Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[249]

 

 

 

Changamoto ya Roma:

Kwa nini Waprotestanti Wanaiadhimisha Jumapili?

(Toleo La 2.0 19980701-20080217)

 

Hii ni jarida la zamani sana la Waadventisti linalohusiana na mlolongo au muandamano wa majarida, yaliyochapishwa na Kanisa Katoliki la Roma huko Marekani mwaka wa 1893, ambalo linaonyesha mitazamo yao kwa somo lao lenye kichwa cha maneno Sabato dhidi ya ibada za Jumapili. Linathibitisha sababu ya kwa nini Waprotestanti waabudu siku ya Jumapili na kuifanya kama ni Sabato iliyokubalika.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 1998, 2008 CCG, ed. Wade Cox)

(tr. 2014)

 

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Changamoto ya Roma:

Kwa nini Waprotestanti Wanaiadhimisha Jumapili?



Wakristo wengi wanadhani kuwa Jumapili ni siku iliyothibitishwa na kukubalika kibiblia kuwa siku ya ibada. Kanisa Katoliki la Roma linapinga kuwa lilihamisha ibada ya Kikristo kutoka Sabato ya kibiblia (Jumamosi) na kuwa Jumapili, na hivyo wanajaribu kupinga kwamba mabadiliko yalifanywa kwenye Biblia kwa namna mbili, yaani kwa kukosa uaminifu na kuyakataa au kuyaasi mamlaka ya Wakatoliki. Kama Uprotestanti unataka kuweka kulalia mafundisho yake kwenye Biblia tu, basi ingefanya ibada zake siku ya Jumapili.

 

Idadi ya miaka kadhaa iliyopita, gazeti linalojulikana kama the Catholic Mirror liliandika mfululizo wa makala likijadili haki ya makanisa ya Waprotestanti kuabudu siku za Jumapili. Makala zilielekeza nguvu na hoja zake kwamba mtu asipokuwa tayari kuyakubali mamlaka ya Kanisa Katoliki kwa kuikubali siku ya kuabudu, Wakristo wangeabudu siku ya Jumamosi. Huu ni uchapaji tena wa makala hizo.

 

Mnmo Februari 24, 1893, Halmashauri Kuu ya Waadventisti Wasabato iliiga maamuzi fulani kwa kuitaka serikali na watu waishio Marekani kutokana na maamuzi ya Mahakama Kuu kulitangaza hili kuwa taifa la Kikristo, na kutokana na vifungu vya sheria za Bunge lao katika kutafakari au kupitisha kwake masuala ya kidini, na malalamiko yao dhidi ya kanuni na matokeo yake yote mabaya ya wakati ule. Mnamo mwezi Machi 1893, Jumuia lijulikanalo kama International Religious Liberty Association (Jumuia ya Kimataifa ya Uhuru wa Kidini) ilichapisha maamuzi haya kwenye kipeperushi kilichoandikwa Appeal and Remonstrance yaani Kata Rufaa na Malalamiko. Kwenye mapokezi ya moja ya hizi, mhariri wa gazeti hili la Catholic Mirror la Baltimore, Maryland, alichapisha mfululizo wa makala nne, ziliyoonekana kwenye jarida lile la Septemba 2, 9, 16, na 23, 1893. Hazeti hili la Catholic Mirror lilikuwa ni chombo mahsusi na maalumu kutumiwa na Kaldinari Gibbons na ofisi ya Papa huko Marekani. Majarida haya, kwa hiyo, ingawa hakuna kilichoandikwa kwa mkono wa Kaldinari mwenyewe, ilionekana kwenye zuio hili rasmi, na kama kuonyesha Upapa kwenye somo hili, inakuwa ni changamoto ya wazi kwa Upapa na Uprotestanti na madai ya Papa kuwa Waprotestanti watajibu kwa Papa sababu ya wao kuabudu siku ya Jumapili na pia jinsi wanavyoiadhimisha.

 

Mambo yafuatayo – ukiondoa maneno yanayoandikwa chini ya ukurasa kufafanua, maandiko ya mhariri kwenye viblanketi kuanzia kwenye ukurasa wa 13 na kuishia kwenye ukurasa wa 14, na Vijarida nyongeza viliwi – ni uchapishaji wa kivebu wa machapisho haya, pamoja na kichwa cha maneno kwenye ukurasa wa 2.

 

SABATO YA KIKRISTO

Uzao Halisi wa Muungano wa Roho Mtakatifu na Kanisa Katoliki Mshiriki Mwenza Wake. Madai ya Waprotestanti kwa Upande Wowote Uliopo Ulithibitisha Kuwa Hauna Mashiko wala Chimbuko Lolote, Uliotengenezwa Kibinafsi na Unahilikisha Kimhanga.

(Kutoka Kwenye Jarida la the Catholic Mirror la Septemba 2, 1893.)

Mkazo wetu umetoewa mwito kwenye somo lililo hapo juuu kwenye juma lililopita kwa kupokea kipeperushi chenye kurasa ishirini na moja iliyochapishwa na shirika liitwalo the International Religious Liberty Association yenye kichwa cha maneno kisemacho, "Kata Rufaa na Malalamiko." Iliyochukua ujumbe wa maamuzi yaliyofanywa na Halmashauri Kuu ya Waadventista Wasabato (Februari 24, 1893). Maamuzi haya yanakosoa na kulaumu, na uchungu kama huu, kitendo cha Bunge la Marekani, na ya Mahakama Kuu, kwa kuzishambulia haki za watu kwa kufunga Maonyesho ya Ulimwengu siku ya Jumapili.

Waadventista ndiyo bodi pekee ya Wakristo waaminio Biblia kuwa mi mwalimu wao, ambaye hawezi kuwa na uhakikisho kwenye kurasa zake wa kubadilisha siku kutoka ile ya saba na kuwa siku ya kwanza. Ndipo waliporufaa kwa kichwa cha maneno “Waadventista Wasabato wa Siku ya Saba”. Kanuni za Kardinari inajumuisha kwa kuitenga mbali siku ya Jumapili kwa ajili ya kuifanya siku ya watu wote kumuabudu Mungu, wakishurutishwa na amri chanya ya Mungu Mwenyewe, ikirudiwa kusemwasemwa kwenye vitabu vitakatifu vya Agano la Kale na Jipya, vilivyotiiwa moja kwa moja na wana wa Israeli kwa kipindi cha maelfu ya miaka hadi siku za leo na vikihusika na mafundisho na matendo au kazi za Mwana wa Mungu wakati alipokuwa hapa duniani.

Pande zote mbili kwa pamoja, Waprotestanti wa dunia hii, Waadventista waliyakubali, pamoja na Biblia ileile kama ndiyo mwalimu wao pekee mwenye kuwaongoza na siye ma makosa, kwa matendo yao, tangia kuonekana kwao kwenye karne ya kumi na sita, pamona na kipindi kinachoheshimika kwa matendo na kazi zake kwa Wayahudi mbele ya macho yao hayajaikataa siku iliyotajwa na kuwekwa rasmi kwa ajili ya kumuabudu Mungu na kudhaniwa kwenye kuikanganya kwa wazi amri yake, na siku yake ya kuabudu ambayo haijatajwa kamwe kwa ajili ya lengo lile, kwenye Nakala Takatifu.

Je, ni jukwaa na hoja gani ambayo Waprotestanti haiwasuti karibu kila Jumapili kwa sauti na pasi na lugha chafu zenye huruma kwa kuihalifu Sabato? Ni nani anasahau makelele ya kiutani ya watumishi wa Kiprotestanti kwa urefu au kina chake chote na pumzi za nchi dhidi ya malango yanayofunguliwa ya Maonyesho ya Kiilimwengu ya Jumapili? Maelfu ya maombi na yakusihi yaliyotiwa saini na mamilioni, ili kuiokoa Siku ya Bwana isiharibiwe? Ni hakika kabisa, msisimuko kama huo na makelele kwa jumla na yaliyoenea kote kote yasingeweza kuwepo bila ya kuwa na hoja za nguvu kubwa kwa upingaji kama huo uliosisimua.

A wakati robo zake wakiwa wamepewa majukumu kwenye Maonyesho ya Ulimwengu kwa dini mbalimbali za Kiprotestanti kwa kuthibitisha makala hizo, ni nani anaweza kusahau msisitizo wa maelekezo ya hasira kali za kifikra zilizothibitishwa na ndugu zetu Wapresbaterian, mara tu baada ya kujifunza maamuzi ya Mahakama Kuu ili isiingilie kwenye ufunguzi wa Jumapili? Magazeti yametuambia kwamba walikataa kabisa katukatu kutoa mwanya ulio kwa mujibu wao, au kufunua maboksi yao, wakidai haki ya kuziondoa makala hizi, na hivyo kuyafifisha mawasiliano yote kwa Uthibitisho wa matendo maovu na uvunjifu wa Sabato.

Pasishaka kabisa, ndugu zetu Wakalvini walistahili na walishiriki kuzihurumia dini zote nyingine, ambazo hata kwa vyovyote vile, zilipoteza fursa ya kufanywa kama wafia dini wakithibitika kuwa kwa ushikaji wa Sabato.

Kwa hiyo basi wakawa "miwani kwa ulimwengu, malaika, na kwa watu," ingawa ndugu Waprotestanti, walioshindwa kushiriki ukiritimba, wakati zilipotolewa pasi kubadilishwa kabisa na kwa nia ya kuutoa usimamaji wao imara na imani yao kwenye kanuni za kidini, kwa majivuno na majigambo ya Kifarisayo na ukaidi wenye madhara.

Nia yetu kuitoa malaka hii ni kuimulika nuru kama hii kwenye swali hili lote la muhimu (kwa pale ambapo swali kuhusu Sabato linaweza kuondolewa kutokana kwenye mimbari za Waprotestanti, dini zijisikie zimepotea, na wahubiri wanyimwe kwa "jibini aina ya Cheshire".) kwamba wasomaji wetu waweze kufanya swali kwenye uchukuzi wao wote, na hivyo, kufikia kushawishika kwa dhahiri.

Ulimwengu wa Kikristo ni, kuongea kimaadili, waliungana kwenye swali na kufanya ibada kumuabudu Mungu siku ya kwanza ya juma.

Waisraeli walitawanywa ulimwenguni kote, wakiitunza na kuitakatifuza siku ya mwisho ya juma kwa kumuabudu Mungu. Kwa jambo hili maalumu, Waadventista Wasabato (wakiwa kama dini ya Kikristo yenye wafuasi wachache sana) wameichagua pia siku hiyohiyo.

Waisraeli na Waadventista wote wawili wameiamini Biblia kuwa ni amri na agizo la Mungu, linalosisitiza mno agizo la kuadhimisha kikamilifu siku hii ya Jumamosi.

Waisraeli wanaheshimu mamlaka ya Agano la Kale tu, lakini Waadventista ambao ni Wakristo wanakubaliana na Agano Jipya kwa kiwango sawa tu na cha Agano la Kale walichukulia kuwa ni maandiko yenye uvuvio pia. Wanaona kuwa Biblia ni mwalimu wao, likidumu kwa sehemu zote, kwamba Mkombozi alipokuwa hapa duniani akiwa na maisha yenye kuweza kufa, hakuweza kuishika na kuiadhimisha siku nyingine yeyote kabisa zaidi ya siku ya Sabato. Injili zinamuonyesha yeye akiwa kwenye ukweli hu wakati kwenye kurasa za kitabu cha Matendo ya Mitume, na Ufunuo, havionyeshi kabisa kubadilishwa au kuondolewa kwa maadhimisho ya Sabato ya Jumamosi kunakoweza kupatikana ushahidi wake.

Kwahiyo Waadventiata wapo pamoja na Waisraeli, walidumu kwenye imani kuliamini Agano la Kale, ambalo imani yake imethibitika na Agano Jipya, yalionyesha maisha na matendo ya Mkombozi na mitume wake mafundisho ya Neno Takatifu kwa kipindi kinachokaribia karne moja ya zama hizi.

Kitarakimu, inachukuliwa kuwa Waadventista Wasabato wanafanya mambo yasiyo na maana kwa kujilinganisha na idadi kubwa ya Waprotestanti walioko duniani, lakini, ina ikiweka maswali kuwa sio idadi yake, lakini ni ya kweli, uhalisia na usahihi, kuwa ni mguso mkubwa wa haki uliokataza kuishutumu au kuilaumu dini hii ndogo bila ya utafiti ulio kimwa na udadisi, nah ii siyo mazishi yetu.

Ulimwengu wa Waprotestanti umekuwa kutoka kwenye uchanga wake, kwenye karne ya kumi na sita, ni kwa kufanana kwake kote na Kanisa Katoliki kwa kuiadhimisha “kitakatifu” sio siku ya Jumamosi, bali Jumapili. Mjadala wa hoja zilizopelekea ananimitia ya kimawazo na matendo kwa kipindi cha karibu miaka 300 kinapaswa kusaidia kuiweka mbele imani ya Kiprotestanti kwene misingi yote kwenye jambi hili lilivyo, yalipendelea malumbano mahala ake kuwashinda wale waliofundishwa na Waisraeli na Waadventista, kwenye Biblia, kumtambua kikamilifu mwalimu wa wadai wote wawili, kuwa mwamuzi au mpatanishi na mashuhuda. Iwapo hata hivyo, kwa upande mwingine, malumbano mwinginw yaliyofuatia, yenye kutatiza na idadi kubwa ya Waprotestanti, madaraja yote mawili ya wenye dawaa au wadai, wakiomba kwa mwalimu wao anayetegemeka, Biblia, sehemu kubwa ya Waprotestanti kwa kiasi kikubwa kutokana na makelele, kama wakifanya la maana kwa kusisitiza kwao kuitunza Jumapili, hakuna njia nyingine iliyoachwa zaidi kukubali kuwa yamekuwa ni mafundisho na matendo kile ambacho Kimaandiko ni uwongo kwa zaidi ya karne tatu, kwa kuyachukua mafundisho na matendo ya kile wanachojifanya kila mara kuliamini kanisa lililokengeuka, kinyume kabisa na kile kilichohakikishwa na mafundisho ya Maandiko Matakatifu. Kwa kuongeza kwenye umakini dhidi ya upotofu wa Kimaandiko na usio sameheka, kunahitaji mtu aliye na msisitizo mkubwa na amri ya Mungu kwa mtumishi wake, mtu, “Mkombozi wa siku ya Sabato, na kuishika kitakatifu."

Hakuna Mprotestanti aishiye leo ambaye hajawahi kuitii amri inayomtaka kulifuata kanisa kengeufu lililotajwa kuliko mwalimu wake, Biblia ambayo tangia kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo, havifundishi fundisho linguine lolote  ambayo Waisraeli na Waadventista Wasabato wanaiona kuwa ni sahihi na kuifuata. Wote wawili wanadai kuwa Biblia kuwa ni mwalimu wao “asiye na makosa”. Hebu na tuiache Biblia iamue kama ni Jumamosi au Jumapili kuwa ndiyo siku ile iliyoamriwa na kutakaswa na Mungu. Moja kati ya mirengo hii miwili lazima uwe unakosea na utakuwa kwenye upande wa uwongo kutokana na lolote linalohusika kutokana na haya yanayoulizwa na adhabu kali itawakumba, iliyoamriwa na Mungu mwenyewe, kwa wanaolivunja hili “agano la milele,” tutaingia kwenye mjadala wa malumbano stahiki yaliyotumika na pande zote mbili. Hakuna hata mmoja kati ya mjadala hii ya somo kuu na muhimu lililo juu au zaidi ya uwezo wa mawazo ya kawaida, wala haihusishi masomo yasiyo ya kawaida. Inahusisha yenyewe na mipango michache unaoweka swali kwenye suluhisho rahisi:

1. Ni siku gani ya juma ambayo Biblia imeagiza iadhimishwe kitakatifu?

2. Je, Agano Jipya limefanya marekebisho kwa maagizo au matendo ya amri ya kwanza halisia?

3. Je, Waprotestanti, wamekuwa waliitii tangu zama za karne ya kumi na sita, amri hii ya Mungu kwa kuitunza na kuiadhimisha “kitakatifu” siku iliyoamriwa na walimu wao asiyekosea, yaani Biblia? Na kama jibu ni sivyo, ni kwa nini isiwe hivyo?

Kutokana na maswali hayo matatu ya hapo juu, tunaahidi kutoa majibu mengi iwezekanavyo ya kiakili na uangalifu ambayo hayatashindwa kuthibitisha ukweli na kuunga mkono mapotofu ya makosa.

(Kutoka kwenye jarida liitwalo the Catholic Mirror la Septemba 9, 1893.)

"Lakini imani, imani kali, mara inaposhikiliwa kikamilifu Kwenye uwongo unaopendeka, inafikia kwenye kikomo au ukingoni"  

Moore

Uthibitisho kwenye jambo letu la mwisho, tunaedelea kufunua na kuweka wazi moja ya makosa makubwa na kutosameheka kabisa kwa kutokuwepo kwa sheria au kanuni za Kibiblia za imani. Tusije kwa namna yoyote ile kushindwa kuelewa, tukidhani ni lazima kudhani kuwa Waprotestanti hawazijui sheria na kanuni za imani, hawana mwalimu, kuokoa “Biblia isiyo na makosa”. Kama Wakatiliki wanavyofanya hukumu zao kwene mambo ya kiroho inavyoonyesha, na kwa kujiamini kusiko na kikomo, kwenye sauti au maamrisho ya kanisa lao, na ndivyo ilivyo pia kwa Waprotestganti hawamjui mwali mwiegine yeyote zaidi ya Biblia. Kiroho chao chote kinatokana na kulinganishwa kwenye mafundisho yao. Ni kwao wao kupitia ndiko sauti ya Mungu inaelekezewa kwao kupitia kwa mwalimu wao mwenye kusisimuka. Anaunganika na dini yake. Imani yake, na matendo yake. Lugha ya Kichillingworth, "Biblia, Biblia yote, na hakuna kingine ila Biblia, ni dini ya Kiprotestanti," ni mtindo mmoja tu wa wazo lenye hisia nyingi kali, zinzotokana na namna nyingine kama vile kitabu cha Mungu," "Alama ya Wokovu wetu," "Mwanzilishi wa Imani yetu ya Kikristo," "Kitabu cha Mungu kwa Wanadamu wote," nk, nk. Kwa hiyo ni ukweli usio na utata kuwa Biblia pekee ndiyo mwalimu wa wa Wakristo wa Kiprotestanti Wanaodhania ukweli huu, na sasa tutaendelea kujadili haki asilia ya swali lililopo kwenye jambo letu.

Kwa kujua kile kisichoweza kukanushika, ukweli wa utata wa moja kwa moja kati ya mafundisho na matendo ya imani ya Ukirsto wa Kiprotestanti – Waadventista Wasabato waliotarajia-kwa upande mwingine, ile ya Wayahudi kwa upande mwingine, wote wawili wakiadhimisha siku tofauti za za juma katika kumuabudu Mungu, tutaendelea kuchukua ushuhuda wa shahidi aliyepo kwenye hoja sawa kama ushuhuda wa mwalimu ujulikanao na mbao sisi tunawasiliana naye kwenye Neno Takatifu, linalopatikana kwenye Mwanzo 2:2:

"Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya."

Rejea inayofuata kuhusu jambo hili inakutikana kwenye Kutoka 20, ambapo Mungu aliamuru siku ya saba iadhimishwe, kwa kuwa yeye mwenyewe alipumzika kutoka kwenye kazi yake ya uumbaji siku hiyo na maandiko matakatifu yanatujulisha kwamba kwa ajili hiyo alipenda iadhimishwe kwa maneno yafuatayo:

"kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

Tena tunasoma kwenye sura ya 31, aya ya 15:

"Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa Bwana;"

Aya ya kumi na sita inasema:

"ni agano la milele. 17 Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika."

Kwenye Agano la Kale, imefanywa rejea kwa kuandikwa mara mia moja na ishirini na sita kuhusu Sabato, na maandiko yote haya yanalenga kwa namna inayoshabihiana katika kuyaelezea mapenzi ya Mungu yanayoamuru siku ya saba kuwa ni ya kuiadhimisha, kwa kuwa Mungu nwenyewe aliiadhimisha kwa nza siku hii, na kuifanyia agizo kuwa itakuwa ni “agano a milele.” Na wala haikutarajiwa kuwa na mtu mjinga kiasi gani hata aiwekee swali agizo na utambulisho wa siku hii ya Sabato ambayo ni Jumamosi au siku ya saba, kwa kuona kwamba wana wa Israeli wamekuwa wakiiadhimisha Sabato tangu kutolewa kwa sheria au Torati yapata mwaka wa Anno Mundi (A.M.) 2514 hadi mwaka 189 3BK, kipindi cha takriban miaka 3383. Amoja na mfano wa Waisraeli ulio mbele ya macho yetu leo, hakuna ukweli au uthibitisho wa kihitoria uliowekwa zaidi ya huu uliotejwa, yaani, kwamba watu wateule wa Mungu, walinzi wa Agano la Kale, wawakilishi waliopo hai leo wa dini ya pekee ya mbinguni iliyoko, kwa kipindi chote cha miaka takriban 1490 ndani ya Ukristo, imeendenda kwa kigezo cha matendo na kazi za kila juma ikiwa ni mapokeo yadumuyo ya tafsiri sahihi ya siku mahsusi ya juma, Jumamosi, kuwa itunza na kutakatifuzwa “kitakatifu kwa Bwana,” ambavyo ni mapokeo waliyoyaeneza kwa matendo yao hadi kwenye kipindi chao cha ziada cha miaka 1893 zaidi, kinachochukua uenezaji kamili cha uenezi wa Ukristo ulimwenguni kote. Tunadhani kuwa ni muhimu kuwa wazi kabisa kwenye jambo hili, kwa sababu ambazo zitaonekana kikamilifu zaidi baadae. Agano la Kale la Biblia-linathibitishwa na mapokeo yaliyopo ya harakati za kila juma kwa takriban miaka 3383 na wateule wa Mungu, waalimu, kisha na mambo mengine kadhaa yaliyo sahihi, kwamba Mungu mwenyewe aliita siku hii na kuamuru “iadhimishwe kitakatifu,”- na siku hiyo ni hii ya Jumamosi, na kwamba tendo lolote la kuihalifu siku hii, adhabu yake itakuwa ni kifo.

"Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.." Kutoka 31:14.

Haiwezekani kugundua adhabu nyingine ili kali zaidi zaidi yah ii iliyotamkwa wazi na Mungu mwenyewe kwenye andiko hilo hapo juu, na neno na amri hii kumhusu yeyote atakayeitia unajisi na adhabu yake imetajwa sio chini ya mara mia moja na ishirini na sita kwenye sheria za zamani au torati. Amri kumi za Agano la Kale hapo mwanzoni kabisa ziliwekwa kwenye kumbukumbu za mtoto wa Mkristo anayeiamini Biblia haraka sana iwezekanavyo, lakini hakuna hata moja ya kumi hizi iliyowekewa mkazo na msisitizo ili izoeleke, bali kote kuwili, yaani kwenye masomo ya Sule ya Jumapili na hata madhabahu, zaidi ya ile ya “kuitakatifuza” siku ya Sabato.

Kwa kuyalinda na kwa hakika mapenzi ya Mungu kwa kuifanya siku hii kuitunza kuwa takatifu, kutoka kwenye Neno lake Takatifu, kwa kuwa alipumzika siku ile, siku ambayo tumethibitishiwa kutokana na matendo ya watu wake wateule kwa kipindi cha takriban miaka maelfu, kiasilia tunalazimika kujiuliza ni lini na wapi Mungu aliibadili siku ya kumuabudu yeye, kwa kuwa ulimwengu umefundishwa kuwa mabadiliko ya siku yamekuwa yakifanyika, na kwa kuwa hakuna dalili wala dokezo la mabadiliko hayo yanayopatikana kwenye kurasa za Agano la Kale, wala matendo ya Wayahudi ambao wanaendelea kwa kipindi cha takriban karne kumi na tisa za kuenea kwa Ukristo, pamoja na Agano Jipya, kwa amri hii ya Mungu kuhusu Jumamosi ya Sabato.

Sisi sasa tunaelekea kwenye kipindi kinachofunia kidogo karne hii ya kumi na tisa, na kuendelea kutafiti iwapo kama mwalimu aliyechukua mbadala—Agano Jipya—kama anamahala palipotpa amri ya kubatilisha mamlaka ya amri zile za zamani, na wakati huohuo, kuibadilisha siku kutoka siku hii iliyowekwa na Mungu ya Sabato ambayo inatokana na sheria za kale. Ni kama Jumamosi ambayo ni Sabato ni siku iliyoteuliwa na kuwekwa wakfu na Mungu. Mamlaka ya Mbinguni tu ndiyo yanayohusika ubatilishaji amri ndiyo yangeweza kuibatilisha siku ya Jumamosi na mamlaka nyingine zote na kuipanga siku nyingine ya kuabudu na “kuitakatifuza” zaidi ya siku hii ya Jumamosi, ni sawa na kuridhika tu na ufahamu au nia ya muumini Mkristo. Biblia kuwa ni mwalimu wa pekee anayetambulika na kukubalika na Mkristo anayeiamini Biblia, Agano la Kale limeshindwa kuonyesha mabadiliko ya siku na wala siku nyingine zaidi yah ii siku ya Jumamosi kuwa ni ya “kuitakatifuza” na maneno ya Biblia, ni matarajio hakika kwa Wakristo Wanamatengenezo kuonyesha kutoka kwenye kurasa za Agano Jipya, amri mpya ya Mungu inayoipinga Jumamosi na kuiingiza Jumapili kuwa mbadala wake, iliyotunzwa na kuadhimishwa wakiisingizia Biblia na wakaanza kuiadhimisha siku hii tangu kuanza kwa zama ya Matengenezo.

Kwa kulitafakari Agano Jipya tangu jalada moja hadi lingine, kwa kumaanisha kabisa, tunakuta Sabato ikitajwa mara sitini na moja. Tunaona pia kuwa Mwokozi mara nyingi sana aliichagua siku ya Sabato kuwahubiria na kuwafundisha watu kwenye sinagogi na kutenda miujiza humo. Injili nne zimeitaja Sabato (Jumamosi) mara hamsini na moja.

Kwa mfano, Mkombozi anajitaja mwenyewe kuwa ni “Bwana wa Sabato,” kama ilivyoandikwa na Mathayo na Luka, lakini wakati wa rekodi yote ya kuishi kwake, alionekana mara nyingi akiishika na kuisisitiza siku hii (ya Sabato). Kwamwe hakuonyesha nia ya kuibadilisha hata mara moja. Mitume wake na rafiki zake mwenyewe wanatufanya tutoshelezwe kuwa ni mfano wa uadhimishaji wao kiumakini wa siku hii baada ya kufa kwake, na wakati mwili wake ikiwa maburini, Luka (23:56) anatuambia:

"Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa." "Lakii siku ya kwanza ya juma mapema asubuhi, walikuja wakiwa wamebeba manukato waliyoyaandaa Ijumaa Kuu alasiri, kwakuwa Sabato ilikuwa imekaribia."Aya ya 54.

Tendo hili la sehemu ya marafiki zake binafsi wa Mwokozi, linathibitisha zaidi ya ukanganyiko wowote kuwa hata baada ya kufa kwake aliitunza na “kuitakatifuza” Sabato na aliichukulia siku ya Jumapili kama sikun nyingine yeyote tu ya juma. Ionnawezekana kwa hiyo kwa kitu chochote kuambatana zaidi zaidi ya kwamba mitume na wanawake mashuhuri na wachamungu walikuwa hawajui kuwa siku ya Sabato ambayo ni Jumamosi hadi kwenye kifo cha Kristo?

Sisi tunakaribia sasa utafiti wa swali hili zuri kwa miaka mingine thelathini iliyofuatia, kama ilivyoelezewa na mwinjilisti, Mtakatifu Luka, kwenye kitabu chake cha Matendo ya Mitume. Kwa kweli, maadhi ya hoja za  ya hoja za  ya hoja za tendo la kutangua linaweza kuonekana kwenye matendo ya mitume wakati wa kipindi kile kinachoelezewa.

Lakini looo! Tunapata pigo tena na kukatishwa tama. Mara tisa tunakuta Sabato inayotajwa kwenye kitabu cha Matendo, lakini ni Jumamosi (Sabato ya zamani). Je, wasomaji wetu wanahitaji uthibitisho? Basi tunawapeleka kwenye sura na aya kwenye kila mfano. Matendo 13:14, 27, 42, 44. Mara nyingine tena, Matendo 15: 21; tena, Matendo 16: 13; 17:2; 18:4.

"Akatoa hoja zake (Paulo) katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani."

Ni Sabato (Jumamosi) ndiyo iliyopo tangu kwenye cha Mwanzo hadi Ufunuo!!! Kwa hiyo, haiwezekani kukuta kwenye Agano Jipya mwingiliano hata mdogo kiasi gani na Mwokozi wetu au Mitume wake kutokana na Sabato yenyewe iliyowekwa, lakini kwa kinyume na Mwokozi wetu au Mitume wake kutokana na Sabato yenyewe iliyowekwa, lakini kwa kinyume, maulizo au wasiwasi wote kuhusu uwekwaji wa kutoka mwanzo, wala uwezo wao wa kutoa na yeye, wakati alipokuwa anaishi, na kutokinzanisha, ushiriki mkubwa wa kuishika siku ile na sio nyingine na mitume kwa miaka thelathini baada ya kufa kwake, kama kitabu cha Matendo ya Mitume kinavyotushuhudia kwa kiasi kikubwa sana.

Kwa hiyo, hitimisho haliepukiki kulinganisha na wale wanaoifuata Biblia kuwa ni kiongozi wao, ambao ni Waisraeli pamoja na Waadventista Wasabato ambao wana uzito usiotenganishika kwa upande wao, wakati kwamba kwa Waprotestanti Waamini Biblia hawana neno la kujitetea kwa kuibadilisha kwao na kuifanya Jumapili iwe badala ya Sabato ya Jumamosi. Kanuni nyingine zaidi.

(kutoka kwenye jarida la the Catholic Mirror la Septemba 16, 1893.)

Waka kujiinua kwake shetani ambaye ni “muuaji tangu mwanzo” “na baba wa uwongo” alipofanya jitihada ya kuyafungua macho ya mama yetu wa kwanza, Hawa, kwa kuipandisha au kuisisimua tama yake kuwa “utakuwa kama Mungu, ukijua mema na mabaya” kitendo chake kwa hiyo kilikuwa ni moja ya juhudi za kusifiwa na zilizofanikiwa zilizofanywa baadae katika kuwadanganya mamilioni ya watoto wake. N kama alivyokuwa Hawa, wao nao wavivu wa kujifunza. Looo! Thamani ya kuvutia yalipelekea kuwadanganya watoto wake wadhaifu kutoka kwenye maagizo na amri za Mungu. Wala somo halihusiani na aina hii ya mjadala kwa mbinu zisizo za kawaida za ukuu wake.

Zaidi ya karne tatu hivi, amewapelekea idadi kubwa ya watu wasioridhika na Wakristo wenye tamaa, matarajio au tamaa kubwa ya mafanikio ya uzinduzi wa “mwondoko mpya,” kwa kuachana na Kanisa lililoanzishwa na Mwana wa Mungu, kama mwalimu wao, na nadharia ya mwalimu mpya—Biblia iliyo kama—ni kigezi chao cha pekee na mkufunzi.

Busara ya kijanja ya Yule muovu ilionekana kabla lakini mafanikio makubwa ya ulaghai huu. Wala matokeo yaliyoangukia kushindwa kwa matarajio karibu yote yalliyosubiriwa na kutarajiwa sana.

Roho ya ujasiri na kuthubutu ndiyo uliohitajika peke yake kufikia matarajio. Kwa yeye maringo ya kishetani mara yakakutikana kwenye dhihaka za za kiukengeufu. Luther, ambaye yeye mwenyewe alishuhudia mara kwa mara kuyafunga mazoea yaliyokuwepo kati ya Bwana wake na yeye mwenyewe, kwa kujibu wa kitabu chake kijulikanacho kama “Maongezi ya Mezani,” na vitabu vingine vilivyochapishwa mwaka 1558, huko Wittenberg, chini ya utafiti wa Melancthon. Mazungumzo au nasaha zake na Shetani kwenye maeneo kadhaa mengi, yanayoshuhudiwa na Luther mwenyewe—shahidi anayestahili kupewa kila aina ya sifa. Uwakala ambao joka alikusudia na kujaribu kuufikia kikamilifu kabisa kwenye bustani, ndio uwakala ambao Luther alifanikisha kuuingiza kwenye ulimwengu wa Kikristo.

"Wape rubani kwenye mruko wao mzuri,

Paka rangi kwenye michoro yake, na kufundishwa na kufundisha uwongot:

Walio na mikono hatarishi ndio wapotoshwe

Kwenye viatu vha adui, wazamishwe mawimbini."

Kama mwishoni akiishia mwenyewe na muovu kwenye mapambano yake na kanisa la Kristo ulikuwa ni kuuangamiza Ukristo, na sasa tumejitoa kuchekecha vifaa vilivyoigizwa kutoka kwake ili kuhakikisha kuwa anafanikiwa. Hata hivyo, wamekutikana kuwa wanawapotosha, wakijikanganya wenyewe, na kudanganyika. Sasa tutaendelea kwa utafiti zaidi ya ukengeufu huu.

Kukiwa kumethibitika kuonyesha kwamba Mkombozi, bila mfano, wakati wa kuishi kweke hapa duniani alionekana na kusisitiza juu ya utunzaji wa Sabato (Jumamosi), inavyoelezewa na hawa wainjilisti wanne na kuandikwa takriban mara hamsini na moja, irgawa alijitambulisha mwenyewe kama “Bwana wa Sabato,” hakuweza iwe ni mara moja au mara nyingine vyovyote kuzuia au kujaribu kuibadilisha siku hii kwa kuiweka siku nyingine na kutoa mwito maalumu kwenye matendo na mwenendo ya mitume na ya wanawake watakatifu wachamungu, jioni ile ile ya kufa kwake, wasiende kumpaka au kutumia manukato na uudi na wakaenda kuupaka mwili wake asubuhi ya baada ya Sabato (Jumamosi) kama Mtakatifu Luka anavyotueleza kwa wazi kabisa (Luka 24:1), na hivyo kuonyesha mfano, matendo ya kimungu na mapenzi ya Mwana wa Mungu wakati wa uhai wake kwa kuitunza Sabato vizuri, na kwa kuwapa mwito wengine wafanye vitendo vinavyoendana na uwakilishi wa maisha yake baada ya kufa kwake, kama ilivyothibitishwa na Mtakatifu Luka na akaandika pia ili wasome wasomaji wake ukweli usiopingika kwamba mitume kwa miaka iliyofuatia thelathini (matendo ya Mitume) hawakufanya kinyume kamwe cha matendo ya Bwana wao aliye mbinguni kwa hakika, kama Mtakatifu Luka alivyoandika kwenye Matendo 18:1 inavyotuthibitishia:

"Akatoa hoja zake [Paulo] katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani."

Waongofu Wamataifa walikuwa kama tunavyoona kutoka kwenye maandiko, wameelekezwa na kufundishwa kisahihi kuwa sawa na Wayahudi, kuishika Sabato, mara tu wanapokuwa wanaongoka kuwa Wakristo siku zile, “Wayahudi na Wayunani” wote kwa ujumla iliwapasa.

Wakiwa pia wanatolewa mwito kwenye maandiko ya Matendo yaliyo na matumizi yasiyojumuishwa ya Sabato kwa Wayahudi na Wakristo kwa miaka thelathini baada ya kifo cha Mwokozi kuwa kama ni siku pekee ya juma aliyoaiadhimisha Kristo na mitume wake, kipindi ambacho kimejumuishwa na rekodi iliyokubalika, ambayo sasa tunaendelea kuweka uthibitisho wetu kwamba Sabato (Jumamosi) ndiyo ilifaidika na fursa hii jumuisho, kwa kuwaasa watu kwa kila mfano uliopo rekori takarifu inataja kuwa ni siku ya wiki.

Mahala ilipotajwa kwa mara ya kwanza Jumapili baada ya ufufuko wa Kristo panaonekana kwenye injili ya Mtakatifu Luka sura ya 24, aya za 33-40, na Mtakatifu Yohana 20:19.

Maandiko yaliyo hapo juu yenyewe tu yanaonyesha nia nzima ya mkutaniko huu kwa sehemu ya mitume. Ilichukua mahala kwenye siku ya ufufuo (Jumapili ya Easter), sio kwa madhumuni ya kuanzisha “mwondoko mpya” kutoka kwenye Sabato ya zamani (Jumamosi) kwa “kuitakatifuza” siku mpya, na sio ashirio lililotolewa na maombi, nasaha, au usomaji wa Maandiko Matakatifu, lakini inaashiria uvunjaji moyo mkubwa kufanywa na mitume kwa kuwaarifu wanadamu kwamba walikuwa wamekusanywa pamoja kwenye chumba kile huko Yerusalemu “kwa kuwaogopa Wayahudi”, kama Yohana Mtakatifu alivyonukuu hapo juu, akituarifu kwa wazi sana.

Sehemu iliyotaja tena ya pili hii Jumapili kukutikana ni kwenye Injili ya Yohana Mtakatifu, sura ya 20 aya ya 26 hadi ya 29:

"Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao."

Mkombozi aliyefufuka alijitoa mwenyewe kwa kukutana na mitume wake wote kuishinda hali ya kutokuamini ya Thomaso, ambaye hakuwepo walipokutanika kwenye jioni ya Jumapili ya Easter. Hii ingewezesha fursa ya dhahabu kwa Mkombozi kubadilisha siku machoni au mbele ya mitume wake, lakini tunaelezea ukweli rahisi kwamba kwenye mazingira kama haya, kama kwenye siku ya Easter, na sio neno lililosema maombi, kusifu, au usomaji wa Maandiko Matakatifu.

Mfano wa tatu ulioandikwa, wakati mitume walipokusanyika siku ya Jumapili, unakutikana kwenye Matendo 2:1;

"Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja." (Sikukuu ya Fentekoste—Jumapili)

Sasa, je, maandiko haya yanatosheleza kuwabadilisha wapendwa ndugu Wakristo wanaoiamini Biblia hata waikubali hoja kuwataka waamini au kukubaliana kuwa Jumapili imechukua mahala pa Jumamosi? Kwa kuwa wakati tunapowafahamisha kuwa Wayahudi walikuwa anaiadhimisha hii Jumapili kwa takriban miaka 1500 na kuwa walikuwa wakiishika kwa kipindi cha karne kumi na nane baad ya kuanza kwa Ukristo, na kwa wakati huohuo wakawa wanaishika na kuiadhimisha Sabato ya kila juma, haionekani kabisa na hata kuonyesha au kuashiria kwenye maandiko. pentekoste ni siku ya hamsini baada ya Pasaka, ambayo ilikuwa inaitwa Sabato ya Majuma iliyokuwa inajumuisha majuma saba yenye siku sabasaba na kuongeza siku moja ya baada ya kuhitimisha Sabato ya juma la saba, ilikukuwa ni siku kubwa ya sikukuu yote ni lazima iwe ni siku ya Jumapili. Kile Waisraeli wasingekichukulia kuwa iwe sababu ya wao kuifanya siku ya kwanza ya juma kuwa siku ya kuiadhimisha na kusema kuwa wamegundua chanzo cha kuishika siku ya kwanza ya juma kwenye maadhimisho ya Pentekoste ambayo imekuwa ikiiadhimishwa na wao kila mwaka kwa kipindi cha takriban miaka 3,000? Ni nani kama sio Wakristo waamini Biblia, waliosukumiwa kwenye ukuta kwa kujifanya kuwa na udhuru kwa kufuru zake zenye kuchukiza na kuitia unajisi kwake Sabato, iliyoadhimishwa wakati wote na Kristo na mitume wake wangechukulia kwenye sikukuu ya Wayahudi ya Pentekoste kwa tendo lake ya kumuasi Mungu na mwalimu wake Biblia.

Mara nyingine tena, watetezi wa Biblia kuhusu ubadilishaji huu wa siku wanatutaka kuangalia kitabu cha Matendo sura ya 20, aya za 6 na 7;

"Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate." etc.

 Kwa mionekano ya maandiko yote ya hapo juu inge kufanya maliwazo nyingine kwenye chuki na kutokuwa na marafiki wa Biblia, lakini kwa kuwa Marplot, hatuwezi kuwaruhusu hata kwenye makombo haya ya faraja. Tunajibu kwa ulaghai: "Quod probat nimis, probat nihil"--"Ni nini kinachotukuka sana, hakina maana yoyote." Hebu na tuwe macho kwa andiko hili hili la Matendo 2:46;

"walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba," etc.

Ni nani asiyeona kwa udani kwamba andiko limefanya uthibitisho halali usiokuwepo wa Jumapili, inayoishia kuyeukia kwenye hewa au anga ya ignis--fatuus—wakati imewekwa kwenye eneo lililo sambamba au mkabala pamoja na aya yake ya 46 ya sura hiyohiyo? Kile Wakristo waamini Biblia wanachodai kutokana na andiko hili kwa Jumapili ekee ni mamlaka yale yale, Luka Mtakatifu anayotuambia kuwa ilikuwa kawaida kwa kila siku ya juma;

"walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba."

Andiko moja zaidi linajieleza mwenyewe, kwa kujifunza zaidi kuhusu ubadilishaji na kuiingiza Jumapili badala ya Jumamosi. Imechukuliwa kutoka kwa Paulo Mtakatifu, I Wakorintho 16:1,2;

"Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu,…Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake," nk.

Kutokana na swali la Mtakatifu Paulo limekuwa likifanyiwa kazi kabisa kwa kututaka kuangalia kile kilichofanyika kila Jumamosi wakati wa uhai wake Mwokozi na kuendelea kwa miaka thelathini baadae, kama kitabu cha Matendo kinavyotuambia.

Wafuasi wa Bwana walikutana “kila Sabato” kusikiliza neno la Mungu; maandiko matakatifu yalisomwa “kila siku ya Sabato”

"Na Paulo kama ilivyokuwa desturi yake alihojiana nao kwenye Sinagogi kla Sabato aliwafundisha jina la Bwana Yesu," nk. Matendo 18:4.

Ni upuuzi mkubwa kiasi gani kuhitimisha kwamba kudhania kwamba usomaji wa Maandiko Matakatifu, maombi, kusifu, kumtukuza na kuhubiri ambako kunapelekea safari za kazi kila Jumamosi, ni kama ilivyothibitika kwa kina zaidi wakati zilipo kuwa kubakia na mshangao kuchukua ukusanyaji kwa siku nyingine ya juma?

Ili kushukuru kikamilifu thamani ya maandiko haya sasa kwa kutilia maanani, inahitajika tu kukumbuka matendo ya mitume na wanawake wachamungu walivyofanya siku ya Ijuma Kuu kabla ya jua kuzama. Walinunua uvumb a na manemane baada ya kuchukuliwa kwake na kupelekwa huko chini kutoka msalabani, walisimamisha kufanya mambo yote hadi Sabato “takatifu kwa Bwana” ilipopita, na ndipo walipochukua hatua kufanya hivyo siku ya Jumapili asubuhi walipoenda kukamilisha mchakato wa kuupaka mwili mtukufu wa Yesu. Kwanini, tusijiulize, kwa nini hawakuendelea na mchakato huu wa kumpaka manukato siku ya Jumamosi?—Kwakuwa walijua vema sana kuwa kitendo cha kuupaka mwili mtakatifu wa Bwana wao kungeingilia kati maadhimisho matakatifu ya Sabato. Maadhimisho ambayo yalikuwa ni ya muhimu nay a kuangalia sana, na hadi hapo itakapoonyeshwa kuwa siku Sabato imekwishapita mara na inaelekea kuwa Jumapili ya maandiko yetu haijaweza kuadhimishwa bado (ambavyo ingekuwa ni uwongo, kwa kuifananisha kama ilivyo kila Sabato inavyoadhimishwa), ombi la Mtume Paulo la kufanya makusanyo siku ya Jumapili haliwezi kulinganishwa na kazi ya kuupaka mwili wa Kristo, ambayo isingeweza kuathiri wala kuingiliana na Sabato, na hatimaye kuingiliana na maandiko kuhusu siku halisi na maalumu, yaani Jumapili au siku ya kwanza ya juma.

Kwa kulipitia kila andiko linalokunakutanika kwenye Agano Jipya linaitaja Sabato (Jumamosi), na kwa siku ya kwanza ya juma (Jumapili), na kuonyeshwa kwa pamoja kutoka kwenye maandiko haya, kwa hiyo haionyeshi tena naandiko yajayo yanaweza kukutikana kwenye Nyaraka Takatifu kuonyesha mabadiliko ya Biblia kuiingiza Jumapili na kwamba iadhimishwe badala ya Sabato ya Jumamosi, na inaonekana tu kwetu kupeleleza au kuitafiti maana ya usemi wa “Siku ya Bwana,” na “siku iliyotengwa na Bwana,” kukutikana kwenye Agano Jipya ambalo tunapendezwa nalo kulifanya kwenye makala ifuatayo, na kuhitisha kwa maelezo mema kwa kupingana nu kunyume na utaratibu na mfumo wa kidini ambao tutathibitisha kuwa asiyejilinda, mwenye kujikanganya, na kujitoa mhanga kwa kujiua.

(Kutoka kwenye jarida la the Catholic Mirror la Septemba 23, 1893.)

"Kupunguza kwa nusu wenye kutegemea na ukubwa usiosawa.

Mguu mmoja kwa ukweli usaidiwao, anayeongopa,

Kwa hiyo I wasiwasi wenye lengo kwa hatua zisizo na maana,

Usikilinde kitu chochote bali kupoteza umbali."

Kwenye makala iliyopo sasa tunashauri kutafiti kwa uangalifu sana upya (na mwisho) mrengo unaodhaniwa kuthibitisha kuwashawishi Wakristo wanaoiamini Biblia ambavyo Mungu ameibadilisha na kuiingiza Jumapili mahali pa Jumamosi kwa ajili ya kumuabudu kwa amri na sheria mpya, na ndiyo mapenzi ya mbingu yanakutikana yamerekodiwa na Roho Mtakatifu kwenye nyaraka na maandiko ya Mitume.

Tunaarifiwa kwamba mabadiliko haya ya ushingo ngumu nay a lazima yamekumbana maelezo, zaidi na zaidi tena, kwenye mlolongo wa mfululizo wa maandiko ambako maelezo na maneno “siku ya Bwana” au “siku aliyoifanya Bwana” yamekutikana.

Mfululizo wa fundisho la maandiko ya Agano Jipya yenye kichwa cha maneno kisemacho “Sabato,” idadi yake inafikia kuwa mara sitini na moja kwenye Injili, Matendo, na Nyaraka, na daraja la pili, ambako “siku ya kwanza ya juma” au Jumapili, kunatathminiwa kwa ukosoaji mkubwa (imeandikwa takriban mara tisa [nane]), na kuonekana kuwa haikidhi viwango vya kushawishi kubadilisha makusudi au mapenzi ya Mungu hadi kufikia siku yake ya kuabudiwa na mwanadamu, nasi bado ttunaendelea kutathimini kundi la tatu na la mwisho ya maandiko unaotegemea kuuokoa mfumo wa Biblia kutokana na mpangilio wa kutafuta kuyaondoleambali ulimwenguni, kwa jina la Mungu maamrisho yake ambayo hayana mkanganyiko mkubwa unaotolewa au mamlaka kutoka kwa mwalimu wao Biblia.

Andiko la kwanza la mrengo huu linapatikana kwenye Matendo ya Mitume 2:20:

"Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri.."

Ni Jumapili ngapi zimeandikwa kuanzia unabii ule ulinenwa? Zaidi sana ni kwamba ni juhudi tu za kuyageuza maana andiko takatifu kutoka kwenye siku ya hukumu hadi kwenye Jumapili!

Andiko la pili la mrengo huu linapatikana kwenye I Wakorintho 1:8;

"ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo."

Kile wanachoshindwa kukiona hawa warahisishaji na wageuza maandiko ni kwamba hapa mtume anaonyesha wazi siku ya hukumu? Andiko linalofuatia kuhusu jambo hili ndilo linalopelekea lenyewe lijikute kwenye Waraka huohuo sura ya 5:5;

"kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu. ?”

Uhusiano haramu wa mapenzi kati ya ndugu wa Mkorintho kwa kweli, aliokolewa Jumapili iliyofuatia baada ya hapo!! Ni jambo lenye uchungu kiasi gani kubadilishwa namna hii!! Andiko la nne, 2 Wakorintho 1:13,14;

"...nami nataraji ya kuwa mtayakiri hayo hata mwisho; vile vile kama mlivyotukiri kwa sehemu, ya kwamba sisi tu sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya Bwana wetu Yesu."

Jumapili au siku ya hukumu, ni ipi> andiko la tano ni kutoka kwenye waraka wa Mtume Paulo kwa Wafilipi, sura ya 1, aya ya 6:

"Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;."

Watu wema wa huko Filipi, kwa kujipatia ukamilifu kwa kufuata Jumapili, wangeweza kuyacheka na kuyashangaa mabadiliko ya haraka ya mpito ya siku hizi!

Tunaomba kupumzika kutoa sababu yetu ya sita, iliyoandikwa kwenye Wafilipi sura ya kwanza, aya ya kumi:

"mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo;"

Siku ile ilikuwa inafuatia Jumapili yake! Na sio mbali kuingojea kabisa. Andiko la saba ni, 2 Petro 3:10;

"Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi;"

Utekelezaji wa andiko hili kuhusu Jumapili linapitia kwenye mtazamo wa kijinga kabisa.

Andiko la nane ni, 2 Petro 3:12;

"mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?" nk.

Siku hii ya Bwana ni ile ile iliyotajwa kwenye maandiko ya huko nyuma, utekelezaji wa zote mbili, yaani Jumapili ifuatayo ingeuachwa ulimwengu wa Kikristo ukishinda macho usiku wa Jumapili uliofuatia.

Tumewapelekea viongozi wetu nane kati ya maandiko tisa yanayotuama kwenye lindi au mto na andiko kutoka Maandiko Matakatifu, juhudi ya kuitia inajisi kimakusudi kuiita kuwa ni “siku ya Bwana” kwa Jumapili, na ni kwa matokeo gani? Kila ushahidi wa kuutoa kama ulivyoonekana mwanzoni wa siku za mwisho, unaotajwa moja kwa moja, kikamilifu, na kiusahihi kabisa.

Andiko la tisa ambapo tunakutana na maneno “siku ya Bwana”, ni la mwisho kupatikana kwenye maandiko na nyaraka za mitume. Kitabu cha Mafunuo au Ufunuo sura ya  1:10, inaielezea kwa maneno yafuatayo ya Yohana Mtakatifu:

"Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana;"

Lakini itaweza kujipatia butudiko zaidi kwa marafiki zetu waanini Biblia kuliko watangulizi wa mchakato huu. Kama Mtakatifu Yohana alivyotumia kuelezea mapema kwenye Injili yake au Nyaraka zake—zenye Msisitizo mkubwa. Wala hakuna mahali panapoitaja Jumapili kabisa?—Ndiyo, ni mara mbili. Ni jinsi gani uingizaji huu wa Jumapili umemudu kufanywa kulinganisha na hali hii? Jumapili ya Easter iliitwa hivyo nay eye (Yohana 20:1) "Siku ya kwanza ya juma."

Tena, sura ya ishirini, aya ya kumi na tisa:

"Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma."

Ni dhahiri kabisa, ingawa linauvuvio, sehemu zote mbili, yaani Injili ya Nyaraka zake, aliita Jumapili kuwa ni “siku ya kwanza ya juma,” ni kwa kigezo gani basi, inaweza kudhaniwa kwamba alitoa ushauri huo? Je, alikuwa amejaa Roho sana wakati alipoandika kitabu cha Ufunuo, au je, alikuwa ameanza kuipa jina jipya lingine la kuitukuza siku hii ya Jumapili kwa kuwa ilikuwa sasa kwenye mkanganyo?

Majibu ya maswali haya hususan kwenye waraka, inaonekana kwamba maelezo yaleyale yametumika mara nane tayari na Watakatifu Luka na Petro wote wakiwa kwenye uvuvio wa Roho Mtakatifu na wasingemtia moyo Mtakatifu Yohana kuiita Jumapili kuwa siku ya Bwana wakati kwamba aliwavuvia Watakatifu Luka, Paulo na Petro, kwa pamoja kuiita siku ya hukumu kuwa “siku ya Bwana." Hesabu au kuchukulia kuwa  wa Dialecticians miongoni mwa nia zisizo na makosa za kuthibitika, nia ya kimaadili ya mlinganisho au mashitaka, kwa yale tunayowezeshwa kuhitimisha na mambo fulani ya maana ya maelezo yaliyotakwa mara nane, tunahitimisha kwamba maelezo hayahaya yanaweza kuwa ni maana yaleyale tu wakati inapotamkwa mara tisa, hususan wakati tunapojua kwamba kwa maeneo tisa maelezo yake yalikuwa na uvuvio wa Roho Mtakatifu.

Wala maeneo yaliyo imara zaidi kwa undani yanataka kuthibitisha kwamba haya ni kama maandiko dada, yanayobeba maana ileile, ya Mtakatifu Yohana (Ufunuo 1:10) inasema:

" Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana;"

Lakini anatuonyesha sisi maelezo kwenye sura ya nne, aya ya kwanza na ya pili;

"Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile…ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo."

Hebu na tupande juu katika roho pamoja na Yohana. Wakati upi na wapi?—ingawa kwamba "mlango wa mbinguni," huko mbinguni. Na ni nini tutakachokiona?--"Mambo ambayo hayanabudi kutokea," Sura ya nne, aya ya kwanza. Aliinuliwa katika roho mbinguni. Aliamriwa na kuongozwa kuandika, kiukamilifu maono ya kile kitakachoweza kuanza kutokea na kuambatana kabisa kwayo, "siku ya Bwana," au siku ya hukumu, maelezo ya “siku ya Bwana” yanayothibitika kwenye Maandiko Matakatifu kuwa ni siku ya hukumu, ikijumuishwa.

Tumekusanywa kistudio na kiusahihi sana kutoka kwenye Agano Jipya kila uthibitisho unaoonekana ambao ungeweza kuwa shahidi kwa kuzipenda sheria au torati na wakihalifu na kuibatilisha siku ya Sabato iliyoagizwa kwenye torati au sheria za kwanza au mtu anayeiingiza siku nyingine kwa Wakristo walioenea kote kote. Tumekuwa waangalifu sana kufanya tofauti ya hapo juu, isije ikaendelea na ile ya tatu (kwenye jarida la jinsi Wakatoliki walivyoigeuza amri ya Sabato na kuiweka kuwa amri ya tatu) amri hii ilitanguliwa kwa walichokiita amri mpya. Aina yoyote ya maombi kama yale yamekuwa yakizidiwa na matendo ya Baraza la Wazee wa Maaskofu wa Kimethodisti kwenye vikao vyao vya kichungaji vya mwaka 1874, na kunukuliwa na gazeti la the New York Herald la mwaka huohuo, la siku iliyofuatia kwa kichwa cha maneno kisemacho; "Sabato ilianza tangu mwanzoni na kuthibitishwa tena na Musa na manabii hawakuitangua kamwe kabisa. Sehemu mojawapo ya sheria za kijamii na kimaadili sio sehemu au wadhifa wa utakaso vimeondolewa mbali." Maelezo rasmi ya hapo juu yamejikita kwamba sehemu kubwa ya Wakristo wanaotumia Biblia kwa kuiendeleza amri hii ya tatu kwa mtindo unaoonekana kwenye hii inayojulikana kama amri au sheria mpya.

Hapa tunaomba kupumzika tena kutoa mwito kwa viongozi wetu kwenye ile ya ishirini ya “makala thelathini na tisa za dini” za Kitabu cha Maombi ya Kawaida isemayo “siyo dhambi kwa kanisa kuingiza kitu chochote kilicho kinyume na neno lililoandikwa la Mungu"

HITIMISHO

Kwenye mfululizo wa makala hizi tumebeba maumivu mengi kuwaelekeza wasomaji wetu na kuwaandaa kwa kuwapelekea idadi ya kweli zisizopingika zilizopatikana kwenye neno la Mungu na kufikia kwenye hitimisho kamili lisilomegeka vipande. Wakati mfumo wa Kibilia unapoingia kwenye mwonekano kwenye karne ya kumi na sita, haukukumba tu umiliki wa kitambo wa Kanisa, bali kwa kutumia vita yake ya kidhalimu ya kidini uliujipaka rangi ya Ukristo, zaidi ya vile ungalivyopasa kuwa, kwa sakramenti zote zilizoanzishwa na Mwanzilishi wake, wa dhabihu takatifu, nk, nk, kwa kuchukua kutoka kwenye Biblia na sio kwingineko, ambavyo wanaoipinga na kwendana kinyume nayo wanadai kuwa mwaliku wao mkuu ni Biblia kwenye mafundisho ya Makanisani mwao na kimaadili.

 

Kuu miongoni mwa makala zao za imani ilikuwa, na hata leo inaendelea kuwa, umuhimu endelevu wa kuitunza Sabato kitakatifu. Kwa kweli, imekuwa hivyo kwa kipindi kilichopita cha miaka 300 makala ekee ya imani ya Kikristo ambayo kwayo kumekuwa na mlingano endelevu wa wakilishi wa Biblia. Kuitunza Sabato kunapelekea hesabu na umuhimu wa dhana ya Biblia. Madhabahu zinalipuka kila wiki na kuendeleza malaulu na misuto yasiyo na maana muhimu ya kuitunza Sabato kwenye nchi za Kikatoliki kama ilivyoknganyishwa na aina makini ya Kikristo, mtindo wa kujiamini na kujitosheleza wa kuishika siku kwenye nchi za Kibiblia. Ni nani anaweza kusahau ujima mkamilifu ulioonyeshwa na wahubiri wa Biblia kwa kupitia urefu na upana wa nchi yetu, kutoka kwa kila madhabahu ya Kiprotestanti kwa kadiri ya swali la ufunguaji wa Maonyesho ya Ulimwengu siku ya Jumapili kulikuwa bado hakujaamuliwa; na ni nani asiyejua leo, kwamba dini kubwa moja, kuifanya takatifu imani yao ya kienyeji kwenye maamuzi, haijawahi kufungua kamwe bado maboksi ambayo yanamakala ndani yake kwenye Maonyesho ya Dunia?

Wakristo hawa wenye uzuri uliobora na laini, wakidanganya kwa kutumia biblia yao kikamilifu, wanaweza kuwakuta washirika wao kwenye daraja fulani la watu wenye tabia na imani nzuri kwenye siku za Mkombozi, aliyemtafuta usiku na mchana, akikatishwa tama na kuwa na kihoro kupita kawaida na akituhumiwa zaidi ya kuvumiliwa, kwa kuwa hakuwa ameishika Sabato ishika Sabato kwa maana iliyonyooka moja kwa moja kama wenyewe.

Walimuwinda kwa kutumia akili za kuzaliwa kwa kuitaja siku, na hakukuta wasifa ulielezewa vyakutosha kwenye bezo kubwa la majivuno yao ya Kifarisayo. Na inawezekana sana kwamba mawazo ya kimungu hayakuweza kurekebisha mtazamo wao leo wakitoa sauti isiyosikika vyema ya kilio kisichojaliwa cha wafuasi wao na wanaowahurumia kwenye kipindi cha mwisho mwa karne hii ya kumi na tisa. Lakini wakati kunapoongeza kwenye kweli hizi zote kwamba wakati Mafarisayo wa zamani walipoitunza Sabato, Mafarisayo wetu wa sasa wanahesabu kutokana na wepesi wa kuamini na urahisi wa madanganyo yao, ambazo hazijawahi kuwepo kabisa maishani mwao fursa ya kuishika Sabato ya kweli ambayo Bwana wao mchamungu aliishika hadi siku ya kufa kwake na mbayo hata mitume waliishika, baada ya mfano wake kwa kipindi cha miaka thelathini na baada ya hapo kwa mujibu wa Rekodi Takatifu za mandiko, mkanganyo mkubwa wa kifikra unaojumuisha makufuru ya makusudi ya kukataa maelezo mazuri na chanya tunayopewa leo kwa matendo ya ulimwengu wa Wakristo wanaoiamini Biblia. Biblia na Sabato vinafanya neno la kuangaliwa na Waprotestanti, lakini tumeonyesha kwamba ilikuwa ni Biblia dhidi ya Sabato yao. Tumeonyesha kwamba hakuna mkanganyo mkubwa sana uliowahi kuwepo ila mawazo yao na matendo. Tumethibitisha kwamba sio mababa zao wa kibiblia wala wao wenyewe waliowahi kuishika na kuiadhimisha siku hii ya Sabato maishani mwao.

Waisraeli na Waadventista Wasabato ni mashahidi wa maadhimisho yao ya kila juma ya siku inayoamriwa na Mungu na kwa kurudiwa rudiwa sana, na wakati wanapoipuuzia na kumlaumu mwalimu wao, Biblia, wanakuwa wameiga siku inayoadhimishwa na Kanisa la Wakatolitki. Kile Waprotestanti wanachoweza kufanya, baada ya kufuatia makala hizi, kwa umakini mkubwa, kuendelea kuziasi amri ya Mungu inayowataka kuiadhimisha siku ya Sabato ambayo ni Jumamosi, ambayo ni amri ambayo mwalimu wake, Biblia kutoka Mwanzo hadi ufunuo, iliyoandika kuwa ni mapenzi ya Mungu?

Historia ya dunia haielezi wala kutoa kielelezo ay sampuli ya kipuuzi zaidi, kujitosheleza kibinafsi ya kutelekezwa kikanuni zaidi ya hii. Mwalimu anataka kwa msisitizo mkubwa kwenye kila ukurasa kwamba sheria ya Sabato ni lazima iadhimishwe kila juma, wote wanaoitambua hii kama  "ni mwalimu pekee aliyevuviwa peke," wakati wanafunzi wa mwalimu yule hawajawa ni wamoja tu kwa kipindi chote cha miaka mla tatu wakiadhmisha na kuiheshimu amri hii kutoka mbinguni! Ukubwa ule wa kundi au mkusanyiko wa Wakristo wanaoiamini Biblia, Wamethodisti wametangaza kwamba Sabato haijatanguliwa bado kabisa, sawa na wafuasi wa Kanisa la Uingereza, pamoja na kanisa dada la Kiaskofu (Episcopal) la Marekani wamejitoa mhanga kwa makala hizi ishirini za kidini, tayari wakinukuu kwa mujibu wa sheria kwamba Kanisa haliwezi kuvunja sheria kuamua kuingiza kitu chochote kile “kilicho kinyume na mapenzi ya Mungu na neno lake lililoandikwa.” Neno la Mungu lililoandikwa linaamuru ibada zake zifanywe na kuadhimishwa siku ya Sabato, Jumamosi, na imerudiwa mara nyingi sana, na kwa msisitizo mkubwa sana, na kwa mkazo mkubwa ulio chanya kwa kuamuru auawe mtu anayeivunja au kuitia unajisi. Dini zote kubwa zinazodai kuitumia Biblia zinakuwa na hali ya kujihesabia haki kuamini kuwa hakuna maelezo yanayoweza kurekebisha, zaidi ya kushindwa kuthibitisha.

Ni kweli kiasi gani maneno ya Roho Mtakatifu yanaendana na hali ya kusikitisha! "Iniquitas mentita est sibi"- "Uovu umejidanganya wenyewe." Kushauri kuifuata Biblia peke yake kama mwalimu, lakini mbele ya ulimwengu, mwalimu huyu akiwa anatupwa nje na kupuuzwa kwa kiasi kikubwa sana, kwa mafundisho na matendo ya Kanisa la Wakatoliki- "mama wa machukizo," wakati inapoendana na malengo yao na kwa hiyo kumstahilisha – aige na kuchukua zaidi ya mkazo hatari uliotamkwa na Mungu mwenyewe dhidi ya wale wanaoasi amri, "Ikumbuke Sabato kuishika Sabato na kuitakatifuza."

Kabla ya kufunga mlolongo wa makala hii, tunawaomba wasomaji wetu kutilia maanani kwa mara nyingine tena kwenye makosa yetu, utambulishaji wa kila moja, dhidi ya, 1. Sabato ya Wakristo, kizazi halisi cha muungano wa Roho Mtakatifu na Kanisa Katoliki mwenzi wake. 2. Madai ya Waprotestanti kwa sehemu yoyote iliyopo yalithibitisha kuwa hayana mashiko, yanajikanganya yenyewe na yanajinyonga kimhanga.

Ushauri wa kwanza unahitaji uthibitisho kidogo. Kanisa Katoliki kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu moja cha kabla ya kuwepo kwa Uprotestanti, kwa kujiona kwake kuwa ina kazi mkakati ya kimungu, lilibadilisha siku hii kutoka Jumamosi na kuwa Jumapili. Tunasema kutokana na mamlaka yake ya kimisheni ya kimungu, kwa kuwa yeye aliyejiita mwenyewe kuwa ni “Bwana wa Sabato,” ametoa wakfu mali zake kanisa hili kwa uweza wake wa kufundisha “Yeye akusikiaye wewe, ananisikia mimi,” likawaamuru watu wote wanaomuamini yeye walisikilize kanisa hili pia, kwa hukumu au adhabu ya kuwekwa na "wapagani wasioamini na watoza ushuru;" na kwamba ameahini kuwa pamoja nalo hadi mwisho wa dunia. Anashikilia nembo kwa kujifanya kuwa ni mwalimu na kumpoka mamlaka ya kuwa hakosei na wa milele. Ulimwengu wa Kiprotestanti ulipoanza uliukuta Ukristo wa Kisabato ukiwa imara na wenye nguvu sana ukiwa imezungushiwa kufikia kiwango cha uwepo wake; na kwahiyo ulituama chini ya umuhimu wa kuridhia kwenye mpangilio, ambao unaonyesha dalili za kulipa haki au uhalali Kanisa kuibadilisha siku, kwa kipindi cha zaidi ya miaka mia tatu. Ukristo wa Kisabato kwa hiyo hadi leo, uzao unaojulikana na Kanisa Katoliki kuwa ni kama mwenza wa karibu wa Roho Mtakatifu bila neno la kupinga kutoka kwenye ulimwengu wa Kiprotestanti.

Hebu na sasa hatahivyo, tuangalie wazo letu la pili, kwa kuitumia Biblia peke yake ikiwa kama mwalimu pekee anayekataza sana na kwa msisitizo mkubwa kufanyika mabadiliko yoyote ya siku kwa sababu muhimu na za msingi. Amri inaliita hili kuwa ni “agano la milele.” Siku iliyoamriwa kuadhimishwa na mwalimu imekuwa haiadhimishwi kamwe kabisa. Hii imefanya kuendeleza kwa upotoe na ukengeufu kutokana na kile kinachodhaniwa kuwa ni kanuni iliyowekwa, inavojikanganya, inayojihesabia haki na hatimayake kujimaliza kama ilivyo nguvu ya lugha inavyosema.

Wala hata vikomo vya kuvunja mioyo watu haviyafikiwa bado. Zaidi ya hiyo. Kujifanya kwao kuwa ni kitovu cha Kanisa Katoliki ulikuwa ni ukengeufu kutokana na ukweli uliofundishwa kwenye neno lililoandikwa. Kujifanya kwao kuwa neno hili lililoandikwa kuwa ndilo mwalimu wao pekee, ambalo wamelibatilisha kwa haraka kama walivyoliacha kwa haraka na ghafla, kama makala hizi zilivyothibitisha kikamilifu, na kugeuza kwa kufanya makosa ya kimakusudi, wanakubaliana na mafundisho ya Kanisa Katoliki kwa kupinga wazi, mafundisho yasiyobadilika na yaliyosimama kama yalivyo ya mwalimu mkuu kwenye fundisho muhimu sana la dini yao, kwa hiyo wakaisisitizia kwa nguvu zote jambo ambalo limewekwa tu mara moja la kile kinachoonekana kama “dhihaka, udanganyifu kukengeusha na mtego kwao."

[Nasaha za Mhariri: Ilikuwa ni kwenye hali hii hii ndipo Matengenezo yalilaumiwa na kushutumiwa na Baraza la Mtaguso wa Trent. Wanamatengenezo wamekuwa wakishitakiwa au kulaumiwa kila mara kama ilivyoelezwa hapa kwamba Kanisa Katoliki liliwakengeusha kutoka kwenye ukweli kama ulivyoandikwa kwenye neno lililoandikwa. Hili “Neno Lililoandikwa,” “Biblia na ni Biblia peke yake,” “Asema Bwana,” haya ndiyo yalikuwa ni maneno yake ya kutuonyesha; na “Maandiko Matakatifu kama yalivyo kuwa ni andiko lililoandikwa, ni kiwango kamili cha kupimia mambo.” Hii ilikuwa ndiyo tamko lililotangazwa kwenye jukwaa la Wanamatengenezo na Waprotestanti. “Maandiko Matakatifu na mapokeo.” Biblia kama ilivyotafsiriwa na Kanisa na kwa mujibu wa vhanzo visivyojulikana vya mababa.” Huu ndio ulikuwa msimamo na madai ya Kanisa Katoliki. Hili lilikuwa ni jambo kuu na muhimu kwenye Mtaguso wa Trent, ambao uliitishwa maalumu ili kushughulikia maswali ambayo yalikuwa yameibuka na kupata nguvu na msukumo mioyoni mwa Wanamatengenezo hawa na Ulaya kote pia. Swali la kwanza kabisa kuhusu imani ambalo lilijadiliwa kwenye mtaguso lilikuwa ni swali lililohusika na kupelekea kwa kikao hiki. Kulikuwa na upande wenye nguvu hata na Wakatoliki waliokuwa kenye hili Baraza lenyewe ambao walikuwa wanapenda kuyaondoa mafundisho ya kimapokeo na kuyatumia Maandiko Matakatifu peke yake, kuwa ndicho kipimo cha mamlaka yao. Mtazamo huu uliamriwa uwe kwenye mjadala kwenye baraza kwamba wawakilishi wa papa kwa kweli walimuandikia kwamba kulikuwa kuwa “kulikuwa na msukumo mkubwa wa kuyaondoa na kuachana na mapokeo yote kabisa, na kuyafanya Maandiko Matakatifu kuwa ni kigezo ekee cha kupimia mambo yote.” Lakini ili kufanya hili kunyeonyesha kabisa ni kwenda mbele zaidi kwenye uhalalisho wa madai ya Waprotestanti. Kwa mgongano huu kulikuwa na maendeleo ya sehemu yote ya Wakatoliki ya kazi ya baraza ya kuwashawishi wengine wakubali kwamba “Maandiko Matakatifu pamoja na mapokeo” vilikuwa ni mambo pekee nay a uhakika ya kuyaamini na kusimamia. Kama hii ingefanyika, baraza lingeweza kufanya tangazo la azimio la kuwalaani Matengenezo, vinginevyo sivyo. Swali lenyewe lilijadiliwa siku hadi siku, hadi baraza lilipolileta kwa haki kwenye msimamo wake. Hatimaye, baada ya kipindi kirefu cha kuchosha akili, Askofu Mkuu wa Reggio alikuja kwenye mtaguso huu akiwa amejipanga kwa hoja zifuatazo kwa wale walioshikilia kuwa maandiko peke yake yatumike kuamua kila jambo: “Waprotestanti wanadai kuwa wanasimamia maandiko peke yake. Wanadai na kujigamba kuwa wanaamini Maandiko Matakatifu peke yake kuwa ndiyo kipimo cha imani yao. Wanauhesabia haki uasi wao kwa madai kwamba Kanisa limekengeuka kutoka kwenye meneno yaliyoandikwa na kwamba limefuata mapokeo. Sasa, madai ya Waprotestanti kwamba wanasimama kwenye neno peke yake siyo ya kweli. Madai yao kwamba wanayashikilia Maandiko Matakatifu eke yake kama ni kipimo cha imani yao ni ya uwongo. HEBU THIBITISHA. Neno au Maandiko Matakatifu yamesisitiza kwa nguvu zote uadhimishaji wa siku ya saba ya juma ambayo si Sabato. Wao hawaiadhimishi siku ya saba ya juma, bali wanaipinga na kuikataa siku hii. Iwapo kama wangekuwa wanayaamini na kushikilia kuwa Maandiko Matakatifu peke yake ndiyo kipimo cha imani yao, basi wangekuwa wanaiadhimisha siku hii ya saba kama ilivyoamriwa kwenye Maandiko Matakatifu kila mahala. Lakini wao sio tu kuwa wanakataa tu kuiadhimisha Sabato iliyoamriwa kwenye maaniko yaliyoandikwa, bali wameichukua na kuiadhimisha kwa wazi siku ya Jumapili, ambayo inatokana na mapokeo tu ya Kanisa. Kwahiyo ndipo madai ya kwamba ni “Maandiko Matakatifu pekee ndiyo kipimo” yanashindwa, na fundisho la kwamba “Maandiko pamoja na mapokeo Matakatifu” kuwa ni muhimu, yanaonekana kuwa na mashiko kikamilifu, na Waprotestanti wenyewe na wawe waamuzi kuhukumu jambo hili."

Hakukuwa na upataji wa karibu wa hii, kutoka kwa Waprotestanti wenyewe wala kwenye msingi wa imani—Ukiri wa Imani wa Augsburg wa mwaka 1530—umekiri kwa wazi kabisa kwamba “uadhimishaji wa siku ya Bwana” uliwekwa na “Kanisa” peke yake.

Malumbano yalipambamoto kwenye kikao cha baraza kama Uvuvio tu, upande wa “Maandiko Matakatifu” ulisalimu amri na kuachana kabisa, na baraza kwa mara nyingine tena liliwalaani tena Waprotestanti na Matengenezo yote na kuwa walifanya uasi usio na maana wala mashiko kutoka kwenye uhusiano wa kimuungano na mamlaka ya Kanisa Katoliki, na wakaendelea hadi, Aprili 8, 1546 "kwenye tangazo la marufuku mbili, moja ni ile iliyofanywa kuwa sheria, chini ya kufuru ya kwamba Maandiko Matakatifu na mapokeo yanapasa kupokelewa na kuchukuliwa kuwa sawa, na kwamba kanuni ya kitorati {vitabu vya apokrifa} kuwa ni sehemu ya vilivyokubaliwa na kanuni ta Maandiko Matakatifu. Marufuku ya pili iliitangazwa tafsiri ya Vulgate kuwa ni kitu thabiti na kamili na tafsiri yenye kiwango ya Kilatini, na inatoa mamlaka kama hayo kama kuuzidi ubora mtihani asilia wenyewe; unaokataza kutafsiri Maandiko Matakatifu kinyume na uelewa uliopokelewa na kukubalika na Kanisa “au hata kinyume a kundi moja la mjumuisho wa Mababa," nk.

Kwa hiyo ulikuwa uliolingana na matendo ya Uprotestanti pamoja na madai ya Waprotentanti yaliyotolewa kwa Kanisa Katoliki utafutaji wake wa muda mrefu na hamu yake yenye hoja yenye hamasa kubwa ambayo inaulaumu na kuulaani Uprotestanti pamoja na vuguvugu lote la Matengenezo kama ni ubinafsi mkubwa na hamasa ya maasi dhidi ya mamlaka ya kanisa. Na kwenye mkanganyo huu mkubwa, ufunguo, ukuu uliotukuka, na maelezo yenye kina na upeo, yasiyolingana ya Waprotestanti ilikuwa ni kuikataa au kuipinga Sabato ya Bwana, ya siku ya saba, iliyoamriwa kwenye Maandiko Matakatifu na uingizaji na kuiadhimisha siku ya Jumapili ambayo imeamriwa au kuwekwa na Kanisa Katoliki.

Na hivi kwa leo ndivyo ilivyo kuwa ni mahali ambapo pande muhimu kwenye mkanganyo huu. Leo, kama jarida hili linavyoonyesha, hili ni jambo kubwa na muhimu ambalo kwamba Kanisa Katoliki linaimiliki au kufanana na imani ya Kiprotestanti, na ambao kwamba linalaani sababu ya uaarufu wa Uprotestanti kuwa “hauna mashiko wala hauwezi kujitetea, unajikanganya, na unaangamiza.” Watafanya nini Waprotetanti hawa, itafanya nini imani hii ya Kiprotestanti?]

Itakuwa kila kasisi mheshimiwa na wengine, ambao wamekuwa na tabia hizi kulaumu na kupiga makelele juu ya kila kitiwacho unajisi wa kweli au inayodhaniwa ya uple wa bandia, Sabato ya Biblia, fikiri vizuni kuingia kwenye upingaji dhidi ya uchambuzi wetu na Maandiko Matakatifu yenye mashiko ya mwenzi wao wa amna mbili, tunaweza kuwaahidi wao kwamba jaribio lolote lenye maana kwa upande wao la kukusanya tabia ya kiafrikasti, na kuifanya upya hii uwepo wake uliopakwa rangi, utapewa mtazamo maalumu na wenye kutiliwa maani zaidi na wa heshima kwa upande wetu.

Lakini tunaweza kuwahakikishia wasomaji wetu kuwa tunawajua makasisi hawa waiga kelele wazuri sana wanaotarajia kuzomewa kwa mguno kubwa na wao kwenye mfano huu. Na wanatujua sisi vizuri sana wakijinyenyekeza kwenye kujiweka nia ambayo ni uchambuzi zaidi kwa haya maswali nanayopinga maandiko ambayo ni lazima kabisa yangeweza kufikia mwisho. Sera yao sasa ni “kukomesha” na wana uhakika wa kuichukua na kuifanyia kazi.

Sehemu ya Nyongeza ya I

Makala hizi zimechapishwa tena, na kijarida hiki kimepelekwa na wachapishaji, kwa kuwa kinatoa habari kutoka kwenye vyanzo visivyoweza kukanushika na kwenye chanzo kisichoonewa mashaka, maandiko au makala ya hivi karibuni kabisa kuhusu mkanganyo wa maadhimisho ya Jumapili, ambayo sasa, na ambayo kwa kweli kwa kipindi fulani yamekuwa, sio kwamba ni swali la kitaifa tu pamoja na uongozi wa mataifa, bali pia ni suala la kimataifa. Sio kuwa tunafurahia kuona iko hivyo; tungeweza kuona hivyo na zaidi vinginevyo. Tungewaona Waprotestanti kila mahali wakiwa kwa uwingi na kikamilifu kwenye ukiri na matendo ambayo yangeweza kuwa hayawezekani kuwa na mashiko kwenye uhusiano kati yao na Roma ambao haujawahi kuwa na sura, ambayo kwa sasa wameichukua.

 

Lakini hali kwenye jambo hili kwa sasa ni kama ilivyokuwa imelazimishwa. Hakuna jinsi ya kuuepuka ukweli huu. Na kwa hiyo inakuwa ni kazi ya Ushirika ujulikanao kama International Religious Liberty Association kuwezesha ijulikane kwa upana sana iwezekanavyo mwonekano wa kweli wa swali hili kuu kama linavyo simama sasa. Sio kwakuwa tunafurahia kuwa nayo kama hivyo, lakini kwa kuwa ipo hivyo, chochote ambacho sisi au mwingine yeyote hawezi kuoenda kuwa nacho.

 

Ni kweli kwamba tumekuwa tukiangalia kwa kipindi cha miaka kadhaa kwenye swali kudhania kikamilifu sana kwamba msimamo ambao sasa unadhaniwa, na ambao umewekwa wazi kabisa na kuandikwa kwenye jarida hili. Tumewaambia watu kwa kurudia rudia, na hususan Waprotestanti, na mambo maalumu tumewaambia wale wanaozitetea sheria za Jumapili na kutambulika kwake na kuhalalisha uanzishaji wake na Wamarekani, ambayo ndiyo sababu ambayo ilikuwa inatafutwa waliyokuwa wanaifanyia kazi moja kwa moja kwenye mikono ya Roma, na hii kwa namna fulani kama walivyofanikiwa, waliweza bila kukwepa kuiita Roma na Roma ikachukua mamlaka pia, kuwaongoza wao na kuwafanya kwa nini Jumapili inaadhimishwa. Jambo hili tumewaambia watu kwa miaka kadhaa sasa, wangeweza kuja kwa hakika. Na sasa hiyo imekuwa, ni kazi yetu tu kufanya ijulikane kwa upana kama inavyodanganya kwa uwezo wetu kufanya.

 

Inaweza kuulizwa, “Kwa nini Roma haikujitokeza kwa ujasiri kama hivi hapo kabla? Kwa nini lilisubiri muda mrefu kama hivi?” halikupenda kufanya hivyo huko nyuma kabla. Wakati liliposonga mbele lilitaka lisonge mbele kwa nguvu, na ni nguvu ambayo halijawahi kuwanayo hapo kabla. Lakini kwa juhudi zao kubwa kwa kuitambua serikali yao kitaifa na kuianzisha kwao Jumapili, Waprotestanti wa Marekani walikuwa wanafanya zaidi kwenye kanisa hili kuliko huenda hata lingalivyoweza kufanya lenyewe kwa jinsi au namna ya kupata mamlaka ya kiserikali mikononi mwake. Hili walilijua kabisa, na kwa hiyo walilingojea tu. Na sasa ndpo Waprotestanti wako kwenye ushirikiano ransi na kanisa hilo, na wamehitimisha kwa mafanikio makubwa kufikia lengo la jambo hili la kutisha na la hatari, na kwa mara nyingine linainuka kwa kiburi cha uenyeji na kwa roho ya zamani, na kuwatolea mwito Waprotestanti kulipa majibu ya kwa nini wanaiadhmisha siku ya Jumapili. Hili pia analifanya kwa kuwa linajina lipo salama kwa nguvu na mamlaka waliyonayo Waprotestanti ambayo wameyasalimisha mikononi mwake na wakawa kwenye hali ya upofu. Kwa maneno mengine ni kwamba nguvu ambazo Waprotestanti wanazo, ndizo walizozisalimisha mikononi mwake na ambazo ndizo litazitumia kwa uharibifu. Je, kuna ushahidi mwingine wowote unaotakiwa kuonyesha kwamba jarida hili maarufu liitwalo the Catholic Mirror (Ambalo linamaanisha kuwa Kaldinari na Kanisa Katoliki la nchini Marekani) limekuwa likiingojea hii, kuliko ile iliyoishia kwenye ukurasa wa 21 wa kijarida? Tafadhali hebu rudi nyuma na angalia kwenye ukurasa ule na tazama nukuu zilizochukuliwa kutoka kwenye gazeti lijulikanalo kama the New York Herald la mwaka 1874, na ambalo sasa linachukuliwa na kueleza hayo. Je, hii haionyeshi kwa wazi kabisa kwamba maneno waliyoyasema maaskofu wa Kimethodisti, kwa wakati ule tu walimaanisha hili? Na zaidi kuliko hili, Waprotestanti watakuta vitu kama hivyo vingine zaidi ambavyo vitakuwa vimeingizwa, na ambavyo vitakuwa vinatumika kwa namna ambayo itakuwa washangaza wote wawili na kuwafadhaisha au kuwashangaza.

 

Hii kwa sasa ni utata kati ya Kanisa Katoliki na Waprotestanti. Kwa kuwa tunatoa tu nyongeza hizi za gazeti hili la the Catholic Mirror. Vitu muhimu vinavyoleta utata ni vile ambavyo vinadaiwa na Waprotestanti wanaoiadhimisha Jumapili, na sio kwetu sisi. Tunaweza kusema kwa ukweli kabisa “Haya wala siyo mazishi yetu."

 

Kama hawatalijibu swali, atakufanya kunyamaza kwao kuwa ndiyo ukiri wao kuwa yuko sahihi, na ataitumia kama silaha dhidi yao kikamilifu sana. Iwapo kama watajibu, basi atalitumia jibu lao kinyume chao kwa maneno yao wenyewe, na kama ilivyo mara nyingi wanaweza kudai mamlaka ambayo wameyaweka mikononi mwake. Kwa hiyo, kwa kadiri anavyoonyesha kuguswa, iwe kama Waprotestanti watajibu ama la, yote ni sawa tu. Na jinsi anavyowaona, na roho ambayo kwayo anashauri na kupendekeza jinsi ya kuwashughulikia, na roho ambayo aliyonayo katika kuwashughulikia na ambayo inaonekana kwa wazi kabisa kwenye changamoto iliyofanyika kwenye kifungu cha mwisho cha makala zilichochapishwa na kutlewa tena.

 

Kuna mahali pengine pamoja tu pa kukimbilia hawa Waprotestanti. Napo ni kuchukua msimamo wao bila kulegalega na kuwa na msimamo kwenye “maandiko matakatifu yaliyoandikwa peke yake,” “Ni Biblia na ni Biblia peke yake,” na kuiadhimsha Sabato ya Bwana. Na kwa hiyo kuitotambua mamlaka nyingine yoyote ila ile ya Mungu eke yake, kutokuwa na utwesi mwingine ila kumsikiliza yeye peke yake (Ezekieli 20:12, 20), kuzitii amri zake, na kujazwa na nguvu zake, ndipo watakuwa na ushindi dhidi ya Roma na washirika wake wote, na kusimama juu ya bahari ya kioo, wakibeba vinubi vya Mungu, ambapo ushindi wao utakuwa wa ni wa kusherehekewa milele (Ufunuo 18, na 15:2-4).

 

Hakujawa na kuchelewa sana bado kwa hawa Waprotestanti kujiokoa wenyewe. Je. Waweza kufanya hivyo? Je, wanaweza kumudu kusimama imara kwa ukiri wa imani ya Waprotestanti? Au je, wataendelea bado kubaki kwenye imani “isiyona mashiko, isiyowezekana kuitetea, inayo jikanganya, na kujimaliza” kwa kudai tu kuwa ni Waprotestanti, lakini wakiwa bado kwenye kundi la Wakatoliki, na huku wakitukanwa na Wakatoliki, na kuvumilia shutuma za Wakatoliki? Je, wataamua kuyachukua maneno matakatifu yaliyoandikwa peke yake, Maandiko Matakatifu peke yake, kama kiongozi wao pekee na kigezo cha cha pekee? Au bado wataendelea kushikilia mafundisho “yasiyeweza kujitete yenyewe, kuwa na mashiko, yanayojikanganya, na yanayojimaliza yenyewe: na kuendeleza kuyafuata matendo yanayoamriwa na mamlaka ya Kanisa Katoliki na kwa kuvaa alama zinazoashiria mamlaka yake? Je, watazitunza Dabato za Bwana, siku ya saba, sawasawa na yalivyoamuru Maandiko Matakatifu? Au je, wataendelea kusali Jumapili kwa kufuata mapokeo ya Kanisa Katoliki?

 

Mpendwa maomaji, ninini utakachokifanya?

 

Sehemu ya Nyongeza ya II

Kwa kuwa toleo la kwanza la chapisho hili limesha chapishwa, lifuatalo linaonekana kwenye kazi ya mhariri kwenye gazeti la the Catholic Mirror la Desemba 23, 1893:

 

"Ushahidi ambao waariri walikuwa wanautafuta, na kuonekana kwa uchapishaji mwingine wa makala hizi na shirika la the International Religious Liberty Association, yaliyochapishwa huko Chicago, yakipewa kicha cha maneno, 'Changamoto ya Roma: Kwa nini Waprotestanti Wanaiadhimisha Jumapili?' na likatolewa liuzwe huko Chicago, New York, California, Tennessee, London, Australia, Cape Town, Africa, na Ontario, Canada, pamoja na uhitaji unaoendelea, umelilazimisha gazeti hili la Mirror kuwa na aina ya kudumu kwao, na hivyo kutosheleza uhitaji.

 

"Kurasa za kipeperushi hiki zinamfunua msomaji moja wapo ya mkanganyo mkubwa na ulioanzishwa unaoendelea kudumu kati ya matendo na elimu-dhana ya ulimwengu wa Waprotestanti, na isiyoweza kuathirika kiurahisi ya sehemu yoyote ya ufumbuzi, dhana inayodai kuwa Biblia pekee ndiye mwalimu, ambayo ndiyo kwa wazi kabisa na kuonyesha upande chanya ikiamuru kuwa Sabato ambayo ni Jumamodi itunzwe na ‘itakaswe,’ wakati matendo yao yakithibitisha kuwa wanaipuuzia kabisa kuipa umuhimu alioamuru mwalimu wao, Biblia, na kuchukua hoja za Wakatoliki kwa karne tatu na nusu, kwa kuacha dhana ya imani yao, walinayoisimamia ulimwenguni leo, wawakilishi wa imani ambayo imekosa mashiko kabisa, wakijikanganya, na kujimaliza ambavyo inaweza kudhaniwa.

 

"Tulihisi kwamba hatuwezi kuwafurahisha zaidi wasomaji wetu ile kuchapisha jalada la ‘Nyongeza’, ambalo shirika la the International Religious Liberty Association, kama shirika kubwa la Kiprotestanti, limeongeza kwenye marudio ya uchapaji wa makala zetu. Ukiperuzi jalada hili la Nyongeza utajifunza na kukubaliana na ukweli kwamba hoja zetu hazijibiwi na kwamba kuwaacha Wakatoliki wengi kwenye maeneo yao waliko ni jambo la ama kuwaacha kwenye maeneo ambako wamekuwa wakipotoshwa kwa kipindi cha takriban karne tatu na nusu, na wakikubaliana na mwalimu wao wenyewe, Biblia, kuwa ni imani nzuri, kama ilivyoshauriwa kwa wazi na waandishi wa jalada hili la ‘Nyongeza,’ linalotangulia kututaka tuishike Sabato ya Jumamosi, siku iliyoamriwa na kuagizwa kwenye Biblia tangu kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo; au kuachana na Biblia kwa kutoifanya kuwa mwalimu wa kamili wa kumfuata, kunakomesha kuwa na msimamo, na kuwa ujenzi udumuo wa kanuni zao wenyewe, na kuziondoleambali nyaraka za kufanyika kuwa raia wa ufalme wa Kristo hapa duniani Kanisa lake- na kutokuwa wahanga tena wa kujidanganya na ulazima wa kujikanganya.

 

"Malumbano yaliyo kwenye jarida hili yametuama sana kwenye neno la Mungu, na yamekuwa yakisomwa kwa ukaribu sana na Biblia mkononi, bila kuwaachia nafasi ya kutoroka Waprotestanri wenye dhamira isipokuwa uachanaji na maadhimisho ya Jumapili na ibada zake, ulioamriwa na mwalimu, Biblia na warudi kwenye Jumamosi, iliyoamriwa na mwalimu, Biblia, au kama hawako tayari kuachana na mapokeo ya Kanisa Katoliki, lililoagiza kuishika siku ya Jumapili, na ambayo wamekubali upinzani usio rasmi na mwalimu wao, Biblia, wanayesisitiza kuwa wanakubaliana naye kwenye mafundisho yake yote. Nia na akili za kibinadamu zinataka kukubaliana na moja au mwingine kati ya fursa hizi, ama Waprotestanti waitunze kitakafitu Jumamosi, au Ukatoliki unaoitakarifuza Jumapili. Mchanganyo hauwezekani."

                                                            q