Makanisa Ya Kikristo ya Mungu

[062z]

 

 

Hitimisho:

Majukumu ya Mwanamke Mkristo

(Toleo 1.0 20021015-20021015)

 

Jarida hili linaangalia majukumu ya wanawake kulingana na Mpango wa Mungu siri ambayo wanawake wamepekabidhiwa kama waumini wa daraja la pili. Kuna Mungu mmoja tu, Kweli moja, Imani moja, Mwili mmoja, Kanisa moja lakini kuna waumini wengi (wanaume kwa wanawake).

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

 

(Copyright ă  2002, Diane Flanagan, ed. Wade Cox)

 

(Summary ed. by Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org and http://www.ccg.org

 

 


Majukumu ya Mwanamke Mkristo

 


Mwanamke anayetaka kujua majukumu yake katika jamii anatakiwa pia kuangalia chanzo maarifa yote yaliyofunuliwa yaliyotolewa na Mungu baba kupitia neon lake. fikra za mwanadamu hazifai kitu na ni ubatili.

 

Mungu anao mpango ambao ni kumpatanisha mwanadamu na kumrudisha kwake mwenyewe, na ametangaza sheria, zenye kufaa kutawala kwa mambo ya kiroho nay a kimwili, katika uzuri na utaratibu (1Kor. 14:40).

 

Ndoa ikiwekwa na Mungu wa Pekee wa Kweli wakati alipowaumba Adamu na Hawa (Mwa. 2:18, 23-24; Marko 10:6-9). Kwa sababu ya dhambi, Adamu na Hawa walifukuzwa kutoka bustanini wakaenda nje duniani ambako waliishi kulingana na Sheria za Mungu (Mwa. 3:23-24)

 

Kwa kupitia uzoefu wa ndoa hizi zetu za kimwili tunajifunza mambo mbalimbali  na kujifunza ni kwa namna gani ndoa yetu na Masihi itakavyo kuwa (Efe. 5:22-33).

 

Mwanamke anafungwa na mumewake kwa wakati ule awapo hai mzima, isipokuwa kwa ajili ya uasherati (au uzinzi) au manyanyaso au kushadhalishwa (Mt. 5:31-32; Marko 10:2-12).

 

Matendo ya uasherati yamekatazwa waziwazi kabisa (1Kor. 6:16-18) na inamaana zote mbili yaani ni uasherati wa kimwili na kiroho katika maisha yote ya mtu. Uasherati wa kiroho ni tendo la kujiunga katika ibada za makanisa ya uongo (yaani ni ukahaba) na kuacha

 

kujiunga katika mwili wa Kristo ambao ni kanisa lake. Hivyo basi hebu na kila mmoja na mke wake mwenyewe vilevile pia wanawake hebu basi wawe na waime zao wenyewe (1Kor. 7:2). Inapotokea mmoja wapo akafa, talaka, nk, hivi ni vitu vya dharura na kuna namna yake ya kimazingira ya jinsi ya kushughulikia.

 

Ndoa inahitaji uaminifu kati ya wahusika wenyewe, ni jukumu la kila mmoja kwa mwenzake (Efe. 5:22-33; Kol. 3:19; Mit. 5:18-19). Ikiwa mume wake akifa, basi huyu mwanamke yuko huru hafungiki na agano lile la ndoa aliloweka kwa mume wake na anakuwa huru kuolewa tena (Rum. 7:1-3).

 

Talaka inaruhusiwa kwa mujibu wa sheria lakini Mungu anachukia kuachana (Mal. 2:16). Eneo linaloelezea suala hili ni katika Kumbukumbu la Torati 24:2-5, na Mathayo 19:7-8.

 

Maandiko matakatifu pia yanafundisha kuhusu migawanyo ya majukumu katika familia (Mwa.3:16; Kol. 3:18; 1Pet. 3:12; 1Tim. 2:11-14; Efe.5:24). Lakini pamoja na hayo, kila mmoja anapaswa kumtii Mungu kwanza (Kum. 10:12-13).

 

Kuhusu ndoa zile zilizofungwa kabla wahusika hawajaamini, yapo maelekezo kwa ajili ya mwezi aaminiye anavyoweza kuwafanya watu wa nyumbani mwake hasa mwenzi wake na watoto waweze kuamini (1Kor. 7:12-16).

 

Mungu hutakasa na kuzitenga familia mbali na uovu, kwa kupitia yule anaye amini kwa jinsi atakavyo onekana akiwa mtii kwa mzazi wake aliyepo mmoja au kama wakiwepo wote wawili (1Kor. 7:14).

 

Maandiko matakatifu yanatuagiza waziwazi kuwa tusifungiwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isiyo sawasawa (1Kor. 6:14). Kwahiyo jambo hili linatakiwa litiliwe maanani sana wakati mtu anapochagua mchumba wa kumuoa.

 

Pia tumeamriwa kuoana na kuzaa watoto tutakaowalea kulingana na maadili na utukufu kwa Mungu (Mwa. 1:28, 2:24, 9:1; 1Tim. 5:14). Watoto ni baraka kutoka kwa Mungu, ambaye ameamuru (Zab. 127:3-5).

 

Ni wajibu wa wazazi kuwalea watoto na kuwafundisha kumcha Mungu, kama wazazi wanavyofanya (Kum. 4:9, 11:19; Mit. 1:8, 22:6; Flp. 6:4). Tunatakiwa tuwafundishe sheria za Mungu kila siku; watoto wanajisikia kujiamini sana wawapo katika familia yenye wazazi wenye bidii wanaoongozwa na mapenzi ya Roho Mtakatifu.

 

1Timotheo 2:11-15 inasema: “mwanamke ataokolewa kwa uzazi wake mwentwe,” hii haimaanishi kuwa wanamke wale tu wenye watoto ndio wanaokolewa. Uokovu unaoongelewa hapa unamaana ya “kulindwa.” Neno hilo kwa mujibu wa kamusi iitwayo SGD 4982-kuokoa-na lina maana nyingi sana yanayohusiana na wokovu.

 

Kutoa mimba kunaruhusiwa kwa mujibu wa Sheria za Mungu ni kwa mahali pale tu inapoonekana kuwa maisha ya huyu mama mzazi yako hatarini (Kut. 21:15), ikifanyika kwa sababu nyingine mbali yah ii ni dhambi na ni kuvunja amri ya sita ya amungu.

 

Katika Mithali 31 hapa tunaonyeshwa na matendo na stahili impasayo mwanamke wa Kikristo kuwanayo katika kumhudumia mume wake, watoto, utunzaji na matumizi ya fedha, ukarimu na huruma katika kuwasaidia wenye uhitaji. Vilevile kuna baadhi ya mabo yahusuyo jinsi ya kuenenda ambayo inabidi ajiepushe nayo, kama vile kuzoelea kufanya makosa, usengenyaji,ibada za sanamu au kupenda vinyago, udanyanyifu, kiburi au majivuno, ubinafsi, nk.

 

Muonekano wa mwanamke katika uvaaji wake na mwenendo wake kwa ujumla lazima utoe ujumbe wa mwanamke anaye mcha na kumuishioa Mungu (1Tim. 2:9-10; 1Kor. 11:5-15; Kum. 22:5). Kumbuka kuwa miili yetu ni mitakatifu kwa kuwa Roho Mtakatifu anakaa ndani yake, kwa hiyo tunatakiwa kuitunza, kwa kuifanya iwe misafi na yenye afya.

 

Maandiko matakatifu yamesema kuwa wanawake ni viumbe dhaifu (1Pet. 3:7). Lakini pia ikumbukwe kuwa wote wawili yaani wanawake na wanaume ni “warithi kwa pamoja wa neema ya uzima.”

 

Katika maisha ya ndoa, kutatokea wakati ambapo mahusiano ya tendo la ndoa itabidi yasifanyike yaani yapumzishwe kwaajili ya kuupisha muda wa maombi ya kawaida au ya kufunga (1Kor. 7:1-9). Wakati mwingine umeelezewa katika Mambo ya Walawi 15:24-33.

 

Mwanamke katika Kanisa anatakiwa awe na uwezo wa kujibu maswali yahusuyo imani ambayo yeye ameamua kuifuata (1Pet. 3:15) na anatakiwa aweze kushikilia kikamilifu upanga war oho na ngao ya imani ili kuitetea kweli kama ilivyo kwa mwanaume yeyote yule (Efe. 6:13-17). Wanawake wanatakiwa wanie mamoja katika nyumba ya Mungu (1Tim. 3:14-16). Wanaume na wanawake wote wameumbwa kwa mfano wa sura ya Mungu kwa hiyo wana nafasi sawa katika mipango ya Mungu.

 

Bidii za pamoja za wanaume na wanawake Kanisani leo hufanya kazi kubwa katika kumpatia Mungu utukufu, na yasiwepo mashindano kati ya wanaume na wanawake kanisani au majumbani. Mambo yote yafanyike kwa nia iliyo njema (1Pet. 3:8-9). Hebu na tuhudumiane wenyew kwa wenyewe na kwa kanisa kwa ujumla (Lk. 22:27).

 

Wanaume wameamriwa kuhudhuria kwenye Sikukuu za Mungu mara 3 kwa kila mwaka (Kut. 34:22-23, 23:14-17; Kum.16:16).

 

Wanawake wanaweza kubakia nyumbani wanapokuwa na dharura kama vile za uja-uzito, kulea watoto wachanga, kuhudumia wazee wasiojiweza au wagonjwa nk. Hatahivyo ilipaswa wote waende ili kwenda kujifunza mafundisho (Yos. 8:35).

 

Neno la Mungu linatoa sheria na kanuni kuhusu ni kwa jinsi gani wanaume na wanawake wafanye Kanisani na mwenendo wa maisha yao katika ujumla wake (1Tim. 2:8-15).

 

Hairuhusiwi kwa wanawake kuongoza ibada siku za Sabato katika hali ya michanganyo yaani kati ya wanawake na wanaume (Mdo. 18:26). Wanawake kanisani wanaweza kufanya maombi na kufunga ili kuwaombea wagonjwa na walioachwa ukiwa kama vile wajane na yatima, kuonyesha huruma kwao yaani kuwahurumia, kutembelea wagonjwa na kuwapelekea chakula, na kuandika barua za kuwatia moyo wengine. Vilevile wanawake wanaweza kuandaa masomo ya kuwafundisha watoto, kuelezea na kufundisha neon la Mungu. Wanawake wanaweza kusimikwa kama Mashemasi, pale inapoonekana kuna ulazima. Hakuna sheria inayokataza wanawake kujishughulisha na mambo yaliyoko majumbani mwao.

 

Wanawake wanayo majukumu kama yalivyoelezewa katika maandiko matakatifu. Wokovu wake upo katika kazi zake (Flp. 2:12). Ni Kristo tu aliye mwombezi kati ya Mungu na wanadamu. Hakuna kuhani, mtumishi, askofu wala papa anayeweza kuifanya kazi ile.kwa hiyo wajibu wa wanawake katika kuushindania wokovu ni sawa kwa kiwango kilekile walichonacho wanaume.

 

Kwa maana hiyo twaweza kusema kuwa kwa kupitia damu ya Kristo iokoayo, wote tumefanyika kuwa ni watoto wa Mungu na warithi pamoja na Kristo (Rum. 8:17; Gal. 3:26-29; Lk. 20:35-36) inaonyesha hali itakavyokuwa katika ufufo.

 

Wokovu kwa pande zote yaani kwa wanaume na wanawake ni mpango unaoendelea. Wanatakiwa wote watembee katika mapito yaleyale ya imani kwa Mungu Mmoja, aliye Wapekee na Wakweli na Mwanae wa pekee Yesu Kristo Aliyemtuma. Wote wanatakiwa kutubu dhambi zao na kubatizwa, na kupokea kipawa cha RohoMtakatifu, ambaye hutusaidia wote kukua katika neema na maarifa.

 

Hebu na tufanyike kama mwanamke aliyetajwa katika Mithali 31:29…mwanamke anayemcha na kumuishia BWANA.

 

q