Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[119]
Ukoo wa Uzao wa Masihi
(Toleo La 2.0 19950604-20050509)
Maana ya
mstari wa ukoo wa Masihi imefafanuliwa kutoka Adamu. Maandiko yaliyo kwenye
Mathayo 1 na Luka 3 yanaelekezewa na kufafanuliwa na mkanganyiko wake uliopo
kati yao na kwenye kitabu cha Nyakati kumefafanuliwa pia. Maana halisi na
sahihi yanaonyesha kwamba kwa kweli Masihi alitumwa ili kuwaokoa wenye dhambi.
Christian Churches of God
Email: secretary@ccg.org
(Hatimiliki ©
1995, 1998, 2005 Wade Cox)
(tr. 2016)
Masomo
haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo
la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna
malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo
pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha
lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia
yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Ukoo wa Masihi ni
kitu muhimu sana ili kuelewa Masihi alikuwa ni yupi. La muhimu zaidi ni kwamba
uzao wake huo unaleta maana ya muhimu sana ya utimilifu wa unabii na pia ya
sheria ya kibiblia. Kufutwa yake kwenye tafsiri ijulikanayo kama the Reader’s
Digest Bible ni makosa makubwa sana nay a bahati mbaya sana.
Kuna idadi kadhaa
ya kanuni za mstari wa kiuzao zinazotakiwa kueleweka pia kutokana mpangilio wa
nje. Ya kwanza ni ile ambayo kwamba ni wanawake tu ndio wanaopitiwa kwao. Hii
inatokana na sheria na tendo la kwamba mwanamke anakuwa amechukuliwa na kuingizwa
kwenye kabila la mume wake anapoolewa. Kulikwa na idadi kadhaa ya sheria,
zilizokataza matendo ya kuoana watu wa jamii moja. Makatazo ya kitendo hiki cha
kuoleana ndani ya ukoo mmoja yalikuwepo kwa sababu za maana sana. Kutokana na
Hesabu 36 tunaona kwamba ardhi ilitolewa kwa ajili ya urithi kwa kuipigia kura
wakipewa wana wa Israeli. Urithi uligawiwa kwa kigezo cha wazawa wa ukoo
husika. Hakuna mwanamke aliyepewa urithi wa makabila ya Israeli angaliyeweza
kuolewa nje ya kabila lake (Hesabu 36:8). Bali alikuwa ni budi aolewe kwenye
familia ya ya kabila la baba yake. Urithi wake usingeweza kuondolewa kutoka
kabila moja hadi jingine. Kila kabila liliwajibika kuuzingatia urithi wao
(Hesabu 36:9). Kwa kuutangaza mwaka wa Yubile ndipo urithi uliorithiwa ulitolewa
na kupewa kabila ambalo mwanamke huyu ameolewa kwalo (Hesabu 36:4). Sheria za
mwaka wa Yubile zilitendeka kwa mujibu sawa na zilivyoagizwa kwenye Mambo ya
Walawi 25. Kwa hiyo basi mstari wa uzawa ulikuwa ni wa muhimu ili kuelewa na
kurekebisha utaratibu wa kiuchumi chini ya torati. Utaratibu huu unadaiwa kuwa
kuanikizwa wakati wa utawala wa Masihi (soma kitabu cha nabii Ezekiel kuona
jinsi utakavyoendelea). Mungu anafuata mistari ya damu ya kiuzao na kuwalinda
hata kipindi cha utawaniko na hata kile cha kwenda kwao utumwani (Amosi 9:9).
Kanuni hizi za
urithi zinawahusu pia Walawi. Nyumba za miji ya Walawi zilikuwa ni mali yao
katika mwaka wa Yubile. Kwa huyo Walawi walihusishwa kwenye sheria hizi za
urithi kwa makundi yote mawili, yaani kwa makuhani na kwa miji na kwa mashamba
ya viungani mwa miji (Walawi 25:32-34). Maelekezo haya ya Walawi yanauhusuano na
unabii kuhusu Masihi, kama tutakavyokwenda kuona.
Mstari wa uzao wa
Masihi kwenye Agano Jipya unajiri na mistari miwili, kwenye Mathayo 1:1-7 na
Luka 3:23-38, na mistari miwili yote inatofautiana kabisa. Zaidi sana, ni
kwamba mstari ulio kwenye Mathayo unatofautiana na jinsi ilivyo kwenye kitabu cha
Mambo ya Nyakati. Kwa hiyo, kunahitajika maeelezo na ufafanuzi wa kina kwenye
mikanganyiko hii, au vinginevyo basi Biblia ichukuliwe kuwa haina nguvu yoyote
ya uvuvio. Ukristo wa sasa umeamua kupuuzia tatizo hili kiasi cha hata kwenda
kwenye uhafidhina tunaouona kwenye kitabu cha Reader’s Digest Bible. Ili kujua
kinachotokea ni kuyakubali matatizo mengine ambayo wengine wameamua kuyapuuzia.
Mathayo na Luka
wote wawili wanaanza na Adamu. Mstari ni mchakato wa kushusha chini umuhimu wa
unabii wa familia fulani kwa kipindi fulani. Uzao wa mwanamke alitokea kwa na
Adamu (Mwanzo 3:15). Uzao huyu wa mwanamke hapa ni mmoja wa kike (zer’a). (Maandiko
ya Mwanzo 17:7; 21:12; na Wagalatia 3:16 yanafanana. Uweza au nguvu za Shetani
zinaondolwewa na utawala wake utaangamizwa kutokana na Waebrania 2:14; 1Yohana
3:8).
Mwanzo 17:7 inaonyesha
kwamba Agano na kwamba yampasa Masihi aje kwa kupitia uzao wa Ibrahimu. Mwanzo 21:12
inauonyesha mstari wa Isaka ambao kwamba uzao wa Utaitwa. Hata hivyo, Ishimaeli
alikuwa pia ni wa uzao wa Ibrahimu na kwa hiyo kulianzishwa taifa. Hata hivyo,
ilikuwa ni kwa kupitia Isaka ndipo uzao huo uliitwa.
Mstari wa Masihi
unaelekezwa zaidi. Yohana 7:42
inaelezea idadi ya unabii kwenye andiko moja.
Yohana 7:42 Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka
katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi?
Maandiko
Matakatifu yanayojiri na maandiko haya yanakutkana kwenye Zaburi 110:1-7 ambapo
kuna Bwana wa Daudi na Kuhani Melikizedeki. Andiko hilo linamhusu Masihi kuhani.
Zaburi 132:6,11 inaonyesha
kwamba Daudi na Efraimu kwamba Mungu ataketi kwenye kiti cha enzi.
Zaburi 132:11 Bwana
amemwapia Daudi neno la kweli, Hatarudi nyuma akalihalifu, Baadhi ya wazao wa
mwili wako Nitawaweka katika kiti chako cha enzi.
Masihi atatokana
na nyumba ya Yese ana atakuwa ni wokovu wa Mataifa kutokana na Isaya 11:1,10.
Isaya 11:1 Basi
litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi
yake litazaa matunda.
Isaya 11:10 Na
itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za
watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia
patakuwa na utukufu.
Kwa hiyo, Masihi
ilimpasa awe ni wa uzao wa Yese, baba wa Daudi. Masihi anatokana na mstari wa uzao
wa Daudi kwa mujibu wa Yeremia 23:5-8.
Yeremia 23:5-8 Tazama
siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye
atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika
nchi. 6 Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli
atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu. 7 Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema Bwana, ambapo
hawatasema tena, Aishivyo Bwana, aliyewatoa wana wa Israeli katika nchi ya
Misri; 8 lakini, Aishivyo Bwana, aliyewapandisha na
kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi
zote nilikowafukuza; nao watakaa katika nchi yao wenyewe.
Andiko hili linakanganya
Ukristo wa kisasa kwa kuwa linaonyesha kwa dhahiri sana kwamba Masihi atatawala
hapa duniani na kwamba kutakuwa na tukio la pili la Kutoka litakalowaimarisha
Israeli na kuanzishwa kwa taifa lao.
Mika 5:2 inaonyesha
kwamba Masihi atazaliwa Bethlehemu.
Mika 5:2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
Kwa hiyo, uzao wa
mwanamke ni wa Adamu kupitia Ibrahimu, kupitia kwa Isaka, kupitia kwa Yuda,
kupitia kwa Daudi na ni kutoka Bethlehemu. Haya ni maelekezo ya kimapokeo ya mstari
huu. Mstari huu unaweza kuelezewa zaidi kuliko hivi.kuna mambo mawili kuhusu
ujio wa Masihi yanayoonyesha kwamba Masihi atakuwa na aina mbili za marejeo kwa
madhumuni mawili. Lengo la kwanza ni kwamba yeye ni kuhani Masihi kuanzisha
ukuhani wa mfano wa Melkizedeki, ili kufanya huduma ya kikuhani tsiotokana na
uzao, ili kwamba iweze kufunguliwa kwa Wamataifa kama zawadi au kipawa toka kwa
Mungu.
Watakatifu
wamesamehewa na kufutiwa makosa yao na Kristo na kufanyika kuwa wafalme na
makuhani (Ufunuo 1:6; 5:9-10).
Ufunuo 5:9-10
Nao waimba wimbo
mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake;
kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na
lugha na jamaa na taifa, 10 ukawafanya kuwa ufalme na
makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
Ukuhani wa Haruni
kwa hiyo unapasa kufikia mwisho na pamoja nao hata kwenye Mahekalu yote mawili,
yaani lile la Yerusalemu na lile la Misri lililoko huko Heliopolis. Hekalu la
Leontopolis kwenye lakabu ya Heliopolis lilianzishwa na kujengwa na Onias IV kwa
kupitia unabii ulio kwenye Isaya 19:19. Lilijengwa kwenye ardhi ya Gosheni ili
kusaidia kutimilika kwa unabii wa Hosea uliotolewa kwa kuwalenga wote wawili,
yaani Israeli na Mesihi, uliosema, Nikamwita
mwanangu atoke Misri (Hosea
11:1; Mathayo 2:15). Hekalu lililokuwa huko Misri lilifanya kazi tangu mwaka 160
KK hadi mwaka 71 BK wakati lilipofungwa kwa amri iliyotolwa na Vespasian baada
ya kuangamia kwa Yerusalemu. Kwa hiyo kufungwa kwake kulihitimisha unabii wa
Yona, uliodumu tangu mwaka 30 BK - 70 BK, na kisha ukatimilika tangu siku ya 1 Abibu,
mwaka 70 BK hadi siku ya 1 Abibu, mwaka 71 BK (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Kuangamizwa
kwa Hekalu (Na. 13)). Mamlaka ya hekalu yaliondolewa baada ya miaka
arobaini kwisha ambayo iliruhusiwa kwa ajili ya kuwapa Yuda muda wa kutunu. Miaka
arobaini iliyofuatia kutoka miaka mitatu ya huduma ya Masihi kwa hesabu ya
kuufananisha mwaka mmoja sawa na siku dhidi ya ile huduma ya Yoha huko Ninawi.
Amri mpya ilikuwa
ni baada ya Melkisedeki (Zaburi 110:4). Kristo alikuwa Kuhani Mkuu wa utaratibu
ule. Wateule ni makuhani, wasiotokana na mstari wa uzao (Waebrnia 7:1-21). Makuhani
hawa wanakuwa pia ni wafalme waliopewa ufalme (Waebrania 12:28). Ni ushahidi
unaojitegemea kwamba Kuhani Mkuu anaweza pia kuwa hivyo kama kuna makuhani
wengine ambao anaoweza kuwatawala. Kwa kutafsiri au kumaanisha twaweza kusema
kwamba hao hawawezi kuwa ni wa Haruni, ingawaje wana wa Haruni nao watakuwa ni
sehemu ya ukuhani huu (Ufunuo 7:7). Dhana ya ukuhani ni pana zaidi kuliko taifa,
kama dhana ya Israeli ilivyopanuka na kujumuisha mataifa yote.
Mstari wa uzao wa
Masihi haukuujumuisha mstari wa Daudi tu bali pia na ule wa Haruni. Unabii
unaonyesha kwamba mistari hii ilikuwa ni ya Daudi kwa kupitia Nathan na Lawi
kupitia kwa Shimei. Unabii huu upo kwenye Zekaria 12:10-14 pia unaonyesha
kwamba Masihi alipaswa kuuawa.
Zekaria 12:10-14 Nami nitawamwagia watu wa nyumba
ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama
yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo
mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo
uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza. 11 Siku
hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya
Hadadrimoni katika bonde la Megido. 12 Nayo nchi
itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake
zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao; 13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao;
jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao. 14 Jamaa
zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao. (kumbuka kwamba tafsiri ya KJV inasomeka
kwamba mimi smbsye wamemchoma ikituama
kwenye nahau za kimagharibi, nahau za kimashariki neno sahihi ni kuwa yeye).
Andiko hili
linaonyesha mistari miwili ya uzao. Wa kwanza ni wa Daudi kupitia Nathani na wa
pili ni wa Lawi kupitia kwa Shimei. Kitendo hiki kilisababisha maangamizi na
maombolezo ya Yerusalemu kama taifa (aya za 11-14). Kwa hiyo unabii uliendana
na maangamizo ya Yerusalemu hadi kifo cha Masihi. Kipindi cha muda uliotolewa
wa miaka arobaini tangu mwaka 30 BK hadi mwaka 70 BK kwa hiyo kina maana yake
fulani. Yerusalemu ilizingirwa na majeshi ya Kirumi tangu siku ya 1 Nisan,
mwaka 70 BK. Hekalu la Yerusalemu liliangamizwa
mwaka wa 70 BK tangu siku ya Upatanisho, hata hivyo, hekalu la Misri liliamriwa
kufungwa mwaka uliofuatia wa 71 BK kwa amri ya Vespasian kukifuatiwa na vita ya
Wayahudi. Maangamizo yaliendelea nchi nzima baada ya kuangamizwa kwa hekalu.
Ni kina Mathayo na
Luka tu ndio wanaohusisha au kuuelezea mstari huu wa uzao wake. Marko na Yohaya
wanaanzia kwa kumuelezea Yesu akiwa ,kubwa, kwa hiyo mstari wao wa uzao hauwezi
kufanana
Kwenye jarida lake (la “The Genealogy of Messiah (Mstari wa Uzao wa Masihi)”,
The Vineyard (Shamba la Mizabibu),
November 1993, kurasa za 10-13, lililochapishwa tena kutoka kwenye lijulikanalo
kama Issues, A Messianic Jewish
Perspective), Dr. Arnold Fruchtenbaum wa Ariel Ministries anasema hivi:
Kwenye Mathayo,
Yusufu alifanya kazi nzuri na ya muhimu, lakini Mariamu (Maria) alifanya kazi hodari
kabisa. Mathayo anaandika habari kuhusu malaika walimtokea Mariamu, Mathayo
ameandika kuhusu mawazo aliyokuwanayo Yusufu lakini hakuna kilichpandikwa
kuhusu alichokuwa anawaza Mariamu. Kwa
upande mwingine, Injili ya Luka inaelezea habari hiyohiyo kwa mtazamo wa
Mariamu. Kwa mtazamo wa kila Injili, ingekuwa ni wazi na shahiri sana kwamba
maelezo ya Mathayo kuhusu mstari huu wa uzao ni kwamba wa Yusufu, na maelezo ya
Luka ni kwamba wa Mariamu.
Ndipo linapoibuka
swali la kwamba: ni kwa nini tunahitaji kuwa na mistari miwili ya uzao, hususan
kwa vile Y’shua (Yesu) hakuwa mwana hasa wa Yusufu? Jibu lijulikanalo sana na
la kawaida ni kwamba: Injili ya Mathayo inatoa mstari wa kifalme, wakati ile ya
Luka ikitoa mstari halisi na wa kweli. Kutokana na dhana hii ndipo dhana
nyingine inaibuka. Kwa kuwa Yusufu anaonekana kuwa ni mrithi mstahili wa kiti
cha enzi cha Daudi, na Yesu alikuwa ni mtoto wa kumlea tu na sio wa kumzaa mwenyewe
Yusufu, basi Yesu angeweza kudai haki kwenye kiti cha enzi cha Daudi.
Kwa upande mwingine
ni kwamba Injili ya Luka inatoa kipindi halisi, kuonyesha kwamba Y’shua mwenyewe
alikuwa ni wa uzao wa Daudi. Kwa kupitia Mariamu, alikuwa mshiriki kwenye nyumba
ya Daudi, lakini angeweza kudai haki ya kuketi kwenye kiti cha enzi cha Daudi
kwa kupitia Yusufu, anayestahili kabisa. Kwa
kweli kabisa, kinyume chake ndiyo ukweli (msisitizo umeongezewa).
Arnold
Fruchtenbaum anaibua mambo ya muhimu sana kwenye kitabu chake, hata hivyo,
hayashikilii na kuyachukulia kuwa ni mambo ya muhimu sana kwenye kuelewa kuhusu
Zakaria kama tunavyoona hapo juu. Kutokana na Zakaria tunaona mstari wa uzao wa
Daudi kwa kupitia Nathani ikitajwa. Hakuna kilichotajwa kuhusu Daudi kupitia
kwa Sulemani na kwa sababu njema sana.
Kama ilivoelezwa
na Fruchtenbaum, kulikuwa na masharti mawili ya uhusiano wa kidugu kwenye
Maandiko Matakatifu ya Kiebrania. Hawa waliasiliwa baada ya kugawanyika kwa
ufalme baada ya kufa kwa Sulemani.
Sharti la muhimu la kuchukua kiti cha enzi cha ufalme wa Yuda lilikuwa ni
kuwa mtu anayetoka kwenye ukoo wa Daudi. Masihi alipaswa kuketishwa kwenye kiti
cha enzi cha Daudi (Isaya 9:7). Mfalme alipaswa atokane tu na Nyumba ya Daudi.
Yeremia 33:20-21 inaonyesha kwamba agano na Daudi na uzao wake, na pia na
Walawi, halikuwezekena kuvunjika. Hila yoyote ya kutangua na kuondolea mbali
nyumba ya Daudi kama tunavyoona kwenye Isaya 7:5-6 ilitabiriwa kuwa itashindwa.
Isaya 7:5-6 Kwa kuwa
Shamu amekusudia mabaya juu yako, pamoja na Efraimu na mwana wa Remalia,
wakisema, 6 Haya, na tupande ili kupigana na Yuda na
kuwasumbua, tukabomoe mahali tupate kuingia, na kummilikisha mfalme ndani yake,
huyo mwana wa Tabeeli.
Kushindwa
kulikotabiriwa kulimaanisha kuulinda ufalme ili kwamba Maandiko yasitanguke.
Masihi atarudi ili kuuchukua ufalme huo sawasawa na ilivyoandikwa kwenye Danieli
2:35,44-45.
Kushindwa kwa
njama zozote zile kumeonekana kwenye Isaya 8:9-15 ambako kunasema kuwa ni Mungu
tu ndiye astahiliye kuogopwa na ndiye wa kumcha.
Isaya 8:9-15 Fanyeni
ghasia, enyi kabila za watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio,
ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande
vipande; Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande. 10 Fanyeni
shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana
Mungu yu pamoja nasi. 11 Maana Bwana aliniambia hivi,
kwa mkono hodari, akanifundisha nisiende katika njia ya watu hawa, akisema, 12 Msiseme, Ni fitina, katika habari za mambo yote ambayo
watu hawa watasema, Ni fitina; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope. 13 Bwana wa majeshi ndiye mtakayemtakasa; na awe yeye hofu
yenu, na awe yeye utisho wenu. 14 Naye atakuwa ni
mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba
za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu. 15 Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika,
na kunaswa na kukamatwa.
Yeyote
aliyejaribu kutawala kwenye kiti cha enzi cha Israeli bila kuruhusiwa na Mungu
alikumbwa na maafa makubwa. Wote waliojitwalia kiti cha enzi cha ufalme wa
Samaria pasipo kuruhusiwa na unabii waliuawa kwa ghafla (1Wafalme 11:26-39;
15:28-30; 16:1-4,11-15; 21:21-29; 2Wafalme 9:6-10; 10:29-31; 14:8-12).
Andiko linguine
la maana na muhimu sana na lakini lililokataliwa na kutotilliwa maanani
linalohusiana na watu wa nyumbani mwa Daudi kwa Masihi ni Zekaria 12:7-9 linalotanguliwa
na lile lililonukuliwa hapo juu lakini kwa kweli linawekwa kwenye mkururo ulio
nyuma ya harakati zilizotajwa kwenye Zekaria 12:10-14. Zekaria 12:10-14 inahusiana
na kuuawa kwa Masihi wakati alipokuja mara yake ya kwanza. Andiko lililoko hapo
juu lipo kwenye Zekaria 12:7-9 linahusiana na kurudi kwake na vita vya nyakati
za mwisho.
Zekaria 12:7-9 Naye Bwana ataziokoa hema za Yuda kwanza,
ili utukufu wa nyumba ya Daudi, na utukufu wa wenyeji wa Yerusalemu, usipate
kutukuzwa kuliko Yuda. 8 Katika siku hiyo
Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao
atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama
malaika wa Bwana mbele yao. 9 Hata itakuwa siku
hiyo, ya kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na
Yerusalemu.
Jambo la muhimu kwenye andiko hili ni kwamba:
1. Yuda ameongoka na kuokolewa kwenye kutangiliwa ili kwamba utukufu wa Nyuma ya Daudi na pia kwamba kwa Yerusalemu hautukuzwi kinyume na Yuda.
2. Yerusalemu utalindwa na Bwana. Yeye aliyedhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi; na Nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana [Yehova] mbele yao.
3. Katika siku hiyo mataifa yote ambayo yalikuwa kinyume na Yerusalemu yataangamia.
Vifungu hivi ni vya muhimu sana. Ili kuvielezea vifungu vya mwisho kwanza, ni wazi sana kwamba tunatatizwa na siku za mwisho na vita vya kinabii vya Bonde la Megido kwenye aya ya 11. Hivyo basi, tukio la mauti ya kwanza linatumiwa ili kuakinisha ushindi wa mwisho dhidi ya mataifa.
Mambo mawili ya kwanza yanaonyesha kwamba kuna tofauti iliyofanya tofauti kati ya Nyumba ya Daudi na kwamba ile ya Nyumba ya Yuda ambapo kiuzoefu majira mamoja ya machipuko hadi mengineyo. Hata hivyo hilo si kitu sana kwa watu wa Nyumbanimwake Daudi katika nyakati za mwisho kwa kuwa imeenea hadi kuwajumuisha Wamataifa chini ya watakatifu kama tulivyoona hapo juu ambapo Wamataifa wanazirithi baraka kwa kupitia Masihi.
Mkururo huu unaonyesha kiwango cha kimwili na cha kiroho. Kwanza kabisa, udhaifu wa Yerusalemu utatiwa nguvu na kuwa kama Daudi. La pili, wakazi wa nyumbani mwake kwenye kipindi hiki watakuwa kama Elohim au Mungu, kama Malaika wa Yehova (au Yahova) aliyekuwa mbele yao. Malaika wa Yehova alikuwa ni Malaika Mkuu wa Ushauri anayetajwa kwenye tafsiri ya LXX, kwenye Isaya 9:6, mungu wa pili wa Waisraeli ambaye ni Malaika wa Yehova (au Yahova) wa Zekaria 12:8. Malaika huyu alikuwa ni elohim na alikuwa ndiye uso wa Mungu, ni Penieli wa Mababa wa imani, ni El Betheli au Mungu wa Nyumba ya Mungu wa Ibrahimu. Malaika huyu alikuwa ni Mungu aliyemtia mafuta kama ni Mungu na Mungu wake kwa mafuta ya furaha juu ya ndugu zake kwa mujibu wa Zaburi 45:6-7 ambaye Waebrania 1:8-9 inatuonyesha kuwa inamtaja Masihi.
Hivyo watakatifu wanafanyika kuwa elohim, kama Kristo alivyo elohim, kama mtangulizi wa Malaika wa Yahovah wa Agano la Kale, na ni kama elohim kwa kufufuka kwake kutoka kwa wafu akiwa kama mwana wa Mungu mwenye mamlaka (Warumi 1:4; Waebrania 1:8-9).
Hii ni dhana yenye nguvu sana. Inaonysha pia ukubwa wa wito wa Mungu na mpango wa Mungu. Imekataliwa kwa kuwa haifanyi kwa mujibu wa mitizamo ya kihafidhina ya Mtaguso wa Kalkedoni uliofanyika takriban mwaka 451.
Kwa hiyo tupo kwene mahala muafaka kuhusianisha na Mathayo na Luka na Maandiko mengineyo kwenye mstakabala wake sahihi. Mstari wa uzao wa Masihi ulio kwenye Mathayo una idadi kadhaa ya mabo yanayotofautiana ambayo inaibua mikururo ya mafundisho ya biblia na kuonyesha kikamilifu kabisa sababu ya ni kwanini mstari ule yapasa uwe ule wa Yusufu. Y’shua au Yoshua asingeweza kuwa Masihi kwa kuhesabiwa tu hivyo na Mathayo peke yake. Hesabu iliyo kwenye Luka inahitaji kuonyesha ni kwa nini licha ya mstari wa Yusufu, angefanyika kuwa mfalme na jinsi Mungu alivyohusika kupatanisha kwa amri au shauri alilolianzisha kwenye mstari wa Daudi na ufalme kwa kupitia nabii Yeremia.
Masihi ametajwa
kwa maelekezo ya mbingu. Jina lake limetolewa kwenye Mathayo 1:21 na Luka 1:31.
Jina limechukuliwa au linatokana na jina la Hoshea
(kama ilivyo kwenye Hesabu 13:16) ambalo kiambishi chake cha Yah kinatamkwa au kuandikwa Jah. Hii inamaanisha kabisa kwamba Mungu ni Wokovu wetu. Kwa hiyo Yahoshua linatumika
kama Yeshua au Yoshua linapotumika, Yesu au Jesus ni uitaji wa Kiyunani wa jina
Yoshua na linatokana na chimbuko lisilo la Kiebrania. Muundo kwenye Kiyunani
unawezekana kabisa kushawishika au kufananishwa na Esus wa imani ya utatu aliyekuwa anaabudiwa kwenye Dini za Wahyperboreani.
Mathayo anauanza
mstari huu kwa kuyakinisha mambo makubwa matatu ya muhimu. Yeshua au Yoshua anayeitwa
Yesu ni Mwana wa Daudi, Mwana wa Ibrahimu. Kwa hiyo basi anaanzisha mstari wa
kuanzia Ibrahimu na kuendelea hadi kwenye mstari wa Yuda. Ndugu ambao wametajwa
tu. Huu ni unabii wenye kueleweka. Mstari unaovuja mapokeo na unamtaja mwanamke
tangu kwenye aya ya 3-6.
Mathayo 1:3-6 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari;
Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu; 4 Aramu
akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni; 5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa
Ruthu; Obedi akamzaa Yese; 6 Yese akamzaa mfalme
Daudi.
Wanawake
wanaotajwa ni Tamari, Rahabu, Ruthu, na Bathsheba ambaye alikuwa ni mke wa Uria.
Maana na umuhimu wa wanawake hawa yanaonyesha somo fulani na maalumu kwenye
mlolongo wa uzao huu. Sara
hakutajwa. Alikuwa na umuhimu na maana isiyo na mashaka kuliko wote. Fruchtenbaum
anaweka pointi za muhimu sana kuhusu wanawake hawa.
Kwanza, wote
walikuwa ni Wamataifa. Hivi ndivyo ilivyokuwa dhahiri kwa Tamari, Rahabu na
Ruthu. Huenda ilikuwa ni kweli kwa Bathsheba, kwa kuwa mu mume wake wa kwanza,
Uria, alikuwa Mhiti. Hapa Mathayo anaongelea kitu fulani na kisha anakiweka wazi
baadae: kwamba wakati lengo kuu la kuja kwa Yesu lilikuwa ni kuja kuwaokoa
kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli, Wamataifa angeweza pia kufaidika na
ujio wake. La pili, watatu kati ya wanawake hawa walikuwa na hatia ya dhambi ya
uzinifu. Bathsheba alikuwa na hatia ya uzinifu, Rahabu alikuwa kahaba na Tamari
alikuwa na tuhuma ya kuolewa na ndugu wa damu. Tena, Mathayo anadokeza tena
vitu kwa kiasi kwamba ambavyo alikuja kuainisha baadae kama: kwamba lengo la
ujio wa Masihi lilikuwa ni kuwaokoa wenye dhambi...
Kuwapatanisha wenye
dhambi kwa Mungu ni hatua ya msingi ya kujitoa kwake dhabihu Masihi. Hii ni hatua ya msingi nay a muhimu ya
Injili.
Ni wale
wasioielewa tu maana ya kiroho ya neema iokoayo ya Masihi ndio wanakuwa wametingwa
na mambo mengi kwa kujaribu kuthibitisha kwamba wanawake hawa hawakuwa
Wamataifa na kwamba hawakuwa wadhambi. Ni muhimu kwamba wadhifa wao ulipewa
wajibu wenye lengo la Masihi azaliwe kupitia kwao. Sadaka yake aliyoitoa
inatosha. Hii haieleweki kikamilifu. Kwa hiyo muda unapotea kwa kujaribu
kuthibitisha kwamba Rahabu alikuwa wa uzao wa Waisraeli wenye asili ya Kikanaani.
Pia ni kwamba alikuwa ni mjane kwa mujibu wa maneno ya Sanskrit kwa mlinzi wake
wa ndani. Ukweli ulikuwa ni kwamba alikuja akitokea kwenye familia mashuhuri.
Watu wake, kwa imani ni kidini ya wakati ule, walikuwa wanafanya ibada za
kingono hekaluni na kwa hiyo ilikuwa ni vigumu sana kuepukana nazo, ukiachana
na ukweli kwamba alikuwa ananyanyapaliwa sana kwa sababu hii.
Muda hautoshi pia
kuthibitisha kwamba Ruthu hakuwa mwanamke wa Kimoabi, kutokana na kuingiliana
kwake ki Mahusiano ya kindoa na Mmoabi, licha ya jinsi yanavyosema maandiko.
Inadaiwa kwamba kwa kweli alikuwa ni wa uzao wa Israeli wa huko Moabi
anayedhaniwa kuwa huenda alikuwa wa kabila la Manase, Reubeni au Gadi (Yoshua
1:12-15). Hilo sio la muhimu, kwamba kwa maneno ya Ruthu mwenyewe yanaonyesha
kwamba mungu wa watu wake alikuwa ni wa tofauti na yule wa Naomi na kwamba hakuapa
kwa Naomi tu peke yake bali pia kwa Mungu wake (Ruthu 1:16).
Ukweli wa mambo
ulikuwa ni kwamba mstari wa familia ya kifalme ulifunguliwa kwa Wamataifa na
kwa wenye dhambi ukianzia kwenye harakati za tangu mwanzoni kabisa za makabila
ya Kanaani. Tendo hili lina maana yake kubwa kwa watakatifu.
Jambo linguine
kubwa kwenye mstari huu wa uzao aliouonyesha Mathayo ni kwamba yeye anachagua
kwa umakini anapoutaja mstari wa uzao. Sulemani anatajwa pia kuwa kwenye udugu
wa damu unaotokana nay eye. Alilijenga hekalu. Hata hivyo, alibobea pia kwenye
ibada za sanamu na mstari wake wa uzao ndipo umeorotheshwa kwa Yekonia
aliyekuwa ni mmoja wa wafalme wa mwisho kabla ya kuanza kwa utumwa wa Babeli.
Mstari wa uzao wa Yusufu kwa hiyo imewekwa kutoka kwa Yekoania hadi Yusufu. Kwa
hiyo, Yusufu ni wa uzao wa Daudi lakini kwa kupitia Yekonia. Jambo hili lina
maana sana.
Yeremia 22:24-30 Kama niishivyo mimi,
asema Bwana, hata Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, angekuwa pete
yenye muhuri katika mkono wangu wa kuume, ningekung'oa wewe hapo; 25 nami nitakutia katika mikono ya watu wale wakutafutao
roho yako, na katika mikono yao unaowaogopa, naam, katika mikono ya Nebukadreza,
mfalme wa Babeli, na katika mikono ya Wakaldayo. 26 Nami
nitakutupa nje, wewe na mama yako aliyekuzaa, mwende nchi nyingine ambayo
hamkuzaliwa huko, nanyi mtakufa huko. 27 Lakini
nchi ile ambayo wanatamani kuirudia, hawatairudia kamwe. 28 Je!
Mtu huyu, Konia, ni chombo kilichodharauliwa, na kuvunjika? Ni chombo
kisichopendeza? Mbona wametupwa, yeye na wazao wake, na kutupwa katika nchi
wasiyoijua? 29 Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la
Bwana. 30 Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu
huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana
hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha
Daudi, na kutawala tena katika Yuda.
Kinia inaundwa
kwa kutokana na kuondolewa kwa neno Ye kutoka
kwenye neno Yekonia au Mwacheni Yehova
(au Jah) atawale. Kuondolwa kwa jina takatifu kunamaanisha kuonyesha
kuondoka wa Mungu kutoka kwa Yekonia. Ashirio lake au mkono wa kuume wa Mungu
unaonekana kwenye aggai 2:23.
Hagai 2:23 Katika siku ile, asema Bwana
wa majeshi, nitakutwaa wewe, Ee Zerubabeli, mtumishi wangu, mwana wa
Shealtieli, asema Bwana, nami nsiitakufanya kuwa kama pete yenye muhuri; kwa
kuwa nimekuchagua, asema Bwana wa majeshi.
Zerubabeli aliorodheshwa
kwenye Mathayo kuwa ni mwana wa Shealtieli. Hata hivyo tunajua kutokana na 1Nyakati
3:18-19 kwamba alikuwa mwana wa Pediya. Tena Mathayo na pia Ezra 3:2; 5:2 wanasema
alikuwa ni mwana wa Shealtieli.
1Nyakati 3:17-19 Na
wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; mwanawe Shealtieli, 18na Malkiramu, na Pedaya, na Shenazari, na Yekamia, na
Hoshama, na Nedabia. 19 Na wana wa
Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na
Shelomithi alikuwa umbu lao;
Mkanganyiko huu
unatatuliwaje? Andko linaonyesha kabisa mahudhui ya tarati.
Kumbukumbu la Torati
25:5-6 Watakapoketi
pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule
aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake
awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe. 6
Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina
lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli.
Kazi hii ni ya
lazima. Kushindwa kumtimizia majukumu haya (kwa mwanamke mwenye tamaa ya
kupenda ngono) ilikuwa ni dhambi ambayo kwayo ilipelekea kuuawa kwa Onani (Mwanzo
38:8-10).
Ndipo Zerubabeli alirithi
kwenye mstari wa uzao wa Sheltieli kwa kuruhusiwa kihalali kulikowekwa na
Pediya aliyekufa baadae. Ndipo Shenaza akafanyika kuwa mwingia nyumba au mlinzi
wa Zerubabeli wakati wa kurudi kwao Israeli kama ilivyoandikwa kwenye Ezra
1:8-11; 5:14-16 wakati alipomrudia Sheshibaza.
Kamusi ya Strong na
nyinginezo zinashikilia kwamba Sheshibaza kuwa ni jina la Kiajemi la Zerubabeli
kwa kuwa kuwa na mtu mwingine haiwezekani kwa kuwa kuwa na mtu mwingine haiwezekani,
na Zerubbabeli ni kijana sana, anahitaji kulijenga hekalu ili lijengwe tena
mahala pake bila kukosewa wakati wa utawala wa Dario II, badala ya kulikosea
wakati wa utawala wa Dario I, ambavyo ndivyo wanavyoamini makundi yote, yaani
marabi wa Kiyahudi na wahafidhina wa Kikristo kwa sababu zao wenyewe (soma
majarida ya Ishara ya Yona
na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu [013]; na la Usomaji
wa Torati Ulivyofanywa na Kina Ezra na Nehemia [250]).
Kutokana na
unabii uliotolewa kupitia Yeremia, mstari wa uzao ulipunguzwa zaidi. Mungu
alitamka kwamba hakuna mtu wa uzao wa Yekonia atakayefanikiwa kuketi kwenye
kiti cha enzi cha ufalme wa Daudi na kutawala tena kutoka Yuda. Hata hivyo,
uzao wa Zerubabeli ulikuwa kwenye mstari, ikionyesha kwamba Mungu aliuchagua
uzao wake kwa kazi fulani maalumu kama pete ya thamani. Kwa maneno mengine, ni
kama mhuri wa Mungu. Hivyo basi Masihi asingeweza kuwa mwana alisia wa Yusufu
na kuketi juu ya kiti cha enzi, pasipokuwa na uthibitisho maalumu wa mbingu
vinginevyo, Maandiko yangekuwa yametanguka. Kristo angekuwa hana vigezo vya
kuketi kwenye kiti cha enzi iwapo kama angekuwa ni mtoto wa kimwili wa Yusufu,
na kwa kuwa Yusufu mwenyewe hakuweza kuwa mrithi kabisa, basi asingeweza
kiritai cheo hiki kwa njia ya kujitwalia. Mungu anaweka kando na kutengeneza
mavunjiko na kuurejesha mstari huo kwa namna nyingine. Mathayo analijua tatizo hili.
Na ndiyo maana anaianza Injili kwa mstari unaoonyesha tatizo na kisha anataja
tukio la bikira kumzaa mtoto jambo ambalo aliliona wazi kuwa ni kama kulishinda
tatizo. Kinachofuatiwa na uzao huu. Mathayo 1:18-25 inaonyesha kwamba
ingefanyika tu kwa mimba ya mwanamwali bikira Mariamu au Miriamu (Maria) na
kwamba ndiye angemzaa Kristo na kuketi kwenye kiti cha enzi. Tukio hili lina
maana yake kwa Wayahudi na kwamba kwa kupitia Masihi ndipo wangeweza kuufikia
ufalme wa kiroho na ukuhani w kiroho.
Kuna
jambo la tatu kwenye mstari wa huu wa uzao wa Zerubabeli ambalo linahitaji
kutathimiwa.
Zorobabeli
alikuwa ni wa kizazi cha 23 kwenye mstari wa wanaume kilichoibuka kutokana na
Mfalme (Na. 1). Alikuwa ni mrithi aliyekubalika. Maelezo ya kina ya jamii yake
ya mababu na suluhu ya mababa wawili vimeorodheshwa kwa yeye kuwa Shealtieli na
Pediya (1Nyakati 3:19) kunafafanuliwa kwenye sharia za Kilawi na ufafanuzi wake
hapo juu. Jambo kuhusiana na mstari huu limefafanuliwa pia kwenye jarida la Kutoka
Daudi na Matukio ya Misafara wa Kurudi Kutoka Utumwani hadi Nyumba ya Windsor
(Na. 67), kwa mujibu wa matukio ya nyakati-zama ua Kiyahudi kwa kutumia mkururo
wa matukio ya Dario I. Hesabu sahihi ya nyakati hizi imefafanuliwa kwa kina
kwenye jarida la Ishara ya Yona
na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu [013].
Zorobabeli
alikuwa ni mrithi stahiki wa jamii ya kifalme ya Kiyahudi na alikuwa kwenye
Msafara wa 3 wa waliorudi kutoka utumwani Babeli mnamo mwaka 545 KK. Alikuwa ni
Liwali wa 8 wa Yudea mnamo mwaka 537-536 KK. Alikuwa ni Mfalme wa Yuda mnamo
mwaka 515 KK, na alikuwa alishitakiwa na kufungwa mwaka 513 KK na akauawa mwaka
510 KK.
Alioa
wanawake watatu. Mke wa kwanza alikuwa ni Amytis Binti Mfalme wa Kibabeloni, aliyeitwa
kuwa ni mwanamke wa kigeni. Alimzalia mtoto aliyeitwa Shazreza, ambalo ni jina
la Kibabeloni. Alikuwa ni mtu aliyetokea kwenye jamii kubwa ya mstari wa mfalme
Daudi.
Mke
wa pili wa Zorobabeli alikuwa Rhoda ambaye alikuwa ni Binti Mfalme wa Kiajemi
ambaye baadae aliolewa tena na Mwana Mfalme wa Kiajemi na aliitwa pia aliitwa
mwanamke wa kigeni. Alimzalia mtoto aliyeitwa Reza (jina la Liajemi). Alisemekana
kuwa ni mjomba wa Dario, mfalme wa Uajemi kwa kupitia mama yake. Ni mstari huu
auliotajwa kwenye uzao wa Mariamu kama tutakuba;iana kwamba mstari wa uzao wa Zorobabeli
kwamba kwa kweli ulikuwa unapitia kwa Nathani na mwana wa kumkuta au wa
kuasiliwa wa Yekonia, aliyeitwa Shealtieli ambaye alikuwa kwa kweli ni mwana wa
Neri(a). kitendo cha Kumvika taji Binti Mfalme Tamari kilikuwa ndiyo sababu ya
kubadilika kwa mstari huu. Hili ni tukio lingine kwa Binti mfalme Tamari lililotumiwa
kubadilisha ufalme. Tutaelezea na kufafanua kwa kina jambo hili baadae hapo
chini.
La
tatu, Zorobabeli alimuoa Esthra, ambaye alikuwa ni binti mfalme wa Kiyahudi. Na
kutokana na yeye mstari wa familia iliyopo ya kifalme umetokea.
Unabii
kuhusu kiti cha enzi na mahali pa Zorobabeli kwenye mchakato unaonekana kuwa ni
sehemu ya mchakato wa haki ya ahadi ya uzaliwa wa kwanza ya siku za mwisho.
Kumbuka
kwamba baba wa Zorobabeli alikuwa ni Shealtieli/Pediya na baba wa Shealtieli kwa
kweli hakuwa Yekonia. Alikuwa ni mwana wa kufikia wa Yekonia na alikuwa ni
mrithi aliyekubalika au anayestahili (Mathayo 1:12). Alikuwa ni mwana wa mke wa
mke wa Mfalme Yehoyakini au Yekonia kwa mke wake wa zamani wa Binti Mfalme
Tamari, aliyeitwa Mwana Mfalme Neri(a). Soma pia Luka 3:27. Sasa ukweli huu
unatoa mwibuko mwingine wa jambo unaotokana na mstari wa uzao wa Zorobabeli au
Zerubabeli ambao kwa kweli ndiyo aliotokea.
Tunaona
kwamba mstari ulio kwenye injili ya Luka ulikuwa ni wa Daudi kwa kupitia kwa Nathani,
na mstari ulio kwenye Mathayo ulikuwa ni wa Daudi kupitia kwa Sulemani. Iwapo
kama ufafanuzi huu unakubalika, kw hiyo mstari wa Yekonia na laana
iliyotangazwa kwa hii imeshindwa kwenye kile ambacho mstari wa kupitia
Zorobabeli kupitia kwa Shealtieli. Hata hivyo, ukweli ni kwamba baba alidaiwa
kuwa ni Pedaya kwa mujibu wa sheria za Kilawi, na kizazi kinaenda hadi kwenye
mstari wa baba yake. Mstari ule kwa kweli ni wa Nathani kupitia kwa Neri au
Neria. Ni sawasawa tu kabisa na kwamba hii ilikuwa ndiyo sababu iliyokuwa imetumiwa
kuishinda laana waliyotamkiwa watu wa jamii ya mstari wa Yekonia. Shealtieli anaonekana
kuwa ni mlengwa kwenye mjumuisho wa mistari hii. Mistari hii kwa hakika
inatuama kwenye kiti cha enzi cha Yuda, ukiishia utumwani, na umefanya vya kutosha kwa karne kadhaa, na
kwa hivi karibuni sana kwa makabila kumi.
Ukweli
mkuu kwa yote haya ni kwamba tunaweza kukioka au ukiibua kizazi hiki kwenye nyumba
za kifalme za Israeli hadi kwenye pande za Kaskazini mwa Ujerumani na Uingereza
ambao ndiyo makabila ya Kaskazini ya Israeli. Ufalme unabakia ndani ya Israeli
hadi sasa hadi atakaporudi Masihi ambaye utakuwa ni haki yake.
Mfalme
Halali wa Yuda
Kuna
umuhimu mkubwa sana kujua kwamba kwenye mstari wa Waliokuwa kwenye Msafara wa
kurudi kutoka utumwani (kama lisemavyo jarida la Cox ibid, (Na. 67) hapo juu), kwamba
mwaka 12 KK ambao ndiyo miaka ya mwanzoni mwanzoni kabisa ya Kristo
aliyotarajiwa kuwa angezaliwa na ambayo kwa kweli ni mwaka wa kutangazwa kwa
amri ya kuhesabu watu iliyotolewa na Augustus ambavyo ni hesabu iliyofanyika mara
kwa mara kwenye Dola ya Kirumi ulitangulia, hakukuwa na Mtoka kwenye Msafara wa
kurudi utumwani aliyetawazwa kwenye kiti cha ufalme wa Yuda. Tangu wakati huu na
kuendelea mbele walifukuzwa. Ilikuwa tu baada ya kuzaliwa kwa Mwasihi mwaka 30 BK
kwamba alikuwepo mtoka kwenye Msafara wa kurudi utumwani aliyetawazwa kupewa
kiti cha enzi cha ufalme wa Yuda. Hivyo basi, Mungu hakuruhusu mfalme bandia
awekwe kwenye kiti cha enzi, au astahilishwe na kupendekezwa au kuchaguliwa
kuchukua kiti cha enzi Yuda wakati wa mzunguko wote wa mchakato wa kuzaliwa kwa
Yesu Kristo ambaye ndiye alikuwa mfalme stahiki wa ufalme wa Yuda.
Kuna jambo
lingine kuhusu mstari huu wa uzao linaloweka taswira nalo ni kwamba kuna idadi
kubwa ya vizazi vilivyotajwa kwenye Mathayo 1:17.
Basi vizazi vyote
tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule
uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli
hata Kristo ni vizazi kumi na vinne.
Kujikusanya kwa
vizazi hivi kunaonekana kuwa na maana kwenye idadi ya makundi. Kundi la uzao wa
Masihi lina maana kubwa sana tangu Adamu. Vizazi saba vya mwanzo tangu Adamu
vina maana kwenye Mpango wa Wokovu. Kitendo cha kugawa makundi kwenye injili ya
Mathayo ya makundi matatu ya kumi na nne kumi na nne kinaonyesha tu utendaji
kazi wa Mungu. Ibrahimu aliitwa na kutengwa mbali na wengine. Vizazi kumi na
nne baadae ndipo Daudi mtu wa kawaida tu aliteuliwa na kutengwa mbali na
wengine (1Samweli 16:13). Daudi akawaweka pamoja Israeli kama mtawala na
kulijenga Heklu kwa kupitia mwanae Sulemani ambaye kwaye, ndpo aliliandaa taifa
na raslimali zake. Viazi kumi na nne vilivyofuatia baadae matokeo ya mwisho ya
utawala wa kibinadamu na ufalme ulikuwa ni tukio la kwenda utumwani. Vizazi
kumi na vinne vilivyofuatia baadae, baada ya taifa kuwa limefanya upya chini ya
ukuhani, ndipo itabidi wahukumiwe kipindi cha kuja kwake Msihi na kutawanyishwa
kwa Ishara ya Yona (soma jarida la Ishara
ya Yona na Historia ya Ujenzi Tena wa Hekalu (Na. 13) ibid.). jambo hili halikueleweka.
La muhimu zaidi
ni kwa,ba kizazi cha 42 kilicho kwenye injili ya Mathayo kuanzia Ibrahimu hadi
Kristo kinatajwa kwenye dhana iliyokutikana kwenye ujenzi wa Hekalu. Hekalu
lilijengwa kwa mpango wa kiroho wa Yubile. Migawanyo sita iliyogawanywa inafananishwa
na neva au mlango unaoonyesha mfano kwamba Masihi aliweka milango mingi kwenye
hekalu inayoweza kuingilika vizuri wakati atakaporudi. Kwa kufa kwake
alilipasua pazia la Hekalu ili kufungua njia wazi hadi mahali paitwapo naos au
Patakatifu pa Patakatifu, ambapo ndipo walipo wateule wake (1Wakorintho 3:16). Njia
hii ilifunguliwa yote kabisa tangu kuangamizwa kwa lile Hekalu lililojengwa kwa
mikono ya wanadamu (Waebrania 9:8).
Vyote viwili,
yaani ukuhani na ufalme vilianzishwa na kuhukumiwa vikitakiwa na Masihi. Kwa
hiyo Masihi alikuwa ni Masihi wa Haruni na wa Israeli; na alikuwa ni wa namna
zote mbili, yaani Masihi-kuhani na Masihi-mfalme. Masihi mmoja mwenye ujio wa
mara mbili alikubalika na Israeli, kama tujuavyo kutokana na magombo
yaliyovumbuliwa yajulikanalo kama Dead Sea Scrolls (soma kitabu cha G. Vermes cha
Gombo za Bahari ya Chumvi (The Dead Sea
Scrolls) kwenye lugha ya Kiingereza, re Damascus Rule VII and the fragment
from cave [mmeguko kutoka pangoni] IV). Vermes, kama walivyo wengine,
anashikilia kuamini kwamba Masihi wa Haruni na Masihi wa Israeli walijulikana
kuwa ni mmoja huyo huyo wa majilio tofauti kutokna na imani ya Wayahudi wa
karne ya kwanza.
Jibu la matatizo haya
yaliyoibuka kutoka kwenye mstari wa uzao ulio kwenye injili ya Mathayo
linajibiwa na yeye kwenye sura ya 1:18. Maibu makuu na ya zaidi kwenye maandiko
haya ni kwenye injili ya Luka. Kwa hiyo, yote mawili yanapaswa yasomwe kwa
muunganiko au kwa kuhusianisha.
Hatua nyingine na
ya muhimu iliyofanywa na Arnold Fruchtenbaum kuhusu mstari wa uzao wa Masihi,
ambao pia una maana pana zaidi ni kwamba mapokeo ya Kiyahudi ya wakati ule.
Anasema hivi kuhusu maelezo ya Luka:
Mbali na Mathayo,
Luka kufuatia kikamilifu mwelekeo na mapokeo yaliyopo hakuruka au kuacha majina
na wala hakuwataja wanawake. Hata hivyo, kama kwa mujibu wa mapokeo ya Kiyahudi
mtu hakuweza kulitaja jina la mwanamke, bali alipenda kuonyesha mstari wake, ni
kwa jinsi gani aliweza kufanya hivyo? Angelitumia jina la mume wake. (Karibu
Agano lote la Kale linaanza kwa tendo hili la kwenye Ezra 2:61 na Nehemia
7:63).
Hiyo ingeibua swali
la pili la kwamba: Kama mtufulani alisoma mstari wa uzao, angewezaje basi iwapo
kama uzao huo ulikuwa ni ule wa mume wake au ni ule wa mwanamke, na iwapo kama
kwa sababu hiyo jina la mume lingetumikaje? Jibu lake sio gumu, tatizo
linatokana na lugha ya Kiingereza.
Kwa Kiingereza siyo grama
nzuri kutumia kiamhishi halisi (the) kabla ya jina halisi (‘the’ Matthew, ‘the’
Miriam); haya hivyo, inaruhusiwa sana kwenye grama ya Kiyunani. Kwenye maandiko
ya Kiyunani ya uzao ulioandikwa kwenye injili ya Luka, kile jina moja
lililotajwa lina kiambishi cha Kiyunani cha ‘the’ pamoja na nyingine isiyo ya
kawaida: jina la Yusufu (Luka 3:23). Mtu anayesoma maandiko yenyewe ya asili anaweza
kuelewa kwa viambishi vingine vinavykosekana kwenye jina la Yusufu kwamba huu
haukuwa mstari halisi wa uzao wa Yusufu bali ni mke wake, yaani wa Mariamu.
Zaidi sana, ingawa
tafsiri nyingi za Luka 3:23 zinasomeka kwamba: “...akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli, ...”, kwa sababu ya
kiambishi muhimu kinachokosekana kwenye Kiyunani cha kabla ya jina la Yusufu,
ni aya hiyohiyo ingeweza kutafsiriwa kama:
“Na akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,...” (msisitizo umewekwa).
Kwa naneno
mengine ni kwamba ingawa Yehoshua (Yeshua, Yoshua au Yesu) alitakiwa kuwa mwana
wa Yusufu, lakini kwa kweli alikuwa ni wa uzao wa Eli ambaye alikuwa ni Baba wa
Mariamu. Tafsiri ya Jerusalem Talmud iliuchukulia mstari huu wa uzao kuwa ni wa
Mariamu na sio wa Yusufu. Inamtaja Mariamu kuwa ni kama binti wa Eli kwenye
Hagigah 2:4.
Kutumika kwa makala
maalumu kwenye uandishi wa Kiyunani pia unauhusiano wake kunapowekwa tofauti
kati ya Masihi na Mungu, kwa mfano kwenye Yohana 1:1,18; 1Yohana 5:20. Hili
limeonekana kutimilika kwa kipindi zama kimoja hadi kingine na dini kwa
kutokubaliana na kile kinachoitwa uhafidhina (mfano ni maandiko ya Socinians; soma
kitabu cha ufafanuzi cha Heydock hadi kwenye marudio ya chapisho ya mwaka 1851 ya
Kikatoliki au tafsiri iitwayo Douay-Reims Bible).
Luka anaonyesha
kumuweka Kristo kwenye zama za nyuma sana hadi Adamu ambapo ni kuonyesha
mchakato wa uzao wa mwanamke tangu Adamu. Andiko hili linauonyesha mstari wa
uzao wa Daudi pamoja na Nathani ambao ni muhimu kwa kutimiliza unabii ulio
kwenye Zekaria. La muhimu sana ni kwamba mbali na mstari wa uzao wa Yekonia
ambao ulikuwa umeondolewa, miongoni mwa mambo mengine ni fanya njia ya utawala
wa Kuhani Mkuu. Kwa hiyo, Yehoshua au Yoshua alikuwa ni wa uzao wa Daudi kutoka
kwa mama yake. Kwa hiyo, kuzaliwa na mwnamwali bikira mbali kunaendelezwa
kwanza na kisha uzao untajwa hapa kwenye Luka. Na kwa hiyo inaanzisha sharti la
kwanza kwa udugu ambao ni wa mstari wa uzao wa Daudi mbali na ule wa Yekonia.
Anaanzisha sharti
la pili la kufanyika kuwa wa mstari wa Nathan na wa familia ya Lawi kwa kupitia
Shimei kwa kando na mlolongo wa uhusiano wa familia ya Miriam hadi kwa
Elisabeth mke wa Zakaria, Kuhani Mkuu wa Zamu ya Abiya (au Abia), ambayo alikuwa
ni wa zamu ya nane ya Kuhani wa Hekaluni (soma 1Nyakati 24:10; Nehemia 12:17). Zamu
au migawanyo ishirini na nne iliundwa baada ya kurudi kutoka kwenye migawanyo
ya njia ya kura, kwa majina yenyewe halisia (soma Comp. Bible fn. na App. 179
III).
Mke wa Zakaria
alikuwa Elisabeth (aliyeitwa jina lake kutokana na jina la mke wa Haruni Elisheba
(Kutoka 6:23) na akamvuvia Elizabeth kwenye LXX). Alikuwa ni binti wa Haruni na
kwa hiyo alikuwa ni Mlawi (Luka 1:5). Alikuwa ni mama yake Yohana Mbatizaji kwa
minajiri ya kimungu. Kwa hiyo Yohana alichaguliwa. Mariamu (Maria) alikuwa ni
wa kutoka familia ya Elizabeth (Luka 1:36). Kwa hiyo ni lazima Mariamu atakuwa
ni wa mstari wa kidamu wa kabila la Lawi pamoja na kuwa ni wa Nyumba ya Daudi.
Tunadhania tu
kiunasibu kwenye mstari wa ukoo wa Lawi kwa kupitia Shimei, hata hivyo inaweza
kudhaniwa au kuchukuliwa, kwa kuwa Maandiko hayawezi kutanguka. Kuonyeshwa kwa mstari
wa ukoo wa Walawi kunatosha. Uvuvio wa kimungu wa Zekaria na Elisabeth na ndipo
jina la Yohana linatupeleka kwenye hatua nyingine inayofuatia.
Walikuwepo
wengine kwenye Nyumba ya Daudi na sio wa mstari wa Yekonia. Hivyo jambo lenyewe
ni lazima liwe ni la kuruhusiwa na mbingu ambapo linaweka kigezo cha sharti la
tatu kwa kufanyika mfalme. Luka anaendelea kuweka vigezo cha kuchaguliwa na
mbingu kwenye Luka 1:30-33.
Luka 1:30-33 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa
maana umepata neema kwa Mungu. 31 Tazama, utachukua
mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. 32 Huyo
atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi
cha Daudi, baba yake. 33 Ataimiliki nyumba ya
Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
Kwa hiyo ndipo
Bwana Mungu alimpa kiti cha enzi cha baba yake Daudi. Alitimiliza vigezo kwa
kupangiwa au kuruhusiwa na Mungu.
Alikuwa ni wa uzao wa mwanamke kama ilivyikuwa imetabiriwa
kwenye kitabu cha Mwanzo. Mathayo inaonyesha ni kwa nini hakuwa mfalme
anayetokana na uzao wa Yusufu bali ni wa kuzaliwa tu na mwanamwali na ni mpango
wa kimungu. Luka anaonyesha kwa jinsi ipi alitimiliza unabii mwingine na
hakueleweka vizuri na ama marabi wa Kiyahudi au Wafafidhina wa Ukristo mkongwe.
Malengo ya marabi kwenye Umasihi wake kwa maana ya kwamba ni lazima iwe ni kwa
kupitia mstari wa baba yake wawe waongo kwa minajiri ya unabii na kigezo cha kuwa
mwana wa Mungu. Elohim wa Israeli asingeweza kuchukua hali ya ubinadamu ma
maana ya kihalisia. Alifanyika mwanadamu kwa kuelekezwa na elohim wake ambaye ndiye
El Elyon, Mungu Aliye Juu Sana. Kigezo hiki kilitabiriwa na nabii Isaya ambaye
alisema:
Isaya 7:14 Kwa
hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa
mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.
Sio kwamba kuitwa
kwake Mungu pamoja nasi kunaweza
kufikiwa tu iwapo kama El aliyetumwa hapo mwanzoni alikuwa elohim na kwa kweli
ni elohim wa Israeli aliyetiwa mafuta kuwa elohim na elohim wake kama
inavyoonekana kwenye Zaburi 45:6-7. Alipata haiba yake ya uwanadamu kikamilifu
sana kutoka kwa mama yake. Kwa hiyo, mapokeo ya taifa la Kiyahudi na
utambulisho wa kikabila vililetwa na kiumbe huyu ili kwamba aweze kufanya
shughuli za kikuhani baada ya Melkisedeki na kisha afanyike kuwa kichwa au
kiongozi kwa utaratibu wa wafalme na makuhani waliochaguliwa mbali na mstari
ila ilifanywa kwa mkabila yote kama tunavyoona kwenye Ufunuo 7:3-8.
Yeye ni mwana wa Daudi na mwana wa Ibrahimu kutokana na Mathayo 1:1. Luka
3:38 kunakomtaja yeye kuwa ni mwana wa Adamu na mwana wa Mungu. Kwa hiyo anajipatia mambo mengi zaidi na
maradufu pia kwenye injili. Akiwa kama mwana wa Daudi, yeye ni Mfalme wa Yuda
yote. Na akiwa kama mwana wa Ibwahimu, yeye ni Mfalme wa Israeli kama mrithi wa
ahadi zilizotolewa na kwa kupitia Yusufu. Yeye pia ni kiongozi au kichwa cha mataifa mengine
ya Ibrahimu. Akiwa kama mwana wa Adamu yeye ni mwanadamu na hivyo anastahili
kuwaongoza wanadamu kwenye wokovu kwa kupitia kifo chake. Akiwa kama mwana wa
Mungu anafika kimo cha wadhifa wa elohim ambacho alikichilia wakati alipokuja
kuzaliwa kimwili, na kwa kufufuka kwake kutoka kwa wafu akiwa kama mwana wa
Mungu mwenye nguvu na uweza (Warumi 1:4). Anastahili kuwa Nyota ya Asubuhi na
atashiriki utawala ule pamoja na watu wote wa nyumbani mwake (Ufunuo 2:27-28;
22:16; sawa na Zekaria 12:8) kama wanavyoshiriki asili na tabia za Mungu kama anavyofanya (2Petro 1:4).
Tafsiri ya The Peshitta inasema:
27 naye atawachunga kwa fimbo ya
chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa
Baba yangu. 28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.
Masihi alikuwa mtii hadi kufa na kwa hiyo anatakiwa pia awe mtiifu na atatupa utawala wa Nyota wa Asubuhi ambaye ni Mwana wa Mungu, akiwa kama elohim kama Malaika wa Yahova aktuongoza. (Zekaria 12:8).
q