemalo Kuanguka kwa Yeriko [142].

 

Wakati Israeli walipokuja katika urithi wao na kuingia katika milki zao wenyewe, waliamriwa hatimaye kuishika Pasaka nje ya nyumba zao (Kum. 16:5-7). Katika asubuhi ile tu ya Mikate isiyotiwa Chachu wakati waliporuhusiwa kurudi majumbani mwao. Vile vile kuanzia wakati huu, ilitakiwa achinjwe mnyama yeyote aliye safi kutoka katika mifugo yao. Pasaka ilikuwa bado, hata hivyo, ilikuwa ni mfano wa mwana kondoo na ilikuwa ni mi kitu cha kawaida na ni mnyama anaye kubalika kwa ajili ya chakula.

 

Tunaweza kuanza kuona baadhi ya mifano na maana ya majira na matendo ya Yesu Kristo katika Pasaka wakati aliposulibiwa.

 

Tunajua bila ya shaka yoyote pale wana kondoo walipouawa wakati wa majira ya hekalu. Mwana zuoni maarufu na mwenye kuheshimika wa Kiyahudi aliyeitwa Josephus anatuonyesha wana kondoo walikuwa wakichinjwa kuanzia saa tisa hadi saa kumi na moja yaani saa 9:00 alasiri hadi saa 11 jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi. Kwa hiyo, wana kondoo walikuwa wanaandaliwa na kuliwa majira ya jioni ya siku ya 15 mwezi wa Nisani kama mlo wa Pasaka. Josephus anaielezea Pasaka ilivyokuwa inaadhimishwa siku za utawala wa mfalme Nero kama ifuatavyo:

Kwahiyo hawa makuhani wakuu wakati ilipokuwa zinakuja sikukuu inayoitwa Pasaka, wakati walipokuwa wanachinja dhabihu zao, kuanzia saa tisa hadi saa kumi na moja, lakini ili kwamba wakisindikizwa na sio chini ya kumi wakihudhuria kila awamu moja ya utoaji dhabihu, (kwa kuwa ni kinyume cha sheria kuandaa sikukuu kwa kila mmoja peke yake), na wengi wetu tuko ishirini katika usindikizaji wetu, tukakuta idadi ya kondoo wa dhabihu ni miambili na hamsini na sita elfu na mia tano; ambayo ni juu ya posho ya sio myingine yeyote bali ni sikukuu zile kumi kwa pamoja, na idadi ya jumla ni watu milioni mbili mia saba elfu na mia mbili.  Inapatikana katika jarida liitwalo (Vita ya Wayahudi, kwa Kiingereza huitwa War of the Jews, Bk. VI, IX,3).

 

Kwa hiyo, alikuwepo mwana kondoo mmoja tu – ambaye kwanza alichinjwa saa 9:00 alasiri ambaye aliwekwa kwa Kuhani Mkuu wakati wa Pasaka.

 

Kwa hiyo tunapata hapa wazo lenye maana nyuma yake lenye mafuatano ya matukio katika siku ya 14 mwezi wa Nisani ambayo alikufa.

 

Desturi ya Pasaka pia ilikuwa ni tofauti. Katika Yudea watu walifanya kazi siku ya 14 Nisani hadi kufikia saa za alasiri, lakini Galilaya hawakufanya kazi yoyote kabisa katika siku hiyo ya 14 Nisani (kwa mujibu wa mwana zuoni Schurer katika jarida lake lisemalo Historia ya Watu Wayahudi katika Siku za Yesu Kristo kwa Kiingereza History of the Jewish People in the Ages of Jesus Christ, vol. II, p. 14).

 

Hali hii ya kukataza kufanya kazi siku ya Pasaka ni kwa sababu ya harakati hizi ilikuwa lazima katika siku ya 14 Nisani kwa mujibu wa Kumbu kumbu la Torati 16:5-7. Huko Galilaya ambako Kristo anatokea, watu walifanya mambo kwa mujibu wa vile Kristo alivyofanya pamoja na mitume wake katika siku ya kutoa dhabihu ya Pasaka walienda katika mahali pa muda walipopatumia kumchinja Pasaka. Katika Yudea, ambapo makusudio na malengo yote yalikuwa katika milki iliyogawanyikana kama tunavyoona katika sheria za Mishnah zihusuzo wake na mali (zikiandikwa kwa vifupisho kama: mKe. 13:10; mB.B. 3:2, jarida la Schurer, ibid.), inaonekana kulikuwepo kukawa na kutegea katika zoezi hili yawezekana ilisababishwa na hali ya umbali na Hekalu na inawezekana ikawa ni sababu sauti halisi ya kazi ilivyokuwa inahitajika mjini Yerusalemu kwa ajili ya utoaji wa dhabihu kwa jioni ile.

 

Hatahivyo, Masihi na mitume walienda kwenye makazi ya muda kama inavyo takiwa au kuagizwa na sheria kwa mujibu wa Kumbukumbu la Torati 16:5-7.

 

Mwana Kondoo wa Mungu

Masihi anatambulika kama ni Mwana Kondoo wa Mungu.

Injili ya Yohana 1:29-37 inasema hivi: 29Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akisema, Tazama Mwana kondoo wa Mungu, achukuaye dhambi za ulimwengu! 30Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 31Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhuihirishwe kwa Israeli ndiyo maana nilikuja nikibatiza kwa maji. 32Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. 33Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizwaye kwa Roho Mtakatifu. 34Nami nimeona, tena mmeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu. 35Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. 36Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana kondoo wa Mungu! 37Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata.

 

Yohana anaelezea hapa juu ya uwepo wa Yesu kabla ya dhana ya kuzaliwa kwake. Yohana Mbatizaji aliye zaliwa kabla ya Kristo na bado anaongelea hapa kuhusu Kristo kama kana kwamba alikuwepo kabla yake kwa sababu alikuwepo kabla yake. Kifungo hiki cha maandiko matakatifu kinafuatia katika aya ya Yohana 1:18 ambapo tunaona kwamba Masihi alikuwa ni mzaliwa wa pekee [aliye zaliwa pekee] na Mungu au kwa Kiyunani [monogenestheos] ambaye ni kiini cha Baba, Yeye humdhihirisha [au humtangaza] [Yeye (nyongeza)] (kwa mujibu wa Kitabi cha Itifaki kiitwacho Concordant Literal New Testament au vile vile Marshall’s Greek-English Interlinear RSV).

 

Mtume Yohana anaelezea pia, hapa, kwamba kwa yeye ulimwengu ulipata kuweko (Yoh.1:10). Naye Neno alifanyika mwili naye akakaa kwetu. Usemi huu wa kimaandiko ulijulikana katika uandishi wa kizamani wa Kiyudea kama Memra. Kima hiki kilikuwa kama Mwana Kondoo wa Mungu aondoaye dhambi za ulimwengu. Mfano ishara wa Mwana Kondoo unaonekana tena na tena katika utoaji wa dhabihu za dhambi na za amani na za mambo mengine.

 

Badiliko la kumsukuma mwana kondoo katika unabii linakuja kutoka katika Isaya 16:1-5. Kifungu hiki kinazungumzia juu ya mwana kondoo.

 

Isaya 16:1-5 inasema: Pelekeni wana kondoo, kodi yake aitawalaye nchi toka Sela kuelekea jangwani, mpaka mlima wa binti Sayuni. 2Na binti za Moabu watakuwa kama ndege waliotiwa hofu, kwenye vivuko vya Amoni. 3Lete shauri, kata neno; fanya kivuli chako kuwa kama usiku kati ya mchana; wafiche walio fukuzwa; usiwachongee waliopotea. 4Watu wangu waliofukuzwa waache wakae pamoja nawe;katika habari za Moabu, uwe sitara kwake mbele ya uso wake anaye haribu; maana yeye atozaye kwa nguvu amekoma; afanyaye ukiwa ametoweka; waliokanyaga watu wametoka katika nchi. 5Na kiti cha enzi kitafanywa imara kwa rehema; na mmoja ataketi juu yake katika kweli, katika hema ya Daudi; akifanya hukumu, akitaka sana yaliyo haki, mwepesi wa kutenda haki.

 

Biblia ya RSV inasema wana kondoo lakini kondoo wa kodi inatokana na tafsiri ya Biblia ya KJV (Companion Bible).

 

Kondoo wa kodi aliatizwa kwenye nto Yordani akitokea Yeriko. Mwana zuoni mwingine maarufu aitwae bullinger anasema kuwa ni mtawala wa nchi niYuda. Kondoo ameletwa kama Mesha mfalme wa Moabu alipokuwa ameenda (2Wafalme 3:4)

 

Sela alijulikana kama Petra katika Mlima Seir, karibu na Mlima Hur (2Wafalme 14:7).

 

Kifungu hiki cha maandiko kilitumiwa ili kuekezea wafuasi wa mwana kondoo atakaa katika Moabu aliyeombwa awafunike katika uzio wa yule mwovu ambaye alikuwa mfano wa Senikarebu. Lakini nabii Isaya 14 kwa hakika anaongelea kama Mwenye kuleta na Mwanga au wa Malaika walioanguka. Aya ya 5 inaongelea kuhusu kuweka kiti cha enzi katika makao ya wenye haki. Kifungu hiki kinaonelea kuhusu uongofu wa watu wa Mataifa na mabinti wa Moabu kufananishwa na wao wazitupao viota vyao au waliosahauliwa kama vivuko vya Armoni. Kazi hapa ilikuwa ni kuwaficha wafuasi wa Masihi kati kati ya watu wa Mataifa na kuhukumiwa kwa ajili yake. Kifungu hiki cha maandiko kina unda msingi wa mfano wa kondoo na mbuzi uliotolewa katika Mathayo 25:31-46).

 

Isaya kuenda mbali zaidi katika ile sura ya 53.

 

Isaya 53:1-12 inasema: Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa BWANA amefunuliwa nani? 2Maana alikuwa mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri, Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. 3Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. 4Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu na kuteswa. 5Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. 6Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. 7Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake. 8Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; na maisha yake ni nani atakaye isimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu. 9Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake. 10Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwaa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi. Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake; 11Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao. 12Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.

 

Mtu huyu wa huzuni nyingi alichubuliwa kwa makosa yetu. Kama Mwana Kondoo apelekwaye mchinjoni na Bwana aliyaweka juu yake maovu yetu yote. Kifungu hiki cha maneno kinatufundisha sisi ni kwa nini mambo mengine yanatokea kama walivyofanya usiku ule uliotangulia kusalitiwa na kukamatwa kwake Masihi.

 

Hakufungua mdomo wake. Alichukuliwa kama mwana kondoo wa kuchinjwa na kama kondoo mbele ya wakatao manyoya akiwa kimya, wala hakufungua kinywa chake. Kwa hiyo, alichukuliwa na kutiwa gerezani na kutiwa hukumuni na kisha akakatiliwa mbali kulingana na unabii huu na Maandiko Matakatifu hayawezi kutanguka (kama ilivyorudiwa katika Matendo 8:32-33 sawa na Yoh. 1:36).

 

Neno alifanyiwa kaburi lake pamoja na waovu lipo kwa kweli Nathan kama ilvyokusudiwa kushikilia hisia hii ilitumika. Kwa hiyo, kaburi lilikusudiwa liwe na wenyedhambi na matajiri kama tunavyoona baada ya kusulibiwa kwake.

 

Aya ya 5 kwa kweli inasema kuwa alichomwa kwa ajili ya maovu yetu ambayo ni hatua ya kuchoma mkuki kwa upande wake. Alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu na adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake. Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Aya hii ya mwisho imerudiwa katika 1Petro 2:24.

 

Swali lisemalo adhabu ya amani yetu inafurahisha sana.

 

Maswali yote ya Isaya 53:1-9 inashughulikiwa na baraza la marabi wa dini ya Kiyahudi kama ilivyo kwa watumishi walioko utumwani wa Israeli inaonekana na watu wa Wababeli au wawakilishi wao, waliokuwa wanajujulikana kama watumishi katika kutahayarika na kufia dini na kwa sasa kinachoonekana kuwa ni kumuinua juu na kutukuza, kuelezea mkandamizo na hisia (kama mwana zuoni Soncino amavyo nukuu sawa na aliyosema mwana zuoni mwingine aitwae Kaspi).

 

Hii kwa kweli ni tafsiri kama Masihi ameitia utumwani Israeli na Israeli ni mwili wa Yesu kristo. Hii ni kweli ulio dhahiri haiwezi kueleweka na baraza la kirabi la kidini ya Kiyahudi ingawaje wanaweza kuona kwamba mtumishi alipingwa na kuteswa kwa ajili ya maovu ya wengine. Walishikilia kuwa mtumishi aliteseka kwamba ilikuwa inawapendeza (sawa na asemavyo Soncino v. 5): hivyo tunaweza kufanya ustawi, alihukumiwa kwa ajili ya hukumu zetu (kama wasemavyo kina Soncino, Rashi na Kimechi). Wanajaribu kukifanyia kazi kile ambacho Yuda walipokuwa utumwani Babeli alikuwa Isareli ambaye alikuwa ni mtumishi wa Mungu wakati ambapo ni dhahiri kabisa alihesabiwa kuwa ni mtumishi wa Mungu katika kutoa kazi ya mafafanuzi; ambayo kwayo Mungu aliiadhibu Yuda kwa ajili ya maovu yao akiwatumia Wababeli kama chombo chake. Hawakuwa safi yaani wasio na hatia.

 

Isaya 53:4-6 inaeleweka kirabi kabisa inavyotambulika kwamba mateso ya mtumishi hayakutokana na dhambi zozote alizozitenda hata kwa namna yoyote ya siri. Ilikuwa sasa ni dhahiri kabisa inajulikana kuwa alikuwa ni madhabuha au muhanga aliye zaa hukumu ya kutisha ambazo maovu ya wengine yamepatikana (sawa na anavyosema Soncino n. 4-6).

 

Rashi na Kimchi wanashikilia usemi usemao magonjwa unaoonekana katika aya ya 4 ni magonjwa ambayo yangeweza kututesa na usemi wa alichukua ina maana ya kwamba aliitwa ili aweze kuyastahimili (sawa na asemavyo Soncino).

 

Ualelewa wa kuwa Wamataifa wa mfumo wa Kibabeli wanaookolewa kwa kupitia mateso ya Masihi, ambaye kwa kweli ni Israeli wa Mungu, ni kiini vilevile cha Biblia na hasahasa kitabu cha Ufunuo.

 

Mambo yote yanatakiwa yashughulikiwe kwa undani na chini ya majarida ya Fundisho la Dhambi ya Asili na lile la Matatizo yaUovu ambayo yatafuatia jarida hili.

 

Majaribu ya Masihi

Masihi alikamatwa kwa hila za makuhani na baraza la kidini lililojulikana kama Sanhedrin ndivyo vilitumika kwa ajili ya jaribu hili kama ilivyokuwa ni muhimu kuwa na idadi ya kawaida chini ya wanachama 23 wawepo kwa ajili ya kusikiliza mashitaka madogo madogo.

 

Yesu aliwekwa majaribuni mbele ya Anasi kwa kusikia kwamba anataka kuanzisha kitu kipya kama kikundi cha kupingana na baraza hili la Sanhedrin. Hii, kwa kweli, lilikuwa limeisha amuliwa lakini ilikuwa ni lazima katika mwelekeo wa kibaraza lile la sheria, kwa njia hiyo ingeweza kutumika kwa ajili yetu.

 

Yohana 18:12-14 inasema: 12Basi wale askari na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi walimkamata Yesu, wakamfunga. 13Wakamchukua kwa Anasi kwanza maana alikuwa mkwewe Kayafa, yule aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule. 14Naye Kayafa ndiye yule aliyewapa Wayahudi lile shauri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.

 

Mafafanuzi ya kina kuhusu makuhani na tarehe na nyakati yametolewa katika majarida haya mawili yasemayo Majira ya Kusulibiwa na Ufufuo [159] na jingine lisemalo Golgota: Mahali pa Fuvu la Kichwa [217] na Majarida mengine yanayohusiana na Pasaka.mahusiano haya ni kuhani mkuu na ya msaidizi wa kuhani mkuu ingawaje dini ya Kiyahudi hujaribu kufanya matumizi ya mahusiano ya Nasi (aliyekuwa ni mwanachama wa Sanhedrin), yawe kwa siku za mbele kidogo.

 

Mwanazuoni mwingine na mtaalamu wa mambo ya Lugha aitwaye Bullinger anamawazo kama ya kuhani mkuu Anasi alivyokuwa alivyotoa udhuru katika mwaka 779 A.U.C. (AUC ni kwa mujibu ya mapokeo ya hesabu ya miaka ya Warumi iliyokuwa inaanzia mwaka kwanza wa kuanza kwa utukufu wa dola ya Rumi), mwaka ambao huduma ya Masihi ilianza. Wengine watatu kati yao walijiondoka na kupandishwa daraja mbele ya Kayafa aliyechaguliwa na Kaisari Valerius Gratus. Bullinger aliyekuwa ni mwana zuoni maarufu katika maaluma ya mambo ya Lugha,  anadhani kwamba Anasi angepata uzoefu zaidi katika sheria ili kufanya mashitaka kukabili yeye. Huu ilikuwa ni ukweli wa taarifa za mwanzo. Schurer anashikilia kuamini kwamba Kayafa alichaguliwa na kupewa ukuhani na Valerius Gratus (yapata kama mwaka wa 15-26 BK) mwaka upatao kama wa 18 BK na alitawala kuanzia mwaka huu wa 18 hadi wa 26 BK. Ananausi mwana wa Sethi alichaguliwa na Kaisari Quirinius (mwaka 6 BK) na alitawala kuanzia mwaka huu wa 6-15 BK. Makuhani hawa wa tatu ambao walikuwa wanafanya kazi zao kwa nyakati zilezile kwa pamoja kwa mujibu wa rejea za Bullinger bila shaka ni Ismaeli mwana wa Fiabi (waliowekwa kwenye ukuhani mkuu na Kayafa kama mwaka 15-16 BK); Elieza mwana wa Ananus (kama mwaka 16-17 BK) na Simoni mwana wa Camithus (kama mwaka 17-18 BK) wote walichaguliwa Gratus (kwa mujibu wa jarida la Josephus liitwalo Maisha katika Zama za Kale za Wayahudi ama kwa Kiingereza linajulikana kama Antiquities of the Jews, BK. XVIII. II. 2; sawa na Schurer, Vol. II, pp. 216,230). Schurer, anashughulika na swali la Nasi na Ab-beth-din na anashikilia kuamini aikutokea hadi baadae. Anashikilia kuamini kuwa neon Nasi inarejea kwa wahuu wa nchi hadi kwenye majumlisho ya Mishna. Yawezekana ikawa kuwa neon lilikuwa halifanyiki kwa makusudi kabisa katika familia ya Herodi na kuwekwa kwa kuhani mkuu kadiri vile nchi ilivyokuwa imegawanywa, kutokana na kumbukumbu za Mishna. Yuda na Galilaya zilichukuliwa kama milki au nchi mbili tofauti kama tulivyoona hapo juu.

 

Matendo yaliyoandikwa kwenye Injili ya Yohana yanahusu hukumu kubwa na utaratibu wa baraza linaloitwa Sanhedrin na kufanyika kwa njia ya sheria. Kwa hivyo kazi za Anasi zaonekana kuwa kama Ab-beth-din au aliyekuwa kama makamu rais wa lile baraza la Sanhedrin aliyekuwa anafanya kazi kama hakimu wa kushughulika na mashitaka.

 

Mmoja wa wanafunzi wake alikwenda na Masihi hadi alipokuwepo kuhani mkuu.

 

Yohana 18:15-18 inasema: 15Wakamfuata Yesu, Petro na mwanafunzi mwingine. Na mwanafunzi huyo alikuwa amejulikana na Kuhani Mkuu, akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani Mkuu. 16Lakini Petro akasimama nje mlangoni. Basi yule mwanafunzi mwingine aliyejulikana na Kuhani Mkuu akatoka, akasema na mngoja mlango, akamleta Petro ndani. 17Basi yule kijakazi aliyekuwa mngoja mlango akamwambia Petro, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi mmoja wapo wa mtu huyu? Naye akasema, Si mimi. 18Na wale watumwa na watumishi walikuwa wakisimama, wamefanya moto wa makaa, maana ilikuwa baridi; wakawa wakikota moto. Petro naye alikuwapo pamoja nao, anakota moto.

 

Akamchukua Patro hadi behewani na mjakazi au mlinda mlango aliyemshuku kuwa alikuwa mmojawapo wa wanafunzi wa Kristo (wajakazi wanawake walikuwa sio watu wa kawaida; mfano ilivyo kwenye 2Sam. 4:6 LXX; Matendo 12:13). Halafu ikafuatia ukano wa Petro. mwanafunzi mwingine hakupewa changamoto lakini anaonekana kuwa anaelewa kama neno lililokuwa linatumika na Petro inaelekea kuwa ilikuwa ni hivyo. Huyu hakuwa ni Yohana ambaye akijiita kila mara Mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda sana (Yoh. 13:23; 19:26; 21:7,20). Mwanafunzi huyu pengine alikuwa ni Nikodemo au Yusufu wa Arimathaya ambao wote walikuwa ni wanachama katika lile baraza la Sanhedrin (sawa kama isemavyo Biblia iitwayo Bullinger Companion Bible, n. to v. 15).

 

Neno lililoko katika aya ya 18 linamaana hasa ya watumwa na wasaidizi wa watumishi na maafisa. Chiliarch na askari wa kirumi walikuwa wameenda wameenda nyuma ya ngomeni Antonia akamwacha Masihi mikononi mwa Wayahudi.

 

Ili kuutimiliza unabii wa Isaya 53, sasa tunaweza kuona mateso na yanayoelekea mwanzo wa mateso

 

Isaya 18:19-24 inasema: 19Basi Kuhani Mkuu akamwuliza Yesu habari za wanafunzi wake na habari za mafundisho yake. 20Yesu akajibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; siku zote nalifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala kwa siri mimi sikusema neno lo lote. 21Ya nini kuniuliza mimi? Waulize wale waliosikia ni nini niliyo waambia; wao wanajua niliyoyanena. 22Basi aliposema hayo, mtumishi mmojawapo aliyesimama karibu alimpiga Yesu kofi akisema, Wamjibu hivi Kuhani mkuu? 23Yesu akamjibu, Kama nimesema vibaya, ushuhudie ule ubaya; bali kama nimesema vema wanipigia nini? 24Basi Anasi akampeleka hali amefungwa kwa Kayafa, Kuhani Mkuu.

 

Imeandikwa kwamba Usimtukane Mungu (yaani kusema maneno maovu dhidi yake), wala usimlaani mkuu wa watu wako (soma Kut. 22:28; Mhu. 10:20; Matendo 23:5; 2Pet. 2:10; Yuda 1:8 na vilevile Yak. 4:3-Kwa Kiyunani: kakos ina maana ya kukosekana kwa nia mbaya) na, hivyo, kuhani mkuu asiweze kunenewa maovu. Hata hivyo, Kristo hapa alikuwa anakanusha mashitaka ya kwamba amevunja sheria. Alikuwa anakanusha shita la kuwa alikuwa amefanya dhambi na kusema kuwa yeye hakufanya dhambi yoyote.

 

Unabii unasema kuwa yeye hakufunua kinywa chake au alinyamaza kimya kama kondoo mbele zao wakatao manyoya na hii ilitimia kwa msimamo wake mbeke ya Pilato. Kwa hiyo, hakujitetea mwenyewe lakini tena kwa ufasaha sana alitoa majibu. Je, huu ulikuwa ni ugomvi? Hapana, haukuwa hivyo. Majibu aliyokuwa ameyatoa ambayo yalikanusha kwa nguvu mashitaka haya ya uvunjaji wa sheria yalikuwa yana nguvu katika kutoa mfano uhusuo jinsi ya kuenenda mbele ya mamlaka. Kama asingeyaji yote haya basi ingekuwa ni vibaya zaidi. Mfano wa historia ingekuwa umeharibu kabisa utaratibu wa kijamii miongoni mwa makundi ya Kikristo mbele ya utaratibu wa kisheria. Ilibidi Injili hizi nne ziweke mfano kulingana na mujibu wa sheria za kibiblia.

 

Anasi alienda mbele kupitia hisia za maandalizi ya shitaka na kumpeleka mbele ya Sanhedrin na kumrudisha kwa kuhani mkuu mhusika mwenyewe anayestahili yaani Yosefu Kayafa.

 

Petro alisema tena.

Yohana 18:25-27 inasema: 25Na Simoni Petro alikuwa akisimama huko, anakota moto. Basi wakamwambia, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi wake mmoja wapo? Naye akakana, akasema, Si mimi. 26Mtumwa mmojawapo wa Kuhani Mkuu, naye ni jamaa yake yule aliyekatwa sikio na Petro, akasema, Je! Mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye? 27Basi Petro akakana tena, na mara akawika jimbi.

 

Hapa tunamwona Petro, akijaribiwa tu na wanajamii, akamkana Kristo kama Kristo alivyokuwa amemwambia kabla kuwa angefanya na baadae jimbi akawika kumuashiria mwisho wa jaribu hili lililotokea ghafla. Sisi sote tulipaswa kujifunza somo kutokana na kuyatazama majaribu yanayolipata Kanisa na wapendwa ndugu zetu wengine na kuwasaidia au vinginevyo tusaidiane kwa kupeana sisi wenyewe kwa wenyewe.

 

Wakati huu wote wa majaribu, tunaona kuwa undani wake ume rukwa kuandikwa katika Injili ya Yohana katikati ya matendo yake katika Yohana 18:27 na maendelezo ya habari hii katika aya ya 28. Habari zaidi kuhusu mahali jambo moja lilipofanyika hadi kufikia sehemu nyingine ipo kati ya Mathayo 26:58 hadi 27:2

 

Mathayo 26:58-75 inasema: 58Na Petro akamfuata akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na mtumishi auone mwisho. 59Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushahidi wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwuua; 60wasiuone ingawa walijitokeza mashahidi wa uongo wengi. 61Hata baadaye wawili wakatokea, wakasema, Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu la Mungu, na kulijenga kwa siku tatu. 62Kisha Kuhani Mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini? 63Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu. 64Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni. 65Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mnahaja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyokufuru yake, 66mwaonaje ninyi? Wakajibu, wakasema, imempasa kuuawa. 67Ndipo wakamtemea mate ya uso, wakampiga makonde; wengine wakampiga makofi, 68wakisema, Ewe Kristo, tufumbulie; ni nani aliyekupiga? 69Na Petro alikuwa ameketi nje behewani, kijakazi mmoja akamwendea, akasema Wewe nawe ulikuwepo pamoja na Yesu wa Galilaya. 70Akakana mbele ya wote, akisema, Sijui msemalo. 71Naye alipotoka nje hata ukumbini, mwanamke mwingine alimwona, akawaambia watu waliokuwako huko, Huyu alikuwapo pamoja na Yesu Mnazareti. 72Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu. 73Punde kidogo, wale waliohudhuria akamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u-mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha. 74Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema, Simjui mtu huyu. Na mara akawika jogoo. 75Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.

 

Kwa hiyo, kuanzia majaribu haya hadi kufikia mwisho wa majaribu ya Petro, tunaona matukio haya katika Mathayo 27:1-2 yanatufikisha hadi kwenye Yohana 18:28.

Mathayo 27:1-2 inasema: Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua, 2wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa Pilato aliyekuwa liwali.

 

Yohana anatuonyesha kuwa hawakupenda kujitia unajisi kwa kufanya mahusiano na Watu wa Mataifa kama Mafarisayo pia walivyokuwa walivyoruhusu mapokeo yao yaharibu watu kuzielewa sheria.

 

Yohana 18:28-40 inasema: 28Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpka Praitorio, nayo ikawa alfajiri lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile Praitorio, wasije wakanajisika bali wapate kuila Pasaka. 29Basi Pilato akawatokea nje, akasema, Ni mashitaka gani mnayoleta juu ya mtu huyu? 30Wakajibu, wakamwambia, Kama huyu asingekuwa mtenda mabaya, tusingemleta kwako. 31Basi  Pilato akawaambia, Haya! Mtwaeni ninyi, mkamhukumu kwa ile torati yenu! Wayahudi wakamwambia, Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu. 32Ili litimie lile lake Yesu alilolisema, akionyesha ni mauti gani atakayokufa. 33Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi? 34Yesu akamjibu, Wewe wasema wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine wamekuambia habari zangu? 35Pilato akamjibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu, Umefanya nini? 36Yesu akamjibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini mfalme wangu sio wa hapa. 37Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu. 38Pilato akamwaambia, Kweli ni nini? Naye akiisha kusema neno hilo akawatokea Wayahudi tena, akawaambia, Mimi sioni hatia yo yote kwake. 39Lakini kuna desturi ya mimi kuwafungulia mtu mmoja wakati wa Pasaka; basi mwapenda niwafungulie Mfalme wa Wayahudi? 40Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa ni mnyang’anyi.

 

Sehemu hii ni mojawapo ya mfano wenye nguvu kuliko yote katika Biblia. Hapa kwa mujibu wa yasemavyo Maandiko Matakatifu, tunaona kuwa Masihi kama mfalme aliyejaribiwa kwa ajili ya dhambi za kujaribiwa na wakuu wa watu wa Mataifa ambao wamesifiwa kutozishika sheria kabisa na kuuawa na Yuda na baraza la Sanhedrin kufanya katika mafundisho ya Mafarisayo na baraza la utawala. Kwa hiyo, walikuwa wanahukumiwa.

 

Imeandikwa, usipokee rushwa na kupotoa hukumu. Aya hii inasema hivi kwa ujumla: “Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwahupofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya mwenye haki”.

Kutoka 23:1-9 inasema: Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu, kuwa shahidi wa udhalimu. 2Usiandamane na mkutano kutenda uovu, wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu. 3Wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake. 4Ukimwona ng’ombe wa adui wako, au punda wake, ameotea, sharti umrudishie mwenyewe tena. 5Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye hali ameanguka chini ya mzigo wake, nawe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie. 6Usipotoe hukumu ya mtu maskini katika neno lake. 7Jiyenge mbali na neno la uongo; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu. 8Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki. 9Usimwonee mgeni, maana, ninyi mwajua moyo wa mgeni ulivyo, kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.

 

Hukmu imasayo mtu aliye potosha hukumu iliondolewa katika hukumu na hiyo ndiyo ilikuwa ni adhabu na hiyo ndiyo ilikuwa ndio hukumu ya baraza la Sanhedrin. Hukumu iliondolewa kwao na likapewa Kanisa. Pia iliondolewa na kupewa kwa mataifa ili kuonyesha tunda lake, kama Kristo alivyosema hatimaye, taifa ambalo linaonekana kuwa ni Israeli zaidi ya Yuda.

Mambo ya Walawi 19:15-16 inasema:15Msitende yasiyohaki katika hukumu, msimpendee mtu masikini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhumu jirani yako kwa haki. 16Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usisimame kinyume cha damu ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.

 

Kwa hiyo, hukumu inatakiwa itolewe katika nchi kwa kufuata haki.

 

Kumbukumbu la Torati 16:18-20 inasema:18Weka waamuzi na maakida katika malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako, kwa hesabu ya kabila zako, nao wawaamuu watu kwa maamuzi ya haki. 18Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usiitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya mwenye haki. 20Yaliyo haki kabisa ndiyo utakayoyafuata, ili upate kuishi na kuirithi nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.

 

Ilikuwa ni haki ya kimamlaka ya baraza la Sanhedrin na makuhani kumhukumu Masihi. Lakini ni lazima iwe ni mambo yanayohusu hukumu au utmwa.

 

Kumbukumbu la Torati 17:8-13 inasema: 8ikiwa limezuka neno lililo zito kukupita wewe, katika maamuzi kati ya damu na damu, na kati ya daawa na daawa, na kati ya pigo kwa pigo, nayo yashindaniwa katika malango yako; ndipo nawe uondoke, ukwee uende mahali atakapopachagua BWANA, Mungu wako; 9uwaendee makuhani walawi, na mwaamuzi atakayekuwako siku hizo; waulize nao watakuosha hukumu ya waamuzi; 10nawe fanya sawasawa na hukumu watakayokuonyesha mahali hapo atakapochagua BWANA; nawe tunza kufanya kwa mfano wa yote watakayokufunza; 11kwa mfano wa sheria watakayokufunza, fanya hivyo; usigeuke katika hukumu watakayokuonyesha, kwenda, mkono wa kuume wala wakushoto. 12Na mtu afanyaye kwa kujikinai, kwa kutomsikiliza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia BWANA, Mungu wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli. 13Na hao watu wote watasikia na kuogopa, wasitende tena kwa kujikinai.

 

Waliamriwa na Mungu chini ya sheria kuonyesha sentenso inayoonyesha kwanza hukumu na hawakufanya hivyo.

 

Wakampa ahukumu watu wa Mataifa na kwa Pilato. Wakamtoa kwa Pilato katika Praitorio kwenye nyumba ya uliwali (kama isemavyo Marko 15:16) au Chumba cha Hukumu ambaco kilikuwa sio nyumbani kwa Herode kama tunavyosoma katika Luka 23:7.

 

Walimwambia Pilato kuwa kama asingekuwa hana kosa yaani mtu mwema basi wasingemtoa kwa Pilato (Yoh. 18:30). Walipomwuliza kama yeye alikuwa mfalme aliwajibu: 

Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.

 

Pilato kwa kuwa alikuwa ameelimishwa na serikali na kuwa ni mwana zuoni wa Teolojia akasema kweli ninini? Kwa kuwa alikuwa bado alikuwa haijui kweli. Unapaswa uitwe kwanza na Mungu ili kupata ufahamu. Kisha Pilato akaenda nje walikokuwa Wayahudi na akasema: silioni kosa lolote kwa mtu huyu.

 

Wlikuwa wamepewa nafasi ya kuangalia tena hukumu yao iliyokuwa sio ya haki kupitia midomo ya watu wa Mataifa waliowadharau na kuwahesabia kuwa hawastahili kuingia Hekaluni.

 

Pilato aliwapa fursa ya kumwachilia Kristo na wakapewa uchaguzi lakini hapa mabadilishano makubwa yasiyo tarajiwa na ya kihistoria yalichukua mkondo wake.

 

walipiga kelele wakisema sio mtu huyu wa kumwachia bali mwachilie Baraba mtu aliyekuwa mnyang’anyi. Jina Baraba maana yake ni mtoto wa baba.

 

Mfano hapa ilikuwa ni kwamba Krista alikufa ili kwamba sisi tuwekwe huru kama mtoto wa Baba.

 

Kabla ya kufuata hatua hiyo, kisha akafuata njia kwa nguvu zote ambapo Rumi ilikuwa ni maarufu, Pilato alijaribu kuwafuatilia tena.

Yohana 19:1-7 inasema: Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi. 2Nao askari wakaokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau. 3Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi. 4Kisha Pilato akatokea tena nje, akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpatekuona kufahamu ya kuwa mimi sioni hatia yo yote kwake 5Ndipo Yesu alipotoka nje, amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, Tazama, mtu huyu! 6Basi wale wakuu wa makuhani na watumishi wao walipomwona, walipiga kelele wakisema, Msulibishe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi basi, mkamsulibishe kwa maana mimi sioni hatia kwake. 7Wayahudi wakamjibu, Sisis tunayo sheria na kwa sheria hiyo anastahili kufa, kwa sababu alijifanya Mwana wa Mungu.

 

Hawakumsikiliza na kusema kuwa amejifanya mwenyewe kuwa ni mwana wa Mungu. Kwa hiyo Pilato alikuwa mwangalifu sana akifahamu kuwa alikuwa anashughulikia mabishano ya kidini ambayo kwama mtu huyu sio tu kwamba alikuwa tu hakuwa na kosa bali pengine huenda alikuwa na mungu mdogo. Hii ilitokana na imani za Warumi na Wayunani kama ilivyo ile ya Wahindu wanaoamini kuwa mungu yaani elohim au theoi alikuwa na uweza wa kufanya makao na wanadamu na kuonekana kama mwanadamu aliye wa uzao wa kimbinguni. Haya ndio mashitaka ambayo kwayo baraza la Sanhedrin walilokuwa wameling’ang’ania zadi kama tunavyojionea katika Mathayo 26:65-66 (pia tazama Wal. 24:16).

 

Hali hii ya kukufuru ilidaiwa imefanyika dhidi ya jina la Mungu tena kwa kujifanya kuwa yeye ni mwana wa Mungu na hii ilichukuliwa kutoka katika Malaki na kuifanya kama matamko ya kweli pale iniposema Je! Sisi sote hatuna baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu?

 

Malaki 2:10 inasema: 10Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda ndugu yake mambo ya hiana, tukilinajisi agano la baba zetu?

 

Kristo alijitetea mwenyewe kabla hata mashitaka hayajaa anza kutolewa.

Yohana 10:33-38 inasema: 33Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa saababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. 34Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika totati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? 35Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu, (na maandiko hayawezi kutanguka); 36je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Umekufuru; kwa sababu nalisema, Mini ni Mwana wa Mungu? 37Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini; 38lakini nikizitenda, hamniamini mimi, ziaminini zile kazi; mpate kujua na kufahamu ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba.

 

Mashtaka haya hayakuwa na msingi wowote na yalituama katika hali ya ujinga wa Wayahudi kwa ajili ya kutojua maandiko yaani sheria wala kutojua mpango wa Mungu. Kwa njia kama hiyohiyo, basi mashitaka ya hovyo yanaletwa dhidi ya wateule siku za leo kwa jina la Ukristo na na wamejiunga pamoja ili kuwauwa kwa muda wa karne nyingi kama walivyofanya kwa Masihi mbele za wateule.

 

Pilato alijaribu kumwachilia tena kwa kusema maneno haya.

 

Yohana 19:8-11 inavyosema: 8Basi Pilato aliposikia neno hilo, akazidi kuogopa. 9Akampiga tena ndani ya Praitorio, akamwambia Yesu, Wewe umetokapi? Lakini Yesu hakumpa jibu lolote. 10Basi Pilato akamwambia, husemi nami? Hujui kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua, nami nina mamlaka ya kukusulibisha? 11Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mkononi mwako yuna dhambi iliyokuu zaidi.

 

Uweza aliokuwa amepewa Pilato ulitoka kwa Mungu. Serikali zote zinazotawala zimeruhusiwa na Mungu kwa ajili ya wateule. Wakati wowote mashitaka ya uwongo au yanapotolewa kwa nia ya kutuhukumu kupitia mashitaka ya uwongo au hukumu isiyo ya haki huchukuliwa kama ni dhmbi kuu sana.

 

Pilato alijitahidi sana kutafuta njia ya kumwachilia Masihi lakini Wayahudi hawakuweza kumsikiliza kabisa wala kumuelewa analolisema. Iwapo kama alikuwa yuko sahihi, walisimama na kumshutumu kwa kutumia sheria ambazo walikuwa wamezigeuza kinyume chake.

 

Yohana 19:12-16 inasema: 12Na tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua, lakini Wayahudi wakapiga makelele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari, kila mtu ajifanyaye kuwa mfalme humfitini Kaisari. 13Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha. 14Nayo ilikuwa maandalio ya Pasaka, yapata saa sita. Akawaambia, Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu! 15Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalame ila Kaisari. 16Basi alipomtia mikononi mwao ili asulibiwe; nao wakampokea Yesu.

 

Kifungu hiki cha kusulibiwa kwenye Injiliya Yohana kinajulikana vizuri sana.

 

Yohana 19:17-22 inasema: 17Akatoka, ali amejichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, na kwa kiebrania Golgotha. 18Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pmoja naye, mmoja huku na mwingine huku, na Yesu katikati. 19Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. 20Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi, maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karihu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani. 21Basi wakuu wa makuhani na Wayahudi wakamwambia Pilato, Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; bali ya kwamba yule alisema, Mimi ni mfalme wa Wayahudi. 22Pilato akajibu, Niliyoandika nimeandika.

 

Usemi huu hapa inaosema huenda kwa upande mmoja. kwa hakika unasemea kinachoitwa enteuthen kai enteuthen yenye maana ya huku na huko kwa tafsiri ya Kiingereza cha zamani. Jambo hili lime fafanuliwa vizuri katika jarida linalosema Msalaba:Chanzo chake na Maana yake [039].

 

Pilato alililazimika kuandika tangazo hili sio kwa sababu ya Roho Mtakatifu, lakini alishawishika na kukubaliana na hali jinsi Masihi alivyokuwa hana hatia na kuona kuwa yeye alikuwa ni bora na mfalme aliyekuwa bora zaidi sana aliye kuwa na huu umati wa watu wasio na haki wanao tafuta kwa kupitia makuhani wao mtu mwema asiye na hatia.

 

Unabii bado unaendelea kutimia kwa kadiri vile kusulibiwa kunavyoendelea.

 

Yohana 19:23-24 inasema: 23Nao askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake, na kanzu nayo, Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu. 24Basi wakaambiana, Tusipasue, lakini tupigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile lisemalo, Wakagawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari.

 

Hii ilitendeka ili kutimiza unabii ulio katika maandiko ya Zaburi 22:18.

 

Zaburi 22:1-8 inasema:Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona u mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu? 2Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hunijibu Na wakati wa usiku lakini sipati raha. 3Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli. 4Baba zetu walikutumaini Wewe, Walitumaini, na Wewe ukawaokoa. 5Walikulilia Wewe wakaokoka, Walikutumaini wasiaibike. 6Lakini mimi ni mdudu wala si mtu, Laumu la wanadamu na mzaha wa watu. 7Wote wanionao hunicheka sana, Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao; 8Husema, Umtegemee BWANA; na amponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye.

 

Hapa tunaona matamko ya Kristo yameorodheshwa katika unabii. Kuanzia aya ya 1, tunaona kilio chake akiwa msalabani. Tunaona katika Zaburi 22:8 ikinukuliwa katika Mathayo 27:43; Marko 15:29; Luka 23:25.

 

Katika Zaburi 22:18 tunaona unabii unaotabiri kuwa watagawana vazi lake kwa kulipigia kura.

 

Katika Zabusri 22:22, tunaona unabii ukinukuliwa kama unavyosema katika waraka kwa Waebrania 2:12.

 

Zaburi 22:22-31 inasema hivi: 22Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu, Katikati ya kusanyiko nitakusifu. 23Ninyi mnaomcha BWANA, msifuni, Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo, mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazao wa Israeli. 24Maana hakulidharau teso la mteswa, Wala hakuchukizwa nalo; Wala hakumficha uso wake, Bali alipomlilia akamsikia. 25Kwako zinatoka sifa zangu Katika kusanyiko kubwa. Nitaziondoa nadhiri zangu Mbele yao wamchao. 26Wapole watakula na kushiba Wamfuatao BWANA watamsifu; Mioyo yenu na iishi milele. 27Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia. 28Maana ufalme wa BWANA, Naye ndiye awatawalaye mataifa. 29Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, humwinamia wote washukao mavumbini; Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake. 30Wazao wake watamtumikia. Zitasimuliwa habari za BWANA, 31Kwa kizazi kitakachokuja, Nao watawahubiri watakao zaliwa haki yake, Ya kwamba ndiye aliyefanya.

 

Tunaona katika Zaburi kwamba Mungu hakuugeuza uso wake kutoka kwa Masihi na wala hakumuacha kama inavyodhniwa mara nyingi kwa sababu ya kunukuu kutoka Zaburi 22:1 lakini Mungu alimuokoa.

 

Waraka kwa Waebrania unatuonyesha sababu za kutolewa dhabihu.

Waebrania 2:10-18 unasema : 10Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo , akileta wana wengi waufikie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso. 11Maana yeye atakasaye na hao waliotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ngudu zake. 12Alisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa. 13Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye, Na tena, Tazama mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu. 14Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti yaani Ibilisi, 15awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. 16Maana ni hakika, haitwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. 17Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. 18Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wanaomkaribia.

 

Kwahiyo basi, mwana kondoo aliruhusiwa achinjwe kwa sababu kwa kifo chake wengi wangeweza kupatikana kwa njia ya imani na kuamini kwao.

 

Ni kwa nini basi Mwana Kondoo huyu wa Mungu ajivulie ule uweza wake wa Kimungu ambao kwayo aliishi kabla hata ya kuzaliwa kwake katika asili ya kiroho na kufanyika mwanadamu lakini asiyeona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho lakini alijinyenyekesha hata kufa, naam, mauti ya msalaba (kama isemavyo Flp 2:5-8).

 

Ni kwa nini basi Mungu anataka dhabihu ya damu-hata kiasi cha kutaka hata ya Mwna wake wa pekee? Hapana! Si kwamba yeye anatamani sana dhabihu.

 

Hosea 6:4-7 inasema: 4Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utokao mapema. 5Kwa sababu hiyo nimewakata kata kwa vinywa vya manabii, nimewauwa kwa maneno ya kinywa changu, na hukumu yangu itatokea kama mwanga. 6Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka ya kuteketezwa. 7Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana.

 

Tuliliona pia wazo hili katika 1Samweli 15:22, Mhubiri 5:1 na Mika 6:8. Tunaona jinsi Samweli anavysema kuwa Mungu anachohitaji ni utii kuliko hata dhabihu. Utii huu ni wa muhimu katika kuuingia uzima wa milele. Uasi ni uvunjaji wa sheria na uvunjaji wa sheria ni dhambi na mshahara wa dhambi ni mauti.

 

Kwa hiyo, upatanisho unahitajika kwa ajili ya uzima wa milele. Ili kuwezeshwa kupatanishwa, tunatakiwa tuwe watii kwa Mungu na kwa sheria zake amazo zinatangulia kwenyw uasili wake (sawa na yasemavyo majarida yasemayo Serikali ya Mungu, Na. 174; na lile linalosema  Upendo na Utaratibu wa Sheria [200].

 

Utii ulienea hadi kwa Yesu Kristo. Ili viumbe waweze kupatanishwa, ilimpasa Kristo ayatoe maisha yake kwa hiyari yake mwenyewe na awe mwanadamu mwenye mwili ili awe na sisi na ajaribiwe kama tulivyofanya sisi. Mungu hakuhitaji dhabihu; alichohitaji kilikuwa ni utii kwa watoto wake wote. Ili awe tayari kutuongoza, ilimpasa Kristo atuonyeshe jinsi alivyokuwa mtii hadi kufikia mauti. Shetani hakuwa na wala hatapata kuwa na utii wa kiasi hicho.

 

Hii ni kazi ya kifo cha Masihi. Hakutofikia kutosheleza baadhi ya mawazo yaliyohitajika ya Mungu. Ama kifo cha Masihi, kwa baadhi ya mawazo ya kipagani yasiyo ya kibiblia huweka mbele katika kuyachanganya Maandiko Matakatifu kama ilivyokuwa kwa baadhi ya vikundi vya bizarre vilivyodai kuwa katika siku za hivi karibuni.

 

Kifo cha masihi kwa kujitoa dhabihu ya hiyari yake mwenyewe ilikuwa ni muhimu ili kuweza kutupatanisha na Mungu, kwa viumbe wa sehemu zote mbili yaani walioko mbinguni na walioko duniani. Njia pekee ambayo ingaliyoweza kufanyika ilikuwa ni kwa mmoja wapo wa Malaika wa Jeshi la Mbinguni akubali kuiachilia nafasi yake kule mbinguni na aeonian ya maisha yake ili afanyike mwanadamu awezaye kufa (tazama majarida yasemayo Hali ya Kutokufa [165]; na ile ya Kusudi la Uumbaji na Dhabihu ya Kristo [160].

 

Kristo ilimbidi aweke mamlaka na uweza wake mbali ili ajitayarishe kufa kwa ajili yake. Ni kwa njia ile tu ingewezekana kuongoza hii.

 

Aina hii hii ya majaribu inatakiwa kwa wateule nandio maana tumekuwa tukijaribiwa na kuuwa nje ya matuo kama vile yeye mwenyewe alivyouawa nje ya matuo. Kwa kuwa tunautarajia mji wa Mungu na utendaji wa serikali ya Yesu Kristo wakati atakaporudi hapa duniani akiwa kama Mfalme Mshindi.

 

Waebrania 13:5-16 inasema: 5Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. 6Hata twa thubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa Mwanadamu atanitenda nini? 7Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neon la Mungu, tena kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao. 8Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele. 9Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni, maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo hao waliokwenda navyo hawakupata faida. 10Tuna madhabahu ambao wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake. 11Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi. 12Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango. 13Basi tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake. 14Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. 15Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamalo jina lake. 16Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.

 

Wakati Paulo alipoandika haya, Hekalu lilikuwa linatenda kazi zake zote kikamilifu. Somo la kujadiliana ni swali la dhabihu na kazi yake kwa wateule na pengine wanyama waliuawa.

 

Kumbuka kuwa sisi ni Hekalu la Mungu na wale watumikao madhabahuni na dhabihu zake hawana haki kula katika madhabahu yetu. Aliteswa nje ya matuo ili kwamba damu yake iweze kuwatakasa watu, na sio kwa ajili ya kutosheleza hitaji la sadaka la Baba.

 

Mfumo mzima wa utoaji dhabihu uliwekwa kwemye mahali pa kuelekezea mteule na Masihi kama kiongozi wa serikali ya Mungu. Idadi yao pamoja ujalizio kwa wakati wote wa mwaka vilikuwa na maana zake maalumu. Mungu hayumo miongoni mwao wasababisha huzuni wanaotaka kila wakati watu wauawe. Atatuita ili tuheshimu sheria zake. Matokeo ya kutozitii yaani kuziasi ni kifo na kuukosa uzima wa milele ambao hautaweza kuwa na sehemu kwa wale wote walio wana wa uasi. Hii ndiyo maana ya kuwa kuna aina mbili za ufufuo wa wafu (soma Ufunuo 20:4-15). Wateule sehemu yao ni katika ule ufufo wa kwanza na uzima wa milele kwa kupitia utii wao na imani yao waliyoiweka kwa Kristo. Imani pasipokuwa na matendo imani hiyo imekufa (Yak. 2:20-26) nasi kwa kupitia matendo yetu tutaonyesha imani yetu (Yak. 2:18) na matendo yetu ni utii kwa Mungu aliye hai kama Masihi alivyoonyesha ili kuumfanya aweze kuwa mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu (Kol. 1:18) na kuwa mwana wa Mungu kwa uweza kupitia Roho Mtakatifu kwa kufufka kwake toka kwa wafu (Rum. 1:4).

 

Kwa hiyo sasa tunaweza kuona kuwa kusulibiwa na kifo cha Mwana Kondoo vilikuwa ni hatua za kuhitimisha wa historia yote hadi kufikia hatua ile na unabii wote. Katika siku ile, ulimwengu mzima na maanguko yake vililitulia mabegani kwa mtu yule aliyefanyika kuwa dhabihu isiyo na hila. Alikubali kuyatoa maisha yake kwa ajili yetu kwa kuwa imeandikwa Nawe mpende jirani yako kama unavyoji penda mwenyewe na hii ndiyo amri ya pili iliyo kuu (soma Mat.19:19). Hii ilijaribiwa hadi mwisho kwa ajili ya upendo mkuu na kamwe hakuna mtu mwingune yeyote zaidi ya huyu aliyekubali kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki yake (Yoh. 15:13). Kwa kuwa Mungu ni upendo (l Yoh. 4:8).

 

Yohana 19:25-42 inaonyesha mwandamano wa matukio katika matendo yake ya mwisho kama mwanadamu. Mtu aliyemkumbuka kumuandalia hatima yake ya maisha yaliyokuwa yamebakia alikuwa ni mama yake. Alihesabiwa pamoja na hatima itakalolipata Kanisa hivyo iliamriwa atunzwe smbamba na Kanisa. Ndugu zake wengine ni dhahiri kuwa hawakufika na kuwepo pale msalabani alipokuwa; ni mama yake tu na shangazi yake ndio walisimama pale pamoja na mtume Yohana ambaye masuala yote ya namna gani atatunzwa alikabidhiwa yote huyu mtume Yohana. Pia ujulikane kwamba inaonekana kuwa Yohana alikuwa na tabia ya ukarimu miongoni mwa ndugu na aliishi na ndugu waliosalia na alimtunza huyu mama hadi alipofikia umri wa uzee.

 

Yohana 19:25-27 inasema hivi: 25Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mama, Mariamu wa Klopa na Mariamu Magdalene. 26Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. 27Kisha akamwabia yule mwanafumzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.

 

Sasa mambo yote yalikuwa yamekamilika isipokuwa kwa nabii chache tu. Moja wapo wa jumbe hizo wa kinabii ulikuwa ni ule wa kwamba aliyakiwa achomwe mkuki.

 

Zekaria 12:8-14 inasema:8Katika siku hiyo BWANA atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliyedhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo numba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa BWANA mbele yao. 9Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakao kuwa wapigana na Yerusalemu. 10Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yeruisalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye wlimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; noa wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza. 11Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido. 12Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake, jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao, peke yao; 13jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao. 14Jamaa ya nymba zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao.

 

Katika unabii huu tunaona imeandikwa kuwa malaika wa Yehova atakuwa katika kichwa cha nyumba yoteya Daudi kwa sababu elohim alitokea kwenye nyumba ya Daudi chini yake. Kisha watamtazama yeye waliyekuwa wamemchoma nao watamwombolezea. Walimchoma elohim aliyetumwa kwao na wataomboleza kama vile mtu aombolezavyo kwa ajili ya mwana wake wa pekee. Hakutakuwa na mwingine awayeyote atakayetumwa ulimwenguni. Alikuwa mstari wa uzao wa Daudi kupitia Nathan (mstari wa uzao wa Mariamu katika Luka 3) na Lawi kupitia Shimei (ambayo ulikuwa ni mstari unaoonekana kama wa Mariamu na Elizabethi mama wa Yohana Mbatizaji kupitia kwa mababuzao wanaofahamika).

 

Yohana 19:28-37 inasema: 28Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona liu. 29Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani. 30Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, imekwisha, Akainama kichwa, akasalimu roho yake. 31Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili silale juu ya misalaba siku ya Sabato, (maana Sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao isivunjwe wakaondolewe. 32Basi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulibiwa pamoja naye. 33Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; 34lakini askari mmoja wapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara akatoka damu na maji. 35Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema kweli ili ninyi nanyi mpate kusadiki. 36Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie; Hapana mfupa wake utakao vunjwa. 37Na tena andiko lingine lanena. Watamtazama yeye waliye mchoma.

 

Kwa hiyo, alichomwa na alimtoa Roho Mtakatifu.

 

Ilikuwa ni saa tisa au 9 alasiri wakati mwana kondoo alitakiwa auawe. Giza likaifunika nchi kwa wakati huu kuanzia alasiri au saa sita hata saa la tisa (Mathayo 27:45; Marko 15:43).

 

Mathayo 27:39-54 inasema: 39Nao waliokuwa wanapita njiani wakamtukana, wakitikisa tikisa vichwa vyao, wakisema, 40Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani. 41Kadhalika na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, Aliokoa wengine hawezi kujiokoa mwenyewe. 42Yeye mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini. 43Amemtegemea Mungu; na amwokoa sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu. 44Pia wale wanyang’anyi waliosulibiwa pamoja naye walimshutumu vile vile. 45Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. 46Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? 47Na baadhi yao waliohudhuria, waliposikia, walisema, Huyu anamwita Eliya. 48Mara mmoja wao akaenda mbio akatwaa sifongo, akaijaza siki akitia juu ya mwanzi, akamnywesha. 49Wale wengine wakasema, Acha, na tuone kama Eliya atakuja kumwokoa. 50Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu akaitoa roho yake. 51Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; 52makaburi yakafunuka; ikaimuka miili mingi ya watakatifu walio lala, 53nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi. 54Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye walimlinda Yesu, waliopoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika wakaogopa sana wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.

 

Kifungu hiki cha Maandiko Matakatifu kinahusisha mwandamano wa matukio kwa ajili ya matendo ya Yohana na kufanya baadhi ya misisitizo. Tunaona katika kifungu kwamba, wakati Roho Mtakatifu alipotolewa na Kristo akafa, pazia la hekalu kikipasuka vipande viwili. Hapa tuliona kusudi ya kweli ya kusulibiwa umefunuliwa kimwili. Hadi wakati ule tu kuhani mkuu aliingia Patakatifu pa Patakatifu na kisha ni mara moja tu kwa mwaka na ni kwa damu tu iliyo mwelekeza au kumwakilisha Kristo kama Masihi na kifo chake hadi kufikia hatua hii. Wakati Masihi alipokufa, alifungulia njia ya kuingia Patakatifu pa Patakatifu ili kwamba tuweze kuwa na ujasiri kukiendea kiti cha enzi cha rehema na kufanya maombezi na dua ya kuwaombea wengine kama Kristo alivyotuombea. Tunafanya haya hadi pale sisi wenyewe tunamiminwa kama sadaka ya kinywaji kwa Bwana. Ufufuo ule uliotokea unahushisha watakatifu hawa wailikuwa na utaratibu mmoja kama wa Lazaro, ambao ulikuwa ni ufufuo wa maisha ya kimwili. Hawakufanya hivyo, kama baadhi ya Waadiventista wanavyodai, kuhusu kupalizwa mbinguni.

 

Baada ya hii, ilimshusha chini kutoka Msalabani na kuzikwa kama Siku Takatifu walikuwa karibu kuanza

.

Yohana 19:38-42 inasema: 38Hata baada ya hayo Yusufu wa Arimathaya, naye ni mwanafunzi wa Yesu, (lakini kwa siri, kwa hofu ya Wayahudi) akamwomba Pilato ruhusa ili auondoe mwili wake Yesu. Na Pilato akampa ruhusa. Basi akaenda, akauondoa mwili wake. 39Akaenda Nikodemo naye, (yule aliyemwendea usiku hapo kwanza). Akaleta mchanganyiko wa manemane na uudi yapata ratli mia. 40Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakamfunga sanda ya kitani pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika. 41Na palepale aliposulibiwa palikuwa na bustani na ndani ya bustani mna kaburi jipya haijatiwa bado mtu yeyote ndani yake. 42Humo basi, kwa sababu ya maandalio ya Wayahudi, wakamweka Yesu, maana lile kaburi lilikuwa karibu.……….

 

Alikuwa ni mwana kondoo na aliwekwa katika kaburi ambapo angebakia kwa muda wa siku tatu kamili yaani mchana kamili tatu na usiku kamili tatu kuanzia mwanzo wa siku ya 15 Nisani yapata saa 12:00 adhuhuri, siku ya Jumatano katika mwaka ule wa 30 BK na alibakia pale hadi Jumamosi adhuhuri ya saa 12 adhuhuri ikiwa ni mwishoni mwa siku ya 17 Nisani akijiandaa kupaa kwenda mbinguni yapata saa 3 asubuhi yaani siku ya Jumapili asubuhi akiwa kama Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa.

 

q