Makanisa ya Kikristo ya Mungu

 [250]

 

 

 

Usomaji wa Sheria Kama Ulivyofanywa na Ezra na Nehemia [250]

 

(Toleo la 1.0 19980711-19980711) Ipo pia Kwenye Mkanda wa Audio

 

Matengenezo ya Kurejesha Uchaji wa amri za Mungu uliofanya chini ya uongozi wa Ezra na Nehemia yalikuwa ndiyo na maana kubwa sana. Jinsi yalifyofanyika na muda yalivyofanyika na kipindi ambacho yalifanyika likuwa ni uendelezaji kimsisitizo ushikaji wa sheria na mfumo au utaratibu wa Yubile. Mfumo huu unafananishwa kwa maana sawa na kwetu sisi leo

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

(Copyright ã 1998 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org and http://www.ccg.org


Usomaji wa Sheria Kama Ulivyofanywa na Ezra na Nehemia

 


Kuyalinganisha matukio ya Ezra na Nehemia

Nehemia alinuia kufanya marejesho au matengenezo ya kuta za mji wa Yerusalem wakati alipoomba ruhusa ya mfalme ili aruhusiwe kurudi na akaujenge  tena mji kuanzia mwezi wa Nisan (Bab. Nisanu) katika mwaka wa ishirini wa kutawala kwake mfalme Artashasta II (Neh. 2:1-20). Alirudi nyumbani na akaandaa mikakati ya matengenezo haya ya marejesho licha ya upinzani alioupata na kukabiliana na maadui wa Yudea.

 

Makuhani waliokuwa chini ya utendaji kazi wa Kuhani Mkuu, walianza kazi ya ujenzi kutoka kwenye lango la kondoo na matengenezo ya mji yaliyopelekea kurejesha hali yake ya kwanza yalifanywa na watu walioshika zamu za maeneo yao (Neh. 3:2-32; na pia tazama jarida linalosema Dhambi ya Yona na Historia ya Ujenzi mpya wa Hekalu (Na. 13)).

 

Kazi hii ilikamilika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa sita ambao anaitwa Elul katika siku hamsini na mbili za mfalme Artashasta II katika mwaka wa ishirini za kuwala kwake. Huu ulikuwa ni mwaka wa matengenezo mapya ya ujenzi wa ukuta, yaliyoanzia kutaka mwezi wa Nisani uliokuwa ni mwezi uliopigiwa mbiu ya ujenzi mpya wa kuta za mji.

 

Ingawaje kunatofauti ya kimaoni na mtazamo, lakini mwaka huu ulianzia katika Mwezi wa Octoba 386 hadi Octoba 385 KK, (kwa kufuatana na Kalenda ya waliokuwa wakitumia watu wa Babeli) haukuwa mwaka wa Sabato, ukipishana na mwaka wa Thalathini na tisa wa Yubile ya tisa kabla ya kuanza kwa huduma ya Masihi. Kuzaliwa kwa Masihi kulikuwa takriban mwaka wa 5 KK katika Yubile iiyotangulia ya mwaka wa 24 KK hadi 27 BK.

 

Jinsi tunavyoweza kujua mambo haya na jinsi tunavyoweza kujua na kuamini na kuzigawa hizi Sabato na yubile hizi ni kwamba tunafuatilia maelekezo kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya kibiblia.

 

Jinsi tunavyozigundua hizi Yubile kutokana na vifungu vingine vya maandiko matakatifu

Kuna vifungu vingine viwli vya maandiko matakatifu ambavyo vinaweza kutumika katika mchakato mzima wa kuweza kuamua jinsi ya kuzipata hizi yubele na kuweka dhidi ya maandko ya vitabu vya kina Ezra na Nehemia ambako tunakuta tendo hili la Usomaji wa Sheria likitajwa na kuandikwa.

 

Andiko la kwanza ni tunalikuta kwenye maandiko ya vitabu vya Agano la Kale na andiko la pili ni kutokana na uandishi unaoelezea kuhusu kukamilika kwa unabii ulionenwa katika Agano jipya kumhusu Masihi.

 

Nukuu tunazozipata kutoka kwenye Agano la Kale ni kutoka katika unabii wa Ezekieli 1:1-3 unavyosema.

Ezekieli 1:1-3 Ikawa katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa pamoja na watu waliohamishwa, karibu na mto Kebari, nbingu zilifunuka, nikaona maono ya Mungu. 2 Siku ya tano ya mwezi, nao ulikuwa ni mwezi wa tano wa kuhamishwa kwake mfalme Yehoyakin, 3 neno la BWANA lilimjia Ezelieli, kuhani, mwana wa Buzi, kwa dhahiri, katika nchi ya Wkaldayo, karibu na mto Kebari; na mkono wa BWANA ulikuwa hapo juu yake.

 

Maana yake kwa undani ya maono haya yamefafanuliwa kwenye jarida lisemalo Maana ya Maono ya nabii Ezekieli, (Na. 108). Hesabu inafikiliza kwenye mwaka wa kumi na tatu wa mwaka wa kalenda takatifu ambao ni mwaka wa tano wa kutiwa kwake utumwani mfale Yehoyakini au mwaka 594 KK. Sabau zenye kufikirika zinapatikana kwenye jedwali lililoongezewa hapo chini.

 

Kwahiyo, inatuama kwenye ujenzi mpya kuanzia wakati uliohesabiwa na Ezekieli, wa yubile inayoangukia mwaka 574/3 na pia miaka ya 524/3 na kasha miaka ya 74/3 na 24/3 iliyokuwa kwenye karne zilizotangulia Kabla Kuzaliwa kwake Kistro (KK) na miaka ya 27/28 na 77/78 kwenye karne za zama hizi.

 

Mtazamo huu unasaidiwa kwa zaidi sana na kweli kuu ya unabii unaohusu Masihi.

 

Baada ya kuanza kwa mwaka wa kumi na tano wa kaisari Tiberio, ambao unaweza kuwa si wa mapema sana zaidi ya mwaka wa kidunia kwenye mwezi wa Octoba wa 27 KK, Yohana Mbatizaji alianza kuhubiri na kuanza kubatiza watu (Lk. 3:1-22). Roho Mtakatifu akamwita Yesu kutoka Nazareti ili akabatizwe na Yohana kipindi fulani baada ya Yohana kuanza huduma yake. Kwa maneno mengine, kuanzia baada ya mwezi Octoba ya mwaka wa 27 BK.

 

Mara baada ya kubatizwa kwake Kristo, alikwenda nyikani ili ajaribiwe kwa muda wa siku arobaini (Lk. 4:1-2).

 

Baada ya kurudi kwake kukatokea kuelewa kwa kiasi kidogo kuhusu maana na kutimilika kwa unabii jinsi alivyotabiriwa.

 

Luke 4:13-21 Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda. 14 Yesu akarudi kwa nguvu za Roho akaenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando. 15 Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote. 16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya Sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. 17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali ilipoansikwa, 18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema, Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa . 20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi, na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.

 

Masihi alirejea Galilaya kutoka kwenye kipindi chake cha kushinda nyikani kwa muda wa siku arobaini na akiwa Nazareti aliutimia unabii huu wa Mungu uliotolewa na nabii Isaya. Andiko hili linapatikana katika Isaya 61:1-2 na pia linaendelezwa kutoka kwenye Isaya 58:6.

Isaiah 61:1-2  inasema:

Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta, niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2 Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao.

 

Aya hizi kama zilivyoandikwa na Luka ieruka ama kuacha kuandika neno kuwaganga waliovunjika mioyo. Maneno yanayosema kuwaacha huru waliosetwa mnyumbulisho kutoka Isaya 58:6 ambayo ilikuwa inaruhusiwa wakati wa kusoma. (kama ilivyo kwenye Biblia iitwayo Companion Bible katika andiko.la Luka. 4:18). Usemi huu wa Mwaka wa Bwana uliokubaliwa unatafsiriwa na Bullinger kama unaashiria kwenye Yubile kwenye uandishi wa vifungu vya maandiko ya nabii Isaya na anasema inawezekana ikawa ni Yubile au ni kwamba inaitwa tu hivyo kwa sababu ni mwaka wa kuanzishwa kwa huduma ya Kristo. Ni vigumu kujua ni kwa namna gani hii inaweza kuwa ni mwanzo wa huduma ya Kristo kwa kuwa Kristo hakuanza huduma yake hadi baada ya Pasaka ya mwaka 28 BK wakati ambao Yohana Mbatizaji alikuwa amefungwa gerezani (kama tusomavyo kwenye Mat. 4:12-17; Mk. 1:12-14; Yoh. 3:23-24). Alitamka maneno haya akiwa huko Galilaya lakini ilikuwa ni baada ya kujaribiwa kwake na kabla ya Pasaka na kabla Yohana Mbatizaji hajatiwa gerezani. Luka 3:18-20 inamwelezea Yohana akitiwa gerezani lakini inaingiza maelekezo ya kimaandiko. Kufungwa hakumaanishi kuingizwa kwenye naandiko haya kama mwongoza muda lakini zaidi sana kwa maana ya kazi 0kamilifu ya siku zijazo. Mfuatano wa matukio ni kama maelekezo yakizungushiwa matendo mengi sana ya Yohana na huduma yake kama alivyomtangulia Masihi na huduma yake ingawaje walipishana kwa kina. Matukio yaliyoandikwa katika Luka sura ya 4:1-20 ni baada ya kujaribiwa kwake na kabla ya miujiza ya Kana na kabla hajawachagua mitume wake na kwenda Yerusalemu katika kipindi cha Pasaka kuanzia siku ya 1 ya mwezi wa Nisan na mchakato wa Utakaso hadi kuelekea kwenye mwisho wa kpindi (soma jarida lenye kichwa cha somo Kutakaswa kwa Hekalu [241]).

 

Kwa hiyo basi, Usamaji wa gombo la nabii Isaya ulifanyika katika mwaka wa yubile, kama italinganishwa na hesabu za muda za nabii Ezekieli, na Biblia inayoitwa Naves Topical Bible inayachukulia maandiko yaha kama yanayopelekea kwenye maana ya Yubile (soma jarida lenye kichwa cha somo Yubile uk. 755). Huu pia ni Mwaka wa Kuwekwa Huru (soma jarida hilohilo, linganisha na Ezek. 46:17). Kwa hiyo Kristo alitangaza Yubile ya katika mwaka wa 27 BK mapema sana mwanzoni mwa mwaka katika siku ya 1 ya mwezi wa Nisani na baada ya matendo ya Yohana Mbatizaji na kubatizwa kwake na kujaribiwa kwake na Ibilisi katika majaribu ya nyikani. Kwa hiyo huduma yake ilianzia katika mwaka wa kwanza wa yubile ya kumi tangia marejesho ya kidini ya Ezra na Nehemia. Kama marejesho mengine ya kidini ya pili yakianza kwenye yubile ya 2027/28 marejesho ya milenia ya mwaka wa 2028 yatakitangulia kipindi cha yubile ya hamsini, au yubile ya yubile, kuanzia marejesho yale na baada ya yubile ya arobaini ya kuwepo jangwani tangia kipindi cha Masihi. Masihi atakuja mapema katika yubile ya 2027/8 kama kipindi hiki kitafupushwa (soma jarida lisemalo, Dhambi ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13)). Aya hii ihusuyo Masihi inabakia kama ushahidi wa pili kwa nabii Ezekieli na inathibitisha kwamba ufafanuzi na majira yaliyoko katika kitabu cha nabii Nehemia yalikuwa ni ya utaratibu au mfumo wa Sabato na Yubile.

 

Kanuni ya Mzunguko wa Sabato na Sheria

Sheria na amri hizi za Mungu zinatakiwa ni lazima kabisa zisomwe katika mwaka wa Sabato kwa mujibu wa Kumbukumbu la Torati 31:9-12. Tukio hili hutokea kila mwaka wa saba siku ya Sabato. Je, tutauhusishaje mgongano huu ulio wazi katika aya hizi za za Biblia? Jibu lake limetuama kwenye maandiko za aya za Nehemia na Ezra. Kuna sikukuu mbili za Vibanda zilizoelezewa kwenye kitabu cha nabii Ezra. Moja ipo kwenye kitabu cha Ezra 3:4-6. Inasema kwamba waliitunza sikukuu ya Vibanda na Miandamo ya Mwezi Mpya, lakini inasema kwamba msingi wa hekalu ulikuwa haujawekwa bado (aya ya 6). Tunajua kutoka kwenye nyaraka zilizoandikwa kwa Lugha ya kiaramu katika gombo kuu za Kielephanti zikisema kwamba Pasaka iliamriwa kufanyika na Dario II mnamo mwaka 419 KK. Hiii ilifanyika mapema kabla ya kutoa changizo au msaada uliofanywa kwa ajili ya kuliweka wakfu Hekalu katika mwaka wa kumi na tano (kwa wazi kabisa na Dario II) (kwa mujibu wa kitabu cha J.B. Pritchard chenye kichwa cha somo Mashariki ya Karibu ya Kale au the Ancient Near East... Vol. 1, Princeton, 1958, pp. 278-279). Kwa hiyo ni kusema kwamba sikukuu zilikuwa zinaadhimishwa na Ezra zinaifanya Yuda ionekane kuwa walikukuwa wakiishika sikukuu ya Vibanda mapema kabla ya kumalizika kwa Hekalu, mara tu baada ya kurudi kwao na mapema sana kulifanyika usomaji huu wa Sheria wakati wa sikukuu ya Vibanda.

 

Je, tutayahusishaje mafungu haya mawili ya maandiko matakatifu na mlolongo au mafuatano ya mambo yalivyo katika kitabu cha Nehemia? Jibu lake linatuama na mafuatano ya matukio yaliyoko kwenye kitabu cha Nehemia. Kutokana na usomaji wa haraka haraka wa aya za kitabu cha Nehemia inaonekana kwamba habari za ujenzi wa ukuta zinaendelea kutoka miaka ishirini ya Artashasta baada ya kutoa kwake lile tangazo la kuamrisha katika mwezi wa Nisani. Hiii ilikuwa ni kama mwezi Machi/Aprili ya mwaka 385 KK. Ukweli wa mambo ni kwamba ilimalizika kwa muda wa siku hamsini na mbili ambayo ilikuwa ni siku ya Ishirini na tano ya mwezi wa sita (uitwao Elul)k. kwa hiyo ujenzi ulianza katika mwezi wa tano, siku ya pili au ya tatu ya mwezi.

 

Kipindi kilichopo kati yake sio cha miezi michache. Kinahusiana na wakati ulio kati ya mwazi wa Nisani wa mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Artashasta II mnamo mwaka 385 wakati Nehemia alipofanywa kuwa liwali na kipindi cha Usamaji wa Sheria za Mungu. Andiko lililopo katika kitabu cha Nehemia 5:14 sawa na hilo linauhusiano na miaka mingine kumi na mbili iliyofuatia hadi kufikia mwaka wa Thelathini na mbili wa mfalme Artashasta II ambao ni mwaka wa yubile unaoanzia katika Sikukuu ya Baragumu ya yubile kulingana na mujibu wa kalenda inayotumiwa na watu wa Babeli na hii kwa kweli ndivyo ilivyotokea Mwaka wa ishirini wa kutawala kwake mfalme Artashasta II ulioanzia mwezi wa Septemba/Octoba ya mwaka mpya ulio kwa mujibu wa Kalenda ya Wababelonia, mwezi wa Teshritu au Tishri, ambao unalingana na jina lililoko kwenye Kalenda ya Kiyahudi, mwezi wa mwanzo wa miaka ni wa mwaka 386 KK. Ombi na maafikiano ya mfalme Artashasta yalitolewa katika mwezi wa Nisan au Nisanu ya mwaka 385 katikati ya mwaka wa ishirini wa Wababelonia.

 

Bullinger anasema kwamba kulikuwepo na tofauti ya nafasi ya kipindi cha miaka mingi kati ya matukio yaliyotokea na kuandikwa katika Nehemia 7:73 na matukio yaliyoandikwa katika Nehemia 8:1, ambayo tungeweza kuona yakitokea katika kipindi kilichofuatia. Hii inaweza kuwa ni jambo au matukio yaliyoonyeshwa katika Nehemia 7:4 na 7:73 ni kwamba yako zaidi ya wakati ule ule ulioainishwa. Inawezakuwa kwamba waraka ule ni jambo na matukio yaliyoko kwenye sura ya 7:73 ikirejesha kwenye uanzishwaji wa taifa kwa ajili ya maandalizi kwa ajili ya kuweka kwao makazi na kufanya matengenezo ya kidini na marejesho ya yubile ambayo ni mwezi wa saba kama tutakavyoweza kuona.

 

Mwaka wa Thelathini wa utawala wa mfalme Artashasta II ulianzia mwezi Octoba siku ya 1 ya mwezi mwaka 374 KK, ambao ulikuwa ni mwezi wa saba wa Kalenda takatifu ya Mungu, lakini mwesho wa mwaka kwa sababu za yubile, na kipindi cha kupigwa baragumu la Yubile ya Upatanisho, ni katika mwaka ule. Mwaka wa Thelathini na tatu ulianzia ulianzia katika mwezi wa saba wa mwaka wa 373/2. Kwa hiyo mwaka wa Thelathini wa kutawala kwa mfale Artashasta II ulianzia kwenye mwaka wa Yubile wa yubile ya tisa iliyotangulia kuanza kwa huduma ya Masihi. Usomaji wa Sheria ungeweza kuanza kwenye Sabato ama ya mwaka wa Arobaini na tisa au kwenye yubile yenyewe. Tutaweza kujionea jinsi itakavyotokea kwenye Yubile yenyewe. Hesabu za Nehemia zililiweka tukio hili kuwa lilifanyika mwaka wa kumi na mbili inaonekana ni mapema tu kabla ya siku ya 1 ya mwezi wa Nisan wa mwaka uliofuatia wa 373 KK. Tutaweza kupima muda wa kufanyika mambo haya kwenye jedwali lililopo hapo chini.

 

Kifundu cha maandiko kilichoko kwenye sura ya 5 ya kitabu cha Nehemiah kinaongelea kuhusu wokovu wa watu wao na hivyo inaonekaka kwamba kukombolewa kwa watu kumefanywa katika kipindi kilekile cha ujenzi na hiki ni kipindi cha matengenezo ya kidini kinachoonekana kuwepo katika yubile (soma Neh. 5:8-11).

 

Kwa hiyo sura ya 6 ya Nehemia inaenda mbali nyuma hadi kwenye kipindi cha kirefu kabla ya matendo yaliyoko kwenye sura ya 5 ambayo yanajitokeza kuwa kwenye marejesho ya yubile ya kipindi cha mwaka wa Thelathini na moja na kuanza kwa kati wa mwaka wa Thelathini na mbili wa kutawala kwake mfalme Artashasta II. Mlingano wa matukio uko kwenye jedwali lililounganishwa na jarida hili.

 

Bullinger katika Biblia inayoitwa the Companion Bible amegundua kikamilifu kabisa kwamba matendo haya kuhusiana na usomaji wa sheria yanahusiana na mwaka wa Sabato lakini mlingano huu ulioko kwenye ukurasa wa Nyongeza Na. 58 wa Biblia hii ya Kiingereza inayoitwa the Companion Bible umekosea kabisa ukilinganisha na jedwali letu la Nyongeza tutakalokuonyesha hapo chini.

 

Tarehe zilizotolewa kwenye Soncino kwa ajili ya shughuli miaka kumi ya Nehemia (soma Soncino uk. 213) hayapo katika uwiano hata wa mamlaka ya marabi wakale (soma Seder Olam Rabbah 30) na mtazamo wao unaona kwamba kifo cha Ezra kilichotokea takriban mwaka 321 KK kilichukuliwa kama kutokea kwa wakati mmoja na kile cha mfalme Iskanda Mkuu. Ufafanuzi unaonekana kuwa ni jaribio la kuangukia kwenye tafsiri za Uprotestant mamboleo na kujiepusha mashutumu ya wazi ya marabi wa Kiyahudi uliofanywa kwa kupitia unabii wa kuhusuriwa kwa mji wa Yerusalemu mwishoni mwa juma la saba la mwaka la unabii wa Danieli 9:25 [ambao umekosewa katika tafsiri iliyoko kwenye Bibli inayoitwa ni ya Tafsiri ya mfalme Yakobo (KJV) lakini sio kwenye tafsiri ya RSV kama vile ile ya Soncino].

 

Mwishoni mwa kaene ya Kumi na mbili wa Nehemia ilikuwa katika mwaka wa Thelathini na tatu wa utawala wa mfalme Artashasta II, ambao ulianzia kuanzia kwenye kalenda yao yakimapokeo upande wa mashariki kuanzia mwezi wa Octoba au mwezi wa saba chini ya mfumo wa Kibabeli Nehemia alihitimisha shughuli zake kunako mwaka wa Thelathini na mbili wakati alipoweka kumbukumbu shughuli zilizofuatia kuanzia kwenye Sabato na Yubile ya mwaka 375/4 na 374/3 KK ilihesabiwa kutoka Siku ya Upatanisho hadi Siku nyingine ya Upatanisho. Aliandika baada ya mwezi wa Tishri wa mwaka 374 na inaonekana kutokea mapema sana mwezi wa Nisan wa mwaka 373. marejesho yote yalifanyika kipindi alipokuwa anaandika.

 

Jambo lingine na la muhimu sana ni kipindi cha kuwepo kwake huko Babeli na kurudi kwao mjini Yerusalemu. Nehemia ananukuliwa katika lile andiko la Nehemia 13:6b kama alikuwa mbali baada ya kipindi kile cha kuhusuriwa au ukengeufu wa Eliashib.

 

Katika mwaka wa Thelathini na mbili alirejea kutoka Babeli. Alikuwepo kule kwa kipindi fulani na mfalme Artashasta. Meneno yaliyoko kwenye kitabu cha Nehemia yanawezekana hayakuthibitishwa kama inavyoonekana kuwa hakuwepo wakati wa usomwaji wa sheria na utenganisho wa makutano ya watu waliojichanganya (Neh. 13:3-6). Eliashib alikuwa bado ni Kuhani Mkuu na alikuwa amemuweka Tobia kwenye Tobia kwenye shughuli za kuhudumia Hekalu. Makuhani hawakupewa huduma zao stahili ingawaje hii haionekani kwa dhahiri kwenye maandiko matakatifu yahusuyo Usomaji wa Sheria kwenye sura ya 8. Andiko linaashiria kuonyesha kuwa huenda hakuwepo kwenye ukengeufu wa Eliashib na kwamba alirudi baadae ili kufanya marejesho haya. Neno lile lisemalo ilikuwa kabla pale kwenye Nehemia 13:4 linakuwa ni somo au kiini kwenye aya hii kwa vile isemavyo kuwa Kwa wakati huu wote katika aya ya 6.

 

Kutokana na hii ndipo tunajua kwamba, kwa mujibu wa Kalenda ya Wababelonia, kwamba ilikuwa ni lazima kwa Nehemia kwamba alirudi wakati aliposikia matatizo ya huko yaliyojiri baada ya Usomaji wa Sheria za Mungu. Bilashaka watu walikuwa na hali ya kutoridhika. Hii inaonekana kutokana na tendo la Kuhani Mkuu kutozisoma hizi Amri na sheria za Mungu na shughuli zote za marejesho ya kidini kufanywa na Ezra aliyekuwa Mwandishi na hatimaye yalishinikizwa na Nehemia aliyekuwa liwali. Tutajionea hapo nbele baadae jinsi ambavyo mafuatano ya matukio haya yalivyokuwa.

 

Hitimisho ni kwamba, sheria zilisomwa na marejesho yalifanyika katika mwaka wa Yubile kuanzia mwaka 375/4-374/3 KK katika mwezi wa saba wa Sabato na kuishia kwenye mwaka wa mwezi wa saba wa mwaka wa Yubile.

 

Usomaji wa Sheria za Mungu

Kutokana na kumbukumbu tunaona kwamba Usomaji huu wa Sheria ulianzia siku ya Baragumu na uliendelea hadi siku ya pili. Kutokana hali hii tunaweza kukisia kwamba sikukuu ya Baragumu iliishia siku ya Ijumaa katika mwaka ule na hatimaye ilifuatiwa na Sabato. Hesabu ya kipindi cha sikukuu na Usomaji wa Sheria vinathibitisha dhana hii, kama tutakavyo kwena kuona

 

Inadhaniwa kwamba katika mwezi wa saba taifa lote zima lilikuwa limeishaundwa na kuunganishwa pamoja, hekalu lilikuwa limefanyizwa upya na makuhani waliwekwa kwenye zamu zao na mavazi yao ya kikuhani yakatolewa na wakapewa (Neh. 7:73). Hii inaonekana kuweka mkanganyiko na jinsi inavyoonekana na kusomeka katika maandiko ya Nehemia 13:11. Huenda ikawa hesabu ya shughuli yaliyopo kwenye 7:73 ni ya mapema zaidi na nafasi ya kipindi kilichopo kati ya sura ya  7 na sura ya 8 ya kitabu hiki cha  Nehemiah. Tutaliona jambo hili hapo baadae.

 

Nehemiah 7:73 Hivyo makuhani, na Walawi, na mabawabu, na waimbaji, na baadhi ya watu, na Wanethini, na Israeli wote, wakakaa mijini mwao. Hata ulipowadia mwezi wa saba, wana wa Israeli walikuwa wakikaa katika miji yao.

 

Kwa hiyo Usomaji huu ulifanyika baadae. Waisraeli wanaonekana wakijikusanya rasmi kwa ajili ya tukio hili. Maelekezo ya aya hii yanasaidiwa na nukuu rejeo za fafanuzi za marabi.

Nehemiah 8:1-18 Na watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja katika uwanja uliokuwa mbele ya lango la maji; wakamwambia Ezra, mwandishi, akilete kitabu cha torati ya Musa, BWANA aliyowaamuru Israeli

 

Marejesho ya kiimani ya taifa yalikuwa ni ya muhimu katika kuzirejesha sheria na amri za Mungu katika ukamilifu wake. Soncino inafafanua aya hii ya 1 kama ifuatavyo:

Pamoja na kukamilika kwa kuta za mji na kujikuta taifa likiwa salama na watu wake kujisikia kuwa usalama umerejeshwa vilivyo viongozi walichukua hatua za kulinzisha tena uimarishaji au ungamano wa taifa kwa kuwaweka watu katika alama ya kimungu ili kwamba ushirikiano wao uzidi kudumu na kuimarika sana

Usemi unaoonekana kusomeka kwa lugha ya Kiebrania hapa kama  mtaa kwa kweli inamaanisha ni mahali pa kubwa. Kitabu hiki cha fafanuzi cha Soncino kinafafanua kwamba "inaweza kuwa ni sawa tu na ilivyo kwenye kitabu cha Ezra 10:9 ambapo inasemekana kuwa ilikuwa imesimamishwa  mbele ya nyumba ya Mungu kati ya ukuta wa mashariki na ule wa upande wa kusini-mashariki mwa Hekalu".

 

Ezra mwandishi na kuhani aliaminika kuwa ni mwanzilishi wa kutaniko lililojulikana kama Keneseth Haggedolah. au Kutaniko Kuu linaloaminika kuwa liliweka uhusiano kati ya manabii na shule za mwanzo za marabi (soma kitabu hiki cha fafanuzi cha. Soncino sehemu yake ya n. hadi v. 1). Mtazamo huu wa muhimu kwa kuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja au mamlaka kwa wakati huu ya kuweko kwa utaratibu au mfumo wa Kifarisayo na Kirabi.

 

Kitabu hiki cha Soncino kinafafanua kwamba ukweli uliopelekea Ezra kutojumuishwa kwenye orodha ya wale waliojenga tena ukuta inamaanisha kwa kuwa alikuwa ni mzee sana kuweza kushiriki kazi hii ya ujenzi. Hili lingekuwa ni suala gumu sana kuonekana hivyo iwapo kama alifariki dunia mwaka 321 KK kwa kufuata mapokeo yanavyosema. Alipewa amri ya kuwapa Walawi sehemu yao na kulitakasa tena Hekalu katika mwaka wa saba wa kutawala kwake mfalme Artashasta II. Lilisimama hivyo tokea kujengwa kwake katika mwaka wa sita wa kutawala kwake mfalme Darius II bila ya ukamilikaji wake kamili Na pia haikuwa na utaratibu wa kumvika) kuhani (Neh. 7:70-71), hadi kufikia mwishoni mwa kipindi hiki kinachopelekea kwenye matukio haya yaliyotukia mwaka wa Thelathini na mbili wa kutawala kwake mfalme Artashasta. Soncino inaonekana kuwa inajaribu kutanga tanga kati ya rekodi za zamani na tafsiri za siku hizi za Waprotestant na inashindwa kuefezea tatizo kama fafanuzi la wazi katika aya ya I inavyoashiria (pia soma jarida lisemalo  Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi mpya wa Hekalu, (Na. 13)). Hakuna dalili kuonyesha kwamba Ezra alikuwa na zama kuu iliyotukuka kwa namna iwayoyote ile hapa. Kwa kweli yeye hakuwa Kuhani Mkuu. Kwa ajili hii ilidhaniwa kwamba huenda yeye alikuwa amerejea kutokea utumwani Babeli baada ya kipindi hiki cha ujenzi wa ukuta (soma Soncino). Kwa vyovyote vile ilivyokuwa, haijalishi, lamsingi ni kwamba yeye alikuwa kwenye nasafi ya kufanya huduma za kikuhani, mwalimu na mwandishi wa sheria aweze kufanya shughuli hizi. Anaonekana kuwa alichukua majukumu yote kama kiongozi mkuu wa Eliashib kwa kweli ni kwa namna isivyovyema kwa ajili ya jinsi vile alivyokufuru na kulinajisi hekalu la Mungu. Kile tunachokiona hapa ni mageuzi au mapinduzi ya kidini ambapo Kuhani Mkuu na wahudumu wake walishindwa na watu wao na marejesho yalikuwa yakifanyika pasipo wao kuwepo, pasipokuwepo kwa Tirshatha au liwali aliyekuweko huko Babeli, lakini akiwa akali akijua hivyo (soma Neh. 13:4-5, 6-7). Inaonekana kwamba hakuwepo. Kutoka kwenye andiko la  Nehemia 13:6, inaonekana kwamba, katika mwanzoni mwa mwaka wa Thelathini na mbili aliomba ruhusa ya kurudi Yerusalemu huenda ilikuwa ni kwa ajili ya kufanya marejesho ya kiimani au kidini, kutengeneza Hekalu kutokana na matatizo tunayoyasoma kuwa yalikuwepo chini ya uongozi wa Eliashib na kuendelea hadi wakati ule. Na wala hakuhesabika kama ni mchangiaji binafsi kiasi kikubwa cha fedha na vifaa zilizotumika kwa ajili ya kufanikisha shughuli hizi za marejezo na kulitabaruku tena Hekalu la Mungu na agano la kikuhani kwa makuhani. Huu ulikuwa ni mwezi wa Octoba wa mwaka 374 kutokana na Mwaka mpya wa Wababelonia kama mwaka wa pili wa Mwaka Mpya wa Wawababelonia wa Teshritu au Tishri ukianza mwaka wa Thelathini na tatu wa kutawala kwake mfalme Artashasta II. Shughuli zote zilikuwa zimehitimishwa mapema kabla ya mwezi wa saba ambao ni wa  Tishri wa mwaka wa 373. Tunaweza kudhania kutokana na livyo hapo chini kwamba Nehemia alirejea mwezi huu wa Tishri kabla ya sikukuu ya Vibanda na inaonekana kuwa kipindi hiki kilikuwa ni kipindi cha sikukuu ya kuzipiga Baragumu. Kwa hiyo katika Nehemia 13:6 lazima iwe imekusudiwa ili kuashiria kuwa alirudi katika mwaka wa Thelathini na mbili na maneno yaliyokosewana yenye kuchekesha kwenye tafsiri, au basi kuna namna nyingine ya kuelezea.

 

2 Naye Ezra, kuhani, akaileta torati mbele ya kusanyiko, la wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza ya mwezi wa saba. 3 Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakakisikiliza kitabu cha torati

Andiko lililoko hapa linamaana ya moja kwa moja na uwezo wa kuelewa kusikia. Maana au wazo hapa sio tu kwamba ni "ya wote bali ni ya watoto" kama inavyoona Soncino lakini zaidi ni kwa wale wenye uwezo wa kutenda yale waliyoyasikia na kuyawekeza kiumilele. Biblia inaitumia dhana hii ya kuwaganga wasiosikia au kusikia pasipo kusikia kwa walio vipofu wa kiroho (soma Mit. 20:12; 28:9; Mhu. 1:8; Isa. 33:15; Mat. 13:13-15; Lk. 8:10; Mdo 28:26-27; Rum. 10:17; Gal 3:2,5). Kusikia kwa imani.

 

Neno hili Siku ya kwanza kuhusu siku ya Baragumu linamaana hapa ya kwamba muda hapa ulikuwa ni wa shughuli za siku mbili. Siku ya Kwanza ilikuwa ni ya Sikukuu ya Baragumu na Mwandamo wa Mwezi Mpya. Tukio hili lilibeba ujumbe wa ufufuo. Je, tunaweza kukifidia kipindi hiki vile tunavyoweza kujifunza kutokwacho?

 

Kipindi cha Mwandamo wa Mwezi katika Yerusalemu kwa mwaka wa  375 KK kilikuwa kama ifuatavyo:

Tarehe 12 Septemba ilikuwa ni saa 12:40 jioni, siku ya Julian 1584709

Tarehe 12 Oktoba. Ilikuwa saa 12:05 jioni, siku ya  Julian  1584739

Siku ya kwanza ya mwezi, kila siku ilikuwa ni tarehe 13 Septemba na Oktoba na kufuatiwa na siku ya Julian siku yake inayofuata kwa kila mwezi.

Siku ya 1 ya Tishri ilikuwa ni Sep. 13 katika mwaka  375 KK. Hii ilianzia mwaka wa Yubile hadi pale ilipopigwa mbiu ya siku ya Upatanisho mwaka 374 KK.

 

Muda wa Mwandamo wa Mwezi katika Yerusalemu kwa mwaka 374 KK ulikuwa:

Tarehe 1 Septemba ilikuwa ni saa 12:27 alfajiri, siku ya Julian 1585062

Tarehe 12 Oktoba ilikuwa ni saa 12:29 alfujiri Julian 1585092

Lwa hiyo kutokana na kanuni yakinifu, siku ya 1 Tishri ilikuwa ni Okt. 1 374 KK.

 

Uhesabuji ulio kwa mujibu wa mwaka huu wa 374 KK unaamua idadi ya mambo fulani muhumu yaliyofichwa au kudharauliwa na mamlaka ya Marabi.

 

Inaonekana kwamba kulikuweko na sera au kanuni fulani ya makusudi ya kufichana mambo miongoni mwa marabi kwa kipindi cha karne kadhaa. Hali ya kweli huongoa mashaka yote na huthibitisha pande zote mbili zinapokosea na ilishutumiwa na mapokeo. Hata hivyo kwa vyovyote vile inaonyesha uaminifu wa mfumo wa Kiyahudi wa utunzaji wa Sabato na kwa juma kikamilifu kwa kipindi chote kizima.

 

Uamuzi wa Kalenda ukihusishwa na mwezi wa Tishri peke yake kama unavyoamuliwa na kipindi cha usiku na mchana kuwa sawa pia kumeonekana kuwa ni uongo hapa. Kipindi hiki cha usawa wa masaa ya usiku na mchana kinaangukia kwenye mwezi wa Septemba na katika mwaka huu ambao ungalioweza kuwekwa Mwandamo wa Mwezi mapema zaidi katika mwezi wa Nisan kwa mujibu wa kanuni za jumla zilizokubalika kuhusiana na kutokea kwa kipindi hiki mnamo mwezi wa Nisan. Kwa vyovyote vile, siku ya Baragumu isingekuwa siku ya Ijumaa lakini ni siku yenye utata zaidi ya Jumapili kwa ajili hii. Iwapo kama kwa namna iwayoyote ile ikiwa kanuni ya kiwango cha mwezi wa Nisan inafuatwa hapa, kama ilivyoeleweka na Kanisa la kwanza na kama ilivyokuwa ikitumika kwenye kipindi cha Hekalu kwa mujibu wa sheria za Kisadukayo na pia na Wasamaria, ndipo hapo basi Oktoba 1 inaweza kuwa ni siku ya kupiga ukumbusho wa Baragumu na hii huangukia kwenye vile tunavyotegemea kutokana na vile yasemavyo maandiko matakatifu, kwamba ni siku ya Ijumaa. Hata hivyo, kuna idadi fulani ya mambo ya kuigiza hapa ambayo yamekomeshwa pia.

 

Kwa hiyo marejesho ni kama yanavyoeleweka kuwa yalitokea kwenye yubile kwa kipindi cha mwezi wa saba kuendelea hadi kufikia siku inayojulikana kama ni Siku ya Mwisho Iliyokuu Kuu na marejesho yaliofanyika kama vile tungalivyoweza kutegemea chini ya sheria. Inaonekana toka kwenye maandiko matakatifu katika kitabu cha Nehemia kwamba walifikia kwenye uelewa kamili kuhusiana na jambo hili wakati wa mwaka ule wa Sabato na kuifanyia kazi mnamo mwezi wa saba wa ile yubile yenyewe na inaonekana kuwa kwenye upinzani na Kuhani Mkuu na wasaidizi wake. Pengine ile inaelezea sababu ya Hekalu limekuwa ni mlengwa wa marejesho haya kwenye Usomaji huu wa Sheria na Amri za Mungu.

 

Utaratibu au mfumo ulioahirishwa unaonekana kuwa haufai kadiri vile Mwandamo Mpya wa Mwezi ulivyoonekana majira ya saa 12:29 alfajiri. pia kuna Sabato za nyuma kwa nyuma zinazohusishwa hapa. Kwa hiyo basi, utaratibu wa kuunganisha unaonekana kuwepo kwenye mahala ambapo tungalipoweza kutagemea kwa akili zetu kama mfumo wa Masadukayo na Wasamaria wa utendaji kazi uliokuwepo wakati wa kipindi cha Hekalu lililopita na kuanzia kwenye Mishnah zikitiliwa maanani zile Sabato za huko nyuma na pia siku ya Upatanisho.

 

Kwa hiyo shughuli hizi zilizoelekezwa hapa katika kitabu hiki cha Nehemia zinahusiana na marejesho na yanakuwa ni kile tungalichoweza kukitegemea kutokea katika Yubile na mwaka wa Sabato. Maandalizi ya mwaka wa Sabato yalifungamanishwa kwenye Yubile na kujulikana kama ni kipindi cha matengenezo makuu ya marejesho ya imani ya kidini ya historia ya kiyahudi.

 

Maandiko yanaonyesha kwamba katika tukio hili la kupigwa kwa Baragumu lilikuwa linafuatia siku inayofuata. Biblia iko kimya na haisemi lolote kuhusiana na kuduku kwa sikukuu ya Baragumu hadi siku ya pili na Marabi wanajaribu wanajaribu kupenyeza kidogokidogo ionekane kwamba hii ilikuwa ni adhimisho la Rosh Hashanah la siku mbili, Mwaka Mpya, siku ya kutaniko takatifu na kunukuu katika kitabu cha Mambo ya Walawi 23:24. Ni kwa vyovyota vile ipo kimwa kwa maana sana kwa maelekezo yaliyo dhahiri ya Mungu kwamba mwezi wa Abib au Nisan na uwe ni mwezi wa kwanza ambao ni mwanzo wa miezi na uwe ni Mwaka Mpya kwa Waisraeli kama isemavyo (Kut. 12:2). Rosh Hashanah, Mwaka Mpya wa Wababelonia katika mwezi wa Tishri, haukuelekezwa hadi kufikia kipindi cha Kimishna tangia karne ya 3 baada ya kifo cha Kriisto (soma jarida la mwandishi Kohn lisemalo Wasabato wa Transylvania).

 

Aya ya 3 inasema kwamba Ezra alisoma sheria hadi majira ya mchana. Hii haimaanishi kwamba watu hawakuendelea baada ya muda huo mchana. Kitabu hiki cha Soncino kinasema kwamba ilikuwa ama kwamba maelekezo yaliendelea na wengine tangia muda ule, au kwamba kulikuwa na mapumziko baada ya joto. Andiko hili linaendelea kwa kuelezea kinaga ubaga kile kilichotokea. Inaonekana kuwa madhabahu yanayoonekana hapa ilikuwepo kwenye ngazi iliyoinuka juu ambayo ilichukua makuhani kumi na nne.

4 Naye Ezra kuhani akasimama juu ya mimbari ya miti, waliokuwa wamefanya kwa kusudi hilo; na karibu naye wakasimama Matithia, na Shema, na Anaya, na Uria, na Hilkia, na Maaseya, mkono wake wa kuume; na mkono wake wa kushoto, Pedaya, na Mishaeli, na Malkiya, na Hashumu, na Hashbadani, Zekaria, na Meshulamu. 5 Ezra akakifungua kitabu machoni pa watu wote; (maana alikuwa juu ya watu wote); na hapo alipokifungua, watu wote walisimama; 6 Ezra akamhimidi BWANA, Mungu mkuu. Nao watu wote wakaitikia, Amina, Amina, pamoja na kuinua mikono yao juu; kisha wakainama vichwa vyao, wkamsujudu BWANA kifudifudi. 7 Tena Yeshua, na Bani, na Sheremia, na Yamini, na Akubu, na Shabethai, na Hodai, na Maaseya, na Kelita, na Azaria, na Yozabadi, na Hanani, na Pelaya, nao ni Walawi,, wakawafahamisha watu torati; na watu wakasimama pahali pao. 8 Nao wakasoma katika kitabu, katika torati ya Mungu, kwa sauti ya kusikilika; wakaeleza maana yake, hata wakayafahamu yaliyosomwa,

 

Mafuatano ya matukio ilikuwa ni kwamba watu walisimama kwa ajili ya kupokea baraka na hatimaye sheria zilisomwa na kufundishwa na makuhani na Walawi watu wakiwa wanasoma sheria (baadhi ya majina yanaonekana tena katika sura hizi za 9:4 na 10:10 nk). Maana yake inaeleweka kama inavyosimama kama inavyosimama au kukitiliwa maanani kwenye usomaji wa sheria na sio mazuzungumzo (soma Ayubu 32:16). Kwa hiyo sio kwamba ni suala la kusoma kwa Torati tu, ambayo vinajulikana kama Kumbukumbu la Torati. Sheria ni lazima zifafanuliwe au kufundishwa kipengele kimoja hadi kingine, hapa kidogo kule kidogo, (Isa. 28:10-13). Mafundisho haya ya Sheria yalieleweka kama yalivyofundishwa pia na Musa kama tunavyojionea wenyewe katika Waebrania 9:19.

 

Maandiko yaliyoko kwenye aya ya 8 yanaashiria kuwa makuhani wote waliokuwepo walikuwa na haki kisheria na waliwafafanulia au kuwahubiria watu. Huenda hii ilifanyika kwa kufuata maeneo ya muda kwa kila mmoja binafsi yake au makuhani walipangiwa kwa kupigiwa kura kasha waelekee kwenye maeneo yao.

9 Naye Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani, mwandishi na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa BWANA, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati. 10 Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilichokitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyeweka kitu; maana siku hii ni takatifu kwa BWANA wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.

 

Siku hii ilielezewa kama ni Takatifu na sikukuu ya Bwana na ingawaje haikuwa ni mojawapo ya Sabato ya kila juma, ambayo ahikuhitaji maelekezo, lakini siku ya Sikukuu ambayo ilikuwa ni siku ya kwanza. Enendeni zenu, mle kilichonona,na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiye na kitu; ni amri inayohusiana na sikukuu na jinsi ya kutoa na kuwapa maskini. Kwa hiyo hii Nehemia 13:6 ilitakiwa ichukuliwe ili kuashiria kwamba alikuwa amerejea kutoka Babeli kwa mwaka ule wa Thelathini na mbili. Isingkuwa ni katika ule mwaka uliofuatia kama anavyosema kuwa ni mwaka wa Thelathini na mbili. Mwaka wa Thelathini na tatu ulianzia katika Mwandamo Mpya wa Mwezi wa Tishri mwaka wa 373 ambao ulikuwa ni Mwaka Mpya wa Wababelonia. Nehemia anaonyesha kwamba haya yote yalitokea kwenye mwaka wa Thelathini na mbili na ili kuyakinisha vifungu vyote viwili vya maandiko matakatifu alipaswa arejee katika mwezi wa Tishri wa mwaka 374. Angeweza kurejea kwa ajili ya tukio hili la muhimu na msaada wake ni dhahiri kuwa ungeweza kuorodheshwa. Anasema kwamba hajawahi kuwa kule wakati wa matukio yaliyotukia siku za mapema kabla ya mwaka wa Thelathini na mbili.

 

Kwa hiyo, kuna fursa kuu za namna tatu zinazoyahusu matukio haya na maandiko yahusuyo siku ya Baragumu ya mwaka wa 374 KK.

 

1. Uwezekano mkuu ni kwamba, Nehemia alirejea kwa ajili ya siku ile ya ukumbusho wa kupigwa kwa Baragumu na kwa ajili ya Marejesho. Maandiko mengine yote yanayofuatia yanaonekana kuashiria ukweli ule pia.

2. Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa maandiko yaliyoko kwenye Kitabu cha Nehemiah, yangemjumuisha na yeye kwa sababu alituma msaada wake na maagizo ya kutolewa kwa dhabihu kama ilivyotakiwa kufanya kwa mujibu wa Sheria lakini yeye mwenyewe aliwasili siku ya Baragumu au kabla ya sikukuu ya Vibanda na kumfanya ahesabiwe kwenye orodha ya shughuli au mambo yaliyofanyika. Bado alikuwa ni Tirshatha au liwali ambaye alikuweko Babeli au Yerusalemu.

3. Uwezekano wa tatu ni kwamba alifika kipindi cha kati kati ya maadhimisho ya sikukuu ya Vibanda na hatimaye na kulijenga hekalu na anatajwa kwenye maandiko matakatifu kwa kulinda tu. Huu ni uwezekanao ambao unathibitishwa na maandiko matakatifu yaliyoko katika kitabu cha Nehemia 13:3-6 yakisomwa kwa utenganisho na kukizingatiwa kwamba alikuweko pale siku kadhaa katika mwaka wa Thelathini na mbili. Hata hivyo, ukisoma kwenye sura ya 7 inaonekana kwamba sura ile ya 13 inajumuisha kwa namna ile ikilificha tukio hili.

 

Nyakati za kutokea kwa matukio haya hata hivyo zimekuwa ni kwa wakati muafaka kwa makusudio ya kuamua mwanzo wa mwezi na miaka na haiachii nafasi yoyote kukosewa. Haiwezi kuwa ni mwaka kabla ya kuanza kutoka mwaka wa kiilimwengu wa Kibabeli na mwka unaofuata unaanzia siku ya Baragumu kwa kufuatana na kalenda ya Kiilimwengu ya Wababelonia iliyoingizwa katika Yudea kwa ajili ya umaarufu wake na ikachukuliwa na kutumiwa na Mafarisayo na hatimaye ikaingizwa kwenye mapokeo ya Marabi iliyorithiwa kutoka kwao.

 

Iwapo kama uhesabuji wake ulichukuliwa kutoka mwezi wa Nisan hadi Nisan nyingine mbali na uhesabuji wa kibiblia basi shughuli hii ingechukua mkondo wake kuanzia mwezi wa Marchi hadi Oktoba ya mwaka 374 KK na hakuna tatizo lingaliloweza kutokea kwa namna yoyote ile. Mfale Darius II ameandikwa kuwa alikufa mwaka wa 405 KK na mwandishi maarufu aitwaye Bernard Grun (katika kitabu chake kiitwacho Ratiba ya matukio ya Historia ama The Timetable of History 3rd ed., Touchstone, 1991, p. 14) ambacho kinaunga mkono nukuu hii; (soma kitabu cha. W. Stein kiitwacho  Kulturfahrplan). Huu kwa kweli ni ufumbuzi wa kweli na una athari kubwa ya kimafundisho kwa mfumo wa Kirabi. Nafasi iliyoko sasa ya serikali ya Wamisri inasema kwamba mfalme Dario II alifariki majira ya Baridi ya mwaka 404 KK (hii ni kwa mujibu wa taafira ya jarida la kitalii liitwalo kama Wizara ya Utalii ya Misri kweye wavuti yake ya http://www.touregypt.net/index.htm). Kamusi ya Kiingereza inayoitwa kama The Oxford Classical Dictionary ("Artaxerxes II" 3rd ed, 1996, p. 182; cf. P. Briant De Cyrus á Alexandre, 1996) inasema kwamba kipindi cha kutawala kwake mfalme Artashasta kilikuwa ni takribani kama kwenye miaka ya 405/404-359/358. Ufumbuzi uko rahisi sana na ni wamuhimu sana kwa Wayahudi walioko leo, Wakristo na Waislamu wote kwa pamoja.

Kelenda ya Kiilimwengu ya Kibabeli haikutumika kwa ajili ya kumbukumbu hapa atika habari za Ezra na Nehemiah. Hili ndilo jambo lingaliloweza kutarajiwa kwa ajili ya marejesho ya kweli ya kidini. ukumbusho ni kwa ajili ya mwaka Mtakatifu unaoanzia katika mwezi wa Nisan. Aina yoyote ya kuhesabu miaka inanzia kutoka mwezi wa Nisan hadi Nisan mwingine na kufanya mwaka uanzie kwenye mwezi wa Nisan na maelezo yaliyopo kwenye kitabu cha Nehemia yanahusiana na tendo la Nehemia kurejea kuwa lilifanyika mwanzoni mwa mwaka wa Thelathini na mbili ikihesabiwa kwa kuhesabu tangia kudhaniwa kwa kifo cha baba yake Darius II. Nehemiah alirejea kipindi fulani kifupi baada ya siku ya 1 ya mwezi wa Nisan na wakati wa kukamilisha ujenzi wa hekalu na kuchukua pahala pake katika Maadhisho ya sikukuu kama ilivyoandikwa kufanywa na Ezra. Haya yalikuwa ni marejesho ya kweli ya Mungu.

Madodoso yahusuyo ukweli huu ni mambo yanayohitaji mafundisho ya kina kwa kweli. Huenda yanaelezea sababu za kudhaniwa kwake na dodoso zake vilitolewa na watu wenye msimamo wa Kiyahudi na Wakristo wakazipenda. Inaonyesha kwamba kalenda ya Kibabeli Mwaka Mpya wa Wababeli vilikuwa ni mtazamo wa  siku za baadae zilizokuweko kabla ya kipindi cha Hekalu ambacho marabi wa Kiyahudi walikirithi kutoka kwa marabi wa Kibabeli. Mfumo wao wa kalenda hauna maana na wala waujawahi kuwa na maana yoyote na mfumo wa kweli wa kuendesha shughuli za Hekalu.  Kwa sababu hii dini ya Kiyahudi inaendana sambamba na utaratibu wa Kiprotestant na inajaribu kuigiza ujenzi wa Hekalu na unabii wa  Danieli katika utawala wa Dario I, badala ya Dario II, licha ya maelekezo ya wazi ya Kitabu cha Ezra na maelekezoo ya maandiko ya marabi wa kwanza, yanayomfanya Ezra awe kwenye utendaji wa wakati mmoja na mfalme Iskanda Mkuu, ambao wote walifariki mwaka 321 KK. Ukweli wa jambo ni kwamba kalenda ya Hillel na ule mfumo wa Rosh Hashanah ni wenye kupingana na ukweli wa kazi iliyofanywa na Biblia ya Marabi wa Kiyahudi wa Kibabelonia na hauna maana yoyote wala kuhusiana na mfumo wa Biblia kama unavyorejeshwa hapa na kina Ezra na Nehemia na kutumika kwenye kipindi cha Hekalu. Rosh Hashanah na kalenda ile ambayo kwamba mingu ya kipagani ya Kiyunani imewekwa ndani yake katika hekalu na Antioko Epifania. Ilikuwa ni mfumo huu mbaya wa kuabudu katika Yerusalemu Hekaluni ndio ulioanzisha ujenzi na Onias IV wa Hekalu lililokuweko huko Heliopolis kuona ulazima kwa mujibu wa maongozi ya Mungu katika kitabu cha nabii Isaya 19:19.

Wakati wa marejesho ya kina Ezra na Nehemia watu walilia kwa uchungu kwa sababu walikuwa wameziacha sheria za Mungu na hawakuwa wakizishika sheria ingawaje imeandikwa kwamba walikuwa wakizishika sikukuu za Vibanda na Pasaka (kama ilivyoandikwa katika Ezra 3:4)

Matokeo ni kama kama yale ya mfalme Yosia katika 2Fal 22:11,19. Kazi ya mfalme ni kutoa dhabihu kutoka kwenye Makusanyo au michango ya Mfalme na kwahiyo huenda ilikuwa ni Nehemia kama Tirshatha (au liwali) anayezungumziwa katika aya ya 10 (kinyume kabisa na madai ya Soncino).

11 Hivyo  Walawi wakawatuliza watu wote, wakasema, Nyamazeni kwa maana siku hii ni takatifu; wala msihuzunike. 12 Na watu wote wakaenda zao kula na kunywa, na kuwapelekea watu sehemu, na kufanya furaha nyingi, kwa sababu walikuwa wameyafahamu maneno yale yaliyohubiriwa.

Kutokana na masomo yao na kuhuzunika kupitia umakini wao wa kukataa kwao Sheria, bado wanakutana na furaha katika hizo Sheria na ukarimu au wema wa Mungu. Walitakiwa wawe Wanajisomea hizi Sheria za Mungu kwa kila mwaka wa Sabato unapowadia na sio tu pale wakati wa Yubile. Hakuna taarifa ya tukio lenye kulinganishwa au aina au mfano wa shughuli za Yubile katika mwaka mwingine uwaowote. Sheria zilisomwa hapa kwenye mwaka huu na inaweka alama au ishara ya mambo yote mawili yaani usomaji na shughuli za marejesho. Inapaswa pia ieleweke kwamba Sheria hizi huenda zinasomwa mwishoni mwa mwaka wa Saba wa Sabato wakati wa Sikukuu ya Vibanda ya Yubile pengine badala yake, lakini kila wakati kwa kuongezea, mwanzoni mwa Yubile katika mwezi wa saba wa mwaka wa Arobaini na tisa na mwaka wa Sabato.

13 Hata siku ya pili wakuu wa mbari za mababa za watu wote, na makuhani na Walawi, wakamkusanyikia Ezra, mwandishi, ili wapate kuyasikiliza maneno ya torati. 14 Wakaona ya kuwa imeandikwa katika torati, jinsi BWANA alivyoamuru kwa mkono wa Musa, ya kwamba wana wa Israeli wakae katika vibanda, katika sikukuu ya mwezi wa saba; 15 na ya kwamba wahubiri na kutangaza katika miji yao yote, na katika Yerusalemu, kusema, Enendeni mlimani, mkalete matawi ya mzeituni, na matawi ya mzeituni mwitu, na matawi ya mihadasi, na matawi ya mitende, na matawi ya miti minene, na kufanya vitanda, kama ilivyoandikwa.

Viungo vilivyoko hapa kama vile manemane au hadas shoteh vilitofautiana kutoka lulab au tawi la mtende kama lilivochukuliwa kwenye sherehe za kidini. Mafuta ya mzaituni mwitu kwa maana ya lugha ya moja kwa moja ni miti yenye mafuta (soma mfano Isa. 41:19; na Soncino).

Andiko lisemalo Booths limukutikana katika kitabu cha Mambo ya Walawi 23:40 na kwa hiyo ilikuwa ni Torah ambayo ilikuwa ikispmwa na sio tukwenye kitabu cha Kumbukumbu la Torati.

16 Basi watu wote wakatoka, wakayaleta, wakajifanyia vibanda, kila mtu juu ya dari ya nyumba yake, na katika nyua zao, na katika nyua za nyumba ya Mungu, na katika uwanja wa lango la maji, na katika uwanja wa lango la Efraimu. 17 Na mkutano wote wa watu, waliorudi waliorudi kutoka nchi ya uhamisho wao, wakafanyiza vibanda, wakakaa katika vibanda hivyo, maana tokea siku za Yoshua mwana wa Nuni, hata siku ile, wana wa Israeli hawakufanya hivyo. Pakawa furaha kubwa sana16 Basi watu wote wakatoka, wakayaleta, wakajifanyia vibanda, kila mtu juu ya dari ya nyumba. 18 Tena siku baada ya siku, tangu siku ya kwanza hata siku ya mwisho, akasoma katika kitabu cha torati ya Mungu. Wakafanya sikukuu muda wa siku saba; na siku ya nane palikuwa na kusanyiko la makini, kama ilivyoagizwa.

Jina hili la Yeshua ni aina tu ya uitaji wa Kiebrania wa lile tunaloliita Yoshua na lenye maana ya Yesu kwa Kiyunani.

Ni jambo lililodhahiri kwamba Sikukuu ya Vibanda iliadhimishwa katika miaka ya mwanzoni ya kurejea kwake kama tunavyoweza kuona katika Ezra 3:4. kwa hiyo sikukuu hii ya Vibanda ilikuwa ni ya tofauti na yanamna ya pekee na zile za kawaida. Soncino inajaribu kuielezea sikukuu hii kuwa ilikuwa ni ya furaha kwa kadiri ile ilivyokuwa inasherehekewa lakini kulikuwa na tatizo jingine. Jibu linatuama kwenye aina ya shughuli inayofanyika. Marejesho ya mali, ya vitu vilivyonyang’anywa na ya ardhi na pia ya Waisraeli wenyewe huyafanya maadhimisho haya yawe ni yatofauti y aina yake kama ya Yubile na nyingine hufuatia kutoka kile ambacho tungeweza kukitegemea kukiona kwenye Sabato na marejesho ya Sheria za Mungu.

Marejesho au urejeshaji wa madeni au kilichoazimwa yalithibitishwa kama inavyotakiwa wakati wa maadhimisho ya mwaka wa Yubile kama tunavyoona katika sura ya 5 ya Nehemia, ambayo kutoka Nehemia 5:14 inaonekana kuchukuliwa nafasi yake katika mwaka waThelathini na mbili wa mfalme Artashasta ambayo ilikuwa ni kuanzia mwezi wa Oktoba 374 KK katika kalenda ya Wababelonia lakini kutoka mwezi wa Nisan kwa kalenda ya Kiebrania kama tutakavyoona katika Nehemia sura ya 5 kuanzia aya ya 14 na kuendelea baada ya matukio yanayoilizwa kuhusiana na mpangilio wa muda ulioelezewa kwa kina.

Mwaka unaoweza kuamuliwa kutoka kwenye kalenda iliyotolewa kwenye miaka ya utawala wake mfalme Artashasta II iliyotolewa kwenye kitabu na miaka ya kalenda takatifu. Utaratibu na hesabu vipo pia kwenye jarida lisemalo Dhambi ya Yona na Historia ya Ujengaji Upya wa Hekalu [013].

Usomaji wa sheria unafanywa katika kila mwaka wa Sabato kwa mujibu wa vile isemavyo kwenye kitabu cha Kumbukumbu la Torati 31:10-12. neno hili linalosomeka kama Kitabu cha sheria linaeleweka kama Torah na kumbukumbu imefanywa pia katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 30:10. Kurudi kwao kunajulikana kama Gombo la Torah. Bullinger anafanya ulinganifu uleule na pia anaelekeza pia kwenye kitabu cha 2Fal 22:8 na 23:25 na anaonyesha kwenye kitadu cha Kutoka 17:14 ambacho anaelezea kama hivyo. Katika 2Fal 22:8-13 ikifananishwa na 23:25 inaonekana kwamba kitabu chote cha sheria kilipaswa kiadhimishwe na kwa sababu halikuwa ni taifa lililadhibiwa (aya ya 14 nk).

Tunaona kutoka kwenye aya ya 18 kwamba sheria zilisomwa siku kwa siku na kwa hiyo hazikukubalika kwa kuzisoma tu kwa ile Siku Iliyokuu ya Mwisho au kwenye siku iwayoyote nyingine. Sikukuu iliadhimishwa kila siku kwa mujibu wa sheria zilivyoelekeza na siku ya saba ilikuwa ni siku ya kufanya kutaniko takatifu ikiwa pia ni ile Siku ya Mwisho iliyo Kuu (kama inavyosema Wal. 23:36; Hes. 29:35 nk) zikiambatana na sadaka ama dhabihu zake takatifu (kama isemavyo Soncino).

Katika siku ya Ishirini na nne ya mwezi wa saba ndipo watu walipojitenga nafsi zao. Soncino inashikilia kuamini kwamba hizi zilikuwa ni siku mbili baada ya sikukuu Vibanda au ni sahihi sana kuamini kuwa ilikuwa ni siku mbli baada ya Siku ya Mwisho Iliyokuu. Bullinger anashikilia kuamini kuwa hili lilikuwa ni tukio tofauti lakini Soncino huenda ipo sahihi kama ilivyokuwa inaadhimidhwa kama siku ya kufunga saumu. Hii ilikuwa ni siku ya kwanza ambayo huenda ililazimu watu kufunga mfungo wa saumu na kufanya shughuli kama ilivyoangukia ile Sikukuu ya Siku ya Mwasho Iliyokuu katika siku ya Ijumaa pia ya mwaka wa 374 KK na kwa hiyo kuifanya siku ya kwanza iliyofuatia sikukuu ilikuwa ni Sabato na kwa hiyo hakuna ufungaji wa saumu ungalioweza kufanyika. Mwaka wa Thelathini na nne ulikuwa ni mwaka wa fursa ya kwanza na pia unathibitisha uhesabuji ulioelezewa hapo juu.

Tendo la kuomba dua ya msamaha kwa ajili ya dhambi zilizofanywa na mababa waliopita sio jambo geni kama tunavyoweza kujionea hapa na katika kitabu cha Zaburi na Ezra 9:6-15. Toba ya kila mtu binafsi yake ilikuwa imefanyika katika taifa la Israeli. Mtu mmoja mmoja binafsi yake ni sehemu muhimu inayounda taifa zima na kwa hiyo kufanya kuweko kwa utambulisho wa jumla katika mambo ya aibu na katika toba iliyofanyika kwa ajili ya dhambi ya kuabudu sanamu iliyoingizwa ama kuletwa kwao na wageni (kama inavyosema Ezra 9:2; Davies, Soncino).

Tunaona kwamba katika siku hii walosoma vifungu kadhaa kutoka katika Sheria na amri za Mungu kwa kipindi cha muda wa robo ya siku na kasha wakaziungama na kutubia dhambi zao mbele za Mungu kwa robo nyingine ya siku. Kwa hiyo, Soncino inasema kwamba walitumia takriban nusu ya muda huu kwa kusikiliza mahubiri na kipindi kingine cha nusu yake walifonya toba ya maungamo na maombi. Hii ilifuatia utaratibu wa kusoma mahalia ambapo Sheria zimeandikwa hadi kufikia katikati ya mchana na hatimaye walizifafanua kwa watu.

Agano la Kitaifa na Mungu ambalo lilifanywa siku ya Ishirini na nne ya mwezi wa Tishri limeanzia kutoka kwenye kitabu cha Mwanzo na linaweza kufananishwa na vifungu vya maandiko haya yafuatayo: Isaiya 43:16; 44:6; Zaburi. 83:19; 1Waf 22:19; Zab. 78:14; 103:21; Kut 3:7; 13:21; 14:15 na pia; 15:10; 18:11; 19:20; Hes. 14:14.

Soncino inashikilia kuamini kwamba kifungu kilichoko kwenye sura ya 9:14 kinahusisha na Sabato Takatifu inafananishwa na mafundisho ya Marabi yasemayo kwamba Sabato huzipima amri zote zilizoandikwa kwenye amri ya torati au Torah (p. Ned. 38b). Hili ni badiliko la haraka ikilinganisha na neno lililonenwa na nabii Isaya ambapo Amri Kuu mbili za Sheria na amri za Mungu zinapitakima chake sawa sawa na jinsi alivyokaririwa pia mwalimu wa sheria aitwaye Gamalieli.

Mtu anaweza wanafahamu kutokana na mtazamo huu kwamba kama sheria hii ya maadhimisho ya mwaka wa Sabato na Usomaji wa Sheria na amri za Mungu kama inavyotakiwa na amri ya haraka ya Mungu iliyotolewa na Musa kupitia Yesu Kristo, basi iwapo kama ingetunzwa basi kusingeweza kuwa na hali ya kuto kueleweka au mchanganyo. Usomaji wa Sheria za Mungu unaondoa uingizaji wa mapokeo na kuwezesha marejesho ya Yubile na Sabato ya mapumziko ya ardhi. Usomaji wa Sheria za Mungu unaonyesha kuyatii mapenzi ya Mungu na kunawapa uweza watu wetu na kuwapa maono ya mpango wa wokovu.

Ni muhimu kujua pia kwamba Sabato ya mwaka wa Arobaini na tisa ya Yubile hii ilionekana kabisa kwamba ilikuwa na mahusiano kwenye juma la saba la miaka sawa sawa na miaka arobaini na tisa iliyonenwa kwenye unabii wa Danieli Danieli 9:25 kama ifuatavyo:

Daniel 9:25-27 Basi ujue na kufahamu ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili, utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. 26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwako; ukiwa umekwisha kukusudiwa. 27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo atakomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuaribu.

Kwa hiyo, marejesho haya yaliyofanyika chini ya Ezra na Nehemia yalitabiriwa kutoka kwa Mungu kupitia nabii Danieli kama ni sehemu ya kile kilichojulikana kama Juma la Saba la Miaka. Pia yalifungamanishwa na mfumo wa Yubile. Siku za mwisho za kufanyika kwa toba ya Wayahudi katika kipindi cha Hekalu kilikuwa basi ni hiki cha mwaka wa Sabato wa 69/70 BK. Lakini hawakuutubia ukengeufu wao na mapokeo yao mabaya na kwa hiyo ilipofika 1 Nisan 70 BK vikosi vya majeshi Kirumi vikiongozwa na Jemadari Tito viliuzingira mji wa Yerusalemu na kuuhusuru. Kila kitu kilifanyika katika mfumo wa Yubile kuu. Kipindi cha mwisho cha miaka saba kilishuhudia kwa watu wa Yudea kwenya utumwani. Miaka saba ya mwisho ya Yubile ya Arobaini na tisa tokea mwanzo wa majuma saba ya miaka yaliyotabiriwa na nabii Danieli na kupelekea marejrsho ya Ezra na Nehemia tutajionea ama kushuhudia kurudi kwa Masihi na kufanya maangamizo kwa wale wote waliofanya maovu.

Mwaka wa Sabato wa mwaka wa Ishirini na moja wa Yubile ya Arobaini tangu kuzaliwa kwa Masihi inayoonekana kwenye andiko hili inaangukia kwenye kama ilikuwa mwaka 1998. Usomaji wa Sheria na amri za Mungu na marejesho ya watu kuufahamu mfumo wa Yubile na calenda takatifu kuliwezeshwa kutokana na shughuli za Siku za Mwisho.

Mwaka wa Sabato wa 1998 ni wa muhimu katika mafuatano ya utaratibu huu kwa kuwa inafuatia mpaka wa kimwelekeo kwenye mafuatano ya mambo yubile ya muhimu na Milenia. Mwaka wa 1996 ulikjuwa ni wa maadhimisho ya 3000 au yubile ya sitini ya tendo la mfalme Daudi la kuingia mjini Yerusalemu. Yalikuwa ni maadhimisho ya 2000 au ni yubile ya arobaini ya kuzaliwa kwa Masihi. Mwaka 1997 unaweka mwisho wa Zama au Kipindi cha Utimilifu wa Mataifa uliohesabiwa kuanzia nyakati saba au miaka 2520 kuanzia kushambiliwa kwa Misri na Wakaldayo yaani Wababelonia chini ya Cambyses mwaka 525 KK ikifuatiwa na kipindi cha miaka mia mbili na arobaini tangia ushindi wa mfalme Nebukadneza alivyowashinda huko Carchemish mwaka 605 KK.

Kipindi kingine cha tatu cha Sabato cha kufikia mwaka 2019 tutajionea maanguko ya mwisho ya mfumo wa ulimwengu kukitangulia ujio wa Masihi. Mwaka wa 2027 ni Yubile ya Arobaini ya kuanzia mwanzo wa huduma ya Masihi. Mwaka 2028 utakuwa ni mwaka wa kwanza wa kipindi kinachitwa kama Yubile ya Yubile, Yubile ya Hamsini tangia amri ya ujenzi wa hekalu na marejesho ya kina Ezra na Nehemia kufanyika. Katika Yubile ile, Mesihi ataanzisha mfumo wa milenia na utawala mpya wa sayari hii ya dunia utakaoongozwa na Sheria na amri za Mungu.

Mpango wa Mungu unafanyika kwa hekima kubwa yenye haiba na utaratibu ukifuatana na Sheria zake na mfumo au utaratibu wa kalenda yake. Na asifiwe Bwana Mungu wa Majeshi ambaye ametupa mwanga na ufunguo wa kurejesha mfumo wake kwa kufuata neno lake.

 

Nyongeza kwenye Usomaji wa Sheria kama Ulivyofanywa na Ezra na Nehemia:

 

Dodoso zinazotupa kipindi cha Yehoyakin kwenda utumwani

Ili kujua kipindi ambacho utumwa ulifanyika kunaendana sambamba na kuujua mwezi wa mwisho wa mwaka ule yaani mwezi wa Adar na pengine unaitwa WeAdar au Adar II kwenye mwaka mkubwa au mrefu. Hii ina maana kuu sana katika kupanga hizi yubile mnamo miaka ya 27/28 na 77/78 au kwenye miaka ya 28/29 na 78/79 ya karne za zama tulizonazo hivi leo. Mwezi wa Adar unaumuhimu wake fulani katika utaratibu wa kuhesabu wa siku za kale ili kufanikisha kufanya mwaka ukamilike kwa nia ya kufanyia hesabu zake. Umuhimu huu unaonekana ukisisitizwa katika ufanyaji maamuzi ya kuupata mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake mfalme Tiberio kama ilivyonukuliwa kwenye Injili ya Luka katika kuanza kwa huduma ya Yohana Mbatizaji (soma jarida lisemalo Jinsi ya Kupata kipindi cha Kusulibiwa na Kufufuka kwa Yesu (Na. 159).

 

Maamuzi ya upatikanaji wa mwezi wa Adar na (We)Adar mnamo mwaka 597 KK yanaamuliwa na mwelekeo wa miandamo ya mwezi. Wayudea (Judaica) waliuwekea ukumbusho wa kuingia kwao utumwani kwamba kulifanyika mwezi wa Adar II sambamba na tarehe 15/16 Machi ya mwaka 597 KK.

 

Kwa mujibu wa kitabu cha maarifa kiitwacho Encyclopaedia Judaica, Volume 6, article Ezekiel, page 1082, footnote 1 inasema hivi:

 

Jinsi ya kuhesabu mwaka kwenye tarehe inaanzia kuanzia kwenda kwake kwenye uhamisho wa utumwani mfalme Yehoyakin kama yasemavyo maandiko haya, (1:2; 33:21; 40:1), kwa jinsi vile iliyofanyiwa hesabu na Wakaldayo huko Babeli kwa kutuatana na hesabu za Mambo ya Nyakati zao hadi kufikia Adar 2 (katikati ya mwezi Machi) mwaka 597. Hata hivyo, II Nyakati. 36:10 inasimulia kwamba utumwa ulianzia kwenye kipindi cha "kupindikia kwa mwaka" – kama vile, mwezi unaofuatia, wa Nisan, wa mwanzo wa mwaka wa 8 wa kutawala kwake mfalme Nebukadneza, kama isemavyo  (II Kings 24:12). Kwa hiyo, kipindi cha utumwa huu kilianzia mwezi wa Nisan (Aprili) 597, na mwaka wake, kama mwaka mfupi wa Wababelonia unavyoonyesha, ulioanzia tangia mwezi wa Nisan hadi Adar.

 

Hiii ni sahihi. Wayahudi wanautaja mwezi huu wa Adar 1 kama Adar na huu wa Adar 2 kama na Adar au ule wa WeAdar. Wao hawatumii kuiita miezi hii kama sisi tunavyoiita leo yaani Adar 1 na 2. Wao hutumia kwa kuiita tu kwa majina ya Adar na Adar.

 

Kumbukumbu iliyoko katika kubadilika kwa miaka kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha 2Mambo na Nyakati 36:10 inapelekea kwenye kipindi kile ambacho usiku na mchana huwa na urefu unaolingana cha mwezi wa Machi. Haielekei kuutaja mwezi wa Nisan. Rejea za Biblia kwa ajili ya mgeuko wa mwaka kuingia mwingine kwa idi ya Vibanda pia unamaanisha kipindi cha usiku na mchana kuwa sawa cha mwezi wa Septemba. Kipindi cha usiku na mchana kuwa sawa cha kichanga kinaangukia kwenye mwezi wa WeAdar mara saba katika kila mzunguko wa mwaka wa kumi na tisa. Kwa hiyo, hakuna mgongano wa aina yeyote ile kati ya kumbukumbu za Mambo ya Nyakati ya Wababelonia na vile kinavyoonyesha kitabu cha Kiyahudi cha 2Mambo ya Nyakati kwa ajili ya habari hii ya tarehe za kutiwa utumwani.

 

Kumbukumbu za nabii Ezekieli zinaelezea kuhusiana na mwaka wa kumi na tatu. Kumbukumbu kama hizi hazihusiani na mwaka wowote wa kumi na tatu unaojulikana kama wa mfalme awayeyote au wakimfumo au utaratibu. Maelezo rahisi yamechukuliwa kama yanavyojulikana kwenye maandiko matakatifu ya Agano la Kale.

 

Pia kuna marejesho mengine yaliyofanywa na Whiston ambayo hayako sahihi, yanayotuama kwenye utaratibu mbaya wa miaka ya kiutawala. Baadhi ya michanganyo inatokana na hii kwa wakati mwingine.

 

Katika kuamua Miandamo ya Mwezi Mpya katika mwaka 597 kunatuonyesha kwamba kulikuwepo na mwezi huu wa mwisho wa mwaka mrefu wa WeAdar katika mwaka huu.

Mwandamo wa Mwezi Mpya ulioangukia katika tarehe 12 Machi majira ya saa 9:00 alasiri huko mjini Yerusalemu kwa majira ya saa za huko (yaani LMT). Mwandamo wa Mwezi uliofuatia uliangukia siku ya tarehe 11 Aprili saa 1:33 asubuhi. Kipindi hiki cha usiku na mchana kuwa na urefu sawa kiliangukia tarehe 27 Machi saa 7:33 mchana kwa kufuata majira ya saa za Yerusalemu (LMT).

 

Ni zaidi ya siku 14 kamili tangia tarehe 12 Machi 597 hadi tarehe 27 Machi 597 alasiri hadi alasiri inayofuatia ambapo tunapata siku kumi na sita. Kwa hiyo basi, mwezi wa Machi hauwezi kuwa ni Mwandamo wa Mwezi ukikaribia kwenye siku ile ambayo usiku na mchana unakuwa na urefu sawa na tarehe 11 Aprili saa 1:33 asubuhi katika Mwandamo wa Mwezi wa Nisan. Kwa hiyo basi tunakuwa na mwezi huu wa WeAdar na ile wa 2 wa WeAdar kwenye tarehe za 14/15 Machi, kiasi cha kukisia kwamba tarehe 13 Machi kama ulikuwa ni mwanzo wa mwezi na sio tarehe hizi za 15/16 Machi kama Wayudea (Judaica) wanavyoshikilia kuamini.

 

Kwa hiyo basi utumwa unakuwa umetokea katika mwaka unaofuatia, tabriban kama kwenye kipindi hiki ambacho urefu.wa usiku na mchana unakuwa sawa, ambacho kilikuwa ni kwenye mwezi wa WeAdar na katika WeAdar 2 au tarehe za 14/15 Machi au tarehe 15/16 Machi kama Wayahudi walivyoichukulia.

 

Kwa hiyo mwaka ulihesabiwa kuanzia mwanzo uliopita katika mwezi wa Aprili 598 KK.

 

Mnamo Aprili 597 KK kwa hiyo ni mwanzo wa mwaka wa pili. Mwaka 596 KK ni mwanzo wa mwaka wa tatu. Mwaka 595 KK ni mwanzo wa mwaka wa nne na mwaka 594 KK ni mwanzo wa mwaka wa tano wa kuweko kwake utumwani mfalme Yehoyakii.

 


 

 

Jedwali la utawala wa mfalme Ahauswero II na matendo ya kina Ezra na Nehemia

 

 

 

 

Mwaka 423 KK

Chini ya Dario II. Tangazo linatangazwa la kuanza ujenzi upya mnamo mwaka 422 KK (Ezra 6:1 na 4:24) (huenda ulikuwa mwaka wake wa pili). Kipindi cha majuma 70 ya miaka kinaanza. Kutika Ezra 5 inaonekana kwamba Hagai na Zekaria wanatabiri mnamo kwenye miaka ya 423 KK na 422 KK. Kipindi cha majuma 70 ya miaka kinaanza kuanzia mwaka 423/22 KK (huenda ikawa ni mwaka wa kwanza wa kipindi cha Yubile mpya). Ujenzi ulikamilika katika mwaka wa sita wa Dario Mwajemi (Ezra 6:15) katika siku ya 3 ya mwezi wa Adar kama mwezi Machi mwaka 418 KK. Dario alifariki dunia kabla ya kipindi kilichoishia mwaka 405 hadi majira ya baridi ya mwaka 404.

Mwaka 404 KK

Artashasta II (Arsakes) anakabiliana na Wamisri wanaopinga na kuasi kurithi kwake ufalme. (majira ya baridi au mwezi wa Nisani mwaka 404.

Mwak 402 KK

Artashata anapoteza umiliki wake kwa Misri.

Mwaka 401 KK

Vita ya kidunia inapiganwa huko Uajemi. Wayunani wanapigwa kwenye mapigano ya Kunansa na wanafanya mapumziko kwenye pwani ya Bahari Nyeusi.

Mwaka 398 KK

Tangazo la kutolewa linatangazwa kwa ajili ya kurejea kwa Ezra na wenzake katika mwaka wa saba, huenda ilifanyika hivyo kwa maana ya kuwatunuku Wayahudi kwa ajili ya utii waliokuwa wameuonyesha (Ezra 7:1-26).

Mwak 387 KK

Artashata anawashinda Waspartani na kukomesha uvamizi wao. Amani ya mfalme inaonekana Waajemi wakiikalia tena Ionia.

Mwaka 385 KK

Nehemia anafanywa kuwa Liwali wa Yudea kuanzia mwezi wa Nisani wa mwaka wa 385-372 KK wakati mji na kuta zikiwa zimeisha jengwa upya tena (Neh. 5:14). Eliashib akiwa ni Kuhani Mkuu (Neh. 3:1). Hii ilikuwa ni barua ya pili ya tangazo la amri la Artashasta. Hii ilikuwa ni kwaajili ya majenzi mapya ya malango ya ngome za Hekalu na kwa kuta za mji (Hekalu lilikuwa limeshajengwa upya tayari - Neh. 6:10-11). Mji ulionekana kuwa ulikuwa umeharibiwa kwa ajili ya mapigano ya ile vita vya kidunia ambayo kwayo, Wababelonia na Wayahudi wa Kiisraeli walimsaidia mfalme kwa wazi wazi na moyo wa dhati. Huu ulikuwa ni mwaka wa Majenzi na Matengenezo ya kidini yakisimamiwa na Ezra na Nehemia. Ilianza kwa tangazo lililotolewa mwezi wa Nisani. Kuta zilikamilika na kwisha katika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa sita katika muda muafaka wa kuanza mkakati wa marejesho na Usomaji wa Sheria za Mungu katika mwaka wa ishirini wa Artashasta II ambao ulikuwa ni mwaka wa thelathini na tisa wa yubile ya tisa kabla ya kuanza kwa huduma ya Masihi.

Mwak 375/4 KK

Hiii inatimiliza unabii uliotolewa katika Danieli 9:25 kuhusu Mtiwa Mafuta wa majuma 7 za miaka ambazo jumla yake ni miaka 49 kuanzia mwaka 423/2 KK - 375/4 KK. Huu pia ulikuwa ni mwaka wa 49 wa Yubile. Jinsi ya kuhesabu ni kuanzia mwezi wa Nisani hadi Nisani.

Mwak 374/3 KK

Nisani ya mwaka wa Yubile wa 374 KK unaanza mwaka wa 32 wa Artashasta II. Haieleweka vizurio na rasmi kama urejeshaji wa ardhi uliofanywa na Nehemia ulikuwa ni kwa ajili ya marejesho ya mwaka wa Yubile. Ulikuwa ni mwaka Yubile na inaonekana kabisa kwamba hili lilikuwa ni jambo fulani lisilowazi, kwa hiyo, ilikuwa ni adhmisho la mwisho la kitu kinachojulikana kama Yubile.

Mwak 374/3 KK

Mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta Nehemia anarudi Yerusalemu kutoka Babeli na analikuta Hekalu kwenye halipo katika hali ya utaratibu mzuri likiwa chini ya uangalizi wa Eliashib na Tobia (Neh. 13:6). Nehemia akalitengeneza tena Hekalu na kuwapa stahili zao Walawi na waimbaji waliorejea na kufanya kazi za Hekaluni (Neh. 13:10-11). Alirejesha teba utaratibu wa utoaji zaka na kuzitakasa Sabato za BWANA (Neh. 13:12-19).

Mwak 321 KK

Ezra anafariki dunia kwa mwaka huo huo pia mfalme Iskanda Mkuu anafariki pia (Seder Olam Rabbah 30)

 

 

 

q