Makanisa ya Kikristo ya Mungu

 [CB002]

 

 

 

Yesu ni Nani?

 

(nakala 2.0 20020512-20061227)

 

Biblia inatuambia ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Wakristo wengine wanasema Yesu ni Nafsi ya pili katika Utatu Mtakatifu. Baba na Roho Mtakatifu wakisemwa kuwa nafsi zingine mbili zinazokamilisha sehemu ya tatu ya umbo la Mungu katika nafsi tatu. Walakini, Biblia inasema kuna Mungu Mmoja tu wa Kweli na ni lazima tumwelewe kama tunataka kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli .

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

 

(Copyright ã 2002, 2006 Christian Churches of God, ed. Wade Cox)

(Tr. 2008)

 

 

Mafunzo haya yanaweza kunakiliwa bure na kutawanywa kwa masharti ya kwamba yatanakiliwa kama yalivyo yote bila kuongeza au kupunguzwa au kubadilishwa au kufanyiwa masahihisho. Jina la mwandishi na anwani yake na haki milki yake lazima vijumlishwe pamoja. Bila kutoza malipo yo yote wakati wa kunakili au katika usambazaji maneno mafupi y anaweza kunakiliwa katika masomo maalum na kutafakariwa bila ya kuathiri haki milki.

 

Mafunzo haya yanapatikana kutoka katika mtandao wa kidunia

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Yesu ni nani?




Utabiri wa kuzaliwa kwa Yesu kulianza kujulikana tangu zamani kabla ya kuzaliwa; kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara.  Tazama, bikira atachukua mamba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Immanuel  (Isa. 7:14).

 

Kupitia katika muujiza huu wa Mungu Mmoja wa Kweli, Mtoto Yesu alichukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na mama mwanadamu, Bikira Mariamu (Lk. 1:26-35; Mt. 1:23). Anaitwa pia kimakosa Mary. Mume wa Mariamu aliitwa Yusufu, lakini hakuwa baba wa kimwili wa Yesu.

 

Nabii Isaya alisema habari zake za kufurahisha na zenye kutia matumaini muda mrefu kabla ya kuzaliwa kwake.

 

Isaya 9:6-7 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake naye atamwita jina lake Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake. Kuuthibitisha na kuutegemeza kwa hukumu na kwa haki, tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa Majeshi ndiyo utakaotenda hayo (KJV).

 

Mfalme anayetajwa kuja anayezungumziwa na Isaya hapo juu alizaliwa miaka 2000 iliyopita katika zizi la ng’ombe na kulazwa katika hori la kulia ng’ombe.  Kuzaliwa kwake ilikuwa ni habari njema na yenye furaha kuu kwa wachungaji na kwa watu wote pia kama ilivyotolewa habari na malaika.  Maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa kwa ajili yenu, mwokozi ndiye Kristo Bwana (Lk 2:8-12)

 

Yesu alizaliwa katika kabila la Yuda (moja ya makabila 12 ya taifa la Israeli).  Katika mji wa Bethlehemu katika nchi ya Yudea katika siku za Herode mkuu (Mt. 2:1). Herode alikuwa mtu wa Edomu, kizazi cha Essau, watu ambao waliokuwa wamejichanganya na watu wa Yuda karibu miaka mia mibli iliyopita, kumbuka, Esau alikuwa ndugu pacha akiwa ni kaka yake Yakobo na walikuwa wana wa Isaka (Mwanzo 26:21-27).

 

Biblia haituelezei wazi ni siku ipi aliyozaliwa Yesu.  Hii ni kwa sababu njema kwa sababu hatupaswi kusherekea siku hii ya kuzaliwa kwake.  Kwa sababu hiyo hatupaswi kusherekea kuzaliwa kwa mtu yeyote.  Angalia somo la Siku za kuzaliwa (Na.  287).

 

Tumeambiwa tukumbuke siku ya kifo cha Yesu, na tunafanya hivyo kila mwaka wakati wa Pasaka.  Hili litaelezwa vizuri katika somo la Siku Takatifu za Mungu (Na. CB022).

 

Watu wengi katika mataifa ya Kikristo leo wanasherekea kuzaliwa kwa Yesu katika siku ya tarehe 25 ya mwezi Desemba.  Hii ndiyo sababu inayowafanya watu wengi washerekee siku ya Krismas.  Lakini tutaona katika somo lingine kwamba ni Desturi za kipagani na mila za Krismas hazina uhusiano wowote na kuzaliwa kwa Yesu (Angalia somo la Kwa nini hatupaswi kusherekea Krismas (Na. CB024).

 

MWANA WA MUNGU

Watu wengi leo wanafikiri Yesu ni Mungu.  Ni kweli kwamba ni Mungu, lakini sio Mungu mmoja wa kweli.  (Angalia pia Yn. 20:27-28).  Yesu ni kristo (Anayemaanisha mtiwa mafuta au Masihi, (Yn. 1:41, mwana wa Mungu aliye Hai (Mt. 16:16).  Eloah ni Jina la Mungu kwa Kiebrania na Yeye ni Masihi wa Mungu na Mungu wetu.  Jina ambalo alipewa Masihi duniani katika Kiebrania ni Yahoshua au Yashua.  Katika lugha ya Kiingereza ni Joshua.

 

Yesu ni Mwana wa Mungu na anashrikiana na wengine katika kutumia jina hilo, ambao pia ni wana wa Mungu.  Yesu anaitwa “Mwana wa Mungu aliye juu sana, aliyetukuka” (Mk. 5:7) walakini, Yesu ndiye mzaliwa wa pekee ambaye Ni Mwana wa Mungu (Mt. 3:17; Yn. 1:18; 1Yoh. 4:9).

 

Kuna Mungu mmoja, ambaye ni Baba na Bwana mmoja, Yesu Kristo ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo (1Kor. 8:6).  Biblia iko wazi ya kwamba kuna Mungu mmoja tu wa kweli na ya kwama alimtuma Yesu kristo kutenda kazi (Yn. 17:3-4).  Sehemu ya kazi hii ilikuwa ni kuwa Mwokozi na mkombozi wetu
(Mt. 14:33; Yon. 8:42; Efe. 1:7; Tito 2:14).

 

Yesu ndiye njia ya kwenda kwa Baba.  Ni kwa kupitia kwa Yesu Kristo tu, ndipo tunaweza kumjua Mungu mmoja wa kweli.  Hii ndiyo sababu tunaomba kwa Baba katika Jina la Mwanae (Yesu Kristo) (Yn. 14:12-14; 15:16).  Hatumwabudu Yesu, lakini tunamwabudu Baba. Hii ndiyo sababu Amri ya kwanza inasema, “Usiwe na miungu mingine ila Mimi (Kut. 20:3) imetupasa kumwabudu Mungu mmoja wa kweli peke yake.

 

Katika wakati fulani, hata kabla ya uumbaji Mungu mmoja wa kweli Baba (Eloah) alikuwa peke yake. Mungu huyu hawezi kufa (1Tim. 6:16). Lakini tutaona katika maandiko ya kwamba Yesu alikufa.  Kwa hiyo tunakuwa na uhakika ya kwamba Yesu Kristo sio Mungu Mwenyezi.  Tunaweza kusema sio mtu wa mwisho katika Ukuu.

 

Kristo anatwambia ya kwamba alitoka kwa Mungu (Yn. 8:42).  Kwa saabu hiyo vyote ni vyake au vyote vyatoka kwake Mungu ambaye ni Baba (Rum. 11:36).  Mwana aliumba kila kitu katika uwezo wa nguvu za Baba.  Kama alivyo katika mfano wa Baba, Mwana anayo haki ya kuitwaMungu na kupokea heshima sawa na Baba
(Yn. 5:22-24) lakini hatuwezi kumwabudu kama Mungu mmoja wa kweli.  Mungu ni mkuu kuliko yote (Yn. 10:29).

 

Baba alimpa Mwanae Uzima (Yn. 5:26).  Yesu alisema alipata Uzima toka kwa Baba (Yn. 6:57).  Alifanya yaliyo mapenzi ya Baba na siyo yaliyo mapenzi yake mwenyewe.

 

Kwa maneno mengine Baba alimuumba mwanae (ambaye alikuja kuwa Kristo) pamoja na majeshi yote ya Kiroho yaliumbwa kabla ya kuumba dunia.  Ukweli ni kwamba majeshi haya ya mbinguni yalikuwepo kabla ya uumbaji wa dunia.

 
Ayubu 38:4-7 ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?  Haya!  Sema, kama ukiwa na ufahamu 5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyaka, kama ukijua?  Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake? 6 Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?  Au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni, 7 Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha? (KJV).

 

Maandiko Matakatifu pia yanatuambia ya kwamba Mungu ambaye ni Baba (Eloah) ni Mungu asiyeonekana au kusikiwa na watu (YN. 1:18; 5:37) sivyo ilivyo kwa Mwana wa Mungu.  Alikuwa ni mfano wa Mungu asiyeonekana (Kol. 1:15) lakini alionekana na kusikiwa na mwanadamu.  Kwa hiyo mwana alimwakilisha Baba kwa kile alichokisema na kutenda.  Katika nyakati za Agano la kale watu walimwona na kuzungumza na Mungu.  Lakini huyo hakuwa Mungu mmoja wa Kweli.  Malaika ni wajumbe wa Mungu ambao waliweza kuongea na watu katika nyakati hizo na waliweza kuonekana kwao.  Biblia inasema Adamu alimwona Bwana Mungu katika Bustani ya Edeni (Mwa. 3:8-19).  Ibrahimu alimwona na kuongea na Bwana
(Mwa. 12:7; 17:1-3), Musa alikutana naye katika mlima (Kuto. 3:2-7). Yoshua alikutana naye Yeriko (Yoshua 5:13 mpaka 6:2) (RSV).

 

Ni kweli walitembelewa.  Ukweli ni kwamba walimwona mtu mwingine na kusikia sauti yake.  Matukio ya namna hiyo ni mengi ambapo Biblia inasema ya kwamba watu walimwona na kuzungumza na Mungu.  Huyu hawezi kuwa yule Mungu mmoja wa kweli kwa sababu hakuna mtu aliyepata kumwona na akaishi tena au kusikia sauti yake (Yoh. 5:37).  Philipo alipoomba kuonyeshwa Baba, Kristo alisema, “Aliyeniona mimi amemwona Baba” (yoh. 14:8-10).

 

KABLA YA KUJA KWA YESU

Hii inajulikana kama Mungu na Bwana na aliyeonekana na kusikiwa alikuwa ni Kristo tu.  Alikuwa anaitwa malaika wa Yehova katika Agano

 

Yohana 17:5 Na sasa, Baba unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako,(KJV)

 

Yohana mbatizaji kwa wazi anasema Kristo alikuwako kabla yake yeye (Yn. 1:15-18). Lakini Biblia inatwambia ya kwmba Yohana mbatizaji alikuwa mkubwa kwa Yesu zaidi yamiezi sita. Kwahiyo ilikuwa haiwezekani kwa Kristo kuwako kabla ya Yohana isipokuwa  alikuwako kabla. Maisha haya ya kabla ya Yesu kuchukua maisha ya kibinadamu, alikuwa kama Mungu, elohim (Kiebrania) au theoi (GK). Elohim ni wingi wa neno katika kiebrania, linalomaanisha Mungu au miungu na inawahusisha wana wote wa kiroho wa Mungu na baadhi ya wanadamu pia. Watu wa zamani za kale walielewa tofauti kati ya Mungu (Eloah) na elohim, aliyeonekana kwa wanadamu na kuzungumza nao.

 

Katika Agano Jipya pia inaonyesha wazi kutokana na maneno ya Kristo mwenyewe ya kwamba alikuwako kabla ya kuwa mwanadamu Yesu kweli alisema.  Kabla ya Ibrahim mimi halikuwako (Yn. 8:58).  Anasema hapa ya kwamba alikuwa tayari anauzima hata kabla ya Ibrahimu hajazaliwa.  Kwamba hiyo alikuwa ni mungu, na alikuwa ni malaika, au mjumbe wa Mungu Mmoja wa Kweli, kama tulivyoona, alizungumza kwa niaba ya Mungu Aliye juu sana (Angalia somo la (Jeshi la malaika (Na.CB 28) Kisha akawa mwanadamu. Angalia pia somo la Yesu Kristo kabla ya kuonekana (Na. 243).

 

KWA NINI YESU ALIKUJA?

Yesu alikuja duniani ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa Milele (Yn. 3:16) Yesu kwa hiari yake mwenywe alikufa ili awape Uzima wa milele kwa watu wake na ambao ni wa Mungu pia.  Adamu alikuwa na nafasi ya kufanya hivi, lakini alitenda dhambi.

 

Kwa sababu ya dhambi hii wanadamu walitengwa na Mungu Mmoja wa kweli.  Dhambi inatutenga na la Kale.  (Angalia somo la Malaika wa YHVH (Na. 24).

 

Biblia inasema ya kwamba Kristo alikuwa na Uzima wa Kiroho mbinguni kabla ya uumbaji wa nchi (Yoh. 6:38; 8:23-58; Flp. 2:5-7, RSV)

 

Mungu. Kwa hiyo tunapokuwa watu wazima ni lazima tutubu na kubatizwa ili tuweze kumpokea Roho Mtakatifu wa Mungu.  Yesu alikuja kutupa Uzima wake (Mauti yake) ili tupate uzima wa Milele katika yeye na Baba.  Kwa Kifo chake wanadamu sasa wanaweza kutubu katika dhambi zao na tena kupata njia ya kwenda kwa Baba kupitia kwa Roho wake Mtakatifu.

 

Wote tutakufa katika Kifo cha kawaida, lakini wote tutakuwa na nafasi ya kuishi tena.  Hatuwezi kuishi milele katika miili ya kibinadamu (Miili ya asili) maana hii ni miili  inayoishi kwa muda mfupi tu.  Wafu wote watafufuliwa kutoka Makaburini (Yn. 5:25-26).  Mungu Mmoja wa Kweli anampango mkuu kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu  (1Kor. 2:1-16). Tutajifunza zaidi juu ya mpango huu baada ya ubatizo.

 

WAKATI WA MAISHA YA YESU

Watu wengi hawakumsikiliza Yesu na walisema alikuwa na pepo (Yn.10:20).  Ambapo Makuhani na viongozi wa dini walitaka kumuua, watu wa kawaida walipenda kumsikiliza.  Alikuwa na kipawa na uwezo na mafundisho yake yalikuwa yenye nguvu (Lk 19:47-48). Watu walishangazwa na mafundisho yake (Mt. 7:28-29).

 

Yesu alifundisha kwa mafumbo k.m. mafundisho yake yalikuwa katika mifano yenye mafumbo yenye maana iliyofichika .  Watu wengi hawakuweza kuelewa mafundisho yake, na Yesu aliwafunulia wanafunzi wake tu.  Maana halisi ya mafundisho yake (Mk. 4:34).

 

Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi!  Na heshima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake (Mt. 11:19) walisemea hayo kwa sababu ya ubinafsi wao wakujihesabia haki yao wenyewe.

 

Katika Mathayo sura ya 4 Ibilisi alimjaribu Yesu kukubali kutenda kazi katika mpango tofauti wa kuitawala dunia. Akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia (Mt 4:9).  Ibilisi alimtaka Yesu amsujudie kama Mungu Mwenyezi na mwenye mamlaka yote.

 

Yesu alikua wazi ya kwamba hii ni kuvunja amri ya kwanza ya Mungu na ndipo Yesu akamwambia imeandikwa, “Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake na kumtumikia” Kisha Ibilisi akamwacha (Mt. 4:10-11).

 

Hatutawasikiliza watu wanaosema ya kwamba Yesu alikuja kuitengua sheria (Mt. 5:17-19) kama Kristo, au Masihi, dhabihu yake ilikuwa badala ya sheria za Torati tu (Ebr.10:1-18).

 

Amri kumi za Mungu bado ziliendelea na zinaendelea kuwepo na kuheshimiwa na zinatufunga sisi wote hadi hvi leo, kwa sababu zilikuwapo tangu zamani tangu uumbaji wa Jeshi la Mbinguni, na hata katika wanadamu wa kwanza kule katika Bustani ya Edeni.

 

MIUJIZA ALIYOTENDA YESU.

Kutokana na uwezo na nguvu katika Roho Mtakatifu wa Mungu Yesu aliweza kutenda miujiza mingi wakati alipokuwa duniani.  Hapa nchini ni baadhi tu ya miujiza aliyoitenda Yesu.  Angalia katika Maandiko matakatifu na soma kuhusu miujiza hii aliyoitenda Yesu.

Aliponya wagonjwa (Mt. 4:23-24)

Alibadili maji kuwa divai (Yn. 2:1-10)

Alitenbea juu ya maju (Mt. 14-22-23)

Alituliza dhoruba (tufani) (Mk. 4:35-41)

Alisamehe dhambi na kumponya aliyepooza (Lk. 5:17-26)

Alimfufua Lazaro kutoka kaburini (Yn. 11:38-44)

Kulikemea pepo (Mk. 5:1-16)

Alilisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili (Lk. 9:10-17).

 

KIFO CHA YESU

Kama ilivyojulikana tangu zamani kwamba Yesu atazaliwa, pia ilijulikana ya kwamba Yesu atakufa na kufufuka baada ya siku tatu mchana na usiku akiwa kaburini (Mt.16:21).  Na baada ya kufufuka kwake atarudi tena mbinguni (Yn. 14:2,3).

 

Kifo (Mateso) na kufufuka kwake Yesu ni matukio muhimu sana katika historia ya mwanadamu.  Lakini watu wengine wa dini hawaelewi Matukio haya vizuri.  Moja ya mambo wanayofundisha kuhusu kifo cha Yesu ni kwamba alisulubiwa msalabani.  Lakini neno la kigiriki stouros linamaanisha mti au nguzo iliyonyooka, iliyotumika kwa ajili ya kuwaadhibu wahalifu kwa kuwapigilia na misumari juu ya nguzo hizo au miti hiyo.  Kwa hiyo Yesu alikufa katika mti wa kuadhibia wahalifu na sio msalabani.  Kwa ufafanuzi zaidi wa jambo hili angalia somo la Msalaba, Mwanzo wake na maana yake (Na. 39).

 

MASIHI ANATAMBULIWA KAMA MWANAKONDOO WA MUNGU

Yohana 1:29-30 siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana – Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30 Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu (RSV).

 

Kama Mwana-kondoo wa Mungu” Yesu aliuawa katika wakati mwafaka.  Vinginevyo kifo chake kingekuwa kama kifo cha kawaida cha mtu yeyote. Tunaona kutoka katika historia ya Jews, Bk, VI, IX, 3) ya kwamba wanakondoo kwa ajili ya Pasaka walichinjwa kuanzia saa tisa hadi saa kumi na moja (k.m.  kuanzia saa 9:00 Mchana hadi saa 11:00 mchana) baada ya mchana wa siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza wa mwaka wa kalenda ya Mungu.  Mwezi huu unaitwa Abibu au Nisani. Wana-kondoo waliandaliwa na kuliwa jioni katika siku ya kumi na tano. Hata hivyo ni mwana-kondoo wa kwanza tu ndiye aliyeweza kuchinjiwa saa 9:00 mchana mbele ya kuhani Mkuu kama dhabihu ya Pasaka kwa mafundisho zaidi angalia somo la Kifo cha Mwanakondoo (Na. 242).

 

Ukweli ni kwamba Yesu alikufa katika siku ya kumi na nne (14) ya mwezi wa kwanza kufuatana na Kalenda ya Mungu.  Alikufa saa 9:00 (tisa ) mchana katika mwaka wa 30 CE.  Wakati huu ulikuwa ni katika utawala wa Kaisari Tiberia.  Kuna utata mwingi kati ya Madhehebu mbalimbali katika wakati huu wa sasa juu ya siku aliokufa Yesu.  Jambo hili limewachanganya watu ambao imani zao hazijakomaa (wenye imani changa).  Sio lazima sana kwa hatua hii kuyajua haya yote.  Jambo la muhimu zaidi ni kujua ya kwamba Yesu alikufa kwa wakati mwafaka wa kalenda ya Mungu kwa mapenzi ya Mungu vinginevyo asingelikuwa Kristo  (Angalia somo la Kalenda Takatifu ya Mungu (Na. CB020).

 

Kwa mafundisho zaidi angalia somo la Nyakati za mateso na kufufuka kwa Yesu (Na. 159). 

 

Watu wengi wanaamini ya kwamba Yesu alikufa siku ya Ijumaa na alifufuka kutoka kaburini siku ya Jumapili iliyofuata.  Lakini jambo wanaloliamini haliwezekani, kama tukiyachunguza Maandiko matakatifu kwa makini.

 

Kama ilivyo kwa Yona alikaa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la yule samaki mkubwa kadhalika Kristo naye ilikuwa ni lazima awe kaburini siku tatu/mchana na usiku kama vile Yona alivyokaa tumboni mwa yule samaki siku tatu mchana na usiku (Mt. 12:39-41). Kusema kwamba Yesu alikufa katika siku ya Ijumaa na kufufuka kutoka kaburini katika siku ya Jumapili iliyofuata ni wazi ya kwamba sio sahihi, kwa sababu hii inamaanisha karibu ni sawa na siku za giza mbili (yaani siku za usiku na mchana) na mchana mmoja.

 

Yesu alikufa siku ya Jumatano na kufufuka kutoka kaburini katika siku ya Jumamosi kukaribia majira ya kutua kwa jua.  Hii ilikuwa kabla ya kuanza kwa siku ya Jumapili, ambayo ni siku ya kwanza ya Juma.  Kumbuka siku zilianza na kuishia baada ya jua kutua au kuwa giza kwa kufuata kalenda ya Mungu, na sio kuanzia saa sita usiku kama iliyo siku hizi katika sehemu nyingi duniani.  Kwa hiyo hebu tufanye hesabu sasa ya siku za mchana na usiku.  Usiku wa Jumatano ulikuwa siku moja, ukifuatiwa na Alhamisi ambayo inakuwa siku moja.  Kisha kulikuwa na usiku wa pili, ukifuatiwa na Ijumaa siku ya pili.  Usiku wa Ijumaa ulikuwa usiku wa tatu ukifuatiwa na Jumamosi siku ya tatu, ambayo iliishia kwa kutua kwa jua au kuwa giza.  Sasa hapa inatimiza siku tatu kamili za mchana na usiku, kama biblia inavyotuambia.

 

Wanafunzi wa Yesu waliamini ya kwamba Yesu alikuwa mwanadamu, Masihi na kizazi cha kimwili cha Daudi kutoka katika kabila la Yuda. Lakini walidhani kuwa atawaokoa kutoka katika utawala wa kiruni na kuchukua mamlaka ya kidunia (Yn. 6:15; Lk. 23:2). Kifo chake kilileta mshituko mkubwa na kuwakatisha tamaa (Lk 23:21).

 

Maaduni zake walitaka kumuua kwa sababu alijiita mfalme. Alipoletwa mbele ya Pilato Yesu aliulizwa kama jambo hili lilikuwa ni kweli na akajibuUfalme wangu si wa dunia hii … (Yn. 18:36).

 

Pilato akamwuliza, wewe u mfalme basi? Yesu akajibu kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni …(Yn. 18:37).

 

Wayahudi hawakuamini ya kwamba Yesu alikuwa Masihi na hawakuamini ya kwamba alikuwa ametumwa na Mungu aliye Baba. Pia walimtegemea Masihi awe mfalme wao wa duniani na mtawala wao. Mamlaka ya kirumi walimchapa mijeledi na kumpa adhabu kali kwa kumpiga Yesu. Pilato alisikiliza matakwa ya wengi kwa sababu walitaka Yesu auwawe. Alikufa katika kifo chenye mateso na maumivu makali kwa muda mrefu. Mateso na maumivu haya makali yanaitwa kusulubiwa, na yaliwa yanatumiwa na Warumi na Wagiriki kwa kuwadhibu wahalifu sugu. Ilikuwa ni njia mbaya sana waliotumia kumtesa hadi kumwua Mwana wa Mungu.

 

Lakini Yesu aliyaelewa haya yote kabla na alijua ya kuwa atakufa katika mateso haya na alihiari mwenyewe kupatwa na haya yote kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Alijaribu kuwaonya wanafunzi wake lakini inaelelea hawakuweza kumwelewa.

 

Luka 9:20-22 Akawaambia, nayi mwasema ya kwamba mimi ni nani? Petro akajibu akasema, ndiwe Kristo wa Mungu, Akawaonya, akawakataza wasimwambie mtu neno hilo; akisema, imempasa mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka (RSV)

(Angalia pia Luka 18:31-34).

 

KUFUFUKA KWA YESU

Tunajua ya kwamba Yesu alifufuka kutoka katika wafu (Rum. 1:3-4). Kufufuka kwa Yesu kutoka katika wafu kwa uwezo na nguvu katika Roho Mtakatifu ni udhihirisho kuwa Yesu ni mwana wa Mungu aliyeshinda mauti.

 

Kuna ushahidi zaidi wa ufufuo wa kristo katika 1Wakorintho 15:3-8 na matendo 1:2-3 kuanzia matendo 1:9-10 Tunaona ya kwamba Yesu alichukuliwa juu mbinguni. Alikuwa mzaliwa wa kwanza wa waliokufa na chimbuko la matunda ya mganda ambako kunafanyika siku ya Jumapili wakati wa Pasaka (Angalia Lawi 23:9-14).

 

Kwa hiyo kama tulivyoelezea hapo juu, Yesu hakufufuka siku ya Jumapili. Walakini, watu wengi bado wanaendelea kuamini ya kwamba Yesu alifufuka siku ya Jumapili na ndiyo maana wanasherekea siku kuu ya kipagani ya Easter.Tabia ya kusherekea sikukuu ya Easter iliingia kanisani baada ya Yesu kupaa na kurudi mbinguni. Tunaelewa kutoka katika Biblia ya kwamba Kristo alifufuka kutoka katika wafu siku ya usiku wa Jumamosi na kisha kusubiri mpaka Jumapili asubuhi akiwa tiyari kupaa kwenda mbinguni.

 

Yohana 20:1 Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona jiwe limeondolewa kaburini.

 

UFALME WA MUNGU

Yesu alizaliwa kuwa mfalme katika ufalme ambao Mugu Baba aliahidi kuusimamisha. Ufalme wake hautakuwa kama ufalme huu wa dunia hii ya sasa dunia ya uovu (Gal 1:4) Amepewa kiti cha enzi cha Daudi kutawala nyumba ya Yakobo (Israeli) milele. Utawala wake hauna mwisho (Lk. 1:32).

 

Yesu alipokea ufalme baada ya Mungu ambaye ni Baba kumfufua kutoka katika mauti (Mt. 28:18). Ameketi sasa katika mkono wa kulia wa Mungu na ni Mfalme na Bwana.

 

Yesu ingawa alikuwa kama mwanadamu yeyote wa kawaida lakini alikuwa na tofauti kubwa sana na mwanadamu yeyote yule. Alijaribiwa lakini hakutenda dhambi (Ebr 4:15). Alikufa na akafufuka na anaishi na kutenda kazi hata leo. Yesu ndiye Mkuu wa Kanisa. Kwa hiyo ana kazi nyingi ya kuchunga watu ambao Mungu Baba amempa awakusanye pamoja Kanisani. Na sisi pia tulio kanisani lazima tufanye kazi pia ya kuleta kondoo wa Mugu Kanisani. Ni lazima tulindane sisi kwa sisi, kila mmoja akimlinda mwenzake na ikiwa kuna mgeni yeyote ambaye Bwana amemleta Kanisani ni wajibu wetu kumkaribisha na kumlinda pia. Imetupasa kukaribishana sisi kwa sisi na kuombeana tupate kuponywa na tusameheana na kusaidiana sisi kwa sisi.

 

Tunafahamu ya kwamba Yesu aliitunza sabato na sikukuu takatifu za Mungu na hivyo hata wanafunzi wake waliendelea kufanya hivyo baada ya kuwaacha na kupaa mbinguni. Ukweli ni kwamba Yesu pamoja na wanafunzi wake walitunza sheria na amri za Mungu. Kwa hiyo na sisi pia ni lazima tutunze na kutii sheria na amri za Mungu.

 

Yesu alikuwa ni mtu wa ajabu na mwenye sifa zote nzuri sana, lakini alikuwa na muda mfupi tu wa kukaa hapa duniani. Alikufa alipokuwa ana umri kama wa miaka 33, na bado alifanya mambo mengi sana kwa muda wake huo aliokaa duniani. Habari njema ni kwamba Yesu ambaye ni Masihi, atarudi tena kutawala mataifa ambayo hayamjui Mungu Mmoja wa Kweli. Mataifa haya hayatunzi wala kushika sheria na amri za Mungu na badala yake wanaabudu miungu na sanamu za uongo. Na wataadhibiwa ili waweze kurudishwa na hatimaye kumjua Mungu Mmoja wa Kweli.

 

Kama wakristo imetupasa kujitahidi kwa bidii zote katika jitihada za kweli kuishi kama Kristo alivyoishi. Kwa kufanya hivi tunaweza kuwa na hakika ya kwamba tunamfurahisha Mungu, pia tutakuwa tukijiandaa (kujitayarisha) kuchukua nafasi zetu katika ufalme wa Mungu.

 

q