Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[170]

Wajibu wa Amri ya Nne katika Historia ya Makanisa ya Mungu Yanayoishika—Sabato

(Toleo la 2.0 19960622-20000122)

Inaaminika kisahihi sana na Makanisa ya Mungu yanayoitunza—Sabato ya kipindi cha takriban karne mbili zilizopita kwamba ujumbe mkuu na alama yenye kutambulisha Ukristo ilikuwa ni Sabato na kwamba makanisa kwa kipindi chote kizima cha kihistoria yalikuwa yanateswa kwa ajili ya kushikilia kwao msimamo wa kuitunza Sabato. Sehemu hii imetegemea kwa sehemu kuwa ni kweli na ni vibaya sana iwapo kama tutaficha mambo ya kweli ya msingi ya imani ambayo kwayo kanisa la Mungu lilipata mateso na mambo mengine yote yanayofanya alama ya mteule. Jarida hili linaonyesha kuwa kwa kweli kuna mlolongo wa ishara nyingine zinazomuonyesha mteule na ambazo zilitumika kuwatenganisha na kuwafanya waonekane watu wa namna ya pekee kwenye jamii kwa zipindi vyote cha mateso yanayojulikana kwa jina maarufu kama kipindi cha hoja cha kanisa la Kirumi.

CHRISTIAN CHURCHES OF GOD

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

E-mail: secretary@ccg.org

 (Copyright © 1996, 1998, 2000 Wade Cox)

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.login.org au http://www.ccg.org

Wajibu wa Amri ya Nne katika Historia ya Makanisa ya Mungu Yanayoishika—Sabato


Utangulizi

Kwenye jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoishika Sabato [122] kulionekana kuwa klikuwa na mnyororo endelevu wa Makanisa yanayoishika Sabato kwa kipindi chote cha kihistoria ambao yalikuwa kwenye upinzani au mapingamizi zaidi au wakati mwingine yalipoa, na kuteswa na mfumo wa makanisa makubwa yenye mfumo wa udini. Inaaminika kisahihi sana na Makanisa ya Mungu yanayoitunza—Sabato ya kipindi cha takriban karne mbili zilizopita kwamba ujumbe mkuu na alama yenye kutambulisha Ukristo ilikuwa ni Sabato na kwamba makanisa kwa kipindi chote kizima cha kihistoria yalikuwa yanateswa kwa ajili ya kushikilia kwao msimamo wa kuitunza Sabato. Sehemu hii imetegemea kwa sehemu kuwa ni kweli na ni vibaya sana iwapo kama tutaficha mambo ya kweli ya msingi ya imani ambayo kwayo kanisa la Mungu lilipata mateso na mambo mengine yote yanayofanya alama ya mteule. Jarida hili linaonyesha kuwa kwa kweli kuna mlolongo wa ishara nyingine zinazomuonyesha mteule na ambazo zilitumika kuwatenganisha na kuwafanya waonekane watu wa namna ya pekee kwenye jamii kwa zipindi vyote cha mateso yanayojulikana kwa jina maarufu kama kipindi cha hoja cha kanisa la Kirumi. Mfumo wa kihafidhina wa makanisa ya mrengo wa kitamaduni ya Kirumi ulitumia alama nyingi zenye kuashiria misimamo ya kiimani kwa kukusanya taarifa na ushahidi kinyume na wateule kwa nia ya kutafuta njia ya kuwaangamiza.

Makanisa ya Mungu ya karne ya ishirini yalifanya yalifanya makosa makubwa yakimsingi kwaa kudhania kwamba walijua vizuri zaidi au walijua kwa ukamilifu sana kuliko ufahamu ambao waliokuwanao makanisa yaliyowatangulia ya nyakati zilizotangulia kabla yao. Hii kwa kweli, ilithibitisha sababu ya kupotea kwa makanisa ya siku zilizofuata na kubakia yakiwa katika hali ya kutoelewa mafundisho ya makanisa ya kwanza na jinsi ya kulitendea kazi fundisho la imani yao. Ni kweli

kabisa kwamba zama zilizofuatia zilionyesha tabia zote mbili yaani za mfumo wa Wasardi na Walaodikia (Ufu. 3:1-6, 14-22). Kwa kutokana na hali hii ya kutokujua, watazua mfumo wa kweli wa Wafiladelfia (Ufu. 3:7-13) ambao unanguvu kidogo lakini ulio na uaminifu kwa amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufu. 12:17; 14:12).

Je, ni nini hasa kinachonenwa na Biblia kuwa ni ishara ya wateule na wajibu ambao Sabato inahukana nalo kwa mchakato wa utambulisho?

Sabato kama Ishara mojawapo ya Kanisa

Sabato ni amri ya nne. Imefanyiwa tathmini kwa kirefu kwenye jarida la Sheria na Amri ya Nne [256] pia tazama jarida lisemalo (Sabato, [031]). inapatikana kwenye Kutoka 20:8,10,11; na Kumbukumbu la torati 5:12.

Sabato imeorodheshwa kama ishara ya watu wa Mungu. Ni ishara katiyetu na Mungu atutakasaye.

Kutoka 31:12-14 inasema: 12BWANA akasema na Musa, na kumwambia, 13 Kisha nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi. 14 Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.

Ni mara nyingi na kwa makosa sana imedhaniwa kuwa Sabato zinazoelezewa hapa ni za aina moja tu ambazo zimetajwa kimakundi kama Sabato ya kila Juma. Hivyo ni kukosea. Sabato zimeendelezwa hadi kupelekea tendo lote zima la ibada kwa Siku Takatifu zilizoorodheshwa kama Sabato za Mungu. Tendo la kuuawa kwa anayeitia unajisi kwa leo linafanyika kwa jinsi ya rohoni.

Sabato haiwezi kutenganishwa kabisa na maana ya ishara ya Kanisa. Pia ni ishara ya wana wa maagano ambao bado hawajaitwa kujiunga na Kanisa. Basi kama zilikuwa ni ishara ya wateule, waumini wa dini ya Kiyahudi wangekuwa na sehemu katika ufufuo wa kwanza, jambo ambalo halitakuwa hivyo.

Ishara au alama nyingine za wateule

Ishara nyingne ya pili ni Pasaka na adhimisho la Mikate Isiyotiwa Chachu.

Kutoka 13:9-16 inasema: Nayo itakuwa ishara kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya macho yako, ili kwamba sheria ya BWANA ipate kuwa kinywani mwako; kwani BWANA alikutoa utoke Misri kwa mkono wenye uwezo, 10 Kwa hiyo utaitunza amri hii kwa wakati wake mwaka baada ya mwaka. 11 Itakuwa hapo BWANA atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, kama alivyokuapia wewe na baba zako, na kukupa, 12 ndipo utamwekea BWANA kila afunguaye tumbo, na kila mzaliwa wa kwanza uliye naye, azaliwaye na mnyama; hao waume watakuwa ni wa BWANA. 13 Kila mzaliwa wa kwanza, wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo; na kwamba hutaki kumkomboa, utamvunja shingo; na kila mzaliwa wa kwanza wa binadamu katika wanao utamkomboa. 14 Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza keshoni, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia, BWANA alitutoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake; 15 Basi ilikuwa hapo Farao alipojifanya kuwa mgumu ili asitupe ruhusa kuondoka, BWANA akawapiga wazaliwa wa kwanza wote waliokuwa katika nchi ya Misri, wa binadamu na wamnyama; kwa ajili ya hayo namtolea BWANA wote wafunguao tumbo, wakiwa waume; lakini wazaliwa wa kwanza wote wa wana wangu nawakomboa. 16 Jambo hilo litakuwa ni ishara mkononi mwako, na utepe katikati ya macho yako; kwa kuwa BWANA alitutoa Misri kwa uwezo wa mkono wake.

Pasaka na adhimisho la Mikate isiyotiwa Chachu ni ishara ya pili ya wana wa maagano. Upanuzi huu wa amri ya nne (kama tulivyojionea hapo juu) ni sawa na kuzipiga sheria za Mungu kwenye matendo (mikononi) yetu na kwenye nia au mawazoni mwetu (usoni katikati ya macho). Ni ishara ya sheria za Bwana (Kum. 6:8) na kwa ukombozi wa Israeli (Kum. 6:10). Kwenye Agano Jipya sheria hii iliendelezwa hata kwa Wamataifa wasio Waisraeli walio katika Kristo (Rum. 9:6; 11:25-26). Tendo la kuielewa Pasaka katika Makanisa ya Mungu katika pikindi cha karne ya ishirini kumekuwa ni kosa kubwa sana. Imedhaniwa kimakosa sana kuwa Wayahudi hatimaye pia waliiadhimisha kimakosa ya kuwa Pasaka ilikuwa ni usiku wa siku ya kumi na nne ya mwezi wa Nisani na ni siku ile iliyojulikana kama ni Usiku wa Kuangaliwa Sana ambayo ilikuwa ni siku ya kumi na nne na kwamba usiku ule ulichukuliwa kwa makosa kuuita ni usiku wa Pasaka na Wayahudi. Hii imefanyiwa tathmini kwa kina na muundo wote wa mpangilio wa uwongo ambao kwayo unategemea umefafanuliwa kwenye jarida Shirikishi lililoongezewa kwenye jarida liitwalo Pasaka, [098].

Ishara ya sheria, Sabato, na Pasaka zimefanyizwa rasmi kwa nia ya kuwalinda na ushawishi wa kujiingiza kwenye ibada za sanamu (kum. 11:6). Ishara hizi mbili zinatakiwa zipigwe mikononi au kwenye vipaji vya nyuso za wateule wa Bwana. Wakiwa na Roho Mtakatifu wanaunda msingi wa utiwaji muhuri wa kwenye Ufunuo 7:3 wa siku za mwisho. Ishara ya wateule kwa hiyo utatuama kwenye amri ya kwanza. Kristo alisema; Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake (au tumikia) (Mat. 4:10; Lk. 4:8). Kutumikia kunamaana ya kufanya ibada kwa usemi wa kibiblia.

Adhimisho la Utapanisho ni ishara nyingine ya wana wa mwagano. Tendo la kuacha au kushindwa kuadhimisha Upatanisho kulitolewa adhabu ambayo ilikuwa ni kukatiliwa mbali na watu wake atendaye hivyo; kwa maneno mengine, kutoka kwenye mwili wa maagano wa Israeli ambao ni kanisa (Law. 23:29).

Ishara ya mwanzo na ya msingi wa wana wa maagano ulikuwa ni tohara (Mwa. 17:14). Hii ilifanywa baadae kuwa ni sawa na tendo la ubatizo (tazama jarida la Toba na Ubatizo [052].

Kwa hiyo, Ubatizo wa Roho Mtakatifu, ni ishara ya mwazo ya msingi ya wateule kwa kupitia damu ya Yesu Kristo kwenye mwili mmoja (Mat. 28:19; Mdo. 1:5; 11:16; Rum. 6:3; 1Kor. 12:13; Ebr. 9:11-28).

Pahala pa fundisho la msingi la Kanisa

Fundisho kuu la msingi lililokuwa la kawaida na kujulikana na wateule laweza kuonekana kutoka kwenye siku za mwanzo kabisa. Kadiri vile tunavyokaribia kwa mtume Yohana ni kwa kupitia kwenye uandishi wa wanafunzi akina Policarp na Irenaeus. Mtazamo kwa mwanzoni kabisa ni kwamba Biblia na kanisa la Agano Jipya walikuwa na mtazamo tofauti kuhusu fundisho la Uungu na vile ambavyo imekuwa ikiendelea kufundishwa kwa takriban kipindi kama cha miaka elfu mbili iliyopita.

Mhimili wa imani yao ulikuwa ni mafundisho yao kuhusu Mungu. Sabato, Miandamo ya Mwezi Mpya na Sikukuu vilikuwa ni mambo mbalimbali yaliyokuwa yanajumuisha kuhusu ibada kwa Mungu. Hii ilikuwa pia inajumuishwa na ushikaji wa sheria za vyakula kwa ambayo ilienea sana au msingi mkuu (tazama jarida la Sheria za Vyakula, [015]. Kwa hiyo, Sabato na mambo mengine yote yaliyotokana nayo, yalikuwa ni shara ya imani juu ya ibada ya Mungu mmja (Yoh. 17:3). Mungu huyu, Eloah, alikuwa kabisa ni yeye yule ambaye aliabudiwa na Yuda na kudhihirika kwenye Agano la Kale. Kwenye Kanisa la kwanza, Biblia ilikuwa na maana ni ile ya Agano la Kale ambayo ilitafsiriwa na kufafanuliwa na Agano Jipya (tazama jarida linalosema, Biblia [164]. Fundisho la kanisa la kwanza kuhusu Mungu limefanyiwa upembuzi katika majarida ya Teolojia ya Mwanzoni ya Uungu, [127] na pia Hali ya Kutokufa, [163], Uungu wa Kristo, [147], Amri ya Kwanza: Dhambi ya Shetani, [153] na pia Kuwa na Nguvu Sawa na Baba, [081].

Msingi wa Kibiblia wa Mafundisho ya Msingi

Msingi wa Kibiblia wa Mafundisho ya msingi imetuama kwenye amri kuu na ya kwanza (tazama jarida la Amri Kuu ya Kwanza [252]. Kwa jinsi hii tunaona kwamba amri ya nne imekuwa inakuwa ni ya nne iliyosawazishwa tu na utaratibu mkubwa zaidi yake. Sabato zote na Siku Takatifu kwa pamoja ni muundo mdogo wa amri ya nne na inahusiana kwa ndani na hizi amri nyingine. Hii imefanyiwa upembuzi kwenye jarida la Matamko ya Kuhusu Imani ya Kikristo [A1].

Kanisa limeamriwa kuzishika na kuzitunza Amri Kumi za Mungu kama zinavyoonekana katika vitabu vya Kutoka 20:1-17 na Kumbukumbu la torati 5:6-21.

Amri ya kwanza inasema:

Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.

Mungu Baba ni Mungu wa pekee wa kweli (Yoh. 17:3) na hakuna elohim mwingine kama yeye au aliyesawa na yeye. Hairuhusiwi kumwabudu au kukifanyia maombi kitu kingine cho chote akiwemo Jesu Kristo.

Amri ya pili inasema:

Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu ya mbinguni, wala kilicho majini chini ya dunia. Usikisujudie wala kukitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Kwa hiyo, imekatazwa kabisa kujifanyia sanamu au mfano wa kitu cho chote hata kwa ajili ya maelekezo ya au matumizi ya ibada za kidini au nembo. Kwa ajili hii, alama ya msalaba pia itakuwa ni miongoni mwa vitu vilivyokatazwa kutumiwa na Makanisa kwa ajili ya kuweka nembo au alama ya mahali pa kufanyia ibada au kuonyesha kuwa ni nembo ya kidini. Amri yenyewe tu kama inavyoonekana huweka muundo wa namna ambayo inatosha kabisa kuwa ni utambulisho au nembo ya mfumo wa kidini na kwa hiyo, yote inajitosheleza.

Amri ya tatu inasema:

Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.

Jina la Bwana Mungu lina mamlaka na kwahiyo amri hii sio tu kuwa inashughulika na namna tu ya makufuru, bali inafikia hata kwenye hatua ya kuhusikana na matimizi mabaya ya mamlaka ya Kanisa na wale wote wanaoenenda vibaya tofauti na maelekezo ya Mungu kupitia Yesu Kristo.

Amri ya Nne inasema:

Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwahiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

Sabato ya kila siku ya saba ya juma, ni ya muhimu sana kwa wokovu na imani yetu. Hakuna Mkristo anayedai kuwa anamuishia Mungu na huku akishindwa na kudharau kuishika Sabato, ambayo kwa kalenda za leo inaangukia siku ya Jumamosi. Tendo la kuanzilisha siku nyingine na kuifanya kuwa ni ya ibada tofauti na ile ya siku ya saba ya juma sio tu kuwa inaitia unajisi bali inakuwa ni miongoni ya ibada ya sanamu ambayo ni chukizo na ni kuyaasi mapenzi ya Mungu. Ni tendo la uasi ambao umefananishwa na dhambi ya uchawi (1Sam.15:23). Ikiunganishwa na amri ya pili ambayo inaongelea kuhusu kumuabudu Mungu peke yake hivyo kukiuka amri ya nne ni ibada ya sanamu. Tendo la kutunga kalenda nyingine ambayo inaiyumbisha kalenda halisi ya wiki kwa kuongeza siku moja mbele katika mzunguko halisi kuna endeleza maana ileile.

Amri hizi nne za mwanzo zinahusu mahusiano kati ya mwanadamu na Mungu na zinajulikana kama ni kundi la amri ya kwanza iliyo kuu isemayo kuwa:

Nawe pende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, (na kwa nguvu zako zote Mk. 12:30). Hii ndio amri iliyokuu tena ni ya kwanza (Mat. 22:37-38).

Utambulisho pekee na Mungu unasimama kwa kuzishika amri hizi na kujilinda na tendo lo lote, anamjua na kumtii Mungu ni kwa kuzishika hizi amri, na kuangalia kutozivunja.

Kwa hiyo, amri ya nne ni miongoni mwa ule mlolongo wa zile nne, ambazo ni za muhimu kwa ile amri kuu ya kwanza. Kwa hiyo, kutokana na midomo ya Yesu Kristo mwenyewe, ynaonyesha kuwa Mungu Baba mhimili na ni kipaumbele wa kwanza kabisa na ndiye wa mwisho juu ya yote mwenye kustahili kulengewa imani yetu (Mat. 22:37-38; Mk. 12:30; Ufu. 1:8). Uwenzo wa kujaliwa kumjua Mungu wa Pekee wa Kweli na Mwana wake Yesu Kristo, aliyemtuma, ni wa muhimu ili kuupata uzima wa milele (Yoh. 17:3, 1Yoh. 5:20). Kwa hiyo, amri ya nne, inajieneza hadi kuumzingira mfumo mzima wa ibada ya kibiblia wa Miandamo ya Mwezi Mpya, Sikukuu na Siku Takatifu na pia mfumo wa utoji wa zaka (tazama jarida la Utoaji wa Zaka  [161] ambao unahusiana na utaratibu wa malimbuko na Mavuno ya Agano (tazama jarida la Maagano ya Mungu [152].

Tumejionea matokeo ya Miandamo ya Mwezi Mpya kwenye kalenda ya Mungu [tazama jarida la Kalenda [156]). Miandamo ya Mwezi Mpya na Sikukuu zinaungana kuunda utaratibu wa Serikali ya Mungu. Baraza la kirabi la Sanhedrin, kwa namna hiyo hiyo moja kama Hekalu la kibinadamu na muundo wake wa kikuhuhani, vilikuwa ni kioo cha mfumo kimbinguni (Ebr. 8:5). Hata hivyo, tunayo madhabahu ambayo kwao wanaotumikia maskani au hema (au utaratibu wa kibinadamu) hawana haki ya kula (Ebr. 13:10). Kwa hiyo, hatuna mji wa kibinadamu wa kudumu bali tunautafuta mji, ambao unakuja. Kwa namna hiyo hiyo ndivyo sadaka zinachomwa nje ya mji, ndivyo ilivyokuwa pia kwa Kristo kawa alisulibiwa nje ya mji na hivyo tunatoka nje ya hema ili kupata aibu ya namna ileile ambayo yeye aliivumilia (Ebr. 13:12-13).

Kwa hiyo tunalitafuta hekalu la wapendwa ndugu zetu waliotutangulia ili kuona jinsi walivyo vumilia na kwa namna gani waliadhibiwa. Maundisho ya kanisa la kwanza yanaonakana kudumu daima yakuaminiwa kama tutajitenga na propaganda za mfumo wa makanisa ya mrengo wa tamaduni za Kirumi.

Jinsi ya kuzitendea kazi tofauti hizi katika mafundisho ya Kanisa la kwanza

Kanisa la kwanza lilikuwa kwa dhati kabisa ni la mfumo wa kuamini juu ya Mungu mmoja, yaani walikuwa ni Waunitaria. Watu wa imani ya kutumia Maarifa yaani “Wagnostiki” na wale wa mrengo wa Kimamboleo yaani “Wamodalistoki” hawakuchukuliwa kama ni sehemu ya Kanisa kwa namna yo yote ile. Hakuna ushahidi wa namna yo yote ile kuwa Kristo au mitume au wanafunzi wao waliwahi kuwa kwenye mrengo wa Wabinitaria au Watrinitaria. Kwa kweli, lakini kuna ushahidi wa wazi kuwa fundisho la Utatu wa Mungu liliendelezwa na watu waliotoka katika mrengo wa Kibinitaria (yaani wenye msimamo mkali juu ya imani ya Mungu mmoja) waliojitenga kwenye takriban karne ya nne waliojiita nao kuwa ni Wakristo. Nafasi ya Watrinitaria, na paoja na watangulizi wailioambatananao, Wabinitaria, kamwe mafundisha haya hayakupokelewa na makanisa yanayoitunza—Sabato hadi kufikia kipindi kilichojulikana kama cha Matengenezo ya kanisa, karne kumi na moja zilizofuata baadae. Kwa kweli, Wabinitaria, walitokana na Wamodalia ambao walitokana na mafundisho ya imani ya kumuabudu mungu Attis wa Roma (tazama jarida la Chimbuko la Christmas na Easter [235].

Ushahidi. Utokanao na Historia na Mateso ya Kanisa

Kanisa la Kwanza

Tunajua haya kutokana na uandishi wa Irenaeus (na mtangulizi wake Policarp) kwamba yeye na Kanisa walikuwa kwa kweli ni Waunitaria na kwamba waliamini kwamba Kristo alitumwa kuwa ni elohim na kwamba wateule walitarajiwa kuwa ni elohim kama Kristo pamoja na Mungu. Waliamini kuwa ni Mungu ndiye aliyeishi milele na kwamba hakuwa na kitu cho chote kilichokuwa sawa na yeye mwenyewe. Hii imechukuliwa kutoka kwenye Zekaria 12:8 na inapatikana ikiwa kinyume kabisa cha mafundishoya uzushi.

Irenaeus anaongelea kuhusu Mungu (katika jarida (Kupinga Mafundisho Mapotovu, III, viii, 3):

Kwa kuwa aliamuru, na vikafanyika (Zab. 33:6),

Irenaeus alishikilia kuamini kuwa:

Ilihakikishwa kiwazi kabisa kwamba hakukuwepo wala nabii au mtume aliyewahi kulitaja jina la Mungu mwingine, au kumwita [yeye] Bwana, isipokuwa ni huyu Mungu wa pekee wa kweli…. Lakini mambo yaliyoanzishwa ni kinyume na yeye aliyevianzisha, na vile vilivyoumbwa kutokana na yeye aliyeviumba. Kwa kuwa yeye mwenyewe hajaumbwa, kote kuwili ya kuwa hana mwanzo wala mwisho, na hapungukiwi na kitu cho chote. Yeye mwenyewe anajitosheleza yeye mwenyewe na zaidi sana, anaweza kuwakirimia kwa wengine wote vitu vyake hivi, huishi; lakini vitu ambavyo vimefanywa na yeye (sawa na hapo juu).

Irenaeus aliendeleza nafasi ya kuwa Mungu (theos au elohim) katika Maandishi (Logos) hapa kama ni tofauti na vitu vingine vilivyoanzishwa (ibid.). Alikuwa ameisha anzisha tayari nafasi ya Mungu na Mwana na ya wale watakaofanyika kuwa theoi au elohim na watoto wote wa Mungu kutokana na Kitabu cha III, Sura ya vi.

Kwa hiyo wala hakuwa Bwana, wala Roho Mtakatifu wala mitume, waliowahi kumuita kama Mungu, kwa nadra wala kwa makusudi, yeye ambaye hakuwa Mungu, isipokuwa ni kwa yule tu aliye ni Mungu wa wa kweli; wala hawakuwahi kumwita mtu ye yote Bwana, isipokuwa ni Mungu Baba anayetawala juu ya vyote, na Mwana wake ambaye alipokea milki kutoka kwa Baba yake juu ya viumbe wote, kama kifungu hiki kinavyoelezea: Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako [Zaburi 110:1]. Hapa [Maandiko Matakatifu] yanamuonyesha Baba akimuelezea Mwana; yeye aliyempa urithi wa mataifa wapagani, na kwamba anawatia maadui zake wote chini ya miguu yake….

Irenaeus alizidi kwenda mbali kwa kusema kuwa Roho Mtakatifu aliwataja wote wawili yaani Baba na Mwana hapa kama Bwana. Alishikilia kuamini kuwa alikuwa ni Kristo yule aliyeongea na Ibrahimu mapema kabla ya kuangamizwa kwa watu wa Sodoma na alikuwa amepokea uweza [toka kwa Mungu] wa kwenda kuwahukumu watu wa Sodoma kwa ajili ya dhambi na maovu yao yote mengine. Na kwa kifungu hiki cha uandishi wake [kama kinavyofuata chini] kusema:

Inavyotangaza ukweli ule ule: “Kiti chako cha, Mungu, ni cha milele na milele, Fimbo ya Yfalme wako ni fimbo ya adili” [Zab. 45:6]. Kwa kuwa Roho alionyesha wote wawili [kati yao] kwa jina la Mungu [theos au elohim]—wote yaani yeye aliyemtia mafuta kama Mwana na yeye aliyehusika kumtia mafuta, ambaye ni Baba. Na tena inasema: “Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; katikati ya miungu anahukumu” [Zab. 82:1]. Yeye [kwa hapa] anamaana ya Baba na Mwana na wale waliopokea uwezo wa kuitwa wana, lakini hawa ni Kanisa kwa kuwa hilo ndilo sunagogi la Mungu, ambalo Mungu—ambaye ndiye Mwana mwenyewe—amekusanyika kwa ajili yake mwenyewe ambaye tena anasema: “Mungu, Mungu BWANA, asema, ameiita nchi, Toka maawio ya jua hata machweo yake” [Zab. 50:1]. Ni nani basi anayemaanishwa na Mungu? Ni yeye ambaye alimnena akisema: “Mungu wetu atakuja wala hata nyamaza, Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote”[Zab. 50:3] ambaye, ni Mwana aliyekuja kudhihirika kwa wanadamu, aliyesema, “…nimeonekana na hao wasionitafuta…” [Isa. 65:1]. Lakini ni kwa miungu gani [anavyosema]? [Ni kwa wale] anaosema, “Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia” [Zab. 82:6]. Kwa wale, bila shaka, walioipokea neema ya kufanyika wana inasema: (…bali mlipokea roho kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani Baba; [Zab. 8:15] (kwa mujibu wa Kitabu kiitwacho kusimama kinyume na Mafundisho potovu yaani Against Heresies, Bk. III, Ch. Vi, ANF, Vol. I, pp. 419).

Hakuna wasi wasi kuwa Ireneaus alikuwa na mtazamo wa Uungu tegemezi na ambao hatimaye aliendelea hadi kufikia mahali pa kuita Mungu (kama theoi au elohim) kwa kuwajumlisha Wana na wale wengine ambao ni waliofanyika kuwa wana. Hii pengine angalau imechukuliwa kutoka katika Zekaria 12:8. Anaonekana kuashiria hapa kuwa Kristo aliwakusanya wateule, ambavyo tunafahamu kutoka kwenye Maandiko Matakatifu kuwa ni Mungu anayewatoa wateule kwa Kristo ili kwamba waweze kukusanyika (Yoh. 17:11-12; Ebr. 2:13; 9:15). Maana ya pamoja ya neno wateule wa kimwili yanaweza yasiwe sahihi kama ilivyotolewa na utendaji kazi wa Irenaeus hapa. Jeshi la Kifalme la Malaika pia hapa limejumlishwa kwenye baraza kwa mujibu wa uelewa wa isemavyo Ufunuo 4 & 5. Hawa Jeshi la kifalme pia ni sehemu ya Kanisa takatifu la Mungu.

Maeneo haya yamefanyiwa upembuzi wa kina na majarida ya Teolojia ya Mwanzo ya Uungu [127] na pia kwenye jarida la Katika Hali ya Kutokufa [165]. Ni muhimu pia kuelewa kwamba fundisho la Hali ya Roho kubakia bilakufa ilichukuliwa kama sio ya kimungu na ni fundisho lenye kuleta makufuru. Mtazamo huu ulishikiliwa na kuaminika hadi kufikia kwenye hatua ya kwamba hata ibada za Jumapili zilipoanza kuingizwa kwenye kanisa, kama ilivyofanyika kadiri ya mapema ya miaka ya 150BK, kutokana na ushahidi wa Justin Mfia dini, bado tungeweza kuona kuwa fundisho la Ungu na ufufuo yalikuwa na msimamo wake thabiti na wala hayakuyumbishwa. Kwa hiyo, Sabato ilikataliwa kabla ya mafundisho ya Uungu na ufufuo kwenye hatua ya mwanzoni kabisa. Hii ilitakiwa irudiwe tena kwenye eneo la baadae la Uungu ikitathminiwa kabla ya mahali pa mafundisho ya Sabato na ya Roho.

Anders Nygren kwenye jarida lake maarufu kama (Agape and Eros, lililotafsiriwa na Philip S. Watson, Harper Torchbooks, New York, 1969) alielewa wazo la uzima wa milele kanisani kwa pale aliposema:

Kanisa la siku za kale lilitofautiana kwenye zaidi sana kutoka kwa imani ya Wahellenia kwa imani yao kuhusu Ufufuo. Utamaduni wa Kikristo unakazia ‘Ufufuo wa miili,’ ambavyo Wateteaji wa Misimamo ya kidini yaani Waapolojistia wakipinga mafundisho haya ya Wahellenia yahusuyo ‘Hali ya Kutokufa kwa roho.’ Upingaji wa maneno ya insha hii ulikuwa macho na wamakusudi, bila kuwa na lengo lolote kiasi cha kuwa ni kinyume na roho ya Kihelenia ilivyoonekana na Wakristo wa siku za mwanzo. Mafundisho ya Kiplatoniki na Kiheleniki ya hali ya Kutokufa kwa roho ilionekana na Watetea dini kuwa kama mafundisho yasiyo ya kimungu na ni kufuru, ni ipi kati ya waliopo hapo juu wanaweza kumshambulia na kumwangamiza (Justin Dial. Lxxx. 3-4).

Kauli-mbiu yao kwa kweli inawezekana sana kuwa ni maneno ya Tatian: ‘Sio Hali ya Kutokufa, Oo Wayunani, ni roho kwa jinsi ilivyo yenyewe, lakini hali ya kufa. Tena inawezekana kwa wenyewe kuto kufa’ (Tatian Oratio ad Graecos, viii. 1).

Tofauti kati ya Wakristo na wasio Wakristo kwa jambo hili ilikuwa ni kubwa sana kwa imani ya ‘Ufufuo wa miili’ ingeweza kuwa ni kipimo kama kile cha Wayahudi cha shibboleth. Mtu anayeamini katika fundisho la ‘roho isiyokufa’ anaonekana kuwa sio ya Mkristo. Kama Justin alivyosema: ‘Kama umeangukia katikati ya wanaoitwa Wakristo…na wanaosema kuwa hakuna ufufuo wa wafu, lakini ni kwamba roho zao wanapokufa, zinachukuliwa na kupelekwa mbinguni; hawakuweza kufikirika kama walikuwa Wakristo’ (Dial. Lxxx. 4) (ibid., pp. 280-281).

Kwa hiyo Kanisa lilikataa fundisho la kuwa Roho Haifi—walikuwa kwa kweli ni Waunitaria, yaani ni watu wanaoamini juu ya Mungu mmoja tu. Hawakuwa wamelikataa tu imani ya Utatu kama ilivyokuwa imeendelea mbele, bali pengine waliweza kumtengwa mtu ye yote aliyeweza kufuata fundisho lile au ushahidi wa Ditheisia kutoka mzunguko wa Kignostiki. Kanisa lilikuwa katika uvumilivu sana, hata hivyo, ili kuwa kwenye mtazamo wa mafundisho mapotofu waliruhusiwa ili kwamba ili kuonyesha aliyekuwa ni Kanisa alikuwa na uthibitisho wa Mungu (1Kor. 11:19). Walifanya hili kwa kupitia masomo (2Tim. 2:15, ukiangalia Biblia za Kiingereza za KJV; RSV zinasema jitahidi kwa kadiri uwezavyo).

Walishikilia kuona kuwa Agano la Kale lilikuwa ndio Maandiko halisi Matakatifu na Agano Jipya lilikuwa ni Maandiko yaliyotafsiriwa kutoka kwenye Maandiko Matakatifu. Waliadhimisha Miandamo ya Mwezi Mpya na Sikukuu na tunaona kuwa Pasaka ilifikia kubishaniwa wakati wa karne ya pili, wakati mfumo wa Easter ilianzishwa na kuchukua mahala pa Pasaka kwa kile kilichojulikana kama utata wa kipindi cha nne cha robo yaani ‘Quarto-deciman’ [tazama jarida la Pasaka [098] na Mabishano ya Kipindi cha Robo [227]).

Kanisa lilianza kuteswa na iliendelea kupanuliwa nje ya Dola ya Kirumi. Kwa hiyo, ilikuwa ni nje ya upeo wa kanisa lenye msimamo wa Kihafidhina la Orthodox hadi kufikia uongofu endelevu wa Waarian walioishia kufikia karne ya nane na tangia kuanzilishwa kwa ililoitwa Dola Takatifu ya Kirumi mnamo mwaka 590. Mateso kwa ajili ya imani yaliishia katika kipindi cha wakati ambao kilizingira mamlaka na utawala wa Dola Takatifu ya Kirumi kuanzia mwaka 590 hadi 1850 [tazama jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoishika—Sabato [122]].

Vuguvugu la Wangoja Majilio ya Kristo huko Waamerika na Makanisa ya Mungu ya Marekani (USA) kwa kipindi cha zaidi ya karne mbili zilizopita walikosea kuhesabu kipindi cha tarehe za Dola Takatifu la Kirumi na cha unabii cha nyakati mbili na nusu wakati au cha siku 1,200. Makosa haya ya kuhesabu yalitokana na kukosakwao kuelewa historia ya Wazungu wa Ulaya na jitihada za kibinafsi za msisimko wa kutimiza kwa unabii huu wa uwongo.makosa haya makubwa yalileta matokeo mabaya ya unabii wa uwongo wa mwaka 1842-44 ya vuguvugu la wanamajilio. Hii ilipelekea kuanzishwa kwa fundisho jingine la uwongo lililoitwa Hukumu ya Kipindi cha Kabla ya Ujio wa Kristo [tazama Jarida la Hukumu ya Kipindi cha Kabla ya Ujio wa Kristo [176]].

 

Baraza la Mahojiano

Tunajua kutokana na ushahidi wa Baraza la Mahojiano kuwa mafundisho ya Kanisa yalikuwaje kwa hatua mbali mbali za mgawanyiko wake.

Tunaweza kueleza kwa uhakika kuwa kanisa linajulikana kwa mfumo wa Kikatoliki, lakini likiwa linaitwa kwa majina mbalimbali kwa maeneo yake mbalimbali ili kujigeuza ueneaji wake kwa maeneo mengi na kufanya muundo wake na mafundisho yake visitofautiane bali wakihakikisha kuwa vinafanana. Hata hivyo, mashirika ya Kanisa la Mungu yalikuwa na maoni tofauti kama kwa kwenye utawala wao na katika mkazo wake (kama vile Wapresbyteria na Waepiscopalia kwa upande wa Magharibi mwa Waldenses). Tunajua kuwa ilikuwa inaitwa Cathar au Cathari na hatimaye Puritan katika Uingereza (yaani English). Pia iliitwa Bulgar, Khazzar, Vallenses, Albigensian, Waldensian, Sabbatharier, Sabbatati, Insabbatati, Passaginians, miongoni mwa nyingine. Jina au Neno Sabbatharier linaonekana kuwa na maana inayounganisha watunza—Sabato wa Arian.

Tunajua kwamba kawaida ya mitazamo ilifahamika kwa ujumla wake na ilijikosoa yenyewe kwa lugha za asili. Kwa mfano, neno poor bugger katika Kiingereza ni ashirio la kawaida kuashiria hali ya huruma kwa mtu aliyefikwa na mkasa anayepitia kwenye majaribu au mateso. Hii mara nyingi imewachanganya Wamerika wa siku hizi na hata kwa Waaustralia, kama bugger na buggery yana maana halisi na yaliyo halali kutumika yanayohusiana na maana ya matendo wa kisodoma. Neno hili hata hivyo lina maana nyingine inayoonyesha maana ya wateule wakati wa Baraza la Mateso. Kamusi ya Kiingereza maarufu kama Oxford Universal Dictionary inaonyesha kuwa neno hili limetokana na Kiingereza cha Kati kutoka kwenye neno la Kifaransa bougre na la Kilatini Bulgarus au Kibulgaria au ni neno lenye makosa (au pia la kawaida sana kimatumizi). Liliaminika kuwa katika kumbukumbu za miongoni.mwa mapotofu yaliyotumika hasa hasa kwa Waalbige. Hii ilikuwa ndio maana ya kwanza. Ya pili na ambayo ni ya asili was katika kuhusiana na matendo ya kisodoma ilikuwa ni usemi uliofuatia baadae kuanzia mwaka 1555 na unaonekama kukielezea kikund cha dini kilichokuwa kinateseka kwa kipindi cha karne tatu. Usemi unaosema pauvre bougre au poor bulgar kama ulivyotumika kwa Waalbigeni ulikuja kuwa na maana ya Kiingereza booger maskini. Matumizi ya maneno kama bogle au boggle Kaskazini mwa Uingereza mnamo mwaka 1505 hayaeleweki yalikochukuliwa lakini yalikuja kuunganishwa na uzushi ambazo kwayo ni jina lililotumika kuwaita mashetani (ambaye bogiemani nk). Kwa hakika, masikini bugger lilikuwa na chanzo chake kwenye Vita vya Kidini vya Waalbige. Hata hivyo, mtu anaweza kusamehewa kwa kuuliza ni jambo gani basi Wabulga wangewafanyia Waalbige? Jibu la swali hili ni rahisi sana. Makanisa ya Mungu kutoka kwenye matawi yake ya kile kinachojulikana kama zama ya Wapergamo (Ufu. 2:12) walioitwa Wapaulicia, walikuja Ulaya wakiletwa na Constantine Capronymous na John Tsimiskes [tazama jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoishika—Sabato [122]]. Ukaazi huu mpya katika mji wa Thrace ulienea hadi huko Bulgars, upande wa Kusini mwa Slavs hususan katika Bosnia na vile vile nhini Hungary na Romania. Walienea pande za Magharibi na, kwa vipindi vya karne mbalimbali, wakiunganishwa na walosalia wakiwa ni washika Sabato waliojulikana kama Wasabatati kwa upande wa Magharibi waliitwa Wavallens au Wawaldensia. Tunaweza kusema kuwa kuna uhusiano fulani mtazamo wa mafundisho yao kuanzia katika kaene ya kumi na tatu na kwa namna fulani kwa matawi ya mashariki, hususan katika Hungary na Romania, ambako kutoka kwenye karne za kumi na tano na kumi na tisa.

Vita ya Kidini ya Waalbigeni

Mwenendo wa Vita ya Kidini ya Waalbigeni wa karne ya kumi na tatu imefafanuliwa katika jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoishika—Sabato [122]. Makundi haya bilashaka yalikuwa ni ya Washika-Sabato. Tanaa au hamu ya Kanisa Katoliki la Kirumi ya kuugeuza ukweli huu ulipelekea kwenye baadhi ya madai ya ziada kuhusiana na mabadiliko ya kilugha ya jina Sabbatati. Hata hivyo, sisi pia tunajua kuwa walikuwa ni waamini imani juu ya Nungu mmoja yaani Waunitaria. Walihesabiwa kuwa walikuwapo kabla ya mwaka 934, walipokuwa wanalalamikiwa na Atto askofu wa Vireulli kama walivyofanyiwa wenyine waliokuwapo kabla yake.

Mwanzoni waliikuwa wakiitwa Wavallense katika mwaka 1179 kwenye mashitaka yao na Raymond wa Daventry. Wazee au, barbes (yaani wajomba), kina Bernard wa Raymond na Raymond wa Baimiac walishutumiwa kama wazushi na Raymond wa Daventry mnamo mwaka 1179 mbele ya Baraza la Lateran, sio kwa ajili ya kuitunza kwao Sabato tu bali pia kwa ajili ya imani yao juu ya Mungu mmoja yaani Uunitaria. Nyaraka za matisho ziliandikwa dhidi yao mnamo mwaka 1180 na Bernard wa Fontcaude kisha akaliondoa jina la Vallenses kwenye cheo ambacho ni Adversus Vallenses et Arianos. Kwa hiyo walikuwa ni wanyenyekevu ambao hawakujitia unajisi na imani ya Utatu yaani Utrinitaria. Kazi hii ya mwaka 1180 inaonekana kuwa imetoweka katika karne hii, lakini kazi ya Liber Contra Vallenses iliyoandikwa mnamo mwaka 1190 na Bernard wa Fontcaude bado inadumu. Wavallense wa siku zile wanaonekana kuwa ni Waunitaria na wanaonekana kuwa ni watu mwenye mtazamo tofauti na Waarian. Huu ni mtazamo sahihi na ni mmoja ambao kwayo Kanisa la Mungu lilipaswa kusisitiza. Imani ya Uariani, ambayo kwa mijibu wa Wakatoliki wanadai kwa bidii zao zote kuwa ni Roho Mtakatifu kama uumbaji wa mwana, ni kitu tofauti kabisa kwa mujibu wa vile imani ya Kibiblia ya Wanaoamini Mungu mmoja yaani Waunitaria inavyosema. Wote wawili walionekana kama wako sawa, au ni mafundisho mapotofu sawa tu na ya Wakatoliki, ambao pia juenda walianzisha mafundisho ya uumbaji Roho na mwana, kana kwamba kulikuwa na kumbukumbu halisi ya jambo hili kwenye vifungu vya maandiko zikimfundisha Arius (tazama pia majarida ya Imani za Uariani na Usemi-Ariani [167] na Imani za Usociniani, Uariani na Uunitaria [185]).

Waalbigeni hawakuwa ni tawi tu la Wavallensi. Waalbigensi walikuwa na makundi mawili, Wavallense au Wawaldensia na Wakathari au Wapuritani wenyeji. Wakathari walikuwa na mtazamo tofauti dhidi ya mtazamo wa kimakosa wa imani ya wema na ubaya uliokuwa umewekewa kama msingi wa imani ya Kignostiki na Wamanichea Udualism. Tofauti iliyokuwepo miongoni mwa wengine, ilifanywa na Ray Roennfeldt kwenye insha yake iitwayo Elimu ya Kihistoria ya Wakristo wa Kikosmiki Wenye Kuamini Kote Kuwili; ya Chuo Kikuu sha Ndrews. (An Historical Study of Christian Cosmic Dualism, Andrews University) [tazama jarida la Imani ya Kulamboga pekeyake na Isemavyo Biblia, [183]]. Imani ilishambukliwa mara kadhaa na hali hii ya kuamini mambo yote mawili. Mahali ambapo Kanisa lilianzishwa, wengi wa wale walioitwa waongofu miongoni mwa utaratibu wa kitawa au umonaki mara nyingi kuliendelezwa mtazamo wa misisimko ya kikale. Wabogomi ni mfano mmoja wapo. Katika mji wa Bogomi na miongoni mwa Wabosnia, mtindo wa kujikna wa kimonaki ulitia nguvu upotovu wa imani ya waamini kuwili na walijaribu kudharau mfumo mzima wa imani. Makosa pia yalitokea kwenye matawi ya mwanzoni ya Wapaulicia. Kosa moja wapo lilikuwa ni lile la kuwa Wamelkizedeki ambao walianzisha utaratibu wa muundo mwingine ulioendelezwa kutoka kwa mtazamo wa waamini Mungu mmoja tu yaani Waunitaria. Huyu Melkizedeki aliaminika kuwa ni malaika mwombezi na Kristo ni mwombezi wa wanadamu aliyekuwa chini yake. Maandiko ya Kikatoliki yanatuama kwenye makundi haya yanayoendana sambamba kiupotofu na kuyadumisha kuaminiwa kwenye Kanisa hadi hivi leo. Wameyaimarisha mafindisho haya mapotofu kwenye Kanisa lao, huku wakiyafunika mafundisho ya kweli yasipate nguvu na kujulikana na wengi wao.

Vita yote ya kidini ya Waalbigensia ilituama dhidi ya mambo haya yote mawili na Roma kwenye karne ya kumi na tatu. Waalbigensia alikuwa na ulinzi kusini mwa Ufaransa chii ya Raymond Count wa Toulouse. Wavallense au Wasabbatati walikuwa ni wengi na waliojieneza sana, na walienea hadi kufika Uhispania. Tunaweza kuyarejesha tena mafundisho ya Wavallense kutoka kwenye matawi ya Kihispania ya Wasabbatati kwa sababu ya mateso makubwa waliyoyapata.

Baraza la Mahojiano na Hukumu la Kihispania

Baraza la Mahojiano la Kihispania lilielekezwa kama ni kuiokoa nchi na kile kilichoitwa Wakristo Wanaoeneza imani ya Kiyahudi. Walipewa jina wakiitwa Marranos (au nguruwe). Kutokana na jina la Baraza hili la Mahojiano na uthibitisho tulionao tunajua kwamba walikuwa sio tu kuwa walikuwa wanaitunza Sabato peke, lakini waliyakataa kabisa mafundisho yanayoamini juu ya miungu wengi hasa Utatu, pia walizishika Siku Takatifu zilizoamriwa ikiwemo Siku ya Upatanisho na pia waliitunza sheria ya vyakula. Sheria au Amri ya Imani inaonyesha namna ambayo kwayo upotofu ungeweza kugundulika. Wayahudi na Waislamu pia walijumlishwa na mateso haya, lakini mateso hayakuwa yamelengwa moja kwa moja kwao lakini kwa Kanisa la Mungu ambalo pia waliliita kwa majina kama vile Sabbatati, Insabbatati au Insabathi. Tangazo la amri ya Alphonse mfalme wa Aragon, nk, la kuwafukuza Wawaldensia au Wainsabbatati kutoka Hispania, kumeandikwa kwa urefu kwenye ukurasa wa 20 wa jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoishika—Sabato, [122].

Cecil Roth katika kazi yake inayoitwa Baraza la Mahojiano la Uhispania (The Spanish Inquisition, Robert Hale Ltd, London, 1937), alitoa maonyo kwenye Utangulizi akisema kwamba historia kwa kawaida hujirudia na kitabu hakikukusudiwa kufanya mzaha kwa kile kilichokuwa kikitokea Ulaya. Wanazuoni wasomi wa Kiyahudi walitaka kuendeleza Baraza hili la Mahojiano na mateso la Kihispania kwa mtindo wa mateso ya Kiyahudi. Pengine huenda jambo baya zaidi kuhusiana na mabadiliko, licha ya utimilifu wake ulio kamili, ni kazi za hivi karibuni zilizofanywa na B. Netanyahu [(Chanzo cha Baraza la Mahojiano la Uhispania katika Karne ya Kumi na tatu huko Hispania) yaani (The Origins of the Spanish Inquisition in Fifteenth Century Spain, Random House, New York, 1995)]. Netanyahu anajaribu kufuawashawishi wasomaji kuwa walengwa wa Baraza lile la Mahojiano walikuwa ni jamii ya Kiyahudi wakti hili likidhihirika kabisa kuwa sio kweli na wanazuoni wameshambulia mawazo yake kwa wazi wazi kabisa. Marabi wa wakati ule walisema bila ya kusita kabisa kuwa waliolengwa hawakuwa Wayahudi bali walikuwa ni Wakristo. Wala kawakuwa ni Wayahudi waliojifanya kuwa Wakristo. Bali walikuwa kwa kweli ni Kanisa la Mungu Idadi ya Mabaraza ya Mahakama kwenye zilizokuwa zinaitwa Ofisi Takatifu katika Uhispania yalifikia idadi ya kumi na tano. Yalidumu yakiwa na kila kitu muhimu katika kuendesha shughuli za kiofisi kamilifu kabisa na vifaa vyake vyote katika miji ya Barcelona, Cordova, Cuenca, Granada, Llerana, Logrono, Madrid, Murcia, Santiago, Seville, Toledo, Valencia, Valladolid na Sargossa. Miji mingine ni katika Visiwa vya Balearic ziliwekwa huko Palma na Majorca.

Maeneo yaliyokuwa ni ya hatari na yenye kutisha zaidi yaliyokuwa yanatekeleza sana na kazi hii yalikuwa ni Madrid, Seville na Toledo kwa sababu ya idadi kubwa ya Wakristo Wapya (kama Roth alivyowaelezea), na matendo makubwa sana katika Mji wa Kale ulijulikana kama Old Castille na Andalusia, na ilikomeshwa baada ya mlipuko wa kwanza wa kiwenda wazimu ulioipunguza katika Catalonia (Roth, ibid., Ch. The Unholy Office, p. 73). Ilikuwa hatimaye ilihusishwas na mwishoni mwa karne ya kumi na tano chini ya mamlaka ya baraza la katikati lililojulikana kwa lugha ya Kihipaniola kama El Consejo de la Suprema y General Inquisición lililochukuliwa kwenye lile la La Suprema, ambalo mwanzoni lilihusiana na lile la Castille. Likiwa na Mabaraza makuu manne ya Serikali chini ya mamlaka ya Ferdinand na Isabella, yakiitwa Mabaraza ya Serikali, ya Fedha ya Castille na ya Aragon, Baraza la Mahojiano lilichukua hatamu zake kwa namna iliyokuwa isiyo na maana ya moja kwa moja ya kutenga kazi kwake kama kwa nguvu za kifalme (tazama jarida la Roth, ibid., p. 74). Mnamo mwaka 1647 iliamriwa kuwa hukumu zote za mabaraza ya mahakama ziweze kupelekwa kwake ili kwa uangalizi au usimamizi. Hii inaonekana ni kuweza kusimamia kabisa makamio yasiyoelezeka kiwango chake ya mateso yaliyofanywa kienyeji. Hali hii mbaya kabisa na yakutisha ilisimamiwa na msingi wa kimakosa ya kiuelewa ya Netanyahu iliyopelekea kwenye kosa [Kitabu cha Chanzo cha Baraza la Mahojiano la Kihispania Katika Karne ya Kumi na Tano Uhispania) Yaani (The Origins of the Spanish Inquisition in Fifteenth Century Spain, pp. 440-459)] ambako makosa yote ya kimawazo yalihukumiwa kama mafundisho potofu kinyume na matamko ya Augustine yanayosema: Mimi naweza kukosea lakini bado mimi nisiwe mkosaji (kwa mujibu wa jarida la De Trinitate, c, 3, n. 5-6). Juan de Torquemada, aliyekuwa Hakimu katika Mabaraza haya, alishambulia jaribio la Toledan kwa sababu ya muonekano wao usio wa kawaida na kuruhusu kwao imani isiyokuwa ya Kibiblia ya kupinga imani ya Usemitiki. Aliuona mtazamo huo kama kuwa kwenye usawa mmoja kama ule wa Hamani dhidi ya Mordekai na Wayahudi (ibid., p. 449). Kwa hiyo alikuwa akikabiliana na tatizo la asili ya Mungu kama ulivyoonwa na Wavallense. Watoleda walisema, kama ilivyokuwa ni dhahiri kwa sehemu nyingine, ni suala la elimu ya watu wote (publica fama) (na pia katika Valencia kama tutakavyoona hapo mbele kuwa wazushi Walifanya tohara, huku wakikataa ukweli kuhusu nafasi ya Kristo kwa mambo ya mbinguni, na kwa kuongezea hapo uwepo wa Mwili wake kwenye Ekaristi, nk. (ibid., p. 444). Watoledani hawakuonyesha, kwa mujibu wa Torquemada, kwamba waongofu hawakuonyeshwa iwe kwa hiyari yake mwenyewe ya ukiri au kwa kwa mashauri ya mashahidi ya watu wasio na hatia au makosa, kama ilivyowahi kusemekana, kuwa baada ya kuupokea ubatizo, kwamba aliamin kila kitu isipokuwa kile kilicho aminiwa na Kanisa Mama lenyewe (tazama kitabu cha Netanyahu, p. 444). Torquemada ayaona mashitaka haya kama ni shutuma za uwongo na zinajidhihirisha zenyewe kuwa ni utanguzi wa majaribio yote (ibid., p. 445). Kwa nini mambo haya yawe hivyo? Tunajua bila ya shaka yo yote kwamba Wavallense waliamini imani ya Uunitaria kwa kipindi cha karne kadhaa. Tofauti ilituama kwenye usaidizi wa mamlaka ya mbinguni wa Kristo. Kwa hiyo, hali ya kuwa na mamlaka ya limbinguni ya Kristo haikupingwa. Lakini kulikuweko na kitu kingine zaidi nyuma yake pale. Torquemada aliona kuwa majaribio ya Watoledani walikuwa ni wapinga Usemitiki na kwamba hakukuwa na msingi wa kibiblia wa kuendekeza hali hii ya ubora wa vyeo. Kwa hiyo, alilazimika kukana kosa hili kwa kutumia lugha kali sana kadiri alivyoweza. Pia tatizo lilituama kwenye ukweli kwamba hali ya tuhuma na mahojiano yaliendelea hadi kwenye kizazi cha nne cha waongofu. Aliipinga dhana hii kutokana na mtazamo wa waongofu wa mambo mengine ya wapinga imani ya Waamini Utatu yaani Watrinitaria, ambao tumeelezea kama makosa ya Wamanichea wakiwemo Wabosnia. Alikabiliana na tatizo la uongofu uaminifu ndani ya Dola Takatifu ya Kirumi.

Torquemada anasema:

Kwa wakati wetu wenyewe walikuwepo walioongoka kutoka kwenye imani za kipagani wakaja kwenye Ukristo mfalme aliyeonyesha mfano wa Poland, baba wa mfalme aliyeko madarakani na idadi kubwa ya watu kutoka kwenye jamii ya kifalme na umati usiohesabika wa watu [Wladislaw II, ambaye zamani aliitwa Jagiello, Grand Duke wa Lithuania, ameongoka wakati alipofanywa kuwa mfalme mwaka 1386. Alikuwa ni baba wa Casimir IV aliyeinukia kuchukua kiti cha enzi cha umfalme mwaka 1447]. Baadae, katika siku za mamlaka ya Papa Eugene IV, mfalme wa Bosnia, Malkia wake, na watu wengine wengi miongoni mwa walio katika jamii ya kifalme waliongoka na kuingia kwenye Ukristo kutoka kwenye imani yenye mapotofu ya  Umanichea [mfalme Stephanus Thomas aliongoka na kuingia imani ya Kikatoliki mnamo mwaka 1445]. Kwa kuongezea hapo, karibu kila tiku wafuasi wengi wa dini ya Kislamu maarufu kwa jina la umma wa Mahommad wanashawishika kuingia [kwenye ukweli wa Wakristo]. Ingekuwa ni tuhuma kubwa sana na matumizi mabaya yasiyovumilika ya vitu vitakatifu kusema kuwa watu hawa wote wangeweza kutuhumiwa, hadi kufikia karibu kizazi cha nne, ya ibada za sanamu na makosa ambazo wao na baba zao waliyashikilia kwa wakati Fulani  (Tractatus, pp. 54-55; cf. Netanyahu, p. 452).

Torquemada aliandika kipeperushi dhidi ya Wabosnia na imani ya Wabogomilia ambacho ni cha (Symbolum pro imformatione Manichaeorum, ed. N Lopez Martinez and V Proano Gil, 1958, p. 23, n. 68 and Netanyahu, n. 119). Hapa tunaona matokeo ya michanganyiko yenye kuingiliana ya Wamanichea wenye kuamini mambo mawili ambako Wapaulicia walianzisha imani ya kuamini Mungu mmoja wa pekee yaani Uunitaria. Kanisa kwa wakati huu lililazimishwa kwenda Herzegovina na kwa upande wa kaskazini [pia tazama jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoishika—Sabato [122]). Tatizo liko dhahiri, lakini sio kwa Netanyahu. Kipindi cha karne ya kumi na tano Wavallense walikuwa wamesukumiwa kwenda mbali sana kwa mtindo wa chini kwa chini jambo ambalo lilikuwa ni kwa wote lakini kwa muonekano walikomeshwa kwa njia ya mateso. Watoledani miongoni mwa wengine walifikia bora sana na wenye kutisha ambao walikuwa wanalitumia Baraza lile la Mahojiano ili kuiokomesha imani ya Kisemitiki kwa utaratibu uliopangiliwa kwa hila. Hii ilipunguza uwezo wa utendaji kazi wa kanisa kwa kuimarisha nguvu ya dola. Torquemada alikabiliwa na kuwadhibiti mianya hiyo ili kwamba baadhi ya maingiliano imara ndani ya dola yangeweza kuathirika, na uongofu ungeonekana kuwapatia faida wale waliolengwa waweze kuongoka. Ujamaa na ufahamu wa Baraza la Mahojiano walikuwa wanatumia carrot hii na, hivyo upanuzi wa kutia hatarini. Torquemada alikuwa mjanja kiasi cha kutosha kujua namna hukumu ya historia au mlolongo wa kesi itakavyokuwa. Kwa hiyo alilazimika kulitawala Baraza hili la Mahojiano, au mahakama. Kwenye tukio, kanisa liliruhusu jambo hili liendelee kwa kipindi kingine cha karne tatu dhidi ya mchakato ule ule na mafundisho ambayo kuwepo kwake kulikataliwa yaani hakukuruhusiwa, na kuharibiwa kabisa nguvu zake yenyewe [tazama jarida la Malachi Martin liitwalo Kufifia na Kuanguka kwa Kanisa la Kirumi] yaani (Decline and Fall of the Roman Church, Secker and Warburg, London, pp. 254 ff.).

Ushahidi kutokana na Kanuni ya Imani

Katika kuanzisha kwa eneo la kuweka Baraza la Mahojiano, utaratibu wa Kisheria ulifuatia. Baada ya Sheria ya Neema ikiwa imeisha chapishwa ili kuwatia moyo wazushi waje mbele na kukiri, kwa kawaida ilichukua kiasi cha takriban siku thelathini au arobaini (kwa mujibu wa Roth, p. 75), kisha Mahojiano yatachukua nafasi yake. Hii ilifanyika kwa mlolongo endelevu wa kutia hatiani. Awamu inayofuatia ilikuwa ni tangazo la kila muhula la Kanuni ya Imani, ambayo ilisaidia kutambua aina au dalili ya mafundisho potofu yaliyotakiwa kupigwa marufuku. Utaratibu wa Ukiri ndio ulilazimisha uovu huu.

Ukiri wa Imani ilianzishwa mnamo huko Valencia mwaka 1519 na Andres de Palacio, aliyekuwa Jaji wa Valencia, na umeandikwa na Roth. Unaweza kuonekana kutoka kwenye Kanuni ya Imani kuwa, kulikuweko na mlolongo mkubwa mambo ya kweli na viinimacho yalioorodheshwa ambayo yaliezea makundi matatu ya watu. Wa kwanza walikuwa ni Wakristo waliokuwa wanashikilia kile kinachoitwa kama kasumba ya Kiyahudi. Kundi la pili lilikuwa ni la Wayahudi wenyewe na kundi la tatu lilikuwa ni la Waislamu. Ilikuwa ni dhahiri kutokana na Kanuni ya imani ndipo mafundisho potofu yaliweza kujipenyeza kanisani kama neno lililonenwa juu ya Ekarist lilijulikana rasmi kama ni alama kwenye Kanuni ya imani. Pia Msalaba, au Ishara ya Msalaba, havikuwa vikitumiwa na Wasabbatati. Kutokana na kupimwa kwa kujaribiwa kwa njia ya Kanuni ya Imani inaonekana kuwa kundi hili lilikataa mafundisho yanayosema kuwa Roho itaendelea kudumu bila kufa, na pia mafundisho ya kwenda Mbinguni na Jehanamu. Waliishika au kuitunza Sabato kuanzia machweo ya jua siku ya Ijumaa hadi machweo mengine ya jua ya siku ya Jumamosi; hakukufanyika kazi yo yote siku hizi za Sabato. Walisherehekea Sikukuu ya Mikate isiyotiwa Chachu na Pasaka na mboga za uchungu. Walifunga saumu siku ya Upatanisho (kwa mujibu wa Roth, pp. 77 ff).

Mtazamo wa jumla na utunzaji wa Wayahudi ulijumlisha kwenye orodha kama unavyoonyeshwa kwenye Kanuni ya imani ili kwamba mfumo ulikuwa unaendeshwa pamoja na ili kuifanya iwe ni vigumu kuitambua kikamilifu tofauti iliyoko kati yao. Walishika sheria ya vyakula na pia kuzika wafu wao kwa mujibu wa desturi ya Kitahudi. Sehemu kubwa ya Kanuni ya imani, inahusisha tabia za kishirikina za uchawi wa kimadhehebu ya kidini (mfano ni kama ilivyoainishwa kwenye ukurasa wa 78). Walikataa imani ya Mariolatry na hii iliunganishwa na imani ya Kiyahudi ya kumkataa Masihi.

Fundisho la Mnyumbulisho la kiini lilikataliwa kama ilivyokuwa katika muundo wa Katoliki wa mafundisho ya Uwepo wa kila Mahali, ambayo ilitokana na mafundisho ya Kiplatoniki na Uanimism (tazama ukurasa wa 78). Makuhani walionekana kushiriki na walifahamika kutokana na kujitakasa na kujitenga kwao. Wakrsto walionekana walikuwa wanavaa kama Wayahudi wakizishika sheria zinazosimamia uvaaji wa mavazi (tazama ukurasa wa 79). Walikutanika kwenye makanisa ya nyumbani na walisoma Biblia na kuhubiriwa au kutafsiriwa kwa lugha zao za kienyeji. Mali za wazushi zilitaifishwa na hii bila shaka ilisaidia kuongeza wivu au bidi ya Majaji wa lile Baraza la Mhojiano na Hukumu.

Roth anaorodhesha kufunguliwa kwa Ofisi mjini Lisbon kabla haijafanywa kuwa ni Jumba la Michezo ya Kuigiza. Wajibu wa mashahidi waliojionea kwa macho yao wenyewe (ililochapishwa kwenye Jarida la Msajili la Kila Mwaka  wa 1821) linaonyesha bilashaka kabisa, kwamba walikuweko wwanadamu waliosalia ambao walipatikana kwenye tundu la simba, ambao walikuwa wakitumiwa (kutoka kwenye uandishi kuhusu kuta za tundu la simba) kwa baada ya mwaka 1809. Hii ilihusisha watawa—wamonaki ambao nguo zao zilikutwa pamoja na wanadamu na masalia mengine yakiwa yamelala kwenye tabaka la tundu hizi na pamoja na ushahidi wa mauaji yote mawili yaani ya zamani na ya hivi karibuni, yakiwa yamewekwa pale (tazama Roth, kurasa za 84-85).

Kipindi cha nafasi ya kati ya miaka mitatu na mine cha kati ya utiwaji mbaroni hadi kuhukumiwa waliwekwa mahali pa kawaida na kwa shitaka moja linalokumbukwa lilichukua kiasi cha kuchukua miaka kumi na nne. Wanawake wenye mimba au wajawazito waliburuzwa kwenye miti ya kutesea na kudhalilishwa na wafungwa, au pengine kugonganishwa na wao, ilimlazimu Kardinali Ximenes mnamo mwaka 1512 kutishia kuwaua ofisa ye yote atakayekutwa amechukua kitu chochote cha hila na mfungwa wake atakaye kutwa naye. Gharama za ufungwaji gerezani zilichukuliwa na mtuhumiwa haijalishi kama itachukua muda gani. Mfano mmoja wa gharama hizo ulitokea katka ufungwaji wa miaka mine mtawa mmoja katika mji wa Sicily, alifungwa na kuachiliwa mnamo mwaka 1703, alikuwa bado analipiwa na warithi wake hadi mwisho wa mwaka 1872 (tazama jarida la Roth, ukurasa wa 87). Kwa kawaida, rasilimali zilikuwa zikitaifishwa wakati ule mtu alipokuwa anatiwa mbaroni.

Marranos au Wakristo Wapya walikuwa hawakubaliki kuwa mashahidi kwenye hatua yo yote ile ya mahojiano. Tendo la kuficha majina ya mashahidi lilianzisha katika karne ya kumi na tatu nia hasa ulkuwa ni kuwalinda wanyonge dhidi ya wenyenguvu walioshitakiwa lakini nii ilikuwa ni desturi na hakuna aliyeweza kukuta majina ya washitaki wao (Roth anaonyesha kwa uangalifu mkubwa sana kwamba hata kufikia mwaka 1836 nchini Uingereza iliwashitaki wakosaji ambao hawakuwa na shauri au kuona nakala za ushushuda baada ya kiapo uliofanywa dhidi yao). Nyakati zenyewe tu zilikuwa ni za kishenzi na Mabaraza haya ya Kimahakama yalijaa ushenzi uzidio.

Mabaraza ya Mahojiano ya Ulaya yalianza kuanzia kusini mwa Ufaransa katika marne ya kumi na tatu na kuishia kwenye Himaya ya Kipapa mnamo mwaka 1846. Kati ya miaka ya 1823 na 1846, watu 200,000 kwenye Himaya ya Kipapa peke yake walihukumiwa kifo, vifungo vya maisha, kupelekwa uhamishoni au ,ashimoni, pamoja na wengine milioni 1.5 waliwekwa chini ya uangalizi mkali [(tazama jarida la Malachi Martin la Kufifia na Kuanguka kwa Kanisa la Kirumi)  yaani (The Decline and Fall of the Roman Church, p. 254 na jarida la Mgawanyo wa Jumla wa Makanisa yanayoishika—Sabato [122], ukurasa wa 29 kwa ajili ya nukuu)]. Roth alinukuu hali ya kuvunjika moyo ya kila mtu binafsi yake kuanzia ilipoanzishwa katika karne ya kumi na tatu kusini mwa Ufaransa.

Nisikilizeni mabwana zanguni! Mimi sio mzushi; kwakuwa ninaye mke na naishi naye kwa upendo mkubwa na tuna watoto, na nakula nyama na kulala na kuapa na mimi ni Mkristo mwaminifu (utasoma haya kwenye Roth, ukurasa wa 90).

Ukanushaji huu wa mambo ya maisha ya useja na imani kali ya kula mboga peke yake ulikuwa ni wa lazima kwa sababu Wamanichaea wenye kuamini mambo mawili waliojulikana  kama Wakathari au Wapuritia, waliotafuta utakaso kwa kutumia misimamo mikali ya kiimani, walikuwa ni wafuasi wa dizi zenye kuamini mafundisho ya kiuzushi ambao hatimaye waliwababisha mateso kwa Wavallense au Wasabbatati. Wamanichaea wenye kutanga tanha walitofautiana na Wavallense na hii ndiyo tofauti ya Wakathari mchanganyiko na Wavallense uliojulikana lakini ilikuwa sio sahihi kama ilivyo kuja kugundulika na Weber. Sheria za Kibiblia zilikuwa ni kishika Sabato kwa wakati wote. Ibada zao zilifanyika kwa siri na hivyo ilikuwa ni vigumu kuzigundua bila kukosea. Kwa vyovyote, tunajua kuwa walishika Sabato na kiwango chao cha juu cha kufanya ibada kinajulikana kutoka matawi ya mashariki ya Wasabbatati.

Wasabbatati wa Mashariki ya Ulaya

Tunajua kwa uhakika kabisa jinsi mafundisho ya makanisa ya Wahungari na Watransylvania yalivyokuwa kutoka kwenye karne ya kumi na tisa. Habari zake zilihifadhiwa na Dr Samuel Kohn, Mkuu wa baraza la Marabi la Budapest, Hungary katika jarida lake la DIE SABBATHARIER IN SIEBENBURGEN Ihre Geschicte, Literatur, und Dogmatik, Budapest, Verlag von Singer & Wolfer, 1894, Leipzig, Verlag von Franz Wagner. Hatua hizi zimeorodheshwa kwenye jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoishika—Sabato (Na. 122) katika ukurasa wa 22.). utaratibu wake wote umeorodheshwa kwenye kitabu cha Wasabato wa Transylvania, cha Samuel Kohn, kilichotafsiriwa na T. McElwain na B. Rook, na kuhaririwa na W. Cox, CCG Publishing, USA 1998.

Tunajua kwa uhakika kwamba tawi hili la Wavallense au Wasabbatati walikuwa ni Waunitaria pamoja na Frances David au Davidis aliyefia gerezani mwaka 1579. Kohn ansema kuwa walirejesha Ukristo wa kwanza (Kohn, uk. 8). Kanisa la Waunitaria lilichanganyikiwa kati ya waabudu Jumapili na watunza Sabato mnamo mwaka 1579. Matawi ya Sabato yakiwa chini ya Eossi yalikuwa ni maaminifu zaidi kwenye kweli.

  1. Waliendeleza ubatizo wa watu wazima.
  2. Waliitunza Sabato na Siku Takatufu, zikiwemo Sikukuu ya Pasaka na Mikate isiyotiwa Chachu, Pentekoste, Upatanisho, Sikukuu ya Vibanda na ya Siku ya Mwisho Iliyokuu na Miandamo ya Mwezi Mpya. Sikukuu ya Baragumu haikuorodheshwa kwa kutenganishwa kwenye vitabu vya nyimbo na inaonekana kuwa ilisgerehekewa kwenye nyimbo za Miandamo ya Mwezi Mpya.
  3. Mafundisho yao yalizungukia kwenye kipindi cha miaka 1,000 ya utawala wa Milenia mwanzoni mwa kipindi ambacho Kristo atarudi na kuwakusanya tena Yuda na Israeli.
  4. Waliitumia kalenda ya Mungu iliyotuama kwenye Miandamo ya Mwezi Mpya.
  5. Walifundisha kuhusu aima mbili za ufufuo, mmoja ni wa uzima wa milele utakaotokea wakati wa kurudi kwake Kristo na wapili ni ule wa hukumu utakaofanyika mwishoni mwa kipindi cha Milenia.
  6. Walifundisha kuhusu wokovu unaopatikana kwa neema na ambao bado lakini sheria ni za muhimu na zinahitajika kuzishika.
  7. Waliamini kuwa Mungu huwaita watu na yakwamba dunia kwa ujumla imepofushwa.
  8. Fundisho lao kuhusu Kristo ilikuwa kabisa imetuama kwenye mrengo wa waamini Mungu mmoja tu yaani Waunitaria.

(haya waweza kuyaona kwenye jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoishika—Sabato [122], uk. 22.

Kwa hiyo, inaweza kuonekana sasa kwamba Kanisa la kwanza la watunza Sabato walikuwa ni Waunitaria, waliozishika sheria za Agano la Kale. Sabato ilikuwa ni alama ya utaratibu wa mfumo wa imani yao, ambayo ilielekeza kwenye ibada yao kwa Mungu wa Pekee wa Kweli. Waliteswa huko Ulaya ya Mashariki kwa ajili ya kuamini kwao imani ya Uunitaria zaidi kuliko kuitunza kwao—Sabato (Francis Davidis alichagua kubakia gerezani, ambako alifia, kuliko kuchangamana na imani ya Waunitaria, hata kama Socinus, mwenyewe M-Unitaria, alijaribu kumshawishi kulegeza ugumu wa moyo wake wa imani ya Unitaria ili kuyaokoa maisha yake). Walikataliwa kwenye muundo wa kinyadhifa za kanisa wakati hata Wayahudi waliiga aina ile ya utaratibu wa kinyadhifa. Walikataliwa kupewa nafasi ya kwenye vyombo vya habari na kwa hiyo kusababisha jumbe zao za kimahubiri kuchapishwa kwa mikono kwenye mnyororo wa mzunguko wa barua. Baraza la Mahakama ya Mahojiano lilikuwa halina huruma katika kukomesha kwake mfumo huu na, kwa upande wa magharibi, watunza—Sabato peke yao ilitosha kuwatesa na kuwakomesha.

Kukua kwa Imani ya Waunitaria, wanaoamini Mungu kuwa ni Mmoja

Pamoja na Matengenezo, imani ya Unitaria ilianza kukua na ilikuwa haikujulikana kwa moja kwa moja kwenye watunza—Sabato. Kwa maneno mengine, nikusema kuwa sio Waunitaria wote walikuwa ni wshirika wa kweliwa Makanisa ya Mungu kama ilivyo kuwa sio Watunza—Sabbath wote walikuwa ni washirika wa kweli wa Makanisa haya.

Jina la Unitarianism linatokana na neno la Kiingereza linalotokana na lugha ya Kilatini unitarius na ilitumika kwa mara ya kwanza na dhehebu lililopata uhalali katika mwaka wa 1600 (hili waweza kuliona kwenye kitabu cha maarifa cha Encyclopedia of Religion and Ethics (ERE), art. Unitarianism, Vol. 12, uk. 519). Hasa hasa lilianzishwa kwa mtazamo wa mwonekano wa umbo la Kuungu wenye umoja, tufauti kabisa na mafundisho ya kihafidhina ya asili yake ya kujigawa kwa sehemu tatu. Neno linaloendana na maana ya imani ya Utatu lilikuwa kwanza lilitumika kwa mtazamo wa kisasa na Servetus mnamo mwaka 1546 (ibid.). Neno Unitarian wakati mwingine limechukuliwa kwa kiwango kilicho zaidi ya Ukrisato (kwa mfano Uislamu na dini ya Kiyahudi pia wao wana msimamo wa mrengo wa Kiunitaria katika misingi yao).

Maandiko ya Kiyunani ta Agano Jipya yalichapishwa na Erasmus (mwaka 1516).

Urukwaji wa sura maarufu za imani ya Kitrinitaria, [kama vile 1Yoh. 5:7], na kuchukiwa kwake na mtindo wake wa kisomi wa mabishano yaliendeleza athari iliyoonekana kwenye mawazo ya wengi (ERE, ibid.).

Utolewaji wa Agano Jipya na Erasmus ulilita msukumo kwa watu waliobobea kwenye lugha ya Kiyunani kuanza kutathimini namna ambayo Watrinitaria wahafidhina walikuwa wameanzisha. Kitu muhimu sana zaidi, ni kwamba, watu wa Ulaya walikuwa huru kuwa wawazi zaidi na Baraza lile la Mahakama ya Mahojiano lilidhibitiwa. Wanazuoni wasomi walianza kuona kuwa Biblia ilikuwa haifunshi wala kuunga mkono aina yo yote ya Utatu na kuwa kwa kweli iliunga mkono mafundisho au msimamo wa wale wanaomwamini Mungu kuwa hana mshirika yaani imani ya Kiunitaria. Hatua ya kwanza ilikuwa ni uchapishaji wa jarida la kawaida lililokuwa linapinga imani na kwazi Utatu kwennye lile Bara lao (kama ilivyopingwa kwenye mafundisho ya makanisa kwanza wakati wa Matengenezo na mashine za kutolea chapa) kama ilivyokutwa kwenye kazi za Martin Cellarius (1499-1564), mwanazuoni wa Reuchlin na mfuasi wa kwanza na rafiki wa Luther (utayapata kwenye ERE, ibid., pp. 519-520). Kwenye kazi yake iliyoitwa de Operibus Dei alitumia neno deus wa Kristo kwa maana ile ile ambayo kwayo Wakristo pia wangeweza kuitwa dei kama ‘wana wa yeye Aliye Juu sana’ (ibid.). Kwa mujibu wa Kumbukumbu za jarida la Teolojia ya Mwanzo ya Uungu [127] itaonyesha kuwa wazo hili lilichukuliwa moja kwa moja kutoka kwa Irenaeus na wanafunzi wa kwanza na mitume wenyewe. Hii ilisababisha majongeleano na jumuia za kisasa za kimasomo zijiingize kwenye majadiliano kufuatana na kazi za Servitus mnamo mwaka wa 1531. Huko Naples, Mhispania John Valdes alianza kundi la kidini kwa ajili ya usomaji wa Maandiko Matakatifu hadi kufa kwake mwaka 1541 (hebu soma ERE, ibid., uk. 520). Kumbuka hapa jina la Valdes. Mtu huyu anaonekana kuwa alikuwa ni Muhispania Mwaldensia kutokana na jina lake na teolojia yake [tazama jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoishika—Sabato [122]]. Mnamo mwaka 1539, Melancthon walimuonya Venetian Seneta wa Waservetia wote wa Kaskazini mwa Italia (ibid.). Kutokana na kundi hili, Bernard Ochino (1487-1565) wa Siena alipita kwa taratibu sana kwa kupitia Uswizi hadi London na akatumika kama mojawapo wa Kanisa la Wageni mwaka (1550-1553) hadi lilipovunjwa na Malkia Mary katika jaribio lake la kuurudisha Ukatoliki. Ochino alifukuziliwa mbali aende Zurich na akakimbilia Poland akajiunga na waliokuwa wanapinga wanaoamini na kufundishwa mafundisho ya Utatu wa kule. Catherine Vogel, mke wa sonara alikuwa ameuawa kwa kuchomwa moto akiwa na umri wa miaka takriban 80 mwaka 1539 huko Cracow kwa ajili tu ya kuamini ‘mafundisho ya kuwepo kwa Mungu ni mmoja tu na hana mshirika, na ambaye ni muumbaji wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana katika dunia, na ambaye asiyeweza kufikirika na kupatikana jibu la jinsi alivyo na wenye hekima wawao wote’ (ibid.). Vuguvugu hili ni kazi ya Ulaya wakati wa majira tunazoziita kama zama za Wathiatira. Vuguvugu la wapinga—Utatu linaonekana pia kwenye sinodi ya pili ya Kanisa la Matengenezo (yaani reformed Church) kunako mwaka 1556 na, mwaka 1558, na Piedmontese George Blandrata akawa ni kiongozi wake. Makanisa ya Kibaptist yaliyokuwa yanaitwa The Dutch Anabaptists pia yalikuwa ni ya imani ya Kiunitaria yakiwa chini ya uongozi wa David Joris wa Delft (mnamo miaka ya 1501-1556). Waunitaria hawa pia kwa sehemu nyingine waliitwa ni Waprotestant. Jarida la ERE linasema kwamba:

Maelfu ya Waprotestant kutoka Ujerumani, Alsace na Nchi za Ukanda wa Chini, waliingia Uingereza siku za utawala wa mfalme Henry VIII, na Kanisa la Wageni chni ya Edward VI pia ndani yake lilikuwa na Wafaransa, Walloons, Wataliano, na Wahispania (soma ERE, ibid., uk. 520).

Watu walitafuta kukimbilia Uingereza kwa msaada wa Kanisa la Waunitarian hapa. Hili lilikuwa ndilo Kanisa la kweli la Mungu. Uingereza ilikuwa iko wazi zaidi katika kuruhusu watu kueleza maoni yao kiuwazi wazi kuanzia karne ya kumi na tano kwa mujibu wa machapisho ya Richard Peacock, askofu wa Chichester. Walollard na Wa-Anabaptist walijificha na kukwepa kwa wakati ule.

Mnamo tarehe 28 Decemba 1548 padri mmoja waliyitwa John Assheton alikula kiapo cha kukana mbele ya Cranmer ‘uzushi unaostahili hukumu ya milele’ kuwa Roho Mtakatifu kwa kusema kuwa‘Roho Mtakatifu sio Mungu, bali ni nguvu Fulani tu za Baba,’ na ‘Yesu Kristo kwamba aliyetungwa mimba yake na Bikira Mariamu hakuwa nabii ... bali hakuwa ni yule Mungu wapekee na wakweli aishiye’. Kwenye mwezi wa Aprili iliyofuatia agizo lilitolewa la kutafuta Wa-Anabaptist, mafundisho yao ya uzushi, au tasbihi zao za Kufanyia Maombi. Idadi kubwa ya wafanyabiashara wa mjini London waliletwa mbele ya baraza hili mwezi wa Mei (soma ERE, ibid.).

Walikuwa ni Waunitarian. Haukuwa Ubinitaria wala Uditheism uliohakikishwa wakati wa kipindi hiki ch awamu Kanisa kwa kupitia mateso yake. Hayakuwa mi mafundisho. Sajenti George van Parris wa Mainz aliuawa mwaka 1551 kwa kusema kwake kuwa Mungu Baba alikuwa ndiye Mungu peke yake na kuwa Kristo hakuwa ni Mungu kwa namna yo yote ile (tazama ERE, op. cit.). Vuguvugu la Waunitaria nchini Poland wakati Blandrata alipofika kule mwaka 1558 ilikuwa tayari sinodi ya Kiprotestant lakini kulihesabiwa miaka saba iliyofuata baadae. Walikataa kuitwa jina lingine lo lote isipokuwa la kuwa wao ni Wakrista (soma ERE, ibid.). Faustus Socinus mnamo mwaka (1539-1604), mpwa wa Lelius Socinus (miaka ya 1525-1562) wa Siena aliyekuwa rafiki wa Calvin na Melancthon, alitmbelea Uingereza na alisafiri hadi Poland. Alitembelea Blandrata huko Transylvania mwaka 1578 akibishana dhidi ya Francis David aliyekataa aina zote za maumbo ya kitu cho chote kukifananisha au kufanya kielelezo kwa ajili ya Kristo. Aliishi huko Poland mwaka 1579. Jina la Wasocinia lilitokana na yeye. Hata hivyo, walimtangulia pale kuwa ni sehemu ya Kanisa tumjuavyo kama Waldensia. [Habari hii imafanyiwa upembuzi kwenye jarida letu la Usociniani, Uariani na Uunitariani [185]].

Kanisa la Waunitariani la Polandi liliteswa ili lipate kuzimwa na Kanisa la Kikatoliki (tazama ERE, op. cit.). Socinus alikiri matumizi ya neno Mungu kwa Kristo kwa maana ya kuwa ni wa chini. Kwa kweli, mtazamo huu ndio ulitumika na Irenaeus kama tunavyoona kwenye jarida la Theolojia ya Mwanzoni ya Uungu [127].

Francis David (au Davidis) wa Kanisa la Wahungari katika Transylvania alifungwa gerezani kwenye gereza la Deva kwa kosa la kukataa kuomba, au kufanya taswira yo yote inayo fanana na Kristo. Alifia humo mwezi Novemba 1579. tunalijua hilo kwa kupitia historia iliyohifadhiwa ya wafuasi wake, kutoka Eossi na kuendelea, kwamba walikuwa sio kwamba tu ni Waunitariani buli pia walizishika Sabato, Miandamo ya Mwezi Mpya na Siku Takatifu. Sikukuu ya Baragumu ilisherehekewa kwa kuimba nyimbo za tenzi kama ilivyokuwa kwa Mwandamo wa Mwezi Mpya ilizidi sana kuliko ile ya tenzi maalumu za Baragumu kama sikukuu. [tazama jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoishika—Sabato [122]].

Jina la Unitarius lilitumika kwanza kama neno na Melius na kwanza lilitojikeza kwenye makabrasha ya cheti cha shahada cha Sinodi ya Lecsfalva mnamo mwaka 1600. Hatimaye ikachukuliwa na Kanisa mwaka 1638. Makanisa ya Wahungari yaliteswa kwa kipindi cha karne mbili baada ya hiki na mali zao zilitaifishwa. Mwanzoni mwa karne hii wazao wao walikuwa na makanisa 140 miongoni mwa Waszekler wa Transylvania na wachache wao nchiin Hungary. Vitabu vyao vya nyimbo vya mwaka 1865 havikuacha aina yo yote ya mwongozo au nafasi ya maelekezo ya nafasi ya kumuabudu Kristo (soma ERE, ibid.). Masalia waaminifu na wakweli wa Kanisa walioachwa sasa wakawa ni Watranscarpathiani ambao bado ni Waunitariani wanaoistunza—Sabato.

Ukuaji wa imani ya Waunitariani katika Uingereza ulisababishwa na nia ya dhati ya kufanya marejesho ya imani sahihi ya mitume. Lilikuwa ni jambo la dhahiri kufikirika kutoka kwenye mawazo ya Waingereza kuwa Agano Jipya halikuwa la mfumo wa Kitrinitariani bali lilikuwa la Kiunitariani na watu wale wenye kufanya mambo yao papo kwa papo waliamua kuanzisha mafundisho ya msingi ya asili ya Kanisa. Mwanzilishi huenda alikuwa ni Richard Hooker (1553-1600) na John Hales (1584-1656). Ufunguaji wa maana ya siri ya Uungu kwenye Maandiko Matakatifu pekeyake kwa sababu ya jambo la katikati. Kazi za William Chillingworth (1602-1644) zimekuwa ni kiini cha jambo hili. Chillingworth alivuta ushawishi wake kutoka kwa Lord Falkland, Mu-Unitariani mkubwa. Kazi za Grotius ziko kimya kuongelea kuhusu asili ya utatu na [kwa mujibu wa Stephen Nye katika jarida la Historia yake Fupi ya Waunitariani na pia walioitwa Wasociniani, yaani: Brief History of the Unitarians also called Socinians, London, 1687) linasema kuwa alitafsiri kazi zake kwa mrengo wa Ki-Unitarian au ni kwa mujibu wa mawazo ya Wasociniani (ERE, uk. 522).

Paul Best (1590-1657) aliongoka wakati wa safari yake ya kwenda Poland. Milton pia alivutiw na Wa-Transylvania Wa-Unitariani (tazama jarida la Aereopagitica, London, 1644 – lililoandikwa kutoka kwenye ERE, ibid.). Makutano wa Kusanyiko la Canterbury na wa mjini York katika mwezi Juni 1640 walikataza uingizaji wa vitabu vya Waunitariani (yaani Wasocinia) naBunge lilipitisha sheria ya kufanya kuwa tendo la kukataa ukiri wa imani ya Utatu kuwa ni kusa kubwa mnamo mwaka 1648. Hata hivyo, John Biddle (katika miaka ya 1616-1662), mara nyingi aliyejulikana kama baba wa Waunitariani Waingereza, alichapisha katekisimu iliyojulikana kama Katekisimu ya Mikunjo Mieili ya Maandiko Matakatifu yaani (A Twofold Scripture Catechism) mnamo mwaka 1654. Imani ya Kiunitariani ikawa ni kuu sana katika Uingereza katika kipindi cha karne ya kumi na saba. Profesa Bronowski, kwenye mfululizo wa vipindi vya Runinga (Television) wa mafundisho yasemayo Kupaa kwa Mwanadamu, alifika mbali sana kiasi cha kusema kuwa Mageuzi ya Nafsi ya Kila mtu yalikuwa ni matokeo ya watu wanaowazia Uunitariani. Licha ya ufunwaji na kupelekwa uhamishoni kwenye Visiwa vya Scilly kwenye miaka ya (1654-1658), Biddle aliwakusanya na kupata wafuasi. Kifo cha Biddle katika mwaka wa 1662 na tendo la kuwafanya walingane kwa usawa waliona vuguvugu kama shirika la kufanyia ibada. Hata hivyo, madai ya makusudio ya moja kwa moja ya Maandiko Matakatifu kulipelekea kufanyika watu wote wa wakati ule kukataa imani ya Utatu yaani Utrinitariani. Hii ilimhusisha Milton. Thomas Firmin aliyeishi kwenye miaka ya (1632-1697) tajiri mwenye rehema alifadhili uandishi wa maandiko kwenye miaka ya 1691-1705. Bunge lilijaribu kulizima jambo hili. Hata hivyo, wana falsafa wakuu waliingia kwenye ulingo huu kwa namna ya John Locke aliyeishi miaka ya (1632-1704). Sir Isaac Newton pia alimfuata Milton kuingia imani ya Unitariani kutokana na mtihani wa Maandiko Matakatifu. Watu hawa maarufu kifikra walifuatiwa na William Whiston aliyeishi miaka ya (1672-1752) aliyamrithi Newton kule Cambridge, kama profesa Lucasian mnamo mwaka 1703 na aliangushwa na kondolewa madarakani mwaka 1710 kwa sababu ya kuamini kwake imani ya Unitariani. Matisho ya Samuel Clarke kwenye miaka ya (1675-1729) kwa ajili ya kilichoitwa Mafundisho ya Maandiko Matakatifu Yahusuyo Utatu yalikuwa pia ni ya muhimu katika kutuliza tatizo hili. Lengo la umilele—saidizi wa mwana lilifanyika hapa kwa mara ya kwanza, ili kunazisha nafasi ya Wabinitariani—kwa sehe,u. Wakati chuo kilichojulikana kama Manchester Academy (ambacho hatimaye kiliitwa Chuo cha Oxford cha Manchester) kilifunguliwa mnamo mwaka 1786, mkuu wake wa chuo hiki wa kwanza alikuwa ni Thomas Barnes ambaye alikuwa ni mtu kutoka imani ya Ki-Unitariani.

Chuo cha Wapresbyteria kilichukuweko mjini Carmarthen kilikuwa ni chombo cha kuendeleza mfululizo wa taasisi za elimu, ya kwanza kati yao ilianzishwa na Samuel Jones ambaye wakati mwingine alikuwa ni mshiriki wa Chuo kilichojulikana kama Chuo cha Yesu cha Oxford yaani (Jesus College Oxford) na ni mmojawapo kati ya wa watumishi 2,000 waliofukuzwa mwaka 1662 (ERE, uk. 523).

M-Unitariani wengine Joseph Priestly aliyeishi katika miaka ya (1733-1804). Rafuki kipenzi Kasisi Theophilus Lindsey aliyeishi kwenye miaka ya (1723-1808) paroko wa Catterick huko mjini Tees alijiuzulu kazi yake baada ya Bunge kushindwa kupitisha mswada wake na akafungua kanisa dogo la Ki-Unitariani katika Mtaa wa Essex Street, Strand mwaka 1774. hili lilikuwa ni kanisa la kwanza kufunguliwa baada ya kipindi cha miaka mingi sana—huenda ikawa hata tangia wakati wa kukomeshwa kwa Kanisa la Wageni.

Kanisa hili aliloanzisha, lilitumia Liturjia ya Wa-Anglikana ambavyo walikuwa wanamuabudu Baba peke yake. Kuchaguliwa kwa Thomas Belsham aliyeishi miaka ya (1750-1829) aliyechaguliwa mnamo mwaka 1789 hadi kwenye ualimu wa elimu ya kitheolojia kwenye chuo cha mjini Hackney kulisaidia sababu ya Waunitariani ya kufunguliwa kwa usomaji wa Maandiko Matakatifu. Hii ilifanyika kwa kupitia kwenye Jamii ya Ki-Unitariani kwa kufadhili utangazaji elimu ya Kikristo na Matumizi ya Taswira Fulani kwa ajili ya Ugawaji wa Vitabu. Kasisi Lindsey, na Belsham walikuwa ndio viongozi wake. Kutanguliwa kwa mwaka 1813, kupitia bidii ilivyofanywa na William Smith aliyeishi kwenye miaka ya (1756-1835) Mbunge wa jimbo la uchaguzi la Norwich na babu wa Florence Nightingale, aliyeweka kifungu cha kisheria kilichojulikana kama Sheria ya Kuvumiliana iliyoamuru kuharamisha imani ya Unitariani ikiona Unitariani ikiendelea. Imani ya hawa Wa-Unitariani pia iliyakataa Mafundisho yanayosema juu ya Roho kuishi ilele bila ya kufa (tazama ERE, p. 524). Thomas Southwood Smith aliyeishi mnamo miaka ya (1788-1861) pia aliingiza mawazo yake ya imani ya Ki-Unitariani kwa Byron, Moore, Wordsworth na Crabbe.

Mtazamo wa Smith ulikuwa tayari umekutikana ukijielezea kutoka kwenye maelezo ya mwanzoni kabisa ya Cromwell (ERE, ibid.). Vita vilivyojulikana kama vita halali vilivyopiganwa katika karne ya kumi na nane ilishuhudia mabadiliko ya mahala pa sheria za majuku ya Kanisa ambayo pia yalikuwa na misingi imara kwa makanisa ya Wa-Unitariani yaliyojiunda yenuewe.

Imani ya Unitariani kama vile ilivyoendelezwa na James Martineau aliyeishi kwenye miaka ya (1805-1900) na kwa shule ya kisasa iliyoachana na kushikilia matendo ya Kimasihi ya Yesu Kristo na haikuwa imetegemewa kwenye Maandiko Matakatifu lakini pia kwenye tafsiri ya Maandiko haya Matakatifu ki fikra. Ufafanuzi huu wa ujenzi mpya wa Tübingen wa Ukristo asili ilichapishwa kwenye Rejea za mjini Westminster na kupelekea kwenye jarida la ERE (uk. 525) ni muhimu kama ilivyokuwa kwenye udhibitisho wa falsafa yake kuhusu roho ya mwanadamu na mambo ya Kimbinguni. Chanzo kilichopelekea imani ya Unitariani kukosea kutafuta kukataa dhana ya kuwepo kwa—Kristo tokea mwanzo yaa ni uwepowake kwa siku kabla ya kuzaliwa kwake duniani.

John James Tayler aliyeishi miaka ya (1797-1869) alianzisha majadiliano ya kwanza ya swali la Johannine huko Uingereza kwenye jarida lake la Jaribio la kutathimini tabia za Injili ya Nne la (London, 1867). Kwa kadiri ile ambayo mlolongo wa wanazuoni ulivyokuwa wakisihi kurejelewa kwa aya za maandiko na za Agano Jipya na George Vance Smith alialikwa kujiunga kwenye kundi la Wapitiaji tena wa maandiko ya Biblia mnamo mwaka wa (1870). Mwanazuoni wa Ki-unitariani yaani wa mrengo unaoamini juu ya Mungu mmoja tu wa pekee na wakweli waliyeitwa James Drummond aliyeishi mnamo miaka ya (1835-1918) alikuwa ni mwana theolojia msomi aliyefanyiza kazi zenye kuashiria maana ya Masihi wa Kiyahudi  mnamo mwaka (1877), Philo Judaeus katika mwaka wa (1888) na Maulizo ya Tabia na Uandishi wa Injili ya Nne  mnamo mwaka wa (1903). John Relly Beard alioyeishi kwenye miaka ya (1800-1876) aliongoza njia au uanzishaji wa kamusi za kisasa za Biblia pamoja na kamusi iliyojilikana kwa lugha ya Kiingereza kama People’s Dictionary of the Bible, yaani Kiswahili chake ni kuwa Kamusi ya Biblia ya Watu wake. Watu wengine maarufu kwenye imani hii ya Unitariani walikuwa ni kina Edgar Taylor, Samuel Sharpe, H A Bright, William Rathbone Greg, Francis William Newman, Frances Power Cobbe, Ralph Waldo Emerson, Theodore Parker na Max Müller. Hii ERE pia hutoa maelekezo juu ya makanisa na migawanyiko yake. Baadhi ya watu maarufu katika masuala ya fikra na kufikiri wa nyakati za sasa, wanapoifanyia utafiti Biblia kwa ajili ya nia yake ya haraka na ya bure wanatheolojia wa Kiyunani wa kutoka shule maafurufu za Alexandria na Cappadocia, wameikubali na kuishikilia imani na mfumo wa Ki-Unitariani kuwa ndio mfumo wa kwanza kabisa wa Kibiblia.

Vuguvugu la Usabato wa Kibaptisti

Wa-Unitarian Wasabato wakawa dhahiri kabisa sasa inhini Uingereza kwenye karne ya kumi na saba, ingawaje baadhi yao waliweza kushuhudia kuendelea kwa kihistoria kutoka siku za mapema zaidi huko nyuma yake. Theolojia ya Kibiblia iliyotokana na Wasomi na wapenda maandiko matakatifu ilianzishwa kwa misingi ya vuguvugu lililojulikana kama Traskite ikiongozwa na John Traske takriban mwaka 1616 huko London. Hamlet Jackson aliijumlisha Sabato kundini kwa kupitia kusomea kwake Biblia. Tafsiri ya moja kwa moja isiyo na fumbo ya Maandiko Matakatifu kulikipelekea kikundi hiki cha Puritan kuelewa sheria ya vyakula ya kitabu cha Walawei pia. Ni kwa kupitia hali hii ndipo wafuasi wake wakaunda ngome ikijulikana kama Kanisa la Mill Yard la Kibaptisti la Wasabato, wakati ambapo wengine waliona chanzo chake kutoka kwenye vuguvugu la miaka ya. Kanisa lilifanyika kuwa maarufu zaidi mnamo mwaka 1661 kwa ajili ya mahubiri ya Tano ya Mtawa maarufu John James, ambaye hatimaye aliuawa kwa ajili ya kupanga hila ya kufanya jaribio la mapinduzi ya kisiasa. Kanisa lilipata ushawishi mkubwa sio tu kwenye masunagogi ya Kiyahudi peke yake yaliyokuwako huko Amsterdam, lakini pia kwa vuguvugu vikundi maarufu zilizofuata mrengo wa kimsihi katika Sabbetai Zwi. Kanisa, kama ilivyo jumla ya Wabaptisti wote wa wakati ule walikuwa ni wenye kufuata kikamilifu imani ya mrengo wa Ki-Unitariani yaani juu ya Mungu mmoja, kama ilivyoonyeshwa na waandishi kadhaa kama vile Edward Elwall mwanzoni mwa miaka ya 1700. Kalenda ya Kibiblia na maadhimisho ya Pasaka siku ya 14 ya mwezi wa Nisani vinavyoendelea leo, ingawa kutokana na kifo cha Mchungaji Albourne Peat kulisababisha kuwa ile bidii ya kushuhudia ya Wa-Unitariani ilianza kupungua kasi yake (kuanzia mwaka wa 1992).

Ingawaje ushahidi wa kihistoria unamapungufu, inaonekana kana kwamba wengi wao kama sio wote miongoni mwao makanisa ya mwanzo ya Kibaptisti ya Kisabato yaliyokuweko nchini Uingereza walikuwa kwenye mrengo wa imani ya Ki-Unitariani vile vile. Jambo la kwanza lililokuwako dhahiri na la aina yake lilikuwa ni kuanzishwa kwa kanisa lililojulikana kama Kanisa la Ukumbi wa Prinner lililoanzishwa na Frances Bampfield mnamo mwaka 1676. kanisa hili lilikuwa ni la Ki-Calvinisti kwa mtazamo wake wa nje, na ingawaje Bampfield hakuwa mfuasi wa mafundisho ya imani ya Utatu, yaani U-Trinitariani katika mtazamo wake, lakini pia hakuwa mfuasi wa mafundisho ya upande wa hasda wa Wa-Unitariani. Mchanganyiko wa Wabaptisti Fulani na katika Ujumla wao ulipelekea kuanzishwa kwa dhana ya Wa-Unitariani asilia wa Kibaptisti wa Kisabato. Wafuasi wa mafundisho ya Utatu wa Mungu yaani Wa-Trinitariani wakawa wanazidi kuendelea mbele zaidi kwa kuanzisha matamko ya ukiri wa imani, hivyo kufanya kuwa makabrasha yasielekee kabisa na misingi ya imani ya msimamo wa Wa-Unitariani. Wa-Unitariani wameamua kimya-kimya sana kuacha kufuata au kuamini mfumo huu wa matamko ya ukiri wa imani. Kwa kusema kweli, yangia kipindi cha Mill Yard hadi wakati huu hawakukubaliana na lolote lingine liwalo miongoni mwake zaidi ya hizi amri kumi za Mungu pamoja na nyongeza ya aya kadhaa chache zinazounga mkono maandiko ya Agano Jipya (hii ni kwa mujibu wa jarida liitwalo Wasabato wa Kibaptisti katika Ulaya na Amerika kwa Kiingereza maarufu kama Seventh Day Baptists in Europe and America, Vol. 1, na Vipeperushi vya Jumuia ya Kisabato ya Waamerika, maarufu kama “American Sabbath Tract Society, Plainfield, New Jersey, 1910, pp. 25-113)”.

Hii ndiyo ilikuwa ni kosa la kimsingi kwa imani ya kanisa la Kibaptisti la Kisabato. Kwa kushindwa kwao kutunga tamko la midingi ya imani yao, wasingeweza kuanzisha kikamilifu na kwa wazi ukiri wa imani. Hivyo kufanya kuwa kueneza sehemu nyingine mbali mbali ukiri wa imani kusiwekane kirahisi. Walishindwa kuwezekana uhuru wao wa kidini na kuendeleza mafundisho yenye uzima na ya kweli kuhusu asili ya Mungu.

Imani ya Mungu Mmoja na Utunzaji wa-Sabato

Wa-Unitariani wa siku za mwanzo, bila ya kitu kingine cha ziada, karibu walikuwa waambatana na Utunzaji-Sabato kama vyote viwili vinavyoelekezwa na tafsiri iliyo wazi ya kibiblia. Imani ya U-Trinitariani haikuwa hata mara moja ikiambatana na utunzaji-Sabato hadi kufikia wakati wa Matengenezo. Baada ya Matengenezo ndipo ikijulikana kwa dhahiri kuwa baadhi ya Watunza-Sabato walikuwa ni wafuasi wa mafundisho ya Utatu yaani Wa-Trinitariani na kwamba hata baadhi ya waamini Mungu mmoja yaani Wa-Unitariani walikuwa washika ibada za Jumapili ingawa haikuwa kama ni jambo la kanuni kwao. Wa-Unitariani walioko leo wamo kwenye kutanga tanga kama aina yoyote ya watu walioko kwenye mfumo wa waabudu ibada za Jumapili.

Katika Asia

Uzoefu wa Sabato katika Asia unaonyesha kuwa ulianzia kwa imani ambayo sio ya Utatu hadi kufikia wakati ule hadi shirika la Wajesuiti walipoanza kazi yao ya umisionary. Wa-Nestorians, na wamisionary wa Kiafrika (tazama jarida la Migawanyo ya Jumla ya Makanisa Yanayoishika—Sabato [122]) walifuata kanisa la kwanza katika Uajemi, India na halafu la Uchina. Imani ya Ki-Unitariani ya Watunza-Sabato lilitatizwa na makamio makuu sana au upinzani na imani ya Kibudha na iliharamishwa na watu wa imani hii ya Kibudha. Makanisa yatunzayo-Sabato katika pia yalikuwa kama ilivyokuwa kawaida yake hayakufuata kabisa mafundisho ya Utatu. Walitunza sheria ya vyakula na pia walikataa ukiri wa imani na mafundisho ya mahala waendako wafu. Migawanyo ya makanisa haya ilifuatia, hasa hasa, kutokana na Mabaraza ya Mitaguso ya Constantinople na Chalcedon.

Wachina walikuwa wameujua na kuuzoea mfumo wa Kikristo na, kama ilivyokuwa kwa maeneo mengine yo yote yale, ki kwamba, Sabato ilikuwa ni ishara ya tafsiri iliyowazi ya kibiblia. Mnamo mwaka 781 ilikuwa tayari imeshaanzishwa [tazama jarida la Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoshika-Sabato [122]]. Utunzaji-Sabato ulikuwa hai na kufanyika vema inchini Uchina hata wakati ule wa kuinuka kwa Mapinduzi yaliyojulikana kama Mapinduzi ya Taiping mnamo mwaka 1850.

Uzoefu Katika Nchi ya Marekani

Makanisa ya Mungu yanayoitunza Sabato nchini Marekani yamejulikana vema na hayataweza kufanyiwa vinginevyo kule. Makanisa ya Mungu yanakua na kuongezeka idadi kwa kufuata mfumo wa Kiingereza, kwa kufuata ushawishi wa Wazungu.

Imani ya Waadiventista wa Kisabato

Vuguvugu la Waadiventista wa Kisabato lilianza kwa kufuata mrengo wa Kiunitariani kwa kipindi chake chote cha kuanzishwa kwake hadi kufikia mwaka 1931 baada ya kifo cha Uriah Smith. Lakini uchukuliaji wa kiofisi ulikuwa kwa wakati mwingine katika ujio na kubakia kwenye huduma. Wa-Adventista Wa-Unitariani waliokuwa wenye nguvu za hoja zenye kufikirika walikuwa ni kina James White, R F Cottrell Snr na Jnr, D T Bordeau hadi kusajiliwa kwake, D M Canright, J N Andrews, Loughborough, John Matteson, A C Bordeau, A T Jones, W W Prescott na Uriah Smith.

Makundi mengine ya vuguvugu la Wa-Adventista yalikuwa:

  1. Wa-Adventista Wakiinjili; na
  2. Wa-Adventa Wakristo.

Wote walishindwa kuelewa asili ya ufufuo na ya hukumu. Wote wawili walikuwa ni wasomi walioamini uwepo wa kipindi cha Milenia ya kimatendo na sio ya kiroho wakifuata maandiko matakatifu ya kibiblia wakati ambapo wafuasi wa mafundisho ya Wa-SDA walifuata na kuamini mafundisho ya kwamba kipindi cha Milenia kitakuwa mbinguni.

Imani ya Kiadventa walikuwa kirasmi kwa ujumla ni ya Kibiblia ya Kiunitariani hadi mwaka 1931 wakati wa ushawishi wa Uriah Smith ulipokoma kwenye kanisa hili na hatimaye Wa-Trinitariani, muda kitambo ndani yake, walianza kushika hatamu. Uriah Smith alijulikiana kama alama ya imani ya Wa-Ariani na waliomrithi cheo chake baadae.

Ellen G White anaaminika kuwa alikuwa niwa kwanza kuanzisha wazo la mafundisho ya Utatu katika ushirika wa kanisa la Waadiventista wa Kisabato kupitia kitabu chake maarugu cha Hamu ya Zama mbali mbali kijulikanacho kwa Kiingereza kama Desire of Ages (1898, uk. 530), kinachoonekana kutofanyiwa uhariri na dhidi ya mtazamo wa haraka wa kanisa (kwa mujibu wa jarida la M L Andreasen la Roho ya Unabii, lililozinduliwa 30 Novemba 1948). Zilikuwepo shule nyingine za Wa-Adventist zilizounda mawazo yenye kufikirika.

M L Andreasen (sawa na hapo juu) anasema kuwa walikionea mashaka kitabu hiki na kukiona kama kinamakosa ya kiuhariri na alifanya safari na kwenda kuongea naye na kuthibitisha kuwa kilikuwa ndicho. Hiki hakikuchapishwa na kutolewa na yeye hadi kufikia mwaka 1948. Kwa mtazamo wa kifikra na kwa mafundisho ya wazee wa kanisa mnamo mwaka 1931, uandishi huu ulidhaniwa kuwa ni wa uhariri wa kughushi. Muunganiko wa Wakristo, ambao kwayo, James White alitokea, ulikuwa ni wa Wa-Unitariani. Hatimaye waliungana na wengine kuunda Kanisa la Muungano la Kristo (yaani United Church of Christ). Mafundisho yalikuwa ni ya kibiblia zaidi kuliko yale ile iliyokuja kuitwa kuwa ni Kanisa la Kiunitatiani la Watu wote yaani (Unitarian Universalist Church). Kanisa lile halina uhusiano wa kweli na mafundisho yaliyochini ya imani ya Kiunitariani yaliyoko miongoni mwa makanisa ya watunza-Sabato.

Kanisa la Waadventista lilikuwa ni miongoni mwa makanisa yanayofuata mrengo wa kuamini juu ya Mungu mmoja tu yaani Unitariani, au kama Waadventista walivyo sasa, yaani Wa-Ariani, hadi kufikia mwaka 1931. Hata hivyo, Imani ya Ki-Ariani kama ilivyotafsiriwa na waamini Utatu yaani na Watrinitariani wanadai kuwa Roho Mtakatifu kuwa ni mwumbaji wa Mwana. Mafundisho haya yanaweza kuwa ni mageuzi ya Watrinitariani kama tunavyoona kuwa fafanuzi za Arius hazina kumbukumbu yo yote ya mafundisho haya. Hata hivyo, kama ilivyotafsiriwa na wafuasi wa imani ya Utrinitariani, imani ya Uariani sio ya Kiunitariani wa kibiblia na sio mafundisho yanayotuama kwenye mafundisho ya Smith au na zama za kanisa zikiwemo zile za Kanisa la Mungu (la Kisabato, maarufu kama Church of God (Seventh Day) au na makanisa yaliyofuatia baadae.

Ni muhimu kukujua kwamba dhehebu la Waadiventista wa Kisabato halikuwahi kuwa rasmi kuwa ni la Kitrinitariani hadi pale baada ya uchapishaji wa jarida lililojulikana kama Maswali au Maulizo kuhusu Mafundisho yaani (Questions on Doctrine) mnamo mwaka 1958. Andreasen alioandika mfululizo wa nakala za nyaraka za kupinga maigo haya ya mwisho. Kwa hiyo, kulikuwa na kipindi cha mpito kati ya miaka ya 1931 na 1958. Matamko ya Ukiri wa Imani kwa Waadiventista wa Ufaransa yalionekana kuwa bado ya mrengo wa Kiunitariani mnamo mwaka 1938, kwa mujibu wa ilivyoonekana kwenye nakala ya vitabu vya Mafundisho ya Kanisa kwa mwaka ule kwa miliki ya Dr Thomas Mcelwain aliyesomea kwenye seminari ya Waadiventista inchini Ufaransa kuanzia mwaka 1968 hadi 1973. alijisomea mwenyewe fafanuzi za kazi hii na kugundua kuwa ile seminari ilikuwa ni ta Kitrinitariani, lakini makutaniko kwa wakati ule yalikuwa ni ya Kiunitariani.

Vuguvugu la Waadventista la mwanzoni mwa miaka ya 1800 (yaani 1842-1844) liliona kuwa Watrinitariani wakiongolewa kwa uwingi kujiunga na mfumo wa Kisabato. Baadhi yao kwakweli hawakuwa wameachana na mfumo wa Kitrinitariani na hii inathibitisha jinsi walivyoshindwa tokea mwanzo kuweka mfumo bora zaidi wa kiimani ya wa Waadventista baada ya kipindi cha uongozi wa Smith mnamo mwaka 1931 wakati Waadventa waamini Utrinitariani walipochukua hatamu za uongozi, hasa hasa kupitia mabadiliko ya muundo wa huduma. Hamu ya kushawishi au kuwavutia waumini wa Kiamerika wa kutoka imani ya Kiprotestanti ilikuwa ndio jambo lililochangia sana kuleta tatizo hilo. Pia kulisababisha kukaribisha ushawishi wa imani ya Kibinitariani kwenye Makanisa ya Mungu kwenye karne ya ishirini na hivyo kusababisha ongezeko maradufu la makosa na migawanyiko kwenye mfumo uliopo leo.

Kanisa la Mungu (la Mrengo wa Siku ya Saba)

Kanisa la Mungu la Mrengo wa Siku ya Saba yaani Church of God (Seventh Day) lilikuwa ni la mrengo wa kibiblia wa mfumo wa Kiunitariani wa watunza-Sabato ambalo halikuwa na utaratibu wa kufuata kuzitunza Siku Takatifu lakini lilijulikana kuwa lilikuwa likifanya hivyo kwa maeneo yake Fulani mengine (kwa mafano ni kule nchini Chile).

Sasa limegeuza kuwa na Watrinitariani kwa utendaji kazi wake na pendine huenda likazidiwa na kusalimu amri ingawaje nguvu zake za sauti ya wapigaji kura za waumini wake, kama ilivyopingwa na uongozi wa huduma, wengi wanaliokoa kwa kusalimu amri kwa haraka kama ilivyoonekana kwenye kanisa lililojulikana kama Kanisa la Mungu Lililoenea Ulimwenguni kote, (yaani Worldwide Church of God). Mnamo mwaka 1997, Kanisa la Mungu (la mrengo wa Siku ya Saba [yaani, Church of God (Seventh Day)] lilijitangaza kuwa linafuata mrengo wa wanaoamini Uungu wa Miungu Miwili, yaani Ubinitariani.

Kanisa la Mungu Lililoenea Ulimwenguni Kote (mwanzoni likijulikana kama Radio ya Kanisa la Mungu)

Herbert Armstrong alianzisha uandishi wa jarida yaani gazeti la Kanisa la Mungu (la Mrengo wa Siku ya Saba), yaani the Church of God (Seventh Day) lililojulikana kama Mtetezi au Wakili wa Biblia, kwa Kiingereza ni Bible Advocate kuanzia mwaka 1927. alianzisha kazi yake ya kihuduma kuanzia mapema sana ya miaka ya 1930 lakini bado ilikuwa kwenye makabrasha ya kumbukumbu za Kanisa la Mungu (la mrengo wa Siku ya Saba) yaani Church of God (Seventh Day) hadi kufikia takriban mwaka 1940. hii ilikuwa baada ya tangazo la vuguvugu hili la Waadiventista kuamua kuwa ni Watrinitariani na sasa sio tu kuishia kuwa na ushirikiano na mafundisho haya.

Theolojia ya dhehebu la Worldwide Church of God ilikuwa ni ya Kiditheisti na kuambatana nayo, lakini haikuwa ni sawa kabisa na mafundisho yenye kupotosha ya Marathonius baada ya kufukuzwa na kuuawa kwa Macedonius baada ya Mtaguso wa Baraza la Constantinople mnamo mwaka 381 BK. Ilitofautiana na asili ya Roho Mtakatifu, lakini bado waliendelea kuamini juu ya miungu miwili. Ilitafsiriwa kimakosa mno na kulikuwa na Waunitariani wengi kwenye kanisa hili la Worldwide Church of God hii ni kwa sababu tu ya utata wa kiutafsiri au utafsiri wa kutoa maana mbili uliotokana na Ufundishaji wa Kozi za Biblia ambao ulichukulia muundo wa Mungu na nafsi ya umoja yaani Eloah.

Kutokana na kuvunjika kwa kanisa hili la Worldwide Church of God kulisababisha kuwepo kwa mlolongo wa vikundi vya makanisa ambayo kwa bahati mbaya sana na kwa makosa walitafsiri mafundisho ya Uungu kwingineko kote. Wengi wao kiujuzi ni Waditheisti yaani wanaoamini juu ya Miungu wawili yaani ab orgine. Wengine wamejitangazia muundo wa Kibinitariani, lakini ni kwa mdhihirisho hafifu sana wa kitheolojia. Vikundi vyote hivyo hutunza Siku Takatifu za Mungu. Na ni vikundi viwili tu ndio hutunza Miandamo ya Mwezi Mpya.

Makanisa ya Kikristo ya Mungu

Umoja wa Makanisa ya Kikristo ya Mungu kama unavyoitwa kwa Kiingereza kama Christian Churches of God ni Kanisa linaloitunza-Sabato na pia linashika maadhimisho ya mambo yote yaliyokuwemo kwenye mfumo wa kanisa la kwanza, kukiwemo imani na mafundisho ya kibiblia yalivyofundishwa kuhusu Umoja wa Mungu katika Uungu wake, yaani U-unitariani. Lina matawi yake kwenye mataifa ambayo hayatumii lugha ya Kiingereza yakitumia jina kwa lugha zao lililotafsiriwa kwa maana moja na ilivyo kwenye lugha ya Kiingereza.

Mashahidi wa Yehova

Mashahidi wa Yehova ni Kanisa linalofuata mrengo wa Kiunitariani, ambalo halizitunzi wala kuzielewa kuhusu Sabato, Miandamo ya Mwezi Mpya na Sikukuu kama zilivyoamriwa na Mungu. Kwa hiyo, wanapungukiwa au kukosa kabisa kuwa na ishara za muhimu za mteule kama zilivyoandikwa kwenye maandiko matakatifu na kufundishwa kwenye jarida hili.

Hitimisho

Sabato ni ishara mojawapo ya kuonyesha kuwa hili ni Kanisa la Mungu. Na sio ishara ya pekee. Ishara ya kwanza kabisa na ya msingi ni Uungu. Huu ndio muundo wa kibiblia wa Kiunitariani. Ubatizo ni ishara ya pili na tendo la kumpokea Roho Mtakatifu ni ishara ya ndani. Ishara inayoonekana kwa nje ni adhimisho la Sabato, na Ushirika wa Meza ya Bwana/Pasaka, ambayo ni ishara ya sheria za Mungu. Hii inafuatiwa na adhimisho la Miandamo ya Mwezi Mpya na Siku Takatifu zilizoamriwa na Mungu. Hizi Sabato zinapingwa na kukataliwa na wanadamu kwa sababu ya kukithiri kwa ibada za sanamu.

Ezekieli 20:16-20 inasema, 16kwa sababu walizikataa hukumu zangu, wala hawakuenenda katika amri zangu, wakazitia unajisi Sabato zangu, kwa maana mioyo yao iliandama vinyago vyao. 17Walakini jicho langu likawahurumia nisiwaangamize kabisa, wala sikuwakomesha kabisa jangwani. 18Kisha nikawaambia watoto wao jangwani, Msiende katika amri za baba zenu, wala msizishike hukumu zao, wala msijitie unajisi kwa vinyago vyao. 19Mimi ni BWANA, Mungu wenu; enendeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda; 20zishikeni Sabato zangu; nazo zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Utiaji unajisi wa hizi Sabato unatokana na kukithiri kwa ibada za sanamu. Sabato hizi hujumlisha siku zote zilizotengwa kando na Mungu kwa ajili ya kufanya ibada kwa kufuatana na mujibu wa Kalenda yake inayotokana na uadhimishaji kiusahihi kabisa wa Miandamo ya Mwezi Mpya. Mungu hulihukumu taifa kwa kuach kwao kumtii yeye na kwa kushindwa kwao kuzishika amri na sheria zake.

Ezekiel 20:21-24 inasema, 21Lakini watoto wao waliniasi; hawakuenda katika amri zangu, wala hawakuzishika hukumu zangu kuzitenda, ambazo mwanadamu ataishi kwazo kama akizitenda; walizitia unajisi Sabato zangu; ndipo nikasema, kwamba nitamwaga dhadhabu yangu juu yao, ili kuitimiza hasira yangu juu yao jangwani. 22Lakini naliuzuia mkono wangu, nikatenda kwa kwa ajili ya jina langu, nisitiwe unajisi mbele ya macho ya mataifa, ambao mbele ya macho yao naliwatoa.  23Tena naliwainulia mkono wangu jangwani, kwamba nitawatawanya kati ya mataifa, na kuwatapanya katika nchi mbalimbali; 24Kwa sababu hawakuzitekeleza hukumu zangu, bali walizikataa amri zangu, nao walitia unajisi Sabato zangu, na macho yao yaliandama vinyago vya baba zao.

Sabato hizi hazitenganiki na amri ya kwanza na sheria. Taifa liliadhibiwa kwa kosa la kuacha kuzitunza kanuni zote za sheria za Mungu. Wateule wameishikilia imani kwa mkazo wenye kumaanisha hadi kufikia kwenye karne za kumi na tisa na ya ishirini wakati ambapo ibada za kumuabudu Mungu Mmoja Wapekee na Wakweli zilirejeshwa na uelewa juu ya Uungu ulionewa mashaka na walio kwenye mrengo wa Kiprotestanti.


Jedwali linaloonyesha Mafundisho ya Msingi ya Makanisa ya Mungu

Fundisho la Kanisa

Kuhusu Uungu

Muundo wa Kidhehebu

Ubatizo

Sabato

Mianamo ya Mwezi Mpya

Siku Takatifu

Meza ya Bwana/Pasaka

Sheria ya Vyakula

Paulo-kwa Waefeso (30 BK nk)

Unitariani wa Kibiblia

Kipresbyteria na kwa sehemu waki-Episcopaliani

Ubatizo wa watu wazima

Wanaitunza Sabato

Waliadhimisha Miandamo ya Mwezi Mpya

Waliadhimisha Siku Takatifu

Huazimisha siku ya 14 ya Mwezi wa Abibu

Wanazishka

Smyrna-Lyons (karne za 2 hadi 9)

Unitariani wa Kibiblia

Kipresbyteria na kwa sehemu waki-Episcopaliani

Ubatizo wa watu wazima

Wanaitunza Sabato

Waliadhimisha Miandamo ya Mwezi Mpya

Waliadhimisha Siku Takatifu

Huazimisha siku ya 14 ya Mwezi wa Abibu

Wanazishka

Wapauliciani (karne za 4-10.)

Unitariani wa Kibiblia

Kwa sehemu Wakujeshi

Ubatizo wa watu wazima

Wanaitunza Sabato

Nivigumu Kujua na hakuna uhakika

Waliadhimisha Siku Takatifu

Huazimisha siku ya 14 ya Mwezi wa Abibu

Wanazishka

Franco-Wavallensia wa Kihispania au Wasabato (Wakialbigeni wa karne za 9 hadi-15)

Unitariani wa Kibiblia

Ufaransa ulikuwa ni wa Kiepiscopaliani usio na vyeo vya madaraka. Huko Uhispania Wakipresbyteriani

Ubatizo wa watu wazima

Wanaitunza Sabato

Wote waliabudu kipindi cha mateso

Waliadhimisha Siku Takatifu

Huazimisha siku ya 14 ya Mwezi wa Abibu

Wanazishka

Waaldensia WasSabato wa zama za kati kabla ya Mwatengenezo

Unitariani wa Kibiblia

Kipresbyteriani. Baraza la wazee, sinodi na usawa wa madaraka.

Ubatizo wa watu wazima

Wanaitunza Sabato

Wote waliabudu kwa siri kipindi cha mateso

Waliadhimisha Siku Takatifu

Quarto-deciman

Wanazishka

Waaldensia wa zama za kati baada ya matengenezo (karne ya 16 nk.)

Kwa sehemu Watrinitariani

Mchanganyiko hadi kufikia hali isiyoeleweka

Ubatizo wa watu wazima

Walifikia pahala pa kuabudu siku ya Jumapili pamoja na Matengenezo

Hawakuadhimisha

Hawakuadhimisha

Waliadhimisha Easter (na kuamini kusulibiwa kwa siku ya Ijumaa na ufufuko wa Jumapili)

Wanazishka

Wasabato wa Ulya ya Mashariki (karne ya 11 pekee)

Unitariani wa Kibiblia

Kipresbyteria kwenye maeneo yaliyo muhimu

Ubatizo wa watu wazima

Liliitunza Sabato-(wakarambaratikia kuabudu Jumapili mwaka 1579)

Waliadhimisha Mwandamo wa Mwezu Mpya

Hawakuadhimisha

Huazimisha siku ya 14 ya Mwezi wa Abibu

Wanazishka

Waanabaptisti/ au Walollards wa zama kabla ya matengenezo (karne ya 9 pekee)

Unitariani wa Kibiblia

Kipresbyteria.

Kundi lilitawanyika katika karne ya 15

Ubatizo wa watu wazima

Liliitunza Sabato-(wakarambaratikia kuabudu Jumapili mwaka 1579)

Hakuna kumbukumbu kuwa waliadhimisha

Kama walivyofanya Waalbigensiani baada ya Matengenezo

Huazimisha siku ya 14 ya Mwezi wa Abibu

Wanazishka

Wabaptisti baada ya zama za matengenezo

Mchanganyiko na (Wabaptisti Wasabato wa zama za kwanza Waunitariani)

Mchanganyiko

Ubatizo wa watu wazima

Mchanganyiko

Hawaadhimishi (baadhi ya makanisa yao leo huadhimisha Sikukuu)

Hakuna Ushahidi kama Waliadhimisha

Wengi wao waliadhimisha Easter

Mchanganiko

Wabaptisti wa Kiamerika

(karne ya 17 pekee)

Mchanganyiko

Mchanganyiko

Ubatizo wa watu wazima

Mchanganyiko

Hawaadhimishi

Hakuna Ushahidi kama Waliadhimisha

Wengi wao waliadhimisha Easter

Mchanganyiko

Waadventa wa Sabato

(karne ya 19 nk)

Waunitariani hadi walipochukua mafundisho ya Utatu mwaka 1931-58 baada ya kifo cha Uriah Smith

Kikatiba Upresbyteria

Ubatizo wa watu wazima

Wanaitunza Sabato

Hawaadhimishi

Walikubali lakini Hawakuadhimisha

Walishika maadhimisho ya Easter (wanaamini kusulibiwa kwa Ijumaa) baada ya Kanisa la Mungu (la Kisabato) kusambaratika

Wanazishka

Kanisa la Mungu (Lakisabato)

Waunitariani lakini sasa wanaanza kubadilika

Kikatiba Upresbyteria

Ubatizo wa watu wazima

Wanaitunza Sabato

Hawaadhimishi

Kwa maeneo mengine Wanaadhimisha

Huazimisha siku ya 14 ya Mwezi wa Abibu

Wanazishka

Kanisa la Mungu enevu Ulimwenguni (Zamani Radio ya Kanisa la Mungu)

Waunitariani pamoja na Kanisa la Mungu (la Kisabato) hadi kufikia kusambaratika kwake na hadi mwaka 1955. walizitafsiri Kimakosa imani za Unitariani/ Ditheisti/ Binitariani na kuchanganya hadi mwaka 1994. wakagawanyika Migawanyo mbali mbali

Kikatiba Upresbyteria tokea Kanisa la Mungu (la Kisabato) lilipoigawanya Katiba na kukataza kupigaji wa  kura. Kwa sasa ni shirikisho la kimadaraka kama zaidi sana kiukoo

Ubatizo wa watu wazima

Liliitunza Sabatoh-hadi mwaka 1996. Wakaanza kuabudu Jumapili. Matawi yake yanaitunza Sabato.

Hawaadhimishi. Baadhi huweka vipindi vya Kujisomea Biblia usiku wa Mwandamo wa Mwezi kwa siku isiyo sahihi kwa kipindi kifupi.

Wanaadhimisha lakini Waadhimishi Mganda wa Kutikiswa.

Huazimisha siku ya 14 ya Mwezi wa Abibu kwa Kalenda ya Kiyahudi kwa Utaratibu wa Pasaka uliokosewa. Haikuadhimishwa kwa baadhi ya maeneo 1996

Wanazishka

Makanisa ya Kikristo ya Mungu

Unitariani wa Kibiblia

Kikatiba Kipresbyteria

Ubatizo wa watu wazima

Wanaitunza Sabato

Wanaadhimisha Miandamo ya Mwezi Mpya

Wanaadhimisha Siku Takatifu

Huazimisha siku ya 14 ya Mwezi wa Abibu

Wanazishka



Nyongeza

Ufafanuzi wa Kimapokeo wa Wapinzani dhidi ya Wenye kuamini-Utatu au

Watrinitariani na Imani ya Mungu mmoja yaani U-unitariani


Katika kifungu cha 150 cha Toleo la II Schaff anaelezea kuhusu madaraja ya wapinzani wa wale wanaoamini Utatu kwa kile alichokipa jina kuwa ni daraja la kwanza la Alogi, Theodotus, Artemon na Paulo wa Samostata. Anasema katika ukurasa wa 572 kwamba:

Hawa Wapinganzani wa dhidi ya Watrinitariani kwa kawaida wanaitwa Wamonarchiani kutoka (monarchia) au Waunitariani kwa ajili ya kuvunjika moyo walituama kwenye idadi yao, umoja binafsi wa Uungu.

Lakini tunapaswa kuwa waangalihu katika kuwatofautisha miongoni mwao madaraja mawili mkabala: Wamonarchiani wenye busara au walio na wenye kutumia nguvu, ambao wamekataa uweza wa kimbinguni wa Kristo, au alifafanua hiki kama “nguvu” za bure [dunamis]; na Wapatripassiani au Wamonarchiani wenye kujihisi, ambao walimlinganisha Mwana na Baba, na kukubaliana kwa kiasi kikubwa kwenye hisia tu ya utatu, ambao ni hisia ya pembe tatu za ufunuo, lakini sio umoja wa utatu wa kibinadamu.

Muundo wa kwanza wa fundisho hili la uwongo, yakihusisha imani ya Mungu mmoja waliyonao

Wayahudi, Kideistiki ikitenganisha kati ya ule uweza wa kimbinguni na wakibinadamu, na kuifanya kuwa bora kwa kiasi Fulani dhidi ya imani ya Kiebioni. Baada ya kushindwa kuaminika mafundisho haya kanisani, yaliinuka nje ya kanisa kwa kiwango kikubwa sana, kama ufunuo uliofanyizwa kiudanganyifu, na kwa mafanikio makubwa ya kushangaza katika imani ya watu wa umma wa Mohammadi ambao wanaweza kuitwa kuwa watu walio kati kama waigizaji wa dini ya Kiyahudi na waigizaji wa imani  ya Kiunitariani ya Kikrito wa upande wa Mashariki.

Aina ya pili ya kimtazamo inatanguliwa kutoka kwenye wazo la juu sana la uungu wa Kristo, lakini kwa sehemu vile vile kutoka kwenye dhana ya imani juu ya miungu mingi waliyokuwanayo makundi ya Uganostiki uliobobea yaani udoceti.

Mtu aliyedharau ukuu wa Mwana, na huyu mwingine ukuu wa Baba, bado hatimayake walifikia mahali pakubwa sana na Ukristo, na wakafikia kwenye kuafikiana kwenye makubaliano makubwa.

Inabidi ikumbukukwe pia kuwa Schaff ni muamini Utatu yaani ni Mtrinitariani na, kwa hiyo, anapingana na msimamo wa kiini cha theolojia inayompinga. Madai yake hayajakamilika kama tutakavyoona huko mbele. Schaff anasema (kwenye ukurasa wa 573) kuwa Wamonarki wote wa daraja la kwanza walimuona Kristo kama ni mtu wa kawaida tu, aliyejawa na uweza wa kimbinguni, lakini alipewa uweza huu wa kimbinguni kama ni kitu kifanyacho kazi ndani yake, sio kwa kuanzia kubatizwa kwake tu, kwa mujibu wa mtazamo wa mawazo ya waebioni, lakini tokea mwanzo, na kuachilia uweza wake wa uzawa wa asili na Roho Mtakatifu. Kisha aliorodhesha madaraja ya madhehebu haya ya Alogi, Theodotus. Kijana mdogo Theodotus alimfanya Melikizedeki kama mwombezi kati ya Mungu na malaika wengi, juu ya Kristo, aliye mwombezi kati ya Mungu na wanadamu (Schaff, uk. 574). Wafuasi wake pia waliitwa Wamelikizedeki. Schaff anaendelea kuorodhesha Wartemoni walio kataa uweza wa kimbinguni wa Kristo na waliwatumia kina Euclid na Aristotle kukataa fumbo za imani na kupinga kutumia imani ya Kiplato kupindisha ukweli wa injili.

Schaff pia anamtia kwenye orodha Paul wa Samostata, askofu wa Antiokia kaunzia mwaka 260, kama mtu maarufu sana miongoni mwa Waunitariani wenye busara na akili.

Alikataa wa Neno tupu yaani Logos na Roho Mtakatifu na kuwachukulia hao wote kama ni nguvu tu za Mungu, kama ilivyo fikra na nia ya mwanadamu, lakini ilitunukiwa kwamba Neno hili Logos lilikaa ndani ya Kristo kwa wingi sana kuliko ilivyokuwa kwa mjumbe awayeyote aliyetumwa na Mungu, na alifundisha kama Wasociniani wa nyakati zilizofuata baadae uinuliwaji wa taratibu wa Kristo, uliotokana na maendeleo yake mwenyewe ya kihisia hadi kufikia kwenye utukufu wa kimbinguni. Alikubaliana kuwa Kristo aliishi bila kutenda dhambi, na kwamba alizishinda dhambi zilizofanywa na mababa walioishi kabla yake, na hatimaye kuwa Mwokozi wa watu wote.

Schaff anachukulia kuwa aina tatu ya Wakristo bado walikuwepo kama Wasamostatiani, Wapauliani, na Wasabeliani. Hata hivyo, anafanya makosa hapa ya kuchanganya chini ya jina Wamonarki makundi mchangvanyiko ambayo ERE (tazama jarida la Imani ya Umonakia) linavyoonya dhidi kama linavyochanganya mambo juu ya jambo.

Kwenye daraja lake la pili la wapinga Utatu, Schaff anawajumlisha Praxeas, Noetus, Callistus na Beryllus. Hapa tunaonekana kuwa na mashindano kati ya Papa Hugh na watunzi wa jarida la ERE kwa upande mmoja na Schaff akiwa upande mwingine. Imani ya Umonarki kwa upeo wake wa juu sana ulichukua kutoka kwa Wapatripasiani kupitia kwa Noetus, na Wasabeliani ambao ni warithi wao. Schaff kwa vyo vyote vile hawaorodheshi kwa kuwatenga Wasabeliani kwenye kifungu cha 152. Ilikuwa ni kuonyesha kosa la imani ya Kimonarki na nafasi ya Wahipolitus kwamba kazi yake ilikuwa imenukuliwa kwenye jarida la Theolojia ya Kwanza ya Uungu [127]. Walifundisha kwamba Mungu mmoja mtukufu kwa hiyari na utashi wake, na kwa tendo la kujidhibiti kwake mwenyewe, alifanyika kuwa mwanadamu ili kwamba Mwana ambaye ni Baba ajivike mwili (Schaff, uk. 576). Utafiti wa kutosha, wa rejea za imani ya Umonarki unapatikana tu kwenye imani ya Utrinitariani ambako mafundisho ya Umonarki na Utabiri au Ubashiri wa kuamua mahusiano ya Uungu.

Imani ya Usabeliani ilianzisha na Athanasius ikafikia kwenye falsafa za Kistoiki na mara nyingi kufanyizwa tena. Sabellius alipinga utofautishaji wa jambo moja au umoja na utatu au mseto wa utatu kwenye asili ya mambo ya kimbinguni. Kwa hiyo, ufunuo wa Baba haukuanzia kwenye uumbuji ambao ulitanguliwa na ufunuo wa Watrinitariani lakini kwa wakati wa utoaji wa sheria au amri za Mungu. Ufunuo wa Mwana ulianzia wakati wa kufanyika kwake mwili na kuzaliwa na kuishia kwenye Upaaji wake kwenda mbinguni. Ufunuo wa Roho Mtakatifu ulianzia kwenye uvuvio na unaendelea kwenye kizazi na utakaso. Anawatolea mfano uhusiano wa wanaoamini imani ya utatu kwa kumlinganisha Baba na mjumuisho wa jua, Mwana kwa uweza wake wa kuangaza, Roho Mtakatifu kwa uweza wake wa kiushawishi wa kutoa joto (tazama pia jarida la mlinganisho wa mshumaa kwa imani ya Utrinitaria mambo leo). Anakataa utendaji kazi au mwonekano wa Baba na pia wa Mwana na Roho Mtakatifu. Anaweka mambo matatu ya muda ya kubuni yanayotimiliza utume wao na kurudi kwenye kwenye jambo lililo kama dhana tu inayowazika (tazama kitabu cha Schaff, mkabala .  kurasa za 581-583 kwa mafundisho). Mfumo huu utatokea teba kwenye vuguvugu la Mfumo wa Zama za Mambo ya Kizazi Kipya ilioja kwa mtindo au jina la Theolojia Endelevu. Ni kinyume cha Unyenyekevu au hali ya kujishusha unaofundisha na Wakristo Waunitariani ambao ni mitume na kanisa la kwanza, na Waunitariani Wanaofanya Marejesho au Matengenezo na kwa sisi wenyewe.

Schaff amekuwa kwenye kiwango cha chini sana cha kuwa mkweli kwa jinsi anavyoshughulika na mafundisho ya kwanza ya wasio-Watrinitariani. Anatumia neno wapinga-Utrinitaria ili kuashiria kwamba kulikuwa na mafundisho ya Kitrinitaria wakati ambapo hayakuwepo. Neno Utatu halikujulikana hapo kabla na wala halikuanzishwa hadi wakati ule wa Mtaguso wa Baraza la Costantinople mnamo mwaka 381 na bado likawa halijaingizwa hadi kwenye Baraza la Mtaguso wa Chalcedon mwaka 451 wakati ambapo idadi ya makanisa muhimu ikiongezeka kisha yakaambukizwa kushiriki imani hii ya Waamini Utatu. Hayataji makanisa haya wala aina ya Theolojia ya Watetea dini wa Kwanza ilivyukuwa, ambayo ilikuwa ni ya Waunitariani wanyenyekevu ama waliojishusha. Irenaeus ni wa muhimu kwa kuwa ni mtu aliyekaribu sana ambaye kwake twaweza kujifunza na kuipata theolojia asilia ya akina Yohana na Polycarp kwa ufafanuzi na uwazi zaidi. Historia za Watrinitarian, hata kama ni ya Waorotestanti au ya Wakatholiki, kwa nadra sana huikubali theolojia, inayokanusha imani yao. Schaff hutumia neno Uunitariani kwa nia ya jumla ya kujieneza, kama ilivyochukuliwa na Watrinitariani, ili kuficha mabishano ya kweli kati ya pande mbili toka kwenye karne ya kumi na tano. Chini ya mjumlisho wa pamoja, Waunitariani, Watrinitariani hujaribu kuingiza michanganyo ya jumla wa Wamodalisti au Wa Wamonarki na warithi wao au wafuasi wao Wapatripassiani pamoja na Waigaji ambao ni waadoptionisti, Wamelikizedeki, na pia Wayahudi na Waislamu, pamojana Waunitariani Wakristo ambao ndio waliopewa jina hilo. Hii huficha nia halisi ya neno. Ni vema zaidi kuliona mambo haya kama Watu wanaoamini juu ya Mungu mmoja tu (Wamonotheisti) na Waunitariani kama ni jozi-ndogo ya imani inayoamini Mungu mmojatu (yaani Monotheism). Hata hivyo, hii ni dhahiri kuwa ingejumlisha Watrinitariani na hivyo haitumiki.

q


 

CONCORDIAS

HECHAS, Y FIRMADAS

entre la jurisdicion Real, y

el Santo Oficio de la

Baraza la Mahojiano (Inquisicion).

MAAZIMIO AU MAAMUZI, Shauri na Sheria ya Mahakama ya kifalme, na Ofisi Takatifu ya Mahojiano

Valencia, 1568 (muungano wa Mwandishi).


UKIRI WA IMANI AU KIAPO

"Sisi, Daktari Andres de Palacio, Hakimu dhidi ya waenezaji wa mafundisho potofu ya uzushi dhidi ya mafundisho halisi ya kitume kwenye mji wa Valencia, nk.

"Kwa Wakristo waaminifu wote, wa jinsia zote mbili yaani waume kwa wake, makasisi wa makanisa madogomadogo, watawa wakiume na makasisi wa namna zote, kiasi na kiwango, mlio makini na kufuatilia jambo hili litakalopelekea kwenye wokovu kwa Bwana Yesu Kristo, wokovu wa kweli, wajuao kwamba, kwa namna ya viapo vingine na maneno ya hukumu ya Waheshimiwa maahakimu, watangulizi wetu, walionywa kujitokeza zao, kwa kipindi kilichotolewa, na kutangaza na kudhihirisha mambo walioyaona, wanayoyajua, na kuyasikia, akiambiwa mtu ye yote au watu fulani, iwe kuwa yu hai ama amekufa, akisema au au kufanya kitu cho chote kinyume na Imani Takatifu ya Kikatoliki, akiendeleza na kufuata sheria za Musa; au ya dini ya umma ya Mohammadi, au kanuni na maadhimisho ya namna ile ile, au kufanya uhalifu wa namna mbalimbali ya upotoe, Kuadhimisha siku za Ijumaa na za Jumamosi, na kubadilisha kuwa ni hariri safi ya mtu binafsi ya siku za Jumamosi na kuvaa nguo bora zaidi kuliko siku nyingine zo zote, kuandaa chakula kwa ajili ya siku za Jumamosi, kwa kutokosa sufuria kwenye moto moto mdogo, ambaye hakufanya kazi saa za jioni za Ijumaa na Jumamosi kama kwa siku nyingine zozote, anayewasha moto au nuru kwenye vinara safi na tambi za taa, saa za jioni za Ijumaa, wakiweka hariri safi juu ya vitanda na nepi safi juu ya meza, wakisherehekea sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, kuula mkate usiotiwa chachu pamoja na saladi na mboga za uchungu, wakiadhimisha ufungaji saumu ya utakaso wa msamaha wa dhambi (yaani Siku ya Upatanisho) wakiwa hawali siku yote hadi kufikia jioni baada ya kuchomoza kwa nyota, wakati wanaposameheana kila mtu na mwenzake na kuishiliza mfungo wa saumu yao, na kwa namna ile ile kuadhimisha mfungo wa saumu wa Malkia Easter, ya tissabav, na rosessena; waombao maombi kama ulivyo mujibu wa sheria ya Musa, wakisimama mbele ya ukuta, wakizongana kwa nyuma na kwa mbele, na kupiga hatua chache kuelekea nyuma, watoao fedha kununua mafuta kwa ajili ya hekalu la Kiyahudi au kwa mahala pengine pa siri pa kufanyia ibada, wanaochinja kuku wa kisasa wa kufuga sawa sawa na sheria za Kiyahudi, na kujinyima kula ya kondoo au aina nyingine yo yote ile ya mnyama aliye najisi, asiyetaka kula nyama ya zilizotiwa chumvi za nguruwe, sungura wakubwa, sungura wadogo, konokono, au samaki asiye na magamba, waogeshao miili ya wafu wao na kuwazika kwenye udongo mpya kwa mujibu wa desturi za Kiyahudi, aliye kwenye nyumba ya matanga wasiokula nyama ila samaki na mayai magumu yaliyochemshwa, walioketi kwenye meza za chini, wanaotenganisha chembe ya donge la linapookwa na kulitupa kwenye moto, linalofanywa, au kujulikana na wengine walotohara, waliotafuta msaada kwa mashetani, na kuwapa heshima anayostahili Mungu peke yake, wasemao kuwa sheria za Musa ni njema na zaweza kuleta wokovu wao, wanaozitenda sheria kanuni nyingi nyinginezo na maadhimisho ya namna ileile moja, wanaosema kwamba Bwana wetu Yesu Kristo hakuwa Masihi wa kweli aliyeahidiwa kwenye Maandiko Matakatifu, wala si mwana wa Mungu, wanaopinga kuwa alikufa kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu wote, wapingao ufufuo na kupaa kwake kwenda mbinguni; na wasemao kuwa Mama yetu Bikira Mariamu sio mama wa Mungu au mwanamwali kabla ya uzawa na baada, wasemao na kuthibitisha mafundisho mengi ya uongo na yenye makosa, wanaosema kwamba kile wanachokikiri mbele ya washitaki au mahakimu haukuwa ukweli, wanaoondoa kanzu za kikasisi na wala kubakia gerezani wala kuadhimisha toba iliyowekezwa juu yake wasemao vitu vya tuhuma dhidi ya Imani yetu takatifu ya Kirumi na dhidi ya maafisa wa Baraza la Mahojiano, au wanaoweka ushawishi aina yo yote ya mambo yasiyo ya uaminifu ambao wangeweza kuvutwa kwenye Ukatoliki kujizuia kuwaingiza, wanaodai kwamba Komunio Takatifu ya madhabahu sio mwili halisi na damu ya Yesu Mkombozi wetu, na kwamba Mungu hawezi kuwa na uwezo wa kuwepo mahali popote, au kuhani ye yote hushikilia maoni yenye madhara, wanaotaja kwa kuimba na maadhimisho ushika wa meza takatifu, wasiosema maneno matakatifu ya kuweka wakfu, wasemao na kuamini kuwa sheria ya Mahomet na kanuni zake na maadhimisho ni mazuri na yanayoweza kuleta wokovu wao, wanaojua kwamba maisha yanajiri katika kuzaliwa na kufa na kwamba hakuna paradiso na jehanamu, na wanasema kwamba kuchukua riba sio dhambi, iwapo kama mtu awaye yote ambaye mke wake anaishi bado, anaoa mke mwingine tena, au mwana mke yule anayeolewa tena, katika kipindi kile kile cha uhai wa mumewake wa kwanza, na iwapo kama wanamjua mtu ye yote anayezitunza desturi za Kiyahudi, na kuwataja watoto wake usiku wa siku ya saba baada ya kuzaliwa kwao na kwa fedha na dhahabu juu ya meza, kwa maadimisho yanayowatiliza kabisa sherehe za Kiyahudi, na iwapo kama kuna anayejua kwamba kama mtu akifa, wanaweka kikombe cha maji na kuwasha mshumaa na baadhi ya nepi ambako wafu waliokufa, na kwa siku kadhaa, hawakuingia pale, kama yeyote anazijua juhudi za Myahudi au mwongofu, kwa siri sana kuhubiri sheria za Musa na kuongoa wengine kwa ukiri huu wa imani, kufundisha maadhimisho yahusuyo kwenye hali yenyewe, ikitoa taarifa kama kwenye tarehe za sherehe na kufunga, ikifundisha maombi ya Wayahudi, kama mtu kuna anayemjua mtu ye yote anayejaribu kujafanya Myahudi, au kuwa Mkristo aendae nje kwa desturi za Myahudi, kama kuna mtu anayemfahmu mtu ye yote, aliyeongoka au vinginevyo, wanaoamuru kwamba uvaaji wake utafanyika kwa turubai na sio kwa hariri, kama Wayahudi wazuri wafanyavyo, kama kuna anayewajua wale ambao, wakati watoto wao wanapo wabusu mikono yao, na kuweka mikono yao kwenye vichwa vya watoto wao bila kuweka alama (ya Msalaba), au baada ya chakula cha jioni au cha usiku, kubariki divai na kumpa mtu ye yote mezani, ambayo mbaraka ujulikanao kama veraha; kama kuna ye yote aijuaye nyuma yeyote, ambayo watu hukusanyika kwa malengo ya kufanyia ibada za kidini, au kujisomea Biblia kwa lugha zao za asili au kuadhimisha sherehe nyingine za Kiyahudi, na kama kuna mtu ajuaye kwamba wakati mtu anapokaribia kuondoka safari, maneno Fulani ya sheria za Musa yanapaswa yanenwe kwa ajili yake, na mkono unatakiwa kuwekwa juu ya kichwa chake bila ya kuwekwa ishara (ya Msalaba). Na iwapo kama kuna mtu anayetumia ukiri wa imani wa sheria za Musa, au mwenye matumaini na marejeo ya Masihi, akisema kuwa Mkombozi wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo bado hajarudi na kwamba kwa sasa Eliya alitarajiwa kuja na kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi, na kama kuna mtu anayemjua mtu ye yote aliyejifanya kufuata nyayo za na kutangatanga mbinguni na kwamba malaika alimpeleka kwenye mashamba ya kijani na kumwambia kwamba ile ilikuwa ni nchi ya ahadi iliyokombolewa kwa ajili ya waongofu wote ambao Eliya aliwakomboa kutoka kwenye utumwa ambako waliishi, na nama kuna mtu anayemjua mtu ye yote au watu ama wawe watoto au wajukuu wa watuhumiwa, na ambao hawastahili, wanaotumia ofisi za umma, au wanaochukua silaha au wanaovaa nguo za hariri au nguo nzuri, au wanaojipamba kwa desturi ya vito vya dhahabu, fedha, lulu au vito vingine vya thamani au marijani, au kufanya matumizi ya kitu kingine cho chote walichokatazwa na kisichotakiwa kuwanacho, na kama kuna mtu kunamtu anayemjua mtu ye yote aliyenazo au kumiliki aina ye yote ya bidhaa zilizotaifishwa, kama vile samani yo yote, fedha, dhahabu, madini ya fedha, au vito vya thamani vilivyo mali ya wale waliotuhumiwa kwa mafundisho ya uzushi, ambazo vingetakiwa viletwe mbele ya mpokeaji wa bidhaa zilizotaifishwa za wale wote waliotuhumiwa kwa ajili makosa ya kueneza au kuamini mafundisho ya uzushi. –Vitu hivi vyote, vilivyoonekana, kusikiwa, au kujulikana, kwenu, kama vilivyoorodheshwa hapo juu, vya Wakristo waaminifu, wamefanyiwa, kwa mioyo ya kuridhika, wakikataa kutangaza na kuonyesha, kwa siasi kikubwa mzigo waliokuwa nao na manyanyaso ya mioyo yao, kukidhaniwa kwamba umefikiri sana matangazo ya makatazo ya sheria za kujinyima yaliyotolewa na baba yetu mtakatifu, na kwa ahadi na misaada ambayo uliifanya, ambayo kwayo umepewa tangazo la hukumu ya kutengwa na faini nyingine kubwa zilizo chini ya sheria ya dola, na kwa hiyo unaweza kutanguliwa kinyume cha kama wale waliokumbwa na mkasa wa kutengwa na kama waliokumbwa na mafundisho ya uzushi, kwa namna mbali mbali, lakini, wakihitaji kufanyiwa ukarimu, na ili kwamba roho zenu zisipotee, kama ilivyo kuwa Bwana wetu hafurahii kifo cha mwenye dhambi bali ageuke na aishi, kwa kutoa kwake huku, tunaondokana na kuweka kando uenezaji imani wa nguvu wa wajulikanao kama mahakimu wa zamani dhidi yako, kwa kadiri uadhimishavyo na kukubaliana na maneno ya sheria hizi, ambazo tunahitajika, tukiomba na kuwaagiza, kwa saburi ya utii mtakatifu, na chini ya lilizo la kutengwa kwa moja kwa moja, kwa kipindi cha siku tisa kutoka wakati ambao sheria iliyopo itakuwa imesomwa kwenu, au myakavyo julishwa kwa namna yo yote ile, li kuelezewa yote mnayoyajua, kuyaona, kuyasikia, au kusikia yakisimuliwa kwa namna iwayo yote, kwa vitu na kwa maadhimisho kama ilivyotajwa hapo-juu, na kujitokeza mbele zetu binafsi ili kutangaza na kujihirisha kile ulichokiona, kusikia, au kusikia kikisimuliwa kwa siri, bila ya kuwa kiliongelewa siku zilizopita na mtu mwingine ye yote, au kutoa ushahidi wa uwongo dhidi ya mtu awaye yote. Vinginevyo, kipindi kilichopita, maonyo ya kikanuni yamekuwa yakirudiwa kwa mujibu wa isemavyo sheria, hatua zitachukuliwa ili kutoa na kutangaza hukumu ya kuwatenga dhidi yenu, hivyo na kwa jinsi ya nakala hizi, na kwa kupitia utengaji huu, tunawataka kwamba mshitakiwe, na kama baada ya kipindi kirefu cha siku tisa, mtabakia kwenye uasi wenu na kutengwa, basi mtatengwa, mtashutimiwa kwa tangazo la kulaaniwa, mtalaaniwa, mtababaguliwa, na kutengwa muonekane kama jumuia ya shetani, na umoja na pamoja na baraza la Kanisa-Mama lililo takatifu, na kwa sakramenti zote kadhalika. Na tunawaamuru wakuu wa makasisi wa mtaa, makasisi wa mtaa wenyewe, makasisi watoao huduma kwenye vitengo maalumu, na wakatekumene na watu wengine wo wote wakidini au wahusika katika uongozi wa kanisa kutilia maanani na kutunza mambo haya yaliyotajwa hapo-juu kama livyotengwa na kulaaniwa kwa kuweza kupatwa na hasira na uchungu wa Mungu Mwenyezi, na ya Bikira Mariamu mwenye kutukuka, Mama yake, na mitume walioteseka yaani Mtakatifu Petro na Mtakatifu Paulo, na watakatifu wote wa Mahakama tukufu, na juu ya waasi kama hawa na watovu wa nidhamu ambao wangeificha kweli kwa mujibu wa mambo yaliyoorodheshwa hapo juu, kuwa yote ni maafa na maneno machafu au matusi yaliyo angukia na kushukia kwa Mfalme Farao na jeshi lake kwa kutokutii amri za mbinguni, na hukumu ile ile ya kutengwa kimbinguni kuwazungukia kama ilivyowazingira watu wa Sodoma na Gomora ambao wote waliangamia kwenye mwali wa moto, na kina Dathani na Abiramu waliomezwa na nchi kwa ajili ya maasi makuu na dhambi walizozifanya kwa ajili ya uasi wao dhidi ya Bwana Mungu wetu, na wengine waliangukia kwenye dhambi ya kula na kunywa, kwa wakati wa kuamka na wa kulala, kwa wakati wa kuja na wa kwenda.wakidhoofika katika dhambi za wakati waishipo na wanapokufa, na kamwe hawakushupaza shingo zao kwa ajili ya dhambi zao, na shetani akiwa kwenye upande wao wa kuume kila mara, na shughuli yao ikiwa ni dhambi, na siku zao kuwa chache na za uovu, na akiba yao ikifaidiwa na wengine, na watoto wao kuwa mayatima, na wake zao kuwa wajane. Na watoto wao kamwe hawakuwa na uhitaji, na hakuna ye yote aliyewasaidia, na hawakuweza kurejea majumbani mwao na bidhaa zao zilichukuliwa kiliza na watozaji wa riba, na wala hakuna ye yote aliyeweza kuwafanya mwenzi wao, na watoto wao wakihusuriwa na kukatiliwa mbali, na majina yao pia, na madhaifu yao yakidumu kwa wakati wote kwenye kumbukumbu za mbinguni. Na maadui wao wakiwashinda na kuwanyang’anya kila wanachokimiliki hapa duniani, nao wanatanga tanga kutoka mlngo huu hadi mlango mwingine bila hata ya kupata nafuu. Na maombi yao kugeuka kuwa machukizo au matusi, na kupungukiwa kwa kiasi kikubwa sana na mkate na divai, nyama na samaki, matunda na vyakula vinginevyo ambavyo wanakula, vile vile nyumba wanazoishi na kanzu wanazovaa, wanyama ambao wanawapanda na vitanda wanavyo vilalia, na meza na leso za kujitandia wanapokula. mezani ktacast. Viliwekwa laana ya Shetani na kwa Lusifa na kwa mapepo yote ya kuzimuni, na hawa kuwa ndio mabwana wao, na kuwafuatiwa kwa usiku na mchana. Amina. Na iwapo kama watu atakumbana na hiyo inayoitwa kutengwa na kudhalilishwa, ili aweze kuendelea kusadiki hayo kwa ajili ya kiwango fulani cha kipindi cha mwaka, wasichukuliwe kama ni wazushi wao wenyewe, na wataweza kushitakiwa kwa anamna hiyo hiyo ya kuwa dhidi ya mafundisho ya uzushi au watuhumiwa wa kosa hilo la kueneza mashundisho ya uzushi. Imetolewa leo tarehe—Machi, katika mwaka wa Bwana wetu Mungu, mwaka wa elfu moja na mia tano na ishirini.”

Nullus omoveat sub pena excommunicationis.

(Dondoo: lisilo na pazia au uficho ni ukiri uliofanywa na mwenye kukiri kwa kufanya utawazo kwa hukumu ya kutengwa ambayo kwamba mzushi mwenye kuhusika na hatia ya uzushi anaweza kushiriki, kutokea wakati wa kufanyika kwa kosa.)

(Dondoo: Wote wanaojua kitu cho chote miongoni mwa mambo yaliyotajwa kwenye sheria hii iliyopo, au kwa ajili ya mafundisho mengine ya uzushi, na wasio fikia kikomo mbele ya kujikanisha na kutangaza vivyo hivyo, kwa hiyo wametengwa na hawawezi kusamehewa na wajoli wao.)

El doctor De Mandato sue
Palacio, inquisidor. Reverende paternitatis,
Petrus Sorell, notarius.

q